Wednesday, 05 July 2023 13:24

Kiswahili Questions and Answers - KCPE 2023 Prediction Papers Set 2

Share via Whatsapp

Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne hapo. Jaza pengo kwa kuchagua jawabu lifaalo zaidi.

Hali ngumu ya maisha ___1___ waja wengi humu nchini ___2___; yaani kupoteza matumaini. ___3___ ya waja hawa ___4___ hata kukimu mahitaji yao ya kimsingi; ___5___. Mambo ___6___ zaidi na uhaba wa nafasi za ajira___7___ idadi kubwa ya vijana___8___. Ipo haja ya ___9___ vijana wakumbatie kazi za ufundi na zaraa ili mambo yao yasizidi ___10___.

   A   B   C   D 
 1.   yamewanya   imewafanya   zimewafanya   limewafanya 
 2.  kuenda nguu   kula mumbi   kula mwande  kuenda mserego 
 3.  Kati ya  Fauka ya   Miongoni   Baadhi 
 4.  mmeshindwa  tumeshindwa   wameshindwa   wameshindikana 
 5.  kujimudu  kujiweza   kujiendeleza   kujitosheleza 
 6.  imezoroteka  yamezoroteshwa   yamezorota  zimeharibiwa 
 7.  ambao  ambavyo   ambapo   ambako 
 8.   haina kazi wala bazi    hawana mbele wala nyuma   hawana kazi wala bazi   haijijui haijitambui 
 9.  kuwatia shime  kuwatia hima  kuwatilia mrija  kuwatia kapuni
 10.   kughafilika  kutambulika  kuajabia  kudidimia

 

___11___, wavyele wa Mwasi wakamwambia huku ___12___ na machozi ya majonzi  usione umepata kazi ukafikiri kuwa hutahitaji tena msaada wetu. Mwasi alikuwa ___13___. ____14___ alipopata kazi yake yenye mshahara mnono, katika idara moja serikalini, alijiona kafika kwelikweli. Wazazi waliamua lao liwe jicho tu hadi siku___15___ afikiwe na fimbo ya ulimwengu.

   A   B   C   D 
 11.   hasidi aangukapo mnyanyue   kutangulia si kufika   usitukane wakunga na uzazi ungalipo   usiache mbachao kwa msala upita
 12.  wamedondokwa  wakidondokwa   walidondokwa  wakadondokwa
 13.   haliki hatafuniki  hamjui aingiaye wala atokayo    hazidishi hapunguzi  haoni hasikii
 14.  Mpaka  Hadi   Lau   Tangu 
 15.  itakaofika  itakakofika   itakapofika  ifikayo

 

Kuanzia nambari 16 mpaka 30, chagua jibu lifaalo zaidi.

