Wednesday, 19 April 2023 07:53

Kiswahili-Lugha Questions and Answers - Grade 6 End Term 1 Exams 2023 Set 2

Share via Whatsapp

Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali 1-5. 

Kila mwaka shuleni kwetu huwa na sherehe za kutoa tuzo kwa walimu, wanafunzi, wafanyakazi na mtu yeyote yule aliyefanya jambo lolote jema au kitendo chochote cha manufaa shuleni. Walimu hutuzwa tuzo kutokana na juhudi zao za kufunza vizuri. Wapishi hutuzwa kwa kuandaa mlo mtamu, usafi na kupika kwa wakati bila kuchelewa. Madereva nao hutuzwa kwa kuendesha magari ya shule kwa utaratibu, kuwa na nidhamu kwa wanafunzi wala kutosababisha ajali yoyote. 

Wafagiaji na wahudumu wengine kama vile mabawabu, waktubi, mahazili na mtarishi pia hutuzwa. Muhula uliopita, sisi wanafunzi tulituzwa kwa maadili, usafi, bidii na matokeo bora katika kila somo. Waliofanya vizuri katika somo la michezo na uhusiano mwema baina ya wanafunzi pia walituzwa. Mimi nilituzwa kwa kuwa bora katika Kiswahili, kuwa na nidhamu kuliko wote, kuwa safi mwaka mzima na pia nikapata tuzo ya kutumia muda wangu vizuri. Nawe pia unaweza ukapata zawadi hata zaidi yangu. Usife moyo kwa sababu ipo siku! 

Maswali 

  1. Kila mwaka shuleni kuna sherehe zipi? Za
    1. kutwezwa 
    2. kutwazwa 
    3. kutuzwa
    4. kutozwa. 
  2. Wafagiaji wa shuleni ni
    1. wapishi
    2. wahazili
    3. waktubi 
    4. matopasi. 
  3. Msimulizi alipata tuzo ngapi? 
    1. Nne 
    2. Nyingi
    3. Moja 
    4. Tano.
  4. Wapishi hupewa zawadi kwa kuzingatia yafuatayo isipokuwa
    1. kupika vyakula vitamu
    2. kupika kwa wakati 
    3. kupika vyakula nadhifu  
    4. kupika haraka.
  5. Ni kweli kusema kuwa
    1. wanafunzi walipewa zawadi za kufuzu masomoni tu
    2. wanafunzi walituzwa kwa kufanya vyema katika nyanja zote shuleni
    3. walimu walipata tuzo kwa kufunza na kuvalia vizuri
    4. madereva walizawadiwa kwa kuendesha magari kwa kasi. 

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 6-10. 

Katika familia au ukoo kuna utaratibu wa maisha. Kuna watu wa rika tofauti. Kuna jinsia tofauti pia. Watu wa familia huishi kwa adabu, heshima na nidhamu zinazofuata umri na jinsia. Kwa hivyo, kuna jinsi ya kusalimiana kwa kuzingatia umri na jinsia. Binadamu ni jamii yenye nidhamu na isiyotenda mambo ovyoovyo kama wanyama wafanyavyo. 

Hata utaratibu wa kula hufuata kanuni na sera maalum. Huo ndio ubinadamu na ubinadamu ndio utu wa watu. Tusifanye mambo shaghalabaghala kama hayawani. Familia isiyo na utaratibu wa nidhamu si familia tena! Familia nyingine hazina salamu wala habari. Hawajiheshimu, hawaheshimu wenzao wala kuheshimiana. Hakuna babu, nyanya, mtoto, baba, mavyaa, halati wala dada. Tukiishi hivyo, yule ng'ombe mwenye mkia na pembe ataishi vipi? 

  1. Ukoo ni kikundi cha watu wanaotokana na
    1. kabila moja
    2. dini moja
    3. nasaba moja
    4. kijiji kimoja.
  2. Binadamu wenye utu na ubinadamu hufanya mambo yao kwa njia gani?
    1. Taratibu 
    2. Ovyoovyo 
    3. Shaghalabaghala 
    4. Kiholela. 
  3. Familia au ukoo ni sawa na
    1. kabila
    2. kijiji
    3. jamii
    4.  jumla.
  4. Ni maamkuzi yapi hutumiwa kulingana na umri? 
    1. Habari 
    2. Sabalheri
    3. Hujambo 
    4. Cheichei. 
  5. Halati ni
    1. dada ya mama
    2. dada ya baba 
    3. kaka ya mama
    4. kaka ya baba. 

Soma shairi hili kisha ujibu maswali 11-15. 

Mkono wa mkulima, ni mgumu kama chuma,
Chakula cha mkulima, ni maharage na sima,
Mtazame mkulima, hatulii juma zima,
Bali huyu mkulima, ndiye mama wa uzima. 

