Wednesday, 15 March 2023 06:09

Kiswahili Questions and Answers - Class 8 Opener Exams Term 1 2023 Set 4

Share via Whatsapp

MASWALI

Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne hapo.

Chagua jibu lifaalo zaidi kati va yale ulivopewa

Sikukuu ya Krismasi ilishangiliwa        1           Makundi ya wakristo        2           makanisani ili          3          Ndugu na jamaa         4         waliziwahi sehemu         5           burudani ili kuburudika kwa furaha na buraha. Watu wengine          6          ili kuwapa mkono waliokuwa hawajiwezi.        7          walizingatia kwamba        8         .

1.A. kwa hamu na ghamu  B. kwa uti wala mauti  C. kwa shangwe na nderemo  D. kwa udi na uvumba 
 2.A. walimiminika  B. yalimiminika  C. watamiminika  D. yatamiminika
 3.A. kusheherekea  B. kushehekea  C. kureshehekea  D. kusherehekea
 4.A. pia  B. ilhali  C. madhali  D. angalau
 5.A. ya  B. kwa  C. za  D. wa
 6.A. walijitolea kibwebwe  B. walijitolea mhanga  C. walijitolea kingoto  D. walijitolea kiguu
 7.A. Kwa kwamba  B. Kwa ajili  C. Kwa hakika  D. Kwa moja
 8.A. kutoa ni moyo, usambe ni utajiri  B. cha mfupi huliwa na mrefu  C. mtegemea cha nduguye hufa maskini  D. fimbo ya mbali haiui nyoka

 

Kiswahili ni lugha mojawapo,        9          katika mazungumzo ya kawaida. Lugha hii       10       sana         11         nyanja anuwai. Wanafunzi shuleni hufundishwa      12        thelathini. Aidha, kuna sauti ghuna ambazo pia huitwa        13         Sauti hizi huunda         14         Mathalani, neno 'kilichoundwa' lina silabi        15          

9.A. zilizotumika  B. iliyotumika  C. zinazotumika   D. inayotumika 
10.A. inadhaminiwa  B. kinathaminiwa  C. inathaminiwa D. kinadhaminiwa
11.A. katika  B. kati ya  C. kwenye D. katikati ya
 12.A. konsonati  B. alfabeti  C. vokali  D. irabu
 13.A. nyepesi  B. sighuna  C. kwaruzo  D. mwambatano
 14.A. neno  B. sentensi  C. silabi  D. aya
 15.A. sita  B. tano  C. kumi na mbili  D. nane

Kutoka swali la 16-30, jibu swali kulingana maagizo uliyopewa.

