Monday, 27 February 2023 13:43

Kiswahili Lugha Questions and Answers - Grade 6 Opener Exam Term 1 2023 Set 1

Share via Whatsapp

Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali 1-5.

(Mwalimu na wanafunzi wamo katika mjadala kuhusu umuhimu wa kuyatunza mazingira
Bi Muli:          Salaam aleikum wanafunzi. M hali gani?
Wanafunzi:    (Wakiamka sawia) Njema Bi Muli, shikamoo.
Bi. Muli:         Marahaba (anawaashiria wakae) Naam, leo ningependa tuzungumze kuhusu namna n umuhimu wa kuyatunza mazingira kwa                         kuwa mazingira machafu huweza kutuletea magonjwa hatari.
Sofa:              Samahani mwalimu, mazingara ni nini? (Akionyesha uso wa kuchanganyikiwa
Bi Muli:          Sofia, si mazingara, ni mazingira. Haya ni yote ambayo...
Peru:              (Akiunyanyua mkono wake) Samahani mwalimu, naweza kulijibu swali hilo. Haya ni yote ambayo yanatuzunguka.
Bi Muli:          Makofi kwa Peru. (Wenzake wanampigia makofi kwa kujibu swali kwa usahihi). Safi. Ili kuyalinda mazingira, tunaweza kukata                        nyasi ndefu zinazowafuga mbu.
Maloba:         Vile vile, tunaweza kuhakikisha vyanzo vya maji vi safi. Hivi ni kama vile mito, maziwa na mabwawa.
Ali:                 Nadhani kuwa kuna hatari aidha katika kutumia mbolea za madukani kiholela. Zikitumiwa kupita kiasi huweza kuathiri udongo                         na hatimaye vyanzo vya maji. 
Bi Muli:           Vyanzo vya maji vinapoathirika, viumbe vya majini kama vile samaki, mamba, mimea na wanyama wengine huweza                                       kuathirika pakubwa. Kesho tutaandika insha kuhusu umuhimu wa kuyatunza mazingira. Kwaherini kwa sasa.
Wote:              Kwaheri ya kuonana mwalimu.

 1. Kulingana na maelezo ya mwalimu, mazingira machafu yana madhara gani? Huweza
  1. kuchafua vyanzo vya maji.
  2. kusababisha magonjwa. 
  3. kudumisha afya bora.
  4. kutukinga dhidi ya magonjwa.
 2. Peru alipigiwa makofi kwa sababu
  1. alilijibu swali la mwanafunzi mwenzake kwa usahihi.
  2. alikuwa mwanafunzi bora darasani mwao.
  3. alijaribu kulijibu swali la Sofia.
  4. alishindwa kulijibu swali la Sofia.
 3. Kulingana na mazungumzo haya, mbolea za madukani zikitumika kupita kiasi 
  1. huweza kusababisha hali mbaya ya anga.
  2. huweza kuchafua hewa.
  3. huathiri udongo na vyanzo vya maji. 
  4. huchafua pakubwa vyanzo vya maji
 4. Vyanzo vya maji vínapoathirika,
  1. wanyama wa porini huangamia. 
  2. nyuni wa angani hufa.
  3. wanadamu hupata taabu.
  4. wanyama wa majini huathirika.
 5. Chanzo gani cha maji hakijatajwa katika mazungumzo haya?
  1. Mito.
  2. Mvua.
  3. Mabwawa.
  4. Maziwa.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswall 6 hadi 8

Rununu yake ilikiriza mara kadhaa lakini akashindwa kuiwahi. Kichwa chake kilimwanga vilivyo. Usiku uliotangulia alikuwa amepiga maji na kulewa chakari. Hakuelewa alivyofika kitandani pake. Mlaraha alikuwa mwizi hatari. Hii ilikuwa shughuli haramu na hatari kweli kweli. Aliitazama simu yake ya mkononi ilivyokuwa imechakaa. Ghafla, mlango wake ukabishwa kwa kishindo. Alisita kidogo huku akijiuliza kama kweli alikuwa na ahadi ya kukutana na yeyote asubuhi hiyo.

