Displaying items by tag: kiswahili
Kiswahili Questions and Answers - Grade 5 End of Term 2 CBC Exams 2022 Set 1
Some mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswall 1-5.
(Mwalimu na wanafunzi wanajadiliana kuhusu umuhimu wa kuyatunza mazingira)
Mwalimu: Hamjambo wanafunzi?
Wanafunzi: (Wakiamka sawia) Hatujambo mwalimu, shikamoo.
Mwalimu: Marahaba (Anawaashiria wakae. Wote wanaketi na kushukuru.) Naam, leo ningependa tuzungumze kuhusu namna na umuhimu wa kuyatunza mazingira kwa hivyo...
Matayo: (Anaunyanyua mkono wake) Samahani mwalimu, mazingira ni nini?
Mwalimu: (Akitabasamu) Matayo huishi vituko! Ndilo nililotaka kueleza. Mazingira ni yale yote yanayotuzunguka. Hebu pendekezeni njia mbalimbali za kuyatunza mazingira
Manyanga: Nadhani ni vyema kukata nyasi ndefu ili kuharibu makao ya mbu.
Kaisari: Ni vyema pia kutunza vyanzo vya maji kama vile mito, chemichemi, mabwawa na maziwa.
Pendo: Nikiongezea, si vyema kutumia mbolea nyingi zaidi hasa za madukani ili tusiyaathiri maji na udongo.
Mwalimu: Nimefurahia mno michango yenu. Zipo njia nyingi za kuyatunza mazingira. Kimsingi, umuhimu wa kuyatunza mazingira ni kuwafanya viumbe waishi maisha salama.
- Mazungumzo haya yaliandaliwa majira ya saa ngapi?
- Saa sita adhuhuri.
- Saa mbili asubuhi.
- Saa kumi jioni.
- Hatujaelezwa.
- Ili kuonyesha heshima kuu, mwalimu alipowaamkia wanafunzi, wote
- walisimama ili kupokea salamu yake.
- walitaka kuchangia katika majadiliano
- walitaka kujua maana ya mazingira.
- walitaja umuhimu wa kuishi katika mazingira safi.
- Ni mwanafunzi yupi aliyemkatiza mwalimu alipokuwa akiongea?
- Manyanga .
- Matayo
- Kaisari
- Pendo
- Kulingana na mazungumzo haya, yote yanayotuzunguka ndiyo
- mazingara.
- hewa.
- miti.
- mazingira.
- Mwishoni, mwalimu alifurahishwa na nini?
- Heshima ya wanafunzi wake.
- Umuhimu wa kuyatunza mazingira.
- Michango ya wanafunzi wake.
- Njia mbalimbali za kuyatunza mazingira.
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 6 hadi 8.
Siku moja paka na mbwa walienda karamuni. Mwenyeji wao, panya, aliwakaribisha kwa mikono miwili. Wageni waliketi sebuleni kwenye makochi maridadi, mekundu, kama damu.
“Habari za mtokako?" Panya aliwaamkia wageni kwa heshima. "Njema sana!” wageni walijibu pamoja huku wakitabasamu. Baadaye, panya aliwasha runinga na kuwaambia wageni wake, “Tazameni televisheni. Mimi naelekea mekoni kuwapikia chakula.” Mara, huyoo! Akaenda jikoni. Haraka, alipika nyama na kuitia mchuzi wa maziwa.
- Paka na mbwa waliandaliwa nini na mwenyeji wao?
- Nyama na maziwa
- Njugu na maziwa.
- Maziwa na mifupa.
- Chai na nyama.
- Kabla ya panya kuelekea mekoni,
- aliwaandalia wageni wake chakula.
- aliwasha televisheni.
- alipika nyama.
- alitia maziwa katika nyama.
- Panya alienda jikoni
- kuwasha runinga.
- kununua chakula.
- kupika chakula.
- kuwakaribisha wageni.
- Kati ya hawa, ni mnyama yupi hajatajwa katika ufahamu?
- Paka
- Panya
- Mbwa
- Sungura
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 9 hadi 12.
Lengo la elimu ni kumsaidia mtoto kukuza ujuzi na vipawa na kukuza maadili ya maisha pamoja na maisha ya kiroho. Leo, mwalimu si mkufunzi au msimamizi bali ni msaidizi na mwelekezi. Hapa, mwalimu hudokeza au kutoa habari za juujuu tu. Ni jukumu la mwanafunzi kuleta umakinifu na kutafuta undani wa habari za mwalimu. Bila shaka, mwalimu anatarajiwa kumsaidia mwanafunzi katika kuufikia undani huo. Mwalimu hampi mwanafunzi ujuzi wowote bali humwonyesha jinsi anavyoweza kuupata ujuzi yeye mwenyewe. Mtoto anapozaliwa, ujuzi huwa ndani yake nao husubiri kuamshwa. Mwalimu amwonyeshe mtoto pale ujuzi ulipo na jinsi anavyoweza kuufanyia mazoezi hadi utokeze vilivyo na kumfaa.
- Kulingana na kifungu, baada ya mwalimu kudokeza jambo fulani, mwanafunzi
- atatafuta ukweli kulihusu.
- atamtegemea katika kila jambo.
- ataweza kupita vizuri katika mitihani.
- atashindwa kabisa kumwelewa.
- Kabla ya ujuzi ulio ndani ya mtoto kuonekana, ni lazima ujuzi huo
- uongozwe.
- uamshwe.
- utokeze.
- ugunduliwe.
- Katika miaka ya sasa, mwalimu ni
- mkufunzi na msimamizi.
- msaidizi na mkufunzi.
- mwelekezi na msimamizi.
- mwelekezi na msaidizi.
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 13 hadi 15.
Serikali ya nchi hii inawataka watoto wote wapelekwe shuleni wakasome kwa sababu masomo ndio ufunguo wa maisha. Watu wanaowaajiri watoto hata wasisome wanafaa kuhukumiwa ili kupunguza maovu kama hayo.
Mtoto ambaye hana elimu siku hizi huwa na shida nyingi kupita kiasi kwa sababu hawezi kupata ajira nzuri ukubwani. Hii ndiyo sababu serikali inahimiza kila mtoto kupata elimu. Zamani, watoto hawakuwa wakisoma kwa sababu hawakujua umuhimu wa elimu maishani
mwao.
Ili kuzuia magonjwa na njaa, elimu huwa muhimu. Ili kudumisha adabu njema na nidhamu, elimu huwa lazima. Watoto waliolemewa na masomo huwa wa kurandaranda mitaani, wezi au watendaji wa mambo mabaya katika jamii.
- Ni gani si kweli kulingana na taarifa?
- Masomo ni muhimu maishani.
- Serikali inataka watoto wote wasome.
- Zamani, watoto wote walisoma.
- Ni vyema kuwaelimisha watoto.
- Kulingana na kifungu, mtoto ambaye hana elimu siku hizi
- huwa na shida.
- hupendwa na wengi.
- hupata kazi.
- huajiriwa.
- Katika aya ya mwisho, tumeambiwa kuwa watoto wasiosoma huweza kuwa
- wezi na wafanyakazi.
- wa kurandaranda na wenye bidii.
- wenye bidii na wezi.
- wa kurandaranda na wezi.
Soma kifungu kifuatacho. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa
Siku hiyo tulikuwa tumeingoja kwa hamu na ghamu. Sote tulifika ____16____ na mapema tukiwa tayari kuabiri ____17____ kuelekea mjini Mwambasani. Hii ilikuwa mara yangu ya ____18____ kuenda huko. Sikuwa nimewahi kwenda huko. Tuliingia ____19____ tukiwa na furaha sana. Mara dereva alilitia gari ufunguo na safari _____20_____
-
- asubuhi
- jioni
- adhuhuri
- usiku
-
- baiskeli
- basi
- ndege
- meli
-
- moja
- mwisho
- tatu
- kwanza
-
- njiani
- safari
- basini
- barabarani
-
- ikaanza
- ukaisha
- ikaendelea
- ukaanza
Katika swali la 21-30, jibu swali kulingana na maagizo uliyopewa.
- Kati ya hizi, ni nomino ipi isiyo katika ngeli ya U-ZI?
- Uteo
- Uzi
- Upishi
- Ufunguo.
- Tulimwona batamzinga akiogelea bwawani. Nomino iliyopigiwa mstari ni
- nominoambata.
- nomino ya wingi.
- nomino dhahania.
- nomino kitenzi jina.
- Kati ya maneno uliyopewa, ni lipi litakuwa la pili katika kamusi?
- Mshikaki
- Mswaki
- Msaada
- Msaragambo
- ii
- iv
- iii
- i
- Mkufu ni pambo ambalo huvaliwa .
- kichwani.
- miguuni.
- shingoni.
- mikononi.
- Chagua sentensi iliyoakifishwa vibaya.
- Juma, Roda na Maria walialikwa shereheni.
- Maembe maparachichi na mananasi hununuliwa wapi.
- Ukimwona, mwambie aje kwangu.
- Je, mliwaona wanyama wapi mbugani?
- Ni upi wingi wa sentensi hii? Karatasi ilichafuliwa na mtoto.
- Karatasi zilichafuliwa na watoto.
- Makaratsi yalichafuliwa na watoto.
- Karatasi zilichafuliwa na mtoto.
- Karatasi ilichafuliwa na watoto.
- Ni yupi kati ya hawa ni ndege wa porini?
- Kuku
- Bata
- Batabukini
- Mwewe
- Kitenzi imba katika kauli ya kutendwa huwa
- imbia.
- imbiwa.
- imbwa.
- imbaimba.
- Chagua kinyume cha sentensi ifuatayo:
Mgeni amesimama karibu na mfalme.- Mgeni hajasimama karibu na mfalme
- Mwenyeji ameketi mbali na malkia
- Mwenyeji amesimama karibu na
- Mgeni ameketi mbali na malkia.
- Kanusha kauli ifuatayo kwa usahihi.
Wewe umeimba vizuri. Wewe- haujaimba vizuri.
- umeimba vibaya.
- hujaimba vibaya.
- hujaimba vizuri.
MARKING SCHEME
- D
- A
- B
- D
- C
- A
- B
- D
- C
- A
- B
- D
- C
- A
- D
- A
- B
- D
- C
- A
- C
- A
- B
- C
- B
- A
- D
- C
- B
- D
Kiswahili Questions and Answers - CBC Grade 6 End of Term 2 Exams 2022 Set 2
MASWALI
Swali la 1 hadi 5. soma mazungumzo haya kisha ujibu maswali.
Mbula: Shikamoo mama?
Mama: Marahaba mwanangu. Umeamkaje?
Mbula: Vyema. Mbona leo umerauka mapema hivyo?
Mama: (Akimwonyesha kalenda) Umesahau leo ni Madaraka Dei?
Mbula: Nilidhani kuwa ni kesho Jumapili!
Mama: Ni muhimu kila mzalendo kushiriki katika sherehe za kitaifa.
Mbula: Asante kwa kunipasha. Sherehe za leo zinaongozwa na nani?
Mama: Zitaongozwa na kiongozi wa kaunti. Unafahamu jina la cheo chake?
Mbula: Naam, Gavana.
Mama: Vizuri sana mwanangu. Ungetaka kuandamana nami?
Mbula: Bila shaka. Sitabaki nyuma.
Mama: Jiandae haraka kwa vile chelewa chelewa utampata mwana si wako.
Mbula: Sawa mama (Anaondoka)
- Kwa nini mama aliamka mapema siku hiyo?
- Ni mazoea yake
- Ili kujiandaa kuenda kanisani
- Ili kujiandaa kuenda siku ya Madaraka
- Ili kutayarisha kiamsha kinywa
- Hatua ya mama na Mbula kuamua kuenda kuhudhuria sikukuu ya Madaraka inaonyesha kuwa wana
- uzalengo
- bidii
- heshima
- hekima.
- Mazungumzo haya yalifanywa siku ya gani?
- Jumanne
- Ijumaa
- Jumapili
- Jumamosi
- Chelewa chelewa utampata mwana si wako ni aina ya
- tashbihi
- Nahau
- methali
- tanakali
- Kiongozi wa nchi huitwa
- Gavana
- Rais
- Seneta
- Chifu
Swali la 6 - 12. soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali
Ni makosa kudhulumu, binadamu duniani
Ni hatia kuhukumu, kwa udhalimu kortini
Ni vyema unapodumu, u mzuri duniani
Tenda wema nenda zako, Jalali atakulipa
Maisha yawe magumu, usiwe mwongo moyoni,
Jikuzeni humu humu, ukinge umaskini,
Ni busara kuhudumu, kwa nia safi mtimani,
Tenda mema nenda zako, Jalali atakulipa.
- Shairi hili ni la aina gani?
- Tathlitha
- Tarbia
- Tathnia
- Takhmisa
- Kila mshororo wa shairi hili una mizani ngapi?
- 16
- 8
- 32
- 64
- Ujumbe wa shairi hili ni kuhusu
- kuwa na bidii pekee
- kuwa mnafiki
- kuwa na utu
- kuwa na heshima pekee
- Neno jingine lenye maana sawa na Jalali ni
- rafiki
- ndugu
- jirani
- Mungu
- Mshororo wa pili katika kila ubeti huitwa
- mwanzo
- mloto
- mleo
- Kibwagizo
- Shairi hili lina beti ngapi?
- Mbili
- Tatu
- Nne
- Moja
- Andiku ukwupi wu nishur uro wu pili ubeti wa kwanza
- Ni vyema unapodumu
- Jikazeni humu humu
- Ni hatia kuhukumu
- Kwa udhalimu kortini
Swali la 13 hadi 15. Soma kifungu hiki kisha ujibu maswali
Kimeu, Ngina, Mwende na Misha walimtembelea mwulimu wuo majilisini. Mwalimu Mumo alikuwa na kazi nyingi ya kuandaa somo. Alikuwa akichora chati kuhusu misimu tofauti.
Wanafunzi hao walimsaidia mwalimu wao katika shughuli hiyo. Kimeu Misha na Nginn walijaza kalamu rangi. Kimeu na Mwende walisaidia kuchora chati. Wote isipokuwa Ngina walisaidia kupaka rangi. Kimeu alisaidia kusafisha eneo la kufanyia kazi nao wasichana wute wakasaidia kuanika chati ukutani.
- Mwalimu alikuwa akifanyia kazi wapi?
- Darasani
- Majilisini
- Uwanjani
- Ofisini
- Ni mwanafunzi yupi hakuanika chati ukutani?
- Ngina
- Mwende
- Misha
- Kimeu
- Mwende alifanya kazi ngapi kwa jumla?
- Tatu
- Mbili
- Nne
- Moja
Swali la 16 hadi 20. soma fungu kate na ulaze natasi kwa ibu sahihi
Wakazi wa kijiji 16 wana uhusiano 17 . Wana bidii kama 18 kazini. Wamepanda miti 19 ili kuyatunza mazingira. Katika msimu wa 20 wao huwa hawahisi jua kali sana kama ilivyokuwa zamani kabla ya kupanda miti hiyo.
-
- wetu
- yetu
- letu
- chetu
-
- mzuri
- zuri
- wazuri
- uzuri
-
- kunguru
- kondoo
- mchwa
- njiwa
-
- mingi
- mengi
- wingi
- nyingi
-
- masika
- kiangazi
- vuli
- choo
Chagua jibu sahihi kujibu maswali
- Kinyume cha neno 'tamu' ni
- chungu
- kali
- mbaya
- chachu
- Mtu anayetunga mashairi huitwa
- manju
- malenya
- mwandishi
- mtunzi
- Chagua neno lililo katika ngeli ya YA-YA.
- magonjwa
- mazingira
- matunda
- ukuta
- Chagua jibu linaloonyesha wingi wa 'uso wangu umeoshwa'
- Nyuso zangu zimeoshwa
- Nyuso zao zimeoshwa
- Nyuso zetu zimeoshwa
- Uso yetu umeoshwa
- Chagua jibu lenye visawe
- Furaha - huzuni
- Hongo - rushwa
- Mshindi - mshinde
- Mtu - jibu
- Chagua sentensi iliyoakifishwa vizuri
- Ala nimeona jitu kubwa sana.
- Mama: alinunua embe tomoko na chungwa
- Je, Leo ni siku gani
- Hoyee! Tumeshinda mbio hizo.
- Neno 'mtoto katika ukubwa ni
- jitoto
- kitoto
- toto
- litoto
- Chagua methali inayoonyehsa ushirikiano
- Mtaka cha mvunguni sharti ainame
- Jifya moja haliinjiki chungu
- Mchagua jembe si mkulima
- Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo
- Ni pambo lipi huvaliwa shingoni?
- Mkufu
- Pete
- Herini
- Kipini
- Tumia kivumishi kirejeshi amba-kukamilisha sentensi:
Mpira ulinunuliwa umepasuka- ambao
- ambayo
- ambacho
- ambalo
KUANDIKA INSHA
Andika insha kuhusu;
Andikia mwalimu mkuu wa shule yako barua rasmi ukiomba ruhusa kujiunga na kikundi cha wanaskauti shuleni:
MWONGOZO WA KUSAHISHA
COMPOSITION / INSHA MARKING SCHEME
- The composition will be assessed according to the following guidelines.
- The maximum mark will be 40 and the minimum mark 01.
Does the script show that the candidate can communicate accurately, fluently and imaginatively in Englis
Accuracy (16 marks)
- Correct tense and agreement of verbs
- Accurate use of vocabulary (4 marks)
- Correct spelling (4 marks)
- Correct punctuation (4 marks)
Fluency (16 marks)
- Correct flow of the story (4 marks)
- Well sequenced sentence and connected paragraphs (4 marks
- Correct spelling (4 marks)
- Ideas developed in logic sequence (4 marks)
Imagination (8 marks)
- Unusual but appropriate use of words (4 marks)
- Variety of structure (4 marks)
NB: Please teachers are requested to scrutinize this marking scheme before use, it is worth
Kiswahili Questions and Answers - CBC Grade 6 End of Term 2 Exams 2022 Set 1
MASWALI
Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali 1-5.
(Ni wakati wa mapumziko shuleni. Mwalimu na mwanafunzi wanajadiliana.)
Mwanafunzi: Shikamoo mwalimu. Nimefurahi kukupata bila shughuli nyingi.
Mwalimu: Marahaba Zigwembe. Nimemaliza kuzikagua insha zenu punde tu. Eh! Naona mnaendelea vizuri katika uandishi.
Mwanafunzi: Siyaamini masikio yangu. Awali tulikuwa mbumbumbu mno katika uandishi. Sina budi kukushukuru kwa juhudi zako tumbi nzima.
