Monday, 04 September 2023 07:52

Kiswahili Questions and Answers - Grade 6 Opener Exams Term 3 2023 Set 1

Share via Whatsapp

Soma kifungu kifatacho kisha ujibu maswali yanayofuata.

G6SwaT3OS12023Q1

Je, ni mambo gani ambayo yanafaa kufanywa na jamii yenu? Dini yenu hufundisha mambo gani ambayo lazima yazingatiwe? Kuna itikadi mbalimbali katika jamii yetu. Kuna itikadi ambazo ni za kidini na zingine za kijamii. Baadhi ya itikadi ni muhimu katika maisha yetu ya kila siku. Itikadi kama hizo ni zile ambazo zinakuza heshima na ushirikiano kati yetu.

Kuna jamii ambazo zinasisitiza hali ya heshima ya mmoja kwa mwingine. Nidhamu katika jamii kama hizo huimarishwa na kila mwanajamii. Vilevile, kunazo imani za kidini ambazo husisitiza maadili kati ya wanajamii wote. Maadili ni tabia nzuri za binadamu. Tabia zisizopendeza na maovu hupingwa katika mafundisho ya kidini.

Hata hivyo, kuna itikadi za kijamii ambazo hazifai hata kidogo. Si vizuri kuwa na dhana kuwa watoto wa jinsia fulani ni bora au muhimu kuliko jinsia nyingine. Watoto wote ni muhimu, wawe wavulana au wasichana. Mtoto ni baraka kutoka kwa Mungu. Mtoto ni zawadi ambayo Mungu hupeana kwa familia. Si vizuri kupewa zawadi na kisha kuidharau. Kuna watu mbalimbali ambao wametekeleza mambo mengi makubwa bila kujali jinsia yao. Kila mtu ana uwezo wake, hakuna jinsia ambayo ni dhaifu.

Isitoshe, si vyema kumlazimisha mtu kuoa ama kuolewa na mtu fulani. Aidha, ndoa za mapema hazifai hata kidogo. Je, ni itikadi gani za kidini na kijamii unazozijua ambazo hazifai?

 1. Ni kweli kuwa mafundisho ya kidini;
  1. hupingwa katika kila jamii.
  2. yanapinga tabia zote katika jamii.
  3. yanashauri kuwa tuwe na tabia nzuri.
  4. husisitiza umuhimu wa maovu maishani.
 2. Ipi si tabia ambayo huweza kufundishwa na dini kulingana na kifungu?
  1. uzalendo
  2. ushirikiano
  3. ukatili
  4. uvumilivu
 3. Zifuatazo ni itikadi zisizofaa isipokuwa;
  1. ndoa za mapema
  2. kuhesimu makabila mengine
  3. kudharau watoto wa jinsia fulani
  4. ndoa za lazima
 4. Mwandishi wa kifungu hiki anatoa ushauri gani?
  1. Hakuna mtoto ambaye ni bora kuliko mwingine.
  2. Watoto wa kike ni bora kuliko wa kiume. 
  3. Hakuna mtoto ambaye ni muhimu katika jamii.
  4. Mtoto anafaa kuwa baraka kwa Mungu.
 5. Kulingana na kifungu hiki, ni kweli kuwa;
  1. Tunafaa kufuata itikadi zote kati jamii.
  2. Itikadi zote za kiafrika hazifai.
  3. Tunafaa kufuata itikadi za wazungu pekee.
  4. Kuna itikadi zinazofaa na zile zisizofaa.

Soma mazungumzo yafuatayo halafu ujibu maswali yanayofuata.

G6SwaT3OS12023Q2
(Katika hospitali ya Tiba, Bi. Siha anaingia akiwa na mtoto wake.)

DAKTARI: Karibu sana mama. Masalkheri?
MAMA:      (Anaketi.) Akheri.
DAKTARI: Je, nikusaidie vipi?
MAMA:      Daktari, mtoto wangu hajalala usiku wote. Anaendesha sana. Lazima ana malaria.
DAKTARI: Pole mama. Hata hivyo huwezi ukajua ugonjwa wa mtoto bila kumpima.
                   (Anasimama na kumchunguza kwa kutumia steshoskopu.) Mpigo wake wa moyo u sawa.
MAMA:      Aha! Mungu ni mwema.
DAKTARI: Hebu uinue mkono huu ili nimwekee kipimajoto. (Anamwekea kipimajoto kwapani.)
                  tutaweza kubaini tatizo lake. Lazima sote tuchange bia ili kuhakikisha kuwa afya Naona ana homa.                    Hebu mpeleke maabarani. Akifanyiwa uchunguzi wa damu, yake inaimarika. 
MAMA:      Asante kwa ushauri wako. Hebu nimpeleke katika maabara kisha nikuletee matokeo. (Anaondoka.)

