Thursday, 16 March 2023 06:43

Kiswahili Questions and Answers - Class 8 Opener Exams Term 1 2023 Set 5

Share via Whatsapp

Jaza nafasi zilizoachwa wazi kuanzia 1 - 15 kukamilisha vifungu vifuatavyo:-

Nina uhakika __1__ mwendo wa usiku wa manane hivi. Mlio wa __2__ yangu ndio ulionigutusha. Niliinua __3__. Lo! Ilikuwa ni sauti ya Mluna wangu aliyekuwa akizimbua __4__ huko ughaibuni. Baada ya maamkizi, alitaka, bila kupoteza mwia, ni atumie maelezo fulani kwa njia ya faksi. Nami kwa kuwa sikuwa na huduma hiyo ya __5__, nilimweleza ningetuma kwa __6__ "Haidhuru." alisema. Kutokana na ukosefu wa __7__ simu ilikatika. Hata hivyo, ujumbe ulikuwa umewasilishwa. Bila kupoteza wakati, nilichukua __8__ na
kuanza kuandika maelezo yale. Kwa ndege nzuri, tarakilishi hiyo ilikuwa imeunganishwa na __9__. Papo hapo nikamtumia ujumbe.

   A   B   C   D 
 1.   ilikuwa   ulikuwa   nilikuwa   mlikuwa 
 2.  rununu   satalaiti  nukulishi   redio
 3.  kuichuna   kupiga  kuibonyeza   kujibu
 4.  unga  maisha  mali  riziki
 5.  kipepesi  satalaiti  arafa  barua meme
 6.  nukulishi  huduma za mhadalishi   runinga  redio
 7.  utandawazi   njia ya mhadili  njia ya mhadihi   barua pepe
 8.  runinga  jokofu  tarakilishi  panka
 9.  wavuti  kidaka  waraka  simu


Kukutana __10__ naye kulikuwa kwa sadfa. Nilikuwa __11__ kondeni __12__. __13__. Mara nikamwona kijana Skambe __14__
barasteni. Hali yake ilisikitisha kutokana na __15__ ulevi haramu

   A   B    C   D  
 10.  kwetu   kwangu   kwao   kwenu 
 11.   ninaelekea   naelekea   nikielekea   kuelekea 
 12.  kunadi   kupalilia   kuinjika   kuabudu 
 13.  Kulikuwa kukinyesha   Mvua ulikuwa ukinyesha   Kulikua kukinyesha   Mvua ilikuwa ikinyesha 
 14.  akipepesuka  akihohosa   akiweweruka   akikweta 
 15.  kunywa   kulewa   kushiriki   kutopea 


