Displaying items by tag: kiswahili

Friday, 10 November 2023 09:43

Kiswahili Questions - KCPE 2023 Past Papers

Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.

Dereva mwangalifu ___1___ kuwa amezingatia sheria za barabarani. ___2___ magari ___3___ yanatakiwa kutimiza kanuni mbalimbali ili yakubaliwe kutoa huduma___4___ usafiri. Madereva wanapaswa___5___  ___6___ magari hayo. Abiria nao wasinyamaze katu madereva___7___ utaratibu ufaao. Ili kuepuka maafa ___8___kila mmoja atahadhari kwani ___9___.

   A  B  C  D
 1.  huhakikishia  huhakikisha  huhakishiwa   huhakikishiana 
 2.  Maadamu  Lau   Mathalani   Japo 
 3.  sote  zote   mote   yote 
 4.  za  kwa   mwa   wa 
 5.  kukaa tutwe  kukaaa doria   kukaa ange   kukaa tayari 
 6.  wanavyoyaendesha  wanapoyaendesha  wanakoyaendesha   wanazoyaendesha 
 7.  wakikiuka  wangekiuka   wamekiuka  wakakiuka 
 8.  inatubidi  inakubidi   inawabidi  inambidi
 9.  mwenye macho haambiwi tazama.  kinga ni bora kuliko tiba.  hakuna marefu yasiyo na ncha.  usilolijua ni usuku wa kiza.


Mchezo ___10___ wa kabumbu yaani wa ___11___ huchezwa kote ulimwenguni. Ni mchezo ___12___ tija kwa ___13___ taifa lake. Huchukua dakika tisini.___14___ timu zinazocheza hazijafungana bao, huongezewa muda wa___15___ kupata mshindi.

   A  B  C  D
 10.  maarufu  stadi   hodari   bingwa 
 11.  soka  voliboli  vikapu  raga
 12.  kwenye  wenye  penye  mwenye
 13.  analochezea  anayochezea  anayechezea  anakochezea
 14.  Hadi  Ingawa  Hata  Iwapo
 15.  kiasi   halafu  ziada  awali

 

Kutoka swali la 16 mpaka 30, chagua jibu sahihi.

  1. Nomino zilizopigiwa mstari katika sentensi ifuatayo ni za aina gani?
    Rembo alinunuliwa manukato katokana na usafi wake.
    1. wingi, dhahania
    2. kawaida, pekee
    3. dhahania, kawaida
    4. pekee, wingi.
  2. Chagua wingi wa sentensi ifuatayo.
    Daktari aliyemtibu ametuzwa na shirika hilo.
    1. Madaktari waliomtibu wametuzwa na mashirika hayo.
    2. Madaktari waliowatibu wametuzwa na mashirika hayo.
    3. Madaktari waliowatibu wametuzwa na shirika hilo.
    4. Madaktari waliomtibu ametuzwa na shirika hilo.
  3. Matumizi ya -po- katika sentensi ifuatayo ni:
    Mwema alipofika tuchezeapo, alimpata katibu wa chama chetu.
    1. mahali, wakati
    2. wakati, mahali
    3. mazoea, masharti
    4. masharti, mazoea.
  4. Chagua sentensi yenye kivumishi cha pekee.
    1. Mkulima atawafuga ng'ombe wale shambani mwake.
    2. Mwanafunzi amenunua vitabu vinne vya Kiswahili.
    3. Hatibu mwenyewe aliwashauri vijana kuhusu masomo.
    4. Mvuvi ambaye anasifika sana anaitwa Pato.
  5. Sarafu huanguka sakafuni tang! ilhali moto huzimika:
    1. pu!
    2. ndi!
    3. fyu!
    4. zii!
  6. Ni sentensi ipi inayoonyesha kuwa tukio moja linategemea lingine?
    1. Tina alimpikia chakula kitamu akafurahi.
    2. Balo angali analima tangu asubuhi.
    3. Tesi na bintiye wameamua kwenda sokoni.
    4. Mose alikuwa ameibuka mshindi katika uogeleaji.
  7. Matumizi ya kwa katika sentensi ifuatayo.
    'Kanusu alisoma kwa bidii akapata themanini kwa mia,' ni:
    1. jinsi, sehemu ya kitu kizima.
    2. sababu, sehemu ya kitu kizima.
    3. umilikaji, sehemu ya kitu kizima.
    4. kulinganisha, sehemu ya kitu kizima.
  8. Chagua jibu lisilo sahihi.
    1. chura kiluwiluwi
    2. njiwa-kipura 
    3. kipepeo - kisuse
    4. papa - kinengwe.
  9. Chagua jibu lifaalo kujaza pengo katika sentensi ifuatayo.
    _____________ nitamwona, nitampasha habari hizo.
    1. Bali
    2. Ikiwa
    3. Angaa
    4. Halafu
  10. Safari yangu itaanza siku ya tatu baada ya jana. Je, itaanza lini?
    1. Mtondo.
    2. Mtondogoo.
    3. Kesho.
    4. Kijoto.
  11. Chagua usemi wa taarifa wa:
    "Mkifika mapema mtauwahi mkutano." Karani alisema.
    1. Karani alisema kuwa wangefika mapema watauwahi mkutano.
    2. Karani alisema kuwa wakifika mapema, watauwahi mkutano.
    3. Karani alisema kuwa wangefika mapema wangewahi mkutano.
    4. Karani alisema kuwa wakifika mapema wangewahi mkutano.
  12. Ni sentensi ipi iliyoakifishwa ifaavyo?
    1. Fisi na Sungura ni maadui Sana.
    2. Fatuma amepika; Chapati, Biriani na kaukau.
    3. "Karibuni nyumbani wanangu," mama aliwaomba.
    4. ng'ombe, mbuzi na kondoo watachinjwa leo.
  13. Sentensi, "Asingalichora vyema, asingalituzwa," ina maana:
    1. Hakuchora vyema, akatuzwa.
    2. Alichora vyema, akatuzwa 
    3. Hakuchora vyema, hakutuzwa. 
    4. Alichora vyema, hakutuzwa.
  14. Chagua jibu lenye nomino za ngeli ya U-U
    1. uyoga, wema, wizi
    2. waya, wali, uzi
    3. uso, ukuta, ugali
    4. werevu, uji, wino.
  15. Akisami, 7/9 kwa maneno ni:
    1. tusui saba
    2. tusui tisa
    3. subui tisa
    4. subui saba.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 31 mpaka 40.

Je umewahi kutafakari kuhusu neno mazingira? Ni neno ambalo daima limekuwa vinywani mwa waja. Mazingira ni ile hali au mambo yanayozunguka mtu mahali anapoishi; nchi kavu, angani na hata majini. Manufaa atakayopata binadamu yanategemea namna anavyoyatunza mazingira yake.

Fikiria vile hali ingekuwa bila mito, miti, maziwa, milima, mabonde na hewa safi! Yakini, hali ingekuwa si hali. Tuchukue kwa mfano mito na maziwa, faida zake ni chungu nzima. Maji tunayoyatumia nyumbani, kupikia, kufulia na kunyweshea mifugo na kwa unadhifu wa binadamu hutoka pale. Aidha, shughuli nyingi za viwandani huhitaji maji kwa wingi. Wakulima nao wanafaidika kwa kuwa wanayatumia maji kunyunyizia mimea yao.

Isitoshe, miti ina tija kubwa kwa jamii. Hutumiwa katika ujenzi, kutengeneza dawa, kutupatia chakula na kama hifadhi ya wanyama na ndege. Vilevile, miti huvuta mvua, husafisha hewa na kuzuia mmomonyoko wa udongo na kurembesha mazingira. Ukataji miti kiholela hum- nyima binadamu faida hizi.

Ni dhahiri kwamba mazingira ni uhai na hatuna budi kuyatunza. Mathalan tuyaondoe maji yaliyotuama kwenye vidimbwi kisha tuvizibe. Vyombo vingine kama vile mikebe na vigae ambavyo vimetapakaa nje huweza kuhifadhi maji kunyeshapo na kutuama hivyo kuwa mahali pa mbu kuzalia. Endapo hatutachukua hatua hii, mbu wanaweza kuzaliana humo na kusababisha malaria. Hali kadhalika watu wanaweza kuyanywa na kuambukizwa uwele wa waba. Hatari hizi zinaweza kuzuiwa kwa kutia kemikali kwenye maji hayo ili kuwaangamiza viluwiluwi waliomo. Vyombo ambavyo vinaweza kuweka maji yasiyohitajika visitupwe ovyoovyo.

Hewa safi ni muhimu kwa maisha ya binadamu. Hewa hii inaweza kuharibiwa na moshi utokao kwenye magari mabovu na pia viwandani. Kutokana na uchafuzi wa hewa, uhai wa bi- nadamu huhatarishwa kwani huenda akapatwa na magonjwa anuwai yakiwemo pumu, saratani kifua kikuu na hata yale ya ngozi. Aidha, uchafuzi wa hewa huwa na athari kwa hali ya anga. Kwa mfano safu ya ozoni ikiharibiwa, joto jingi hutokea na huweza kuathiri afya ya binadamu na wanyama. Misimu na majira pia hubadilika jambo ambalo huweza kuathiri kilimo na miundo misingi. Ili kukabiliana na janga hili, magari mabovu yanayotoa moshi mwingi yakarabatiwe au kuondolewa barabarani. Wenye viwanda wanastahili kubuni mikakati kabambe ili kudhibiti gesi na majitaka yatokanayo na shughuli za kuzalisha bidhaa.

Mazingira ya nyumbani nayo ni muhimu. Tunafaa kuyatunza kulihali kwani tusipotahadhari tutajilaumu wenyewe. Mabaki ya chakula husababisha uvundo katika nyumba zetu yasipohifad- hiwa vizuri. Zaidi ya hayo, picha tuipatayo katika baadhi ya nyumba inachukiza. Utapata taka zimeenea kote; si maji machafu, si maganda ya ndizi na parachichi, si kaka za mayai, si karatasi na matunda yaliyooza na kuozeana. Ni nani mwingine atakuja kudumisha usafi wa nyumba zetu ila sisi wenyewe? Hatari inayotukodolea macho ni kubwa. Kuna uwezekano kuwa umewahi kuteleza na kuanguka kutokana na kukanyaga ganda la ndizi lililotupwa shelabela. Wa kulaumiwa ni nani? Wahenga walig'onga ndipo waliposema mwiba wa kujichoma hauambiwi pole. Kila mmoja katika familia ana jukumu la kuhakikisha kwamba taka zote za nyumbani zimetupwa kwenye jalala.

Ni wazi kuwa mazingira ni a hidaya ambayo tunapaswa kuithamini lau sivyo tutakuwa chachandu anayejipalia makaa.

  1. Kwa mujibu wa aya ya kwanza:
    1. Watu wengi hupendezwa na mazingira yao.
    2. Mazingira hutawaliwa na hali kavu.
    3. Anga inaweza kuyaboresha maisha ya binadamu.
    4. Binadamu atafaidika akiyazingatia yaliyomo katika maeneo anamoishi.
  2. Aya ya pili imedhihirisha kuwa:
    1. Maji yana faida zaidi nyumbani kuliko mahali pengine.
    2. Maisha ya binadamu yatakuwa magumu bila mazingira.
    3. Kilimo hakihitaji maji mengi kama uzalishaji bidhaa.
    4. Maziwa yana manufaa mengi zaidi yakilinganishwa na milima.
  3. Jibu lisilo sahihi kuhusu miti kwa mujibu wa aya ya tatu ni:
    1. Chombo cha kusafisha hewa na kuchangamsha viumbe.
    2. Kiungo cha tiba na huwalisha binadamu. 
    3. Pambo la mazingira na hukinga udongo usisombwe.
    4. Chanzo cha mvua na ni makazi ya viumbe.
  4. Aya ya nne imebainisha kuwa lazima tuyatunze mazingira ili
    1. tuepuke kunywa maji machafu.
    2. tukwepe kutupa toka ovyo.
    3. tuzuie mbu kuongezeka. 
    4. tuwe na siha njema.
  5. Kwa mujibu wa kifungu:
    1. Mbu hupendezwa na maeneo yoyote yaliyo na maji.
    2. Maji yaliyotiwa dawa hutibu magonjwa yaletwayo na mbu.
    3. Uharibifu wa hali ya anga huweza kuvuruga shughuli za ukulima.
    4. Mabadiliko ya hali ya anga huchangia kuwepo kwa hewa safi.
  6. Jukumu la wenye viwanda katika utunzaji mazingira kulingana na aya ya tano ni:
    1. Kudhibiti mvuke utokanao na mitambo itumikayo viwandani.
    2. Kuimarisha harakati za kuzalisha bidhaa za viwandani.
    3. Kuzua njia zifaazo za kukabiliana na vichafuzi votakavyo viwandani. 
    4. Kushirikiana na wenye magari makuu kuu kuzuia moshi kuchafua mazingira.
  7. Ni jibu lipi ambalo si ushauri kwa mujibu wa aya ya sita.
    1. Ni wajibu wa kila mja kunadhifisha mahali anakoishi.
    2. Chakula kilichosalia kinastahili kutunzwa kwa njia ifaayo.
    3. Uchafu hutapakaa kote katika baadhi ya nyumba.
    4. Majaala ya kutupia taka yanapaswa kuwekwa kila mahali.
  8. Maana ya kauli 'miti ina tija kubwa' ni:
    Miti ina
    1. gharama kuu. 
    2. mvuto mkubwa.
    3. tiba nyingi.
    4. manufaa mengi.
  9. Chagua maana ya methali, "Mwiba wa kujichoma hauambiwi pole" kwa mujibu wa kifungu.
    1. Ukiweka maji machafu nyumbani mwako utajisababishia madhara mengi.
    2. Ukieneza kaka za mayai na karatasi usitarajie kuhurumiwa.
    3. Ukitupa taka ovyo hufai kusaidiwa upatapo hasara.
    4. Ukikanyaga maganda ya matunda utajiumiza wewe mwenyewe.
  10. Kauli "tutakuwa chachandu anayejipalia makaa' imetumia tamathali gani ya usemi?
    1. sitiari.
    2. methali.
    3. nahau.
    4. tashbihi.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 41 mpaka 50.

"Ngomeni washuke! Ngomeni washuke!"Sauti ya utingo ilihanikiza kote kuwahimiza abiria ambao walikuwa wamejaa pomoni kwenye daladala hii kushuka. Sauti hii ndiyo iliyoniamsha kwenye usingizi mzito. Sikujua nilikuwa nimelala kwa muda gani. Nililokumbuka ni kwamba mara tu baada ya kuhakikisha kwamba nimekihifadhi kirununu changu kibindoni, usingizi uliniiba, nikalala bila hata kuwazia kwamba nilikuwa mwana genzi wa safari. Licha ya kwamba hii ndiyo iliyokuwa mara yangu ya kwanza kuondoka nyumbani peke yangu, ilikuwa pia mara yangu ya kwanza kwenda jijini. Hakika jiji la Tugawane nilikuwa nasikia habari kulihusu ama kutoka kwa marafiki wangu wachache waliobahatika kuwa na jamaa huko, au kupitia magazeti ambayo hayakuchelewa kuandika visa vya kuchangamsha, kushangaza na kuhuzunisha kuhusu jiji hili.

"Ndugu, umelala sana," alisema abiria aliyekuwa ameketi karibu nami, akanitazama tena kisha akaendelea, "Unaenda wapi huku Tugawane? Naona tunakaribia kufika kituo cha mwisho. Hawa wakishuka, tunastahili kujitayarisha kwani tukifika kwenye kituo cha mabasi cha Hamaniko sote tutahitajika kushuka".

Maneno ya abiria mwenzangu yalinitanabahisha kwamba kwa kweli sikujua nilikokuwa naelekea. Sikujua kwa sababu baba yangu aliniambia tu kwamba ami yangu angenipokea huko kituoni. Sikuona haja ya kukumbuka jina la mtaa nilikokuwa naenda kwani baba aliniandikia nambari ya ami, nikaihifadhi kwenye kirununu changu, japo kwa kweli alinitajia jina lenyewe. Nilijua kwamba ningempata ami kituoni na kama ningechelewa, ningempigia simu.

"Sijui ninakoenda," nilimwambia abiria mwenzangu; ami yangu atakuja kunipokea kituoni. Kesho atanipeleka chuoni, Mwenge." Abiria mwenzangu aliniangalia akatikisa kichwa kisha akanitazama tena kana kwamba ananiambia, "Utafungaje safari bila kujua uendako kisha unalala? Naona ubwabwa wa shingo haujakutoka. Nakuhurumia kwa yatakayokupata."

Hatimaye gari lilipunguza mwendo na kupinda kuelekea kituo cha Hamaniko. Kibarabara kilichoelekea huko, kilikuwa kimeshiba kikatapika. Si maelfu ya magari, na rukwama zilizosheheni mizigo ya wachuuzi wa vyakula, si matusi ya mahamali waliotaka kupishwa, si wauzaji wa vipande vya matunda vilivyofungwa kwa karatasi za plastiki... Hata sauti nene ya utingo ilipotangaza, "Shukeni haraka! Tulikuwa tumechukua saa mbili ushei kusafiri masafa ya kilomita tano tu. Mara tu utingo alipotoa tangazo abiria mwenzangu alikurupuka na kushuka haraka bila kunipa hata kwaheri. Niliinuka nikaingiza kiganja changu kibindoni ambamo nilikuwa nimekihifadhi kirununu changu. "Mungu wangu!" Nilisema kwa sauti ya jitimai iliyomshtua hata utingo. "Nini kijana?" Aliuliza utingo. "Sioni rununu yangu," nilimwambia huku nikizuia kilio. "Humo ndimo nilimokuwa nimehifadhi nambari ya simu ya ami yangu. Ami anakuja kunipokea kituoni," Nilimweleza utingo zaidi.

