Monday, 10 July 2023 13:50

Kiswahili Questions and Answers - Class 8 Mid Term 2 Exams 2023 Set 2

Share via Whatsapp

Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne hapo. Chagua jibu lifealo zaidi kati ya yale aliyopewa.

Lugha ya Kiswahili hutumika __1__ waafrika __2__ wakoloni. Jukumu la lugha __3__ ile kama wenzo wa mawasiliano__4__kupuuzwa. __5__kila kabila huwa na lugha yake ambayo __6__ kitamaduni na kimila.

   A   B   C   D 
 1.    kuwatambulisha na kuwaunganisha   kuwahamasisha na kuwalinganisha   kuwadumisha na kuwajenga   kuwastawisha na kulenga 
 2.  juu ya  dhidi ya  kando na   kando ya 
 3.  zozote  lolote   yoyote   chochote 
 4.  haiwezi  hauwezi   hayawezi   haliwezi 
 5.  Aghalabu  Lau  Angalau  Ingawa 
 6.  hulitambulisha  huitambulisha  huwatambulisha  hututambulisha 

 

Ni muhimu kufahamu kuwa kiini cha lugha ya Kiswahili ni sauti. __7__ sauti hizi ni zile zinazotetemesha nyuzi za koromea yaani __8__ Mfano wa sauti hizi ni __9__.  __10__. kuna lugha nyingi __11__ulimwenguni, lengo kuu hasa huwa ni __12__ mawasiliano kwa namna __13__. Kila jamii inafaa __14__ lugha yake bila kuiona fedheha maadamu __15__.

   A   B   C   D 
 7.   Katikati ya   Miongoni mwa   Baina ya   Mojawapo ya 
 8.  sighuna  mwambatano   ghuna   changamano 
 9.  b,d,g,z  ch,h,s,tu   f,p,sh,e   w,y,sh,f,h 
 10.   Aidha  Minghairi ya hayo   Ijapokuwa   Waama
 11.  mote  pote   kote   kwote 
 12.  kuyafaulisha   kutufaulisha  kuyatosheleza   kututoshelezea 
 13.  yafaayo  ifaavyo   ifaayo   yafaavyo 
 14.  kuzithamini  kuzidhamini  kuithamini  kuidhamini
 15. mzigo u kichwani, kwapa lakutokeani jasho  mwacha kiwi hanacho na chema kimpotelee  mwacha mila ni mtumwa  bura yangu sibadili na rehani

 

Kutoka swali la 16 mpaka 30, chagua jibu sahihi.