 1. Tambulisha sentensi inayoonyesha hali ya masharti.
  1. Mwadime alijikwaa akaumiza dole lakc.
  2. Lau ungefika mapema ungemkuta mjomba kwake.
  3. Mtoto alikuwa akilia kwa sababu ya njaa.
  4. Msichezee karibu na barabara yenye magari.
 2. Chagua maelezo sahihi kati ya haya.
  1. Manju ni mcheza ngoma stadi. 
  2. Mghani hutunga na kuimba mashairi.
  3. Mshenga ni mtu ambaye hupeleka habari za posa.
  4. Mjumu ni fundi wa kutia nakshi katika vyombo vya madini.
 3. Tumia viambishi mwafaka. 
  Shoka ______________________ lilomkata ndi ________________________ hili.
  1. li, lo
  2. i, yo
  3. u, o
  4. ki vyo
 4. Andika umoja wa sentensi ifuatayo.
  Mbao zilizoletwa zitatumiwa kujengea mabanda.
  1. Mbao iliyoletwa itatumiwa kujengea banda.
  2. Ubao ulioletwa utatumiwa kujengea banda.
  3. Mbao iliyoletwa itatumiwa kujengea kibanda.
  4. Ubao ulioletwa utatumiwa kujengea kibanda.
 5. Nomino ipi ya makundi imekamilishwa ipasavyo.
  1. Mkuo wa sabuni.
  2. Wingu la moto.
  3. Halmashauri ya wanafunzi.
  4. Kaumu ya ng'ombc.
 6. Chagua sentensi iliyotumia kiambishi ku kama kiwakilishi cha nafasi.
  1. Ulipofika hukujua tulikuwa chumbani.
  2. Kuliko na gharika kunahitaji msaad
  3. Kulipopambazuka nyinyi mlianza shughuli papo hapo.
  4. Alipokuona alikukimbilia kwa furaha tele.
 7. Gao ni ukubwa wa ngao. Aidha gao ni
  1. Mahali palipohamwa na hapana watu waishio hapo.
  2. Samaki mwenye rangi nyeupe tumboni na ya kijivu mgongoni.
  3. Kiganja cha mkono kilichokunjwa kwa ajili ya kutia kitu.
  4. Chombo cha seremala cha kushikia mbao.
 8. Andika usemi wa taarifa wa sentensi;
  Mwalimu aliwaambia wanafunzi, "Liwekeni darasa lenu safi kila siku."
  1. Mwalimu aliwaagiza wanafunzi wawe wakiliweka darasa lao safi kila siku.
  2. Mwalimu aliwaambia wanafunzi kuwa yeye hutaka darasa liwe safi kila siku.
  3. Mwalimu aliwaomba wanafunzi wawe wakilisafisha darasa lao kila siku.
  4. Mwalimu alisema kuwa angetaka wanafunzi wawe wakiliweka darasa lao safi siku hizo
 9. Kidani ni kwa shingo kama ilivyo ______________________ kidevuni.
  1. furungu
  2. kikuba
  3. utondoti
 10. Nomino zipi hupatikana katika ngeli wa YA-YA pekee?
  1. Manukato, mazingira
  2. Magari, maegesho
  3. Mate, mapato
  4. Mashaka, maembe
 11. Upi ni muungano sahihi wa sentensi ifuatayo?
  Mvua ilinyesha vizuri. Mavuno hayakuwa mengi.
  1. Mvua ilinyesha vizuri aghalabu mavuno hayakuwa mengi.
  2. Lau mvua ilinyesha vizuri mazao hayakuwa mengi.
  3. Mazao hayakuwa mengi almradi mvua ilinyesha vizuri.
  4. Mazao hayakuwa mengi licha ya mvua kunyesha vizuri.
 12. Ipi ni sifa iliyoundwa kutokana na nomino.
  1. dhoofu- dhaifu
  2. wema - jema
  3. refusha - urefu
  4. kimbia - kimbilio
 13. Ni sentensi ipi iliyo na kivumishi cha idadi.
  1. Wanafunzi wote watapewa vipakatalishi mwakani.
  2. Maswali mengine hayakuweza kujibika.
  3. Watalii huja hapa mara kwanmara.
  4. Tulipanda miti kadhaa msimu.
 14. Tunasema mrefu kama mlingoti na pia mwaminifu mithili ya
  1. jua
  2. malaika
  3. mchana
  4. kondoo
 15. Chagua jozi ya methali zenye maana sawa.
  1. Kuishi kwingi ni kuona mengi. 
  2. Moto wa kumvi hudumu.
  3. Ngoma ya wana haikeshi.
  4. Jungu kuu halikosi ukoko.
  5. Mwana wa kuku hafunzwi kuchakura.
   1. (ii), (iv)
   2. (i), (iii)
   3. (ii), (v)
   4. (i), (v)

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali kuanzia 31 mpaka 40

Mwendo wa saa mbili na ushei, lange la tarabe lilifunguliwa taratibu. Ni mara chache sana ambapo Mwapuza aliweza kuiona sehemu ya nje ya lango hilo. Awali, aliliona pale tu yeye na wafungwa wenzake walipopelekwa chini ya ulinzi mkali ama kunadhifisha sehemu za umma mjini au kushiriki shughuli nyinginezo kama walivyohitajika. Lango hili lilikuwa limemdhibiti kwa nusu mwongo sasa, japo kwa Mwapuza hii ni miongo mitano! Lakini leo, imesibu kuwa hauchi hauchi unakucha. Wake umekucha che! Na kumwangazia waa! Kwa nuru ya uhuru.