Kutoka swali la 16 mpaka 30, jibu kila swali kulingana na maagizo yake:-

  1. Nyambua kitenzi kilichopigwa mstari katika kauli ya kufanyiwa. KUFA
    1. Hapo ndipo alipofiliwa
    2. Hapo ndipo alipofia
    3. Hapo ndipo alipokufiwa
    4. Hapo ndipo alipofiwa
  2. Tambulisha nomino tadunisha na nomino kuza ya neno kiti ni
    1. Kijiti - Jiti
    2. Kikiti - Jikiti
    3. Kijikiti - Jikiti
    4. Kijikikiti - kiti
  3. Chagua sentensi moja yenye maana sawa na ile uliyopewa katika sentensi iliyo hapo chini
    Ni heri nivumilie shida kuliko kuiba
    1. Ni bora niibe nikiwa na shida
    2. Afadhali nisiibe hata nikiwa na shida
    3. Nisingekuwa na njaa nisingeiba
    4. Niliiba kwa vile nilikuwa na njaa
  4. Tumia kilinganishi sahihi
    Matilda-
    1. Anafanana na dada yangu
    2. Anakaa kama dada yangu
    3. Anafanana kama dada yangu 
    4. Analingana kama dada yangu
  5. Mbio za farasi ni _________________________
    1. kupupira
    2. kutekela
    3. kuparakasa
    4. kunyiririka
  6. Mzazi wa mke humwita mume wa binti
    1. mlamu
    2. mkaza
    3. mwana
    4. mkwerima
  7. Taja kiwakilishi katika sentensi
    Ninakipenda chakula hiki kwa sababu chenyewe ni kitamu.
    1. chakula
    2. hiki
    3. chenyewe
    4. kitamu
  8. Taja neno moja tu linalosimamia fungu zima.
    Kabaila alizivua nguo akaosha mwili.
    1. Oga
    2. Osha
    3. Nawa
    4. Pangusa
  9. Eleza tofauti baina ya sentensi katika jozi (sawia)
    1. Mvua ilinyesha ndogo ndogo
    2. Mvua ilinyesha kidogo kidogo
      1. Mvua haikunyesha kwa wingi.
        Mvua ilikuwa kiasi kidogo.
      2. Mvua ilikuwa kiasi kidogo.
        Mvua ilikuwa matone madogo madogo 
      3. Mvua ilikuwa kiasi kidogo kidogo.
        Mvua ilikuwa chache
      4. Mvua ilikuwa matone madogo madogo.
        Mvua ilikuwa kiasi kidogo kidogo.
  10. Andika jina la kitendo na mtenzi kutokana na KITENZI ulichopewa
    Rehemu __________________      _________________
    1. Rehemu - Rehema
    2. Rehema - Rahimu
    3. Rahimu - Rehema
    4. Rahimu - Rehemu
  11. Badilisha sentensi hii kwa wingi.
    Malkia wa kijiji ana macho ya kikon:be. 
    1. Malkia wa vijiji wana macho ya kikon:be 
    2. Malkia wa vijiji wana macho ya vikombe 
    3. Malkia wa kijiji ana jicho la vikombe 
    4. Mamalkia wa vijiji wana macho ya vikombe
  12. Kumramba mtu kisogo ni
    1. kulamba kisogo chake
    2. kumdharau
    3. kumwangalia kwa dharau
    4. kumsema vibaya asipokuwepo
  13. Badilisha sentensi ifuatayo katika wakati RUDUFU 
    Mgeni anakuja kwangu
    A. Mgeni akaja kwangu
    B. Mgeni yuaja kwangu
    C. Mgeni huja kwangu
    D. Mgeni aja kwangu
  14. Ni kikundi kipi kilicho na viarifa pekee?
    1. Angua, chomoa, zana, vizuri
    2. Vunja, sana, chora, lia
    3. Polepole, upesi upesi, mbiombio
    4. La, pa, ita, ona
  15. Kamilisha methali ifuatayo:Asiyeona nafsiye _____________________________
    1. haoni akionyeshwa
    2. hana ajifunzalo
    3. ni malaika
    4. hanong'onezewi neno

Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali 31-40:-

Ilikuwa Jumamosi. Nilifika nyumbani kwangu saa moja jioni. Tangu nistaafu miaka miwili awali sikupenda kuchelewa Taarifa ya Habari.

Mwezi mmoja ukawa umepita tangu nipewe pesa za kiinua mgongo. Mwezi mmoja mzima nilkuwa katika shughuli za kulipa karo huku. Kuwekeza kwenye mradi ule na kununua hili. Sasa shilingi laki mbili tu zilikuwa zimesalia katika benki.

Watu wengi walinishawishi nijaribu kilimo cha mahindi. Bei ilikuwa imeanza kuimarika. Katika taarifa ya habari jioni hiyo, Waziri wa Kilimo alitangaza bei mpya. Shilingi 1,500 kwa kila gunia. Nami nilikuwa naaza kuumakinikia mradi huu.

Baada ya taarifa, nilikoga, nikala na nikaenda kulala. Kwa sababu ya uchovu, usingizi ulinichukua mara moja. Usingizini niliota. Katika ndoto niliutekeleza mradi wangu. Msimu huo wa kulima nilitenga ekari kumi za shamba langu. Wataalamu walinishauri kuwa wakati mzuri wa kulima ni wa kiangazi. Mwezi wa Januari ulipoanza tu nilitafuta trekta na kulima. Malipo yalikuwa shilingi 1,200 kila ekari. Katikati ya mwezi wa Machi, nilitafuta treka la kutifua shamba tena kwa gharama ya shilingi 15,000 ekari zote kumi. Kufuatia ushauri wa manyakanga wa kilimo, nililipa shilingi elfu kumi na tatu kupiga shamba lote haro.

