Tuesday, 30 August 2022 07:00

Kiswahili Questions and Answers KCPE 2022 Prediction Papers Set 3

Share via Whatsapp

Maswali

Soma vifungu vifuatavyo, Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne hapo. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.

Taifa    1    la Kenya shughuli     2    zimekwama. Ugonjwa wa Covid-19 umetetemesha kila kona ya taifa    3   . Ni vizuri kuelewa kuwa, gonjwa hili     4    nchi yetu tu     5     pia ulimwengu mzima. Hata mataifa yenye uwezo mkubwa kiteknolojia, kiuchumi na elimu ya juu     6     adha ya ugonjwa huu tandavu wa Covid19. Ili kujikinga, yafaa tunawe mikono    7     sabuni, kutoshiriki mikutano na ikiwezekana tufanye kazi      8     nyumbani.

  A B C D
1  nzima  zima  mzima  lizima 
2  zote  yote   lote  vyote
3  yetu  zetu  wetu  letu
4  limetisha  umetisha  halijatisha  litatisha
5  bali  hata  kumbe  ikiwa
6  haijaepuka  hayajaepuka  haujaepuka  halijaepuka
7  ya  na  kwa  za
8  katika  kwa  kwenye  kutoka


Waswahili walisema     9     .Hali hii ilijitokeza pale Kadongo aliyekuwa na mali     10     alipoamua      11     masomo ya yatima mmoja. Uamuzi wake huo uliwashangaza wengi kuona matajiri wengi    12    kusaidia      13     kuwa wamiliki wa mali yafuatayo       14    majumba, magari, mashamba na viwanda. Ni vyema kuwa na     15     kama Kadongo.

  A B C D
9  hiari yashinda utumwa  mtu hujikuna ajipatapo  kutoa ni moyo usambe ni utajiri  mwenye shibe hamjui mwenye njaa 
10  madogo  ndogo  nyingi  kidogo
11  kuyathamini  kuthamini  kuyadhamini  kuidhamini
12  walidinda  walikubali  waliamini   waliamua
13  sembuse  ili  licha ya  kabla ya
14 ; : _ !
15  mkono mzito  mkono wa birika  mkono wa buli  mkono wazi


Kutoka swali la 16 mpaka 30, chagua jibu lililo sahihi.

 1. Katika neno, ‘alisahaulika' tambua kiambishi kiwakilishi cha nafsi na cha wakati.
  1. ka
  2. li, li
  3.  li, ka
  4. Ali
 2. Andika katika wingi:
  Chuma kilichovunjika kiliwekwa nyuma ya pazia.
  1. Vyuma vilivyovunjika viliwekwa nyuma ya mapazia.
  2. Chuma zilizovunjika ziliwekwa nyuma ya pazia.
  3. Vyuma vilivyovunjika viliwekwa nyuma ya pazia.
  4. Machuma yaliyovunjika yaliwekwa nyuma ya mapazia.
 3. Andika katika udogo:
  Mzee alipiga ngoma kwenye mji.
  1. Zee lilipiga goma kwenye jiji.
  2. Vizee vilipiga vigoma kwenye vijiji.
  3. Kizee kilipiga kigoma kwenye kijiji.
  4. Mzee alipiga kigoma kwenye jiji.
 4.  Tegua kitendawili kifuatacho:
  Kikigongwagongwa wanawe hutoka.
  1. Kizimba
  2. Kichuguu
  3. Mzinga
  4. Chungu
 5. Chagua sentensi yenye kivumishi cha pekee.
  1. Gari lolote lililoendeshwa pasipofaa litaondolewa.
  2. Ndugu yangu atasafiri kesho
  3. Ndizi mbovu zimeliwa na ng'ombe.
  4. Kabati hilo ndilo lililotengenezwa
 6. Chagua methali yenye maana kuwa mtu anaposababisha shida huishia kuwahusisha jamaa wake.
  1. Mla nawe hafi nawe ila mzaliwa nawe.
  2. Mchumia juani hulia kivulini.
  3. Kikulacho ki nguoni mwako.
  4. Mchuma janga hula na wa kwao.
 7. Kanusha sentensi ifuatayo: Kujitahidi kwangu kuna manufaa.
  1. Kujitahidi kwangu hakuna manufaa.
  2. Kutojitahidi kwangu hakuna manufaa.
  3. Kujitahidi kwangu hakutakuwa na manufaa
  4. Kutojitahidi kwangu hakutakuwa na manufaa.
 8. Jina "shughulika" lina silabi ngapi?
  1. 10
  2. 8
  3. 4 D
  4. 6
 9. ‘Cherahani' ni jina katika ngeli gani?
  1. KI-VI
  2. I-ZI
  3.  U-ZI
  4. LI-YA
 10. Ni kiungo kipi cha mwili kinachosafisha hewa?
  1. Ini 
  2. Wengu
  3.  Figo
  4. Pafu
 11. Unganisha sentensi ifuatayo: Mama alipika wali. Wali ulikuwa kwa.cah.
  1. Wali ulipikiwa kwa Leah ta mama.
  2. Mama alipikiwa wali kwa Leah
  3. Leah alipikiwa wali kwa mama.
  4. Wali ulipikwa na Leah kwa mama.
 12. Tambua maneno yaliyopigiwa kistari: Vitabu vizuri vitanunuliwa kesho.
  1. Kielezi, nomino
  2. Kivumishi, nomino
  3. Kivumishi, kielezi
  4. Kielezi, kiwakilishi
 13. Andika katika usemi wa taarifa:
  "Tutapiga kambi hapa kesho," wanajeshi walisema.
  1.  Wanajeshi walisema watapiga kambi hapo kesho.
  2. Wanajeshi walisema walipiga kambi hapo kesho.
  3. Wanajeshi walisema kuwa wangepiga kambi hapo baadaye.
  4. Wanajeshi walisema kuwa wangepiga kambi hapo siku amiayo ingefuata.
 14. Mkopo usiotozwa riba huitwaje?
  1. Arbuni
  2. Chirimiri
  3. Kadhongo
  4. Karadha
 15. Andika kwa tarakimu.
  Milioni sita, mia tisa iisini na tisa eltu, mia tiga tisini na nane.
  1.  6,996,998
  2. 6,999,988
  3. 6,999,998
  4. 6,909,098