 1. Chagua sentensi iliyo sahihi kimantiki.
  1. Pale mlipoketi pana unyevu.
  2. Kule mlikoketi mna unyevu.
  3. Mle mlipoketi mna unyevu.
  4. Kule mlimoketi kuna unyevu.
 2. Tambua viambishi vya neno 'walipelekana'
  1. wa-li-pe-le-ka-na
  2. wa-li-a-na
  3. pe-le-ka-na
  4. wa-li-pe-le-k
 3. Chagua sentensi yenye -ni- ya wingi.
  1. Wao ni wanafunzi watiifu.
  2. Majoka yale yalijificha.
  3. Yatunzeni mazingira yenu ipasavyo
  4. Mliponielekeza njia nilifurahi sana.
 4. Kanusha sentensi ifuatayo:
  Utafiti uliofanywa uliridhisha wachache
  1. Utafiti usiofanywa haukuridhisha wachache.
  2. Utafiti uliofanywa uliridhisha wengi.
  3. Utafiti uliofanywa haukuridhisha wachache.
  4. Utafiti usiofanywa hauridhishi wengi.
 5. Chagua methali yenye maana sawa na hii:
  Mzigo wa mwenzio ni kanda la usufi.
  1. Usitukane wakunga na uzazi ungalipo.
  2. Bura yangu siibadili na rehani.
  3. Zigo la kuliwa halilemei.
  4. Maji ya kifuu ni bahari ya chungu.
 6. Ni sentensi ipi inayoonyesha kusudi la tendo.
  1. Suna aliingia zizini akawafungulia ng'ombe akaelekea malishoni.
  2. Malikia alituambia twende tukavue samaki.
  3. Wafanyakazi walifanya bidii wakamaliza kazi hiyo.
  4. Wageni watakuja watakapokamilisha shughuli.
 7. Chagua jibu lenye maelezo sahihi.
  1. Surua ni ugonjwa wa watoto unaosababishwa na majipu mwilini.
  2. Ukoma ni ugonjwa wa kukatika kwa viungo vya mwili.
  3. Pumu ni ugonjwa wa mapafu unaosababisha kukohoa damu.
  4. Machapwi ni ugonjwa wa kutoa damu na kuvimba fizi.
 8. Chagua usemi halisi wa sentensi hii:
  Kamaliza alisema kwamba wangeenda kuogelea siku ambayo ingefuata.
  1. "Tutaenda kuogelea kesho,” Kamaliza alisema.
  2. "Mtaenda kuogelea siku inayofuata," Kamaliza alisema.
  3. " Nimeenda kuogelea kesho,” Kamaliza alisema.
  4. ' utaenda kuogelea siku inayofuata,” Kamaliza alisema
 9. Komba ni mnyama mdogo jamii ya kima anayelialia wakati wa usiku. Komba aidha ni 
  1. chakula maalum anachokula bwana harusi.
  2. kukusanya vitu na kuviweka mahali pamoja.
  3. kitu kilicho na kina kidogo kama vile
  4. chombo cha miyua, ngozi au kamba kinachotumiwa kurushia mawe.
 10. Chagua wingi wa sentensi ifuatayo:
  Mtume alisimama karibu na ua wa nyumba hiyo.
  1. Mitume walisimama karibu na nyua za nyumba hizo.
  2. Watume walisimama karibu na maua ya nyumba hizo.
  3. Mitume ilisimama karibu na maua ya nyumba hizo.
  4. Watume walisimama karibu na nyua za nyumba hizo.
 11.  Chagua sentensi iliyounganisha sentensi zifuatazo ifaavyo:
  1. Timu yetu ilicheza vizuri.
  2. Hatukushinda mechi hiyo.
   1. Hatukushinda mechi hiyo kwani timu yetu ilikuwa imejiandaa vizuri.
   2. Ingawa timu yetu ilikuwa imejiandaa vizuri hatukushinda mechi hiyo.
   3. Aidha timu yetu ilikuwa imejiandaa vizuri hatukushinda mechi hiyo.
   4. Hatukushinda mechi hiyo maadamu timu yetu ilikuwa imejiandaa vizuri.
 12. Yapi si matumizi ya alama ya mshazari
  1. Kuonyesha neno lenye maana sawa au kuonyesha 'ama'
  2. Kuandika tarehe.
  3. Kutenganisha shilingi na senti
  4. Kuonyesha maneno au maelezo yasiyokuwa ya lazima. 
 13. Ainisha maneno yaliyoangaziwa katika sentensi hii.
  Mwanafunzi hodari ametuzwa tena.
  1. Kielezi, kiwakilishi
  2. Kivumishi, kielezi
  3. Kitenzi, kiwakilishi
  4. Kiunganishi, kielezi
 14. Tegua kitendawili kifuatacho:
  Nimemwona bikizee amejitwika machicha.
  1. Upango wa jogoo
  2. Nyota angani
  3. Mvi
  4. Chawa
 15. Sentensi ifuatayo itaandikwaje katika kauli ya kutendewa? Farida aliandika barua akamtumia Rukia.
  1. Farida alimtumia Rukia barua aiyoandika
  2. Rukia alitumiwa barua aliyoandikiwa na Farida
  3. Farida aliandikiwa barua na Rukia akatumiwa.
  4. Barua iliandikwa na Farida na kutumwa kwa Rukia.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 31 mpaka 40.

