Tuesday, 30 August 2022 06:52

Kiswahili Questions and Answers - KCPE 2022 Prediction Papers Set 1

Share via Whatsapp

Maswali

Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi umepewa mujibu manne hapo. Jaza pengo kwa kuchagua jawabu lifaalo zaidi.

Ni vigumu kwa jamii yoyote kupiga hatua      1      kuwawekea vijana msingi      2     wa malezi. na afya, yaani     3   ,watoto hupewa chanjo ya kuzuia maradhi ya     4      Njia nyingine ni kuanzisha vyuo vya kiufundi vitakavyowapa     5     za kujiendeleza.     6      , utoaji wa elimu bila malipo      7     fursa ya kusomea taaluma mbalimbali pamoja na     8     vipawa vyao. Jamii     9     watambua vijana huwa haina matarajio mema ya uongozi wa baadaye.

  A B C D
1 minghairi ya licha ya  mithili ya fauka ya
2 nzuri mbora jema thabiti
3 staha rai ari hulka
4 malaria, pumu, waba kichocho, tauni, kifafa pepopunda, surua, kupooza mafua, malaria, ukambi
5 stadi maarifa ujuzi hekima
6 Ama Lau Ilhali Halikadhalika
7 inawapa kumewapa  umewapa tunawapa
8 kuyakuza kurikuza kuikuza kuwakuza
9 wakikoza mkikosa likikosa ikikosa


Moyo wa Amina ulijaa     10    Machozi yalijikusanya kwenye macho yake     11    matone makubwa makubwa na     12     daftari alilokuwa akiliandikia. Hata hakutanabahi mwalimu    13      na kusimama mbele yake. Mwalimu akamwita ofisini kumsaili na kumliwaza. Kumbe wavyele wake walikuwa      14    ya kumwoza! Ndipo mwalimu akamtafutia mhisani wa kuyadhamini masomo yake, Ama kweli    15   

  A B C D
10 machozi simanzi nyemi ukiwa 
11 yakamdondoka yakamchuruzika  yakatiririka yakambubujika
12 kuilowesha kuyalovya kulowekana kulilovya
13 alivyoingia alioingia alipoingia akaingia
14 wamekula nyama wamepika majungu wameshika miko wametia mrija
15 mwana akibebwa hutazama kisogo cha nina Mungu akiziba hapa huzibua pale mpanda farasi wawili hupasuka msamba mla nawe hafi nawe ila mzaliwa nawe

 