"Basi wewe shuka. Utamsubiri ami yako huko kwenye ubao huo," alisema kisha akajiondokea bila hata kuniuliza kama namjua mwingine yeyote katika jiji hili.

"Maskini ami asipokuja sijui nitafanya nini," nilijisemea, "Kumbe, mwenzangu huyu alijua aliyotenda? Kumbe ndiyo maana akaondoka bila kunijulia la heri wala la shari?"

  1. Kulingana na aya ya kwanza:
    1. Msimulizi alikumbuka alikuwa na kirununu onda kibindoni aliposikia sauti ya utingo ikitangaza washuke.
    2. Utingo alizungumza kwa sauti nzito ili msimulizi na abiria wasikie aliyosema. 
    3. Hii ndiyo mara ya kwanza kwa msimulizi kusikia habari za yale yanayoendelea mjini. 
    4. Baadhi ya habari alizo nazo msimulizi kuhusu Tugawane zinatoka kwenye vyombo vya habari.
  2. Aya ya kwanza imeonyesha kwamba:
    1. Utingo wa daladala za Tugawane walikuwa na mazoea ya kujaza abiria.
    2. Abiria alilala kwa sababu mizigo yake ilikuwa salama kwenye gari.
    3. Awali msimulizi alikuwa akiandamana na jamaa kila mara alipotoka nyumbani.
    4. Ngomeni kulikuwa na watu waliowahuzunisha na kuwashangaza wengine kwa maneno yao.
  3. Chagua jibu sahihi kulingana na kifungu.
    1. Abiria mwenzake msimulizi alimwamsha ili msimulizi ajue anakoenda.
    2. Kituo cha mabasi cha Hamaniko kilikuwa hatua chache kutoka Ngomeni. 
    3. Baba ya msimulizi alikuwa amemtajia mahali ambapo alikuwa anaenda. 
    4. Rununu ilihifadhiwa kibindoni kwani ilikuwa inahitajika mwishoni mwa safari.
  4. Msimulizi amekosa uwajibikaji kwani:
    1. Alimwambia mwenzake anakoishi bila kuwaza kuwa ni mgeni kwake.
    2. Alipuuza maelekezo aliyopewa na baba yake kwa kutegemea kirununu.
    3. Alitarajia kufika chuoni Mwenge bila kujua njia ya huko.
    4. Alisahau kwamba alikuwa ameketi kando ya abiria ambaye alihitaji simu.
  5. Kauli, 'Utafungaje safari bila kujua uendako kisha unalala?" inaonyesha hasa kwamba abiria
    1. anamhuzunikia msimulizi kwa kushikwa na usingizi.
    2. anamlaumu msimulizi kwa kukosa makini.
    3. anamtahadharisha msimulizi kuhusu hatari ya safari za ugenini.
    4. anachukizwa na ukosefu wa kumbukumbu ya msimulizi.
  6. Chagua matatizo yanayoukumba mji wa Tugawane kwa mujibu wa aya ya tano.
    1. Wachuuzi wengi, ukosefu wa heshima.
    2. Kelele nyingi, wizi kituoni.
    3. Uchafuzi wa mazingira, msongamano wa magari.
    4. Barabara zenye mashimo, ukatili garini.
  7. Ushirikiano wa kifamilia unahimizwa katika kifungu kwani:
    1. Baba aliandika nambari ya simu kumtambulisha msimulizi.
    2. Baba alijua kwamba msimulizi akipoteza simu ami atamngojea Ngomeni amwelekeze.
    3. Ami alifahamu kwamba msimulizi atampigia simu gari likichelewa ili tampokee.
    4. Ami alichukua nafasi ya baba ya kumpeleka msimulizi Chuoni.
  8. Kulingana na kifungu, utingo
    1. alikosa kutilia maanani hali ambayo ingemkumba msimulizi.
    2. alijua kwamba abiria alikuwa mwizi.
    3. alichukizwa na kelele ya msimulizi.
    4. alifahamu mahali ambapo ami huwangojea wageni wake.
  9. Kauli, "Maskini, ami asipokuja sijui nitafanya nini; inamaanisha kwamba msimulizi
    1. anajihurumia kwa yale ambayo yatamfika.
    2. anashangazwa na kuchelewa kwa ami yake.
    3. anajilaumu kwa kuzungumza na abiria mwenzake.
    4. anasikitishwa na mazingira mageni mjini.
  10. Chagua kisawe cha, 'ilihanikiza' kulingana na kifungu.
    1. Ilisikilizwa
    2. Ilitangazwa
    3. Ilienea
    4. Ilivutia.

INSHA

Umepewa dakika 40 kuanndika insha yako.

Andika insha itakayomalizika kwa maneno yafuatayo.

Ni wazi kuwa kufanikiwa kwangu maishani kulitokana na ushirikiano huo.

Tagged under
Thursday, 09 November 2023 12:11

Kiswahili Questions - Grade 6 KPSEA 2023 Exams

Swali la 1 hadi la 5

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.

(Ni jioni. Leni na Kibo wamekutana mtoni. Ni msimu wa kiangazi.)

Leni: (Akitabasamu.) Bingwa, hujambo? Ha! Ha! Ha! Umejitwika mtungi kichwani kutafuta maji!
Kibo: (Akionyesha kukasirika.) Sijambo, lakini mimi si bingwa. Ubingwa gani na hata tone la maji sina?
Leni: Samahani kaka. Sikudhani unaweza kukosa maji. Ajabu! Matangi yako makubwa yamekauka?
Kibo: Bila shaka. Unavyoona kiangazi kimetuathiri sisi sote. Hali ya anga isipobadilika tutaangamia.
Leni: (Akionyesha kuhuzunika.) Ni kweli unavyosema mwenzangu. Lakini hiyo anga itabadilikaje ilhali miti inakatwa ovyo?
Kibo: Ipo haja ya sisi kushirikiana ili kutunza na kuhifadhi mazingira yetu. Kumbuka tusipoziba ufa...
Leni:  (Akikubaliana naye.) Tutajenga ukuta. Nasikitika hali hii ikiendelea tutakosa chakula. Wanyama na ndege nao watakosa makao.
Kibo:  Mwandani wangu, hakika utunzi wa mazingira ni wajibu wetu.
Leni:   Kweli kabisa. (Wanaagana na kuondoka)

  1. Leni alimwamkua Kibo, hujambo? Ni salamu gani nyingine ambayo Leni angetumia kumwamkua Kibo?
    1. Chewa?
    2. Masalkheri?
    3. Sabalkheri?
    4. Shikamoo?
  2. Leni alitumia lugha ya adabu alipokuwa akizungumza na Kibo. Chagua kauli aliyoitumia inayoonyesha adabu.
    1. Umejitwika mtungi kichwani kutafuta maji!
    2. Wanyama na ndege nao watakosa makao.
    3. Matangi yako makubwa yamekauka?
    4. Ni kweli unavyosema mwenzangu.
  3. Katika mazungumzo, msikilizaji anaweza kukamilisha kauli ya anayezungumza. Chagua kauli iliyotumiwa kukamilisha nyingine katika mazungumzo haya.
    1. Bila shaka.
    2. Tutajenga ukuta.
    3. Kweli kabisa.
    4. Samahani kaka.
  4. Leni alimweleza Kibo athari za kutotunza mazingira. Ungekuwa Kibo, ungetaja athari gani nyingine?
    1. Kiwango cha joto kuongezeka.
    2. Wanafunzi kuacha shule.
    3. Mahusiano baina ya watu yataharibika. 
    4. Vyombo vya usafiri wa umma vitapungua.
  5. Neno mwandani limetumika katika mazungumzo. Chagua neno lenye maana sawa na mwandani.
    1. Ndugu.
    2. Jirani.
    3. Sahibu.
    4. Mwenza.

Swali la 6 hadi la 9

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.

Ushuru ni malipo yanayotozwa na serikali kama ada ya kuingiza bidhaa ndani ya nchi au kuziuza nje ya nchi. Pia, ni ada inayotozwa raia kwa kuuza au kununua huduma mbalimbali. Nchi yetu hutegemea ushuru ambao wananchi hutozwa ili kuendesha shughuli zake.

Shirika lenye jukumu la kukusanya ushuru nchini Kenya ni Halmashauri ya Ukusanyaji Ushuru almaarufu KRA. Shirika hili limepewa mamlaka ya kikatiba kukusanya aina zote za ushuru: ushuru wa mapato, ushuru wa forodhani, ushuru kutokana na shughuli za kitalii na nyinginezo.

Serikali huandaa bajeti kila mwaka ili kuhakikisha matumizi yafaayo ya fedha. Bajeti huwa na makadirio ya mapato na mgao wa fedha kwa matumizi mbalimbali. Makadirio hayo husomwa bungeni na Waziri wa Hazina ya Kitaifa kisha kuidhinishwa.

Ni wajibu wa kila mwananchi kulipa ushuru ili taifa letu liweze kujitegemea. Tukifanya hivyo, tutaweza kupiga hatua kimaendeleo. Tutakuwa na miundomsingi bora, huduma nzuri za kimsingi kama vile afya na elimu na hata nafasi zaidi za ajira

  1. Kulingana na kifungu, maendeleo ya taifa hutegemea:\
    1. bidhaa zinazouzwa.
    2. bajeti ya taifa.
    3. huduma za kimsingi.
    4. ushuru unaotozwa.
  2. Kifungu kimeonyesha kuwa ni haki ya KRA kukusanya ushuru kwa sababu:
    1. bajeti huandaliwa kila mwaka.
    2. imepewa mamlaka kikatiba. 
    3. ni muhimu kuhakikisha matumizi yafaayo ya fedha.
    4. bidhaa nyingi huuzwa ndani na nje ya nchi.
  3. Miundomsingi ikiimarika:
    1. viwanda vya uzalishaji bidhaa vitaimarika.
    2. wakulima watapata mazao mengi. 
    3. idadi ya watu itaongezeka.
    4. uharibifu wa mazingira utapungua.
  4. Chagua maana ya neno kuidhinishwa kama lilivyotumiwa katika kifungu.
    1. kuwasilishwa.
    2. kuchunguzwa.
    3. kukubaliwa.
    4. kukamilika.

Swali la 10 hadi la 12

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.

Likizo iliyopita nilitumia muda wangu wa mapumziko kumsaidia mlezi wangu kuwatunza mifugo wetu. Jambo hilo lilimfurahisha sana mlezi wangu akanizawidi ndama wa kike. Nilimpa ndama wangu jina, Simati.

Nilijitolea kwa hali na mali kumtunza Simati. Anapendeza kwa rangi yake nyeupe na madoa meusi. Matarajio yangu ni kwamba siku za usoni atapata ndama wake. Wakati huo utakapofika, nitamkama maziwa.

Maziwa nitakayoyapata nitayagawa kwa matumizi ya nyumbani na mengine nitayauza kwa usaidizi wa mlezi wangu. Hela nitakazopata kutokana na mauzo ya maziwa hayo, nitaziweka kama akiba kwani akiba haiozi.

  1. Kulingana na kifungu, msimulizi alipewa zawadi kwa sababu:
    1. alifika nyumbani kwa likizo.
    2. alimsaidia mlezi wake.
    3. alimpa ndama jina Simati.
    4. alitamani kuuza maziwa.
  2. Chagua jibu linaloonyesha kuwa msimulizi anafahamu uwekezaji.
    1. Anatumia likizo yake vizuri.
    2. Anatarajia Simati atapata ndama.
    3. Anafurahisha sana mlezi wake.
    4. Anapanga kuuza maziwa ili apate pesa.
  3. Msimulizi alimsaidia mlezi wake kuwatunza mifugo wao. Kuwatunza ni:
    1. kuwalinda.
    2. kuwatayarisha.
    3. kuwapenda.
    4. kuwafurahisha.

Swali la 13 hadi la 15

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali

Kesho ni Ijumaa. Itakuwa sikukuu ya Mashujaa nchini. Kutakuwa na sherehe ya kuadhimisha siku hiyo. Jena na Joana watakariri shairi kuhusu mashujaa. Tangu juzi, wamekuwa wakifanya mazoezi ili kujiandaa. Mtondogoo watarejea shuleni. Watawasimulia wenzao kuhusu matukio ya siku hiyo.

  1. Jena na Joana watarejea shuleni mtondogoo. Mtondogoo itakuwa siku gani?
    1. Jumamosi.
    2. Jumapili.
    3. Jumatatu.
    4. Jumanne.
  2. Chagua vitendo vinavyoonyesha kuwa Jena na Joana wanapenda nchi yao.
    1. Kuhudhuria sherehe, kukariri shairi. 
    2. Kurejea shuleni, kukariri shairi.
    3. Kusimulia matukio, kuhudhuria sherehe.
    4. Kusimulia matukio, kurejea shuleni.
  3. Maana ya kujiandaa kulingana na kifungu ni:
    1. kujitambulisha.
    2. kujitayarisha.
    3. kujinufaisha.
    4. kujiburudisha.

Soma kifungu kifuatacho. Kina nafasi 16 hadi 20. Umepewa majibu manne hapo. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.

Kuwa na afya yaani ____16____  bora ni jambo muhimu kwa binadamu. Mlezi wangu husema kuwa lishe bora na mazoezi ya viungo vya mwili ni njia ____17_____ ya kutupatia afya njema. Yeye huhakikisha kwamba ____18____ matunda, mboga, mihogo na maharagwe ____19____ wingi. Tukiwa
na afya njema, tutaweza kufanya kazi kwa bidii kama ____20____.

   A  B  C  D
 16.  uhai  nguvu   kimo   siha 
 17.  kuzuri  nzuri  mzuri  vizuri
 18.  tunakula  tungekula   tukila   tulikula 
 19.  ya  kwa  ni  vya
 20.  kiwavi  mchwa   tausi   njiwa 


Kutoka swali la 21 hadi la 30, chagua jibu sahihi.

  1. Chagua umoja wa:
    "Majembe yatatumiwa kupalilia mipapai yao michanga".
    1. Jembe litatumiwa kupalilia mipapai yake michanga.
    2. Jembe litatumiwa kupalilia mipapai yake mchanga
    3. Jembe litatumiwa kupalilia mpapai wake mchanga.
    4. Jembe litatumiwa kupalilia mpapai wake michanga.
  2. Chagua jibu sahihi kujaza pengo.
    Jakaya amekuwa akiwasaidia ______________________ zamani.
    1. hadi
    2. kisha
    3. tena
    4. tangu 
  3. Ukitaka kwenda chooni utamwomba mwalimu ruhusa kwa kumwambia unataka kwenda ________________________.
    1. bafuni.
    2. majifichoni.
    3. msalani.
    4. chumbani
  4. Matu ni fundi wa nguo. Rinda la Anna limeshonwa na Matu. Kwa hivyo, Anna __________________________ rinda na Matu.
    1. wameshonewa
    2. wameshonesha
    3. ameshonewa
    4. ameshonesha
  5. Chagua jibu sahihi kujaza nafasi.
    Mlango _______________________ darasa ni safi.
    1. za
    2. ya
    3. wa
    4. la
  6. Mjomba wako alikuletea zawadi juzi. Ikiwa leo ni Jumamosi, mjomba wako alikuletea zawadi siku gani?
    1. Jumanne.
    2. Jumatano.
    3. Alhamisi.
    4. Ijumaa.
  7. Tamu ni kwa chungu ilhali mwepesi ni kwa:
    1. mzito.
    2. mkubwa.
    3. mnene.
    4. mpana.
  8. Chagua jibu linaloonyesha ukanusho wa sentensi ifuatayo:
    Munira amesoma kitabu hicho. A
    1. Munira hasomi kitabu hicho. 
    2. Munira hatasoma kitabu hicho. 
    3. Munira hakusoma kitabu hicho. 
    4. Munira hajasoma kitabu hicho.
  9. Mtu anapomhimiza mwenzake kufanya kazi, tunasema anamtia shime. Je, mtu anapomsaidia mwenzake katika jambo fulani huwa:
    1. anamfanyia hima.
    2. anampiga jeki. zamani.
    3. anachapa kazi.
    4. anatia fora
  10. Katana na Kombo hawapendi kushirikiana na wenzao kufanya shughuli za vikundi darasani.
    Chagua methali inayoweza kutumiwa kuwashauri kubadilisha tabia hii.
    1. Asiyesikia la mkuu huvunjika guu.
    2. Chelewa chelewa utakuta mwana si wako.
    3. Mchagua jembe si mkulima.
    4. Jifya moja haliinjiki chungu.
Tagged under

Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne hapo. Jaza kila pengo kwa kuchagua jawabu lifaalo zaidi.

