Monday, 27 March 2023 12:31

Kiswahili Questions and Answers - Grade 5 Mid Term 1 Exams 2023 Set 2

Share via Whatsapp

KUSIKILIZA NA KUZUNGUMZA  

Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali  

G5SWAT1TW23002P1

(Sofi na Patu wako darasani wakifanya shughuli ya wawili wawili katika kipindi cha Kiswahili)
Sofi:  Patu, sogeza dawati lako upande huu tuanze kazi yetu.
Patu: Naam Patu. Chelewa chelewa utapata mwana si wako.
Sofi:  Tutajadiliana kuhusu:Aina za vyakula, viungo vya mapishi, njia za mapishi na vifaa vya upishi.
Patu: Nitaandika tutakayoyajadili nawe utayawasilisha mbele ya wanafunzi wengine.
Sofi: Naam! Tuanze na aina mbalimbali za vyakula.
Patu: (akijikuna kichwa) Kuna wali, pure, ugali na mchuzi...
Sofi:  (akimkatiza) ongeza chapati, nyama, pilau, mahamri na viazi.
Patu: Mifano hiyo inatosha sasa. Tujadili viungo vya kupikia. Anza
Sofi:  (Huku akiwaza) nyanya, dania, tangawizi, pilipili na boga.
Patu:  Pia kuna iliki, pilipili hoho, kitunguu saumu, chumvi na mdalasini.
Sofi: Vizuri sana sahibu. Nazo njia za kupika ni gani?
Patu: (kwa upesi) Kuna kutokosa, kuchemsha, kuoka, kukaanga, kuchoma na kusonga.
Sofi: (kwa mshangao) Inaonekana wewe ni mpishi wa wapishi! Mimi na upishi ni kama samaki na maji.
Sofi: Nakubali. Mimi sasa nitataja vifaa vya kupikia. Kuna sufuria, nyungu, legeni, kikaango, mwiko na...
Patu: (akimsaidia) kinu, mchi, upawa na joko.
Sofi: Ninaona kama tumekamilisha shughuli yetu ya wawili wawili. Naona mwalimu akitaka kutupatia nafasi ya kuwasilisha kazi                yetu.
Patu: Niko tayari.
Sofi:  Kila la heri!

 1. Mazungumzo uliyoyasoma yalifanyika katika somo gani?
  1. Kiingereza
  2. Mapishi
  3. Kiswahili
  4. Sayansi
 2. Ni jambo gani ambalo Sofi na Patu hawakujadiliana?
  1. Aina za vyakula
  2. Njia za kupika
  3. Vifaa vya kupikia
  4. Viunganishi
 3. Ni kweli kusema kuwa :
  1. Sofi na Patu hawaelewi umuhimu wa kufanya kazi pamoja.
  2. Patu anaelewa msamiati wa mapishi kuliko Sofi.
  3. Sofi na Patu hawako katika darasa moja.
  4. Sofi aliwasilisha kazi aliyoiandika mbele ya wanafunzi wenzake.
 4. Mazungumzo haya yanatufunza maadili gani hasa?
  1. Ushirikiano
  2. Bidii
  3. Utengano
  4. Nidhamu
 5. Baada ya Sofi kumwambia Patu kila la heri, angemjibu vipi?
  1. Aleikum salaam
  2. Ya kuonana
  3. Asante
  4. Binuru

Swali la 6 hadi la 9

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.

G5SWAT1TW23002P2

Katika kijiji cha Samaki paliishi mvuvi mmoja kwa jina Adili. Šiku moja alimpa rafiki yake Wema kazi ya kuipaka boti rangi. Wema alikuja na rangi na brashi kama alivyoagizwa na Adili. Alipokuwa akipaka rangi aliona shimo dogo chini ya boti na akaamua kuliziba.

Alipomaliza kazi yake alilipwa ujira wake na akaenda zake.Siku iliyofuata Adili alienda kwa Wema na kumpatia kitita cha pesa. Pesa hizi zilikuwa zaidi ya malipo ya kupaka rangi. Wema alishangaa na kumwambia Adili kuwa alikuwa ameshamlipa pesa zake. Wema alimwambia kuwa pesa hizo zilikuwa za kuziba shimo lililokuwa chini ya boti.

Wema alimwambia Adili kuwa hakufaa kumlipa tena kwani hiyo ilikuwa huduma ndogo sana ambayo haikufaa kulipwa pesa hizo zote. Adili alimwambia kuwa hakujua alichomfanyia. Alimwambia kuwa alisahau kumpa kazi ya kuziba shimo. Boti ilipokauka watoto wake waliichukua na kwenda kuvua na hawakujua kuwa kulikuwa na shimo naye hakuwa nyumbani. Aliporudi alishtuka kuona wamechukua boti. Alifikiri wangezama ziwani.