Mwalimu: Hilo ndilo jukumu langu; kuwanoa muwe wembe. (Kimya kidogo) Haya kibibi, ungependa nikusaidieje leo?
Mwanafunzi: (Huku akiketi mkabala na mwalimu) Bi. Chui, suala la kutofautisha vihisishi na vihusishi linaniiemea pakubwa. Sijui ni...
Mwalimu: (Akichanua uso kwa tabasamu angavu) Zigwembe, ni kama kwamba ulijua. Hilo ndilo funzo linalofuata baada ya kipindi hiki cha mapumziko. Nitatoa ufafanuzi kemkem darasani.
Mwanafunzi: (Akiinuka kuondoka) Sawasawa mwalimu, tukutane darasani niupate uhondo huo.
- Kilichomfurahisha mwalimu mwanzoni mwa mazungumzo haya ni
- kutokuwa na shughuli nyingi.
- hatua waliyoipiga wanafunzi wake katika uandishi.
- kuwa hapo awali, wanafunzi wake walikuwa mbumbumbu.
- kwamba alikuwa amemaliza kuhakiki insha.
- Yawezekana kuwa mazungumzo haya yalitukia mnamo majira ya
- alfajiri.
- usiku.
- adhuhuri.
- asubuhi.
- Unadhani ni kwa nini mwanafunzi hakuyaamini masikio yake?
- Hakuyaamini maneno ya mwalimu.
- Mwalimu aliyatilia chumvi maelezo yake.
- Hakuamini kuimarika kwao ghafla katika uandishi
- Maneno ya mwalimu hayakuwa na ukweli wowote.
- Kulingana na mazungumzo haya, ni kweli kusema kuwa mwalimu huyu ni
- hodari.
- hatari.
- mjanja.
- mwongo.
- Je, kwa nini Bi. Chui hakumfafanulia
Zigwembe tofauti baina ya vihisishi na vihusishi?- Alikuwa na shughuli chungu nzima.
- Alitaka awaeleze wote darasani katika kipindi kilichofuata.
- Alihitaji wanafunzi wengi ili kutoa maelezo yake.
- Wakati ulikuwa umeyoyoma.
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 6 hadi 8.
Serikali inapaswa kuwaelimisha wakulima nchini. Hivi ni kwa sababu ya upungufu wa mazao ya kilimo. Wakulima wengi wamepungukiwa na ujuzi wa shughuli za ukulima. Hivyo basi, kuna haja ya kuwafunza njia za kunyunyizia mazao yao dawa. Pia inafaa wafunzwe njia bora za upanzi. Kwa wengine, kutumia mbolea huwa ni jambo wasilolijua wala kulithamini. Hii hupunguza mazao ikiwa mashamba hayana rutuba.
Kwa wanaofuga wanyama na ndege kama vile kuku, wanapaswa kufundishwa mbinu za kukabiliana na magonjwa kama ville sotoka kwa ng'ombe na kideri kwa kuku. Maafisa wa kilimo kukabiliana na magonjwa kama vile sotoka kwa ng'ombe na kideri kwa kuku. Maafisa wa kilimo hawana budi kuwa katika mstari wa mbele katika kuwapa wakulima misaada ya kila aina maana kilimo ni uti wa mgongo wa taifa letu.
- Kulingana na taarifa, ni kwa nini mazao ya kilimo yamepungua?
- Wakulima hawafanyi bidii.
- Wakulima hawana ujuzi unaohitajika.
- Kuna upungufu mkubwa wa mvua.
- Kwa sababu kuna ukame uliokithiri nchini.
- Taarifa hii inasema kuwa, kwa wakulima wengine, matumizi ya mbolea
- ni kitu muhimu mno.
- ni jambo geni wasilolielewa.
- hustalili kufunzwa na maafisa wa kilimo.
- ni jambo walilo na mazoea makuu nalo.
- Kulingana na ufahamu, si kweli kusema kuwa
- serikali haina budi kuwapa wakulima mafunzo kemkem.
- mashamba yasiyo na rutuba huhitaji mbolea.
- sotoka huwaathiri sana kuku huku ng'ombe wakiugua kideri.
- si wakulima wote wanatambua mbinu bora za kilimo.
- Sehemu iliyopigiwa mstari mwishoni mwa taarifa hii ina maana gani?
- Taifa letu linategemea sana kilimo.
- Wananchi wengi wa nchi hii ni wakulima.
- Wananchi wote wa nchi hii ni wakulima.
- Wakulima wa humu nchini hawana budi kuongeza bidii kazini.
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 9 hadi 12.
Juzi tulipokuwa sebuleni tukitazama runinga, mjomba alianza kutusimulia jinsi ambavyo mwalimu wao alikuwa akiwaeleza kuhusu umuhimu wa miti. Alianza kwa kusema kuwa mwalimu wao alisema kuwa miti huwa ni maskani ya wanyama mbalimbali, sanasana nyuni ambao hutengeneza viota vyao na kutagia mayai humo. Aliendelea kutuambia kuwa wanyama wengine wanaotegemea miti kama makazi ni wanyamapori kama vile simba, chui, pundamilia na wengine. Si hayo tu, aidha, alisema kuwa miti huweza kutumiwa kujengea, kuundia samani na pia kutumika kama dawa ambapo sehemu mbalimbali za miti hutumika kutibia magonjwa mbalimbali. Tulipokuwa tumechoka kumsikiliza, alituaga na kila mmoja wetu akaelekea kulala ili turauke siku iliyofuata.
- Msimulizi na wenzake walikuwa wakisimuliwa kuhusu nini?
- Madhara ya wanyama.
- Matumizi ya maji.
- Umuhimu wa miti.
- Wanyama wa porini.
- Yawezekana kuwa masimulizi haya yalifanyika
- adhuhuri.
- asubuhi.
- alasiri.
- usiku.
- Kulingana na habari hii, miti hutusaidia katika haya yote ila kutupa
- dawa
- kuni.
- vifaa vya ujenzi.
- vifaa vya kutengenezea samani.
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 13 hadi 15.
Hapo zamani za kale, palikuwa na sungura na mbwa. Wanyama hawa walikuwa marafiki wa kufa kuzikana. Naam, walipendana kama uta na upote. Wanyama hawa walipokuwa makaoni mwao, mbwa alimwambia sungura kuwa yeye alihisi njaa sana. Aliendelea kumwambia kuwa angependa kumla yeye kwa kuwa sungura huwa na nyama nzuri na tamu. Kusikia vile, sungura alijifanya kutojali ingawa alishtuka sana moyoni. Punde kidogo wakati mbwa alikuwa ameangalia kando, sungura alitoweka na kuingia kichakani. Tangu siku hiyo, mbwa aliana kumwinda sungura mahali popote wakati wowote.
- Kulingana na taarifa hii, unadhani ni kwa nini sungura hujificha kichakani?
- Asipatikane na mbwa.
- Anaendelea kumtafuta mbwa.
- Anaaibika anapomwona mbwa
- Anatafuta mawindo humo.
- Kwa maoni yako, mbwa alikuwa
- rafiki wa dhati.
- rafiki mnafiki.
- na nyama bora zaidi.
- rafiki mzuri.
- Sungura alipata mwanya wa kutoweka pale ambapo
- mbwa alimwambia nyama yake ilikuwa tamu.
- walikuwa wamekaa maskanini kwao.
- mbwa alikuwa ameangalia kando.
- mbwa alitoweka na kuingia kichakani.
Soma kifungu kifuatacho. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa
Visa vya watu kuwaua wake, waume au watoto wao vimekuwa _16__ sana siku hizi. Si jambo _17_ mtu kufikia hatua kama _18_ . Hakika, ni_19_ mkubwa. Si hayo tu, wengine hufikia hatua ya kujiangamiza wao wenyewe kwa kujitoa uhai. Binadamu wanafaa kujua njia_20_ za kusuluhisha matatizo yao kuliko kuchinjana na kuuana.
-
- mingi
- wengi
- nyingi
- vingi
-
- jema
- nzuri
- baya
- mbaya
-
- hili
- hiyo
- hizi
- huo
-
- mnyama
- wanyama
- unyama
- kinyama
-
- mzuri
- fupi
- ndefu
- bora
Katika swali la 21-30. jibu swali kulingana na maagizo uliyopewa.
- Chagua sentensi ambayo haina kivumishi cha sifa.
- Tuliambiwa kuwa Mombasa kuna joto jingi.
- Rama alilila tunda bichi.
- Chakula tulichoandaliwa kilikuwa kitamu.
- Mwalimu wetu wa lugha ni mnene.
- Hii, huyu na lile vyote ni
- vielezi vya mahali.
- vivumishi viashiria.
- viwakilishi vionyeshi.
- vivumishi halisi.
- Sehemu inayosukuma damu ienee mwilini ni
- ini
- ubongo.
- figo.
- moyo.
- Tegua kitendawili hiki. Hawa wanaingia, hawa wanatoka.
- Samaki.
- Maji.
- Nyuki.
- Nzi.
- Chagua orodha ya vivumishi vya aina moja.
- Nene, wako, vyetu.
- Hii, wao, chafu.
- Letu, yao, chake.
- Huyu, wangu, bovu.
- Jibu la alamsiki ni
- marahaba.
- nawe pia
- jaala.
- binuru.
- Ni neno lipi kati ya haya litakuwa la mwisho katika kamusi?
- Kibindo
- Kibanda
- Kibarua
- Kibanio
- Chagua sentensi yenye matumizi yasiyo sahihi ya amba.
- Ambao waliwasili mapema walipata nafasi.
- Wanyama ambao waliogongwa na lori wameondolewa.
- Mafunzo ambayo tulipewa yametufaa.
- Ambao hawana vitabu wasome magazeti.
- Msimu wa mvua nyingi huitwa
- masika.
- vuli.
- mafuriko.
- 'iangazi.
- Chagua sentensi iliyotumia lugha ya adabu.
- Mtoto amekojoa kitandani.
- Shangazi yangu amejifungua salam
- Wanawake wenye mimba wapewe viti.
- Mgonjwa alihara hadi akafa.
MWONGOZO WA KUSAHISHA
Kiswahili Questions with Answers - CBC Grade 4 End of Term 2 Exams 2022 SET 1
MASWALI
SEHEMU YA A: KUSIKILIZA NA KUZUNGUMZA
Jibu maswali kwa kutamka (Alama 5)
- Ni nini wingi wa neno daftari?
- Bendera yetu ina rangi ngapi?
- Eleza maana ya "kutiwa nguvani"
- Kamilisha methali ifuatayo, "Asiyesikia la mkuu....
- Taja vazi moja la kike unalolijua.
KUSOMA KWA SAUTI
Soma kifungu hiki kwa sauti (Alama 10)
Shule yetu inaitwa Bidii Jumanne ilikuwa ni siku ya sherehe ya kutia zawadi. Walimu wetu waliwasili mapema kwa matayarisho. Mgeni wetu wa heshima alipowasili, alipewa shada la maua. Shehe na kasisi walituombea kabla ya kuanza sherehe. Wanafunzi thelathini wa gredi ya nne walituzwa. Shangazi yangu alihudhuria kwa naiba ya mama yangu. Thuluthi mbili ya watu ambao walihudhuria walikuwa kina mama.
SEHEMU YA B: SARUFI
Andika visawe vya maneno yafuatayo
- Tembo
- Nyanya
- Jogoo
- Barua
- Motokaa
Nyambua vitenzi vifuatavyo katika kauli ya kutendwa.
- Chora
- osha
- tuma
- panga
- lipa
Unganisha sentensi kuwa joja kwa kutumia kiunganishi sahihi
- Alitekwa nyara. Hakudhulumiwa
- Maria amevaa koti. Maria anahisi baridi
- Utavaa jaketi. Utavaa koti
- Nilienda katika kituo cha mabasi. Nilisafiri Lamu
- Juma hakuvaa mlapa. Juma hakuvaa daluga
Taja majina ya heshima unayotumia kuwaita wafuatao.
- Mzazi wa kiume
- Ndugu wa kiume wa baba yako
- Baba wa mama yako
- Ndugu wa kiume.
- Ndugu wa kike
Andika nomino zozote tano
Andika kwa wingi
- mpira
- kiatu
- ndizi
- ua
- chungwa
SEHEMU YA C: UFAHAMU
Soma ufahamu kisha ujibu maswali (Alama 5)
Auni anamiaka kumi. Wazazi wake waliaga dunia. Anaishi na nyanya yake. Kila siku Auni na nyanya yake hula mihogo. Siku moja, Auni aliugua utapiamlo kwa kula mihogo pekee. Auni hakupata aina zote za vyakula.
Kuna aina nyingiya vyakula. Kuna vyakula vya kujenga mwili kama vile maharagwe. Kuna vyakula vya kupatia mwili nguvu kama vile mihogo. Kuna vyakula vya kuongeza kinga ya mwili kama vile matunda.
Auni hakuwa anaenda shuleni. Hatari hii ilimfikia chifu Stela. Chifu Stela alienda kumwona nyanya yake Auni. Auni alipelekwa katika kambi ya watoto mayatima. Huko alipewa lishe bora.
- Auni alikuwa na umri wa miaka mingapi?
- Auni aliugua ugonjwa wa
- Taja aina ya vyakula vya kujenga mwili
- Auni alipelekwa wapi
- Habari za Auni kutoenda shuleni zilimfikia nani?
SEHEMU YA D: KUANDIKA
Mwandikie binamu yako barua ya kirafiki ukimwalika kwa sherehe ya kuzaliwa kwako.
MWONGOZO WA KUSAHIHISHA
|
(21-25) Sahihisha jibu sahihi |
|
Kiswahili Questions and Answers KCPE 2022 Prediction Papers Set 4
Maswali
Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi tumepewa majibu manne hapo. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya pale uliyopewa
Bwana Hamisi ni seremala 1 sana katika mtaa wetu. Ana 2 kubwa ambapo yeye huundia samani maridadi sana. Ufikapo hapo, hutakosa kuviona vifaa mbalimbali, kama vile 3 wanaonunua katika kazi yake. 4 vijana wengi wanaokosa karo kumwendea kwa mafunzo ili waweze kujitegemea baadaye. Yeye pia ana 5 maadamu. huwapa vijana hawa ujira kila jioni ili nao wajiendeshee maisha yao. Sifa zake 6 kote mtaani. Hupenda kusema kuwa siri ya maisha ni bidii huku akihimiza kuwa 7 .Vijulanga 8 na uhaba wa kazi 9 nchini hayana budi kuiga mfano wake.
A | B | C | D | |
1 | hatari | maalum | mahiri | marufuku |
2 | karakana | kiwanda | maabara | ofisi |
3 | kekee, fuawe, kembeo na pinamaji | utepe bisibisi, jiriwa na patasi | vipuli, mvukuto, timazi na nyundo | msumeno, kekee , chelezo na mvuo |
4 | Kwani | Lakini | Ijapokuwa | Aghalabu |
5 | mkono wazi | mkono birika | mkono mzuri | mkono mwepesi |
6 | zimesambaratika | zimetanda | zimesheni | zimetalii |
7 | ukipanda upepo utavuna tufani | bandu bandu humaliza gogo | cha kuzama hakina rubani | mgagaa n aupwa haondoki patupu |
8 | waliadhirika | walioathiriwa | walioadhiriwa | walioathirika |
9 | kote | wote | zote | yote |
Vita 10 niliadarretsi vya 11 mzaha hata kidogo. Hili ni janga linalotishia kuwasomba vijana kwa mkupuo nimoja. Wakwasi wenye 12 wa darahima wanawauzia wana wetu sumu kali bila kujali lolote. Wavyele ambao 13 kuwa 14 cha kuigwa nao wamejitia hamauzo kucheza ngoma watakazo. Si ajabu kuinwona baba au mama akirejea mastakimumi huku amelewa kama 15 tha kwanza kuwafokea wanawe.
A | B | C | D | |
10 | juu ya | baina ya | dhidi ya | kutokana na |
11 | kufanya | kufanyiwa | kufanyia | kufanywa |
12 | umero | tamaa | shauku | ukata |
13 | watarajwa | wangetarajiwa | walitarajiwa | wanatarajiwa |
14 | kielezi | kielelezo | chombo | chelezo |
15 | pombe | mjinga | komba | nyani |
Kuanzia swali la 16 mpaka 30, ibu kila swali kulingana na maagizo uliyopewa.
- Kati ya viteuzi vifuatavyo, kipi kinaonyesha kuendelea kwa kitendo?
- Jua lachoma vikali leo.
- Walizioka keki tamu wakaziuza,
- Ukifanya bidii utapita mtihani.
- Tulikuwa tukitembea mvua ilipoanza kunyesha.
- Ni orodha gani inayoonyesha viclczi pekee?
- Mombasa, kesho, vibaya, kila siku.
- Kwake, zuri, polepole, chochote.
- Vigumu, baya, kubwa, aghalabu.
- Baada ya vyote, taratibu, chekesha.
- Mibuni hutupatia kahawa. Je, mibono huzaa nini?
- Mabono
- Mbarika
- Tunguja
- Kanju
- Tegua kitendawili kifuatacho:
Iluwafanya watu walie huku wakicheka.- Kifo
- Pilipili mboga
- Kiboko.
- Moshi
- Tambulisha sentencsi iliyoaki fishwa barabara.
- Ala? Kumbe unaishi katika mji huu!
- Je? Huu ni uungwana kweli?
- Nilipofika huko sikumpata; alikuwa amesafiri.
- Tafadhali niletec, maji, sabuni, dodoki
- Maelezo yapi hayana maana ya panga?
- Kaa mahali kwa makubaliano fulani.
- Chombo cha kuleta baridi kinachozungushwa na umeme
- Weka vitu kwa utaratibu mzuri.
- Mahali maalum pa kufanyia matambiko.
- Badili sentensi ifuatayo katika ngeli ya PA-KU-MU.
Shule yao ina wanafunzi wengi.- Shule zao zina wanafunzi wengi.
- Shudeni mwao kuna wanafunzi wengi.
- Shuleni pao mna wanafunzi wengi.
- Shuleni mwao mna wanafunzi wengi..
- Upi ni usemi wa taarifu wa senteni hii...!
Mama alisema, “Tafadhali niwashic jiko .. nitelekechungu".- Mama alimwomba amwashie jiko ili ateleke chungu.
- Mama aliagiza awashiwejiko ili atelcke chungu.
- Mama alisema angewashiwa jiko angeteleka chungu.
- Mama aliin wambia amwashie jiko wateleke chungu.
- Andika udogo wa:
Mlango mpana umefunguka.- Lango pana limefunguka.