Naikumbuka siku hiyo vizuri. Niliamka alambichtayari kuanza safari kutoka kijijini mwetu hadi mji mkuu. Hii ndiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kuzuru mji huu. Moyoni nilikuwa na furaha isiyokuwa na kifani maadam siku hiyo ningeuona mji ambao sifa zake nilikuwa nikizisikia tu kutoka kwa wenzangu waliobahatika kuutembelea. Hamu ya kuona majengo marefu, barabara zilizosakifiwa, magari mengi, watu wa asili mbalimbali na bustani za starehe ilinigubika, nikawa sijifai kwa matumaini.

Mjini aliishi rafiki yangu kwa jina pendo. Basi baada ya kuamka niliweza kumkumbusha mama kuhusu ziara ya kumtembelea rafiki yangu aliyekuwa ameandaa sherehe ya kuzaliwa kwake. Mwenyewe nilikuwa nimepata mwaliko wa kushiriki katika karamu ya kuadhimisha mwaliko wa kushiriki katika karamu ya kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa. Kawaida yangu niliamini kuwa safari ya kesho hupangwa leo. Hivyo basi niliweza kumwarifu mama mapema japo matumaini yangu hayakuwa makubwa kwa sababu mama hakumpenda Pendo asilani. Haya yote yalisababishwa na ukweli kwamba Pendo alitoka katika familia tajiri. Kulingana na mama, watoto matajiri kutokana na kudekezwa, waliishia kuwa watovu wa nidhamu.

Msimamo wa mama asubuhi hiyo ulikuwa ule ule usiotetereka. Hakutaka kamwe nijihusishe na Pendo. Hapo aliweza kunitaka kuvuta taswira niuone usuli wangu wa umaskini ulionifanya kama muwele wa ukoma. Ukosefu wa karo ulikuwa ukinitishia kuniambia kuwa muda wangu wa masomo ulikuwa umekwisha. Mama aliendelea kunisimanga akinikumbusha jinsi alivyochumia juani kunilisha mimi. Alinitapikia yote yaliyokuwa moyoni mwake na kulitua zigo lake la siku nyingi. Mawazo yaliendelea kunijia nikajipata nikilia kwa kite na shake. Kwikwikwi zangu za kilio zikahanikiza chumbani mote. Ghafla nikajipata na ujasiri wa Simba. Nilimkabili mama na kumwambia kuwa ningehudhuria haramu ya Pendo na liwe liwalo. Hapo ndipo mama alinikumbusha kuwa asiyesikia la mkuu huabiri mtumbwi wa mfinyanzi. Hata hivyo maaso haya yote yaliangukia masikio yaliyotiwa tomo.
yangu

Kwa kufuata kauli yangu nilianza kujitayarisha kuhudhuria karamu ya Pendo. Kutokana na ukaidi wangu mama alinikodolea macho kana kwamba hakuwahi kuniona nami nikazidi kujipodoa. Akajaribu kunikataza lakini alikuwa akimpigia mbuzi gitaa. Kuna wale husema siku njema huonekana asubuhi nayo hiyo iliharibiwa na mama. Aidha mkesha wa siku hiyo ulishuhudia milio mingi ya bundi hivyo basi kunitia shaka na shauku. Nikaanza kujisemea kimoyomoyo huku nikinyambua nyayo zangu kuelekea kwenye kituo cha basi. “Hivi ni lazima nihudhurie hii? Huu mlio wa bundi una maana gani? Lakini potelea mbali, na liwe liwalo. Lazima nihudhurie.

