0 votes
18.9k views
in Chozi la Heri by

1 Answer

0 votes
by
1.kuonyesha maudhui ya uwajibikaji-Selume anajinunulia glavu ili kumhudumia mwanamke aliyekuwa anataka kujifungua katika hospitali ya umma.
2.kuonyesha maudhui ya ufisadi-Kijana aliyevaa shati lililoandikwa hitman mgongoni alikiri kuwa walipokea hongo kutoka Kwa viongozi ili kuwafanya ajuza kuchagua viongozi wabaya.
3.Kuonyesha maudhui ya utamaduni-Chandachema anaeleza kuwa kulingana na jamii Yao mtoto ni wa Baba.
4.kuonyesha mchango wa wanyonge katika kukandamizwa kwao-Familia ya akina Shamsi ilikosa kujitetea walipoonyeshwa hatimiliki bandia na kunyang'anywa shamba na bwana Mabavu.
5.Kuonyesha ukosefu wa uwajibikaji Kwa viongozi-Selume anaeleza kuwa wasimamizi wa hospitali walichukuwa shehena za dawa na kupeleka kwenye maduka ya dawa ya kibinafsi.
6.Kuonyesha dhima ya dini-Lily Nyamvula alikuwa "born again" Kwa hivyo hakutaka Mwangeka ajiunge na vikosi vya usalama Kwa kuwa alishikilia kwamba haihalisi muumini wa kweli kumpoka binadamu mwenzake uhai.
7.Kuonyesha adhari za ghasia za baada ya uchaguzi-Wahafidhina wengi waligeuka kuwa wakimbizi katika msitu wa mamba baada ya matokeo ya uchaguzi.
8.kuonyesha maudhui ya ukabila-Subira alirejelewa na mavyaa wake kama muki Kwa kuwa alitoka katika jamii ya bamwezi.
9.kuonyesha maudhui ya ukiukaji WA haki za wafanyikazi-Pete alikuwa analipwa malipo duni na mwajiri wake Patel.
10.Kuonyesha shida zinazoikumba asasi ya ndoa-Annette alimwacha mumewe Kiriri na kuhamia ughaibuni hivyo kumwacha mumewe Kwa upweke.
11.kuonyesha ukiukaji wa haki za watoto-Mamake Pete hakutaka kujua lolote kuhusu ukuaji wa Pete.
12.kuonyesha maudhui ya umaskini-Pete alikosa sodo na hivyo kulazimika kutumia tambara la blanketi na kanzu kuukuu.
13.kuonyesha sifa za wahusika-Tila alitaka kuwa jaji mkuu ili aweze kusikiza kesi za jinai ambazo zimeselelea mahakamani Kwa miongo miwili au zaidi bila kusikizwa.
     (NA ZAIDI...)

Welcome to EasyElimu Questions and Answers, where you can ask questions and receive answers from other members of the community.

6.4k questions

9.6k answers

6 comments

590 users

...