Kumbukumbu za Mwapuza zilimregesha katika siku zake za kisogoni, akakumbuka akiwa danga la mwana katika shule ya msingi ya Hekima. Wavyele wake walalahai walijikaza masombo mwana wao akapata hiki na kile, almradi aweze kujitegemea na kuwa taa ya jamaa na jamii iwapo yatakuwa majaliwa. Siku zote Mwapuza akawa akiahidi kuinamia cha mvunguni na kuibuka na mzo wa maarifa.

Mnamo mwaka wake wa saba katika shule ya msingi, Mwapuza alipatana na wasena watundu akanolewa akapata. Kufumba na kufumbua akajipata ameabiri dau la mihadarati. Kila uchao, wavyele wake walisikika wakilaani kuwa fulusi zao zilitoweka kimiujiza. Ambalo hawakujua ni kuwa njenje zao zilitumika kugharimia starche za mwana wao. Baadhi ya vitu vya thamani chengoni aidha vilianza kuota mbawa ́ kiajabuajabu.`

Baada ya kushauriana, wavycle walikata shauri la kutohifadhi ghawazi nyumbani. Waliafikiana kwa kauli moja kuwa benkini ndiko mikono mirefu isikofika kwa urahisi. Mwapuza alipohojiwa alikula mori na kuanza kuwafokea wazee wake. "Hivi mmenikosea thamani kiasi cha kuanza kuniita pwagu?" Akauliza kwa ukali. Hapo alilia hadi kifua chake kikalowa na kabisa kwa machozi. "Tazameni mlivyonitelekeza," akaendelea. "Hata masrufu hamnipi tena. Mbona mlinizaa kuja kunitesa," alisaili kwa uchungu.

Mama mtu alipojaribu kumtuliza mwanawe, alifunguliwa mfereji wa matusi akapigwa na mughma. Hakuamini masikio yake. "Huyu ni yule mwanangu niliyemzaa, nikamwamisha na kumchuchia alipolia hadi akatulia? Leo hii anathubutu kunivunjia heshima kiasi hiki? Ama kweli, ivushayo ni mbovu." Machozi yalimdondoka njia mbilimbili; machozi ya uchungu wa mwana ambao aujuaye ni mzazi.

Jioni iyo hiyo, Mwapuza aliwasimulia wasena wake masaibu yote yaliyomsibu. Wakamsikitikia sana. Papo hapo, walikula nyama ya kuguria mjini. Walipowasili huko, walitumia fulusi kichele walizokuwa nazo kununulia mihadarati na kushiriki anasa. * Walilosahau ni kuwa chovyachovya humaliza buyu la asali.

Pesa zilipotindika, waliamua kuingilia uhalifu ili kukidhi mahitaji yao. Awali, walivamia gereji moja na kuiba vipuri vya magari. Baadaye waliviuza kwa bei ya kutupa na kuendesha maisha yao. Ujanja wao uliishia jangwani usiku mmoja waliponaswa na polisi walioshika doria. Hawakuweza kueleza vizuri walikotoka usiku huo wala walikopata vipuri vya magari. Basi walinda usalama wakajijazia. Visa vya wizi wa vipuri vilikuwa vimeshamiri mjini humo.

Hatimaye Mwapuza na wenzake walifunguliwa mashtaka na kuhukumiwa. Mwapuza mwenyewe hakuona haja ya kukata rufaa. Ushahidi dhidi yake haukuwa na ati-ati. Wenzake walishindwa kuvumilia mateso gerezani wakasalimu amri. Mmoja wao aliugua na kutangulia mbele ya haki. Mwenzake naye alishiriki mapigano akaangamizwa na mfungwa mwenzake. Kwa Mwapuza, ilikuwa heri nusu ya shari kuliko shari kamili.

Wakati huu, Mwapuza aliona jambo moja tu. Alitaka kuwaona wavyele wake awaangukic miguuni na kulia kama mtoto mdogo. Alitamani afike kama yule mwana mpotevu na kuomba radhi kwao. Tayari machozi ya majonzi yalikuwa yakimdondoka ndo ndo ndo!