Baada ya kujisuta moyoni, niliondoka na kuelekea kwenye kituo cha magari. Likaja basi moja ambalo lilisheheni abiria kupindukia. Nilijisukuma ndani na basi likaanza mwendo. Nikajipata nimening'inia kibavuni pa basi huku nikibinywa na abiria wenzangu. Gari nalo likazidisha mwendo nikaanza kujisuta na kujiuliza ni kwa nini niliingia katika basi hilo. Hapo wazo la kushuka likanijia ili niabiri jingine lakini ujasiri wangu ukanipa kufikiri kuwa kwa shujaa huenda kilio na kwa mwoga huenda kicheko. Lakini kushuka kwangu kungenifanya nionekane limbukeni. Nikiwa katika wazo hilo basi hiliingia katika mtaa wa akina Pendo. Hapo nilitia mkono kibindoni na kumkabidhi utingo nauli yangu Hatimaye basi lilitia nanga na hapo nikashusha pumzi na kushuka. Mimi sikutaka kudekeza hisia za wengi kuwa bundi ni ishara ya mkosi.

Nilipiga masia hadi nyumban pa akina Pendo. Huko sherehe za kila nui ndizo ziliwaongoza wote hata waliokuwa na akili razini. Nani nikajiona nikiumezea mate uhondo niliouona. Walikuja wasena wengi, maghulamu kwa mabanati wengi nisiowajua. Tukaanza kujiburudisha kwa kila aina ya muziki, ya kufokafoka na mengineyo. Vinywaji navyo vikaletwa vile vikali na visivyo vikali. Walio wazoefu wa kunywa vile vikali wakajituma karamuni bila kujali. Nami kwa kuhofia kuonekana limbukeni nikajiingiza katika kumbo hilo. Nikaanza kushiriki ugimbi huo ili kusahau kero za mama. Nikamimina chupa ya kwanza, ya pili na hata ya tatu. Hapo nikajiona nikielea hewani. Nilihisi vyema sana.

Baada ya muda fulani, usiku ukaufumbata ulimwengu nazo sherehe zikaanza kunoga zaidi. Tukawa tunakula na kusakata ngoma bila kujali mpito wa wakati. Kutahamaki nikajipata nikikabiliana na kiza cha usiku wa manane. Magari ya abiria hayakuwa hivyo basi hatukuwa na jingine ila kuabiri gari la akina Pendo. Pendo akawa ndiye dereva wa gari hilo licha ya kuwa alikuwa akitawaliwa na kinywaji. Hata hivyo hatukuwa na jingine la kufanya ila kuridhika na usafiri uliopatikana. Hapo tulijitoma garini tukiwa wanane. Katika hali yetu hakuna aliyefikiria kufunga mikanda ya usalama. Gari likaanza kuserereka kwa kasi. Mara, Lo! Gari letu likakosa kujipinda kwenye kuruba. Hapo ndipo niliona dari la gari letu, miguu ya wenzangu juu ya dari hilo huku wingu kubwa la moshi likipaa juu. Hatimaye kiza cha kaniki kikatanda.