Usawa wa jinsia ni suala __1___ kwa muda mrefu hapa ___2___. Tabia ya kumpendelea mtoto wa jinsia moja __3___ nyingine imeepigwa na wakati. Mtoto yeyote __4____ ipasavyo anaweza kufanikiwa na kuifaa jamii __5___. ___6__ kumdhulumu mtoto kwa misingi ya kijinsia humfanya ajione duni, yaani __7___. Ni vyema tushikane mikono kukabiliana na __8___ wa kijinsia kwani ___9___.

   A
 1   uliojadiliwa   lililojadiliwa   iliyojadiliwa   yaliyojadiliwa
 2   kwetu   mwetu   yetu   petu
 3   kuliko   kumliko   kuiliko   kuwaliko
 4   akilewa   angelelewa   akilelewa   angelewa
 5   yetu   yako   yake   yenu
 7   Ilhali   Hata hivyo   Juu ya hayo   Angaa
 8   ajichukie   ajishuku   ajitwaze   ajibeze
 9  uso wa kufadhiliwa    u chini.  ukibebwa   usilevyelevye  miguu.   pasi na viganja viwili     kofi hazilii.  papo kwa papo kamba   hukata jiwe.


Mwalimu ___10___ kwamba Fatu alikuwa_11___, alimwita faraghani ili ___12___ na kupata kiini cha huzuni yake. Huku __13___na matone ya machozi, Fatu alimweleza mwalimu huyo kuwa wavyele wake walikuwa na mipango ya kumwachisha shule na __14___ kwa __15___wa rika la babu yake. Mwalimu alimhimiza asiwe na wasiwasi maadamu angemsaidia kuepuka kadhia hiyo

   A
 10  aligundua  akagundua  alivyogundua  alipogundua
 11  amejishika tama  amepiga mafamba  amekula mwande  ametia mrija
 12  amsajili  amsaili  amsitiri  amsaliti
 13  amedondokwa  anatiririkwa  akidondokwa   akitiririkwa
 14  kumwoa  kumwolesha  kuoleka   kumwoza
15  buda  ajuza  kaimu  barobaro


Kuanzia swali la 16 hadi la 30, chagua jibu lifàalo zaidi kulingana na maagizo uliyopewa.

  1. Chagua sentensi iliyotumia "ki" kuonyesha vitendo sambamba.
    1. Uzi huo ukivutwa sana utakatika.
    2. Msukaji aliimba akisuka vikapu.
    3. Kijiji hicho kiliwavutia wageni kwa wenyeji.
    4. Wacheza ngoma wote walivalia kitamaduni.
  2. Upi ni ukanusho ufaao wa sentensi; Mahali kuliko na mlipuko wa maradhi kunahitaji msaada.
    1. Mahali kusiko na mlipuko wa maradhi kunahitaji msaada.
    2. Mahali kuliko na mlipuko wa maradhi hakutahitaji msaada.
    3. Mahali kuliko na mlipuko wa maradhi hakujahitaji msaada.
    4. Mahali kusiko na mlipuko wa maradhi hakuhitaji msaada.
  3. Ni jibu lipi lililo na maneno ambayo hayalingani?
    1. Chawa, funza, utitiri, kunguni.
    2. Singe, manowari, bunduki,kombora.
    3. Wengu, nyongo, pafu, waridi
    4. Robo, humusi, thuluthi, sudusi
  4. Andika kauli ya kutendewa ya sentensi;
    Masogora waliingia ukumbini wakacheza ngoma.
    1. Ngoma ilichezewa ukumbini na masogora.
    2. Ukumbini mlichezwa ngoma na masogora.
    3. Masogora walichezea ngoma ukumbini.
    4. Ngoma ilichezwa na masogora ukumbini.
  5. Ni ulinganifu upi ulio sahihi?
    1. Jimbi - mtamba
    2. Fahali - koo
    3. Mjomba - halati
    4. Kipora - mbarika
  6. Andika katika hali ya umoja.
    Nyuta hizo zilitumiwa na wasasi hodari.
    1. Ukuta huo ulitumiwa na msasi hodari.
    2. Uta huo ulitumiwa na msasi hodari.
    3. Uta huo ulitumiwa na msasi mhodari.
    4. Ukuta huo ulitumiwa na msasi mhodari.
  7. Chagua sentensi yenye kihusishi cha kulinganisha.
    1. Wageni waliwasili baada ya sherche kuanza.
    2. Timu yetu ilicheza dhidi ya Miamba angu wa Pwani.
    3. Kilate alimwendea mwalimu kwa ushauri.
    4. Jengo hilo lilikuwa kubwa mithili ya mlima.
  8. Aka ni kwa mwashi kama ilivyo kwa msasi.
    1. saka
    2. sasa
    3. saa
    4. susia
  9. Badilisha katika usemi wa taarifa:
    "Mtoto wako atatibiwa leo," daktari alimwambia mama huyo.
    1. Daktari alimwambia mama huyo kwamba mtoto wake atatibiwa siku hiyo.
    2. Daktari alimwambia mama huyo kwamba mtoto wake angetibiwa siku ambayo ingefuata.
    3. Daktari alimwambia mama huyo kwamba mtoto wake angetibiwa siku hiyo.
    4. Daktari alimwambia mama huyo kwamba mtoto wake anatibiwa siku hiyo.
  10. Chagua vielezi katika sentensi ifuatayo. Wanafunzi wote walitembea taratibu hadi ukumbini.
    1. walitembea, hadi
    2. hadi, ukumbini
    3. taratibu, ukumbini
    4. taratibu, wote
  11. Tegua kitendawili kifuatacho;
    Akiona miale ya jua hufa.
    1. Umande
    2. Samaki
    3. Kobe
    4. Mvua
  12. Kipi ni kisawe cha nahau enda upogo?
    1. enda mserego
    2. enda joshi
    3. enda masia
    4. enda mrama
  13. Chagua maelezo yasiyo sahihi.
    1. Ngonjera ni shairi la majibizano.
    2. Arudhi ni kanuni za utunzi wa mashairi.
    3. Utenzi ni shairi lenye vipande viwili katika mishororo.
    4. Vina ni silabi zinazofanana katikati au mwishoni mwa mishororo.
  14. Pora ni jogoo ambaye hajaanza kuwika. Pora pia ni
    1. chopoa kwa nguvu kitu alichoshika mtu.
    2. mnyama jamii ya nyegere alayc asali.
    3. tendo la kuondoa magamba ya samaki.
    4. funga kitu kwa kukaza sana.
  15. Mzazi au kiongozi anapoondoka, wale waliomtegemea hutaabika sana.
    Chagua methali inayolingana na maclczo haya.
    1. Mkuu hukua kwao.
    2. Mti ukianguka ndege hutawanyika
    3. Akikalia kigoda mtii
    4. Mti hauendi ila kwa nyenzo.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali kuanzia 31 mpaka 40

Kwa muda mrefu jamii imekuwa ikimpigia debe mtoto wa kike. Jambo hili limewekwa katika nyanja tofauti tofauti; elimu, afya, nafasi za ajira, katika dini na kwingineko. Kuwezeshwa huku kwa mtoto wa kike kumekithiri na dalili zimejitokeza katika hali mbalimbali. Dalili iliyo kubwa zaidi ni kutelekezwa kwa mtoto wa kiume. Yeye amesahaulika kabisa kiasi kwamba hakuna kundi au juhudi za kiutawala ambazo zimewekwa kuhakikisha kuwa naye hajaachwa nyuma kama mkia.

Kutelekezwa kwa mtoto wa kiume kumeanza kuonyesha matokeo yasiyoridhisha. Suala la kwanza lililo dhahiri ni matumizi ya mihadarati. Jamii haina wakati wa kumshughulikia mtoto wa kiume. Hali hii imemwacha huru kufanya maamuzi yake. Uhuru usiodhibitiwa ni hatari. Uhuru huu umemfanya kutumia wakati wake apendavyo. Njia mojawapo ni katika kutumia mihadarati na kushiriki hulka nyingine ambao zina madhara makubwa. Yeye akiendelea kufanya hivyo, mwenzake wa kike anaendelea kutunzwa kwa hali na mali hata katika kiwango cha kudekezwa.

Kupuuzwa kwa mtoto wa kiume kumemfanya abaki nyuma kielimu. Hatukuwa tukishuhudia kudorora kwa matokeo ya mitihani kwa watoto wa kiume? I lakuna aliyethubutu kuhoji sababu labda kwa kuhofia kubandikwa nembo ya taasubi ya kiume. Mtoto wa kiume anapoendelea kufanya vibaya katika masomo hubaki nyuma na hata katika kuchukua nafasi za ajira baadaye. Hali hii hudhihirika kiuchumi ambapo wanaume wengi hawawezi kufikia mishahara ambayo wenzao wa kike wanapata. Wanawake pia wamepanda hata kuchukua nyadhifa muhimu katika ngazi za kitaifa na kimataifa.

Tuhuma za kuwanyanyapaa wale ambao wamekuwa wakiunga mkono juhudi za mwanamume kujiendeleza zimekuwa sumu. Sumu hii imeleta matokeo ya kuibuka kwa taasubi ya kike. Mmea wa taasubi hii umepaliliwa na kunyunyiziwa maji na mashirika ya kijamii yanayompigia debe mwanamke na hata katika vyombo vya habari kupitia kutetea haki za wanawake. Kwa muda mrefu hatukuwa na shirika lolote lililotetea haki za mtoto wa kiume au hata vipindi vilivyopigia debe juhudi za kuwainua watoto hao.

Mawazo ambayo yamekuwa yakipigiwa upatu na mashirika ya kutetea haki za mtoto wa kike na hata vyombo vya habari yamekita mizizi hata akilini mwa wazazi. Nani atapinga hili? Ithibati ya jambo hili i wazi kabisa. Ukitembea mitaani utawapata watoto wa kiume wakicheza bila suruali huku wa kike wakiwa wamevalishwa nguo nadhifu.

Nyumbani utawapata watoto wa kiume wakila vyakula vigumu huku wenzao wakila mapochopocho. Hata katika majina hili linajitokeza. Wazazi hufanya juhudi kubwa kuwachagulia majina wanao wa kike. Si ajabu nafasi ya mwanamume imeendelea kubanwa. Visa vya wanaume kupigwa na wanawake ni mojawapo ya matokeo.

Hali hii ya kuinuliwa kwa mtoto wa kike imekuwa ikifanywa bila kuzingatia mambo mengi muhimu. Jambo moja ambalo hakuna aliychoji ni; Kwa nini mtoto wa kike ainuliwe? Ikiwa ni ili afikishwe kiwango cha mwenzake wa kiume, basi alimfikia na kumpita. Kama hali ndiyo hii, basi ni muhimu mtoto wa kiume naye ainuliwe. Hili litaafikiwa ikiwa mbinu zilezile zilizotumiwa kwa mtoto wa kike zitakumbatiwa.

Suluhu itapatikana vipi? Tatizo la kutelekezwa kwa mtoto wa kiume litapewa ufumbuzi ikiwa tutapiga hatua nyuma tujiulize ni kwa nini tulihitaji kulinda haki za mtoto wa kike. Bila shaka, jambo moja litakuwa wazi kuwa mtoto wa kike alikuwa akibaki nyuma kutokana na sababu za kimazingira hasa ya kijamii. Ikaibuka haja ya kumsaidia kukabiliana na changamoto za mazingira hayo. Abadan kataan kutelekezwa kwa mtoto wa kiume hakukuwa mbinu mojawapo ya kutetea haki za mtoto wa kike.

  1. Chagua maelezo sahihi kulingana na aya ya kwanza
    1. mtoto wa kiume amepuuzwa kwa muda mrefu.
    2. jamii imetekelezwa mikakati mbalimbali ya kumwinua msichana.
    3. watawala ndio wanaochangia zaidi. kudhalilishwa kwa mvulana.
    4. haki za watoto wote zimepigiwa debe na mashirika mbalimbali.
  2. Jambo analopinga mwandishi katika aya ya pili hasa ni
    1. kumpa mvulana uhuru mwingi kupindukia.
    2. jitihada nyingi kuelekezwa katika malezi ya msichana.
    3. vijana kutumia mihadarati kupindukia.
    4. mvulana kujikulia bila maelekezo yafaayo.
  3. Si kweli kusema kuwa;
    1. wanaume hawapati nyadhifa nzuri kitaifa na kimataifa.
    2. msichana anabembelezwa kupita kiasi."
    3. maovu katika jamii yanadhihirisha pengo katika malezi.
    4. kumpa mtoto wa kike nyadhifa mbalimbali ni jambo la busara.
  4. Kwa nini wengi hawakuthubutu kuhoji kiini cha kudorora kwa elimu ya mtoto wa kiume?
    1. Jambo hilo lilitokea bila wengi kujua.
    2. Matokeo duni kwa mvulana lilikuwa jambo la kawaida.
    3. Kumtetea mvulana kulichukuliwa kama kupinga maendeleo ya msichana.
    4. Kumwinua mvulana kupita kiasi kungemnyima msichana nafasi ya kufanya vyema.
  5. Kwa nini wanaume hawana mishahara mizuri kama wenzao wa kike?
    1. Wanaume wananyimwa nafasi ya kujitetea kazini.
    2. Wanawake ni wengi kuliko wanaume
    3. Wanawake wengi wameelimika kuliko wanaume.
    4. Waajiri wengi hivi sasa ni wanawake.
  6. Mashirika ya kijamii na vipindi katika vyombo vya habari;
    1. hupendelea jinsia ya kiume zaidi.
    2. vinapaswa kutekeleza shughuli kwa usawa
    3. vimetekeleza wajibu wao sawasawa.
    4. hutumiwa kumdhalilisha mtoto wa kike.
  7. Aya ya tano imedokeza kuwa
    1. mvulana amenyimwa hata haki za kimsingi.
    2. watoto wa kiume wanahimizwa kucheza bila mavazi.
    3. mtoto wa kike anatimiziwa haki zake zote.
    4. wavulana wasiovalia suruali hudharauliwa na wasichana wenye mavazi nadhifu michezoni.
  8. Msimamo wa mwandishi wa makala haya ni kuwa
    1. kuinuliwa kwa msichana kumeleta madhara mengi kuliko manufaa katika jamii.
    2. juhudi za kumwimarisha msichana zinafaa kusitishwa ili mvulana naye aangaziwe.
    3. mvulana anapaswa kusaidiwa ili naye ampiku mwenzake wa kike.
    4. juhudi za kupigania usawa wa kijinsia zinapaswa kulenga watoto wa jinsia zote.
  9. Kauli yamekita mizizi imetumia tamathali gani ya usemi?
    1. Sitiari
    2. Tashbihi
    3. Chuku
    4. Nahau
  10. Neno kuwanyanyapaa kulingana na muktadha lina maana ya
    1. kuwapinga
    2. kuwabeza.
    3. kuwazomea
    4. kuwadhihaki

Soma kifungu hiki kisha ujibu maswali kuanzia nambari 41 mpaka 50

Siku ya Geza na mwanawe kutoka hospitalini ilifika. Muuguzi aliwashauri wamtunze mtoto huyo vyema; kwamba mtoto mwenyewe hakuwa na dosari kubwa, ila alihitaji utunzaji wa makini zaidi. Maneno hayo yaliangukia masikio yaliyokuwa yametiwa nta. Hisia za unyonge na maonevu zilimkubatia Geza kiasi cha kuuycyusha utu wake. Mumewe alikuja kumchukua kutoka hospitalini.

Nyumbani mwa Geza na Kataa hamkusikika vigelegele vya kuzaliwa kwa kiumbe kipya. Geza alitoka garini kakipakata kitoto chake kama kifurushi cha karatasi ya shashi. Akafululiza moja kwa moja hadi chumbani mwake ambamo angekificha kitoto hicho kwa miaka mingi. Wageni waliwasili kukiona kitoto, wakatiliwa huku na kutolewa kule. Mara kitoto kina homa, mara kimelala...... almradi kila mara mama mtu alikuwa na uongo wa kuwazulia watu. Nao adinası hawakuwa mazumbukuku kiasi kile. Walikuwa wamesikia tetesi kutoka kwa akina pangu pakavu wa humo kijiji kuhusu hali ya mtoto huyo, navyo vitendo vya Geza viliwasaidia kupiga muhuri mawazo yao. Jambo lililowashangaza wapenda haki ni vipi mama ataweza kumfungia mtoto wake chumbani. Vipi mama huyo hakuweza hata kumpeleka mwanawe hospitalini kwa matibabu na
msaada zaidi?

Vitendo vya kikatili vya Geza havikumzuia mtoto kukua. Mwanatabu alitambaa, akasota, akasimama dede japo kwa taabu hadi akachukua hatua yake ya mwanzo na kuanza kutembea. Mama mtu aliyatazama hayo bila kuridhika Daima alimlinganisha mwanawe na wale wa majirani. Alishindwa kuelewa kwa nini mtoto wake bado anaboboja maneno tu badala ya kuzungumza kama watoto wa wifi yake.

Hata mtoto alipofikia umri wa kuenda shule, Geza alidinda kumpeleka hadi mume wake Kataa alipomlazimisha kufanya hivyo. Japo Kataa alitaka mtoto huyo apelekwe katika shule mahsusi za watoto wanaohitaji kushughulikiwa kwa makini, Geza alikataa katakata. Alimpeleka katika shule mojawapo ya umma hapo karibu akidai kuwa hapana pesa kwani mtoto wao wa kiume ambaye alizaliwa miaka miwili baada ya Mwanatabu kuzaliwa, alihitaji kushughulikiwa pia.