- Jilango pana limefunguka.
- Kilango kipana kimefunguka.
- Kijilango kipana kimefunguka.
- Kanusha sentensi ifuatayo kwa usahihi:
Maji yasingepatikana upesi mifugo yetu ingcangamia.- Maji yangalipatikana upesi mifuo yetu isingeangamia.
- Maji yangepatikana upesi mifugo yetu isingeangamia.
- Maji yasingepatikana upesi mifugo yetu isingeangamia.
- Maji yangepatikana upesi mifuo yetu ingeangamia.
- "Gao huwa chombo wakatiwe" ni kwa wanziovidharau vitu vikuu; kama vile uncler la muwa la jana chungukaona kivuno"ni kwa wale
- wanaovidharu vitu vidogo.
- wanaopuuza msaada mkubwa.
- wanaopuuza mali ya wengine.
- wanaotamani mali ya wengine.
- Ugonjwa wa macho unaoweza kusababisha upofuni
- ukoma
- inachapwi
- trakoma
- alkani
- Ni sentensi ipi iliyo na kivunishi cha pekee?
- Wazee wengi walitou micliango yao.
- Wazee wale walitoa michango yao.
- Wazee wenu walitoa michango mizuri.
- Wazee wengine walitoa michango mikubwa.
- Mtu anayeongea kwa richa ya ulimi huitwa
- kithembe
- kigugumizi
- kiduko
- kiduvya
- Kamilisha kwa ufasaha:
Mtoto huyu, huyo na Yule- mnifuate
- wazifuate
- anifuate
- tufuate
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 31 – 40
Bwana Aisee aliporejea jijini alifungua ofisi kubwa aliyoipamba kwa samani za hali ya juu. Kisha aliwasiliana na waandishi wa magazeti mbalimbali. Alidai kuwa kulikuwako na mradi kabambe wa kuhakikisha kuwa vijana waliokosa amali wangeajiriwa kazi za maana kwenye hoteli za kitalii huko Uarabuni na Ulaya na hata kwenye meli za kifahari. Viongozi wengi walimshehenezea Bwana Aisee sifa kemkemu, “Huyu ni mzalendo kindakindaki! Anawakumbuka raia wenzake ambao hawana bahati kama yeye!"Vijulanga waliokuwa na hamu na ghamı ya kuenda ugenini walifurika ilipokuwa ofisi yake.
Walichohitajika kufanya tu ni kulipa ada ya shilingi elfu tano pamoja na kiasi kingine kama hicho kugharimia vyeti vya usafiri. Licha ya kuwa wengi wao hawakuwa na namna ya kuzipata pesa hizo, walikuwa radhi kukopa wahakikishe kuwa wamepata nafasi hizo adimu. Vijana hao pia walitakiwa kuenda hospitali fulani ya kibinafsi kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu. "Aisee bwana, huo ndio ustaarabu wa wenzetu walioendelea.. Ukitaka kumwajiri mtu lazima uijue siha yake ikoje," Bwana Aisee. aliwakumbusha. Hamna aliyejali. Kilichokuwa muhimu ni kuwa, baada ya miezi miwili wangepata kazi ambazo zingewafanya waipige kumbo la milele ukata uliotishia kuwagubika kama wingu.
Baada ya kuzikusanya hela hizo zilizolipwa na vijana zaidi ya elfu thelathini, Bwana Aisee aliwaambia wangoje kwa muda wa miezi miwili. Muda waliokuwa wamepewa wa kungoja mambo yaive ukapita. Tarehe ya kusafiri kuenda kuanza kazi zao ikaahirishwa. Taarifa iliyotoka katika ofisi kuu huko ulaya ilidai kuwa kuahirishwa huko kalitokana na hali mbaya ya usalama. Tarehe hizo zilipokwisha kuahirishwa mara nyingine mbili, kila mmoja alianza kutuhumu kuwa palikuwa na jambo. Malalamishi ya kila aina yalianza kusikika kwenye vyombo vya habari. Wakaanza kumsaka Bwana Aisee. Lakini hawakujua kumbe bwana huyo alikuwa ameingia mitini.
Uchunguzi wa historia ya Bwana Aisee ulianza kufanywa. Jamaa waliosoma naye walitoa habari zake zote bila kusaza lolote. Walieleza jinsi alivyokua fundi wa kuongea kizungu. "Lakini huyu si fundi wa kizungu tu bali na mizungu pia!" Walisema wengine kwa hasira walipozisikia habari hizo. Serikali ilianza mipango kabambe ya kumsaka Bwana Aisee. Ilibidi kuwashirikisha wachunguzi wa polisi wa. kimataifa, INTERPOL, katika swala zima. Haikuchukua muda kabla ya kugunduliwa kuwa mashirika yaliyodaiwa kuhusika na suala la ajira hizo yalikuwa bandia.
Mambo yaliendelea kukanganya wakati ofisi ya Bwana Aisee iliyokuwa jijini ilipochomeka siku moja wakati wa usiku na vyeti vyote kuteketea. Nayo hospitali waliyokuwa wameenda kufanyiwa uchunguzi wa kiafya wale walioenda kuomba kazi ilifungwa ghafla na daktari aliyehusika kutoweka. Ilikuwa wazi sasa kuwa watu walikuwa wametapeliwa.
Kashfa hii ilizungumziwa na wengi kote nchini si katika redio wala runinga bali pia magazetini na kwingineko. Adinasi waliapiza. Lakini njia ya mwongo ni fupi. Aisee alibambwa na polisi wa kimataifa alipokuwakatika uwanja wa ndege wa Frankfurt huko Ujerumani akijitayarisha kuabiri ndege kuelekea Afghanistan alikopanga kujificha kwa muda hadi mambo yatulie.
Baada ya kutiwa mikononi, Bwana Aisee alisafirishwa chini ya ulinzi mkali hadi jijini Nairobi alipofikishwa mbele ya hakimu. Kesi yake ilihudhuriwa na mamia ya vijana waliohasirika. Mwishowe Bwana Aisee alitumbukizwa gerezani kwa miaka minane ikiandamana na kazi za sulubu. Mizungu yake ilikuwa imegota mwamba.
- Lengo la Bwana Aisee kuwasiliana na wanahabari lilikuwa ni
- kuwafahamisha kuhusu ofisi yake.
- kuwaeleza kuhusu mradi wake.
- kutoa tangazo kuhusu mradi wake
- kutoa tangazo kuhusu ofisi yake.
- Wengi waliosikia kuhusu mipango ya Bwana Aisec . .. .
- walimsifu kuwa mpenzi kamili wa nchi yake.
- walimwona kama adui mkubwa wa nchi.
- walimsifu kwa kuleta mapinduzi nchini:
- walimshuku kuhusu nia ya kazi yake,
- ni kusajiliwa kila mhusika atihitaji kulipa shilingi elfu
- tano, kufanyiwa uchunguzi wa kiafya.
- kumi, kuchangazwa afya yake.
- tano, kuwasilisha vyoli vya usafiri.
- kumi, vyeti vya usafiri na kuchungu wa
- Watu walianza kutuhumu kuwa mambo hayakuwa sawa
- baada ya tarehe ya kuanza kazi kuahirishwa.
- tarehe ya kusafisi ilipoahirishwa tena,
- Bwana Aisec alipotoweka kutoka jijini.
- tarehe ya usafiri ilipoahirishwa kwa mara ya tatu. .
- bwana huyo alikuwa ameingia mitini' maana yake ni kuwa alikuwa
- ametoweka haada ya kufanya uhalifu.
- ameshiriki uhalifu wa kuibia umma..
- ameshepatwa na mabaya.
- amijitia katika mambo asiyoyafahamu.
- Historia ya Bwana Aisee ilibainisha kuwa alikuwa na hulka ya
- kuwaibia watu
- kusema kimombo
- kusafiri uarabuni
- kuwapenda watu
- Inaonekana kuwa asiki ya kuchomeka kwa olisi ya Bwana Aisee ilikuwa
- kuficha laistoria yake.
- hasira za vijana walioibiwa.
- kuharibu ushahidi dhidi yake.
- harakati polisi wa INTERPOL.
- Badala ya kusema alibambwa, pia tunaweza kusema
- alibakwa
- alinaswa
- alikahwa
- alionekana
- Kulingana na makala haya, Bwana Aisee alikuwa
- jangili
- jambazi
- mkwepuzi
- lapeli
- Kichwa mwalaka kwa makala haya ni ...
- Wajinga ndio waliwao.
- Akili nyingi huondoa maunlai
- Alive juu mgojec chini.
- Mbio za sakafuni huishia ukingoni,
Soma makala yafuatayo kisha wjibu maswali 41-50
Tarakilishi ama kompyutani kati ya teknoloji mpya ambayo inatumiwa siku hizi karibu kila mahali mathalani katika kampuni kubwakubwa, benki, masoko makubwa, viwandani, viwanja vya ndege, meli, idara za serikali, vyuo, shuleni na kadhalika. Katika shule za upili, tarakilishi ni somo ambalo. linashughulikiwa kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne na hutahiniwa katika mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne. Aidha, serikali iko katika harakati za kuwapa vipakatalishi wanafunzi wote wa darasa la kwanza katika shule zote za umma nchini. . .....
Tarakilishi imegawanyika katika sehemu mbili muhimu, programu mfumo na maunzi. Maunzi ni : nenojumlishi ambalo hutumika kwa kurejeleavifaa vyote vya kompyuta kwa mfano kichapishi, kishalekezi. kiwambo au skrini, kipanya m mashine chapishi. Programu mfumo ni neno jumlishi ambalo hurejelea programu zote zinazoweza kutumika katika kompyuta.
Vifaa vinavyotumika katika kompyuta ni vingi. Kiwambo hutumika kwa kuonyesha data ambayo inashughulikiwa, nacho kichapishi hutumika katika kuvugulia data hiyo kwa kompyuta. Kishelekezi ni kifaa ambacho huwaka kikizimika kwenye skrini nacho huashiria mahali ambapo data inayovuguliwa itaingia. Pahali pa kishalekezi panaweza kubadilishwa kwa kutumia kipanya. Kipanya ni kidude chenye mkia mithili ya panya. Baada ya kazi kukamilika nadata kuwa habari mashine chapishi huichapisha. habari hiyo kwenye karatasi ili isomwe na watu wengi iwezekanavyo, pahali penginapahali popote.
Tarakilishi ina sifa nyingi muhimu. Chombo hiki kina uwezo wa kufanya hesabu na kazi nyinginezo kwa kasi sana. Sifa nyingine ni kwamba tarakilishi huhifadhi ujumbe mwingi sana kwa matumizi ya baadaye. Maclekezo huchukuliwa na kuwekwa kwa ajili ya kufuatwana chombo hiki. Mfululizo wa maelekezo haya ndiyo huongoza kompyuta katika wajibu wake na huitwa programu ambayo huandikwa kwa letgha ya kikompyuta. Kompyuta hufuata maelekezo haya kwa kuamshwa na binadamu. Sheria hizi huwa sahili na kompyuta ina uwezo wa kuzitumia ili kufikia uamuzi wa jinsi ya kutenda
Kuwasiliana na mifumo minginc yakompyutani muhimu sana na kompyuta ina uwezo wa kufanya hivyo. Kompyuta huingizwa data ambayo huchakatwa ili kuleta maana, na uzao wa kuchakatwa huku ndio huitwa habari. Programu ni mfumo wa utaratibu ambao umeandikwa kwa lugha ya kikompyuta. Programu huiwezesha kompyuta kuchakata data na kuifanya iwe habari kwa mfano, inaweza kuongeza rumbari mbili au zaidi na kukupa jibu.
Katika kompyuta habari inaweza kuhifadhiwa katika diski ngumu au diski tepetevu. Diskingumu ni nafasi inayopatikana katika kompyuta yenyewe na inaweza kuhifadhi maktaba inzima. Diski tepetevu niile nafasi ambamo disketi huwekwa ili habari inayochakatwa ihifadhiwe kwa disketi. Disketi ni kilaa kidogo mithili ya kaseti. Nafasi hizi za kompyuta zimegawanywa katika viendesha diski kwa mfano ukitaka kuhifadhi habari yako katika diski ngumu, utatumia kiendesha diski A. Ilhali ukitaka kuhifadhi kazi yako katika diski tepetevu utatumia kiendesha diski C.
Kwa hivyo kwa muhtasvi, tunaweza kusema kuwa kompyuta ni kifaa au chombo ambacho hufanya kazi kwa kuongozwa na programu iliyohifadhiwa. Kompyuta hujiendesha yenyewe kwa kukubali na kuchakata data ili iwe habari.
- Kulingana na makala tarakilishi hutunika
- benkini, viwanjani, shuleni na idara za serikali.
- benki kubwa, shule zote, viwanjani na sokoni.
- masoko makubwa, viwanja vya ndege, benkini na vyuoni.
- mashambani, shuleni, vyuoni na nyanjani.
- Vipakatalishi vitatolewa kwa wanafunzi
- wote wa shule za umma.
- wote wa darasa la kwanza.
- wa kidato cha kwanza hadi cha nne.
- wa darasa la kwanza katika shule za ..umma.
- Mfano wa maunzi katika kompyuta ni
- programu, kiwambo, kishalekezi, kipanya.
- baobonye, mulishi, kipanya, kishalekezi.
- baobonye, programu, data, disketi ngumu.
- data, diski, tepelevy, skrini, kipanya
- Sehemu kuu za kompyuta kulingana na makala haya ni ngapi?
- Mbili
- Tatu
- Таnо
- Sita
- Umuhimu wa kompyuta ni kuwa
- hufanya kazi kwa kasi, huhifadhi ujumbe mwingi.
- hurahisisha kazi, hutumia nguzu za umeme.
- huongozwa na programu wala si mwanadamu.
- ina akili hata kuliko binadamu, ni rahisi kutumia.
- Sheria hizi huwa sahili, maana yake ni kuwa huwa
- chache
- nyingi
- rahisi
- ngumu
- Kulingana na makala haya habari hupatikaria baada ya
- kuhifadhiwa kwenye diski yoyote.
- data kuingizwa na kuchakatwa.
- kupelekwa kwa watangazaji.
- kufikia hadhira iliyolengwa: .
- Watu pia hutumia tarakilishi kuwasiliana kwa njia ya .
- kipepesi
- simutamba
- nyaraka
- barua pepe
- Lengo la kuchapisha maandishi kwenye karatasi ni kuwa itaweza
- kusomwa na yeyote.
- kusomewa mahali popote.
- kufanyiwa marekebisho.
- kusomwa kwa vyovyote.
- Kichwa ki faacho kwa makala haya ni:
- Sehemu za tarakilishi.
- Teknolojia ya kisasa.
- Manufaa ya kompyuta.
- Jinsi ya kutumia kompyuta.
INSHA
Umepewa dakika 40 kuandika insha yako.
Andika insha isiyopungua ukurasa mmoja na nusu kulingana mna mada uliyopewa.
MADHARA YA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA
Majibu
- C
- A
- B
- D
- A
- C
- D
- B
- A
- C
- B
- A
- D
- B
- C
- D
- A
- B
- D
- C
- B
- D
- A
- C
- B
- A
- C
- D
- A
- B
- C
- A
- B
- D
- A
- B
- C
- B
- D
- D
- C
- D
- B
- A
- A
- C
- B
- D
- B
- A
Kiswahili Questions and Answers KCPE 2022 Prediction Papers Set 3
Maswali
Soma vifungu vifuatavyo, Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne hapo. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.
Taifa 1 la Kenya shughuli 2 zimekwama. Ugonjwa wa Covid-19 umetetemesha kila kona ya taifa 3 . Ni vizuri kuelewa kuwa, gonjwa hili 4 nchi yetu tu 5 pia ulimwengu mzima. Hata mataifa yenye uwezo mkubwa kiteknolojia, kiuchumi na elimu ya juu 6 adha ya ugonjwa huu tandavu wa Covid19. Ili kujikinga, yafaa tunawe mikono 7 sabuni, kutoshiriki mikutano na ikiwezekana tufanye kazi 8 nyumbani.
A | B | C | D | |
1 | nzima | zima | mzima | lizima |
2 | zote | yote | lote | vyote |
3 | yetu | zetu | wetu | letu |
4 | limetisha | umetisha | halijatisha | litatisha |
5 | bali | hata | kumbe | ikiwa |
6 | haijaepuka | hayajaepuka | haujaepuka | halijaepuka |
7 | ya | na | kwa | za |
8 | katika | kwa | kwenye | kutoka |
Waswahili walisema 9 .Hali hii ilijitokeza pale Kadongo aliyekuwa na mali 10 alipoamua 11 masomo ya yatima mmoja. Uamuzi wake huo uliwashangaza wengi kuona matajiri wengi 12 kusaidia 13 kuwa wamiliki wa mali yafuatayo 14 majumba, magari, mashamba na viwanda. Ni vyema kuwa na 15 kama Kadongo.
A | B | C | D | |
9 | hiari yashinda utumwa | mtu hujikuna ajipatapo | kutoa ni moyo usambe ni utajiri | mwenye shibe hamjui mwenye njaa |
10 | madogo | ndogo | nyingi | kidogo |
11 | kuyathamini | kuthamini | kuyadhamini | kuidhamini |
12 | walidinda | walikubali | waliamini | waliamua |
13 | sembuse | ili | licha ya | kabla ya |
14 | ; | : | _ | ! |
15 | mkono mzito | mkono wa birika | mkono wa buli | mkono wazi |
Kutoka swali la 16 mpaka 30, chagua jibu lililo sahihi.
- Katika neno, ‘alisahaulika' tambua kiambishi kiwakilishi cha nafsi na cha wakati.
- ka
- li, li
- li, ka
- Ali
- Andika katika wingi:
Chuma kilichovunjika kiliwekwa nyuma ya pazia.- Vyuma vilivyovunjika viliwekwa nyuma ya mapazia.
- Chuma zilizovunjika ziliwekwa nyuma ya pazia.
- Vyuma vilivyovunjika viliwekwa nyuma ya pazia.
- Machuma yaliyovunjika yaliwekwa nyuma ya mapazia.
- Andika katika udogo:
Mzee alipiga ngoma kwenye mji.- Zee lilipiga goma kwenye jiji.
- Vizee vilipiga vigoma kwenye vijiji.
- Kizee kilipiga kigoma kwenye kijiji.
- Mzee alipiga kigoma kwenye jiji.
- Tegua kitendawili kifuatacho:
Kikigongwagongwa wanawe hutoka.- Kizimba
- Kichuguu
- Mzinga
- Chungu
- Chagua sentensi yenye kivumishi cha pekee.
