Wednesday, 08 March 2023 09:05

Kiswahili Questions and Answers - Grade 4 Opener Exams Term 1 2023 Set 3

Share via Whatsapp

Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali 1-5

G4swaT1T23001P1

Amani: (Kwa furaha) Hujambo Johari!
Johari: (Akitabasamu) Sijambo Amani. Umeamkaje? Amani: Vyema labda wewe.
Johari: Ningetaka tujadiliane vile tutakavyoyatunza mazingira ya shule yetu muhula huu.
Amani: Aha! Naona unayajali mazingira yetu.
Johari: Naam! Baada ya likizo ndefu takataka zimeenea kila mahali, nyasi ni ndefu na madarasa yamejaa vumbi.
Amani: Ni jukumu letu kama wanafunzi kuhakikisha tumeifanya shule yetu kuwa safi.
Johari: Tunafaa kutafuta fyekeo, reki na fagio ili kutekeleza shughuli yetu.
Amani: Mwalimu wetu wa darasa atatusaidia kupata vifaa hivyo katika stoo ya shule.
Johari: Tunafaa tuongee na wanafunzi wenzetu ili tujipange  vizuri kutekeleza shughuli hii.
Amani: Tutajigawa katika vikundi mbalimbali ili kila mahali shuleni pawe safi.
Johari: Haya basi twende tukaongee na wenzetu.

  1. Mazungumzo uliyoyasoma yalifanyika wakati gani?
    1. Jioni
    2. Adhuhuri
    3. Asubuhi
    4. Usiku
  2. Amani na Johari wanazungumza kuhusu nini?
    1. Usafi wa mazingira ya shule
    2. Usafi wa nyumbani kwao
    3. Usafi wa darasa lao
    4. Usafi wa uwanja wa shule
  3. Wanafunzi watatumia kifaa gani kufyeka nyasi ndefu?
    1. Ufagio
    2. Reki
    3. Jembe
    4. Fyekeo
  4. Ili kila mwanafunzi apate kazi yake wanafaa kufanya nini? 
    1. Kujigawa katika makundi. 
    2. Kuzungumza
    3. Kumwomba mwalimu awapatie vifaa
    4. Kuosha darasa kwanza
  5. Ni gani kati ya hizi si shughuli ya kutunza usafi wa mazingira
    1. Kufagia
    2. Kufyeka
    3. Kuoga
    4. Kuokota takataka

Soma hadithi ifuatayo kisha ujibu maswali 6-9   

G4swaT1T23001P2

Bwana Bakari alikuwa mfugaji hodari wa kuku. Alikuwa na majogoo watano na kuku arubaini na watano wa kutaga mayai. Kuku hawa huitwa koo.

Koo walikuwa wameanza kutaga na kwa hivyo baada ya siku kadhaa wangeyalalia mayai na kuangua vifaranga.

Bwana Bakari aliwatunza kuku wake vizuri. Aliwapatia chakula na maji ya kutosha. Pia aliwachanja kila mara ili wasipate magonjwa.

Wanafunzi hupenda kumtembelea Bwana Bakari ili kujifunza ufugaji wa kuku.

  1. Bwana Bakari hufanya kazi gani?
    1. Kulima
    2. Kuuza mayai
    3. Kufuga kuku
    4. Kuangua vifaranga
  2. Kuku anayetaga mayai huitwaje?
    1. Koo
    2. Jogoo
    3. Kifaranga
    4. Pora
  3. Bwana Bakari hakuwatunza kuku wake kwa _________________________
    1. kuwapa chakula
    2. kuwapa maji
    3. kuwachanja
    4. kuwaosha
  4. Kwa nini Bwana Bakari aliwachanja kuku wake?
    1. Ili wasipate magonjwa
    2. Ili wapate vifaranga
    3. Ili watage mayai mengi
    4. Ili waongezeke

Soma hadithi ifuatayo kisha ujibu maswali 10-12

G4swaT1T23001P3
Mwema alitumwa dukani na mama yake kununua bidhaa. Alipewa noti ya shilingi mia mbili. Alimpata mwuzaji na kuagiza bidhaa zifuatazo:

  1. Sukari nusu kilo - shilingi sabini na tano.
  2. Mkate - shillingi sabini
  3. Maziwa pakiti moja - shilingi hamsini

Baada ya kupewa bidhaa hizo alipatiana pesa, akapewa risiti na baki ya pesa.

  1. Tunaweza tukamwita Mwema nani?
    1. Mnunuzi 
    2. Muuzaji
    3. Mchuuzi
    4. Dalali
  2. Ni bidhaa gani ghali kuliko zote?
    1. Mkate
    2. Sukari
    3. Maziwa
    4. Zote
  3. Mwema alipewa baki ya shillingi ngapi?
    1. Kumi
    2. Kumi na tano
    3. Tano
    4. Hatujaambiwa

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 13-15.

Mcheshi alisafiri na kwenda marekani. Aliishi katika nchi hiyo kwa miaka mitano. Hata hivyo hakuwahi kuisahau nchi yake ya Kenya. Kila wakati alipoikumbuka nchi yake alitamani siku ya kurudi ifike haraka.

