Wednesday, 08 March 2023 09:02

Kiswahili Questions and Answers - Grade 4 Opener Exams Term 1 2023 Set 2

Share via Whatsapp

Soma kifungu hiki kisha ujibu swali la 1-5.
GRD4KISW1

Siku moja tulienda shambani na mwalimu wetu Bi. Zawadi. Ilifaa darasa letu la 4B watoe magugu shambani, wanafunzi wa darasa la 4A. Walifyeka nyasi ndefu zilizokuwa karibu na vyoo vya wasichana, nao wanafunzi wa darasa la 4D walipalilia miharagwe. Tulifanya kazi kwa bidii sana. Tulilima hadi jioni wakati tulipowaona viboko wawili wakija upande wetu. Tulijawa na woga mwingi sana. Kila mmoja wetu alikimbia huku na kule akipiga nduru. Wanafunzi wawili wa darasa la 4D walianguka chini na kuumia vibaya. Mmoja wa darasa letu alitegwa na kuchomwa na mwiba. Alipelekwa hospitalini kwa haraka. Walimu walikuja na kuwafukuza viboko hao. Ilikuwa siku mbaya sana kwetu!

Maswali

 1. Mwanafunzi anayezungumza ni wa darasa gani?
  1. 4C
  2. 4D
  3. 4A
  4. 4B
 2. Wanafunzi wa Gredi ya 4D walifanya nini?
  1. Kupalilia mahindi.
  2. Kulima.
  3. Kupalilia miharagwe.
  4. Kufyeka nyasi.
 3. Ni nini kilichomfanyikia mwanafunzi aliyepelekwa hospitalini?
  1. Alidungwa na mwiba.
  2. Alitegwa na mkulima.
  3. Alichomwa na mkuki.
  4. Alikanyagwa na viboko.
 4. Wanafunzi wangapi wa darasa la 4D walioumia vibaya?
  1. Wanne
  2. Wawili
  3. Watatu
  4. Wote.
 5. Ni shughuli ipi haikufanyika shambani?
  1. Kufyeka
  2. Kuvuna
  3. Kupalilia
  4. Kulima.

Soma makala haya kisha ujibu swali 6-10.

Juma ni mwanafunzi mwenye bidii sana. Yeye huja shuleni kila siku. Mara nyingi humaliza kazi yake upesi sana. Kazi yenyewe huwa bila makosa yoyote. Walimu, wanafunzi na wazazi wake wanampenda sana. Juma huwasaidia wanafunzi wenzake wanaoshindwa na kazi walizopewa darasani. Siku moja ya Ijumaa, Juma alitoka kwenda kwa rafiki yake Joni. Alikuwa amekamilisha kazi zake zote za siku hiyo. Alitoka nje ya lango lao na kulifunga. Kabla ya kulifunga lango, mtu mmoja alimshika mkono. Moyo wake ulimpiga kwa kasi kwa sababu hakumjua mtu huyo. Alijaribu kutoroka lakini hakuweza Mtu yule alimwamuru Juma warudi nyumbani kwao amfungulie mlango. Juma alipiga mayowe. Majirani walikuja kumsaidia kumkamata yule mwizi. Polisi walipigiwa simu wakaja na kumtia pingu kisha kumpeleka jela.

Maswali

 1. Juma hufanya kazi yake
  1. polepole.
  2. kiholela
  3. kwa haraka
  4. bila kujali.
 2. Watu wafuatao wametajwa kwenye kifungu kama wanampenda Juma isipokuwa
  1. wazazi
  2. wafanyakazi
  3. walimu
  4. wanafunzi.
 3. Juma alitaka kwenda kwa rafiki yake lini?
  1. Ijuma.
  2. Alhamisi
  3. Ijumaa.
  4. Jumamosi
 4. Ni nani aliyemshika Juma mkono?
  1. Rafiki yake.
  2. Mama yake.
  3. Mwizi.
  4. Polisi.
 5. Polisi walipokuja walifanya nini?
  1. Walimtia pingu mwizi.
  2. Walimfungulia mlango Juma.
  3. Walijaribu kumtoroka.
  4. Walimpiga mwizi.

Soma ufahamu kisha ujibu swali 11-15.