 1. Chagua jibu sahihi kwa mujibu wa aya ya kwanza.
  1. Aghalabu lango lilifunguliwa baada ya saa mbili.
  2. Haikuwa kawaida kwa Mwapuza kuwa huru nje ya lango. 
  3. Mwapuza alizoca kuenda kudumisha usafi mjini.
  4. Tofauti na awali, Mwapuza alijifungulia lango mwenyewe.
 2. Kulingana na makala, ni kweli kusema kuwa wazazi wa Mwapuza
  1. walichelea mwana kulia wakalia wao.
  2. walikuwa na uhitaji mkubwa wa kifedha.
  3. walikuwa watu wenye nafasi na hali katika jamii.
  4. walikuwa watu wa kima cha kati.
 3. Jambo linalodhihirisha kuwa wavyele wa Mwapuza ni wenye busara ni kwamba:
  1. wameamua kumwekea mwana wao msingi ufaao.
  2. walijinyima kila kitu wakampa mwanao mahitaji yote.
  3. hawataki kugombana na mwanao licha ya kupotoka.
  4. wanatarajia mwana wao awafae atakapohitimu masomo.
 4. Msemo, 'akanolewa akapata' kama ulivyotumika una maana ya
  1. akashauriwa na kukaidi. 
  2. akacrevushwa na kuerevuka.
  3. akarubuniwa na kupotoka.
  4. akahimizwa na kuzingatia.
 5. Chagua madhara ya mihadarati yaliyojitokeza katika kisa hiki.
  1. Madhara ya kiafya na kuingilia uhalifu.
  2. Kuwa mwizi na kutiwa nguvuni.
  3. Kupotosha maadili na kuingilia uhalifu.
  4. Kujiunga na marafiki na kuwaibia wazazi.
 6. Mwapuza alishiriki haya yote ila
  1. kujibizana na mamaye.
  2. kuyaasi masomo yake.
  3. kutoroka nyumbani.
  4. kumpiga mamaye.
 7. Kilichochangia kutiwa mbaroni kwa Mwapuza na wenzake hasa ni kuwa
  1. wizi wa vipuri ulikuwa umekithiri mjini.
  2. walipatikana na bidhaa zilizokuwa zikitafutwa.
  3. ilikuwa haramu kutembea na vipuri usiku.
  4. walionyesha mienendo ya kutiliwa shaka.
 8. Kwa nini Mwapuza hakukata rufaa?
  1. Hakuona uwezekano wa kushinda kesi.
  2. Alikuwa amekata tamaa kabisa maishani.
  3. Hakuwa na pesa za kuwasilisha rufaa.
  4. Hakuwa na maarifa kuhusu kesi yake.
 9. Kichwa kifaacho zaidi kwa makala haya ni
  1. Mui huwa mwema
  2. Majuto ni mjukuu.
  3. Siku za mwizi ni arubaini.
  4. Ivushayo ni mbovu.
 10. Masrufu kulingana na muktadha ni;
  1. pesa za kufidia masomo shuleni.
  2. fedha za matumizi ya kila siku.
  3. malipo ya kununulia vitu vya masomo.
  4. pesa za kununulia mihadarati.

Soma kifungu hiki kisha ujibu maswali kuanzia nambari 41 mpaka 50

Ugatuzi ni mfumo wa kiutawala ambapo baadhi ya mamlaka huhawilishwa kutoka kwa serikali kuu hadi kwenye maeneo mengine kama magatuzi au majimbo. Nchini. Kenya, mfumo huu ulianza kutekelezwa wakati katiba ya mwaka wa elfu mbili na kumi ilipoanza kutekelezwa. Tangu kuanzishwa kwake, mfumo huu umekuwa na manufaa tele. Hata hivyo, kuna changamoto ambazo zimeukumba. La kutia moyo ni kuwa manufaa yake yamezipiku.

Kwanza, ugatuzi umchakikisha kuwa kuna ugavi sawa wa rasilimali za umma. Ilali. hii imetokana na ukweli kuwa kila jimbo hutengewa kiasi fulani cha fulusi za maendeleo. Hii ni kinyume na ilivyokuwa hapo awali, ambapo baadhi ya maeneo yaliendelea kunawiri kimaendeleo huku wengine yakidorora. Tumeshuhudia miradi ya miundombinu ikiendelezwa katika sehemu mbalimbali za magatuzi zilizokuwa zimetengwa kimaendeleo.

