Friday, 31 March 2023 05:59

Kiswahili Questions and Answers - Grade 6 Mid Term 1 Exams 2023 Set 5

Share via Whatsapp Written by
Rate this item
(0 votes)

Soma kifungu hiki kisha ujibu swali la 1-5.

G6cwaT1J23002P1

Tuta na Twita walikuwa wavulana. Walipendana kama chanda na pete. Walisoma katika shule moja.
Ajabu ni kwamba wote walikuwa na umri sawa. Walikuwa wakisoma kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa.
Jumamosi na Jumapili walipumzika nyumbani kwao na kufanya kazi za ziada kutoka shuleni. Baada ya
kumaliza kazi za ziada, walipendelea kuenda kucheza.

Siku moja Tuta na Twita waliamua kwenda msituni kuwinda ndege kwa manati. Ilikuwa siku ya
Jumapilii. Walipofika msituni, waliendelea kuwawinda ndege. Waliendelea na mchezo wao hadi masaa ya
adhuhuri. Tuta akamwuliza Twita," Rafiki yangu,tutakula nini? Mimi ninahisi njaa!" Twita akasema "Mimi
nina kiporo ndani ya mfuko wa kaptura yangu. Sina wasiwasi!"

Maswali

  1. Tuta na Twita walikuwa wavulana ndiko kusema
    1. walikuwa vijana
    2. walikuwa watoto wa kiume
    3. walikuwa duma
    4. walikuwa wanaume.
  2. Walipendana kama chanda na pete inamaanisha
    1. walipendana sana
    2. walipendana kidogo tu
    3. walipenda pete na chanda
    4. walikuwa wapenzi. 
  3. Wote wawili walikuwa na umri sawa. Kumaanisha walikuwa
    1. pacha
    2. ndugu
    3. marika
    4. kaka.
  4. Ni yupi aliyehisi njaa walipokuwa msituni?
    1. Hatujaambiwa 
    2. Twita
    3. Tuta
    4. Rafiki.
  5. Twita alikuwa na kiporo. Hiki ni chakula
    1. cha nyama
    2. cha ugali
    3. kilicholala
    4. cha msituni.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali la 6-10.  

Mama aliniacha nyumbani na mtoto wetu mdogo. Nilimpenda sana mtoto wetu Nurika. Tulicheza na kucheka pamoja. Nilimwimbia wimbo mzuri. Nurika alikuwa mtoto mwenye furaha. Mara nilisikia mlango wa nyumba ukigongwa. Nikaitikia, "karibu!" Nilidhani ni rafiki yangu Sifu aliyekuja kwetu kucheza
nami.

Nilipoufungua mlango, nilimwona mtu mgeni kabisa Akaniuliza, "Mama yako yuko wapi?" Nilimjibu, "Ameenda sokoni." Mgeni aliketi hata kabla nimwambie aketi.Akaniambia:"Mimi ni rafiki ya mama yako. Nitamngoja mpaka aje kutoka sokoni. Nenda dukani ukaniletee soda ninywe nikimsubiri, Nina kiu sana!" Alinipa pesa.Nikakimbia dukani kumletea soda.

Nilipotoka dukani, sikumkuta. Alitoweka na mtoto wetu Nurika. Polisi bado wanamtafuta mama huyo.

Maswali.

  1. Mwandishi alipoondoka alimwachia nani mtoto?
    1. Mama yangu
    2. Mama mgeni
    3. Nyanya
    4. Nurika.
  2. Aliyebisha mlango bila shaka alisema nini?
    1. Karibu
    2. Hodi
    3. Niingie
    4. Nani yupo?
  3. Mgeni aliyeingia alikuwa
    1. mwanamke
    2. rafiki
    3. askari
    4. mwanamume.
  4. Mgeni alimtuma mwandishi soda ili
    1. akunywe
    2. anywe
    3. akule
    4. ya kukunywa.
  5. Kulingana na kisa hiki mgeni alikuwa na tabia gani?
    1. Mkweli
    2. Mzalendo
    3. Mwema
    4. Mwenye mkono mrefu.

Soma kifungu hiki kisha ujibu maswali 11-15.   