Maisha ya mkulima, ni ya shida tangu zama,
Kibanda cha mkulima, huvuja na kutetema,
Mgongo wa mkulima, daima umeinama,
Bali huyu mkulima, ndiye mama wa uzima. 

Nafasi ya mkulima, mara nyingi ni ya nyuma,
Magarini mkulima, kazi yake kusimama,
Hadharani mkulima, huambiwa hana jema,
Bali huyu mkulima, ndiye mama wa uzima. 

Maswali 

  1. 'Ni mgumu kama chuma' ni fani gani ya Lugha? 
    1. Kitendawili 
    2. Istiara 
    3. Methali 
    4. Tashbihi. 
  2. Kwa nini mgongo wa mkulima daima umeinama? Kwa sababu 
    1. ya kazi yake 
    2. ni mzee
    3. ana shida
    4. nyumba yake ni ndogo.
  3. Hili ni shairi la aina gani? 
    1. Tathlitha 
    2. Tarbia
    3. Ngonjera 
    4. Ukulima.
  4. Kibwagizo cha shairi hili kina maana gani? 
    1. Mkulima ndiye atupaye uhai. 
    2. Kwa chakula cha mkulima tunaishi. 
    3. Mkulima ni mama yetu. 
    4. Mtoto wa mkulima anaitwa Uzima.
  5. Kuna uwezekano mkubwa wa mkulima kupanda mbegu msimu upi? 
    1. Kiangazi 
    2. Kipupwe
    3. Mchoo 
    4. Mafuriko. 

Jaza mapengo kwa majibu mwafaka. 

Kila mnyama ____16____meno ____17____  ya juu na ya chini. Binadamu mtu mzima huwa na meno thelathini na ___18___ .Wanyama wote wana meno ____19____ambayo ____20____sumu kali. 

   A   B    C    D 
 16.   ako na   yuko na   ana   anazo 
 17.   makali  kali   mikali   kubwa 
 18.  miwili  mbili   mawili   viwili 
 19.  mengi  nyingi   mingi   mwingi 
 20.  zina  yana   una   ina 

 

Jibu maswali kulingana na maagizo. 

  1. Maskani  ________________________ hufagiliwa.
    1. zetu
    2. mwetu
    3. petu
    4. yetu 
  2. Baba akikasirika huwa mkali kama ______________________
    1. moto
    2. pilipili
    3. simba
    4. jua
  3. Andika ukubwa wa sentensi ifuatayo. 
    Ndoo zetu zimepasuka.
    1. Mandoo zetu zimepasuka.
    2. Madoo yetu yamepasuka. 
    3. Ndoo zetu zimepasuka.
    4. Mandoo yetu yamepasuka.
  4. Tumia kiashiria sahihi. 
    Ugonjwa _____________________ ni hatari. 
    1. hiyo 
    2. ile 
    3. huo 
    4. iyo 
  5. Nilipokuwa katika ziara, niliona _____________________ ya milima.
    1. safu
    2. mabunda
    3. msafara
    4. milolongo 
  6. Baba yangu amenunua gari _____________________
    1. mpya 
    2. kipya
    3. zipya
    4. jipya.
  7. Chagua kiwakilishi cha idadi katika sentensi ifuatayo. 
    Watu wengi wana gari moja lakini wachache wana pikipiki mbili.
    1. wengi
    2. moja
    3. wachache
    4. mbili.
  8. Kati ya viwakilishi vifuatavyo, ni kipi cha nafsi ya tatu katika wingi? 
    1. Zao 
    2. Yeye 
    3. Nyinyi
    4. Wao.
  9. Tambua kivumishi katika sentensi hii.
    Mama huyo alitembea haraka akafika vizuri.
    1. mama
    2. huyo 
    3. haraka
    4. vizuri 
  10. Kipi si kiungo cha kusafisha damu?
    1. Pafu
    2. Buki
    3. Figo 
    4. Nso. 

INSHA 

Umepewa dakika 40 kuandika insha yako. 

Andika insha ya kusisimua kuhusu mada ifuatayo; 

UCHAGUZI SHULENI MWETU. 

MARKING SCHEME

  1. C
  2. D
  3. A
  4. D
  5. B
  6. C
  7. A
  8. C
  9. D
  10. A
  11. D
  12. A
  13. B
  14. B
  15. C
  16. C
  17. A
  18. C
  19. A
  20. B
  21. D
  22. C
  23. B
  24. C
  25. A
  26. D
  27. C
  28. D
  29. B
  30. A
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili-Lugha Questions and Answers - Grade 6 End Term 1 Exams 2023 Set 2.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students