Kuanzia nambari 16 mpaka 30, chagua jibu Ifaalo zaidi

  1. Chagua kauli ya kutendewa ya:
    Titu alichukua pete ya zawadi
    1. Pete ya Zawadi ilichukuliwa na Tatu.
    2. Pete ilichukuliwa Tutu kwa Zawadi.
    3. Zawadi alichukuliwa pete na Tatu.
    4. Zawadi alichukuliwa pete kwa Tatu.
  2. Maneno yafuatayo yatafuatana vipi katika kamusi?
    1. mchuzi
    2. mchumba
    3. muhogo
    4. muhina
      1. (ii), (i), (iv), (iii)
      2. (iv), (iii), (ii),(i)
      3. (i). (i). (iii), (iv)
      4. (ii),(ii), (iv), (iii)
  3. Chagua sentensi yenye kwa inayoonyesha’ pamoja na’
    1. Seme alipendwa kwa heshima yake.
    2. Tulienda moja kwa moja hadi uwanjani.
    3. Wake kwa waume walishirikisherehe hiyo.
    4. Nuru alipata alama saba kwa kumi.
  4. Mtu mwenye ujuzi wa kufua visu ni
    1. mjume
    2. mjumu
    3. mhandisi
    4. mhazili
  5. Chagua kukanusha kwa
    Kocha alikuwa akiwapongeza na kuwahimiza wachezaji
    1. Kocha hakuwa akiwapongeza kwa kuwahimiza wachezaji.
    2. Kocha alikuwa hawapongezi bila kuwahimiza wachezaji.
    3. Kocha alikuwa hawapongezi ila kuwahimiza wachezaji
    4. Kocha hakuwa akiwapongeza wala kuwahimiza wachezaji
  6. Maneno yaliyopigiwa mstarini
    Vijana hawa walifika mapema lakini wale walichelewa
    1. nomino, kielezi, kiunganishi, kiwakilishi
    2. kivumishi,Kielezi, kiunganishi, kiwakilishi
    3. kiwakilishi, kivumishi, kielezi, kivumishi
    4. kivumishi, kiwakilishi, kiunganishi,kivumishi
  7. Chagua jibu lenye maneno yasiyoambatanishwa ipasavyo.
    1. kikuku - mguu
    2. kipini - pua
    3. ushanga-shingo
    4. kikuba-kiwiko
  8. Ni jibu lipi lenye nomino iliyoundwa kutokana na kitenzi?
    1. nyweka nywesha
    2. ogopa - ogofya
    3. saka - usasi
    4. arnini-aminifu
  9. Onyesha sentensi iliyo katika hali ya mazoea
    1. Magari ya usafiri wa umma hayupiti hapa
    2. Mvua ya masika haijaanza kunyesha
    3. Mto ukifurika hawatavuka
    4. Vazi hilo halikushonwa vizuri.
  10. Andika wingi wa sentensi ifuatayo
    Baharia huyu amevaa kotizuri.
    1. Baharia hawa wamevaa makoti nzuri
    2. Mabaharia hawa wamevaa koti zuri
    3. Mabaharia hawa wamevaa makoti mazuri
    4. Baharia hawa wamevaa makoti mazuri
  11. Sogora kwa ngoma ni kama kwa mapambo
    1. mhuri
    2. kaimu
    3. mjumu 
    4. sonara
  12. Ukubwa wa sentensi:
    Mtoto huyu hataweza kukibeba kikapu hicho ni
    1. Toto hilo halitaweza kulibeba kapu hili.
    2. Jitoto hili halitaweza kulibeba kikapu hicho.
    3. Toto hili halitaweza kulibeba kapu hilo.
    4. Kitoto hiki hakitaweza kulibeba kapu hilo
  13. Ni jibu lipi lenye maneno ya aina moja?
    1. ua, embe, chelewa
    2. andikiwa, ruka, chezesha
    3. dawati, agiza, kaka
    4. waka, salama, tena
  14. Neno mkadamu lina silabi ngapi?
    1.  4
    2. 3
    3. 7
    4. 6
  15. Teka alikabiliwa na shida nyingi maishani. Akajitahidi kuzisuluhisha na hatimaye hali yake ikaimarika. Methali inayojumuisha ujumbe huu ni
    1. Mbio za sakafuni huishia ukingoni.
    2. Achanikaye kwenye mpini hafi njaa.
    3. Mtembezi hula miguu yake.
    4. Kinga na kinga ndipo moto uwakapo.

Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali kuanzia 31 mpaka 40

Amani ni hali ya utulivu ambayo hupatikana pasipo na vita wala machafuko yoyote. Mara nyingi hali hii hupatikana pasipo na gharama yoyote. Hili hasa ndilo linalowafanya wengi kutotilia maanani umuhimu wa amani. Lakini kama walivyosema wahenga, asiyejua thamani ya mwangaza aingie gizani. Ushahidi kuhusu matokeo ya ukosefu wa amani umeenea vururu katika jambu nyingi.

Yamkini nikikuuliza kama unajua umuhimu wa amani utakuwa mwepesi wa kusema ndio. Lakini pengine ukituama na kuwazia matukio mbalimbali yaliyowahi kutokea karibu nawe, au hata kwa mchango wako binafsi, utagundua kuwa umewahi kuchangia kuvuruga amani kwa njia moja au nyingine. Unakumbuka siku ambapo ulieneza uvumi kuhusu mwenzako darasani? Labda ulilichukulia tukio hilo kuwa la kawaida tu. Ambalo hukujua ni kwamba kwa kufanya hayo, ulimsababishia kutengwa na marafiki, ukamfanya ajione duni na kumnyima amani. Bila shaka, ulimwumiza sana kihisia. Ieleweke kuwa tabia ni ngozi. Matendo ya aina hii yasipothibitiwa huweza kuwa msingi wa kusambaratisha mshikamano wa kitaifa baadaye.