- Gari lolote lililoendeshwa pasipofaa litaondolewa.
- Ndugu yangu atasafiri kesho
- Ndizi mbovu zimeliwa na ng'ombe.
- Kabati hilo ndilo lililotengenezwa
- Chagua methali yenye maana kuwa mtu anaposababisha shida huishia kuwahusisha jamaa wake.
- Mla nawe hafi nawe ila mzaliwa nawe.
- Mchumia juani hulia kivulini.
- Kikulacho ki nguoni mwako.
- Mchuma janga hula na wa kwao.
- Kanusha sentensi ifuatayo: Kujitahidi kwangu kuna manufaa.
- Kujitahidi kwangu hakuna manufaa.
- Kutojitahidi kwangu hakuna manufaa.
- Kujitahidi kwangu hakutakuwa na manufaa
- Kutojitahidi kwangu hakutakuwa na manufaa.
- Jina "shughulika" lina silabi ngapi?
- 10
- 8
- 4 D
- 6
- ‘Cherahani' ni jina katika ngeli gani?
- KI-VI
- I-ZI
- U-ZI
- LI-YA
- Ni kiungo kipi cha mwili kinachosafisha hewa?
- Ini
- Wengu
- Figo
- Pafu
- Unganisha sentensi ifuatayo: Mama alipika wali. Wali ulikuwa kwa.cah.
- Wali ulipikiwa kwa Leah ta mama.
- Mama alipikiwa wali kwa Leah
- Leah alipikiwa wali kwa mama.
- Wali ulipikwa na Leah kwa mama.
- Tambua maneno yaliyopigiwa kistari: Vitabu vizuri vitanunuliwa kesho.
- Kielezi, nomino
- Kivumishi, nomino
- Kivumishi, kielezi
- Kielezi, kiwakilishi
- Andika katika usemi wa taarifa:
"Tutapiga kambi hapa kesho," wanajeshi walisema.- Wanajeshi walisema watapiga kambi hapo kesho.
- Wanajeshi walisema walipiga kambi hapo kesho.
- Wanajeshi walisema kuwa wangepiga kambi hapo baadaye.
- Wanajeshi walisema kuwa wangepiga kambi hapo siku amiayo ingefuata.
- Mkopo usiotozwa riba huitwaje?
- Arbuni
- Chirimiri
- Kadhongo
- Karadha
- Andika kwa tarakimu.
Milioni sita, mia tisa iisini na tisa eltu, mia tiga tisini na nane.- 6,996,998
- 6,999,988
- 6,999,998
- 6,909,098
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 31 mpaka 40
Aghalabu kila wakati nilipomtembelea nyanya yangu, alikuwa akinitambia hadithi. Basi nilipomtembelea mwezi Juni, aliweza kunitambia hadithi kuhusu Mzee Hekima na bibi yake. Waliishi katika kijiji cha Madongo. Mzee Hekima alijaliwa na Mola na watoto wengi wavulikya magashi. Nao waliwalea wanao vyema kwa kuwalisha vizuri vyakula vya tumboni na kiroho. Usisahau kuwa Mzee Hekima alikuwa tajiri wa mali na moyo. Mamia ya wanakijiji waliofika kwake kumjulia hali aliwasubilia kwa vyote. Kuna wale waliopewa riziki kwa kulima shambani, wengine kufagia boma lake bora tu kila mmoja alifaidika na mkono karimu wa bwana huyu.
Kati ya watoto wake wengi, Mzee Hekim alimpenda zaidi kitindamimba na alimpendelea kwa mengi. Kutokana na hali hii kitindamimba alianza kujivuna na kuwadharau wakubwa wake. Alionyesha kiburi, unyeti na dharau. Mwishoni tabia yake ilianza kuingia ufa. Mambo yalizidi kuzorota zaidi kiasi cha mtoto huyo kuwa mbaya zaidi. Wazazi walipogundua uovu wa mtoto huyo, mambo yalikuwa yamekwisha kithiri. Baada ya kujaribu kulihali kumwongoa na kulemewa walimtupa jongoo na mti wake.
Kila mmoja aliepuka kitinda mimba huyu kama kinyamkera. Hakushirikishwa michezoni wala katika matembezi. Ajabu ni kwamba, hakurekebisha tabia yake hali aliendelea kuwa mkaidi zaidi kuliko hata mkia wa nguruwe. Mzee Hekima naye alizidi kuzeeka na kugotika kadiri siku zilivyosonga.
Mzee Hekima alianza kuwausia wanawe. Aliweka kila kitu wazi. Alisema pesa zote za banki zingegawanywa kwa wanawe wote wa kiume. Nayo mali yaliyohaki yagawatywe kulingana na umri wa kila mrithi. Jukumu la uandishi wa wosia huu lilipewa kitindamimba. Naye akawa amepata nafasi murua ya kufanya hila. Alijiandikia nafasi kubwa ya urithi wa mali ya baba yake. Hekima alipoaga dunia yule kitindarnimba aliazimia kuuza shamba lile. Hapo alimtafuta mnunuzi na kumpata Mzee Kolera. Walipalana bei lakini hakulipwa pesa taslimu ila waliandikiana mkataba
Nakumbuka siku moja, mtoto wa Mzee Johara alienda mtoni kuogelea akiwa ameandamana na marafiki zake. Mto Kingo ulijulikana kwa kuwa na mamba wengi waliowashambulia wakazi wa eneo hilo. Kwa bahati mui mwanawe Mzee Johara alishikwa mgutini na maka Alivutwa na kuelekezwa kwenye maji makuu. Watoto wenzake walipoona hivyo walipiga usiahi kwa hofu waliomba msaada. Kwa bahati nzuri, wana wawili wa yule Mzee Hekima walikuwa wakipita njia karibu na mto huo. Wakasikia mayowe na kelele. Basi bila kulimatia wakaenda haraka kuangalia kelele zilikuwa za nini.
Baada ya kufika mtoni, waliambiwa habari za mtoto yule aliyechukuliwa na mamba. Walipotupa macho walimwona mtoto yule wa Mzee Johara akizamia lulu majini. Bila chelewa chelewa, vijana hawa walivua nguo zao na wakajitosa majini na kumfuata mamba yule. Walishambulia mamba yule kwa sime zao mpaka akamwachilia mtoto yule wakamchukua na kuogelea naye hadi ufuona mato. Hapo walimpa ganga ganga za mganga Anazomwacha mgonjwa na matumaini.
Mtoto huyo alikuwa amejeruhiwa vibaya mguuni kutokana na kuumwa kwa meno ya mamba. Baada ya kumpa huduma ya kwanza, waliamua kumpeleka kwa baba yake ili kumsimulia kisa chote. Mzee Johara alifurahishwa sana na kitendo cha watoto hao na akawaombea dua ya Mola awasaidie.
Baada ya kuwapa makaribisho aliamua kuwasindikiza wana wale wawili huku yeye akielekea kumlipa kitindamimba pesa zake. Basi wote watatu waliaondoka Wana wale walienda nyumbani naye Mzee Johara akielekea kumlipa ujira wake kitindamimba. Mzee Johana aliwaomba kwa unyenyekevu waandamane naye ili wawe mashahidi wake. Vijana wale wawili walikubali bila ya wao kujua ni shamba gani lililokuwa likiuzwa.
Mzee Johara na ndugu wale wawili walipofika kwa wenyeji wake, alianza kuwaelezea jinsi walivyopatana bei ya shamba. Ndugu wale wawili walishtuka sana na kukasirika. Papo hapo wakamweleza Mzee Johara kisa chote kuanzia mwanzo hadi mwisho. Mzee Johara kusikia hivyo alighairi kununua shamba hilo. Ujanja wa kitindamimba kikagonga mwamba.
- Chagua kauli isiyo ya kweli kulingana na aya ya kwanza
- Mzee Hekima na mkewe walijaliwa watoto wa kike na kiume.
- Mzee Hekima na familia yake walikuwa wacha Mungu.
- Wavulana walikuwa wengi kuliko wasichana.
- Mzee Hekima aliweza kutoa mwongozo mzuri wa familia yake.
- Mzee Hekima alikuwa tajiri wa moyo kwa kuwa
- Mamia ya wakazi walifika kwake kumlilia hali.
- Alikuwa na mashamba makubwa yaliyohitaji usaidizi wa wanakijiji.
- Nyumbani kwake kulishiba watu walioenda kwake ili kufagia na wengine kulima.
- Aliwafaa wengi ambao hawakujiweza kiuchumi.
- Wazazi walipogundua uovu wa mtoto huyo, mambo yalikuwa yamekwisha kithiri.Ni methali gani inayokubaliana na kauli hii?
- Chelewa chelewa utampata mwana si wako
- Asiyesikia la mkuu huvunjika guu.
- Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.
- Mwana wa nyoka ni nyoka.
- Kitindamimba aliharibika
- kwa kuwa yeye ndiye alikuwa mtoto wa mwisho kuzaliwa.
- kwa kupendelewa na baba yake kuliko watoto wale wengine.
- kwa kupewa majukumu mengi yakiwemo yale ya ugavi wa shamba.
- kutokana na vijana wa hirimu yake.
- Zifuatazo ni sifa za Mzee Hekima kulingana na aya ya nne ila
- alikuwa mwenye busara.
- alikuwa mwenye ubaguzi.
- alikuwa mwenye uwazi.
- alikuwa mwenye fitina.
- Kitinda mimba kulingana na kifungu, alifaa
- kupata sehemu ndogo kabisa miongoni mwa warithi.
- kupata sehemu kubwa kabisa miongoni mwa warithi.
- kuliuza shamba lake baada ya kugawiwa.
- Kumtafuta mnunuzi wa shamba lao bila kuwahusisha ndugu zake.
- Ujasiri wa ndugu zake kitindamimba unaonekana pale
- walipompeleka ndugu yao kortini kwa njama ya kuliuza shamba lao.
- walipoandamana na Mzee Johara hadi kwao kushuhudia ununuzi na uuzaji wa shamba lao.
- walipokabiliana na mamba na kumwokoa mtoto wa Mzee Johara.
- walipomkataza Mzee Johara kulinunua shamba lao bila idhini ya wote.
- Ni sadfa kuwa
- Mzee Johara aliwaomba wanawe Mzee Hekima kushuhudia ununuzi wa shamba lao.
- marafiki wa mwanawe Mzee Johara hawakujua kuogelea.
- wana wa Mzee Hekima hawakuwahi kuacha sime kila walipotembea.
- kitindamimba hakuwa amelipwa pesa na badala yake waliandikiana mkataba.
- Ni msemo gani unaoonyesha Mzee Hekima alichoshwa na kitindamimba?
- Mzee Hekima alimpendelea kitindamimba kuliko wote.
- Mzee Hekima alimpa dhima ya kuandika wosia.
- Mzee Hekima aliamua kugawa mali yake kulingana na umri wa kila mrithi.
- Mzee Hekima aliamua kumtupa jongoo na mti wake.
- Sime ni
- upanga wenye makali kuwili.
- kiboko chenye ncha ya chuma.
- miundi inayotumiwa kulimia.
- ni bastola ya kufyatua risasi.
Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali 41 mpaka 50.
Maisha ya binadamu huimarika kutokana na urafiki. Urafiki hufanya watu wanaopendana kuwa na mvuto fulani ambao huwapa kiu ya kutaka kuonana mara kwa mara. Umbali kwao huwa si chochote si lolote. Watafanya juu chini ili waweze kuwasiliana hata kama ni kwa kupigiana simu, kuandikiana nyaraka au hata kutembea kilomita nyingi mradi tu wakutane.
Manufaa ya urafiki ni gani? Nia kuu ya urafiki ni kuondoleana ukiwa, kuliwazana, kubadilishana fikira na kusaidiana wakati wa shida. Pasi na urafiki duniani kungejaa madhila, uhasama, zahama na maovu mengine ya kukiriha moyo.
Urafiki bora ni ule wa kujuliana hali, kufaana wakati wa dhiki, urafiki wa kupigiwa mfano yaani ule wa kufa kuzikana. Hata hivyo urafiki huu umeadimika kama milango ya pikipiki. Ni nadra na adimu kumpata rafiki shakiki. Kila mtu sasa ameanza tu kuamba ngoma akivuta kwake. Ya mwenzake hayamghasi, ni kanda la usufi ati.
Kile ninachojaribu kusema ni kuwa, urafiki mwingi ni ule wa juu juu. Ule wa nipe nikupe. Iwapo wewe ni maskini, ole wako! Watakwambia kuwa mkono mtupu haurambwi na utapewa kisogo. Ukiwa tajiri pia huna bahati. Utaandamwa kama nzi na kugandwa kama kupe na wanaotaka kikalia mrija. Siku ya kuonyeshwa mlango kazini watakuhepa labda uauniwe na ndugu yako
Kulonga mithaki urafiki mwingi ni ule wa idumakawili Ni ule wa kulana kivuli. Wale wanaojitapa hadharani kuwa marafiki zako shakiki ukiwapa siri, kesho utazisikia barazani. Ulimthamini lakini yeye hafai ni mfano wa kikulacho ki nguoni mwako. Ni makauleni wakubwa. Ni vycina kila mmoja ajue kuwa, ule urafiki wa zamani wa kufaana kwa jua na la mvua umezikwa katika kaburi la liliwala.
Kinyume na vile watu wengi wanavyodhaniás urafiki unahitaji uvumilivu, uaminifu, ukarimu, upendo, usamehevu na kujitolea mhanga kama kukuahatarishaye maisha yake ili kumwokoa kifaranga.
Je, urafiki una faida? Ndiyo. Kumbuka ukiwa na marafiki huwezi kuteseka sana. Wahenga walisema kuwa mtu ni watu na hakuna mtu anayeweza kujitosheleza. Majanga yapo. Mengine makubwa yanayozidi uwezo wa mtu binafsi. Chukulia kwa mfano shughuli za mazishi. Utachimbaje kaburi na ubebe jeneza peke yako. Hapo ndipo utahitaji marafiki.
Tujue kuwa tuko pia na urafiki wa kuharibiana tabia. Kwa mfano watu wasio na msimamo kimaisha kazi yao ni kufuata wengine kama bendera. Tumewaona wengi wakijitoa kikaangoni na kujiingiza motoni bila kujali. Hawa sana sana ni wale ambao huwa hawaambiliki wala hawasemezeki. Hata wakiambiwa wasitembee na watu waovu kwa kuwa samaki mmoja akioza na mtungo pia huwa hawasikii. Huonyesha kiburi na unyeti mwishowe huishia kujipalia makaa.
Tamu ikizidi sana huwa sumu. Nao-urafiki ukizidi sana wakati mwingi huwa na madhara yake. Unajikuta kwa kuwa ati mtu ni rafiki yako, unaamua kuchukua hatua bila hata kumhusisha. Kumbe uamuzi uliochukua ni sumu kwake.
- Ni wazi kuwa
- kama si urafiki watu hawangekuwa wakionan
- pesa haziwezi kuwa kizingiti kwa watu ambac wanataka kuonana.
- urafiki huumua maisha ya binadamu.
- urafiki umeanza juzi wakati wa teknolojia mpya.
- Lipi si lengo la urafiki?
- Kufarijiana.
- Kubadilishana mawazo.
- Kufaana wakati wa dhiki.
- Kukirihisha moyo.
- Aya ya tatu inaonyesha kuwa
- hakuna urafiki wa kweli kokote dunianti.
- marafiki wengi ni wanafiki,
- lengo la urafiki wowote ni kudhuriana.
- mzigo wa mwenzio ni kanda la usuf
- Chagua methali mwafaka inayolenga mwis wa aya ya nne.
- Mla nawe hafi nawe ila mzaliwa nawe.
- Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki.
- Nzi kufa juu ya kidonda si hasara
- Ndugu ni kufaana si kufanana.
- Yaonekana kuwa
- urafiki wa leo ni bora kuliko ule wa zamani
- urafiki wa zamani ulikuwa bora kuliko wa leo.
- urafiki wa leo umeathiriwa pakubwa na urafiki wa zamani.
- hakuna tofauti ya urafiki wa zamani na ule wa leo.
- Taja tamathali mbili zinazojitokeza katika kauli hii: Kujitolea mhanga kama kuku ahatarishaye maisha yake ili kumwokoa kifaranga.
- Chuku, tashbihi
- Tashhisi, kinaya
- Naha, istiara
- Nahau, tashbihi
- Mwandishi ametumia mfano wa mazishi
- ili kuonyesha hatima ya kila mtu ni mauti.
- kwa kuwa ni sherehe ambazo huleta majonzi katika jamii.
- kuonyesha kuwa kuna haja ya kusaidiana wakati wa shida.
- kionyesha ubora na thamani ya urafiki.
- Aya ya inatuonyesha kuwa,
- kuna watu wanaotumia urafiki kwa manufaa yao ya kiuchumi,
- urafiki wa dhati upo na unafaa kuigwa na wote
- wengi wa marafiki tulio nao wametufaidi sana katika shughuli zetu za kila siku,
- hakuna msingi wa urafiki mwema.
- Kujipalia makaa ina maana ya
- kujinufaisha wao pekee
- kujiletea matatizo.
- kujisalimisha kwa kushindwa.
- kukosana na watu wote.
- Aya ya mwisho inaonyeshe kuwa
- jambo zuri linaweza kuleta athari mbaya.
- rafiki ana uwezo wa kujua shida ya mwenza.
- hatufai kuwa na marafiki wasiojua hisia zetu.
- ni vigumu sana rafiki kujua yale yanayomsumbua mwenzake.
Majibu
- B
- A
- D
- C
- A
- B
- C
- D
- C
- D
- C
- A
- C
- B
- D
- D
- A
- C
- B
- A
- D
- B
- C
- A
- D
- A
- C
- D
- D
- C
- C
- D
- A
- B
- D
- A
- C
- A
- D
- A
- C
- D
- B
- A
- B
- D
- D
- A
- B
- A
Kiswahili Questions and Answers - KCPE 2022 Prediction Papers Set 2
Maswali
Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne hapo. Jaza kila pengo kwa kuchagua jawabu lifaalo zaidi.
Serikali 1 wananchi wote kutunza afya 2 . Wananchi wenye afya 3 kutekeleza shughuli mbalimbali za kuindeleza nchi kiuchumi 4 watapunguzia serikali gharama ya kushughulikia matibabu. Hata hivyo, 5 . Kufanikiwa kwa juhudi za serikali 6 kwa kiasi kikubwa jinsi wananchi wenyewe 7 kujitunza.
Miongoni mwa 8 iliyowekwa ni bima ya afya inayohakikisha kuwa wananchi wanapata matibabu bila malipo.