Mwanatabu aliingia shuleni na kujipata katika lindi kubwa la simanzi. Kwa vile alikuwa amezoea kuishi amefungiwa ndani asije akaonekana na kuchekwa na watu, alipata shida nyingi kuingiliana na watoto wengine. Kila alipowaona wenzake alikimbilia mwalimu kwa usalama. Mawasiliano nayo yalikuwa magumu kwani Mwanatabu hakuwa amemudu kuzungumza vyema. Mwalimu alipozungumza naye Mwanatabu alikenua meno tu na kusema maneno ambayo yalimwia vigumu mwalimu kuyafasiri.

Siku za mwanzomwanzo mwalimu alivumilia akidhani hilo lilikuwa tatizo dogo tu. Baadaye aliona kwamba hafikii popote, kwani kwa sababu ya kutoweza kuwasiliana vyema na wanafunzi wenzake, mwana huyu alizua mbinu ya kuwawezesha wenzake kumsikiliza. Alianza kuwachapa na kuwawinga kama ndege wawingwavyo kutoka shamba la mtama. Mwalimu hakusita kuwaita wavyele wa Mwanatabu ambao bila shaka walikiri mtoto wao alikuwa na tatizo tangu kuzaliwa.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo aliwashauri wampeleke Mwanatabu katika hospitali ambamo mna kliniki ya kuwazoesha watoto kuzungumza. Aidha, aliwatafutia shule mahsusi ya watoto walio na tatizo kama la Mwanatabu.

Hivi sasa, Geza hukumbuka kwa uchungu na jitimai kubwa jinsi alivyokuwa amepania kumtelekeza mwanawe katika hali mbaya ati kwa sababu kazaliwa na upungufu wa kihali na kimwili. Mara tu baada ya Mwanatabu kupelekwa kwa matibabu zaidi na kusomea katika mazingira yaliyomfaa zaidi hali yake ilianza kuimarika. Aliweza kuzungumza. Maendeleo yake katika masomo yaliimarika, nao walimu hawakusita kutambua hayo na kumpeleka katika shule ya kawaida. Hivi sasa amehitimu masomo ya chuo kikuu. Amewafaa watoto wengi walio na matatizo ya kimaumbile. Maisha yake ni funzo na dhihirisho kuwa hakuna binadamu ambaye hawezi kutekeleza majukumu kama wengine akipewa fursa ipasavyo. Upungufu wa kimaumbile si kutojiweza. Haifai kuwabagua adinasi kwa misingi ya tofauti za kimaumbile.

  1. Ni maelezo yapi sahihi kulingana na kifungu?
    1. Muuguzi alijua kuwa Geza asingemtunza mwanawe ipasavyo.
    2. Geza alitilia maanani nasaha aliyopewa na muuguzi.
    3. Muuguzi alitekeleza wajibu wake ipasavyo.
    4. Geza alijihisi mnyonge kutokana na maneno ya muuguzi,
  2. Nyumbani mwa Geza na Kataa hamkusikika vigelegele kwani,
    1. watu hawakufika kwa sherehe ya kumpokea mtoto.
    2. mtoto hakupokelewa kwa bashasha kama ilivyotarajiwa.
    3. mke na mume waligombana kutokana na hali ya mtoto.
    4. mtoto alikuwa mwenye kasoro nyingi za kimaumbile.
  3. Waliofika nyumbani kwa Géza,
    1. hawakupewa fursa ya kumwona mtoto.
    2. walitaka kumdhihaki mtoto na mwanawe.
    3. walieneza uvumi kila mahali.
    4. ni jamaa wa karibu wa Geza na Kataa pekee.
  4. Pesa anazotoa mtu ili kumshika mioto mchanga kwa mara ya kwanza huitwaje?
    1. Ridhaa
    2. Arbuni
    3. Kifunguamkoba
    4. Fola
  5. Si kweli kusema kuwa,
    1. wapo waliojua hali ya mtoto wa Geza.
    2. vitendo vya Geza vilichangia watu kuongea zaidi.
    3. Geza na Kataa walikuwa na watoto wawili
    4. watu hawakujali dhuluma alizopitia Mwanatabu.
  6. Kwa nini Mwanatabu hakupelekwa mapema katika shule ya watoto wenye mahitaji maalum?
    1. Wavyele wake walikosa maarifa.
    2. Ulikuwepo ugumu wa kumtunza yeye na mnuna wake.
    3. Mama yake alimbagua kutokana na hali yake.
    4. Ilimchukua muda mrefu kuzungumza na kutembea.
  7. Kulingana na aya ya sita,
    1. tatizo katika mawasiliano huweza kuchangia visa vya utovu nidhamu.
    2. kuchelewa kuenda shule hutatiza mawasiliano ya wanafunzi na walimu.
    3. kutowasiliana ipasavyo huwafanya wanafunzi wasimwelewe mwalimu.
    4. kutishwa na wengine huwafanya wanafunzi wajitenge na wenzao shuleni.
  8.  Akina pangu pakavu kulingana na makala haya ni
    1. walio na upungufu wa kimaumbile.
    2. wenye tabia ya kufitini.
    3. wanaochunguza ukweli.
    4. watu wanyonge.
  9. Mambo yaliyomsaidia Mwanatabu kufanikiwa katika kifungu hiki hasa ni A
    1. kutangamana na wengine na himizo la mwalimu mkuu.
    2. matitabu na kusomea katika mazingira yafaayo
    3. ushauri wa walimu na kusomea katika shule ya umma.
    4. kupelekwa shule na msimamo thabiti na baba yake.
  10. Funzo linalopatikana katika kifungu hiki ni kuwa;
    1. Wanaowapuuza wanyonge huaibika baadaye.
    2. Binadamu ni ng'amba hawakosi la kuamba.
    3. Ukimlea mwana mwema na mui mlee.
    4. Hakuna msiba usiokuwa na mwenziwe.

INSHA

Umepewa dakika 40 kuandika insha yako.
Wewe ni kiranja mkuu wa shule yako. Andika hotuba utakayowatolea wanafunzi wenzako wa darasa la nane kuhusu umuhimu wa kuzingatia maadili hata baada ya kukamilisha mtihani wa kitaifa.

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

  1. B
  2. D
  3. A
  4. C
  5. C
  6. B
  7. D
  8. A
  9. C
  10. D
  11. A
  12. B
  13. C
  14. D
  15. A
  16. B
  17. D
  18. C
  19. A
  20. C
  21. B
  22. D
  23. A
  24. B
  25. C
  26. B
  27. D
  28. C
  29. A
  30. B
  31. B
  32. D
  33. A
  34. C
  35. C
  36. B
  37. A
  38. D
  39. D
  40. B
  41. C
  42. B
  43. A
  44. D
  45. D
  46. C
  47. A
  48. B
  49. B
  50. C

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata.

G6SwaET3S12023Q1

Siku moja wakati wa likizo, nyanya alitusimulia kisa cha kuhuzunisha mno. Sote tulikusanyika karibu na moto na kutulia tuli. Kila mmoja alikuwa kwa hamu na hamumu ili kupata uhondo wa hadithi ambayo angetutambia.

Baada ya kutulia kama maji ya mtungi na kujikohoza kidogo, alianza hivi, "Hadithi, hadithi..."Sote tulijibu,
"Hadithi njoo." Kisha akaendelea, "Hapo zamani za kale, zama za kuumbwa kwa ulimwengu, binadamu walifaa kupewa ujumbe muhimu mno. Ujumbe huo ndio uliofaa kuamua iwapo wangekuwa wakifa au waishi milele. Wapo walioomba ili ujumbe mzuri uwafikie. Kila mmoja alisubiri akielewa kuwa subira huvuta heri. Kinyonga ndiye aliyepewa ujumbe wa uhai. Ndege naye alipewa ujumbe wa kifo. Yule ambaye angetangulia kufikisha ujumbe, ndiye ambaye angeamua hatima ya binadamu. Wote walipewa amri kuwa waondoke kuelekea kwa binadamu.

Kinyonga alikuwa kobe kama ilivyo desturi yake. Ndege naye alipaa angani kwa kasi kama umeme. Kufumba na kufumbua, binadamu walimwona ndege akiwasili na kifurushi cheusi tititi kama makaa. walikipokea huku nyoyo zao zikidunda dududu! Wote waliangua kilio kwa huzuni walipotambua kuwa kifurushi hicho kilikuwa kimebeba kifo. Kinyonga alionekana akijikokota kwa mbali akiwa na ujumbe wa uhai. Tangu siku hiyo, binadamu walianza kufa." Baada ya kisa cha nyanya, tulijikokota kwa huzuni tukienda kulala.

  1. Maneno 'kutulia kama maji ya mtungi' ni mfano wa fani gani ya lugha?
    1. nahau
    2. istiara
    3. tashbihi
    4. kisawe
  2. Hali ya kinyonga ilifaa kurekebishwa kwa methali gani?
    1. Haraka haraka haina baraka.
    2. Chelewa chelewa utapata mwana si wako.
    3. Asiyesikia la mkuu huvunjika guu.
    4. Achanikaye kwenye mpini hafi njaa.
  3. Kulingana na kifungu, ni kweli kuwa;
    1. binadamu alianza kufa tangu alipoumbwa. 
    2. binadamu walianza kufa baada ya kupokea ujumbe wa kinyonga.
    3. ndege ndiye aliyepewa habari za uhai.
    4. kifo cha binadamu kilitokana na kupokezwa ujumbe wa kifo kwanza.
  4. Maneno 'nyoyo zao zikidunda dududu' yanaonyesha kuwa binadamu walikuwa na;
    1. wasiwasi
    2. woga
    3. hasira
    4. huzuni
  5. Mwandishi anaposema kuwa 'kinyonga alikuwa kobe', ana maana gani?
    1. Alijifunika kama gamba la kobe
    2. Alilemewa na uzito wa mzigo aliobeba
    3. Alishindana na ndege kwa kasi
    4. Alienda polepole kama kobe
  6. Unadhani kwa nini wajukuu walijikokota kwa huzuni wakielekea kulala?
    1. Walimhurumia kinyonga
    2. Walikasirishwa na haraka ya ndege 
    3. Hawakufurahia tukio lililosababisha kifo
    4. Walihuzunishwa na uzee wa nyanya

Soma ufahamu unaofuata kisha ujibu maswali yanayofuata.

G6SwaET3S12023Q2

Juma, Hekima, Hidaya na Malkia ni wafanyabiashara. Wao ni wafanyabiashara ambao hulipa ushuru wa mapato kila mwisho wa mwezi. Juma huuza
vipuri vya magari, magari yenyewe na pikipiki. Hekima huuza magurudumu ya magari, baiskeli za watoto na pikipiki. Hidaya naye huuza baiskeli za watoto, pikipiki, vioo vya magari na magurudumu. Malkia huuza bidhaa zote zinazouzwa na Juma pamoja na fanicha katika duka jingine.

Juma ana maduka katika miji ya Kisumu, Mombasa na Kericho. Ukitaka kupata maduka ya Hekima, utayapata katika miji yote iliyo na maduka ya Juma pamoja na Nairobi na Naivasha. Hidaya naye ana maduka katika miji ya Molo, Nakuru, Naivasha na Mombasa. Malkia ana maduka katika miji yote kunakopatikana maduka ya Hidaya pamoja na Nairobi na Kisumu.

  1. Bidhaa gani ambazo huuzwa na kila mwanabiashara?
    1. pikipiki
    2. baiskeli za watoto
    3. magurudumu
    4. magari 
  2. Ni nani aliye na maduka katika miji mitano?
    1. Juma
    2. Hekima
    3. Hidaya
    4. Malkia 
  3. Mji gani ambako maduka ya wafanyabiashara hawa wote yanapatikana?
    1. Nairobi
    2. Naivasha
    3. Kisumu
    4. Mombasa

Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata.
(Wanafunzi wawili wanaonekana uwanjani wakati wa jioni, baada ya masomo ya siku.)

NZOLA : Hujambo Njeri? Unaendeleaje? (Akimnyoshea mkono.)
NJERI:    (Anamwangalia kwa makini, akimsalimia.) Sijambo rafiki yangu Nzola. Ninaendelea vyema. Nimefurahia sana kipindi cha leo kuhusu                         usafi  wa kibinafsi.
NZOLA: Enhe! Niambie mwenzangu.
NJERI:   Nimebaini umuhimu wa vitu kama vile mswaki, taulo, hanchifu, sabuni na kadhalika.
NZOLA(Akitikisa kichwa kuonyesha kuelewa.) Nami vilevile nimeelewa kuwa sifai kutumia vifaa kama vile mswaki, taulo na hanchifu pamoja na                   watu wengine.
NJERI:   Ukweli, hivyo ni vifaa vya kibinafsi.
NZOLA:  Kuanzia leo nitahakikisha kuwa ninaangua kucha na kupiga mswaki bila kuchoka.
NJERI:    Aha! Nami sina budi kuoga na kuinawa mikono yangu kwa njia inayofaa.
NZOLA:  Hewala Njeri. (Mlio wa kengele unasikika.)
NJERI:    Twende nyumbani mwenzangu. (Wanaondoka.)

  1. Kulingana na mazungumzo, ni kweli kuwa;
    1. Njeri hakujua umuhimu wa baadhi ya vifaa vya usafi.
    2. Nzola alielewa faida ya kutumia vifaa vya usafi pamoja na wengine.
    3. Njeri alifahamu kuwa si vizuri kutumia vifaa kama vile hanchifu na wengine.
    4. Njeri alijua umuhimu wa baadhi ya vya usafi.
  2. Yawezekana kuwa wanafunzi hao walipokutana, jua lilikuwa upande gani?
    1. mashariki
    2. kaskazini
    3. kusini
    4. magharibi
  3. Mwandishi alimaanishi nini aliposema kuwa 'nami sina budi'?
    1. Ninajua umuhimu
    2. Ninalazimika
    3. Ninafahamu
    4. Nina hiari
  4. Nahau 'ninaangua kucha' ina maana gani jinsi ilivyotumika katika mazungumzo?
    1. Ninakata kucha
    2. Ninaosha kucha
    3. Ninapangusa kucha
    4. Ninalinganisha kucha
  5. Mazungumzo haya ni mfano wa;
    1. mazungumzo katika muktadha rasmi
    2. mazungumzo yasiyofuata sheria
    3. mazungumzo katika muktadha usio rasmi 
    4. mazungumzo yasiyo na manufaa
  6. Kipi si kifaa cha kibinafsi kati ya vifaa vifuatavyo kulingana na mazungumzo?
    1. hanchifu
    2. mswaki
    3. taulo
    4. sabuni

Jaza nafasi zilizoachwa kwenye kifungu kifuatacho kwa jibu linalofaa.

Kulipa ushuru kuna manufaa sio tu kwa mtu binafsi ___16___ kwa nchi yote. Taifa ___17___ wananchi wanaolipa ushuru. ___18___ hatua kimaendeleo kila siku. Kulipa ushuru ___19___ kuwa mtu huyo ni mzalendo. Ombi ___20___ kwa kila mmoja wetu ni kuwa tulipe ushuru bila kuchelewa ili kuimarisha Kenya.

   A  B  C  D
 16.  mbali pia  lakini pia  bali pia  wala tena 
 17.  yenye  lenye   chenye   zenye 
 18.  hupigwa  hupigia  hupiga  hupigisha
 19.  kunaonyesha  unaonyesha  anaonyesha  wanaonyesha
 20.  langu  yangu  wangu  changu


Jibu maswali yafuatayo kulingana na maagizo.  