Watu wengi huinyoshea serikali kidole wakati yanapozuka machafuko yoyote nchini. Utawala uliopo hukashifiwa kwa kushindwa kutekeleza jukumu lake la kulinda raia wote. Hata hivyo watu wawa hawa ndio kwa mfano wanaowasetiri washukiwa serikali inapojaribu kunyoosha mkono kuwafikia. Watu hawa wakiombwa na vyombo vya dola watoe ushahidi utakaochangia kushtakiwa kwa washukiwa wenyewe, wao hufyata ndimi zao. Isitoshe, wanasiasa wachochezi hukimbilia kutafuta hifadhi za makabila yao pale wanapokabiliwa na mashtaka ya kuvuruga amani nchini. Hata pale tunapodekeza hali hii, ni vyema tukumbuke kuwa vita havina macho.

Gharama ya kutokuwepo amani huwa kubwa katika jamii yoyote ile. Watu hulemazwa huku wengine wakipoteza roho zao. Mali yaliyochumwa kwa muda mrefu huharibiwa katika muda wa kufumba na kufumbua. Katika maeneo kama haya, wawekezaji hutoweka, jambo ambalo huwanyima vijana nafasi za kujiendeleza. Maeneo kama haya huselelea nyuma kiuchumi.

Ni vyema tumaizi kuwa jukumu la kulinda amani haliwezi kuachiwa asasi za kiusalama pekee. Lazima tushikane mikono kupigana na hali yoyote inayotishia usalama wetu kwa hali na mali. Taasisi za kielimu na kidini ziwe katika mstari wa mbele kuhubiri amani. Wanaotumia madhabahu kuwagawanya watu kwa misingi ya kidini watengwe na kukashifiwa. Viongozi wa kijamii nao wachangie kupiga vita mila potovu kama vile wizi wa mifugo na uvamizi. Wanasiasa wachochezi watemwe wakati wa uchaguzi. Vijana nao wajiunge katika vilabu vya kutangaza amani kote nchini.

  1. Chagua jibu sahihi kulingana na aya ya kwanza
    1. Amani ni hali ya utulivu palipo na vita.
    2. Watu wengine hupuuza thamani ya amani
    3. Ukiingia gizani utajua umuhimu wa amani,
    4. Gharama ya amani huwa kubwa sana.
  2. Ni kweli kusema kuwa,
    1. lazima msomaji anajua umuhimu wa amani.
    2. Visa vya utovu wa amani hutokea karibu na watu.
    3. Amani yetu huvurugwa na wale tunaowazia.
    4. Amani huweza hata kuvurugwa na matendo tusiyotilia maanani.
  3. Unapoeneza uvumi dhidi ya mtu fulani.
    1. humwumiza kihisia na kumfanya akose kujistahi.
    2. unawatenga marafiki zako na kujiumiza kihisia.
    3. unamkosesha utulivu na kumwinulia hadhi yake.
    4. huwezi kujua kuwa ufanyayo si haki.
  4. Msimamo wa mwandishi ni kuwa
    1. vurugu za watoto ndizo zinazosambaratisha jamii.
    2. ukosefu wa amani humfanya mtu ajiondoe katika jamii.
    3. tabia isipodhibitiwa mapema inaweza kuleta utengano katika jamii.
    4. mambo madogomadogo hayawezi kuathiri misingi ya kijamii.
  5. Ni kawaida ya watu
    1. kukashifu watawala utulivu unapokosekana.
    2. kuwakashifu wahasiriwa usalama unapodorora.
    3. kuitetea serikali usalama unapovurugiku.
    4. kujua umuhimu wa amani pale inapokosekana
  6. Raia katika kifungu wamclaumiwa kwa
    1.  kutowajua wanaotekeleza vitendo vya kihalifu.
    2. kuwaonya wenzao wanapotaka kutoa ushahidi
    3. kuwafichua washukiwa wanaotafutwa na serikali.
    4. kukosa kusaidia serikali kuwahakikishia usalama.
  7. Njia bora zaidi ya kukabiliana na wanasiasa wanaoeneza chuki katika jamii ni
    1. kueneza habari zao katika vyombo vya habari
    2. kuwaondoa mamlakani wakati wa kupiga kura
    3. kuwatia mbaroni na kuwanyamazisha kabisa.
    4. kuwaacha wapige domo kwani watanyamaza tu.
  8. Yafuatayo ni madhara ya ukosefu wa amani isipokuwa,
    1.  watu kupoteza maisha
    2. uharibifu wa mali.
    3.  kudidimia kwa uchumi.
    4. kuenea kwa ukame.
  9. Wazo kuu linalojitokeza katika aya ya mwisho ni kuwa
    1. mila potovu ndizo zinazovuruga amani nchini.
    2. asasi za kijamii hazihusiki katika kudumisha amani.
    3. jukumu la kulinda amani ni la kila mwanajamii.
    4. tukishirikiana katika vita amani ya kudumu itapatikana.
  10. Huinyoshea serikali kidole ni sawa na
    1. kuilaumu serikali 
    2. kuikejeli serikali
    3. kuikosea serikali. 
    4. kuitukana serikali.