Mwishoni mwa mwezi huo, nilienda mjini kutafuta pembejeo. Kwanza, nililipa shilingi 20,500 kwa magunia 15 ya mbolea. Kisha nilinunua magunia manne ya mbegu ya mahindi yenye uzani wa kilo 25 kwa shilingi 3,300 kila gunia. Mwezi wa Aprili ulipotimia tu, niliamua kupanda. Ili nipate mazao bora, nilipanda kwa tandazi. Gharama ilikuwa shilingi 1,000 kila ekari. Mvua ilinyesha vizuri na baada ya siku saba, mahindi yalianza kuota. Ilifurahisha kuhesabu mistari ya kijani iliyonyooka. Hali hii iliwezekana tu baada ya kuajiri vijana wa kuwafukuza korongo na vidiri ili wasifukue mbegu mchangani.

Baada ya mwezi mmoja, hatua ya kupalilia ilifika. Nilitafuta vibarua wa kupalilia. Malipo yalikuwa shilingi 700 kila ekari. Kumbe kupalilia kulichochea mtifuko wa mahindi. Punde yakawa yananifikia magotini, Hii ikawa ishara kuwa yanahitaji kumwagiwa mbolea ya kunawirisha iitwayo 'amonia'. Gharama yake ikawa shilingi 1,300 kila gunia. Hivyo, nikalipa shilingi 19,500 kwa magunia kumi na matano.

Mahindi yalibadilika kimiujiza. Ghafla tu yalirefuka na kunenepa mashina. Yalibadilika rangi yakapiga weusi. Shamba liligeuka likawa kama msitu wa rangi ya kijani iliyokolea. Wapita njia walistajabia mimea na juhudi zangu. Shamba langu sasa likawa kielelezo. Maafisa wa kilimo wakawa kila siku wanawaleta wakulima wengine kujifunza siri ya ufanisi wangu. Hapo nikaanza kuhesabu mavuno nitakayopata na kukadiria faida. Nilipuuza kabisa ushauri wa wahenga kuwa 'Usikate majani, mnyama hajauawa.

Bila taarifa wala tahadhari mvua ilitoweka. Hayakupita majuma mawili mahindi yakaanza kubadilika. Juma moja baadaye mahindi yalinyauka. Badala ya mahindi, shamba likageuka la vitunguu vilivyochomwa na jua. Makisio yangu ya faida yaliyeyuka jinsi ufanyavyo moshi.

Lakini 'Muumba ndiye Muumbua.' Siku moja mawingu yalitanda na mvua ikanyesha. Muda si muda mahindi yalianza kunawiri. Kumbe tukio lililonivunja moyo lilikuwa laja. Siku moja mvua kubwa ilinyesha. Asubuhi nilipotoka nje nilipigwa na butwaa. Barafu ilitapakaa pote. Shamba lilikuwa limetapakaa barafu huku majani ya mahindi yamechanika kama nyuzi. Niliugua. Baada ya wiki moja, nilipata nafuu. Nilipotazama upande wa shamba niliona dalili za majani mapya ya mahindi yakianza kuchomoza. Maumbile ni kitu cha ajabu kweli.