  1. Chagua matumizi ya 'kwa' kurejeleamchanganyiko
    1. Walitembea kwa miguu hadi shuleni.
    2. Wazee kwa vijana walihudhuria sherehe hizo.
    3. Timu hizo zilifungana mabao matano kwa sita.
    4. Aliadhibiwa kva utundu wake.
  2. Hazama ni kwa puani kama vile ni kwa sikio.
    1. mkufu
    2. kidani
    3. kipete
    4. mapete
  3. Chagua wingi wa sentensi hii Ua wa dobi ulinivutia sana
    1. Maua ya madobi yalituvutia sana.
    2. Nyua za madobi zilinivutia sana.
    3. Maua ya dobi yalituvutia sana.
    4. Nyua za madobi zilituvutia sana.
  4. Chagua kiambishi 'ku' cha ukanusho
    1. Kusoma huku kunafurahisha
    2. Hakusoma kitabu hicho cha hadithi
    3. Aliyekupiga ametiwa mbaroni
    4. Mchezo huo ulichezwa kule.
  5. Fidia ni
    1. malipo ya kumvunjia mtu heshima
    2. malipo ya kwanza ya kumshika mtoto
    3. malipo kwa ajili ya hasara au maumivu
    4. malipo ya kwanza ya kukinunua kitu dukani.
  6. Kanusha:
    Jengo lililojengwa kwa uhafifu limebomolewa
    1. Jengo lisilojengwa kwa uhafifu limebomolewa
    2. Jengo lililojengwa kwa uhafifu halijabomolewa
    3. Jengo halikujengwa kwa uhafifu limebomolewa
    4. Jengo lisilojengwa kwa uhafifu halijabomolewa.
  7. Ni nini maana ya msemo huu?
    Kumvisha mtu kilemba cha ukoka
    1. Kumtegemea mtu kwa kila jambo.
    2. Kumsema mtu katika mafumbo.
    3. Kumweka mtu katika hatari.
    4. Kumdanganya mtu kumhusu.
  8. Chagua jibu lenye ala za muziki pekee
    1. Filimbi, udi, mvukuto, chapuo.
    2. Siwa, zeze, upatu, nembo..
    3. Njuga, tari, kinubi, fidla.
    4. Harimuni, marimba, msondo, maleba.
  9. 5/6 kwa maneno ni
    1. sudusi sita
    2. humusi sita
    3. sudusi tano
    4. humusi tano.
  10. Ni kundi lipi la nomino ambalo lipo katika ngeli ya LI-YA?
    1. Maji, marashi.
    2. Gitaa, povu.
    3. Maskani, mavazi.
    4. Maagizo, maarifa.
  11. Onyesha sentensi yenye kielezi cha mahali
    1. Mwajuma alisafisha nyumba alfajiri.
    2. Kule kuna miti mirefu.
    3. Wawili walisajiliwa chuoni.
    4. Gari limefika asubuhi.
  12. Chagua jibu lenye nomino ya makundi isiyofaa
    1. Mzengwe wa wagomaji.
    2. Numbi ya nyuki.
    3. Shungi la moto.
    4. Thurea ya nyota
  13. Kauli, 'Jedi ni sungura maishani; imetumia tamathali gani ya usemi?
    1. Jazanda.
    2. Kinaya.
    3. Tashhisi.
    4. Nahau.
  14. Ikiwa juzi ilikuwa Jumanne, mtondo itakuwa
    1. Ijumaa.
    2. Jumatatu.
    3. Jumapili.
    4. Jumamosi.
  15. Chagua jibu lenye kivumishi kilichoundwa kutokana na kitenzi.
    1. Ita -  mwito
    2. Vumilia - uvumilivu
    3. Agiza - maagizo
    4. Sahau - sahaulifu.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 31 - 40.

Kuku aliketi nje ya nyumba yake huku amejishika tama. Moyo wake ulijawa na huzuni mpwitopwito. Je, angewezaje kuujenga urafiki wake upya na mwewe mwandani wake wa chanda na pete? Tatizo sugu lililokuwa limeubomoa urafiki wao wa kufa kuzikana ni wembe. Kuku alishangaa namna ambavyo kitu kidogo kama hicho kingesababisha mgogoro kama huo mkubwa. Mawazo kedekede yalizidi kumzunguka akilini mithili ya pia.

Mwewe naye kwa upande wake pale kiotani alitabasamu kwa furaha mzomzo. Aliurarua mnofu wa nyama wake kifaranga mtoto wa kuku. Kwake alijiambia kuwa, “Sasa ninazidi kujilipa deni langu la wembe. Mtu hawezi kuwa ananipotezea rasilimali zangu pasipo kuzingatia hisia zangu pia. Bado atakuja kunitambua! Atabaki mzazi bila vikembe hadi atakapolipa deni lote!"