G6cwaT1J23002P2

Magari yoyote ya kuwabebea abiria huitwa matwana. Katika matwana mna mabasi au kwa umoja basi. zipo matatu au kwa jina jingine ni daladala. Magari yote haya hulipisha nauli ndipo yatoe huduma za usafiri. Anayelipa nauli ili asafiri huitwa abiria. Mahali ambapo magari yote huegeshwa ili yaanze safari tena upya huitwa kituoni au stesheni ya mabasi au kituo cha matwana.

`Anayeendesha gari huitwa dereva. Anayemsaidia dereva kupanga abiria ni utingo. Yeye ndiye
anayepokea nauli. Hulipisha abiria kulingana na mahali wanapoenda iwapo ni mbali au karibu. Matwana
husimama kwa muda mfupi stanini ili kushusha au kubeba abiria. Madereva wanafaa kuyaendesha magari kwa utaratibu mkubwa ili kuzuia ajali.

Maswali  

  1. Magari ya kuwabeba abiria kwa jina maalum ni
    1. matwana
    2. matatu
    3. mabasi
    4. daladala.
  2. Malipo anayotozwa abiria ili asafiri ni
    1. tikiti
    2. ada
    3. risiti
    4. nauli.
  3. Watu wanaotumia magari kusafiri wanaitwa
    1. wasafiri
    2. wafanyikazi
    3. abiria
    4. utingo. 
  4. Dereva ni mtu ambaye ________________________________ gari.
    1. huongoza
    2. huendesha
    3. hupeleka
    4. huchukua
  5. Ajali nyingi husababishwa na madereva
    1. wasiomakinika
    2. wenye utaratibu
    3. wanaomakinika
    4. waangalifu.

Jaza mapengo kwa majibu sahihi. 

Chakula ___16___ kitamu watu hufurahia. Mimi hupenda chakula ___17___ na ___18___. Sitaki ___19___
chakula ___20___kwa sababu husababisha maradhi ya tumbo

   A   B   C   D 
 16.   kikiwa   ikiwa   ukiwa   yakiwa 
 17.  nzuri  mzuri   tamu   kitamu
 18.  kisa  safi  mzuri  nyingi
 19.  nile  nikule   kukula   kuikula 
 20.  chafu  kichafu   mchafu   uchafu 


Chagua jibu mwafaka kulingana na maagizo.  

  1. Kiungo cha kusafisha hewa ni
    1. maini
    2. figo
    3. moyo
    4. pafu. 
  2. Miti _________________________ ilikatwa ni hii.
    1. ambao
    2. ambaye
    3. ambayo
    4. ambazo 
  3. Mchezo wa kuvutana kwa kamba ni
    1. ndondi
    2. njugwe
    3. jugwe
    4. mwereka
  4. Ukubwa wa nguo ni
    1. manguo
    2. guo
    3. kiguo
    4. vinguo
  5. Kitenzi 'cheza' katika hali ya mazoea ni
    1. hucheza
    2. amecheza
    3. hajacheza
    4. atacheza.
  6. Kivumishi kionyeshi ni kipi katika sentensi ifuatayo?
    Watoto hao watacheza vizuri sana
    1. Sana
    2. Vizuri
    3. Hao
    4. Watoto.
  7. Kiambishi cha nafsi ya pili katika wingi ni
    1. yeye
    2. wewe
    3. wao
    4. nyinyi. 
  8. Akifisha sentensi ifuatayo.
    Mbona unatembea polepole
    1. !
    2. ?
    3. :
    4. ,
  9. Chagua jozi ya vitate.
    1. cheka - chora 
    2. fika - pika
    3. buda - bunda
    4. gamba - gumba
  10. Msimu wa baridi kali ni
    1. kipupwe
    2. kiangazi
    3. vuli
    4. masika.

INSHA

Mwandikie rafiki yako barua ukimshauri jinsi ya kufaulu katika masomo.

MARKING SCHEME

  1. B
  2. A
  3. C
  4. B
  5. C
  6. B
  7. B
  8. A
  9. B
  10. D
  11. A
  12. D
  13. C
  14. B
  15. A
  16. A
  17. D
  18. B
  19. A
  20. B
  21. D
  22. C
  23. B
  24. B
  25. A
  26. C
  27. D
  28. B
  29. C
  30. A
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Grade 6 Mid Term 1 Exams 2023 Set 5.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Read 1863 times Last modified on Monday, 03 April 2023 08:18

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.