Muda si mrefu mahindi yalirudia hali yake tena, kisha yakakomaa. Harakati za kutafuta watu wa kuyakata na kuyakusanya zilianza. Gharama ya shughuli hii ikawa shilingi 5,000. Kuvuna, kusafirisha kutoka shamba na kukoboa kwa mashine magunia 200 yakachukua shilingi 20,500. Kufikia hapo nilikuwa nimetumia takribani shilingi 192,700. Gharama nyingine zilikuwa za usafiri, gharama ya dharura na usimamizi, usumbufu wangu binafsi, gharama ya magunia na kadhalika. Mahindi yalipokuwa tayari kwenye magunia, nilifunga safari kwenda mjini kutafuta soko.. Niliposhuka tu niliona gazeti. Habari motomoto siku hiyo ilikuwa: 'MAHINDI GUNIA 900/= Niligutuka usingizini

  1. Andika kichwa mwafaka kwa kifungu hiki
    1. Mahindi gunia
    2. Mashaka ya kilimo cha gunia
    3. Kiinua mgongo
    4. Usingizi
  2. Msimulizi alikuwa na kiasi gani cha fulusi baada ya mradi kukamilika?
    1. Elfu mbili tu
    2. Laki mbili tu
    3. Elfu saba mia tatu
    4. Laki moja mia tisa, mia saba
  3. Kwa mujibu wa kifungu hiki msimulizi alikuwa na matatizo matatu makuu katika zaraa ila
    1. tishio la korongo
    2. tishio la kiangazi
    3. mvua ya barafu
    4. gharama ndogo
  4. Kwa mujibu wa kifungu methali "Muumba ndiye muumba" imetumika. Ni methali ipi iliyo na maana sawa na hiyo?
    1. Aliyekupa wewe kiti ndiye aliyenipa kumbi 
    2. Hulka njema sawa na mali
    3. Bahati ya mwenzio usiilalie mlango wazi
    4. Baada ya dhiki faraja
  5. Pamoja na kiwango cha chini cha mavuno ni jambo lipi jingine lililosababisha msimulizi kutopata faida?
    1. Gharama ya kilimo
    2. Kushuka kwa bei
    3. Kutoweka kwa mvua
    4. Tangazo lililokuwa gazetini
  6. Eleza maana ya kiinua mgongo kama lilivyotumika katika kifungu
    1. Mshahara wa mwezi
    2. Mkopo wa kilimo.
    3. Malipo ya kustaafu
    4. Kuinuliwa mgongo juu
  7. Kwa mujibu wa aya ya tano jambo lipi ambalo lilikuwa la mwisho kutendewa na msimulizi
    1. Kuhesabu mistari ya kijani iliyonyoka 
    2. Kuenda mjini kutafuta pembejeo
    3. Kuajiri vijana kuwafukuza vidiri na korongo
    4. Kupanda kwa tandazi ili apate mazao bora
  8. Maana ya yalinyauka ni
    1. kauka
    2. kufa
    3. nawiri
    4. stawi
  9. Katika aya ya nane maoni ya msimulizi ni kuwa faida yaliyeyuka ufanyavyo moshi. Huu ni mfano wa
    1. tashbihi
    2. tashdidi
    3. istiari
    4. tanakali
  10. Kulingana na kifungu ni kweli kusema kuwa
    1. mavuno hayakuwa mema
    2. mavuno yalikuwa haba
    3. msimulizi hakutumia ngwenje nyingi
    4. msimulizi alikuwa amestaafu

Soma habari ifuatayo kisha ujibu maswali 41 - 50:-  

Ama kwa hakika, dunia uwanja wa fujo. Vituko vya ulimwengu haviishi. Huzuka kama mizuka kila kunapokucha. Maajabu yaja yakienda. Yote hayo ni mawimbi ya maisha yanayomkumba mwanadamu katika kuishi na kuisha kwake. Lo! Hayo ndiyo malimwengu ulimwenguni.

Nikikaa na kutafakari, huku nikivuta taswira ya mambo kuhusu haya na yale nywele hunisimama, moyo hunidunda, mifupa hunikengeta, nayo damu hunisisimka. Na damu isipowasha hunyeza! Lakini tufanyeje sisi waja wa Mungu ilhali tunajua na kuelewa fika kuwa mja hana hiari na liandikwalo ndilo liwalo? Tunaishi na tuishi kwa rehema na majaliwa ya Jalali. Ewe Mola tunakuhimidi!