 1. Kulingana na aya ya kwanza
  1. wenzake msimulizi waliwahi kupata fursa ya kuishi katika mji mkuu.
  2. barabara za mji mkuu hazikuwa na mashimo.
  3. mji mkuu una majumba mengi na marefu.
  4. msimulizi ana mwao na hali ilivyo katika mji mkuu.
 2. Kulingana na aya ya pili
  1. mwanzoni mama alikuwa amempa msimulizi ruhusa.
  2. mama wa msimulizi hakumruhusu kutangamana na vijana wenzake.
  3. mama yake msimulizi alikuwa mwenye ubaguzi wa kitabaka.
  4. msimulizi hakumtarajia mama yake kumkatalia katika ombi lake
 3. Ni wazi kuwa
  1. msimulizi alisomeshwa kwa taabu kutokana na umaskini wa familia yao. 
  2. msimulizi hakumaliza masomo yake kutokana na umaskini wa hali ya juu.
  3. msimulizi alisomea katika shule za kifahari alikosomea Pendo.
  4. urafiki wa Pendo na msimulizi ulichipuka walipokuwa katika shule ya upili.
 4. Kibindoni ni
  1. mfuko mdogo ndani ya suruali.
  2. mfuko mdogo mbele ya suruali
  3. mkunjo wa nguo uliyoshonwa kiunoni.
  4. mkunjo wa nguo uliofungy
 5. Taja tamathali mbili za lugha zinazojitok katika kauli hii.
  Huko sherehe za kila nui ndizo zilizowaongoza wote hata waliokuwa na akili razini.
  1. Kinaya, semi
  2. Tashhisi, nahau
  3. Chuku, nahau
  4. Uhuishi, ishara
 6. Kwa nini msimulizi alitumia vinywaji vikali japo hakuvizoea?
  1. Alitaka kusahau kero alizokuwa amepata asubuhi kutoka kwa mama yake.
  2. Alitaka hiyo iwe siku yake ya kwanza kuonja kinywaji kikali.
  3. Alichelea kuonekana duni na wanarika wenzake.
  4. Alichelea kuondolewa kundini na wenzake.
 7. Kwa nini msimulizi wa wenzake waliamua" kutumia gari la wazazi wa Pendo?
  1. Magari ya uchukuzi hayakupitia katika mitaa ya mabwanyenye.
  2. Kupita kwa wakati kulifanya magari yakosekane mtaani humo.
  3. Ulevi wao uliwafanya washindwe kufika kituoni.
  4. Wenyeji wao waliwaomba watumie gari hilo badala ya usafiri wa umma.
 8. Alipofika karamuni, mwandishi aliwapata
  1. wake kwa waume.
  2. marafiki zake.
  3. vijana wa kike na kiume.
  4. pendo, vijana na wazazi wao.
 9. Ni methali pani mwafaka kuelezea jumla ya mbe kauli hii?
  Hata hivyo hatukuwa na jingine la kufanya la kuridhika na usafiri uliopatikana.
  1. Akosaye la mama hata la mbwa huamwa. 
  2. Msafiri ni aliye pwani.
  3. Ajiingizaye kwa yasiyomhusu hupata yasiyo mridhi.
  4. Cha mlevi huliwa na mgema.
 10. Hatimaye kiza cha kaniki kikatanda. Yaani
  1. kukawa na giza totoro.
  2. kukawa na weusi mkubwa.
  3. msimulizi akapoteza uwezo wa kuona.
  4. msimulizi akapoteza fahamu.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 41 mpaka 50

Somo la Historia hujikita sana katika uwezo wa mtu kukumbuka. Leo hii kuna wale hutusimulia yaliyotukia wakati wa ukombozi na taifa letu. Si ati hawa hawajui wanachosema. Kile wanachosema ni kutokana na uwezo wao wa kukumbuka. Uwezo huu umeweza kudhibitiwa na mambo anuwai. Uwezo huu si wa binadamu pekee. Hata wanyama hukumbuka mengi yaliyotokea awali.

Nao uwezo wa kuyakumbuka mambo ni hazina kwa mtu yeyote yule aliye hai. Uwezo huu ni mojawapo ya shughuli changamano za ubongo. Shughuli hii hutekelezwa ubongoni kwa namna tatu. Kwanza ubongo wenyewe hunasa jambo kisha hulihifadhi. Baadaye huanzisha mfumo wa kutoa kilichohifadhiwa ubongoni humo. Ubongo ukiathirika kwa namna yeyote katika njia hizi, basi uwezo wa kuyakumbuka mambo huvurugika vururu vururu.

Ukweli unaoaminika ni kuwa uwezo huu hurithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Hata hivyo wataalamu wa masuala ya kiakili wanabaini kwamba uwezo huu unaweza kuimarishwa. Uimarishaji huu huhitajika mikakati madhubuti. Hii ni kwa sababu kwa kawaida jambo haliwezi kufanyika au kufanikiwa bila ya kuwepo kwa vitu fulani au taratibu zifaazó kulifanyia.