 1. Yawezekana kuwa mazungumzo haya yalifanyika wakati gani?
  1. alfajiri
  2. adhuhuri
  3. magharibi
  4. macheo
 2. Kwa nini daktari alimshauri mama aende katika maabara?
  1. Ili apewe dawa
  2. Afanyiwe uchunguzi wa damu
  3. Aeleze kuwa mtoto alikuwa na homa 
  4. Ili mtoto adungwe sindano
 3. Daktari aligundua kuwa mtoto alikuwa na tatizo gani?
  1. Moyo ulikuwa ukipiga haraka
  2. Joto la mwili lilikuwa la juu
  3. Alikuwa akiendesha sana
  4. Hakuwa amelala usiku wote
 4. Kulingana na mazungumzo, haiwezekani; 
  1. kujua tatizo la mtoto kabla ya kupimwa.
  2. kumtibu mtoto anayeendesha sana. 
  3. kujua ugonjwa wa mtoto baada ya kupimwa.
  4. kujua tatizo la mtoto kabla ya kumpa dawa.
 5. Nahau 'tuchange bia' ina maana gani jinsi ilivyotumika katika mazungumzo haya?
  1. tuwe makini
  2. tufuate ushauri
  3. tufanye matibabu 
  4. tushirikiane

Soma makala yanayofuata halafu ujibu maswali yafuatayo.

G6SwaT3OS12023Q3

Juma mapesa alikuwa dereva aliyejulikana sana kwenye barabara ya kutoka Nairobi hadi Kakamega. Alipenda sana kuendesha gari kwa kasi iliyopita kiwango. Ingawa alionywa na wazazi wake pamoja na maafisa wa polisi, hakujali. Kila alipopita maafisa wa trafiki, angeendesha gari hilo kwa kasi kama umeme. Ajabu ni kuwa abiria wengine walipenda sana gari hilo. Walisikika wakisema kuwa hiyo ilikuwa njia rahisi ya kufika mapema. Haja kubwa ya Mapesa kuendesha gari haraka ilikuwa tamaa ya kutaka kufanya safari nyingi mno. Alitaka kupata kiasi kikubwa cha pesa kufikia mwisho wa siku.

Siku moja, saa kumi na mbili kasorobo, gari hilo la abiria kumi na wanne lilikuwa tayari kuanza safari. Baada ya wanawake saba kuingia ndani, wanaume waliongezeka hadi likajaa. Mapesa alishika usukani kisha wakang'oa nanga. Kama kawaida, gari lilipepea kama upepo barabarani huku abiria wengi wakifurahia ngoma. Mara Mapesa alifika mahali ambapo barabara ilipinda. Alijaribu kulielekeza gari kwa njia inayofaa lakini hakufua dafu. Sauti iliyosikika ilikuwa ya 'krrrrr', kisha 'ku'. Hapo ndipo mapesa alipovunjikia miguu yote miwili. Sasa yeye hutumia kitimaguru kutoka mahali pamoja hadi pengine.

 1. Mapesa alikuwa na tabia inayoweza kulinganishwa na ya kiumbe gani?
  1. simba
  2. fisi
  3. kunguru
  4. chiriku
 2. Maneno 'kwa kasi kama umeme' ni mfano wa fani gani ya lugha?
  1. nahau
  2. istiara
  3. methali
  4. tashbihi
 3. Safari inayozungumziwa ilianza saa ngapi?
  1. 5:45
  2. 12:15
  3. 6:15
  4. 11:45
 4. Methali gani isiyoweza kutumika kurejelea ujumbe katika kisa hiki?
  1. Haraka haraka haina baraka.
  2. Asiyesikia la mkuu huvunjika guu.
  3. Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.
  4. Tamaa mbele mauti nyuma. KISWAHILI: LUGHA
 5. Chagua mpangilio unaofaa wa matukio katika makala haya.
  1. kuanza safari, kuvunjika mguu, gari kujaa
  2. ajali kutokea, kuvunjika miguu, kutumia kitimaguru
  3. gari kujaa, kutumia kitimaguru, kuvunjika miguu
  4. ajali kutokea, kuvunjika miguu, kuanza safari

Chagua jibu linalofaa kati ya majibu uliyopewa ili kujazia nafasi zilizoachwa.