Kufumba na kufumbua, pu! Mlango ulipigwa teke na kuanguka kando. Mlangoni walisimama maafisa wanne wa polisi na bastola huku wawili wakiwa na pingu mikononi. Mlaraha aliinua mikono juu ishara ya kusalimu amri. Moyoni alijua kuwa zake arubaini zilikuwa zimetimia. Naam, uhalifu haulipi chochote.

 1. Mlaraha hakuweza kuiwahi rununu yake kwa kuwa
  1. kichwa chake kilikuwa kizito.
  2. ilikuwa mbali.
  3. hakutaka kufanya hivyo.
  4. aliogopa kuzungumza na aliyekuwa akipiga.
 2. Chagua orodha ya sifa za Mlaraha kulingana na kifungu.
  1. Mwizi, mpole.
  2. Mlevi, mwizi.
  3. Mjeuri, mlevi.
  4. Mwizi, katili.
 3. Ni kweli kuwa waliobisha mlango walikuwa
  1. wenzake Mlaraha katika wizi.
  2. majirani waliotaka kumjulia hali Miaraha.
  3. maafisa wa polisi.
  4. waumini wa dhehebu aliloshiriki.
 4. Methali gani inayoweza kutumika kufupishia kisa hiki?
  1. Pwagu hupata pwaguzi.
  2. Mgaagaa na upwa hali wali mkavu. 
  3. Kawia ufike.
  4. Siku za mwizi ni arubaini.

Sema kifungu kifuatacho kisha ulibu maswoll 10 hadi 12   

Uhalifu ni hali ya kutenda kinyume na zinavyohitaji sheria za nchi ambazo siku zote huongozwa na katiba. Kunavyo viwango mbalimbali vya uhalifu katika jamii. Uhalifu hutendeka katika maeneo mbalimbali. Hata hivyo, kuna njia kadhaa za kukabiliana na uhalifu. Kwanza, wananchi wakiacha tabia za kuwaficha wahalifu miongoni mwao, uhalifu utapungua. Vile vile, wale ambao hupokea hongo wanastahili kufunguliwa mashtaka. Si hayo tu, uhalifu aidha huweza kupungua iwapo sehemu mbalimbali za umma kama vile afisini zitawekewa kamera za siri. Kwa jumla, kila mwanajamii akisimama kidete kupambana na uhalifu, tutaweza kujivunia kupungua kwa uhalifu.

 1. Mwandishi ametaja njia ngapi za kukabiliana na uhalifu?
  1. Tano.
  2. Nne
  3. Mbili.
  4. Tatu.
 2. Kulingana na habari hii, kamera za siri zinaweza kudhibiti uhalifu
  1. nyumbani.
  2. afisini.
  3. shuleni
  4. sokoni.
 3. Kwa jumla, jukumu la kudhibiti uhalifu ni jukumu la nani?
  1. Serikali.
  2. Watu wazima.
  3. Kila mmoja.
  4. Wazazi.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 13 hadi 15.

Shughuli kama vile kuogelea, kandanda, riadha na urukaji viunzi huitwa michezo. Shughuli hizi si muhimu tu katika kuijenga miili yetu bali pia huchangia kuwaleta watu pamoja. Michezo baina ya shule mbalimbali huwaleta wanafunzi pamoja ambapo wao huweza kubadilishana mawazo yanayoweza kuinua viwango vyao vya kimasomo. Shughuli za kimichezo aidha huchangia kutukinga dhidi ya magonjwa kama vile uzito wa mwili, ambayo hatimaye huweza kusababisha maradhi ya moyo. Baadhi ya wananchi hutumia michezo kama kitegauchumi cha kuwaletea pesa. Baadhi ya wanaspoti wamewahi kuiletea nchi yetu nishani na medali mbalimbali na hivyo kuiweka nchi yetu katika nafasi bora kimichezo.

 1. Chagua kauli isiyo sahihi kulingana na ufahamu.
  1. Shughuli za kimichezo si muhimu katika kuijenga miili yetu.
  2. Michezo haichangii katika kujenga miili yetu pekee.
  3. Wakati mwingine michezo huandaliwa baina ya shule mbalimbali.
  4. Baadhi ya watu hutumia michezo kama njia ya kujipatia riziki.
 2. Kulingana na habari hii, uzito wa mwili hatimaye huweza kusababisha
  1. mauti.
  2. uvivu.
  3. maradhi ya ngozi.
  4. maradhi ya moyo.
 3. Nchi yetu inapopata nishani na medali, 
  1. wananchi wengi hujiunga na spoti.
  2. hadhi yake kimichezo huinuka.
  3. hupoteza heshima yake kimichezo 
  4. huwa miongoni mwa mataifa yaliyotajirika.