A | B | C | D | |
1 | ingekuwa iliwahimiza | inakuwa ikiwahimiza | imekuwa ikiwahimiza | ilikuwa ingewahimiza |
2 | zao | zenu | zake | yako |
3 | wanawez tu | hawawezi tu | hawawezi kamwe | wakaweza kamwe |
4 | kwani pia | bali pia | mbali na | ilhali |
5 | hakuna mchele ukosao ndume | kitanda usichokilalia hujui kunguni wake | penye miti hapana wajenzi | ukibebwa usilevyelevye miguu |
6 | inategemea | zinategemea | kunategemea | watategemea |
7 | wanavyojitahidi | wanaojitahidi | wanayojitahidi | wanapojitahidi |
8 | hatua | mikakati | lengo | mambo |
Ziara yetu katika eneo la Bonde la Ufa 9 sana. Tulijionea 10 ya kupendeza kama vile Kasoko ya Long’onot, Ziwa Naivasha na ndege wa ziwani waitwao 11 . Walimu wetu 12 kwamba haya ni 13 muhimu sana kwa uchumi wetu. Huko Olkaria, 14 kuona umeme ukizalishwa kwa nguvu za mvuke 15 ardhini.
A | B | C | D | |
9 | ilifaa | ilifana | ilifaana | ilifanana |
10 | mandari | mazingara | mandhari | maajabu |
11 | chozi | nondo | bundi | heroe |
12 | walitujuza | wealitujulia | walitujulisha | waliwajulisha |
13 | rasilimali | malighafi | mazigazi | maliasili |
14 | tunaajabia | tukiajabia | tulijiabia | tungeajabia |
15 | zitokazo | itokayo | zitokapo | utokao |
Kuanzia nambari 16 mpaka 30, jibu kulingana na maagizo uliyopewa.
- Chagua sentensi yenye kiwakilishi cha nafsi ya tatu.
- Wanaenda mashambani mwao.
- Nilikipata kijiko pale.
- Unataka nikusaidie vipi?
- Tutaanza kusoma moja kwa moja.
- Bainisha matumizi mwafaka ya ritifaa.
- Kuonyesha kuwa kuna orodha inayofuata.
- Kutambulisha sauti inayotamkiwa puani.
- Kuonyesha sauti ambayo ni ghuna.
- Kutambulisha maneno halisi yaliyotamkwa.
- Ni orodha ipi iliyo na kasoro?
- Nyigu, panzi, kumbikumbi.
- Kizibao, kanzu, bwelasuti
- Kitovu, shavu, kisigino.
- Ujira, ubwete, pete.
- Andika sentensi ifuatayo katika kauli ya kutendwa.
Mtoto alikula chakula akashiba.- Mtoto aliliwa chakula akashiba.
- Chakula kililiwa mtoto akashiba.
- Chakula kililiwa na mtoto akashiba.
- Mtoto alilishwa chakula akashiba.
- Tambulisha kihusishi katika sentensi ifuatayo.
Mtama wote ulianikwa nje ya nyumba ile.- ile
- nje ya
- wote
- nyumba ile
- Tamko lipi hutolewa na mtu anayetarajia kutamka maneno ambayo huenda yakaudhi hadhira yake?
- Ashakum
- Simile
- Samahani
- Pole
- Tumia kiulizi kifaacho zaidi.
Musila aliumia mguu_____?- ipi
- mgani
- mbona
- lini
- Bainisha sentensi iliyo na ‘kwa’ kuonyesha sababu.
- Alitembea kwa madaha ya tausi.
- Wazee kwa vijana walifika hapo.
- Fundi alilipanda jengo kwa ngazi.
- Ulikemewa kwa utovu wa nidhamu.
- Kanusha sentensi ifuatayo.
Mgeni akiondoka tutaanza shughuli nyingine.- Mgeni asipoondoka hatutaanza shughuli nyingine.
- Mgeni akiondoka hatutaanza shughuli nyingine.
- Mgeni asipoondoka tutaanza shughuli nyingine.
- Mgeni hataondoka wala hatutaanza shughuli nyingine.
- Mahali jikoni penye bomba la kuoshea vyombo ni
- dohani
- karo
- kichaga
- shubaka.
- Chagua jozi iliyo na methali zenye maana moja.
- Aliye kando haangukiwi na mti.
- Usipoziba ufa utajenga ukuta.
- Cheche ya moto huchoma msitu.
- Tone na tone huwa mchirizi.
- (ii) na (iii)
- (i) na (iv)
- (iii) na (iv)
- (ii) na (iv)
- Korija moja hujumulisha vitu vingapi?
- Viwili
- Kumi na viwili
- Ishirini
- Mia.
- Chagua jibu sahihi.
- Mjusi alituuzia mchuzi mtamu.
- Doa yao haikuwa na doa hata kidogo.
- Alikaanga kanga vizuri tukafurahia.
- Danda alidadia lori lilipopita hapa.
- Shairi lenye mishororo miwili katika kila ubeti ni ______ ilhali shairi la majibizano huitwa _______.
- tarbia, utenzi
- tathlitha, ngonjera
- mizani, utenzi
- tathnia, ngonjera
- Ni sentensi gani iliyo na kiigizi sahihi?
- Aisee! Mambo usemayo ni ya kitoto.
- Hewala! Hilo usemalo haliwezekani.
- Oiyee! Tumefunga bao la ushindi.
- Kefule! Nitakusaidia utakavyo.
Yasome makala yafuatayo kisha ujibu maswali 31- 40.
Ulemavu ni hali ya kuwa na kasoro katika viungo vya mwili. Upungufu huu huchangiwa na mambo mbalimbali. Pengine mtu anaweza kushindwa kutekeleza baadhi ya shughuli za kawaida kama vile kuongea, kutangamana na wengine, kusoma au hata kujitegemea kwa mambo mbalimbali. Mara nyingi ulemavu huwa wa kudumu japo kuna ule uwezao kuisha baada ya kipindi fulani.
Baadhi ya watu hupata ulemavu kutokana na kasoro wakati wa kufanyika kuwa motto tumboni. Huenda mzazi akajifungua salama lakini baadaye akagundua kuwa mtoto wake amekosa kiungo fulani. Pia, mtoto anaweza kuendelea kukua bila kugunduliwa lakini mabadiliko yanayotarajiwa katika vipindi mbalimbali vya ukuaji yakakosekana. Hata hivyo, wakati mwingine mabadiliko yanaweza kuchelewa lakini mwishowe yakatokea tu.
Mbali na hayo, binadamu anapotangamana na mazingira yake, anaweza kuambulia ulemavu kutokana na majeraha ya viungo, ya ubongo au uti wa mgongo. Magonjwa kama vile kisukari na shinikizo la damu pia yanaweza kuchangia ulemavu. Baadhi ya watu waliokuwa wazima hivi majuzi tu wameambulia ulemavu kupitia ajali mablimbali. Ni vyema mtu ajizatiti kuepuka hali yoyote inayoweza kuhatarisha afya yake.
Unaweza kufikiria kuhusu siku uliyoteleza mlipokuwa mkicheza na wenzako, ukateguka mguu au mkono? Pengine unakumbuka namna ulivyoteseka kwa kushindwa kujifanyia mambo muhimu kama vile kuoga, kutembea kuenda haja au hata kula. Yamkini utaniambia kuwa lililokuuma zaidi ya uchungu wa jeraha hilo hilo ni kule kukosa fursa katika shughuli za kila siku. Hata wenzako walipokuzuru kukujulia hali, ulifurahi lakini ukavaliwa na ukiwa pindi tu walipokupa mgongo. Walemavu wengi hupitia hali kama hizi aushi yao yote.
Wakati mwingine watu huzitonesha nyoyo za ulemavu bila kujali hisia zao. Utamsikia mtu kwa mfano akisema, ‘Niitie huyo chongo nimtume’ au ‘Msaidieni huyo kiwete jamani.’ Sharti ieleweke kwamba walemavu ni binadamu wa kawaida na kila mtu anao ulemavu wa aina fulani. Hakuna aliye na wepesi wa kufanya kila kitu. Hata kuwa na moyo wa harara ni ulemavu mkubwa. Tukumbuke ya wahenga kuwa hucheka kovu asiyefikwa na jeraha. Watu hawa wana majina yao. Tusiwadhalilishe kwa kuwarejelea kwa maumbile yao.
Wapo wazazi wanaowaficha wana wao walemavu na hata kukosa kuwapeleka shuleni. Huu ni ukandamizaji wa hali ya juu. Mtu yeyote akipata nafasi ya kutangamana na mazingira yake ipasavyo, bila shaka atabuni njia ya kutekeleza shughuli zake kadri awezavyo. Walemavu wengine wameinukia kuwa watu wa kutegemewa sana na jamii, hata kiasi cha kuwafikia kuwafaa wale wasio na uatilifu wowote.
Kila binadamu ana haki zake. Ni vyema jamii ikubali kuwa waatilifu ni binadamu wanaohitaji huduma kama wengine wowote. Haki zao zitambuliwe na maumbile yasiwe kigezo cha kuwadhalilisha kwa vyovyote vile.
- Chagua maelezo sahihi kulingana na aya ya kwanza.
- Ulemavu ni hali ya mtu kushindwa kufanya jambo.
- Huenda mlemavu akashindwa kujihudumia ipasavyo.
- Ulemavu wowote ule huwa ni hali ya kudumu.
- Walemavu hushindwa kabisa kutekeleza shughuli muhimu maishani.
- Kipi si kiini cha ulemavu?
- Kuhusika katika ajali.
- Kasoro za kimaumbile.
- Mwili kukosa kuendelea ipasavyo.
- Uchelewaji kaitika kukua
- Waliokuwa wazima kulingana na makala haya ni wale
- ambao kasoro zao hazikuwa zimegunduliwa
- ambao si watoto kwani wamekomaa
- wasiokuwa na kasoro zozote za kimaumbile
- waliofikiria kuwa hawawezi kuathirika.
- Kulingana na aya ya nne
- kuteleza kwa msimulizi kulimfanya mlemavu
- mwandishi ana uhakika kuwa msomaji aliteleza michezoni
- watoto waliopata majeraha hawaogi wala kutembea
- kushindwa kujumuika na wengine huathiri hisia zaidi.
- Ni hali gani ambazo mwandishi anasema walemavu wengi hupitia auishi yote?
- Hali ya upweke na kunyimwa nafasi ya kushiriki.
- Ukiwa baada ya marafiki waliozuru kuaga haraka
- Majeraha ya viungo na kulala siku nzima.
- Kupuuzwa na marafiki na kuhitajika kutoa msaada.
- Si vizuri kuwataja watu kulingana na kasoro zao kwani
- huku ni kuwaumiza hisia zao
- wana majina yanayojulikana na wote
- huenda wasijue maana ya majina hayo
- hata sisi ni walemavu kama wao.
- ‘Chongo’ kulingana na makala haya ni
- mtu ambaye mboni za macho yake zimeelekea kombo
- mtu asiye na uwezo wa kuona kabisa
- mtu ambaye jicho lake moja limepofuka
- mtu mwenye nundu mgongoni pake.
- Wazazi huwanyima watoto wao walemavu haki zipi?
- Elimu na malezi.
- Utangamano na makazi.
- Mapenzi na makazi.
- Shule na hiari.
- Maana ya kuwa na ‘moyo wa harara’ ni
- kushtuliwa na mambo madogo
- hali ya kukasirika upesi
- kutumia maneno makali kwa wengine
- kuwa na maradhi ya moyo.
- Kichwa kifaacho zaidi kwa makala haya ni
- Haki za walemavu.
- Vyanzo vya ulemavu.
- Aina mbalimbali za ulemavu.
- Ukarimu wa malemavu.
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 41 – 50.
Daktari Maluki alikaa katika chumba cha matibabu akijisikilizia muziki kwenye rukono yake. Alikuwa amefika kazini saa chache zilizopita. Akili zake zilikuwa mbali kidogo.Aliwaza kuhusu kima cha pesa na muda aliotumia kusomea taaluma hii. Akalinganisha na ‘ mshahara tonge’ aliopata kama alivyouita yeye, japo mshahara wenyewe ulikuwa wa kuliliwa ngoa na akina yahe. Aliona kweli kwamba dunia haina huruma. Alipiga darubini na kuwaona jinsi viongozi wakuu walivyojilimbikizia donge nono licha ya kuwa walifanya kazi kwa muda mfupi sana.
Baada ya kutia na kutoa, aliibuka na uamuzi aliohisi kwamba ungemfaa bila ‘kuwaathiri sana’ waliosaka huduma yake. Kwanza, yeyote aliyesaka huduma yake angelipa kifunguamkoba cha shilingi elfu mbili ili apate nafasi ya kumwona. Maadamu, alikuwa daktari mkuu, uamuzi wake haukupingwa sana pale hospitalini. Si kila mmoja anafahamu vyema kuwa mkono mtupu haurambwi? Tena yeye Daktari Maluki hakumwalika yeyote kuja kumwona. Si wanaletwa na shida zao tena kwa hiari yao?
Mradi huu ulifanikiwa sana na kumfurahisha Daktari Maluki. Sasa kipaji kilionekana kumnawiri wakati wote akiwa kazini. Aidha, aliiraukia kazi mapema sana ili aweze kuwahudumia wagonjwa wengi kadri ilivyowezekana. Kufanikiwa kwa mradi huu kulimfanya azuke na mwingine. Alifungua duka kubwa la dawa mkabala wa hospitali ile. Wagonjwa waliokuwa wakija kwa matibabu walikuwa wakipewa dawa dukani pale. Serikali ndiyo iliyolaumiwa kwa kukosa kuleta dawa hospitalini. Lakini sikwambii kuwa dawa zizo hizo zilizokuwa halali na haki yao ndizo walizozilipia pale dukani.
Daima dawamu mbio za sakafuni huishia ukingoni. Siku moja, wasamaria wema walikuja na mgonjwa aliyehusika katika ajali ya barabarani. Alikuwa akivunja damu sana hivyo basi alihitaji kushughulikiwa kwa haraka. Daktari aliitwa lakini hakubanduka pale kitini mwake. Alitaka kujua ni nani angegharamia matibabu. Wasamaria wema hawakutaka kufanya hiyo maadamu hawakuhusiana na mwele yule kwa damu wala usaha. Basi mgonjwa akaachwa kuendelea kuvunja damu.
Watu waliokuwepo walishauriana na kuafikiana kuchanga angaa kifungua mkoba ili mgonjwa ahudumiwe. Hata zilipotosha walimwendea mgonjwa ili wampeleke kwa daktari. Lo! Walishangaa walipogundua kuwa mwili wake ulikuwa u baridi tayari. Daktari alitia fulusi kibindoni na kuagiza aletwe. Alipompimapima, aligundua kuwa amekata kamba. Hata hivyo, alivutiwa na jingine. Ni uso wa mtu aliyemfahamu sana. ‘Haiwezekani......mama........ mam....’ Daktari akazirai.
Kumbe mamaye Maluki alikuwa amekuja kumzuru mwanawe mjini alipopigwa dafrau na gari kabla ya kufika kwa mwanawe. Sasa alikuwa kaenda jongomeo baada ya kunyimwa huduma na mwanawe aliyemzaa, akamlea na kumsomesha kwa shida. Ama kweli, kigumba ni kwa nguruwe, kwa binadamu ki uchungu.
- Kulingana na aya ya kwanza, Daktari Maluki
- aliketi ofisini kusikiliza muziki kwenye redio
- alizingatia sana muziki wa rukono yake
- hakuwa amekaa sana baada ya kufika kazini
- hakuwa na hamu ya kuwahudumia wagonjwa.
- Kwa nini Daktari Maluki alijipata akiwaza?
- Alihisi kuwa malipo yake hayakulingana na hadhi yake kikazi.
- Alitumia pesa na muda mrefu kusoma kuliko wenzake.
- Mshahara wake ulikuwa ukililiwa ngoa na kina yakhe.
- Alitaka kuwa kiongozi wa serikali apate donge nono.
- Kulingana na aya ya pili
- waliotafuta msaada kwa daktari hawakuathirika kwa uamuzi wake
- nafasi ya Daktari kazini iliufanya uamuzi wake kufuatwa bila swali
- mtu akiwa na shida hafai kupewa hiari ya kuwa na usemi wowote
- mtu akitaka msaada bila kutoa chochote hafai kuhudumiwa popote.
- Kunawiri kwa kipaji cha Daktari Maluki ni ishara kuwa
- watu sasa wameanza kuja kwake kwa hiari yao
- kuongezewa mshahara kazini kumempa raha aliyotamani
- huduma anayotoa kwa wateja ni bora kuliko awali
- shughuli ya kifisadi aliyoanza inampa kipato alichotamani.
- Si kweli kusema kuwa
- Daktari alipofika kazini mapema aliwajali wagonjwa
- Daktari alianzisha biashara karibu na hospitali aliyofanyia kazi
- watu walilipia ada kwa sababu ya kukosa hiari
- wagonjwa walipata baadhi ya dawa pale hospitalini.
- Chagua sifa za Daktari Maluki kulingana na makala haya.
- Mzingatifu na mkatili.
- Fisadi, asiye na utu.
- Katili na mwenye bidii kazini.
- Mlafi na anayetafuta kutambuliwa.
- Kwa nini Daktari hakubanduka kitini alipoitiwa mgonjwa?
- Alikuwa amezama mawazoni.
- Hakujua kuwa mgonjwa alikuwa hatarini.
- Hakuwa na hamu ya kazi siku ile.
- Mgonjwa hakuwa amelipiwa ada iliyohitajika.
- ‘Hawakuhusiana na mwele yule kwa damu wala usaha’ ina maana kuwa
- wasamaria wema hawakujuana na mgonjwa
- daktari hakutaka kujihusisha na Mjeruhiwa
- wasaidizi hawakuwa wa nasaba ya mjeruhiwa
- wasamaria wema hawakuwa na uhusiano na Daktari.
- Kilichochangia kifo cha majeruhi ni
- kutelekezwa
- kukosa kufungua mkoba
- kuchelewa kufika hospitalini
- kupewa matibabu yasiyofaa.
- Aya ya mwisho imetufahamisha kuwa
- mtu anapoadhibiwa kwa makosa yake hafai kuhurumiwa
- mtu akitendewa dhuluma atendeazo wengine hawazii matendo yake
- mtu anapotendewa uovu uo huo aliozoea huona uchungu sana
- Mtu anaweza kufurahi anapowadhulumu wengine lakini adhulumiwapo hivyo huona uchungu.
INSHA
Umepewa dakika 40 kuandika insha yako.
