0 votes
1.9k views
in Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine by

“Aliyeumwa na nyoka akiona ung’ong’o hushtuka .”

  1. Weka dondoo hil katika muktadha wake. 
  2. Eleza namna mzungumziwa alivyoumwa na nyoka. 
  3. Eleza vile mzungumziwa anaendeleza maudhui ya ushauri na ukosefu wa utu. 

1 Answer

0 votes
by
  1. Maelezo ya mwandishi /Msimulizi kuhusu Otii pale nyumbani Kitandani Otii alirejelea maisha yake ya awali, aliumia mguu na kupoteza umaarufu wake.
    Otii alikuwa amerejeshwa pale nyumbani mwake kwa amri ya daktari angojee kifo.
    Otii alipovunjika mguu na kutumia mikongojo miezi sita, alikataa kurejelea kandanda uwanjani.
  2. Otii alikuwa uwanjani akichezea timu ya bandari FC.
    1. Kutokana na uhodari wake alikuwa mwiba kwenye timu kinzani ya Yanga kwene kinyang’anyirocha kuwania kombe la klabu bingwa Afrika mashariki na kati.
    2. Alikuwa amewala chenga mabeki wote wa Yanga na kuelekea kufumua kiki kali kwenye eneo hatari , ndiop jibabajoja la miraba minne lilipomkwaa akaanguka
    3. Alianguka vibaya kama gunia la chumvi. Picha ya eksirei ilionyesha kuwa amevunjika mfupa wa muundi na nguyoni.
    4. Baada ya kuumia aliterekezwa kabisa na maafisa wa Bandari FC
    5. Hata maafisa wa serikalini hawakumjali hata kidogo
    6. Alitupwa kama masimbi na hakuna aliyemkumbuka
    7. Maumizu na mateso hayo ndiyo kuumwa na nyoka.
  3.  
    1. Ukosefu wa utu
      • Mwandishi anonyesha kuwa utu umepotea na haupo tena katika jamii.
      • Otii anatoa mchango mkubwa kwa kuichezea timu ya Bandari FC na hatatimu ya taifa ya Harambee lakini anapovunjika mguu hakuna anaejali kipaji chake.
      • Hakuan fidia anayopewa hata baada ya kuacha mchezo huo kwa kuumizwa.\
      • Chama cha waqu wa nyumbani wananza kujadili mazishi ya mtu akiwa bado hai.
      • Wanachama wa chama cha nyumbani wanakosa utu na kuanza kujadili kusafirisha maiti ya Otii wakati Otii bado yu hai an anawasikiliza.
      • Rehema anakosa utu kwa kumwambukiza Otii Maradhi.
    2. Umuhimu wa kuzingatia ushauri
      • Otii anaitwa na rafiki yake na kushauriwa dhidi ya kujihushisha na msichana mrembo Rehema Wanjiru.
      • Otii anapuuza ushauri huo na kusema kuwa yuko radhi kuwa nzi na kufia kidondani.
      • Matokeo ni kuwa rehema anamuambukiza ugonjwa wenye dalili za Ukimwi.Wote wawili wanafariki mtawalia.
      • Otii anamshauri mwenyekiti wa chama nyumbani azikwe Mombasa.Wao walikataa ushauri huo.
      • Baadaye wanapata ajali mbaya.
Welcome to EasyElimu Questions and Answers, where you can ask questions and receive answers from other members of the community.

6.4k questions

9.6k answers

6 comments

590 users

...