Wednesday, 05 July 2023 13:14

Kiswahili Questions - Class 8 Opener Exams Term 2 2023 Set 7

Share via Whatsapp

Soma vifungu vifuatavyo. Kwa kila nafasi, umepewa majibu manne. Chagua jibu lifaalo zaidi.
Katika kila ___1___ kuna waja tofauti. Kila mwanajamii ana ___2___ lake ___3___ kutekeleza. Wazee huwa __4___ jukumu ___5__ la kuongoza wanajamii ____6__ vijana hulinda na jamii. ___7___ na kulinda jamii, vijana ___8___ huungana na wazee kuongoza jamii kwani wao ndio viongozi __9____ kesho.

Kila jamii ina __10____ wao wa kufunza wasichana na wavulana mambo ___11___ Wazee huelekeza wavulana nao ___12___ ___13____ wasichana. Haya ___14___ hufanywa ___15___ kuwahamasisha vijana jinsi ya kukabiliana na maisha yao ya usoni.

 
 1  jamaa  jamii   kikao   jamia 
 2  majukumu  kazi   uwezo   jukumu 
 3  ya  la   kwa   wa 
 4  kwa  na   wa   kwa 
 5   lote   yote   wote   yoyote 
 6  hata  ilhali   kwani   nanyi 
 7    Mbali  Bali  Bari  Kuliko
 8   pia  nao  wao  wetu
 9  ya  mbali  mwa  wa
10  hatua  kikao  mlengo  mwamko
11   mingi  nyingi  mengi  zingine
12  mamayo  mamazo  akina mama  wamama
13   hufuata  hutuliza  hufunza  hutoa
14   yote  kwote  yoyote  kwao
15  hili  ili   kwao   bila 

 

Kutoka swali la 16 mpaka 30, jibu swali ukifuata maagizo uliyopewa.

  1. Sehemu jua linapochomoza huitwa mashariki au
    1. machweo
    2. matlai
    3. mapambazuko
    4. mgharibi
  2. Fundi hutumia ______ kupima urefu wa ukuta.
    1. timazi
    2. filifili
    3. utepe
    4. dira
  3. Nini umoja wa:-
       Nyaya za runinga zimenunuliwa.
    1. Waya za runinga umenunuliwa.
    2. Waya wa runinga umenunuliwa
    3. Waya ya runinga imenunuliwa
    4. Waya ya runinga umenunuliwa
  4. Kanusha:-
       Ningeenda shuleni ningemwona.
    1. Ningeenda shuleni nisingemwona.
    2. Ningekwenda shuleni nisingemwona.
    3. Nisingenenda shuleni ningemwona.
    4. Nisingeenda shuleni nisingemwona.
  5. Kwenye mguu wa jogoo ukucha wa nyuma wa kidole huitwa
    1. kucha
    2. kining'inio
    3. kipi
    4. kikwaru
  6. Nini kinyume cha konda?
    1. Wanda
    2. Wandi
    3. Mnono
    4. Kondoka
  7. Unda jina kutokana na kitenzi amka?
    1. Kuamka
    2. Kuamkua
    3. Mwamko
    4. Mwamkue
  8. Pesa zinazotolewa kuanzisha au kupanua biashara huitwa
    1. kianzishi
    2. mali
    3. mtajio
    4. mtaji
  9. Mlio wa tembo ni mteteo, kwa hivyo ndovu
    1. huteta
    2. hutatea
    3. hutetea
    4. hutea
  10. Ishara hii ya barabarani ina maana kuwa
    C8KISWAHILIMT2S72023Q1
    1. nenda kushoto
    2. nenda kulia
    3. barabarani inapinda kushoto
    4. barabara inapinda kulia
  11. Kichala ni cha matunda kama vile kipeto ni cha
    1. kuni
    2. kipepeo
    3. barua
    4. ndizi
  12. Nini kisawe cha kiamshakinywa?
    1. Chai
    2. kisebeho
    3. Staftahi
    4. kisebeho
  13. Tegua kitendawili:-
       Anakukondolea macho lakini hakujui.
    1. Kioo
    2. Mbwa
    3. Picha
    4. Televisheni
  14. Maana ya tashbihi "Banana kama kuni uchangani" ni
    1. ingia mchangani kama kuni
    2. songamana sana katika sehemu fulani
    3. sukumana kama kuni kwenye tita
    4. ingiliana bila kubaguana
  15. Sayari ipi ni jangwa lenye mchanga mkavu wa rangi ya hudhurungi?
    1. Dunia
    2. Zuhura
    3. Mshtarii
    4. Mirihi

Soma ufahamu ufuatao kwa makini kisha ujibu maswali 31-40.

Yamkini watu kadha wa kadha nchini Kenya wamejawa na mawazo ya kughadhabisha sana. Hili linatokana n matukio mbali mbali nchini mwetu. Mara kwa mara nchi ya Kenya hukumbwa na visanga si haba. Sio vya afya, sio vy.. elimu, sio vya kisiasa hata vya hali ya anga vyatokea.

Katika ulingo wa elimu, wengi hawakubaliani na mabadiliko. Kwa nini? Wanaoshika usukani wanahofiwa kuendelez maudhui yao bila kujali maslahi ya washikadau wote. Kwa mfano, wanafunzi wengi nchini, mathalani shule za msingi n Daraja ya awali ya upili, wanaipata elimu lakini katika hali duni.

Imechukua takribani muhula mmoja kupata vitabu vya kuwaongoza masomoni. Hili limechangia pakubwa kuzu malumbano kati ya washikadau.