Ukosefu wa mvua ___16___ ukame mkubwa nchini. Wakazi ___17___taifa letu wamekuwa ___18___ sana kutokana na ukosefu wa chakula, maji safi na mahitaji mengine. ___19___ kubadilisha hali ya mambo, ni vyema tupande miti na kuitunza ili iwe mikubwa. Miti yote ___20___ na kuwa mikubwa, huweza kuvutia mvua na kubadilisha hali ya mambo.

   A   B   C   D 
 16.   imesababishwa  umesababishwa   imesababisha   umesababisha 
 17.  katikati  kwa   katika   ndani mwa 
 18.  wameteseka  wanateseka   wakiteseka  watateseka
 19.  Ili  Ila  Lakini  Wala
 20.  yakitunzwa  ikitunzwa  ukitunzwa  zikitunzwa

 

Jibu maswali yafuatayo kulingana na maagizo.

 1. Chagua ukubwa wa sentensi ifuatayo.
  Ndovu alisimama karibu na nyumba ya mzee huyo.
  1. Jidovu lilisimama karibu na jinyumba la zee hilo.
  2. Kidovu kilisimama karibu na kijumba cha kizee hicho.
  3. Dovu lilisimama karibu na jumba la jizee hilo.
  4. Dovu lilisimama karibu na jumba la zee hilo.
 2. Kama jana ilikuwa Ijumaa, mtondo itakuwa lini?
  1. Jumapili
  2. Jumatatu
  3. Jumanne
  4. Jumatano
 3. Onyesha ukanusho wa;
  Wewe ulikuja nyumbani.
  1. Wewe hukuja nyumbani.
  2. Wewe haukukuja nyumbani.
  3. Wewe hukukuja nyumbani.
  4. Wewe huakuja nyumbani.
 4. Tambua aina za maneno yaliyopigiwa mistari.
  Wawili walienda nyumbani kwao mapema.
  1. kiwakilishi, kielezi, kielezi
  2. kivumishi, kielezi, kielezi
  3. kiwakilishi, nomino, kielezi
  4. kiwakilishi, kielezi, nomino
 5. Sentensi gani iliyo katika hali timilifu?
  1. Juma husoma kwa bidii.
  2. Rehema amefua nguo zake zote.
  3. Zahra alipanda miti mingi.
  4. Ninapenda kula mboga na matunda.
 6. Nomino gani isiyopatikana katika ngeli moja na zingine?
  1. mafuta
  2. manukato
  3. mazingira
  4. mabua
 7. Yaf uatayo ni matumizi ya koloni isipokuwa;
  1. kutanguliza orodha
  2. kuunganisha sentensi mbili
  3. kutenga saa na dakika
  4. kutenga maneno katika orodha
 8. Onyesha sentensi iliyotumia kiwakilishi kiulizi.
  1. Mwanafunzi gani aliye na kalamu? 
  2. Chakula hicho kitapewa yupi?
  3. Nyumba mpya ni ya akina nani?
  4. Wote wameenda wapi?
 9. Chagua nomino iliyonyambuliwa katika kauli ya kutendua.
  1. fua
  2. angua
  3. tambua
  4. anua
 10. Maagano gani ambayo hutumika wakati wa jioni?
  1. kwaheri
  2. buriani
  3. alamsiki
  4. siku njema

INSHA

Mwandikie mwalimu wako barua ukimweleza kwa nini hukuja shuleni juma lililopita.

MARKING SCHEME

 1. C
 2. C
 3. B
 4. A
 5. D
 6. C
 7. B
 8. B
 9. A
 10. D
 11. B
 12. D
 13. A
 14. C
 15. B
 16. D
 17. C
 18. C
 19. A
 20. B
 21. D
 22. C
 23. A
 24. A
 25. B
 26. D
 27. B
 28. B
 29. D
 30. C
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Grade 6 Opener Exams Term 3 2023 Set 1.


Tap Here to Download for 30/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students