Njia mojawapo ya kustawisha uwezo wa kukumbuka ni kupitia kwa lishe. Vyakula vilivyosheheni vitamini B vyenye Amino Asidi ni muhimu sana. Mifano ya vyakula hivi ni mboga, nyama, (hasa maini), bidhaa za soya, matunda, maziwa, ngano, samaki na mayai. Vyakula vingine muhimu katika ustawishaji huu ni vile vyenye madini ya chuma. Haya huwezesha usambazaji wa hewa katika ubongo wa wepesi. Vyakula ambavyo vina madini haya ni mboga za kijani, mawele, ndengu, soya, matunda kama maembe, ufuta (simsim), nyama hasa maini na mayai. Ukizingatia haya unakuwa na uwezo wa kukumbuka hata yaliyofanyika kabla ya wewe kuzaliwa

Ubongo wa adinasi aliye hai hufanya kazi wakati wote, awe macho au awe amelala. Utendaji kazi wake huendeshwa na glukozi mwilini. Kwa hivyo, vyakula vyenye aina hii ya sukari ni muhimu kuliwa. Hata hivyo, lazima mtu awe mwangalifu kuhakikisha kuwa mwili una kiwango cha sukari kisichohatarisha maisha. Haya yanawezekana kwa kula vyakula vyenye nyuzinyuzi kama vile mboga na matunda.

Vileo navyo vyafaa kupigwa marafuku mathalani nikotini na pombe. Hii ni kwa sababu vileo hivi huathiri utaratibu wa kunasa, kuhifadhi na kutoa yaliyo ubongoni. Mtu hujipata amesahau hata yale hakujua.

Iwapo mtu ana matatizo ya kuyakumbuka majina ya watu, ni vyema kufanya mazoezi ya kusikiliza kisha kurudia majina haya wakati wa mazungumzo. Ni bora kulihusisha jina na sura ya mtu. Kwa njia hii ubongo utanasa jina na kile kinacholengwa.

Woga na kuvurugika kiakili ni mambo mengine tunayopaswa kuepuka kila wakati. Ni kawaida mtu kupata woga anapokabili jambo asilokuwa na uhakika na mahojiano. Lakini anapaswa kuwa makini. Woga huo usikiuke mipaka na kumvuruga kiakili. Vurugu hizi huathiri kilichohifadhiwa ubongoni na pia namna ya kukitoa.

Aidha mwili wenye rai njema huhakikisha kuwa ubongo ni timamu. Wataalamu wengi wa afya wanakubali kuwa mazoezi ya kunyosha viungo hustawisha ubongo na hivyo kuhakikisha kuwepo kwa uwezo wa kukumbuka mambo. Ni muhimu kuwa na utaratibu wa kunyoosha viungo kila wakati. Fauka ya hayo, mazoezi ya kiakili kama vile kusoma makala yanayovutia, kujaza mraba na michezo mingine kama mafumbo na vitanzandimi ni muhimu katika kustawisha uwezo huu.

Jamii yenye uwezo wa kuyakumbuka mambo hupiga hatua kubwa kimaendeleo. Ni jukumu la kila mmoja wetu kuandama sera za kuimarisha uwezo wa kukumbuka kila wakati. Yeyote ambaye atakiuka sera hizi, lawama zote zafaa kumrudia yeye