Alipowaona wamerudi moyo wake ulijawa na furaha kubwa. Alikagua boti na kuona hakukuwa na shimo. Wema alikuwa ameokoa maisha ya watoto wake. Alimwambia hivi akitokwa na machozi ya furaha.

Kusema kweli ni vizuri kuwafanyia wengine mema hata kama ni jambo dogo. Inaweza kuokoa maisha ya wengi bila wewe kujua. Mungu pia huona wema huu na kutulipa kwa Baraka kubwa.

 1. Adili alikuwa akifanya kazi gani?
  1. Kufua
  2. Kuvua
  3. Kurekebisha boti.
  4. Kupaka boti rangi
 2. Baada ya kazi yake, Wema alipata mapato ambayo yanaitwa ________________________
  1. pesa
  2. ujira
  3. mshahara
  4. nauli
 3. Nini maana ya kitita cha pesa kulingana na kifungu? 
  1. Pesa kidogo
  2. Noti
  3. Pesa nyingi
  4. Malipo madogo
 4. Kulingana na kifungu tunajifunza kuwa _____________________________
  1. tusipuuze kufanya wema kwa wengine.
  2. tufanye wema tukitarajia kulipwa.
  3. tufanye wema kwa marafiki zetu pekee.
  4. mtu akifanya wema hulipwa pesa nyingi.

Swali la 10 hadi la 12  

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali. 

G5SWAT1TW23002P3
Mwaka uliopita, Stevo alikuwa amepata ajali uwanjani akicheza kandanda. Alikuwa ameumia kichwa na goti. Baada ya kutibiwa na kurudi shuleni, mwalimu alimpa nafasi aelezee hatua zilizochukuliwa na walimu na maskauti wakimpa huduma ya kwanza. Alielezea yafuatayo:

 1. Walichunguza kubaini jinsi nilivyoumia na iwapo wangeweza kunibeba.
 2. Nilibebwa na kupelekwa kwenye hema ya kufanyia huduma ya kwanza.
 3. Nililazwa chini na kuhakikishiwa kuwa niko sawa.
 4. Mwalimu alivaa glovu na kuniosha goti na kichwa kwa dawa ya kuua viini.
 5. Baadaye nilifungwa bandeji gotini na kichwani.
 6. Bila kupoteza wakati mwalimu aliagiza ambulensi nikapelekwa hospitalini na kufanyiwa uchunguzi zaidi.
 7. Nilitibiwa majeraha yale, nikapewa dawa na kuruhusiwa kwenda nyumbani.
  Baada ya maelezo hayo mwalimu na wanafunzi walimpigia makofi kwa kueleza
 1. Kulingana na hatua ambazo Stevo alielezea ni kweli kusema kuwa:
  1. Mtu akiumia hafai kubebwa.
  2. Ni lazima tuwe waangalifu tunapotoa huduma ya kwanza. 
  3. Huduma ya kwanza hufanyiwa hospitalini.
  4. Baada ya huduma ya kwanza majeruhi hupelekwa nyumbani.
 2. Kwa nini mtu hupewa huduma ya kwanza?
  1. Kutibu viungo vilivyovunjika.
  2. Ili kumwezesha kufika hospitalini kupata matibabu.
  3. Ili apone.
  4. Ili aweze kurudi uwanjani acheze.
 3. Tunajifunza nini kutokana na kifungu?
  1. Utaratibu wa kumpa majeruhi huduma ya kwanza 
  2. Jinsi ya kumtibu mtu.
  3. Matibabu ya uwanjani.
  4. Ajali uwanjani.

Swali la 13 hadi la 15

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.

G5SWAT1TW23002P4

Siku ya maonyesho ya mapambo shuleni kwetu ilikuwa ya kufana mno. Kila mwanafunzi alikuwa na pambo au mapambo yake ya kuonyesha. Katika maonyesho haya yaliyofanyika katika ukumbi wa shule yetu tulikuwa tukipigwa picha na kuchukuliwa video.

Baadhi ya wanafunzi hasa wasichana walichukua zamu kuonyesha mapambo ya kichwani. Walikuwa wamefunga vibanio nyweleni, wengine walikuwa wamezipaka wanja na wengine kuvaa taji. Masikioni walikuwa na vipuli. Kwenye upande wa pua walivaa vishaufu na kwenye uti wa pua wakavaa vipini. Kuna wengine waliovaa jebu videvuni na kupaka mduwaa midomoni. Baadhi yao walikuwa wamevaa vikuba, mikufu na vidani shingoni.