  1. Soma ni kwa 'somea' kama vile fua ni kwa ______________________________
    1. fuliwa
    2. fuliana
    3. fuia
    4. fulia  
  2. Neno gani lililo na silabi nne?
    1. lima
    2. kimbiliwa
    3. mbio
    4. lia
  3. Sentensi gani iliyoakifishwa kwa usahihi? 
    1. Walikula matunda kadhaa: mananasi, machungwa na maparachichi.
    2. Salaala! kumbe anaupenda usafi kiasi hicho.
    3. Je! Mwalimu wenu wa Kiswahili ni nani?
    4. Ngombe yule wa mjomba atafungwa wapi?
  4. Chagua sentensi inayoonyesha hali ya masharti.
    1. Waliokuwa wakisoma wameenda kula. 
    2. Angali anamsaidia mzee huyo kuvuka mto.
    3. Amina na mwikali husoma mara kwa mara.
    4. Ukimsaidia kijana huyo utabarikiwa na Mungu.
  5. Sentensi ipi inayoonyesha istiara?
    1. Mwanafunzi mwenye bidii kama mchwa ametuzwa.
    2. Yeye anajua kuwa bidii hulipa.
    3. Tumia hanchifu unapopenga kamasi.
    4. Babu yangu ni kobe, hajafika nyumbani.
  6. Tambua wakati na hali ya sentensi inayofuata.
    Walikuwa wakiandika mvua ilipoanza kunyesha.
    1. wakati uliopita, hali endelezi
    2. wakati ujao, hali endelezi
    3. wakati uliopita, hali timilifu
    4. wakati ujao, hali timilifu
  7. Nomino zipi zinazopatikana katika ngeli moja?
    1. mafuta, maradhi, matunda
    2. minyoo, mikahawa, mirathi
    3. chai, damu, kahawa
    4. kunguru, kuimba, kutu
  8. Onyesha ukubwa wa sentensi inayofuata.
    Jicho la ndovu liliumizwa na miti hiyo. 
    1. Jijicho la dovu liliumizwa na jiti hilo.
    2. Jijicho la dovu liliumizwa na majiti hayo.
    3. Kijicho cha kidovu kiliumizwa na kijiti hicho.
    4. Jijicho la jidovu jiliumizwa na majiti hayo.
  9. Chagua kinyume cha sentensi inayofuata
    Buda alicheka aliponunuliwa pora na kijana mnene.
    1. Shaibu alilia alipouziwa tembe na mzee mwembamba.
    2. Ajuza alilia alipouziwa tembe na mzee mwembamba.
    3. Buda hakucheka aliponunuliwa pora na kijana mnene.
    4. Bikizee alilia alipouziwa tembe na msichana mkonde.
  10. Halima alianza safari saa mbili kasorobo, safari hiyo ilichukua muda wa saa moja na robo. Je, aliwasili saa ngapi?
    1. 9:00
    2. 3:00
    3. 3:30
    4. 9:30

INSHA

Andika insha ya kusisimua ukianzia kwa maneno haya:-

Kipenga kilipolia, wachezaji wa timu zote mbili walijitosa uwanjani

MARKING SCHEME

  1. C
  2. B
  3. D
  4. A
  5. D
  6. C
  7. A
  8. B
  9. D
  10. A
  11. D
  12. B
  13. A
  14. C
  15. D
  16. C
  17. B
  18. C
  19. A
  20. A
  21. D
  22. B
  23. A
  24. D
  25. D
  26. A
  27. C
  28. B
  29. B
  30. A

Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne hapo.
Jaza pengo kwa kuchagua jawabu lifaalo zaidi.

Ni jambo la ___1____ kumfunza mtoto maadili___2____. Jamii __3____mapema huja___4___ baadaye na matendo ya mtoto huyo. Ndiposa wahenga wakasema___5___ Kitendo cha baadhi ya wazazi kuwaachia walimu jukumu la kuwarekebisha watoto___6__kwani huonyesha ukosefu wa___7____katika malezi. Watoto nao wasiwe___8__, ___9___wakionywa wakubali kubadili mienendo yao.

   A
 1.  dharura  muhali   muhimu   hiari 
 2.  tangu  hadi   angaa   lau 
 3.  wasipomfunza  lisilomfunza   isiomfunza   isipomfunza 
 4.  kuathirika  kuathirirwa   kuathiri   kuathiria 
 5.  kambare mkunje angali mbichi.  mwacha mila ni   mtumwa  asiyesikia la mkuu   huvunjika guu  jaza ya hisani ni   hisani.
 6.  halifai  haifai   hakifai   hakufai 
 7.   ukandamizaji  uwajibikaji  uchangamfu  utulivu
 8.  wali wa daku  wategemea nundu  wenye pupa  sikio la kufa
 9.    :  .  ''  ;

 

Amani ni hali inayofaa___10___ na kila__11____ humu nchini mwetu. Ukosefu wa usalamahuwa na gharama kubwa___12___ katika taifa lolote lile.__13____ madhara ya ukosefu wa usalama ni kupungua kwa wawekezaji __14_____ wengi wengi wao huhofia kupoteza mali yao.
Uchumi wa nchi nao huzidi__15____.

 10   kudunishwa     kubezwa    kuenziwa  kudhalilishwa
 11  mzalendo     mlowezi    msaliti  mhafidhina
 12  lisilolipika     isiolipika    usiolipika  isiyolipika
 13  Baadhi ya     Kati ya    Mithili ya  Fauka ya
 14  ambayo     ambapo    ambavyo  ambaye
 15  kuchuchumaa     kuimarika    kunawiri  kudidimia

Kuanzia nambari 16 mpaka 30, chagua jibu lifaalo zaidi

  1. Andika usemi wa taarifa wa sentensi ifuatayo:
    "Mtawapeleka ng'ombe machungani kesho," baba alimwambia mwanawe.
    1. Baba alimwambia mwanawe kuwa watawapeleka ng'ombe machungani kesho.
    2. Baba alimwambia mwanawe kuwa angewapeleka ng'ombe machungani siku ambayo ingefuata.
    3. Baba aliwaambia wanawe kwamba wangewapeleka ng'ombe machungani siku ambayo ingefuata.
    4. Baba alimwambia mwanawe kwamba wangewapeleka ng'ombe machungani siku ambayo ingefuata.
  2. Chagua maelezo yaliyo sahihi kati ya haya.
    1. Karadha ni pesa za ziada anazopata mkopeshaji.
    2. Ujira ni malipo anayopewa mfanyakazi mwishoni mwa mwezi.
    3. Bahashishi ni zawadi anayopewa mhudumu kwa huduma njema.
    4. Ridhaa ni malipo anayopewa mtu aliyesababishiwa hasara.
  3. Zipi ni nomino za ngeli ya U-YA 22 pekee
    1. ua, upishi
    2. ugonjwa, wembe
    3. ugali, ubaya
    4. ubele, ulezi
  4. Badili katika hali ya wingi:
    Waraka ulioupokea ulitumwa kutoka kijijini.
    1. Nyaraka ulizozipokea zilitumwa kutoka vijijini.
    2. Nyaraka mlizozipokea zilitumwa kutoka vijijini.
    3. Nyaraka mliyoipokea ilitumwa kutoka vijijini.
    4. Nyaraka walizozipokea zilitumwa · kutoka vijijini.
  5. Konokono ni kwa kombe ilivyo kuku kwa
    1. kizimba
    2. Zeriba
    3. kichuguu
    4. kitala.
  6. Chagua sentensi yenye nomino ya dhahania
    1. Kuimba kuzuri kulimfanya apate tuzo
    2. Huyo anathaminiwa kwa uaminifu wake.
    3. Mazingira yakitunzwa vizuri yatapendeza.
    4. Alishambuliwa na bumba la nyuki akilima.
  7. Neno daktari lina silabi ngapi?
    1. Nne
    2. Saba
    3. Tatu
    4. Sita
  8. Tambulisha sentensi iliyoakifishwa ipasavyo.
    1. Wanafunzi wengi (wale waliofanya mtihani) wamejiunga na shule za Dupili.
    2. Wachezaji walioshiriki walitoka katika nchi mbalimbali; Uhabeshi, Misri, Uganda na Moroko.
    3. Ukifika mjini, "akaniambia,"utafute zilipo afisi za wizara ya elimu.
    4. Watu wengi, wanajua kusoma, na kuandika; humu nchini.
  9. Kutokana na kitenzi vumilia, tunapata nomino;
    1. vumiliana
    2. vumilivu
    3. vumilika
    4. uvumilivu
  10. Unganisha sentensi zifuatazo kwa usahihi:
    Bakari alitoka nje ya darasa. Bakari hakuomba idhini ya mwalimu.
    1. Bakari alitoka nje ya darasa licha ya kuomba idhini ya mwalimu.
    2. Bakari alitoka nje ya darasa fauka ya kuomba idhini ya mwalimu.
    3. Bakari alitoka nje ya darasa minghairi ya kuomba idhini ya mwalimu.
    4. Bakari alitoka nje ya darasa dhidi ya kuomba idhini ya mwalimu.
  11. Tambulisha matumizi ya kiambishi ka katika sentensi.
    Kaka alienda shambani akapalilia mahindi.
    1. kuonyesha kuendelea kwa vitendo.
    2. kuonyesha kufuatana kwa vitendo.
    3. kuonyesha kutegemeana kwa vitendo.
    4. kuonyesha kukamilika kwa vitendo.
  12. Watu wakiagana bila matumaini ya kuonana kwa muda mrefu huambiana je?
    1. Buriani
    2. Makiwa
    3. Ashakum
    4. Inshallah
  13. Chagua methali yenye maana tofauti
    1. Damu ni nzito kuliko maji.
    2. Zimwi likujualo halikuli likakumaliza.
    3. Mla nawe hafi nawe ila mzaliwa nawe.
    4. Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki.
  14. Dungu ni ushindi upatikanao katika mchezo wa mpira. Dungu aidha ni
    1. maziwa ya kwanza ya mnyama baada ya kuzaa.
    2. tunda la mkanju ambalo bado ni bichi.
    3. sehemu anamokaa rubani katika ndege.
    4. angusha chombo cha angani kwa bomu au risasi.
  15. Tegua kitendawili kifuatacho;
    Nzi hatui juu ya damu ya simba.
    1. Maji
    2. Moto
    3. Nyuki
    4. Mbu

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali kuanzia 31 mpaka 40

Enco la Mafuko lilipakana na mbuga ya wanyama ya 'T'unza. Wakazi wengi walikuwa wakulima na wafugaji. Sehemu hiyo ilijaliwa udongo wenye rutuba na mvua ya kutosha msimu baada ya msimu. Mimca ya kila aina ilinawiri na kushiba rangi ya chanikiwiti iliyokoza. Wazee kwa vijana walijawa na siha kutokana na lishe bora. Ukarimu wa wenyeji hawa ulipigiwa mfano karibu na mbali.

Chambilecho wahenga hakuna masika yasiyokuwa na mbu. Licha ya neema iliyoletwa na hali nzuri ya anga, wakazi walikabiliwa na changamoto moja. Wanyamapori walifika kijijini mara kwa mara na kuharibu mazao shambani. Ilibidi wakazi wakeshe mashambani mwao ili kuwinda ndovu, nyani, na viboko waliotoka mbugani kuja kujichumia mashambani humo. Mgogoro huo wa binadamu na wanyamapori haukusababisha uharibifu wa mali tu bali pia majeraha na mauaji ya wakazi. Ilibidi hatua mwafaka zichukuliwe ili kukabiliana na hali ile.

Alasiri moja, Bwana Chifu aliwaita wakazi katika mkutano. Mbiu ya mgambo ilipigwa nao wakazi wakaitikia kwa kauli moja mwito wa kiongozi wao. Yamkini walifahamu fika kuwa mtu hakatai mwito bali aitiwalo. Waliketi chini ya miti iliyokuwa uwanjani wakatega masikio yao ndi.

Bwana chifu alianza kwa kuwapa wananchi nafasi ya kueleza shida zao. Walitaja mambo mengi kama vile ukosefu wa maji safi, kuzagaa ovyo kwa mabiwi ya taka na uharibifu uliosababishwa na wanyamapori. Hatimaye Bwana Chifu aliwaomba wapendekeze suluhisho mwafaka kwa masaibu yao. Wengi walisimama kadamnasi na kuongea kwa ukali, "Serikali imezembea! Kwa nini tukiwaua wanyama tunatiwa mbaroni ilhali binadamu akiumia hatua za dharura hazichukuliwi? Tangu lini mnyama akawa na thamani kuliko binadamu? Lazima tulipwe fidia! Fidia!" Hapo umati ulilipuka kwa makofi.

Ni katika hali hiyo ambapo kijana mmoja aliunyosha sana mkono wake. Kwa idhini ya Bwana Chifu, akapewa nafasi ya kueleza hoja zake. "Wakazi wenzangu, ninasikitika kwa masaibu yanayotusibu. Hakika eneo letu limefikwa na changamoto chungu nzima katika siku za hivi karibuni. Hata hivyo, ashakum si matusi, dhiki zetu ni kama mwiba wa kujichoma ambao hauambiwi pole." Hapo alitua kidogo kutazama athari ya maneno kwa hadhira.

Baada ya muda aliendelea, "Hebu tujiulize, mabiwi ya taka tunayolalamikia yanatapakazwa na nani? Ukitokea utovu wa usalama, wahalifu wanatoka wapi? Tena, ni kina nani wanaovunja ua ulioizingira mbuga ili waingize mifugo, kukata kuni na kuchoma makaa kiholela? Majangili wanaowaangamiza ndovu, vifaru,chui na mbogo wanatoka wapi? Tukiweza kuyajibu maswala haya tutakuwa tumepiga hatua kubwa katika kuiondolea mbali dhiki inayotukumba". Kijana alihitimisha kauli yake hadi akatembea taratibu hadi lilipokuwa kundi la vijana wenzake. Umati ulimzindikiza kwa macho kimyakimya kisha makofi, shangwe, vifijo na nderemo zikafuatia...

Maneno ya kijana yalizua mjadala mkali miongoni mwa wakazi. Mwishowe waliafikiana kuchukua hatua zifaazo badala ya kuilalamikia tu serikali. Walielewa kuwa mambo ni kikoa. Halikadhalika, walikubaliana kuwafichua wote walioonyesha mienendo ya kutiliwa shaka miongoni mwao.

Bwana Chifu alijiunga kwa kuchangia ajenda ya siku hiyo kwa uwazi.Alihaidi kuwa ofisi yake isingelegeza kamba katika kuwachukulia hatua wote walioshiriki maovu yaliyotishia kuiangamiza jamii. Hatimaye, umati ulifumukana huku kila mmoja akijiahidi kimoyomoyo kufanya jambo lifaalo,

  1. Kulingana na aya ya kwanza,
    1. Mvua ilinyesha katika eneo la Mafuko wakati wote.
    2. Wakazi wa Mafuko walikuwa wenye bidii, ardhi yao ilikuwa na mbolea ya kutosha.
    3. Kupakana na mbuga ya wanyama kuliwaletea neema wakazi wa Mafuko.
    4. Vijana walipigiwa mfano na watu waliopakana na eneo la Mafuko.
  2. Methali hakuna masika yasiyokuwa na mbu jinsi ilivyotumika ina maana kuwa;
    1. kila inaponyesha mvua kubwa huwa kuna mbu.
    2. hakuna jambo lisilowezekana hata liwe gumu vipi.
    3. hata jambo lionekanalo baya huwa na manufaa yake.
    4. kila jambo zuri huwa na matatizo yake.
  3. Ni maafa yapi yaliyosababishwa na wanyamapori?
    1. Kuharibu mimea na kusababisha vifo.
    2. Kuwajeruhi watu na kuharibu ua wa mbuga.
    3. Kuharibu miti na kusababisha vifo.
    4. Kuwakosesha watu usingizi na kuharibu makazi.
  4. Badala ya kusema, mbiu ya mgambo ilipigwa, mwandishi pia angesema
    1. taarifa ilitumwa.
    2. watu walienda mbio.
    3. tangazo lilitolewa.
    4. mkutano uliitishwa.
  5. Si kweli kusema kuwa;
    1. matatizo yote ya wakazi yalisababishwa na wanyama.
    2. Bwana, Chifu anayajali maslahi ya wakazi wake
    3. wakazi waliendeleza uharibifu wa mazingira.
    4. baadhi ya watu waliofika mkutanoni walijawa uchungu moyoni,
  6. Wakazi wanailaumu serikali kwa.
    1. kuwalinda wanyama
    2. kutosikiliza maoni yao
    3. kuleta mbuga kwenye makazi
    4. kupuuza hasara yao.
  7. Hoja alizotoa kijana katika makala zilionyesha,
    1. upuuzaji wake
    2. ukomavu wake
    3. ujana wake
    4. ukaidi wake
  8. Kijana alianza, maelezo yake kwa kusema ashakum si matusi'; Bila shaka, kauli hii inaonyesha kuwa
    1. anaomba usikivu wa hadhira ile 
    2. anakubaliana na yaliyosemwa na watangulizi wake.
    3. anawaomba wasikilizaji wake. msamaha
    4. anapinga kauli zilizotolewa awali na wenyeji
  9. Chagua maelezo sahihi kulingana na aya ya sita
    1. wakazi walishindwa kuyajibu maswala ya kijana
    2. maafa yaliyowasibu wakazi yalichangiwa na matendo yao.
    3. serikali iliwakabili vikali waliojitafutia malisho mbugani
    4. ilichukua muda mrefu kwa umati kumwelewa kijana.
  10. Mtazamo wa mwandishi wa makala haya kwa jumla ni kuwa;
    1. shida nyingi hutokana na kutoafikiana wananchi na serikali.
    2. wanaopakana na mbuga za wanyama hupitia changamoto nyingi.
    3. wananchi wenyewe kwa kiasi kikubwa huwa na suluhisho la shida
    4. serikali huwa haina suluhisho kwa matatizo ya wananchi.

Soma kifungu hiki kisha ujibu maswali kuanzia nambari 41 mpaka 50

Je, umewahi kuwaza kuhusu umuhimu wa utunzaji wa mazingira? Pengine jibu lako kwa swali hili ni 'ndiyo'. Hata hivyo, nikikuuliza kuhusu mchango wa vijana katika kuyahifadhi mazingira utatatizika kujibu swali hili. Hii ni kwa sababu vijana, hususan watoto wa shule hudhani kwamba shughuli za uhifadhi wa mazingira zinahitajika kuendelezwa na serikali au watu wa makamo.