Andika insha isiyopungua ukurasa mmoja na nusu ukifuata maagizo uliyopewa.
Umechaguliwa kutoa hotuba kwa niaba ya wanafunzi wenzako siku ya kutoa tuzo kwa wanafunzi waliotia for a katika tofauti tofauti. Andika hotuba yako.
Majibu
- C
- A
- B
- B
- D
- C
- A
- B
- B
- C
- D
- A
- D
- C
- D
- A
- B
- D
- C
- B
- A
- D
- D
- A
- B
- A
- C
- C
- D
- C
- A
- D
- C
- D
- A
- A
- C
- B
- B
- A
- C
- A
- B
- D
- A
- B
- D
- C
- A
- D
Kiswahili Questions and Answers - KCPE 2022 Prediction Papers Set 1
Maswali
Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi umepewa mujibu manne hapo. Jaza pengo kwa kuchagua jawabu lifaalo zaidi.
Ni vigumu kwa jamii yoyote kupiga hatua 1 kuwawekea vijana msingi 2 wa malezi. na afya, yaani 3 ,watoto hupewa chanjo ya kuzuia maradhi ya 4 Njia nyingine ni kuanzisha vyuo vya kiufundi vitakavyowapa 5 za kujiendeleza. 6 , utoaji wa elimu bila malipo 7 fursa ya kusomea taaluma mbalimbali pamoja na 8 vipawa vyao. Jamii 9 watambua vijana huwa haina matarajio mema ya uongozi wa baadaye.
A | B | C | D | |
1 | minghairi ya | licha ya | mithili ya | fauka ya |
2 | nzuri | mbora | jema | thabiti |
3 | staha | rai | ari | hulka |
4 | malaria, pumu, waba | kichocho, tauni, kifafa | pepopunda, surua, kupooza | mafua, malaria, ukambi |
5 | stadi | maarifa | ujuzi | hekima |
6 | Ama | Lau | Ilhali | Halikadhalika |
7 | inawapa | kumewapa | umewapa | tunawapa |
8 | kuyakuza | kurikuza | kuikuza | kuwakuza |
9 | wakikoza | mkikosa | likikosa | ikikosa |
Moyo wa Amina ulijaa 10 Machozi yalijikusanya kwenye macho yake 11 matone makubwa makubwa na 12 daftari alilokuwa akiliandikia. Hata hakutanabahi mwalimu 13 na kusimama mbele yake. Mwalimu akamwita ofisini kumsaili na kumliwaza. Kumbe wavyele wake walikuwa 14 ya kumwoza! Ndipo mwalimu akamtafutia mhisani wa kuyadhamini masomo yake, Ama kweli 15
A | B | C | D | |
10 | machozi | simanzi | nyemi | ukiwa |
11 | yakamdondoka | yakamchuruzika | yakatiririka | yakambubujika |
12 | kuilowesha | kuyalovya | kulowekana | kulilovya |
13 | alivyoingia | alioingia | alipoingia | akaingia |
14 | wamekula nyama | wamepika majungu | wameshika miko | wametia mrija |
15 | mwana akibebwa hutazama kisogo cha nina | Mungu akiziba hapa huzibua pale | mpanda farasi wawili hupasuka msamba | mla nawe hafi nawe ila mzaliwa nawe |
Kuanzia nambari 16 mpaka 30, chagua jibu Ifaalo zaidi
- Chagua kauli ya kutendewa ya:
Titu alichukua pete ya zawadi- Pete ya Zawadi ilichukuliwa na Tatu.
- Pete ilichukuliwa Tutu kwa Zawadi.
- Zawadi alichukuliwa pete na Tatu.
- Zawadi alichukuliwa pete kwa Tatu.
- Maneno yafuatayo yatafuatana vipi katika kamusi?
- mchuzi
- mchumba
- muhogo
- muhina
- (ii), (i), (iv), (iii)
- (iv), (iii), (ii),(i)
- (i). (i). (iii), (iv)
- (ii),(ii), (iv), (iii)
- Chagua sentensi yenye kwa inayoonyesha’ pamoja na’
- Seme alipendwa kwa heshima yake.
- Tulienda moja kwa moja hadi uwanjani.
- Wake kwa waume walishirikisherehe hiyo.
- Nuru alipata alama saba kwa kumi.
- Mtu mwenye ujuzi wa kufua visu ni
- mjume
- mjumu
- mhandisi
- mhazili
- Chagua kukanusha kwa
Kocha alikuwa akiwapongeza na kuwahimiza wachezaji- Kocha hakuwa akiwapongeza kwa kuwahimiza wachezaji.
- Kocha alikuwa hawapongezi bila kuwahimiza wachezaji.
- Kocha alikuwa hawapongezi ila kuwahimiza wachezaji
- Kocha hakuwa akiwapongeza wala kuwahimiza wachezaji
- Maneno yaliyopigiwa mstarini
Vijana hawa walifika mapema lakini wale walichelewa- nomino, kielezi, kiunganishi, kiwakilishi
- kivumishi,Kielezi, kiunganishi, kiwakilishi
- kiwakilishi, kivumishi, kielezi, kivumishi
- kivumishi, kiwakilishi, kiunganishi,kivumishi
- Chagua jibu lenye maneno yasiyoambatanishwa ipasavyo.
- kikuku - mguu
- kipini - pua
- ushanga-shingo
- kikuba-kiwiko
- Ni jibu lipi lenye nomino iliyoundwa kutokana na kitenzi?
- nyweka nywesha
- ogopa - ogofya
- saka - usasi
- arnini-aminifu
- Onyesha sentensi iliyo katika hali ya mazoea
- Magari ya usafiri wa umma hayupiti hapa
- Mvua ya masika haijaanza kunyesha
- Mto ukifurika hawatavuka
- Vazi hilo halikushonwa vizuri.
- Andika wingi wa sentensi ifuatayo
Baharia huyu amevaa kotizuri.- Baharia hawa wamevaa makoti nzuri
- Mabaharia hawa wamevaa koti zuri
- Mabaharia hawa wamevaa makoti mazuri
- Baharia hawa wamevaa makoti mazuri
- Sogora kwa ngoma ni kama kwa mapambo
- mhuri
- kaimu
- mjumu
- sonara
- Ukubwa wa sentensi:
Mtoto huyu hataweza kukibeba kikapu hicho ni- Toto hilo halitaweza kulibeba kapu hili.
- Jitoto hili halitaweza kulibeba kikapu hicho.
- Toto hili halitaweza kulibeba kapu hilo.
- Kitoto hiki hakitaweza kulibeba kapu hilo
- Ni jibu lipi lenye maneno ya aina moja?
- ua, embe, chelewa
- andikiwa, ruka, chezesha
- dawati, agiza, kaka
- waka, salama, tena
- Neno mkadamu lina silabi ngapi?
- 4
- 3
- 7
- 6
- Teka alikabiliwa na shida nyingi maishani. Akajitahidi kuzisuluhisha na hatimaye hali yake ikaimarika. Methali inayojumuisha ujumbe huu ni
- Mbio za sakafuni huishia ukingoni.
- Achanikaye kwenye mpini hafi njaa.
- Mtembezi hula miguu yake.
- Kinga na kinga ndipo moto uwakapo.
Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali kuanzia 31 mpaka 40
Amani ni hali ya utulivu ambayo hupatikana pasipo na vita wala machafuko yoyote. Mara nyingi hali hii hupatikana pasipo na gharama yoyote. Hili hasa ndilo linalowafanya wengi kutotilia maanani umuhimu wa amani. Lakini kama walivyosema wahenga, asiyejua thamani ya mwangaza aingie gizani. Ushahidi kuhusu matokeo ya ukosefu wa amani umeenea vururu katika jambu nyingi.
Yamkini nikikuuliza kama unajua umuhimu wa amani utakuwa mwepesi wa kusema ndio. Lakini pengine ukituama na kuwazia matukio mbalimbali yaliyowahi kutokea karibu nawe, au hata kwa mchango wako binafsi, utagundua kuwa umewahi kuchangia kuvuruga amani kwa njia moja au nyingine. Unakumbuka siku ambapo ulieneza uvumi kuhusu mwenzako darasani? Labda ulilichukulia tukio hilo kuwa la kawaida tu. Ambalo hukujua ni kwamba kwa kufanya hayo, ulimsababishia kutengwa na marafiki, ukamfanya ajione duni na kumnyima amani. Bila shaka, ulimwumiza sana kihisia. Ieleweke kuwa tabia ni ngozi. Matendo ya aina hii yasipothibitiwa huweza kuwa msingi wa kusambaratisha mshikamano wa kitaifa baadaye.
Watu wengi huinyoshea serikali kidole wakati yanapozuka machafuko yoyote nchini. Utawala uliopo hukashifiwa kwa kushindwa kutekeleza jukumu lake la kulinda raia wote. Hata hivyo watu wawa hawa ndio kwa mfano wanaowasetiri washukiwa serikali inapojaribu kunyoosha mkono kuwafikia. Watu hawa wakiombwa na vyombo vya dola watoe ushahidi utakaochangia kushtakiwa kwa washukiwa wenyewe, wao hufyata ndimi zao. Isitoshe, wanasiasa wachochezi hukimbilia kutafuta hifadhi za makabila yao pale wanapokabiliwa na mashtaka ya kuvuruga amani nchini. Hata pale tunapodekeza hali hii, ni vyema tukumbuke kuwa vita havina macho.
Gharama ya kutokuwepo amani huwa kubwa katika jamii yoyote ile. Watu hulemazwa huku wengine wakipoteza roho zao. Mali yaliyochumwa kwa muda mrefu huharibiwa katika muda wa kufumba na kufumbua. Katika maeneo kama haya, wawekezaji hutoweka, jambo ambalo huwanyima vijana nafasi za kujiendeleza. Maeneo kama haya huselelea nyuma kiuchumi.
Ni vyema tumaizi kuwa jukumu la kulinda amani haliwezi kuachiwa asasi za kiusalama pekee. Lazima tushikane mikono kupigana na hali yoyote inayotishia usalama wetu kwa hali na mali. Taasisi za kielimu na kidini ziwe katika mstari wa mbele kuhubiri amani. Wanaotumia madhabahu kuwagawanya watu kwa misingi ya kidini watengwe na kukashifiwa. Viongozi wa kijamii nao wachangie kupiga vita mila potovu kama vile wizi wa mifugo na uvamizi. Wanasiasa wachochezi watemwe wakati wa uchaguzi. Vijana nao wajiunge katika vilabu vya kutangaza amani kote nchini.
- Chagua jibu sahihi kulingana na aya ya kwanza
- Amani ni hali ya utulivu palipo na vita.
- Watu wengine hupuuza thamani ya amani
- Ukiingia gizani utajua umuhimu wa amani,
- Gharama ya amani huwa kubwa sana.
- Ni kweli kusema kuwa,
- lazima msomaji anajua umuhimu wa amani.
- Visa vya utovu wa amani hutokea karibu na watu.
- Amani yetu huvurugwa na wale tunaowazia.
- Amani huweza hata kuvurugwa na matendo tusiyotilia maanani.
- Unapoeneza uvumi dhidi ya mtu fulani.
- humwumiza kihisia na kumfanya akose kujistahi.
- unawatenga marafiki zako na kujiumiza kihisia.
- unamkosesha utulivu na kumwinulia hadhi yake.
- huwezi kujua kuwa ufanyayo si haki.
- Msimamo wa mwandishi ni kuwa
- vurugu za watoto ndizo zinazosambaratisha jamii.
- ukosefu wa amani humfanya mtu ajiondoe katika jamii.
- tabia isipodhibitiwa mapema inaweza kuleta utengano katika jamii.
- mambo madogomadogo hayawezi kuathiri misingi ya kijamii.
- Ni kawaida ya watu
- kukashifu watawala utulivu unapokosekana.
- kuwakashifu wahasiriwa usalama unapodorora.
- kuitetea serikali usalama unapovurugiku.
- kujua umuhimu wa amani pale inapokosekana
- Raia katika kifungu wamclaumiwa kwa
- kutowajua wanaotekeleza vitendo vya kihalifu.
- kuwaonya wenzao wanapotaka kutoa ushahidi
- kuwafichua washukiwa wanaotafutwa na serikali.
- kukosa kusaidia serikali kuwahakikishia usalama.
- Njia bora zaidi ya kukabiliana na wanasiasa wanaoeneza chuki katika jamii ni
- kueneza habari zao katika vyombo vya habari
- kuwaondoa mamlakani wakati wa kupiga kura
- kuwatia mbaroni na kuwanyamazisha kabisa.
- kuwaacha wapige domo kwani watanyamaza tu.
- Yafuatayo ni madhara ya ukosefu wa amani isipokuwa,
- watu kupoteza maisha
- uharibifu wa mali.
- kudidimia kwa uchumi.
- kuenea kwa ukame.
- Wazo kuu linalojitokeza katika aya ya mwisho ni kuwa
- mila potovu ndizo zinazovuruga amani nchini.
- asasi za kijamii hazihusiki katika kudumisha amani.
- jukumu la kulinda amani ni la kila mwanajamii.
- tukishirikiana katika vita amani ya kudumu itapatikana.
- Huinyoshea serikali kidole ni sawa na
- kuilaumu serikali
- kuikejeli serikali
- kuikosea serikali.
- kuitukana serikali.
Soma kifungu hiki kisha ujibu maswali kuanzia 41 mpaka 50
Nilipomaliza mtihani wa kitaifa wa darasa la nane, nilijua kuwa ningepata liziko ndefu kuliko kawald Baada ya kukaa mjini kwa siku mbili-tatu, niliwaomba wavyele wangu kibali cha kuenda kijijini kuwazuru babu na bibi: Japo sikuzielewa sana shughuli za shamba, nilijua kuwa msaada wowote kwa wazee wang ungewafaa sana hasa ikizingatia kuwa walikuwa wamebugia chumvi ya kutosha. Waamia, auni ni aun hakuna auni duni.
Siku ya safari ilipowadia, baba na mama walinipeleka kituoni pa mabasi na kuniaya. Nilijawa na wahaka kiasi na kujiuliza, "Itakuwaje gari likinipitisha? Je, nitaweza kukitambua kituo chao vizur Nilitoa shajara yangu na kuhakiki tena maelezo niliyoandika. Njia panda baada ya stoo mbili, nishike njia ya kulia. Hata nilimwuliza utingo kama alikifahamu kituo hicho naye akanihakikishia nisiwe na shaka. Nilimshukuru na kutulia.
Safari yangu ilikuwa shwari bila shari. Njiani nilijisaili maswali anuwai. Nilijiona nikawafaa babu na bibi kwa njia nyingi. Nikajionea nikiwafunza vijana wa mashambani mambo mengi ya mji. "Nitawatoa ushamba kabisa," nikajiambia. Kutahamaki, gari lilisimama, utingo akaniashiria nishuke na kumsaidia kutua mzigo wangu. Kinyume na matarajio yangu, babu alikuwa pale kituoni akinisubiri, Nilimlipa hamali anibebee furushi lile la bidhaa, nikajibebea shanta yenye nguo zangu na kumwandama babu unyounyo.
Kijiji cha akina babu kilijaa utulivu wa kuridhisha. Nilipokelewa vizuri. Hata hivyo jambo moja lilinisumbua akilini. Vijana wenzangu walinisalimia kwa heshima lakini hakuna aliyesema jingine zaidi ya salamu. Sijui kama ni mimi niliyefikiria hivyo, lakini nilihisi kiasi fulani cha chul hasa kutoka kwa wazazi wa kike. Jambo hili lilininyima raha kwani nilidhani kijijini kulitawaliwa na hisia za udugu kama nilivyozoea kusikia ikiwa haya yalifanyika mjini ningeelewa.
Siku moja, mkazahau aliniita chemba na kunipasulia mbarika. Mavazi yangu hasa ya suruali zilizonibana ndiyo yaliyowafanya wengi kujitenga nami. Kumbe kile nilichoita ustaarabu kutokana mjini kilionekana kama utovu wa maadili mjini. Hapo ndipo nilipoujua ukweli ya methali, ukila pamwe na namiriigiza zao desturi. Mkazahau alinifunza mengi kuhusu maisha ya mashambani. Nami nikaafiki methali kuwa kinolewacho hupata.
Polepole nilianza kuwapata wenza. Tulifanya mengi pamoja. Tulibeba maji kwa mitungi migongoni na kuleta matita ya kuni msituni. Nilizifurahia shughuli hizi sana. Kila mara wenzangu hawakusita kunitahadharisha. “Usiuguse upupu huo utawashwa" au "chaka hilo linaweza kuwa na nyoka tahadhari!" Hata wakati wa kurudi mjini ulipofika, niliona uchungu kutengana na wasena wale.
- Ni maelezo yapi yaliyo sahihi?
- Ilikuwa likizo ya mwisho katika darasa la nane.
- Msimulizi alisafiri pindi tu alipofunga shule.
- Mwandishi hakupendelea kuishi mashambani.
- Mwandishi alinuia kuwasaidia babu na nyanya yake.
- Msemaji anakiri kwamba,
- hakuzoea kushiriki shughuli za shambani.
- ilikuwa mara ya kwanza kumzuru bibi yake,
- anazifurahia sana kazi za mashambani.
- hatajifunza shughuli za shambani.
- Maneno wamebugia chumvu ya kutosha yametumia tamathali gani ya usemi?
- sitiari
- nahau
- chuku
- tashhisi
- Kulingana na aya ya pili, tunaweza kusema kwamba mwandishi,
- ni mwenye papara
- hana mwao kuhusu aendako
- ni mwoga
- ni mwenye makini
- Utoaji bora wa huduma unaojitokeza kwa kuwa,
- babu alimlaki msimulizi kituoni.
- hamali alimbebea mwandishi furushi lake
- utingo alimpa mwandishi msaada aliohitaji.
- mwandishi aliandika maelezo kwenye shajara.
- Si kweli kusema kuwa,
- mwandishi alibebewa mizigo yake yote.
- msimulizi hakutaabika kufika kwa babu.
- mwandishi hakutarajiwa kupokelewa kituoni.
- msimulizi alitarajia kuwafunza wenyeji wale ustaarabu
- Jambo lililomsumbua mwandishi ni
- kukosa kusalimiwa na wanakijiji.
- kutengwa na baadhi ya wanakijiji.
- kutowaona vijana kijijini.
- hali ya utulivu iliyoshamiri kijijini.
- Wazazi wa kike walimwonyesha chuki msimulizi kwa kuwa
- hakupenda kuvalia jinsi alivyoagizwa.
- aliwapotosha wanao kwa mienendo ya mjini.