Kisa na maana? Hebu nikukumbushe machache tu. Akali ya vituko na vitushi vya hivi karibuni. Bila shaka
nitakuwa nimekusaidia na kukufaa ushughulishe kumbukumbu zako nawe urejee nyuma kidogo. Wazee hukumbuka,
vijana hukumbushwa.

Si miaka mingi sana ulimwengu wetu ulipokumbwa na mvua za mafuriko ya Elnino. Maafa mangapi kama si misiba iliyotusibu. Baadaye tukakumbwa na uhasama wa Osama! Roho nyonge zikanyongwa. Yakaja mawimbi ya kabobo, nyinyi mnayaita Sunami! Vifo vilifisha wengi. Baada ya kidonda moyoni, msumari wa moto juu ya dondandugu. Kabla ya kupona wakazuka ndugu wawili Artur magariani na mwenzake. Nyinyi mkawaita mamluki. Shangaa. Kesho yatazuka yapi? Tahadhari iko wapi? Roho mikononi. Ndugu amkeni tulale tukiwa macho.

  1. Dunia imemithilishwa na uwanja wa fujo kwa nini?  Kwa sababu
    1. Kuna vituko vingi mno vya kushangaza
    2. Fujo hutokea duniani
    3. Watu wanafurahishwa na fujo za dunia
    4. Furaha za watu ni kufanya fujo
  2. Tunaambiwa kuwa
    1. vituko vina mwisho, vimeisha
    2. maajabu hayana mwisho, huja yakienda
    3. maajabu ni malimwengu
    4. vituko vya dunia havimtishi mwanadamu
  3. "Kuishi na kuisha" kuna mantiki gani?
    1. Kufurahia kuishi na kuisha
    2. Huwezi kuisha bila kuishi
    3. Ukiisha utaishi
    4. Watu wanakuwa hai huku wengine wakifa.
  4. Kulingana na kifungu, nini maana kuvuta taswira?
    1. Kuona picha
    2. Kupiga mambo picha
    3. Kusoma na kuelewa
    4. Kuyakumbuka matukio kwa makini
  5. Nywele husimama, moyo hudunda. Kichwa _________________ ilhali tumbo __________________
    1. huvuma, hudorota
    2. hutafuna, huzunguka
    3. huwanga, husokota
    4. huruka, huchanganya
  6. Taarifa inatuambia kwamba tunaishi
    1. kwa kudra za Mwenyezi Mungu 
    2. kwa kuwa tuna nguvu nyingi
    3. kwa kutumia ujanja
    4. ili Mungu atusaidie
  7. Baadhi ya maafa yaliyowahi kutokea ni pamoja na
    1. yote yaliyosababishwa na uzembe wetu
    2. yaliyo zaidi ya uwezo wetu kuzuia
    3. mengi ambayo tungezuia
    4. dhambi za wanadamu wenyewe
  8. Maafa yaliyosababishwa na nguvu za maji ni kama vile
    1. Elnino na uhasama
    2. Kabobo na Artur
    3. Osama na Artur
    4. Kabobo na Elnino
  9. Miongoni mwa walioaga dunia walikuwepo
    1. Mamluki
    2. Wenye hatia
    3. Wasio na hatia
    4. Waliosababisha kabobo
  10. Bila shaka taarifa hii ni
    1. Kuhusu msiba na huzuni ya maafa
    2. ya kuchekesha
    3. hadithi ya porojo tu
    4. mambo yaliyopita ambayo hayana umuhimu.


MARKING SCHEME

  1. B
  2. A
  3. C
  4. D
  5. A
  6. B
  7. C
  8. D
  9. A
  10. A
  11. C
  12. B
  13. D
  14. A
  15. C
  16. D
  17. C
  18. B
  19. A
  20. C
  21. D
  22. C
  23. A
  24. D
  25. B
  26. A
  27. D
  28. C
  29. D
  30. A
  31. B
  32. C
  33. D
  34. A
  35. B
  36. C
  37. C
  38. A
  39. A
  40. D
  41. C
  42. B
  43. B
  44. B
  45. C
  46. D
  47. A
  48. A
  49. B
  50. A
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Class 8 Opener Exams Term 1 2023 Set 5.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students