Ni dhahiri kwamba watoto wa shule wana nafasi bora ya kuyatunza mazingira. Wakiwa shuleni, wanaweza kujihusisha katika shughuli ndogondogo za kuyanadhifisha mazingira yao. Mathalani, wanaweza kukata nyasi, kukusanya na kuchoma taka, kufagia na kupiga deki madarasa yao. Halikadhalika, wanafunzi wanaweza kuanzisha vyama ambavyo vitaendeleza shughuli za kupambana na uharibifu wa mazingira. Hakika wapo wanafunzi ambao, kwa kuelekezwa na walimu walezi, wameanzisha vyama vya walinda mazingira. Wanafunzi hawa hutenga muda wao wa mapumziko kusafisha mazingira si shuleni mwao tu bali pia katika ujirani wa shule. Isitoshe, kwa vile wanafunzi wana ushawishi mkubwa ya hulka kwa wenzao, wanaweza kuwazindua na kuwahamasisha wengine dhidi inayopalilia uharibifu wa mazingira.

Fauka ya hayo, wanafunzi wanaweza kushiriki katika shughuli za upanzi wa miti shuleni na hata katika maeneo mengine. Hili litasaidia katika kuhifadhi misitu na vyanzo vya maji. Kupitia kwa upanzi wa miti, wanafunzi wanashiriki katika juhudi za serikali za kuchangia utoaji wa chakula kwa binadamu na wanyama. Vilevile, upandaji huu wa miti utasaidia kuyafanya mazingira kuwa ya kuvutia kwa wanafunzi na hata wanajamii wengine. Ikumbukwe pia kuwa juhudi za wanafunzi za kupanda miti zitawahakikishia wanyama kama vile tumbili makao.

Juu ya hayo, wanafunzi wanaweza kuanzisha miradi ya kuyatunza mazingira ili kuifaidi jamii. Kwa mfano, wanaweza kupanda vitalu vya miche ambayo watawauzia watu. Pia, ikiwa kuna vijito na vidimbwi shuleni mwao, vinaweza kunadhifishwa na kutumiwa kufugia wanyama wa majini kama vile samaki. Hii ni njia mufti ya jamii kujiinua kiuchumi. Wanafunzi wanaposhiriki katika shughuli hizi hujifunza stadi za kujitegemea maishani. Kadhalika, wanafunzi wawa hawa wana nafasi kubwa ya kuhifadhi wanyama wadogo wa kufuga. Wanaweza kuanzisha chama cha ufugaji wa kuku, bata na hata sungura. Litakuwa jambo la kuchangamsha kumpata kijana mdogo akionea fahari idadi kubwa va yeye na wenzake wamefuga chini ya uelekezi wa mwalimu wao haitakuwa ajabu hata wao katika maonyesho ya kimataifa ya kuwaona wanafunzi hawa wakiwapeleka kilimo!

Manaa kuu kuhusu umuhimu wa kuhifadhi mazingira huhitaji kusambazwa na kurithishwa. Nyimbo na mashairi yanayotungwa na wanafunzi ni nyenzo kuu za kutekeleza hayo. Wanafunzi wanaposhiriki katika tamasha za muziki hubuni nyimbo zinazosifu mbinu chanya za uhifadhi wa mazingira. Nyimbo hizi pia hutumiwa kukashifu wale ambao wanaendeleza uharibifu wa mazingira. Kwa mfano, zipo nyimbo ambazo huonya dhidi ya kuendeleza kilimo kinachochangia katika mmomonyoko wa udongo. Pia, katika hafla hizi, wanafunzi hutumia uigizaji kuonyesha madhara ya uwindaji haramu, uchomaji wa misitu na upandaji wa miti itakayokausha vyanzo vya maji.

Mtoto akibebwa hutazama kisogo cha nina, Nao wanajamii hawana budi kuwa kielelezo chema kwa vijana. Ikiwa watu wazima ndio vigogo wa uharibifu wa mazingira, kwa manufaa yao, juhudi za vijana zitaambulia patupu

  1. Chagua jibu sahihi kulingana na aya ya kwanza.
    1. labda msomaji amearifiwa kuhusu umuhimu wa vijana katika kuyatunza mazingira.
    2. angalabu watoto huwaachia waliokomaa shughuli za watunza mazingira.
    3. huenda msomaji ametafakari kuhusu faida za kuhifadhi mazingira.
    4. kawaida watoto hutarajia walio kwenye uongozi kuhimiza utunzaji mazingira.
  2. Kifungu kimebainisha kwamba,
    1. watoto wanawashinda watu wazima katika utunzaji wa mazingira.
    2. shule zina uwezo mkubwa zaidi wa kuonyesha utunzaji wa mazingira.
    3. madarasa yana mahali kwingi zaidi kwa kuendeleza utunzaji wa mazingira.
    4. wanafunzi wanaweza kushughulikia utunzaji wa mazingira zaidi ya watu wazima.
  3. Kulingana na aya ya pili,
    1. nasaha kutoka kwa marika huwezesha kuondoa mienendo inayochangia kutohifadhiwa kwa mazingira.
    2. uanzishaji wa vyama husaidia kutenga muda wa kunadhifisha maeneo.
    3. maelekezo ya walezi huyawezesha maeneo jirani kuwa safi.
    4. kushiriki kwa walimu kwenye mazingira huimarisha mikakati zaidi ya uzoaji taka.
  4. Chagua mifano ya kukithi miti kwa mujibu wa kifungu
    1. Kuhifadhi msisituni shuleni, kutunza kunakotokea maji
    2. Kujitosheleza kwa chakula, kuimarisha sura ya mandhari
    3. kushirikisha serikali, kutunza wanyama, kustawisha hali ya kuvutiwa kwa wanafunzi.
    4. kuwapa wanafunzi fursa kujihusisha, kuwa na makazi ya wanyama.
  5. Miradi ya kuyatunza mazingira inasaidia,
    1. kupunguza kuchafuliwa kwa vidimbwi shuleni
    2. kuwaelekeza wanafunzi kuhusu uanzishaji wa ukulima.
    3. kuimarishwa kwa akiba ya miti.
    4. kuwashirikisha wanachama katika maonyesho ya kutangazia bidhaa.
  6. Ni dhahiri kwamba shughuli za kuhifadhi mazingira,
    1. huhakikisha ongezeko la wanyama wa majini.
    2. husaidia kuzidishwa kwa shughuli za kutafuta pesa.
    3. huelekea kutoa ushauri kuhusu namna ya kuongeza idadi ya mifugo.
    4. huwapa vijana maarifa ya kuendesha maisha yao hata bila michango ya wengine.
  7. Tungo zinazobuniwa na wanafunzi,
    1. huelezea njia za kubuni mafunzo kuhusu mazingira
    2. huwahimiza wale wanaopendekeza njia nzuri za kutumia ardhi.
    3. huwaonya wale wanaopunguza idadi ya wanyama kwenye mazingira.
    4. hukosoa mitindo mibaya ya matumizi ya ardhi.
  8. Kulingana na aya ya mwisho,
    1. viongozi ndio wanaokwamiza juhudi za kusafisha maeneo.
    2. ubinafsi ndicho kichocheo kikuu cha uharibifu wa mazingira.
    3. wanajamii wanahitaji kuwaonya vijana dhidi ya kufanya mambo kujifaidi.
    4. uelekezaji unatakiwa kuhimizwa ili vijana watende kama
  9. Kisawe cha ''haitakuwa ajabu'' ni?
    1. ibra
    2. kosa.
    3. shida.
    4. nadra
  10. "Mtoto akibebwa hutazama kisogo cha nina", ina maana kuwa,
    1. tabia ya mtu huathiriwa na wanaomzunguka kwao.
    2. mwenendo wa mtu huathiriwa na wanaomshinda madaraka.
    3. hulka ya mtu huathiriwa na wanaofunzwa pamoja.
    4. desturi ya mtu huathiriwa na wanaomtegemea kihali.

INSHA

Umepewa dakika 40 kuandika insha yako. Endeleza insha ifuatayo kwa maneno yako mwenyewe huku ukiifanya iwe ya kusisimua zaidi.
Mgeni alifika mapema kama ilivyotarajiwa. Kengele ilipigwa ili....

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

  1. C
  2. A
  3. D
  4. B
  5. A
  6. C
  7. B
  8. D
  9. D
  10. C
  11. A
  12. D
  13. B
  14. B
  15. D
  16. D
  17. C
  18. D
  19. B
  20. A
  21. B
  22. C
  23. A
  24. D
  25. C
  26. B
  27. A
  28. D
  29. C
  30. B
  31. B
  32. D
  33. A
  34. C
  35. A
  36. D
  37. B
  38. C
  39. B
  40. C
  41. C
  42. B
  43. A
  44. B
  45. B
  46. D
  47. D
  48. B
  49. A
  50. B

Soma mazungumzo haya kisha ujibu swali 1 hadi 5

                                                                          EngmidtermQ2

Tumbo: Ami siku ___1____  sana sijakuona! Nimefurahi sana kukuona leo. U hali gani?
Ami Tambo: Njema Tumbo. Mpwa wangu Tumbo, nimefurahi sana kukuona. Karibu sana hapa nyumbani.
Tumbo: Pole ami naona umelifunga goti __2____ kwa bendeji. Kuna nini?
Ami Tumbo: Nilikuwa nikiteremka ___3___ uwanjani. Niliteguka ___4____ kuanguka. Palikuwa na jiwe pale nikaliangukia likagusa goti langu. Damu ilitiririka ___5___. Nilihisi uchungu.

      A    B    C    D 
 1.  mingi  kingi  nyingi  mengi
 2.  lako  yako  chako  pako
 3.  kule  pale  uko  yake
 4.  kwa  la  badala  na
 5.  kidogo  mdogo  ndogo  midogo


Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 6 hadi 9

Mjomba wangu na aila yake wanaishi karibu na msikiti. Wakati mwingi hunialika kwake, Mimi hufurahi kukutana na wakoi wangu. Wakoi wangu pia wananipenda mno. Sisi huhusiana kama ndugu wa toka nitoke. Nyumbani kwa mjomba kuna sebule, jiko, vyumba vya kulala na msala. Msalani hutumika kwenda haja ndogo na haja kubwa.

Mara yangu ya kwanza kumuona shehe ilikuwa nikiwa kwa mjomba. Shehe alikuwa anaelekea msikitini. Shehe huyo alimsalimu mjomba, "salaam aleikum!" "Aleikum salaam," mjomba alimjibu. Mwadhini alikuwa anaendelea na kutangaza kuwa wakati wa kusali ulikuwa umefika. Wengi wa waumini walioelekea msikitini walikuwa wanaume na wavulana.

Kanzu walizovaa waumini hao ziliwasitiri vyema.

  1. Mjomba na familia yake wanaishi karibu na nini?
    1. shuleni
    2. kanisani
    3. msikitini
    4. barabarani
  2. Nyumba ya mjomba ilikuwa:-
    1. kubwa
    2. ndogo
    3. mbali
    4. ya nyasi
  3. Eleza maana ya shehe
    1. Immam
    2. Kiongozi chini ya Imam
    3. Mola
    4. madrasa
      ya imam
  4. Kinyume cha neno "mjomba" ni:-
    1. Shangazi
    2. Ami
    3. Babu
    4. Nyanya

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali 10 hadi 13
                                                                                        EngmidtermQ4

Ugonjwa hatari wa Korona ni ugonjwa wa kuambukizwa ambao ni hatari. Ugonjwa huu umeleta maafa mengi na kusababisha wengi kuipungia dunia mkono wa buriani. Kuna njia mbalimbali za kujikinga kutokana na ugonjwa wa Korona. Njia mojawapo ni kuvaa maksi. Tunashauriwa kuvaa maksi safi na inavyostahili. Pia, maksi ivuliwe kwa njia inayofaa na kuanikwa. Ni bora pia kupigwa pasi inapokauka.

Mtu anaweza kujikinga dhidi ya ugonjwa wa Korona kwa kunawa mikono kwa sabuni na maji safi mara kwa mara. Sabuni huua virusi kutokana na maradhi ya Korona. Wataalamu wanahimiza watu kila uchao kukaa umbali wa mita moja na nusu au zaidi hasa wakati wa
mkurupuko wa ugonjwa huu.

  1. Ni kweli kusema kuwa:-
    1. Korona huambukizwa
    2. Korona haiui
    3. Korona huleta mema
    4. Korona si ugonjwa
  2. Ni jukumu la nani kuangamiza Korona?
    1. kila mtu
    2. madaktari
    3. walezi
    4. serikali
  3. Ukitaka kuzuia ugonjwa wa Korona si lazima:-
    1. Kuvaa maksi
    2. Kupata chanjo
    3. Kukaa mbali
    4. Kuhamia kwingine
  4. Ugonjwa wa Korona unapatikana kupitia:-
    1. maji
    2. vumbi
    3. hewa
    4. mbu

Soma kifungu kifuatacho. Kina nafasi 14 hadi 18. Umepewa majibu manne hapo.
Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.

Watoto majirani walikuwa na urafiki ___14___ dhati. Urafiki __15___uliwafanya kushiriki ___16__ mbalimbali kila walipopata nafasi.
Siku moja walimwona mtu wasiyemjua. Mtu __17___ alitabasamu alipowakaribia. Aliwaita ati awape ___18___. Werevu wao uliwaepusha kutekwa nyara. Mtu huyo hakuwa na nia njema.

               A           B            C             D 
 14.  wa  ya  cha  la
 15.  yao  wao   lao   yanu 
 16.  micheso  mchezo  michezo  machezo
 17.  huyu  hawa  yule  huyo
 18.  sawadi  peremende  zawadi  kipindi


Kutoka swali 19 hadi 30, chagua jibu sahihi kulingana na maagizo uliyopewa.

  1. Tambua neno lililopigiwa mstari.
    Kamene na zawadi walitembea haraka.
    1. kitenzi
    2. kielezi
    3. kiulizi
    4. kiwakilishi
    5. </ol start=20>
  2. Umbo hili ni:-
                                                           EngmidtermQ3
    1. Duara
    2. Kopa
    3. Mche
    4. Hiram
  3. Chagua sentensi sahihi.
    1. Vipepeo sita wamepaa.
    2. Vipepeo wasita wamepaa.
    3. Vipepeo visita vimepaa.
    4. Vipepeo sita vimepaa.
  4. Jibu la Sabalkheri ni:-
    1. masalkheri
    2. Buriani
    3. Aherii
    4. Asante
  5. "Kifaru" ni mnyama wa pori. Neno "kifaru" liko katika ngeli gani?
    1. KI - VI
    2. A - WA
    3. LI - YA
    4. U - U
  6. Andika sentensi hii kwa hali ya wingi
    Taa inawaka vizuri
    1. Taa zinawaka vizuri
    2. Mataa zinawaka vizuri.
    3. Taa yamewaka vizuri.
    4. Taa inawaka vizuri.
  7. Maana ya Istiari ''yeye ni njiwa'' ni:-
    1. Yeye ni mdogo.
    2. Yeye ni ndege.
    3. Yeye ni mpole.
    4. Yeye ni mkorofi.
  8. Nguo _____ ilianikwa baada ya kufuliwa.
    1. mzuri
    2. zuri
    3. nzuri
    4. mazuri

Chagua jibu sahihi ili kukamilisha sentensi.

  1. ______ amevali viatu vilivyopigwa rangi
    1. Kile
    2. Wale
    3. Huyu
    4. Mle
  2. Andika kinyume cha sentensi ifuatayo.
    Dobi alianika nguo alizofua.
    1. Dobi alianua nguo alizofua.
    2. Dobi alianikwa nguo alizofua.
    3. Dobi hakuanika nguo alizofua.
    4. Dobi alianua nguo
  3. Kamiilisha methali ifwatayo
    Bidii ni _____
    1. nguvu
    2. upepo
    3. jua
    4. mawingu
  4. Tumia -pi kwa ufasaha
    Chungu ______ kilinunuliwa sokoni jana?
    1. yupi
    2. kipi
    3. vipi
    4. lipi

INSHA

Andika insha murwa kuhusu;

SIKU YA KANDANDA SHULE YETU

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

  1. C
  2. D
  3. B
  4. A
  5. C
  6. C
  7. B
  8. D
  9. C
  10. C
  11. A
  12. B
  13. A
  14. B
  15. C
  16. A
  17. A
  18. C
  19. D
  20. D
  21. B
  22. A
  23. B
  24. C
  25. C
  26. D
  27. C
  28. C
  29. D
  30. B

Soma mazungumzo haya kisha ujibu maswali 1 hadi 5: 

G5SwaMT3S12023Q1

Mwalimu Mkuu: Vicky! Vicky! Uko na shida gani?
Vicky:                  Asante ana Madam Lydia. Naomba niongee na wewe kidogo kama mamangu. Mimi nateseka sana ninapoishi.                              Nimepewa majukumu mengi sana nyumbani.
Mwalimu Mkuu: Pole sana. Wacha kulia ndio uniambie ukweli.
Vicky:                  Kazi nyingi ya jikoni, kufua na kupika. Kama jana nililala saa tano na nusu na sina hata saa ya kufanya kazi ya                              ziada. Kichapo na matusi nimezoea siku hizi. Shida kubwa tena, walimu pia kila asubuhi wanangoja kazi zao                                za ziada na sijafanya. Nakuomba unisaidie mwalimu. Nimeshindwa. Sijui kwa nini wazazi wangu waliniacha!                                  Kifo haina huruma!
Mwalimu Mkuu: Hayo yote ni ya Mungu. Nitakusaidia Vicky. Usiwe na wasiwasi. Nitamwita mlezi wako tukae chini tukomeshe                                ili jambo. Haifai kukufanyia mambo haya mabaya.
Vicky:                  Asante sana mwalimu. Ninamatumaini kama ya tai kuwa kila kitu kitakuwa vizuri. “Mola" akubariki sana.
Mwalimu Mkuu: Kuja hapa kwa ofisi uchukue barua umpeleke mlezi wako ukifika wakati wa kurudi nyumbani.