Giza la usiku lilikumbatia siku yenyewe. Sauti za mbwa zikawa zinasikika kwa umbali. Bado kuku pamoja na vifaranga wake watatu walikuwa hawajalala. Biwi la simanzi liliwaangukia kuku. Mtoto wake wa kiume alikuwa amenyakuliwa na mwewe. Mwewe asiye na utu wala msamaha. Mbona asingengoja hata siku moja imalizike kabla ya kuanza kujilipa yeye mwenyewe? Kwa nini basi asingekuja wapange mikakati namna ya kulipwa? Utitiri wa mawazo ulimtembea akilini mwake bighairi ya kuwa na mwisho. Hatimaye, kuku aliwageukia wana wake ambao ndio chanzo cha kupotea kwa wembe wake mwewe. Aghalabu, alikuwa amewakanya dhidi ya kuchezea vitu vya wenyewe bila ya ruhusa. Kuku alijua siku moja mchezo wao huo ungewatumbukiza katika kidimbwi cha moto. Sasa moto huo ulikuwa umeanza kuwateketeza mno. Kuku akaishia laiti ningalijua na vyanda vi mkononi. Hata hivyo, akaamua kulitafuta suluhisho la kudumu ifikapo asubuhi.

Jua la asubuhi liliramba umande wa alfajiri huku likimzizimua kobe ambaye alitoka nyumbani mwake asteaste. Mzee kobe alisifika sana kwa maarifa yake na akili tambuzi alizokuwa nazo hasa katika kuyatatua mambo baina ya wenzake. Aliketi pale nje huku akibukua tabu kubwa kuhusu migogoro. Kuku jirani yake aliwasili kwake kwa kishindo. Hapo kobe akatambua ya kwamba lazima kuna jambo. Huku amenyong'onyea kama mkufu. Kuku alimpasulia mbarika mzee kobe kuhusu tatizo lake. Jungu kuu halikosi ukoko. Baada ya kikao hicho cha saa tatu naye mzee kobe, kuku alirudi nyumbani akiwa na matumaini kwamba suluhu limepatikana. Mzee kobe alibaki katika kina kirefu cha fikra ili kulipata suluhisho hilo la kudumu na kumpiga jeki jirani yake. Kwa hakika, ni heri jirani kuliko ndugu yako wa toka nitoke wa mbali.

  1. Chagua maana ya ‘kushika tama' kwa mujibu wa kifungu. |
    1.  kuhangaika
    2. kuhuzunika
    3. kunung'unika
    4. kukasirika
  2. Kulingana na aya ya kwanza, kuku
    1.  aliketi ndani ya kiambo chake
    2. alikuwa jasiri na mkakamavu
    3. aliwazia kiini cha ufa uliokuwa umetokea
    4. hakushangaa kiini cha mgogoro..
  3. Kulingana na aya ya pili, mwewe anaonekana kuwa
    1. mwenye ubinafsi
    2. mwenye urafiki wa dhati
    3. mwenye huzuni nyingi
    4. mwenye maarifa chungu nzima.
  4. Kitendo cha mwewe kuamua kujilipishia deni lake kinaweza kulinganishwa na methali gani?
    1. Asante ya punda ni mateke.
    2. Tamaa mbele mauti nyuma.
    3. Mtu ni watu.
    4. Uzuri wa mkakasi ndani kipande cha mti.
  5.  "Biwi la simanzi lilimwangukia kuku,"
    imetumia tamathali gani ya usemi?
    1. Ishara.
    2. Sitiari.
    3. Chuku.
    4. Tashhisi. 
  6. Kwa nini mzee kobe alisifika? 
    1. Kwa sababu alipenda kusoma mabuku.
    2.  Kwa sababu alikuwa mstahimilivu.
    3. Kwa sababu alikuwa mwenye akili pevu.
    4. Kwa sababu alipenda kuliota jua.
  7. Kulingana na aya ya mwisho si sahihi kusema
    1. kikao hakikuzalisha matunda.
    2. jirani anaonekana kuwa na umuhimu.
    3. mzee Kobe aliwazia jambo hilo.
    4. kikao kilichukua saa tatu.
  8. Kifungu kinabainisha kwamba
    1. mwewe alikuwa mwandani wa dhati.
    2. kuku hakuwajali watoto wake.
    3. mzee kobe hakupenda kisomo kwa dhati.
    4. kuku alimwelezea kobe mambo dhahiri.
  9. Maana ya, "biwi la simanzi' kulingana na kifungu ni
    1. mkusanyiko wa hasira
    2. mkusanyiko wa taka
    3.  kuwa na kiasi kikubwa cha huzuni
    4.  kuwa na kiasi kikubwa cha uka.
  10. Kichwa kifaacho kifungu hiki ni sana ni
    1. Mzee Kobe mwenye magamba.
    2. Elimu nyingi huondoa maarifa.
    3. Urafiki wenye unafiki.
    4. Vifaranga vya kompyuta.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 41 - 50.