Soma kifungu hiki kisha ujibu maswali kuanzia 41 mpaka 50

Nilipomaliza mtihani wa kitaifa wa darasa la nane, nilijua kuwa ningepata liziko ndefu kuliko kawald Baada ya kukaa mjini kwa siku mbili-tatu, niliwaomba wavyele wangu kibali cha kuenda kijijini kuwazuru babu na bibi: Japo sikuzielewa sana shughuli za shamba, nilijua kuwa msaada wowote kwa wazee wang ungewafaa sana hasa ikizingatia kuwa walikuwa wamebugia chumvi ya kutosha. Waamia, auni ni aun hakuna auni duni.

Siku ya safari ilipowadia, baba na mama walinipeleka kituoni pa mabasi na kuniaya. Nilijawa na wahaka kiasi na kujiuliza, "Itakuwaje gari likinipitisha? Je, nitaweza kukitambua kituo chao vizur Nilitoa shajara yangu na kuhakiki tena maelezo niliyoandika. Njia panda baada ya stoo mbili, nishike njia ya kulia. Hata nilimwuliza utingo kama alikifahamu kituo hicho naye akanihakikishia nisiwe na shaka. Nilimshukuru na kutulia.

Safari yangu ilikuwa shwari bila shari. Njiani nilijisaili maswali anuwai. Nilijiona nikawafaa babu na bibi kwa njia nyingi. Nikajionea nikiwafunza vijana wa mashambani mambo mengi ya mji. "Nitawatoa ushamba kabisa," nikajiambia. Kutahamaki, gari lilisimama, utingo akaniashiria nishuke na kumsaidia kutua mzigo wangu. Kinyume na matarajio yangu, babu alikuwa pale kituoni akinisubiri, Nilimlipa hamali anibebee furushi lile la bidhaa, nikajibebea shanta yenye nguo zangu na kumwandama babu unyounyo.

Kijiji cha akina babu kilijaa utulivu wa kuridhisha. Nilipokelewa vizuri. Hata hivyo jambo moja lilinisumbua akilini. Vijana wenzangu walinisalimia kwa heshima lakini hakuna aliyesema jingine zaidi ya salamu. Sijui kama ni mimi niliyefikiria hivyo, lakini nilihisi kiasi fulani cha chul hasa kutoka kwa wazazi wa kike. Jambo hili lilininyima raha kwani nilidhani kijijini kulitawaliwa na hisia za udugu kama nilivyozoea kusikia ikiwa haya yalifanyika mjini ningeelewa.

Siku moja, mkazahau aliniita chemba na kunipasulia mbarika. Mavazi yangu hasa ya suruali zilizonibana ndiyo yaliyowafanya wengi kujitenga nami. Kumbe kile nilichoita ustaarabu kutokana mjini kilionekana kama utovu wa maadili mjini. Hapo ndipo nilipoujua ukweli ya methali, ukila pamwe na namiriigiza zao desturi. Mkazahau alinifunza mengi kuhusu maisha ya mashambani. Nami nikaafiki methali kuwa kinolewacho hupata.

Polepole nilianza kuwapata wenza. Tulifanya mengi pamoja. Tulibeba maji kwa mitungi migongoni na kuleta matita ya kuni msituni. Nilizifurahia shughuli hizi sana. Kila mara wenzangu hawakusita kunitahadharisha. “Usiuguse upupu huo utawashwa" au "chaka hilo linaweza kuwa na nyoka tahadhari!" Hata wakati wa kurudi mjini ulipofika, niliona uchungu kutengana na wasena wale.