Pia, ugatuzi umeleta ushindani chanya baina ya majimbo; hivyo kuharakisha maendeleo. Jambo hili limetokana na hofu ya baadhi ya magavana kushindwa kimaendeleo. na wenzao. Wengi wao humotishika kutekeleza miradi mbalimbali ili kutimiza ahadi kwa raia waliowachagua ili waweze kuchaguliwa tena. Viwanda mbalimbali kama vile vya maziwa, vya majani chai na hata vya maembe vimeanzishwa katika baadhi ya kaunti. Hii imeimarisha uchumi wa majimbo haya.

Isitoshe, nafasi za kazi zimeweza kubuniwa kutokana na mfumo wa ugatuzi. Si jambo la mjadala kusema kuwa kuna watu wengi walioajiriwa kufanya kazi katika afisi mbalimbali za kaunti na hata viwandani. Wengi wameweza kuyakidhi mahitaji ya kila siku huku maisha yao yakiboreka. Kutokana na hali hii, kiwango cha uhalifu kimepungua Baadhi ya vijana waliokuwa wametamauka hapo awali wamepata matumaini maishani baada ya kupata kazi katika serikali hizi.

Vilevile, huduma za serikali kwa wananchi zimeletwa karibu nao. Ukweli ni kuwa hapo awali, baadhi ya wananchi walihitajika kusafiri mbali kama vile hadi Nairobi kw lengo la kuhudumiwa. Wengi walikuwa wakichelewa, hivyo kuyafanya mambo yao kuenda mvange baada ya kukosa huduma walizohitaji. Hivi leo mambo ni tofauti madhali huduma nyingi wanazohitaji zinapatikana majimboni. Hili linasababisha uokoaji wa muda ambapo huweza kutumia muda wao kutekeleza kazi za kimaendeleo.

Zaidi ya hayo, climu imeboreshwa pale ambapo baadhi ya ujenzi wa shule umefadhiliwa na serikali za kaunti. Watoto wengi wameweza kujiunga na shule na kupat elimu. Nafasi za ajira kwa walimu wanaopata kazi katika shule mpya zinazoanzishwit wamenufaika pakubwa. Hapo awali, watoto katika maeneo yaliyokosa shule waliscleic kwenye mwina wa urumo bila matumaini ya nyota yao kung'aa maishani.

Kwa kuwa hakuna masika yasiyokuwa na mbu, serikali za kaunti zimekumbwa n changamoto mbalimbali. Ukabila ni tatizo mojawapo ambalo limezivamia serikali hizi.. Baadhi ya magavana wamekuwa wakiwaajiri watu kutoka kaunti zao pekee. Wengine wamekuwa wakipendekeza asilimia kubwa ya nafasi za kazi zipewe watu kutoka majimbo yao. Hali hii inahatarisha utangamano nchini. Kutokana na serikali za magatuzi, ufisadi umeshamiri. Pamekuwa na visa vingi vinavyoripotiwa ambapo baadhi ya watumishi wa kaunti wamekuwa wakibadhiri mali ya umma, Hali hii imedumaza maendeleo katika majimbo kama haya.

Licha ya serikali za ugatuzi kukumbwa na changamoto, ni ukweli kuwa zina manufaa tele. Kwa kuwa umoja ni nguvu utengano ni udhaifu, viongozi wa majimbo pamoja na wananchi wanafaa kushirikiana kupambana na changamoto hizi. Hili likitekelezwa, serikali hizi zitaendelea kuwafaa wananchi. Majimbo husika yatapiga hatua kubwa za kimaendeleo na kuboresha maisha ya wananchi.