Siasani malumbano hayakomi. Baada ya kupata katiba mpya miaka zaidi ya kumi, bado wanasiasa wana uroh wa kuibadilisha. Hili ni kwa maslahi yao bali sio wananchi. Wengine wao huwashawishi wananchi kuandamana ili kujifai wenyewe. Imebidi viongozi wa kidini na maslahi ya kijamii kuingilia kati kuokoa Wakenya.

Je, Wakenya watampata mwelekezi mwema lini?

  1. Kwa nini Wakenya wana mawazo ya kughadhabisha?
    1. Wameona mengi
    2. Wanafanya vituko vingi
    3. Vituko mbalimbali nchini
    4. Vituko vya kisiasa
  2. Kulingana na taarifa ni kweli kuwa
    1. Kenya kuna visanga vingi
    2. kuna visanga vinne
    3. Kenya haina visanga
    4. Kenya kuna visanga vya siasa
  3. Kwa kurejerea taarifa ni nani haaminiki?
    1. Mwananchi
    2. Wanasiasa
    3. sekta ya elimu
    4. Hakuna
  4. Maana ya shika usukani kama ilivyotumika ni
    1. kuendesha gari
    2. kuelekeza
    3. kuongoza
    4. kushika vitu vingi
  5. Elimu iko katika hali "duni" kumaanisha
    1. haifai
    2. hali isiyoeleweka
    3. haifuati kanuni zinazofaa
    4. ni nzuri
  6. Kulingana na taarifa hii Kenya ina viongozi
    1. walafi
    2. werevu
    3. wana harakati
    4. wazuri
  7. Kenya imechukua muda mrefu kupata
    1. viongozi wema
    2. elimu
    3. washikadau
    4. malumbano
  8. Nani wanaohusika kwenye malumbano ya kubadili katiba?
    1. Wanasiasa
    2. Viongozi
    3. Wananchi
    4. Wote
  9. Taarifa hii ina mafunzo yapi?
    1. Wananchi wanataka katiba
    2. Taifa linahitaji kila mtu
    3. Bila elimu hakuna nchi
    4. Wakenya hawana mwelekezi
  10. Kichwa mwafaka cha taarifa hii ni
    1. Masaibu ya Wakenya
    2. Kenya mpya
    3. Viongozi wa Kenya
    4. Kenya na Wakenya

Soma shairi hili kisha ujibu maswali 41-50.

Waja nawaulizeni, binadamu ndiye nani?

Ni swali mboga nadhani, hivyo basi nijibuni,

Ni elimu ya shuleni, wanajigamba wengine,

Binadamu sio kimo, bali ni utu jamani.

 

Kawa na sura murua, kajiringa ana utu,

Kajikwatua kwatua, eti katatua utu

Mja sio sura safua, urembo pia sio mtu,

Binadamu sio kimo, bali ni utu jamani.

 

Karauka kutafuta, mapeni aitwe mtu,

Wakajirimbikita, sikini kanyimwa katu,

Ukatae katakata, kudhulumu asi kitu,

Binadamu sio kimo, bali ni utu jamani.

 

Hasimu ukimpenda, ni utu ninakwambia,

Kuwa na nidhamu dada, binadamu utakua,

Kaka heshima sio donda, utu bora natambua,

Binadamu sio kimo, bali ni utu jamani.

  1. Mloto katika ubeti wa kwanza una mizani mingapi?
    1. 16
    2. 7
    3. 4
    4. 15
  2. Kulingana na mshairi mja hujigamba kwa nini?
    1. Ana mali mengi
    2. Ana utu
    3. Ana elimu yake
    4. Ana elimu ya shuleni
  3. Taja mleo wa ubeti wa tatu.
    1. Binadamu sio kimo, bali ni utu jamani
    2. Wakajirimbikita, sikini kanyimwa katu
    3. Ukatae katakata, kudhulumu asi kitu
    4. Mja sio sura safua, urembo pia sio mtu
  4. Shairi hili ni la bahari gani?
    1. Tarbia
    2. Tathnia
    3. Tathlitha
    4. Tashlitha
  5. Mja hutafuta mapeni
    1. apate mali
    2. apate utu
    3. aonekane na utu
    4. aonekane mwenye utu
  6. Kulingana na mshairi utu huletwa na
    A. kuwa mrembo
    B. kuwa na elimu
    C. wale wenye mali na elimu
    D. nidhamu na heshima
  7. Kujikwatua kama ilivyotumika ina maana
    1. kutafuta utu
    2. kuwa na utu
    3. kutafuta urembo
    4. kujiringa
  8. "Binadamu sio kimo, bali ni utu jamani" ni
    1. kichwa cha ushairi
    2. kituo cha ushairi
    3. mkarara wa ushairi
    4. mwisho wa ushairi
  9. Kutokana na ushairi huu, tunajifunza kuwa
    1. utu hupatikana kwa wenye elimu
    2. jikwatue upate utu
    3. bila heshima na nidhamu huna utu
    4. hakuna mja asiye na utu
  10. Kichwa mwafaka cha ushairi huu ni
    1. Kimo cha binadamu
    2. Binadamu na utu
    3. Binadamu ni utu
    4. Utukufu

INSHA

Umepewa dakika 40 kuandika insha yako.

Andika insha ya kusisimua ukianzia kwa maneno haya:

Siku yenyewe ilikuwa angavu. Joto la kadiri lilishamiri huku upepo mwanana ukivuma kutoka mashariki kuelekea magharibi. Ilikuwa siku iliyongojewa..........................

Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions - Class 8 Opener Exams Term 2 2023 Set 7.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students