GRD4KISW2

Sokoni ni pahali panapouzwa bidhaa mbalimbali kama vile mboga, matunda, nafaka, nguo, mifugo na vitu vinginevyo. Soko pia huitwa cheto. Mimi hupenda soko safilisilo na wadudu hatari wanaosambaza magonjwa. Soko chafu huwavutia wadudu hatari kama vile nzi ambao wanaweza eneza ugonjwa wa kipindupindu. Soko letu linaitwa Sufi. Soko hili hupendeza sana kwa sababu huwa safi na lina vitu vingi ajabu! Hupata wateja wengi sana hata kutoka kaunti nyingine. Siku ya Ijumaa ndiyo siku maalum ya biashara ya matunda na mboga Watu hufurika sana sokoni kwetu siku hiyo ili wanunue matunda kama vile matufaha, machungwa, mapapai, mifenesi, limau na maparachichi. Mifugo huuzwa na kununuliwa siku ya Jumanne. Fahali haswa ndio wauzwao siku hiyo. Naipenda soko Sufi sana!

Maswali

 1. Kipi kisichouzwa sokoni kulingana na kifungu?
  1. Vitanda
  2. Nafaka.
  3. Matunda
  4. Mavazi.
 2. Wadudu wanaoletwa na uchafu husambaza ugonjwa gani?
  1. Malaria
  2. Tumbo
  3. Kipindupindu
  4. Kansa.
 3. Mbona soko Sufi hupata wateja wengi?
  1. Lina bidhaa nyingi.
  2. Kuna watu wengi huko.
  3. Ni kubwa.
  4. Vitu ni bei rahisi.
 4. Wanyama huuzwa siku gani?
  1. Ijumaa.
  2. Jumamosi.
  3. Jumanne.
  4. Jumatano.
 5. Fahali ni mnyama yupi? Ng'ombe
  1. jike
  2. dume
  3. mdogo
  4. mnono.

Soma mtungo ufuatao kisha ujaze mapengo kwa kutumia maneno uliyopewa

Kenya ni                  ya kupendeza sana. Watalii wengi hufurahia kuzuru taifa                    .Kuna mbuga                       sana Kenya. Mojawapo ya mbuga hizo ni Maasai Mara. Mbuga hii ina wanyama wengi kama vile                       ambao huiletea Kenya pesa za kigeni. Nalipenda taifa langu sana. Mimi ni                  .

16. A. inchi    B. nchi   C.mahali    D. nji  
 17. A. hilo   B. lile    C.hili    D. hii 
  18. A. nyingi    B. mingi   C. mengi   D. wengi 
 19. A. suala    B. swali    C.suara   D. swara 
 20. A. jambazi   B. mzalendo    C. mwafrika    D. mbunge  
 1. Kanusha sentensi hii; Vikapu vinauzwa.
  1. Vikapu haviuzwi.
  2. Vikapu havitauzwa.
  3. Kikapu kinauzwa.
  4. Vikapu havikuuzwa.
 2. Tegua kitendawili: Fatuma mchafu
  1. Nyumba.
  2. Ufagio
  3. Nguruwe
  4. Nzi
 3. Chagua alama ifaayo ya uakifishi.
  Je, ulimtembelea shangazi
  1. .
  2. ,
  3. ?
  4. !
 4. Tarakimu '82' kwa maneno ni
  1. thelathini
  2. themanini na mbili
  3. thelathini na mbili
  4. nane mbili.
 5. Chagua sentensi iliyo kwenye nafsi ya tatu wakati ujao.
  1. Mimi nitachora.
  2. Yeye anasoma.
  3. Wewe ulicheka.
  4. Wao watacheza.
 6. Jaza pengo: Februari, Machi, Aprili,                    
  1. Juni
  2. Julai
  3. Mei
  4. Agosti
 7. Chagua neno lenye sauti mbili zinazotamkwa pamoja.
  1. maji 
  2. bidii
  3. fyeka
  4. kazi.
 8. Anayewatibu wagonjwa huitwa
  1. nesi 
  2. tabibu
  3. rubani
  4. muuguzi.
 9. Tumia -angu' kujaza pengo katika sentensi hii.
  Mkate                   
  1. zangu
  2. yangu
  3. wangu
  4. langu.
 10. Paka ameketi wapi?
  GRD4KISwqn30
                  ya meza.
  1. Chini 
  2. Kando
  3. Ndani
  4. Nje.

Andika insha fupi kuhusu picha hii.
GRD4KISWinsha

MWONGOZA ;

 1. D
 2. C
 3. A
 4. B
 5. B
 6. C
 7. B
 8. C
 9. B
 10. A
 11. A
 12. C
 13. A
 14. C
 15. B
 16. B
 17. C
 18. A
 19. D
 20. B
 21. A
 22. B
 23. C
 24. B
 25. D
 26. C
 27. C
 28. B
 29. C
 30. A
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Grade 4 Opener Exams Term 1 2023 Set 2.


Tap Here to Download for 30/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students