- alipenda kuwadharau wanakijiji.
- alikiuka utamaduni wao
- Methali ukila pamwe na namiri, igiza zao desturi inahimiza
- tukiingiliana na watu wenye sifa kama zetu tujaribu kuwa tofauti
- tukijua kuwa watu wana sifa tofauti tujiepushe tusiathiriwe na nyendo zao.
- tukiingiliana na watu wenye sifa tofauti tutafute mbinu za kuingiliana vizuri nao.
- Tukiwa na sifa tofauti tuwahimize wengine wajaribu kuwa kama sisi.
- Aya ya mwisho inatufunza kuwa,
- kugusa upupu humfanya mtu awatambue marafiki.
- uhusiano unaweza kuimarishwa hata katika mazingira mapya.
- kukemewa kwa sauti humfanya mtu atambue mazingira.
- Uchungu wa kutengana huzidi mtu anapoenda mjini.
INSHA
Umepewa dakika 40 kuandika insha yako.
Endeleza insha ifuatayo kwa maneno yako mwenyewe huku ukiifanya iwe ya kusisimua zaidi.
Mwendo wa saa nne asubuhi, milolongo ya magari ilionekana ikielekea.........
Majibu
- A
- D
- B
- C
- A
- D
- C
- B
- D
- B
- A
- C
- B
- C
- A
- C
- A
- C
- A
- D
- B
- D
- C
- A
- C
- D
- C
- B
- A
- B
- B
- D
- A
- C
- A
- D
- B
- D
- C
- A
- D
- A
- B
- D
- C
- A
- B
- D
- C
- B
Kiswahili Questions and Answers - Standard 7 Term 2 Opener 2022 Set 2
MASWALI
Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne hapo. Jaza kila pengo kwa kuchagua jawabu lifaalo zaidi.
Matukio ya siku hiyo yangali_1_akilini kwa wino usiofutika. Tulikuwa darasani tukifunzwa viunganishi kama vile_2_Ghafla bin vuu mlango ulibishwa_3_ Mwalimu aliacha kuandika na kuelekea kunako mlango aufungue. Ghafla mlango ulipigwa_4_na kufungika. Hapo nje _5_yalisimama majitu mawili yenye macho mawenge na miguu yenye matege iliyopinda kwa nje. Mikononi yalikuwa yamejihami_6_. _7_ "Watoe Salma na Aisha!" Jitu moja liliguruma. "Hamwezi kuingia hapa_8_ya ruhusa. Nisubirini _9_ " Bi. Somi aliwajibu kwa sauti nzito.
-
- imeandikwa
- zimeandikwa
- limeandikwa
- yameandikwa
-
- angalau, kidogo, mbali
- ila, maadam, mradi
- kefu, daima, safi
- aisee, wallahi, mathalan
-
- kijeshi
- kinguru
- kimadharau
- kikobe
-
- dhoruba
- kibao
- kibobwe
- kachombe
-
- :
- ,
- /
- ;
-
- kwa
- na
- bila
- kuzidi
-
- jambia,pantoni,singe
- Kikero, kigwe,rungu
- mikuki,ngao, marungu
- jambeni,keekee,kipini
-
- bali
- mradi
- haidhuru
- ghairi
-
- pambajioni
- maabarani
- maktabani
- darasani
Maji ni kiowevu kinachopatikana_10_na mvua katika bahari, maziwa na mito. Chambilecho wahenga_11_ Hii ni kwa sababu maji_12_huwa na manufaa kochokocho. Maji hutumiwa katika_13_, kunywa na hata kuogea. Wakulima pia huyatumia_14_mimea yao isije_15_ Maji yanastahili kutumiwa vizuri bila kumwagwa ovyoovyo.
-
- kutoka
- kutokana
- kwa
- kulingana
-
- maji ya kifuu hufuata bahari ya chungu
- maji ni uhai
- maji yakimwagika hayazoleki
- maji mkondo
-
- ii hii
- hii hii
- haya yaya
- yaya haya
-
- kupika
- kupikisha
- kupakia
- kupikia
-
- kuinyunyuzia
- kuinyuzia
- kuinyunyizia
- huinyunyizia
-
- ikastawi
- ikanawiri
- ikapogoa
- ikanyauka
Kutoka swali 16 - 30. jibu kulingana na maagizo
- Chombo kinachotumiwa kukunia nazi huitwaje?
- Mbuzi
- Kata
- Susu
- Kifumbu
- Chagua usemi wa taarifa wa:
"Wanafunzi wanaosomea katika shule hii wana bahati ya mtende," Maridhia alisema.- Maridhia alisema kuwa wanafunzi wanaosomea katika shule hiyo wana bahati ya mtende.
- Maridhia alisema kuwa wanafunzi waliokuwa wakisomea katika shule hiyo walikuwa na bahati ya mtende.
- Maridhia alihimiza kuwa wanafunzi wa shule hiyo walikuwa na bahati kama mtende
- Maridhia alitangaza kuwa wanafunzi ambao wangesomea katika shule hiyo wangekuwa na bahati ya mtende.
- Chagua sentensi iliyotumia kihisishi kwa usahihi
- Hewala! Sikuamini, siwezi kukusaidia
- Ebo! Ni mwanafunzi gani huyu asiyetofautisha mbu na mbung'o!
- Pukachaka! Tumepita mtihani vizuri.
- Simile! Naomba urudie swali lako
- Maneno yaliyopigwa mstari katika sentensi ifuatayo ni Mwanafunzi hodari hufaulu lakini mvivu hufeli sana.
- Kielezi, kiwakilishi
- Kivumishi, kielezi.
- Kielezi, kivumishi
- Kivumishi, kiwakilishi.
- Neno mapendekezo lina silabi ngapi?
- Tano
- Kumi
- Sita
- Kumi na moja
- Tegua kitendawili
Mgeni wangu anavaa nguo nyingi.- Mwanajeshi
- Mwanaharusi
- Msitu
- Askari
- Neno lipi limeambatanishwa na ukubwa wake sahihi
- Jina - majina
- Mzigo - zigo
- Kitabu - kijitabu
- Mtu - Jimtu
- Badilisha sentensi hii iwe katika hali ya kutendesha. Murasi alimpeleka binti yake Zawadi akaolewe na Musa
- Murasi limwoesha binti yake Zawadi kwa Musa
- Zawadi binti yake Murasi aliolewa na Musa.
- Musa aliozesha binti yake Zawadi na Murasi.
- Murasi alimwoza binti yake Zawadi kwa Musa
- Orodha gani iliyo na nafaka pekee
- Ngano, mawele, shayiri, mtama
- Limau, fenesi, tikiti, nazi
- Wimbi,mpunga, karafuu, mbuyu
- Ndizi, iliki, dania, bizari
- Kutokana na kitenzi aka tunaweza tukaziunda nomino hizi zote isipokuwa
- uashi
- mwaka
- kuaka
- mwashi
- Maelezo yapi hapa ni sahihi?
- Ngonjera ni shairi la kihistoria
- Tasdisa ni shairi lenye mishororo sita katika kila ubeti.
- Silabi za mwisho zinazofanana katika kila upande huitwa mizani.
- Mleo ni mshororo wa mwisho wa kila ubeti.
- Kanusha sentensi ifuatayo kwa usahihi.
Usiku huo ulikuwa na mbalamwezi kama nilivyotabiri.- Usiku huo haukuwa na mbalamwezi kama nilivyotabiri.
- Usiku huo haukuwa na mbalamwezi kama nilivyokosa kutabiri.
- Usiku huo haukuwa na mbalamwezi kama ambavyo sikutabiri.
- Usiku huo ulikuwa na mbalamwezi kama nisivyotabiri.
- Chagua jina lilioambatanishwa na ngeli yake kamili.
- Mwiba -U-U
- Jivu -I-ZI
- Moshi -U-ZI
- Malezi - U-YA
- Kamilisha, 'Lingana kama
- kinu na mchi'
- sahani na kawa'
- kiko na digali'
- kalamu na karatasi
- Ikiwa juzi ilikuwa Alhamisi, Jumatano itakuwa:
- Kesho
- Keshokutwa
- Kitojo
- Mtondogoo
Soma kifungu kisha uyajibu maswali 31 - 40
Jioni hiyo kama jioni nyinginezo, sisi wajukuu pamoja na vitukuu tuliketi kando ya moto tukisikiliza ngano kutoka kwa laazizi wetu, bibi. Mbalamwezi ilihakikisha kwamba hatupungukiwi na mwanga. Kila tulipomtembelea bibi, tulipata nafasi ya kusikiliza ngano.
Tuliuzingira moto pale nje ya nyumba yake ya msonge kama ilivyo kawaida kupata kopo la uji kwake bibi, tulilekiwa nacho. Baada ya kila mmoja kupata haki yake sasa nafasi ikawa ni ya mwenye masikio kuyatega ndi na kutulia tuli hadi mpasuko wa vicheko vya radi. Sasa tulikuwa tumejituliza kwenye vingoda vyetu bibi alipoanza masimulizi yake kama ilivyokuwa desturi yake. Alitanguliza na kusafisha koo. "Wajukuu wangu wapendwa, zamani sana nikiwa mdogo kama nyinyi hivi, pamoja na watoto wenzangu tulikuwa tukifunzwa kunga za kikwetu na bibi zetu. Ingawa tulihudhuria mafunzo hayo, wengine wetu hawakuyathamini vile kwani yalitunyima fursa ya kucheza michezo tuliyoipenda.
Siku moja nyanya aliyependa kutusimulia kwa mafunzo yake alikuwa ndio mwanzoa ameanza tu kutufundisha. Mkononi alikuwa na kigozi cha sungura alichokitumia kama wenzo wa kutufundishia jinsi ya kutunga vazi la kujisetiri, Sote tulimpa masikio na macho ingawa shingo upande.
Mara pakatokea Ibra! Kulianguka kutoka juu mtini tulipoketi hadi kwenye kile kigozi. Kilitambaa taratibu na kuja nilipokuwa kikapanda juu ya mkono wangu wa kushoto kabla ya kuteremka na kuyoyomea gizani. Nilishindwa kujisongeza wala kujitikisa. Niliogopa upeo wa kuogopa maana huyo alikuwa nyoka mwenye sumu hatari sana. Wenzangu nao pia walizimika ardhini wasijisongeze. Nyanya alijuzuia kusonga wala kufanya lolote. Nadhani aliogopa kutushtua au hata kumshtua huyo nyoka.
Ni kwenye hali hii nyoka huyo alipotokomea, alikojitendea ndipo kila mtu aliponijia kwa shangwe. na vifijo. Wote waliniambia kuwa kutokana na jinsi nilivyoonyesha ujasiri wakati wa hatari hiyo, basi nilihitimu kuwa kiongozi wao. Yakini, chanda chema huvikwa pete.
Mara moja nikatengenezewa vazi la ngozi, tena ngozi ya mbuzi na kutawazwa papo hapo kuchukua hatamu za uongozi. Wote wakaahidi kutii amri kwani akikalia kigoda mtii. Wajukuu wangu je mmejifunza funzo lipi kutokana na kisa changu?"
- Ni nani alipeana ngano?
- Msimulizi
- Mbalamwezi
- Nyanya
- Mjukuu
- Kwa mujibu wa kisa mjukuu ni:
- Mwana wa kitukuu
- Mwana wa nyanya
- Mwana wa mwana
- Mwana wa kining'ina
- Kwa nini bibi wanamwita iaazizi.
- Walipenda ngano zake
- Wao walimuenzi mno
- Hakuwa na jina rasmi lake
- Alichukia kuitwa kwa jina lake
- Ni nani alikalia kigoda karibu na moto.
- Wote
- Nyanya
- Msimulizi
- Wajukuu pekee
- Ni nani aliangukiwa na nyoka.
- Msimulizi
- Hatujaambiwa
- Nyanya
- Mjukuu
- Kwa nini woga ulimpata bibi?
- Bibi alimwonya
- Nyoka alikuwa mkali
- Nyoka alikuwa mwenye sumu
- Nyoka alimuuma
- Ni kweli kuwa
- msimulizi ni kitukuu
- msimulizi hajawahi kuumwa na nyoka
- nyoka ni mnyama wa kuogopwa
- kiongozi sharti awe mwoga
- Methali ipi yaweza kutupambia kisa hiki.
- Adui mpende
- Mtoto wa nyoka ni nyoka
- Ushikwapo shikamana
- Ukibebwa usilevyelevye miguu
- Wanaofundisha kunga za maisha huitwa?
- Kungwi
- Mkunga
- Bibi
- Wahenga
- Ishara gani inayoashiria umaskini kwenye kifungu.
- Nyoka
- Kiambo cha msonge
- Makopo ya uji
- Bibi mzee
Soma kifungu kifuatacho kisha uyajibu maswali 41 - 50
Nilikuwa mpigabuku wa skuli ya Wema, mwaka jana. Sikuwa na shaka kuibuka galacha katika mtihani wa kitaifa. Nilielewa lazima ja ibada nijifunge kibwebwe na kuuzika uzembe kwenye kaburi la sahau ili niupasi mtihani wa kitaifa. Aku zote ningerauka alfajiri na mapema na kuyabwaga mabuku mezani. Ningejipinda mgongo shabiku upinde na kuvivamia va bin vuu ya nsige gundani la mihogo. Yakini niliuma vitabu we! Kisa na maana sikuwa na namna nyingine ya kuinusuru mbari yangu iliyolemazwa na uchochole si haba. Joho la bidii lilisalia kuwa mwandani wangu.
Taabu na madhila ya baba wa kambo hayakunizuia hata chembe kutia bidii. Vioja vyake kila jioni vilinipa maudhui na vidokezo vya insha ya kila nui kesho yake. Hata kama kuna siku mama alifurushwa akapata hifadhi kwa jirani, mie sikukosa kuzimaliza gange za ziada za walimu. Wakufuu wetu nao walijitolea kwa vyovyote vile kuhakakikisha tunaelewa vyema. Ukweli walijaribu juu chini kufanikisha ndoto zetu. Hakika tenda wema nenda zako Mola atakulipa Wakufuu wa masomo ya sayasi na hisabati walirauka mapema kabla umande kukaushwa na miale ya asubuhi. Walituelezea hadi tukaelewa dhahiri shahiri. Mola daima twamwomba hasa bwana Manywele aliyejinyima hata kishuka kutupa mazoezi ya Sayansi ampe fadhila
Mtihani wa kitaifa ulipowadia hatukuwa na wasiwasi wala kihoro cha nja maji kwani yote tuliyofunzwa yalikuwa tamulini. Tulidurusu hadi misamiati, surufu na fomula zikatuzoea. Kila mmoja wa watahiniwa hasa mimi tulikuwa ngangari kukabiliana na mitego yote ya mtahini. Lo! Siku moja kabla, hofu iliniteka nyara, nikapumbaa na kukosa la kufanya. Mlilikuwa mkikimkiki na mkukumkuku kuwa halambe halambe. Utulivu uliokuwepo ulipasuliwa na vifijo na vifoli. Mkufuu mkuu akaturaushia kadi ya heri njema. Mwalimu majitamu naye akatupa nasaa na wosia wa kutokuwa na woga. Alisema mtihani ni mtihani hivyo basi hakukuwa na haja ya kuwa na mishemishe wali jekejeke la woga.
Asubuhi na mapema tukafika na kuwasili skulini. Tuliukalia ule wa Hisabati siku ya Mosi. Somo la sayansi saa nane huku insha tukiandika mwendo wa alasiri. Jua lilivibusu vilele vya milima nalo giza la kanika kuanza kubisha hodi. Siku ya pili tulianzia na somo la Mapishi pamwe na Kiswahili mwendo wa saa tano. Saa nane nilimalizia na Insha ya methali "Mchuma janga hula na wa kwao."
uliukalia ule wa somo la Kiingereza na kutamatisha elimu ya skuli za msingi. Ilibidi sasa tuwe wavumilivu na punda bila wasiwasi wala shaka. Kwa hamu na hamumu tuliyasubiri matokeo.
Hayawi hayawi huwa. Bidii na juhudi zetu mazao yake yangejulikana na pesa siku hiyo ya alhamisi mwezi Januari. Nakumbuka fika nilivyobumburushwa na kugutushwa na sauti ya redio. "Waziri wa elimu Bw. Matiang'i atayasoma matokeo mwendo wa saa tatu za alfajiri". Waja wa aila ya Joshua walijaa na kujazana pale kiamboni petu. Kama ilivyo mila na desturi, kwamba ufanisi ni wa kila mwanajamii. Yakini kwao, si kwa mchuma janga kula na wa kwao. Mwia usio na chupa kuoza vituo vyote runinga vilihinikiza hewani matangazo ya moja kwa moja.
Jina la mtaluniwa bora nchini likatajwa "Bora mufti ndiye shiyaa wa mwaka huu." Picha ikaonyeshwa nayo haikuwa ya mwingine bali mie mwana wa mzee Mufti. Shangwe na vigelegele vya heri njema na heko vilihinikiza hewani. Uwanja wetu muda si muda ulijazana na kujaa hadi na nusura kuwatapika wengine. Vimulimuli vya kamera nusura viunde jua. Kila mmoja alisheheni furaha ya ufanisi wangu. Kijiji chetu ambacho hakikutambulika sasa kikijulikana nchini. Ndoto yangu ya kuwa mhazigi ikiwa si ya alinacha. Shukrani tumbi za kumsifu Maulana zikihinikiza hewani.
- Msimulizi alisomea shule gani?
- Mpigabuku
- Wema
- Ya msingi .
- Hatujaambiwa
- Methali gani inao ujumbe wa aya ya kwanza
- Baada ya dhiki faraja.
- Mavi ya kale hayanuki
- Ukiona vyaelea vimeundwa
- Damu ni damu si kitarasa
- Ni kweli____
- msimulizi alipenda gonezi
- alilelewa na baba asiyemzaa
- alikuwa kitinda mimba
- alikuwa pacha,
- Ni walimu wa masomo gani walirauka
- Sayansi pekee
- Hisabati na Kiswahili
- Sayansi na Hisabati
- wote
- Siku ya kwanza watahiniwa hawakufanya mtihani wa
- Sayansi
- Hisabati
- Insha
- Kiingereza
- Mitihani ilifanyika kwa siku ngapi?
- 4
- 5
- 3
- 2
- Mwalimu Manywele alifundisha.
- Asubuhi pekee
- Saa nane na jioni
- Sayansi
- Saa zote
- Ni kweli___
- bora mufti alikuwa wa kwanza somo la Hisabati.
- baba yake aliacha kutiwa miaka mingi iliyopita.