Wanafunzi wengine walionyesha mapambo ya mikononi, miguuni na kiunoni. Kuna wale waliovalia bangili na saa kwenye viwiko vya mikono, mishipi viunoni na kugesi miguuni. Wengine walikuwa wamejipaka hina mikononi na miguuni. Kama ungewaona wanafunzi siku hiyo hata wewe ungewamezea mate.

 1. Siku inayoelezewa ilikuwa na shughuli gani?
  1. Kupigwa picha.
  2. Maonyesho ya mapambo.
  3. Wasichana kujipamba.
  4. Wavulana kuonyesha mapambo.
 2. Ni pambo gani limeambatanishwa sawasawa na mahali linapovaliwa?
  1. Kipuli - mguuni
  2. Kikuba - mkononi
  3. Kishaufu - puani
  4. Bangili - shingoni
 3. Ungewamezea mate inamaanisha:
  1. Ungefurahia
  2. Ungekasirishwa nao
  3. Ungevaa kama wao
  4. Ungevutiwa nao

Soma kifungu kifuatacho. Kina nafasi 16 hadi 20. Umepewa majibu manne hapo. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.

Juma ___16___ nilienda dukani ___17___ mkate.  Mimi kama ___18___ nilimpa muuzaji ___19___ mia moja. Nilipewa mkate ___20___ na kuelekea nyumbani.

   A   B   C   D 
 16.   iliyopita   Lililopita   Kilichopita   aliyepita 
 17.  kununua   kuuza   kuwekeza   kulipa 
 18.  mtaji  bidhaa   mteja   mwekezaji 
 19.  pesa  shilingi   noti   sarafu 
 20.  changu  langu  yangu  wangu

 

Swali la 21-30

SARUFI

 1. Neema amekutana na shangazi yake barabarani asubuhi akielekea shuleni. Je,  atamwamkuaje?
  1. Hujambo
  2. Sabalkheri
  3. Shikamoo
  4. Umeamkaje?
 2. Kati ya nomino hizi ni gani nomino ya pekee?
  1. Kenya
  2. Maji
  3. Uzuri
  4. Meza
 3. Ni kitendawili gani kinalingana na picha hii?
  G5SWAT1TW23002P5
  1. Wafaa lakini wavaliwa bila matumizi maalum.
  2. Ananitazama hasemi hasikii.
  3. Lapendeza rangi lakini halidumu.
  4. Dhahabu yangu ya thamani haisimami.
 4. Ni sehemu gani ya kompyuta imeambatanishwa vizuri na jina lake?
  G5SWAT1TW23002P6
 5. Ni maneno gani yaliyopangwa vizuri kialfabeti?
  1. Saa,saumu, saidia na samaki
  2. Kalamu, karamu, karimu na kaumu
  3. Paa, pesa,pata na pia
  4. Tua, tuzo, tuza na tunu
 6. Kamilisha sentensi hii kwa tashbihi ifaayo: Mjomba alipokuwa akiingia kwenye mlango wa nyumba yetu aliinama kwa sababu yeye ni _______________________
  1. mrefu kama twiga.
  2. mfupi kama nyundo.
  3. mwembamba kama sindano.
  4. mkondefu kama ng'onda.
 7. Badilisha sentensi hii katika ukubwa. Mti uko karibu na mto.
  1. Kijiti kiko karibu na kijito.
  2. MTI UKO KARIBU NA MTO.
  3. Jiti liko karibu na jito.
  4. Miti iko karibu na mito.
 8. Sentensi kama hii huitwaje? " Shirika la reli la Rwanda larejelea shughuli zake rasmi.
  1. Silabi
  2. Konsonanti
  3. Irabu
  4. Kitanzandimi
 9. Kanusha sentensi hii: Umepewa huduma ya kwanza.
  1. Hujapewa huduma ya kwanza.
  2. Mmepewa huduma ya kwanza.
  3. Hutapewa huduma ya kwanza.
  4. Hukupewa huduma ya kwanza.
 10. Kati ya methali hizi ni gani haihusu malezi?
  1. Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.
  2. Mtoto wa nyoka ni nyoka.
  3. Mtoto hutazama kisogo cha nina.
  4. Haraka haraka haina baraka.


MARKING SCHEME

 1. C
 2. D
 3. B
 4. A
 5. C
 6. B
 7. B
 8. C
 9. A
 10. B
 11. B
 12. A
 13. B
 14. C
 15. D
 16. B
 17. A
 18. C
 19. B
 20. D
 21. D
 22. A
 23. D
 24. C
 25. B
 26. A
 27. C
 28. D
 29. A
 30. D
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Grade 5 Mid Term 1 Exams 2023 Set 2.


Tap Here to Download for 30/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students