  1. Ni kwa nini Vicky alimtembelea Mwalimu Mkuu?
    1. Alikuwa mgonjwa
    2. Hakujua la kufanya
    3. Alitaka kumsalimia
    4. Alitaka kuripoti jambo fulani
  2. Neno "Mola" inamaana gani?
    1. Yatima
    2. Kazi ngumu
    3. Mateso
    4. Mungu
  3. Wazazi wa Vicky walikuwa wapi?
    1. Walikuwa nyumbani
    2. Walienda ng'ambo
    3. Hatujaambiwa
    4. Walifariki
  4. Vicky alikutana na Mwalimu Mkuu wapi?
    1. Darasani
    2. Njiani
    3. Ofisini
    4. Nyumbani
  5. Vicky angesaidiwa vipi na Mwalimu Mkuu?
    1. Kumwonya wazazi wake
    2. Kumwita mwalimu wake wa kanisa
    3. Kumwongelesha mlezi wake
    4. Kumripoti mlezi wake kwa polisi

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali la 6 hadi 9.

G5SwaMT3S12023Q2

Tura ni mkulima. Yeye ni mkulima shupavu sana. Ana shamba kubwa sana karibu na mto. Amepanda mimea na matunda ya aina tofautitofauti. Katika shamba lake, amepanda matunda kama vile mnazi, mbuni, mzabibu, mlimau, mparachichi na hata mpapai.

Bwana Tura pia hupanda mimea kama vile mhindi, mharagwe, mtama na hata mboga mbali mbali. Yeye hutumia maji kutoka mtoni kunyunyizia mimea na matunda. Ana mashini ya kunyunyizia maji. Yeye huuza mazao kutoka shamba lake na kupata fedha ya kuikimu familia yake.

  1. Kazi nyingi ya Tura inapatikana wapi? 
    1. sokoni
    2. shambani
    3. nyumbani
    4. mtoni
  2. Neno "fedha" iko na maana gani?
    1. pesa
    2. mazao
    3. hodari
    4. mvua
  3. Ni mimea gani haipatikani kwenye shamba la Tura?
    1. Mharagwe
    2. Mparachichi
    3. Mtama
    4. Pilipili hoho
  4. Mzabibu inatumika kutengeneza nini?
    1. chai tamu
    2. pombe
    3. mkate
    4. keki

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali 10 hadi 13

Saumu alikuwa msichana mrembo na mwerevu shuleni. Ndoto yake ilikuwa ni kusafiri nchi za ulaya. Siku moja wakati wa likizo, alikutana na kijana mmoja mwekezaji aliyekuwa tajiri. Alivutiwa sana na habari kuwa kijana huyo alipenda kusafiri nchi za ng'ambo katika biashara zake. Saumu alishawishika kuingia katika ndoa ya mapema ili kutimiza ndoto zake.

Jambo ambalo hakujua ni kuwa yote yang'aayo si dhahabu. "Msichana mwerevu kama wewe unatakiwa kuishi maisha ya starehe." Mapunda alimshawishi Saumu. "Unaweza kutengeneza pesa nyingi kwa muda mfupi."

Jumatatu moja wakati wa alasiri, Mapunda alifika kwa akina Saumu akiwa na tikiti ya kusafiri pamoja na pasipoti. Saumu alifurahi sana. Mapunda alijieleza kwa ufasaha kiasi cha mtu yeyote kushuku njama yake. Wazazi walilazimisha Saumu kufunga ndoa.

Saumu alivalia nguo kitalii. Rinda maridadi na kofia kubwa kichwani pake. Mrembo wa mtu alishuka ndege katika uwanja wa Uingereza. Upepo ulipeperusha rinda lake maridadi. Ilibidi watu washike marinda yao kujiepusha aibu. Hilo halikumgusa Saumu. Alishikilia kofia yake na kuacha upepo kupeperusha rinda lake kiasi cha kuonyesha uchini wake. Askari katika uwanja huo wa ndege walishangazwa na kitendo cha Saumu kushikilia kofia yake. Baada ya ukaguzi kwenye kofia yake ya thamani ya juu, mihadarati aina ya heroini ya thamani ya shilingi milioni tatu ilipatikana. Baada ya mabishano mafupi, Saumu alitiwa mbaroni na baadaye akapokezwa kufungo cha miaka kumi na miwili kwa ulanguzi wa dawa za kulevya.

Ndoa yake ya mapema haikumfaa kwa lolote wala chochote.

  1. Saumu alikuwa na ndoto gani?
    1. kupanda ndege
    2. Kuvaa kofia
    3. Kusafiri nchi za ng'ambo
    4. Kuuza dawa za kulevya
  2. Rinda huvaliwa na ________________________________
    1. Mwanaume
    2. Askari wa ndege
    3. Msichana
    4. Kasisi
  3. Kwa nini watu walishikilia marinda yao katika uwanja wa ndege?
    1. Ilikuwa baridi sana
    2. Askari alikuwa karibu
    3. Kulikuwa na upepo kali
    4. Walivaa nguo safi
  4. Dawa gani ilipatikana kwenye kofia ya Saumu?
    1. Heroini
    2. Bhangi
    3. Pombe
    4. Mandasi

Soma kifungu kifuatacho. Kina nafasi 14 had 18. Umepewa majibu manne hapo. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.

Siku moja, sungura na fisi ___14___ kuhudhuria harusi ya mwana wa simba. Marafiki ___15___ wawili walijipamba kwa ajili ya starehe.

Walijirashia __16___ na manukato ya kupendeza. Walionekana warembo sana. Mkononi sungura alibeba ___17___ uliokuwa na ___18___ kama vile mafuta ya kupakia, sukari na maziwa ya kupikia chai.

   A  B   C   D 
 14.  yalikuwa  mlikuwa   walikuwa  tulikuwa
 15.  hao  wao  huo  lao
 16.  marasi  marashi  malashi  marazi
 17.  mkopa  mukoba  mikopa  mkoba
 18.  zawadi  malipo  sawadi  mazuri

 

Kutoka swali 19 hadi 30, chagua jibu sahihi kulingana na maagizo uliyopewa

  1. Tegua kitendawili hiki: Mtoto umleavyo ndivyo
    1. akuavyo
    2. mpende
    3. njema
    4. ni mkorofi
  2. Umbo hili huitwa ______________________________
    Oval 2
    1. Duara
    2. Mraba
    3. Yai
    4. Duara dufu
  3. Tambua neno lililopigiwa mstari:
    Viti vizuri vimetengenezwa.
    1. Kielezi
    2. Kitenzi
    3. Kivumishi
    4. Kiwakilishi
  4. Je, neno "mwavuli" iko katika ngeli gani?
    1. U-YA
    2. LI-YA
    3. A - WA
    4. U - I
  5. Ni ndege yupi asiyekuwa wa porini?
    1. Mwewe
    2. Chiriku
    3. Bata
    4. Kanga
  6. Andika kwa wingi:
    Kitabu changu kimeraruka.
    1. Vitabu vyangu vimeraruka. 
    2. Vitabu vyetu vimeraruka.
    3. Vitabu vyao vimeraruka.
    4. Vitabu vyenu vimeraruka.
  7. Ni msamiati upi unapatikana hospitalini?
    1. Maabara, makaa
    2. Seredani, bendeji
    3. Machela, bendeji
    4. Meko, godoro
  8. Sabalkheri ni salamu za wakati gani?
    1. Asubuhi
    2. Jioni
    3. Usiku
    4. Mchana
  9. Kikombe kiko ____________________________________ya meza.
    G2EngMT3S12023Q6
    1. juu
    2. kando
    3. chini
    4. ndani
  10. Mtoto wa kuku huitwa? _________________________________
    1. kifaranga
    2. ndama
    3. mayai
    4. kiluilui
  11. Jaza pengo kwa neno mwafaka:
    Chakula ______________________________ hupendwa na watoto wadogo.
    1. tamu
    2. kitamu
    3. nzuri
    4. mtamu
  12. Kanusha sentensi hii: Nitatumia tarakilishi yangu.
    1. Sitatumia tarakilishi yangu.
    2. Sikukutumia tarakilishi yangu
    3. Situmii tarakilishi yangu.
    4. Nitatumia tarakilishi yangu.

INSHA

Andika insha ya kusisimua kuhusu;

UMUHIMU WA MAJI

MARKING SCHEME

  1. D
  2. D
  3. D
  4. C
  5. C
  6. B
  7. A
  8. D
  9. B
  10. C
  11. C
  12. C
  13. A
  14. C
  15. A
  16. B
  17. D
  18. A
  19. A
  20. D
  21. C
  22. B
  23. C
  24. B
  25. C
  26. A
  27. A
  28. B
  29. A

Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali 1 hadi 5

G4SwaMT3S12023Q1

Becky: ___1___ Tenzy.
Tenzy: Sijambo Becky.
Becky: Habari ___2___kwenu? Na wazazi wako? Mimi niko salama kwa neema ya mungu. Na unaelekea wapi?
Tenzy: Nimetumwa sokoni na nyanya kumnunulia ___3___vya jioni.
Becky: Mbona leo unaenda sokoni peke yako? Wakina Njeri na Pembo hawako? Je kwa familia yenu mko watoto ___4___
Tenzy: Ukianza hadithi ya watoto utaendelea kusoma kweli. Hizo ni maswali za upuzi na ujinga. Ongea na mimi mambo ya masomo ama swali inahusu watoto kama mimi na ___5___
Becky: Pole sana Tenzy kama nimekukosea!

   A  B  C  D
 1.  Shikamoo  Hujambo   Alamsiki   Hatujambo 
 2.  Za  ya  la   cha 
 3.  Vyakula  viakula   Sokoni   Pesa 
 4.  Mingapi  ngapi   vingapi  Wangapi 
 5.  sisi  nyote  wewe  nami


Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 6 hadi 13

Hapo zamani za kale paliondokea marafiki wawili walipendana kama chanda na pete. Hawa wanyama walikua pundamilia na fisi. Walipendana na kufanya kazi zao zote pamoja. Wanyama hawa walifanana kwa rangi. Walikuwa na mchanganyiko wa nyeusi kwenye nyeupe.

Siku moja pundamilia alienda kutafutia watoto wake Vyakula akawacha watoto wake wawili wakilala.Kurudi pundamilia hakupata mtoto wake mmoja. Kuuliza, fisi,akajibu, alimwona akikimbia kuelekea mtoni. Ni kama alienda kuchota maji na atarudi tu.Fisi aliendelea tu kulala,kwenye "kitanda"chake.

Pundamilia alingoja mpaka jioni bila kuona mtoto wake.

  1. Pundamilia na fisi walikua
    1. Maadui
    2. Marafiki
    3. Majirani
    4. Wazazi
  2. Mtoto wa pundamilia alienda wapi?
    1. mtoni
    2. kucheza
    3. alikulwa na fisi
    4. alibebwa na maji
  3. Wingi wa neno “kitanda” ni
    1. kitanda
    2. vitanda
    3. Makitanda
    4. vitandani
  4. Pundamilia hula ___________________________
    1. Nyasi
    2. nyama
    3. wadudu
    4. Wanyama wengine
  5. Katikati ya wanyama hawa yupi alikuwa na watoto?
    1. pundamilia
    2. Fisi
    3. Farasi
    4. punda
  6. Rangi ya pundamilia ni
    1. nyekundu
    2. nyeusi
    3. samawati
    4. kijani
  7. Ni kweli kusema
    1. Fisi hukula nyama
    2. Fisi ni kubwa kama pundamilia
    3. Pundamilia anafanana na tembo kwa rang
    4. Pundamilia anataga mayai kubwa
  8. Kwa nini Pundamilia aliwacha watoto wake peke yao?
    1. Kutembea kiasi
    2. Kuinda wanyama wengine
    3. Kutafuta Vyakula
    4. Kuchota maji mtoni

Jaza pengo kutoka swali 14 hadi 18

Mwikali na Kanini ___14___. Magharibi ya mji  ___15___ Kangundo. Wao ___16___ shule ya Msingi ya Mkengesia. Shule hiyo huwa ___17___ na kwao na huwabidi watumie pikipiki ili kufika shuleni. Wao huchukua ___18___ wa saa moja kufika huko.

   A  B   C   D 
 14.  wanaishi  waliishi   walikaa   huketi 
 15.  wa  za  ya  la
 16.  husoma  husomwa  husomea   husomewa 
 17.  bali  mbali   karibu   kuliko 
 18.  mda  wakati   dakika   muda 

 

Kutoka swali 19 hadi 30, chagua jibu sahihi kulingana na maagizo uliyopewa.

  1. Neno "mwanafunzi” iko katika ngeli gani?
    1. LI - YA
    2. A - WA
    3. KI - VI
    4. U-I

Tambua neno lililopigiwa mstari

  1. Darasa letu ni safi kuliko lenu.
    1. Nomino
    2. kitenzi
    3. Kielezi
    4. Kivumishi
  2. Kinyume cha neno "simama" ni
    1. Inama
    2. Anguka
    3. Keti
    4. lala
  3. Nguo hili huvaliwa na ________________________
    G1ILAMT3S12023Q10
    1. Wasichana
    2. Babu
    3. Wavulana
    4. Mapacha
  4. Andika kwa wingi
    Kichwa changu kina nywele.
    1. Vichwa vyangu vina nywele
    2. Kichwa changu kina nywele
    3. Vichwa vyetu vina manywele
    4. Vichwa vyetu vina nywele
  5. Umbo hili ni _____________________________________
    Oval 2
    1. Duara dufu
    2. Mraba
    3. Duara mche
    4. Duara
  6. Robo tatu kwa nambari ni _____________________________
    1. 4/3
    2. 2/4
    3. 3/4
    4. 3/3
  7. Paka yuko ____________________________ meza.
    G4SwaMT3S12023Q26
    1. kando ya
    2. juu ya
    3. ndani ya
    4. chini ya

Kanusha sentensi hii

  1. Kazungu alioga jana
    1. Kazungu alioga juzi
    2. Kazungu alioga juzi
    3. Kazungu hajaoga jana
    4. Kazungu hajaoga jana

Kamilisha methali

  1. Mtoto wa ___________________________ ni nyoka
    1. kiluilui
    2. mayai
    3. nyoka
    4. sumu
  2. ____________________________ hutumia dira
    1. Mseremala
    2. Mwalimu
    3. Rubani
    4. Mkulima
  3. Mwala ni mfupi kama
    1. meza
    2. ndovu
    3. mlingoti
    4. nyundo

MARKING SCHEME

  1. B
  2. A
  3. A
  4. D
  5. C
  6. B
  7. C
  8. B
  9. A
  10. A
  11. B
  12. A
  13. C
  14. A
  15. C
  16. A
  17. B
  18. D
  19. B
  20. C
  21. C
  22. A
  23. D
  24. A
  25. C
  26. D
  27. Kazungu hakuoga jana
  28. C
  29. C
  30. D

Soma kifungu kifatacho kisha ujibu maswali yanayofuata.

G6SwaT3OS12023Q1

Je, ni mambo gani ambayo yanafaa kufanywa na jamii yenu? Dini yenu hufundisha mambo gani ambayo lazima yazingatiwe? Kuna itikadi mbalimbali katika jamii yetu. Kuna itikadi ambazo ni za kidini na zingine za kijamii. Baadhi ya itikadi ni muhimu katika maisha yetu ya kila siku. Itikadi kama hizo ni zile ambazo zinakuza heshima na ushirikiano kati yetu.

Kuna jamii ambazo zinasisitiza hali ya heshima ya mmoja kwa mwingine. Nidhamu katika jamii kama hizo huimarishwa na kila mwanajamii. Vilevile, kunazo imani za kidini ambazo husisitiza maadili kati ya wanajamii wote. Maadili ni tabia nzuri za binadamu. Tabia zisizopendeza na maovu hupingwa katika mafundisho ya kidini.

Hata hivyo, kuna itikadi za kijamii ambazo hazifai hata kidogo. Si vizuri kuwa na dhana kuwa watoto wa jinsia fulani ni bora au muhimu kuliko jinsia nyingine. Watoto wote ni muhimu, wawe wavulana au wasichana. Mtoto ni baraka kutoka kwa Mungu. Mtoto ni zawadi ambayo Mungu hupeana kwa familia. Si vizuri kupewa zawadi na kisha kuidharau. Kuna watu mbalimbali ambao wametekeleza mambo mengi makubwa bila kujali jinsia yao. Kila mtu ana uwezo wake, hakuna jinsia ambayo ni dhaifu.

Isitoshe, si vyema kumlazimisha mtu kuoa ama kuolewa na mtu fulani. Aidha, ndoa za mapema hazifai hata kidogo. Je, ni itikadi gani za kidini na kijamii unazozijua ambazo hazifai?