 1. Kulingana na aya ya kwanza, umeweza kudhibitiwa" ina maana gani?
  1. Umeweza kuondolewa.
  2. Umeweza kuzuiliwa.
  3. Umeweza kutibiwa wote.
  4. Umeweza kupunguzwa wote.
 2. Aya ya pili imeonyesha wazi kuwa 
  1. mtu yeyote ana uwezo wa kuyakumbuka mambo.
  2. uwezo wa kukumbuka unaweza kuwepo hata bila uhai.
  3. si lazima mtu awe na uwezo mzuri wa kukumbuka
  4. kuyakumbuka mambo huhusisha ungo vyote mwilini.
 3. Kwa mujibu wa aya ya tatu
  1. uwezo wa kukumbuka mambo ni jambo la kujifunza.
  2. mtu hawezi kuathiri uwezo wake wa kukumbuka.
  3. watu huzaliwa na uwezo sawa wa kukumbuka ila wengine hujiimarisha.
  4. uwezo wa kukumbuka hutegemea sana maumbile ya mtu. 
 4. Ni kundi lipi la vyakula vinavyoimarisha uwezo wa kukumbuka?
  1. Asidi, nyama na mboga.
  2. Mboga, sukari na mayai.
  3. Maini, ngano na mayai.
  4. Soya, matunda na vileo.
 5. Kulingana na aya ya tano, mtu anapolala
  1. uwezo wake wa kukumbuka huimarika.
  2. ubongo wake huendelea kufanya kazi.
  3. ubongo wake huacha kazi ili kupumzika.
  4. bado unaelewa kila jambo linalotokea.
 6. Yapi ndiyo manufaa ya nyuzinyuzi zinazopatikana katika mboga na matunda? 
  1. Zinatoa sukari ya kuendesha shughuli mwilini.
  2. Hupatia mwili madini muhimu ya chuma. 
  3. Huwezesha usambazaji mzuri wa hewa mwilini.
  4. Huchangia kudhibiti kiwango cha sukari mwilini.
 7. Athari za kutumia vileo kwa wingi ni
  1. kuimarisha uwezo wa mtu wa kukumbuka.
  2. hudhoofisha utendakazi wa ubongo.
  3. hunyima mwili viwango vifaavyo vya Sukarı
  4. humnyima mtu hamu ya kujikumbusha mambo.
 8. Hii ni tamathali gani ya lugha?
  Mtu hujipata amesahau hata yale hakujua.
  1. Chuku
  2. Kinaya
  3. Ishara
  4. Tabaini
 9. Rai kulingana na kifungu ni
  1. kusema na mtu kwa maneno mazuri.
  2. kutia mtu chakula mdomoni.
  3. maoni ya mtu juu ya jambo fulani.
  4. hali ya mwili kuwa na afya nzuri.
 10. Chagua methali inayoweza kujumuisha ujumbe wa kauli hii:
  Uimarishaji huu huhitaji mikakati madhubuti. Hii ni kwa sababu kwa kawaida jambo haliwezi kufanyika au kufanikiwa bila ya kuwepo kwa vitu fulani au taratibu zifaazo kulifanyia.
  1. Mti huchongewa ni tundaze.
  2. Mti upigwao mawe ni wenye matunda.
  3. Mti ukupigwao ndio ukufunzao.
  4. Mti hauendi ila kwa nyenzo.

INSHA

Umepewa dakika 40 kuandika insha yako.

Andika insha itakayoanzia kwa maneno yafuatayo:

Nilipomtazama, niliamini kuwa uzembe hauna manufaa ....................................................\

MARKING SCHEME

 1. A
 2. B
 3. C
 4. D
 5. A
 6. A
 7. D
 8. C
 9. A
 10. A
 11. C
 12. A
 13. C
 14. C
 15. D
 16. A
 17. B
 18. C
 19. B
 20. D
 21. B
 22. B
 23. A
 24. A
 25. A
 26. B
 27. D
 28. B
 29. C
 30. B
 31. D
 32. C
 33. A
 34. D
 35. B
 36. C
 37. B
 38. C
 39. A
 40. D
 41. B
 42. A
 43. C
 44. C
 45. B
 46. D
 47. B
 48. A
 49. D
 50. D
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Class 8 Mid Term 2 Exams 2023 Set 2.


Tap Here to Download for 30/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students