Mcheshi alikuwa na sababu nyingi za kuipenda Kenya. Nchi ya Kenya ina wananchi wanaopenda amani. Kuna milima na mabonde ya kupendeza. Kuna mito, maziwa na bahari. Isitoshe Kenya ina wanyamapori wengi kama vile: Simba, ndovu, chui, kifaru na twiga.

Siku ya kurudi ilipofika, Mcheshi alipanga mizigo yake, akaenda katika uwanja wa ndege, akaiabiri na kurudi Kenya. Alipofika aliwapata baba na mama yake wamemsubiri. Walikumbatiana kwa furaha kisha wakaenda nyumbani.

  1. Mcheshi alisafiri kwenda nchi gani?
    1. Kenya
    2. Marekani
    3. Uingereza
    4. Ethiopia
  2. Kulingana na kifungu gani kati ya hizi si sababu ya Mcheshi kuipenda Kenya?
    1. Wananchi wenye amani
    2. Milima na mabonde
    3. Wanyamapori
    4. Kilimo
  3. Katika uwanja wa ndege, Mcheshi alikuwa amesubiriwa na _______________________
    1. wazalendo
    2. wazazi wake
    3. ndugu zake
    4. marafiki

Jaza pengo kwa kutumia majibu yafaayo

Bendera ___16___ Kenya ina rangi ___17___. Rangi iliyo juu kabisa ni ___18___ katikati ya bendera yetu kuna mikuki ___19___ na ngao. Shuleni huwa tunaipandisha bendera ili kuonyesha ___20___ wetu.

   A   B   C   D 
 16.   wa   ya   cha   la
 17.  nne   minne   wanne   minne 
 18.  nyeupe   nyeusi   nyekundu   kijani 
 19.  mbili  wawili   mbili   miwili 
 20.  uzalendo   urafiki   uadui   uhodari 
  1. Tazama picha hizi kisha ujibu swali
    G4swaT1T23001P4
    Vifaa hivi hutumika wapi?
    1. Shuleni
    2. Sokoni
    3. Shambani
    4. Dukani
  2. Musa amemsindikiza rafiki yake hadi kituo cha mabasi. Wanapoagana Musa atamwambiaje?
    1. Kwaheri
    2. shikamoo
    3. Usiku mwema
    4. majaliwa
  3. Ni sentensi gani si sahihi?
    1. Mimi ninacheza. 
    2. Wewe unasoma
    3. Yeye anaandika
    4. Wewe anacheka
  4. Tazama picha hii kisha utumie kihusishi mwafaka.
    G4swaT1T23001P5
    Maua yako __________________ meza.
    1. juu ya
    2. kando ya
    3. chini ya
    4. mbele ya
  5. Kanusha sentensi ifuatayo: Uliwasimulia wanafunzi hadithi.
    1. Hutawasimulia wanafunzi hadithi.
    2. Hatawasimulia wanafunzi hadithi.
    3. Hukuwasimulia wanafunzi hadithi. 
    4. Huwasimulii wanafunzi hadithi.
  6. Badilisha sentensi hii katika wingi: Kitabu chake kimepotea.
    1. Vitabu vyao vimepotea.
    2. Vitabu vyake vimepotea.
    3. Kitabu chao kimepotea.
    4. Vitabu vyetu vimepotea.
  7. Ni kitendo gani hakijaambatanishwa na kinyume chake?
    1. Cheka - lia
    2. Enda-rudi
    3. Kubali-kataa
    4. Andika - soma
  8. Jaza mapengo kwa jibu sahihi:
    Farasi alikimbia _________________________ naye kobe alitembea ______________________________.
    1. polepole, haraka
    2. haraka, polepole
    3. polepole, polepole
    4. haraka, haraka
  9. "Ni sentensi gani yenye kikomo?
    1. Unataka nini hapa?
    2. Kesho nitatuzwa zawadi:
    3. Kumbe unanidanganya.
    4. Nilikula wali, chapati, ugali.....
  10. Tazama picha kisha ujibu swali.
    G4swaT1T23001P6
    Ndege huyu and twa nani? 
    1. Tausi
    2. Mbuni
    3. Bata
    4. Njiwa

INSHA

Kuandika(Alama 10)

Umepewa dakika 40 kuandika insha yako. Andika insha juu ya 

                                                 MWALIMU WANGU WA DARASA

______________________________________________________________________________________

MARKING SCHEME

  1. C
  2. A
  3. D
  4. A
  5. C
  6. C
  7. A
  8. D
  9. A
  10. A
  11. B
  12. C
  13. B
  14. D
  15. B
  16. B
  17. A
  18. B
  19. D
  20. A
  21. C
  22. A
  23. D
  24. A
  25. C
  26. A
  27. D
  28. B
  29. C
  30. B
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Grade 4 Opener Exams Term 1 2023 Set 3.

Tap Here to Download for 30/-

Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students