  1. Ni maelezo yapi yaliyo sahihi?
    1.  Ilikuwa likizo ya mwisho katika darasa la nane.
    2. Msimulizi alisafiri pindi tu alipofunga shule.
    3. Mwandishi hakupendelea kuishi mashambani.
    4. Mwandishi alinuia kuwasaidia babu na nyanya yake.
  2. Msemaji anakiri kwamba,
    1. hakuzoea kushiriki shughuli za shambani.
    2. ilikuwa mara ya kwanza kumzuru bibi yake,
    3. anazifurahia sana kazi za mashambani.
    4. hatajifunza shughuli za shambani.
  3. Maneno wamebugia chumvu ya kutosha yametumia tamathali gani ya usemi?
    1. sitiari 
    2. nahau
    3. chuku
    4. tashhisi
  4. Kulingana na aya ya pili, tunaweza kusema kwamba mwandishi,
    1. ni mwenye papara
    2. hana mwao kuhusu aendako
    3. ni mwoga
    4. ni mwenye makini
  5. Utoaji bora wa huduma unaojitokeza kwa kuwa,
    1. babu alimlaki msimulizi kituoni.
    2. hamali alimbebea mwandishi furushi lake
    3. utingo alimpa mwandishi msaada aliohitaji.
    4. mwandishi aliandika maelezo kwenye shajara.
  6. Si kweli kusema kuwa,
    1. mwandishi alibebewa mizigo yake yote.
    2. msimulizi hakutaabika kufika kwa babu.
    3. mwandishi hakutarajiwa kupokelewa kituoni.
    4. msimulizi alitarajia kuwafunza wenyeji wale ustaarabu
  7. Jambo lililomsumbua mwandishi ni
    1. kukosa kusalimiwa na wanakijiji.
    2. kutengwa na baadhi ya wanakijiji.
    3. kutowaona vijana kijijini.
    4. hali ya utulivu iliyoshamiri kijijini.
  8. Wazazi wa kike walimwonyesha chuki msimulizi kwa kuwa
    1. hakupenda kuvalia jinsi alivyoagizwa.
    2. aliwapotosha wanao kwa mienendo ya mjini.
    3. alipenda kuwadharau wanakijiji.
    4. alikiuka utamaduni wao
  9. Methali ukila pamwe na namiri, igiza zao desturi inahimiza
    1. tukiingiliana na watu wenye sifa kama zetu tujaribu kuwa tofauti
    2. tukijua kuwa watu wana sifa tofauti tujiepushe tusiathiriwe na nyendo zao.
    3. tukiingiliana na watu wenye sifa tofauti tutafute mbinu za kuingiliana vizuri nao.
    4. Tukiwa na sifa tofauti tuwahimize wengine wajaribu kuwa kama sisi.
  10. Aya ya mwisho inatufunza kuwa,
    1. kugusa upupu humfanya mtu awatambue marafiki.
    2.  uhusiano unaweza kuimarishwa hata katika mazingira mapya.
    3. kukemewa kwa sauti humfanya mtu atambue mazingira.
    4. Uchungu wa kutengana huzidi mtu anapoenda mjini.

INSHA
Umepewa dakika 40 kuandika insha yako.

Endeleza insha ifuatayo kwa maneno yako mwenyewe huku ukiifanya iwe ya kusisimua zaidi.

Mwendo wa saa nne asubuhi, milolongo ya magari ilionekana ikielekea.........

Majibu

  1. A
  2. D
  3. B
  4. C
  5. A
  6. D
  7. C
  8. B
  9. D
  10. B
  11. A
  12. C
  13. B
  14. C
  15. A
  16. C
  17. A
  18. C
  19. A
  20. D
  21. B
  22. D
  23. C
  24. A
  25. C
  26. D
  27. C
  28. B
  29. A
  30. B
  31. B
  32. D
  33. A
  34. C
  35. A
  36. D
  37. B
  38. D
  39. C
  40. A
  41. D
  42. A
  43. B
  44. D
  45. C
  46. A
  47. B
  48. D
  49. C
  50. B
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - KCPE 2022 Prediction Papers Set 1.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students