- mama yake hakupenda masomo.
- alikuwa rakamu ya kwanza nchini.
- Msimulizi aliania kuwa
- daktari wa meno
- daktari wa viungo vya mwili
- mhadhiri wa chuo kikuu
- mwalimu wa sayansi
- Jamii ya Joshua yaathamini methali:
- Kila mwamba ngona huvuta kwake.
- Mmoja ni nguvu utengano udhaifu.
- Mtegemea cha nduguye hufa hali maskini
- Bendera hufuata upepo.
INSHA
Mwandikie kaka yako aliye mjini barua. Mjulishe jinsi unavyoendelea tangu shule zilipofungwa hadi sasa
MWONGOZO WA KUSAHIHISHA
|
|
|
|
|
Kiswahili Questions and Answers - Standard 7 Term 2 Opener 2022 Set 1
MASWALI
Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi / mpaka 15. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne. Chagua jibu lifaalo zaidi.
Kutokana na hali _1_ya hewa taifa la Kenya huwavutia watalii_2_kutoka kila pembe ya dunia. _3_. hali ya hewa hutofautiana sana kutoka sehemu moja hadi_4_ Ukizuru maeneo ya milimani hasa milima Kenya na Abadea utapata hali ya baridi. _5_ kilele kuna theluji ilhali kwenye nguu kuna msitu. Iwapo utatembelea maeneo ya Pwani na Ziwa Viktoria utapata kuna viwango vya juu vya joto. Aidha ipo misitu iliyojaa wanyamapori wa kila aina. Isitoshe zipo mbuga na hifadhi za wanyamapori. Hali ya uchukuzi_6_ kuelekea kwenye mbuga _7_. Pia kuna hoteli za kifahari. Hoteli hizo zinawahudumia wageni hawa. Ukitembea kwenye baadhi ya mito kuna maanguko ya maji. _8_. janibu za Thika kuna Thika na Chania. Maeneo ya Nyahururu kuna Thompson. Kenya kweli imebarikiwa sana.
-
- shwari
- shari
- swali
- hali
-
- chungu kubwa
- chungu kizima
- chungu nzima
- chungu mzima
-
- Kwa hivyo
- Hata hivyo
- Kama vile
- Kwa vile
-
- kwingine
- pengine
- jingine
- nyingine
-
- Kwenye
- Penye
- Katikati
- Kati ya
-
- imedunishwa
- imedidimishwa
- imeimarishwa
- imechukiza
-
- hizo
- hiyo
- ile
- hilo
-
- Maadamu
- Mathalani
- Minghairi
- Aghalabu
Maridhia alikuwa kijana _9_ kwa mapenzi _10_ na wazazi wake. Ingawa walikuwa mafukara, wazazi wote wawili walijitolea kwa _11_kumkidhia mtoto wao mahitaji yake ili akue kama mtu _12_angeifaidi jamii Hawakukosa kumrudi au kumtahadharisha dhidi ya hulka _13_ ya utu kwani walielewa kuwa _14_. Maridhia alifuata mwongozo wa wazazi na akatokea kupendwa na wengi kwa sababu ya nidhamu _15_
-
- aliyelewa
- aliyelelewa
- aliyekopoa
- aliyezaa
-
- makubwa
- kidogo
- kubwa
- matele
-
- udi na uvumba
- uta na upote
- maji na maziwa
- kinu na mchi
-
- ambao
- ambazo
- ambayo
- ambaye
-
- yenye
- isiyo
- iliyo
- zisizo
-
- juhudi si pato
- sikio halipiti kichwa
- kinolewacho hupata
- cha kuvunda hakina ubani
-
- yake
- yao
- zetu
- yangu
Kutoka swali la 16 mpaka 30, chagua jibu lililo sahihi.
- Kutokana na nonimo tiba, tunapata kitenzi
- matibabu
- tabibu
- utibaji
- tibu
- Andika wingiwa:
Mnyororo ulikatwakatwa ukatupwa jaani.- Minyororo zilikatwakatwa zikatupwajaani.
- Minyororo ilikatwakatwa ikatupwa majaani,
- Minyororo ilikatwakatwa ikatupwa jaani.
- Maminyororo ilikatwakatwa ikatupwa majaani
- Ni sifa gani kati ya zifuatazo isiyochukua kiambishi cha nyeli?
- -bora
- -ororo
- -chafu
- -ekundu
- Ni sentensi ipi iliyoandikwa katika hali tegemezi?
- Nitakuletea kikapu unitilie mboga.
- Zeda hukanza maji kabla ya kuoga.
- Hawajakuwa wakipita huku.
- Shule yetu ingepata ufadhili ingejengwa vizuri.
- Chagua kikundi kilicho na vivumishi pekee.
- Pole, sana, taratibu, tangu.
- Ebo! Ala! A kha! Lo!
- Sisi: wewe, wao, nyinyi.
- Wote, salibaya. yake.
- Kati ya nomino hizi.ipi iliyo katika ngeli ya LI-YA?
- Manukato
- Mali
- Madoa
- Manowari
- Nilijipaka poda usoni
- Wangu
- pangu.
- yangu.
- mwangu.
- Tunasema eupe kama theluji na zito kama
- nanga
- mzigo
- usuli
- kanini
- Ni sentensi gani iliyo sahihi?
- Wanafunzi huenda shuleni kwa miguu.
- Nyanya aliingia kwa kanisa akasali.
- Mlangoni wenye kufuli umefungwa.
- Tutaenda ziarani na basi.
- Ni sentensi ipi iliyotumia kirejeshi amba ipasavyo?
- Majaribio ambao yalifanywa yalifaulu.
- Gari ambalo lenye tuliabiri ni la mjomba.
- Huo ndio wimbo ambao nilitamani ucheze
- Sukari ambayo iliyotiwa katika chai ni nyingi
- Ni sentensi gani inayoonyesha wingi wa sentensi hii? Mama yangu amewasili.
- Mama yetu amewasili.
- Mama wetu amewasili.
- Mama zetu wamewasili
- Akina mama zetu wamewasili.
- Jaza kwa vivumishi vifaayyo:
Kiatu____ ni hiki- wenye, jingine
- vyenyewe, vingine
- chenyewe, kingine
- zenyewe. nyingine
- Kanusha:
Umesafiri mapema sana.- Haujasafiri mapema sana.
- Hujasafiri mapema sana.
- Hakusafiri mapema sana.
- Huwa husafiri mapema sana.
- Nilikuwa wa kwanza kufika darasa ndiko
kusema, nilifika___watu wote.- baada ya
- mbele ya
- kabla ya
- nyuma ya
- Andika udogo wa:
Mkono wake ni mkubwa.- Kono lake ni kubwa.
- Makono yake ni makubwa.
- Mikono yake ni mikubwa.
- Kikono chake ni kikubwa.
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 31 mpaka 40.
Kila mwanadamu ulimwenguni ana haki ambazo ni faradhi kila mmoja kuzingatia kile kinachonitia kiwewe ni kwamba wengi wetu tumekuwa tukizipigania haki zetu na kuzizika katika kaburi la liliwala zile za watoto. Ajabu zaidi ni kwamba wazazi wa watoto hawa ndio waliotia fora katika kuji watoto. Wanazivalia miwani hasa. Ninashikwa na jitimai na kibuhuti kikubwa, nikiona namna wavyele hawa wanavyosahau dhima na wajibu wao wa kuwatunza watoto wao. Wao, uajibikaji wa kuwalea watoto wao kwa njia nyofu na ongofu wameutia katika kaburi la sahau. Ikumbukwe kuwa kila mtoto ana haki zake na ni sharti kama mauti haki hizo zipewe kipaumbele na yeyote aliyewikwa jukumu hilo na Mola Mkawini.
Mathani, tunaelewa kuwa watoto wana haki ya kupata elimu. Wazazi wapende wasipende, watake wasitake, ni jukumu lao kuwapeleka watoto wao shuleni kusoma. Kwani haijawafikia masikioni kuwa climu ni taa gizani huzagaa? Enzi za zamani za uwaacha watoto kuzurura mitaani kivoloya bila lengo wala nia, zimepitwa na wakati. Elimu ndiyo nuru ya jamii. Tukiwaclimisha wana wetu, tutaupiga vita ulalahoi. Tutakuwa na wataalamu waliotaalamika katika nyanja na bila shaka tutajivunia watoto wetu.
Mtoto anayo haki ya kulelewa vizuri. Mlezi ama mzazi wake hana budi kuhakikisha kuwa mtoto amepatilo chakula cha kutosha na chenye lishe bora. Isitoshe watoto wanayo haki ya kuvishwa mavazi yatakayowakinya dhidi ya baridi yabisi na jua kali. Ukipita mitaani, utapigwa na butwaa kuviona vitoto vikicheza cheza vikiwa raham: wazazi hawa kwani hawaoni soni? Vikiwa katika harakati zao za kucheza, hujipata wakichezea takataka vilizosheheni makombo ya vyakula vilivyooza na kuozeana. Kwa hivyo, wanajipata wakivitumbukiza vinywani na hatimaye kuugua maradhi mbalimbali.
Sikonei hapo katu, lazima aidha nikujuze kuwa watoto wana haki ya kupata malazi bora na kuishi katika nyumba ili kumkinga na mabadiliko ya hali ya anga kama vile mvua, baridi na jua. Alalapo sharti pawe pazuri.
Asiachwe alale sakafuni penye baridi kali kama barafu. Husemwa, mwana wa yungi hulewa sembuse wa mwanadamu?
Familia iwe na watu watulivu, wenye mapenzi na wanaowajibika. Tusiwarushie watoto maneno makali ya kuwaumiza kwa udhuru wa kuwarekebisha. Akikosea, mtoto ascmezwe kwa upendo na aonyeshwe kuwa alilolifanya si zuri na asirudie. Endapo atarudia, basi aadhibiwe kama mwanadamu bali si kama mbwa aliyetabawali msikitini
Mtoto akilelewa vyema katika mazingira mazuri na matulivu, atainuka kuwa mwajibikaji wa kutegemewa na jamii yote. Aidha akilelewa vibaya, atakua akiwa mzigo sio tu kwa wazazi wake, bali pia jamii nzima. Sote tushirikiane zaidi ya kiko na digali, kinu na mchi ili kwa pamoja tumlee mtoto vizuri kwa kuzingatia haki zote zote ili tukijenge kizazi kijacho..
- Ni jambo lipi kulingana na aya ya kwanza, linamtia wasiwasi mwandishi?
- Watu wengi wanazingatia haki za watoto.
- Watu wengi wanazingatia haki zao.
- Watu wengi wanazipigania haki zao na kuzisahau za watoto."
- Watoto huzipigania haki zao wenyewe.
- Maneno "waliotia fora" yametumika, yana maana gani?
- Waliofanikiwa kim:
- Wasiotetea haki za watoto.
- Waliopata ufanisi katika kupigania haki za watoto.
- Waliopendelea haki za watoto kuliko zao.
- Ni akina nani wanaostahili kuwa katika mstari wa inbele kupigania haki za watoto?
- Watoto wenyewe.
- Wazazi na watoto.
- Serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali.
- Wote walitwika jukumu la kuwalea watoto.
- Ni kwa nini inasemekana kuwa ni lazima watoto wapate elimu? Elimu
- itayaboresha maisha ya baadaye ya mtoto.
- inatolewa bure na serikali.
- inapatikana popote.
- ni vigumu kuipata maishani.
- Elimu ni taa, gizani huzagaa ni
- methali.;
- balagha.
- nahau.
- msemo.
- Wazazi watajivunia watoto wakati gani?
- Watakapocheza pamoja na kujichafua.
- Watakapoelimika na kuwa watu wa. kutegemewa.
- Watakapovaa mavazi mazuri kila siku.
- Watakapokaidi kukosolewa na wakubwa wao
- Taka wazichezeazo watoto,
- huwa majalalani na zimefunikwa vizuri.
- huchezwa tu na mbwamwitu.
- huwa ni chafu na zer ye mabaki ya chakula
- huwa zinatumiwa na watoto kutoka familia tajiri.
- Kulingana na aya ya nnc, mtoto
- ana haki ya kukomewa anapokosea.
- anahitaji kulishwa vyema.
- anastahili kupata elimu ya kutosha.
- anafaa apewe malazi ya kuishi
- Aghabu sakafu nyingi,
- zina baridi kama barafu.
- hutengenezwa vizuri.
- Lulaliwa na watoto wengi
- huwa makao mazuri ya familia nyingi.
- Watu hushirikiana kwa namna zote hizi ila
- kiko na digali.
- tui na maziwa.
- jembe na mpini.
- kinu na mchi.
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 41 mpaka 50.
Maisha yangu yalikuwa yale ya Sultan bin Jerere. Nilichokihitaji nilikipata bila kutoa jasho hata. Wazazi wangu walinionyesha mapenzi ya dhati. Nyumbani kwetu kulikuwa peponi. Hakuna kilichokosa na endapo kilikosa, kilikuwa kimeendewa popote ulimwenguni. Nguo zetu hazikutengenezwa barani sembuse nchini? Magari ya kifahari yaliyonunuliwa ghali yasingehesabika. Nilipelekwa shuleni kwa shangingi na kusubiriwa na dereva wangu mpaka wakati ule ningemaliza masomo. Sikupata masaibu katu na niliishi maisha ya raha mustarehe kweli.
Hata hivyo, raha yangu ilifikia tamati ya ghafla. Ajali isiyojali ilinipokonya wazazi wangu wapenzi. Ndege waliyokuwa wakisafiria ilianguka baada ya kupata hitilafu za kimtambo na kuwasafirisha jongomeo abiria pamoja na wote waliokuwa humo. Vifo hivyo vya ghafla bin vuu, viliyabadilisha maisha yangu. Maajabu ni kuwa mali ya wazazi wangu yalitoweka ghafla. Sijui mali hiyo walitoa kupi wazazi wangu.
Wajomba wangu pamoja na jamaa kwa jumla walitoweka nyusoni. Nilibaki peke yangu bila wa kunilea wala kuniongoa. Hakuna aliyenijali, marafiki wa wazazi wangu nao waliniambaa na kutoweka zaidi ya umande wa alfajiri jua lichomozapo,
Hapo ndipo wazazi wa rafiki yangu Zena walipoamua kuingilia kati na kunichukua. Hii ni baada ya rafiki yangu kuwasimulia masaibu yaliyokuwa yamenisibu. Faraja iliyoje! Bwana Fadhila alikuwa mzee aliyebugia chumvi si haba. Aliishi na mkewe Bi. Moyo. Ingawa walikuwa hawana hawanani, waliona ni heri umaskini wa mali na utajiri wa utu na wema, Bwana Fadhula na mkewe walishirikiana kama kiko na digali kulusomesha mimi na rafiki yangu wakinichukua kama mmoja wa watoto wao. Tulipokosa, walituadhibu sawia bila kutubagua Chakula tulikula pamoja, kiwe wali ama pure. Upendo ulikuwa katika familia hii ulizidi utajiri wowote.
Nami niliamua kukaza kamba masomoni ili nisije nikawaibisha wafadhili wangu. Aidha nilimhimiza Zena kuuma uzi shuleni ili kujijengea mustakabali aula. Shuleni tulitia fora na kuenziwa na kila mmoja shuleni. Tulimaliza masomo ya shule ya upili na kujiunga na chuo kikuu ambapo mimi nilisomea udaktari naye Zena akiridhika na uhasibu. Pamoja, tulikuwa kama mtu na kivuli chake.
Kwa kurudisha mkono wa fadhila, tuliwajengea nyumba nzuri na kuwaajiri wafanyakazi wa kuwasaidia nyumbani na shambani. Niliamini kuwa miili yetu ni kama mimea. Ikitunzwa inanawiri vyema. Wazee hawa walibadilika na kuwa kama vijana. Waliishi maisha ya raha mustarehe walifurahia juhudi walizozifanya kumtunza mtoto wa watu, mwanamkiwa ambaye sasa amegeuka kuwa mwana wa maana katika uzee wao.
- Maisha ya mwandishi yalikuwa ya aina gani?
- Ya kikabwela.
- Ya kilalahoi.
- Ya kitajiri.
- Yakimaskini.
- Maisha yake mwandishi yalitatizwa na nini?
- Masaibu
- Sherehe
- Kutosoma
- Vifo vya wazazi wake
- Jamaa na marafiki wa wazazi wake mwandishi
- walikuwa wenye huruma na utu.
- walikuwa wanafiki ambao hawakumsaidia.
- walikuwa wengi na walimfaa sana.
- walikuwa watu wazuri lakini mikono mirelu.
- Mali ya wazaziwe mwandishi ilipatikana vipi?
- Biashara walizofanya.
- Ajira ya donge nono.
- Mwandishi hakubaini.
- Kufuga mifugo mengi.
- Ni nani aliyemsaidia mwandishi hamda ya kukosa mhisani?
- Zena rafikiye.
- Wazazi wa Zena
- Wajomba wake wandishi
- Marafiki wake mwandishi
- Taarifa ya uhitaji wake mwandishi uliwafikiaje wazazi wa Zena?
- Zena ndiye aliyewaambia wazazi wake
- Wazazi wa mwandishi waliwasiliana na Bwana Fadhila kabla ya kifo chake
- Wazazi wake mwandishi walikuwa wameandika urithi.
- Wajombawe walimwomba Bw. Fadhila amsaidie mwandishi.
- Kulingana na aya ya nne, ni sahihi kusema
- Bwana Fadhila na mkewe walikuwa wazee
- Bwana Fadhila na mkewe walikuwa matajiri sana.
- Familia ya Fadhila ilikuwa na watoto wengi.
- Wazazi wa Zena walimbagua mwandishi.
- Nami niliamua kukaza kamba. Maneno haya yana maana kuwa mwandishi
- aliaga dunia
- alianza kuzembea.
- alifanya bidii.
- alihuzunishwa na kifo cha wazaziwe.
- Rafikiye mwandishi alisomca kazi gani?
- Wanasheria
- Uhandisi
- Uandishi
- Uhasibu
- Ni methali gani inayoweza kuelezea kifupi taarifa hii?
- Asiye na wake aeleke jiwe.
- Kuvunjika kwa mwiko si mwisho wa upishi.
- Mwana akibebwa hutazama kisogo cha nina
- Aisituye mvua imemnyea
INSHA
Umepewa dakika 40 kuandika insha yako
Kamilisha insha hii kwa kuifanya iwe ya kusisimua zaidi.
Tulimaliza kula chajio na kuingia vyumbani mwetu kulala. Punde si punde......
MWONGOZO WA KUSAHIHISHA
|
|
|
|
|