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 31 mpaka 40

Aghalabu kila wakati nilipomtembelea nyanya yangu, alikuwa akinitambia hadithi. Basi nilipomtembelea mwezi Juni, aliweza kunitambia hadithi kuhusu Mzee Hekima na bibi yake. Waliishi katika kijiji cha Madongo. Mzee Hekima alijaliwa na Mola na watoto wengi wavulikya magashi. Nao waliwalea wanao vyema kwa kuwalisha vizuri vyakula vya tumboni na kiroho. Usisahau kuwa Mzee Hekima alikuwa tajiri wa mali na moyo. Mamia ya wanakijiji waliofika kwake kumjulia hali aliwasubilia kwa vyote. Kuna wale waliopewa riziki kwa kulima shambani, wengine kufagia boma lake bora tu kila mmoja alifaidika na mkono karimu wa bwana huyu.

Kati ya watoto wake wengi, Mzee Hekim alimpenda zaidi kitindamimba na alimpendelea kwa mengi. Kutokana na hali hii kitindamimba alianza kujivuna na kuwadharau wakubwa wake. Alionyesha kiburi, unyeti na dharau. Mwishoni tabia yake ilianza kuingia ufa. Mambo yalizidi kuzorota zaidi kiasi cha mtoto huyo kuwa mbaya zaidi. Wazazi walipogundua uovu wa mtoto huyo, mambo yalikuwa yamekwisha kithiri. Baada ya kujaribu kulihali kumwongoa na kulemewa walimtupa jongoo na mti wake.

Kila mmoja aliepuka kitinda mimba huyu kama kinyamkera. Hakushirikishwa michezoni wala katika matembezi. Ajabu ni kwamba, hakurekebisha tabia yake hali aliendelea kuwa mkaidi zaidi kuliko hata mkia wa nguruwe. Mzee Hekima naye alizidi kuzeeka na kugotika kadiri siku zilivyosonga.

Mzee Hekima alianza kuwausia wanawe. Aliweka kila kitu wazi. Alisema pesa zote za banki zingegawanywa kwa wanawe wote wa kiume. Nayo mali yaliyohaki yagawatywe kulingana na umri wa kila mrithi. Jukumu la uandishi wa wosia huu lilipewa kitindamimba. Naye akawa amepata nafasi murua ya kufanya hila. Alijiandikia nafasi kubwa ya urithi wa mali ya baba yake. Hekima alipoaga dunia yule kitindarnimba aliazimia kuuza shamba lile. Hapo alimtafuta mnunuzi na kumpata Mzee Kolera. Walipalana bei lakini hakulipwa pesa taslimu ila waliandikiana mkataba

Nakumbuka siku moja, mtoto wa Mzee Johara alienda mtoni kuogelea akiwa ameandamana na marafiki zake. Mto Kingo ulijulikana kwa kuwa na mamba wengi waliowashambulia wakazi wa eneo hilo. Kwa bahati mui mwanawe Mzee Johara alishikwa mgutini na maka Alivutwa na kuelekezwa kwenye maji makuu. Watoto wenzake walipoona hivyo walipiga usiahi kwa hofu waliomba msaada. Kwa bahati nzuri, wana wawili wa yule Mzee Hekima walikuwa wakipita njia karibu na mto huo. Wakasikia mayowe na kelele. Basi bila kulimatia wakaenda haraka kuangalia kelele zilikuwa za nini.