  1. Ni kweli kuwa mafundisho ya kidini;
    1. hupingwa katika kila jamii.
    2. yanapinga tabia zote katika jamii.
    3. yanashauri kuwa tuwe na tabia nzuri.
    4. husisitiza umuhimu wa maovu maishani.
  2. Ipi si tabia ambayo huweza kufundishwa na dini kulingana na kifungu?
    1. uzalendo
    2. ushirikiano
    3. ukatili
    4. uvumilivu
  3. Zifuatazo ni itikadi zisizofaa isipokuwa;
    1. ndoa za mapema
    2. kuhesimu makabila mengine
    3. kudharau watoto wa jinsia fulani
    4. ndoa za lazima
  4. Mwandishi wa kifungu hiki anatoa ushauri gani?
    1. Hakuna mtoto ambaye ni bora kuliko mwingine.
    2. Watoto wa kike ni bora kuliko wa kiume. 
    3. Hakuna mtoto ambaye ni muhimu katika jamii.
    4. Mtoto anafaa kuwa baraka kwa Mungu.
  5. Kulingana na kifungu hiki, ni kweli kuwa;
    1. Tunafaa kufuata itikadi zote kati jamii.
    2. Itikadi zote za kiafrika hazifai.
    3. Tunafaa kufuata itikadi za wazungu pekee.
    4. Kuna itikadi zinazofaa na zile zisizofaa.

Soma mazungumzo yafuatayo halafu ujibu maswali yanayofuata.

G6SwaT3OS12023Q2
(Katika hospitali ya Tiba, Bi. Siha anaingia akiwa na mtoto wake.)

DAKTARI: Karibu sana mama. Masalkheri?
MAMA:      (Anaketi.) Akheri.
DAKTARI: Je, nikusaidie vipi?
MAMA:      Daktari, mtoto wangu hajalala usiku wote. Anaendesha sana. Lazima ana malaria.
DAKTARI: Pole mama. Hata hivyo huwezi ukajua ugonjwa wa mtoto bila kumpima.
                   (Anasimama na kumchunguza kwa kutumia steshoskopu.) Mpigo wake wa moyo u sawa.
MAMA:      Aha! Mungu ni mwema.
DAKTARI: Hebu uinue mkono huu ili nimwekee kipimajoto. (Anamwekea kipimajoto kwapani.)
                  tutaweza kubaini tatizo lake. Lazima sote tuchange bia ili kuhakikisha kuwa afya Naona ana homa.                    Hebu mpeleke maabarani. Akifanyiwa uchunguzi wa damu, yake inaimarika. 
MAMA:      Asante kwa ushauri wako. Hebu nimpeleke katika maabara kisha nikuletee matokeo. (Anaondoka.)

  1. Yawezekana kuwa mazungumzo haya yalifanyika wakati gani?
    1. alfajiri
    2. adhuhuri
    3. magharibi
    4. macheo
  2. Kwa nini daktari alimshauri mama aende katika maabara?
    1. Ili apewe dawa
    2. Afanyiwe uchunguzi wa damu
    3. Aeleze kuwa mtoto alikuwa na homa 
    4. Ili mtoto adungwe sindano
  3. Daktari aligundua kuwa mtoto alikuwa na tatizo gani?
    1. Moyo ulikuwa ukipiga haraka
    2. Joto la mwili lilikuwa la juu
    3. Alikuwa akiendesha sana
    4. Hakuwa amelala usiku wote
  4. Kulingana na mazungumzo, haiwezekani; 
    1. kujua tatizo la mtoto kabla ya kupimwa.
    2. kumtibu mtoto anayeendesha sana. 
    3. kujua ugonjwa wa mtoto baada ya kupimwa.
    4. kujua tatizo la mtoto kabla ya kumpa dawa.
  5. Nahau 'tuchange bia' ina maana gani jinsi ilivyotumika katika mazungumzo haya?
    1. tuwe makini
    2. tufuate ushauri
    3. tufanye matibabu 
    4. tushirikiane

Soma makala yanayofuata halafu ujibu maswali yafuatayo.

G6SwaT3OS12023Q3

Juma mapesa alikuwa dereva aliyejulikana sana kwenye barabara ya kutoka Nairobi hadi Kakamega. Alipenda sana kuendesha gari kwa kasi iliyopita kiwango. Ingawa alionywa na wazazi wake pamoja na maafisa wa polisi, hakujali. Kila alipopita maafisa wa trafiki, angeendesha gari hilo kwa kasi kama umeme. Ajabu ni kuwa abiria wengine walipenda sana gari hilo. Walisikika wakisema kuwa hiyo ilikuwa njia rahisi ya kufika mapema. Haja kubwa ya Mapesa kuendesha gari haraka ilikuwa tamaa ya kutaka kufanya safari nyingi mno. Alitaka kupata kiasi kikubwa cha pesa kufikia mwisho wa siku.

Siku moja, saa kumi na mbili kasorobo, gari hilo la abiria kumi na wanne lilikuwa tayari kuanza safari. Baada ya wanawake saba kuingia ndani, wanaume waliongezeka hadi likajaa. Mapesa alishika usukani kisha wakang'oa nanga. Kama kawaida, gari lilipepea kama upepo barabarani huku abiria wengi wakifurahia ngoma. Mara Mapesa alifika mahali ambapo barabara ilipinda. Alijaribu kulielekeza gari kwa njia inayofaa lakini hakufua dafu. Sauti iliyosikika ilikuwa ya 'krrrrr', kisha 'ku'. Hapo ndipo mapesa alipovunjikia miguu yote miwili. Sasa yeye hutumia kitimaguru kutoka mahali pamoja hadi pengine.

  1. Mapesa alikuwa na tabia inayoweza kulinganishwa na ya kiumbe gani?
    1. simba
    2. fisi
    3. kunguru
    4. chiriku
  2. Maneno 'kwa kasi kama umeme' ni mfano wa fani gani ya lugha?
    1. nahau
    2. istiara
    3. methali
    4. tashbihi
  3. Safari inayozungumziwa ilianza saa ngapi?
    1. 5:45
    2. 12:15
    3. 6:15
    4. 11:45
  4. Methali gani isiyoweza kutumika kurejelea ujumbe katika kisa hiki?
    1. Haraka haraka haina baraka.
    2. Asiyesikia la mkuu huvunjika guu.
    3. Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.
    4. Tamaa mbele mauti nyuma. KISWAHILI: LUGHA
  5. Chagua mpangilio unaofaa wa matukio katika makala haya.
    1. kuanza safari, kuvunjika mguu, gari kujaa
    2. ajali kutokea, kuvunjika miguu, kutumia kitimaguru
    3. gari kujaa, kutumia kitimaguru, kuvunjika miguu
    4. ajali kutokea, kuvunjika miguu, kuanza safari

Chagua jibu linalofaa kati ya majibu uliyopewa ili kujazia nafasi zilizoachwa.

Ukosefu wa mvua ___16___ ukame mkubwa nchini. Wakazi ___17___taifa letu wamekuwa ___18___ sana kutokana na ukosefu wa chakula, maji safi na mahitaji mengine. ___19___ kubadilisha hali ya mambo, ni vyema tupande miti na kuitunza ili iwe mikubwa. Miti yote ___20___ na kuwa mikubwa, huweza kuvutia mvua na kubadilisha hali ya mambo.

   A   B   C   D 
 16.   imesababishwa  umesababishwa   imesababisha   umesababisha 
 17.  katikati  kwa   katika   ndani mwa 
 18.  wameteseka  wanateseka   wakiteseka  watateseka
 19.  Ili  Ila  Lakini  Wala
 20.  yakitunzwa  ikitunzwa  ukitunzwa  zikitunzwa

 

Jibu maswali yafuatayo kulingana na maagizo.

  1. Chagua ukubwa wa sentensi ifuatayo.
    Ndovu alisimama karibu na nyumba ya mzee huyo.
    1. Jidovu lilisimama karibu na jinyumba la zee hilo.
    2. Kidovu kilisimama karibu na kijumba cha kizee hicho.
    3. Dovu lilisimama karibu na jumba la jizee hilo.
    4. Dovu lilisimama karibu na jumba la zee hilo.
  2. Kama jana ilikuwa Ijumaa, mtondo itakuwa lini?
    1. Jumapili
    2. Jumatatu
    3. Jumanne
    4. Jumatano
  3. Onyesha ukanusho wa;
    Wewe ulikuja nyumbani.
    1. Wewe hukuja nyumbani.
    2. Wewe haukukuja nyumbani.
    3. Wewe hukukuja nyumbani.
    4. Wewe huakuja nyumbani.
  4. Tambua aina za maneno yaliyopigiwa mistari.
    Wawili walienda nyumbani kwao mapema.
    1. kiwakilishi, kielezi, kielezi
    2. kivumishi, kielezi, kielezi
    3. kiwakilishi, nomino, kielezi
    4. kiwakilishi, kielezi, nomino
  5. Sentensi gani iliyo katika hali timilifu?
    1. Juma husoma kwa bidii.
    2. Rehema amefua nguo zake zote.
    3. Zahra alipanda miti mingi.
    4. Ninapenda kula mboga na matunda.
  6. Nomino gani isiyopatikana katika ngeli moja na zingine?
    1. mafuta
    2. manukato
    3. mazingira
    4. mabua
  7. Yaf uatayo ni matumizi ya koloni isipokuwa;
    1. kutanguliza orodha
    2. kuunganisha sentensi mbili
    3. kutenga saa na dakika
    4. kutenga maneno katika orodha
  8. Onyesha sentensi iliyotumia kiwakilishi kiulizi.
    1. Mwanafunzi gani aliye na kalamu? 
    2. Chakula hicho kitapewa yupi?
    3. Nyumba mpya ni ya akina nani?
    4. Wote wameenda wapi?
  9. Chagua nomino iliyonyambuliwa katika kauli ya kutendua.
    1. fua
    2. angua
    3. tambua
    4. anua
  10. Maagano gani ambayo hutumika wakati wa jioni?
    1. kwaheri
    2. buriani
    3. alamsiki
    4. siku njema

INSHA

Mwandikie mwalimu wako barua ukimweleza kwa nini hukuja shuleni juma lililopita.

MARKING SCHEME

  1. C
  2. C
  3. B
  4. A
  5. D
  6. C
  7. B
  8. B
  9. A
  10. D
  11. B
  12. D
  13. A
  14. C
  15. B
  16. D
  17. C
  18. C
  19. A
  20. B
  21. D
  22. C
  23. A
  24. A
  25. B
  26. D
  27. B
  28. B
  29. D
  30. C

Soma mazungumzo haya kisha ujibu maswali 1 hadi 5.

G4SwaT3OS12023Q1

Halima: Hamjambo wanangu?
Wendy na Lucy: ___1___ mama u hali gani?
Halima: Wendy nenda utayarishe meza ili tuandae kiamsha ___2___.
Wendy: Aya mama.
Halima: Lucy peleka chungu ___3___ kwa moto.
Lucy: Mama chungu kizito, sikiwezi.
Halima: Najua wewe ni ___4___ basi nenda ukasaidie dada ___5___ kuandaa meza.
Lucy: Sawa mama.

   A   B   C   D 
 1.   Sijambo   Hujambo   Hatujambo   Jambo 
 2.  Kimya  Kinywa   Kinyua   Kunywa 
 3.   hiki  hii    hili   huu 
 4.   msembe   mzebe   mzembe   mizembe 
 5.  lako  wako  zako  yako


Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 6 hadi 9.

Kazungu ana tabia ya wizi. Siku moja alikata kauli kwenda katika sherehe za kuanzia mwaka. Aliandamana na watoto wenzake waliomcheka kwa sababu hakuwa na hata shilingi moja mfukoni ya matumizi madogo. Kazungu alikasirika sana. Alisukumana nao na kuwatisha wampe pesa walizo nazo.

Watoto hao waliogopa na kuanza kukimbia ovyo. Kazungu alifanikiwa kuiba pesa za sarafu pekee. Watoto hao walienda moja kwa moja hadi kituo cha polisi. Walimshtaki Kazungu. Uchunguzi ulipofanyika na ukweli wote kupatikana na Kazungu aliadhibiwa.

  1. Jina jingine la pesa ni:-
    1. hela
    2. karibu
    3. kituo cha polisi
    4. aibu
  2. Ni kweli kusema:-
    1. Kazungu ni mtoto mzuri.
    2. Kazungu alizembea.
    3. Kazungu alikuwa na hela zake.
    4. Kazungu aliiba pesa za watoto wenzake.
  3. Kazungu aliiba pesa gani?
    1. Pesa za sarafu.
    2. Pesa za nauli.
    3. Pesa za karo.
    4. Pesa za noti.
  4. Nani aliyeadhibu Kazungu?
    1. watoto wenzake
    2. kituo cha polisi
    3. afisa wa polisi
    4. mwalimu mkuu

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 10 - 13.

Ni muhimu sana mzazi kutunza mtoto wake. Malezi ya wazazi si kama ya mtu yeyote yule. Si haki kumnyima mtoto nafasi ya kupata malezi bora. Ni jukumu la mzazi kumpa mtoto chakula, makaazi, matibabu yaliyo bora na elimu.

Pia inapaswa mtoto apate mavazi safi. Inasikitisha kuona wazazi wengine wakiwatoa watoto wao shule. Pengine watoto hao huamriwa kufanya kazi kwa majumba au mashamba ya watu.

Tuwape watoto wetu mapenzi na tukatae malezi duni. Malezi duni hufanya watoto kwenda kuzurura mtaani. Tujitahidi kutunza watoto wetu inavyotakikana.

  1. Ni kazi gani ambazo hufanywa shambani? 
    1. kupalilia
    2. kusoma
    3. kushika nyoka
    4. kuwinda
  2. Tusipo watunza watoto, nini kitatokea?
    1. viakula
    2. machakula
    3. vyakula
    4. vyaakula
  3. Tusipo watunza watoto, nini kitatokea?
    1. watoto watakuwa werevu.
    2. watakuwa matajiri
    3. watalipwa pesa zao.
    4. watoto wataanza kuzurura mtaani.
  4. Gani si mambo muhimu mzazi anatakiwa ayatekeleza kwa mtoto wake?
    1. kuajiri mtoto
    2. kuelimisha mtoto
    3. kupatia mtoto chakula
    4. kununulia mtoto vazi.

Tumia maneno haya kwa kujaza mapengo 14 hadi 18.

Nyumba ni makazi ___14___ wanadamu. Vitu ___15___ hupatikana katika nyumba. Sebuleni kuna viti na ___16___ pia kuna rafu ya kuweka vitabu. Jiko huwa na mboga mbalimbali kama ___17___ nyanya, vitunguu, limau na ___18___.

   A   B   C   D 
 14.   cha   ya   la   mwa 
 15.  kingi   nyingi   kwingi   vingi 
 16.  sofa  randa   kitanda   jiko 
 17.  kile  lile   vile   mle 
 18.  viasi  vyazi   viazi   viaazi 

 

Kutoka swali 19 hadi 30, jibu kulingana na maagizo.

  1. Majina kama mayai, maembe, malori yako katika umbo gani?
    1. Pembe tatu
    2. Mraba
    3. Mstatili
    4. Duara
  2. Ni vazi lipi kati ya haya huvaliwa na mwanaume?
    1. kanchiri
    2. kaptura
    3. rinda
    4. kitambaa
  3. Tegua kitendawili hiki.
    Nifungue nikufunike, _____________________________________
    1. mwavuli
    2. nyumba
    3. viatu
    4. nguo
  4. Kamilisha sentensi.
    Kikombe ___________________________ kiko jikoni.
    1. cherefu
    2. virefu
    3. mrefu
    4. kirefu
  5. Kitambaa cha kusafisha sakafu kwa maji na sabuni huitwa _________________________________.
    1. nguo
    2. pazia
    3. dodoki
    4. hankachifu
  6. Chagua kitenzi ilichonyambuliwa katika kauli ya kutendwa.
    1. ruka
    2. uliwa
    3. oshwa
    4. mshororo
  7. Mstari moja katika shairi huitwa?
    1. beti
    2. tarbia
    3. sentensi
    4. mshororo
  8. Udogo wa neno “mtu" ni _________________________________
    1. kitu
    2. jijitu
    3. kijitu
    4. jitu
  9. Andika kwa wingi.
    Giza limetanda angani.
    1. Angani kuna giza mingi.
    2. kiko jikoni.
    3. Giza mingi zimetanda angani.
    4. Giza zimetanda angani.
  10. Tunasema nzito kama _________________________________
    1. vitabu
    2. meza
    3. nanga
    4. pamba
  11. Sehemu ya dira R ni:-
    G4SwaT3OS12023Q29
    1. Kusini
    2. Magharibi
    3. Mashariki 
    4. Kaskazini mashariki
  12. Vazi hii huitwaje?
    G4SwaT3OS12023Q30
    1. Suruali
    2. Rinda
    3. Kaptura
    4. Chupi

INSHA

Andika insha murwa kuhusu.

UMUHIMU WA MAJI:

MARKING SCHEME

  1. C
  2. B
  3. A
  4. C
  5. D
  6. A
  7. D
  8. A
  9. C
  10. A
  11. C
  12. D
  13. A
  14. B
  15. D
  16. A
  17. C
  18. C
  19. D
  20. B
  21. D
  22. D
  23. C
  24. B
  25. B
  26. C
  27. D
  28. B
  29. C
  30. D
Page 1 of 14