Afya au siha ni hali ya kutokuwa na maradhi. Hali hii humwezesha mtu kuhifadhi nguvu zake za mwili na kumwezesha kufanya kazi katika mawanda mbalimbali. Mtu mwenye afya bora huweza kutekeleza mengi bila masumbuko. Kwa mfano, yeye huweza kujirausha na kujishughulisha hadi jioni bila kuhisi uchovu mwingi.

Chombo hakiendi ila kwa makasia, nayo afya nzuri haimjii tu mtu. Afya hustahili kupaliliwa na kutunzwa kwa namna anuwai kama vile kula vyakula vyenye viinilishe, kufanya mazoezi na kuandama mienendo miadilifu. Usafi wa mv ili na mazingira pia huchangika katika kuimarisha afya. Ni bayana kwamba mazingira yakiwa machafu hukosa kuvutia na kusababisha kusambaa kwa harufu inayokirihisha. Isitoshe, uchafu huwa hali mufti ya kuzaana kwa wadudu kama vile chawa, nzi, kunguni na mbu ambao ni maadui wakuu wa afya. Tabia ya binadamu huathiri afya yake. Wapo watu ambao wameambulia magonjwa kama vile saratani ya mapafu na kifua kikuu kutokana na mazoea ya pombe, sigara na dawa za kulevya. Wengine hujiponza kwa kuingilia vitendo viovu kama vile kushiriki mapenzi kiholela na kujisababishia magonjwa. Magonjwa haya ni kama vile kisonono na ukimwi ambao umewapukutisha watu kama majani makovu kutoka mtini.

Aidha, watu hujiharibia afya kwa kufanya kazi mfululizo bila kupumzika. Licha ya kwamba bidii ni muhimu katika maendeleo ya jamii yoyote ile, utendaji kazi pasipo kupumzika huweza kuwa na athari hasi. Kuna baadhi ya watu ambao wamewahi kupata maradhi ya moyo, ya kiakili na hata shinikizo la damu kutokana na hali kama hii. Wengine hujihasiri kwa kula vyakula vingi kupindukia. Kadhalika, wapo wengine ambao hupata magonjwa kwa kula vyakula visivyofaa katika kundi hili kwa wale ambao hawadiriki kufanya kazi wala mazoezi. Hawa hujinenepea na kudhoofisha utendakazi wao.

Hali ya umaskini pia huchochea kuzoroteka kwa afya. Asilimia kubwa ya watu nchini humu haimudu huduma bora za afya na lishe bora kutokana na hali ya ufukara. Wengine, kwa kukosa fedha hawapati elimu ya kimsingi kuhusu afya. Hawa huweza kujizulia magonjwa kwa kutojua na kutofuata sheria za afya. Pamoja na hayo, kuna wale ambao wanarithi magonjwa ya kiukoo kama vile bolisukari kutoka kwa wazazi wao. Umuhimu wa afya hauwezi kupuuzwa. Nchi yenye kizazi chenye afya hustawi kiuchumi. Afya ikidumishwa wanajamii huweza kutumia fedha zao kuwekeza katika miradi badala ya kuzitumia kujiunga na kuwauguza wenzao. Ni jukumu la kila raia kuhakikisha kwamba anailinda afya yake na ya wengine kwa vyovyote vile. Walio na mazoea ya kupuuza ushauri wa wanaotoa huduma za afya na lishe wajiase, la sivyo watakuja kujiuma vidole.