Soma kifungu kifuatacho. Chagua jibu lifaalo zaidi kati va vale uliyopewa.

Mtoto ana haki ___16___. Yapo inahitaji ya kimsingi ambayo ni makazi, lishe na ___17___ haki ya mtoto kupata elimu___18___serikali ikaanzisha elimu ya bure katika shule za umma.___19___ anayemnyima intoto nafasi ya___20___shuleni lazima afikishwe mahakamani.

       A       B          C        D 
 16.   mingi   chache   zote   kadhaa 
 17.  elimu  makao  mavazi   maji 
 18.  sababu   maana   ili   ndipo 
 19.  Wowote   Yeyote  Yoyote   Wote 
 20.  kuenda  kufika  kusomesha   kuanguka 

 

Kutoka swali la 21-30. jibu swall kulingana na maagizo uliyopewa.

 1. Chagua kitenzi kilicholinganishwa visivyo na kinyume chake.
  1. Funga       fungua
  2. Shona       shonua
  3. Nuna         tabasamu
  4. Lia             cheka
 2. Kamilisha tashbihi hii: 
  Mariamu ana maneno mengi kama
  1. chiriku.
  2. tausi.
  3. kasuku.
  4. njiwa.
 3. Chagua ukubwa ws:
  Ndizi hizi ni ndogo.
  1. Dizi hili ni dogo.
  2. Kidizi hiki ni kidogo.
  3. Madizi haya ni madogo.
  4. Vidizi hivi ni vidogo.
 4. Chagua ukanusho wa sentensi ifuatayo:
  Wewe ulikuwa mgonjwa.
  1. Wewe haukuwa mgonjwa.
  2. Wewe hujawa mgonjwa.
  3. Wewe huwi mgonjwa.
  4. Wewe hukuwa mgonjwa.
 5. Chagua sentensi iliyo katika hali timifu.
  1. Mboso atauimba wimbo mpya.
  2. Kadogo amemaliza kuandika.
  3. Upepo haukuvuma kwa fujo.
  4. Walimu wanazungumza mkutanoni.
 6. Chagua wingi wa sentensi ifuatayo:
  Ufagio ulinunuliwa sokoni.
  1. Fagio zilinunuliwa masokoni.
  2. Ufagio zilinunuliwa sokoni.
  3. Fagio ulinunuliwa masokoni. 
  4. Ufagio ulinunuliwa masokoni.
 7. Chagua orodha ya nomino zilizo katika ngeli tofauti.
  1. Cheo, chupa.
  2. Magari, maua.
  3. Kiwavi, kipofu.
  4. Mitego, mikoba.
 8. Ni sentensi gani iliyo katika nafsi ya pili?
  1. Mlitutembelea jana kwa sherehe. 
  2. Alinunuliwa mwanasesere maridadi.
  3. Nimeamua kufanya bidii.
  4. Mwalimu aliyekuwa darasani ametoka.
 9. Chagua methali iliyo tofauti na nyingine kimatumizi.
  1. Kidole kimoja hakivunji chawa.
  2. Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu.
  3. Mkono mmoja haumlei mwana.
  4. Mgaagaa na upwa hali wali mkavu.
 10. Chagua orodha ya majina ambayo ni visawe.
  1. Runinga, redio
  2. Ndovu, Pombe
  3. Mbung'o, ndorobo
  4. Ugonjwa, malaria


MARKING SCHEME

 1. B
 2. A
 3. C
 4. D
 5. B
 6. A
 7. B
 8. C
 9. D
 10. D
 11. B
 12. C
 13. A
 14. D
 15. B
 16. D
 17. C
 18. D
 19. B
 20. A
 21. B
 22. A
 23. C
 24. D
 25. B
 26. A
 27. A
 28. A
 29. D
 30. C
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Lugha Questions and Answers - Grade 6 Opener Exam Term 1 2023 Set 1.


Tap Here to Download for 30/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students