0 votes
3.1k views
in Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine by
Ubadhirifu wa mali ya umma umetamalaki katika hadithi ya Shibe Itatumaliza. Jadili kwa kutoa mifano mwafaka.

1 Answer

0 votes
by
  1. Mzee Mambo analipwa msharahra mnono kama mkuu wa wizara zote ilhali kila wizara ina waziri wake.
  2. Sherehe kubwa za viongozi wa serikali ziantumia mali ya umma. Hivyo basi kuchangia ubadhilifu wa mali katika jamii.
  3. Viongozi huendeleza ubadhirifu kwa kutumia mali ya umma kwa manufaa yao wenyewe. Magari ya serikari ykanatumika katika sherehe na kazi za nyumani kama vile kuleta maji katika sherehe.
  4. Vyakula katika sherehe vinanunuliwakwa jpesa za umma. Pesa hizi zingetumika kuendeleza asasi za kijamii.
  5. Ubadhirifu unadhihirishwa na DJ jpale anapokea mabilioni ya pesa kwa kuwatumbuiza wageni katika sherehe.
  6. Ubadhirifu unadhihirishwa na viongozi wa serikali wanaowachukua watu wao wa karibu na kuonelea wamefaidika kutokana na rasilmali za wanajamii bila kuzitolea jasho.
  7. Viongozi wa serikali kama vile Sasa na Mburawanaamua kujipakulia chakula kupita kiasi katika shereh za mzee mambo na jamii yake ubadhirifu wa mali ya umma unaonekaran ambapo mali ya umma inatumika kuwaajiri mawaziri wawili wenye majukumu sawa katika wizara moja kazini . Kazi hii ingefanyw ana waziri mmoja na mshahara wa waziri wa pili ungechangia katika kuinua sekta nyingine.
  8. Upeperushaji wa matangazoa ya sherehe ya kiongozi binafsi katika vyombo vya haari kitaifa kwa siku nzima ni ubadhirifu wa mali ya umma. Pesa zilizotumika zinagechangia pakubwa katika kuinua uchumi wa taifa.
  9. Uuzaji wa dawa zilizotolewa katika bohari la kitaifa katika duka la DJ ambayo ni biashara ya mtu binafsi ni ubadhirifu wa mali ya umma.
  10. DJ kulipwa kutumbuiza watu katika sherehe ya Mzee Mambo na kulipwa mabilioni ya fedha ni ubadhirifu wa mali ya umma.
  11. DJ kupewa kazi ya mipango na mipangilio katika sherehe ilhali kuna mawaziri wawili wanaolipwa mshahara kwa kazi hiyo ni ubadhirifu wa mali ya umma.
Welcome to EasyElimu Questions and Answers, where you can ask questions and receive answers from other members of the community.

6.4k questions

9.6k answers

6 comments

590 users

...