  1. Kulingana na aya ya kwanza siha
    1. hukuza maendeleo katika maeneo mbalimbali
    2. humwondolea mtu matatizo mwilini
    3.  humpunguzia mtu mazoea ya uchovu
    4. huimarisha matokeo ya utendakazi.
  2. Ni muhimu kutunza mazingira kwa kuwa
    1.  tutamaliza vikwazo tofauti tofauti vya afya
    2.  tutazuia ongezeko la wadudu waharibifu
    3. tutaepuka kuenea kwa harufu
    4. tutarudisha hali ya kupendeza.
  3. Mwandishi anapinga hali gani hasa katika aya ya tatu?
    1. Uambukizaji wa magonjwa.
    2. Kuhusiana bila mpango.
    3. Vifo vya watu wengi.
    4. Matumizi mabaya ya mihadarati.
  4. Chagua jibu ambalo ni sahihi kulingana na aya ya nne
    1. Jambo jema husababisha maradhi
    2. Kazi nyingi husababisha moyo kuharibika
    3. Mazoezi hayawezi kudhibiti afya.
    4. Mapumziko huimarisha hali ya mtu kiakili.
  5. Kufanya kazi kidindia
    1. huboresha maendeleo ya taifa
    2.  huweza kusababisha uharibifu wa afya
    3. huwa na athari chanya
    4. hupunguza shinikizo la damu.
  6.  Maana ya 'inayokirihisha' ni
    1.  inayochukiza
    2. inayoenea
    3.  inayoaibisha
    4. inayodhuru.
  7. Maana ya "chombo hakiendi bila ya makasia' imejitokeza vipi katika kifungu?
    1. Wanaonyoosha viungo vyao huwa wakakamavu.
    2. Wanaozingatia mienendo mizuri hudumisha afya.
    3. Wanaoepuka kazi hawapati shinikizo la damu
    4.  Wanaokula vyakula vyenye viinilishe huzuia kunenepa.
  8. Chagua funzo linalojitokeza katika aya ya mwisho
    1. Wanaokosa kuzingatia maelekezi hupata majuto.
    2. Mtu hawezi kufaidika kiafya bila kupata ushauri.
    3. Wanaodharau watu wenye hekima hupata magonjwa.
    4. Nchi haiwezi kupiga hatua bila raia wote kuzingatia maradhi.
  9. Umuhimu wa afya hauwezi kupuuzwa kwa vile
    1. mipango nchini hukwama wahudumu wakikosekana
    2. watu wagonjwa hawawezi kuizalisha mali
    3. maradhi husababisha kuzorota kwa maendeleo
    4. pesa nyingi hutumiwa kuwatunza walio hospitalini.
  10. Kisawe cha 'kujiuma vidole" ni
    1. kupiga vijembe
    2. kutia nanga.
    3. kupigwa butwaa.
    4. kujuta hatimaye.

INSHA

Andika insha ya kusisimua ukiendeleza kwa maneno haya:

Nilikuwa nimeketi sebuleni nikisoma kitabu cha hadithi

MWONGOZO 

  1. C
  2. B
  3. D
  4. A
  5. C
  6. B
  7. C
  8. A
  9. D
  10. C
  11. A
  12. B
  13. C
  14. C
  15. B
  16. B
  17. D
  18. D
  19. B
  20. C
  21. B
  22. D
  23. C
  24. C
  25. B
  26. C
  27. B
  28. A
  29. C
  30. D
  31. B
  32. C
  33. A
  34. D
  35. D
  36. C
  37. A
  38. D
  39. C
  40. C
  41. D
  42. A
  43. D
  44. D
  45. B
  46. A
  47. B
  48. A
  49. C
  50. D

 

Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Class 8 Opener Exams Term 1 2023 Set 4.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students