 1. Ni nini maana ya ugatuzi kulingana na kifungu?
  1. Kuhawilisha mamlaka kutoka scrikali moja hadi nyingine.
  2. Kuhamisha baadhi ya mamlaka kutoka serikali kuu hadi serikali za majimbo.
  3. Kuhawilisha majukumu ya serikali za ugatuzi hadi kwenye serikali kuu. 
  4. Kuhamisha baadhi ya majukumu ya serikali za magatuzi au majimbo. 
 2. Kenya ilianza kutekeleza mfumo wa ugatuzi lini?
  1. Mwaka wa elfu mbili na mbili.
  2. Kabla ya mwaka wa elfu mbili na mbili.
  3. Wakati katiba mpya ya Kenya ilipokuwa ikipitishwa.
  4. Katika mwaka wa elfu mbili na mbili ilipoanza kutekelezwa.
 3. Si kweli kusema kuwa, mfumo wa ugatuzi una
  1. manufaa pekee.
  2. faida na madhara.
  3. manufaa tele.
  4. changamoto zake.
 4. Kulingana na aya ya pili,
  1. mfumo wa ugatuzi umeimarisha usawa wa kimaeneo.
  2. ugatuzi umesaidia baadhi ya maeneo kuendelea kuliko mengine.
  3. awali, miundombinu ilikuwa imepuuzwa na serikali.
  4. hakuna eneo lililoendelea kuliko jingine chini ya mfumo wa ugatuzi.
 5. Maoni ya mwandishi ni kuwa;
  1. ushindani ni adui wa maendeleo.
  2. bila ushindani maeneo hayawezi kujiendeleza
  3. ushindani ukitumiwa vizuri unaweza kuharakisha ustawi.
  4. ushindani nzuri unaweza kuathiri maendeleo kwa njia hasi.
 6. Uchumi wa majimbo utaimarishwa zaidi na;
  1. kuzinduliwa njia mpya za uzalishaji.
  2. migao inayotolewa mara kwa mara.
  3. mikopo kutoka mataifa ya kigeni. 
  4. juhudi za viongozi za kutaka wachaguliwe tena.
 7. Kifungu kimedokeza kuwa uhalifu huchangiwa na;
  1. kupuuzwa kwa maeneo mengi na serikali.
  2. kukosa namna ya kujikimu kimaisha.
  3. ukosefu wa utawala madhubuti katika taifa.
  4. kutokuwepo kwa viwanda katika . maeneo.
 8. Huduma zikiletwa karibu na wananchi,
  1. watakuwa na muda wa kupumzika kwani hawaendi popote.
  2. watahudumiwa kwa wingi na wahudumu wachache.
  3. watapata huduma zenyewe bila gharama yoyote.
  4. watapata muda zaidi wa kufanya shughuli za ujenzi wa taifa.
 9. Ni kweli kuwa hakuna masika yasiyokuwa na mbu maadamu ugatuzi,
  1. umeimarisha miundomsingi shuleni, umeongeza maendeleo mashinani.
  2. umeleta tatizo la ukabila, umesababisha ubadhirifu wa mali ya umma.
  3. umerahisisha utoaji huduma, unavuruga umoja wa kitaifa. 
  4. umeongeza nafasi za kazi, umesababisha kubaguliwa kwa wenyeji wa magatuzi.
 10. Kulingana na aya ya mwisho;
  1. changamoto za ugatuzi ni manufaa kwa wananchi.
  2. kufanikiwa kwa ugatuzi .kunategemea ushirikiano wa watawala na watawaliwa.
  3. ufisadi umedumaza maendeleo katika baadhi ya maeneo.
  4. si vizuri kutoa nafasi za kazi kwa watu wa maeneo mengine.

INSHA

Umepewa dakika 40 kuandika insha yako. Endeleza insha ifuatayo kwa * maneno yako mwenyewe huku ukiifanya iwe ya kusisimua zaidi.

Tulikuwa tumeisubiri ziara hiyo kwa hamu na ghamu. Asubuhi ilipofika.....................

MARKING SCHEME

 1. B
 2. A
 3. C
 4. C
 5. D
 6. B
 7. C
 8. A
 9. A
 10. D
 11. C
 12. B
 13. A
 14. C
 15. C
 16. A
 17. C
 18. A
 19. B
 20. A
 21. D
 22. C
 23. A
 24. D
 25. B
 26. D
 27. B
 28. D
 29. C
 30. A
 31. B
 32. D
 33. A
 34. C
 35. C
 36. D
 37. D
 38. A
 39. B
 40. B
 41. B
 42. D
 43. A
 44. A
 45. C
 46. A
 47. B
 48. D
 49. C
 50. B
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - KCPE 2023 Prediction Papers Set 2.


Tap Here to Download for 30/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students