Baada ya kufika mtoni, waliambiwa habari za mtoto yule aliyechukuliwa na mamba. Walipotupa macho walimwona mtoto yule wa Mzee Johara akizamia lulu majini. Bila chelewa chelewa, vijana hawa walivua nguo zao na wakajitosa majini na kumfuata mamba yule. Walishambulia mamba yule kwa sime zao mpaka akamwachilia mtoto yule wakamchukua na kuogelea naye hadi ufuona mato. Hapo walimpa ganga ganga za mganga Anazomwacha mgonjwa na matumaini.

Mtoto huyo alikuwa amejeruhiwa vibaya mguuni kutokana na kuumwa kwa meno ya mamba. Baada ya kumpa huduma ya kwanza, waliamua kumpeleka kwa baba yake ili kumsimulia kisa chote. Mzee Johara alifurahishwa sana na kitendo cha watoto hao na akawaombea dua ya Mola awasaidie.

Baada ya kuwapa makaribisho aliamua kuwasindikiza wana wale wawili huku yeye akielekea kumlipa kitindamimba pesa zake. Basi wote watatu waliaondoka Wana wale walienda nyumbani naye Mzee Johara akielekea kumlipa ujira wake kitindamimba. Mzee Johana aliwaomba kwa unyenyekevu waandamane naye ili wawe mashahidi wake. Vijana wale wawili walikubali bila ya wao kujua ni shamba gani lililokuwa likiuzwa.

Mzee Johara na ndugu wale wawili walipofika kwa wenyeji wake, alianza kuwaelezea jinsi walivyopatana bei ya shamba. Ndugu wale wawili walishtuka sana na kukasirika. Papo hapo wakamweleza Mzee Johara kisa chote kuanzia mwanzo hadi mwisho. Mzee Johara kusikia hivyo alighairi kununua shamba hilo. Ujanja wa kitindamimba kikagonga mwamba.

 1. Chagua kauli isiyo ya kweli kulingana na aya ya kwanza
  1. Mzee Hekima na mkewe walijaliwa watoto wa kike na kiume.
  2. Mzee Hekima na familia yake walikuwa wacha Mungu.
  3. Wavulana walikuwa wengi kuliko wasichana.
  4. Mzee Hekima aliweza kutoa mwongozo mzuri wa familia yake.
 2. Mzee Hekima alikuwa tajiri wa moyo kwa kuwa
  1.  Mamia ya wakazi walifika kwake kumlilia hali.
  2. Alikuwa na mashamba makubwa yaliyohitaji usaidizi wa wanakijiji.
  3. Nyumbani kwake kulishiba watu walioenda kwake ili kufagia na wengine kulima.
  4. Aliwafaa wengi ambao hawakujiweza kiuchumi.
 3. Wazazi walipogundua uovu wa mtoto huyo, mambo yalikuwa yamekwisha kithiri.Ni methali gani inayokubaliana na kauli hii?
  1. Chelewa chelewa utampata mwana si wako
  2. Asiyesikia la mkuu huvunjika guu.
  3. Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.
  4. Mwana wa nyoka ni nyoka.
 4. Kitindamimba aliharibika
  1. kwa kuwa yeye ndiye alikuwa mtoto wa mwisho kuzaliwa.
  2. kwa kupendelewa na baba yake kuliko watoto wale wengine.
  3. kwa kupewa majukumu mengi yakiwemo yale ya ugavi wa shamba.
  4. kutokana na vijana wa hirimu yake.
 5. Zifuatazo ni sifa za Mzee Hekima kulingana na aya ya nne ila
  1. alikuwa mwenye busara.
  2. alikuwa mwenye ubaguzi.
  3. alikuwa mwenye uwazi.
  4. alikuwa mwenye fitina.
 6. Kitinda mimba kulingana na kifungu, alifaa
  1. kupata sehemu ndogo kabisa miongoni mwa warithi.
  2. kupata sehemu kubwa kabisa miongoni mwa warithi.
  3. kuliuza shamba lake baada ya kugawiwa.
  4. Kumtafuta mnunuzi wa shamba lao bila kuwahusisha ndugu zake.
 7. Ujasiri wa ndugu zake kitindamimba unaonekana pale
  1. walipompeleka ndugu yao kortini kwa njama ya kuliuza shamba lao.
  2. walipoandamana na Mzee Johara hadi kwao kushuhudia ununuzi na uuzaji wa shamba lao.
  3. walipokabiliana na mamba na kumwokoa mtoto wa Mzee Johara.
  4. walipomkataza Mzee Johara kulinunua shamba lao bila idhini ya wote.
 8. Ni sadfa kuwa
  1. Mzee Johara aliwaomba wanawe Mzee Hekima kushuhudia ununuzi wa shamba lao.
  2. marafiki wa mwanawe Mzee Johara hawakujua kuogelea.
  3. wana wa Mzee Hekima hawakuwahi kuacha sime kila walipotembea.
  4. kitindamimba hakuwa amelipwa pesa na badala yake waliandikiana mkataba.
 9. Ni msemo gani unaoonyesha Mzee Hekima alichoshwa na kitindamimba?
  1. Mzee Hekima alimpendelea kitindamimba kuliko wote.
  2. Mzee Hekima alimpa dhima ya kuandika wosia.
  3. Mzee Hekima aliamua kugawa mali yake kulingana na umri wa kila mrithi.
  4. Mzee Hekima aliamua kumtupa jongoo na mti wake.
 10. Sime ni
  1. upanga wenye makali kuwili.
  2. kiboko chenye ncha ya chuma.
  3. miundi inayotumiwa kulimia.
  4. ni bastola ya kufyatua risasi.

Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali 41 mpaka 50.

Maisha ya binadamu huimarika kutokana na urafiki. Urafiki hufanya watu wanaopendana kuwa na mvuto fulani ambao huwapa kiu ya kutaka kuonana mara kwa mara. Umbali kwao huwa si chochote si lolote. Watafanya juu chini ili waweze kuwasiliana hata kama ni kwa kupigiana simu, kuandikiana nyaraka au hata kutembea kilomita nyingi mradi tu wakutane.

Manufaa ya urafiki ni gani? Nia kuu ya urafiki ni kuondoleana ukiwa, kuliwazana, kubadilishana fikira na kusaidiana wakati wa shida. Pasi na urafiki duniani kungejaa madhila, uhasama, zahama na maovu mengine ya kukiriha moyo.

Urafiki bora ni ule wa kujuliana hali, kufaana wakati wa dhiki, urafiki wa kupigiwa mfano yaani ule wa kufa kuzikana. Hata hivyo urafiki huu umeadimika kama milango ya pikipiki. Ni nadra na adimu kumpata rafiki shakiki. Kila mtu sasa ameanza tu kuamba ngoma akivuta kwake. Ya mwenzake hayamghasi, ni kanda la usufi ati.

Kile ninachojaribu kusema ni kuwa, urafiki mwingi ni ule wa juu juu. Ule wa nipe nikupe. Iwapo wewe ni maskini, ole wako! Watakwambia kuwa mkono mtupu haurambwi na utapewa kisogo. Ukiwa tajiri pia huna bahati. Utaandamwa kama nzi na kugandwa kama kupe na wanaotaka kikalia mrija. Siku ya kuonyeshwa mlango kazini watakuhepa labda uauniwe na ndugu yako

Kulonga mithaki urafiki mwingi ni ule wa idumakawili Ni ule wa kulana kivuli. Wale wanaojitapa hadharani kuwa marafiki zako shakiki ukiwapa siri, kesho utazisikia barazani. Ulimthamini lakini yeye hafai ni mfano wa kikulacho ki nguoni mwako. Ni makauleni wakubwa. Ni vycina kila mmoja ajue kuwa, ule urafiki wa zamani wa kufaana kwa jua na la mvua umezikwa katika kaburi la liliwala.

Kinyume na vile watu wengi wanavyodhaniás urafiki unahitaji uvumilivu, uaminifu, ukarimu, upendo, usamehevu na kujitolea mhanga kama kukuahatarishaye maisha yake ili kumwokoa kifaranga.

Je, urafiki una faida? Ndiyo. Kumbuka ukiwa na marafiki huwezi kuteseka sana. Wahenga walisema kuwa mtu ni watu na hakuna mtu anayeweza kujitosheleza. Majanga yapo. Mengine makubwa yanayozidi uwezo wa mtu binafsi. Chukulia kwa mfano shughuli za mazishi. Utachimbaje kaburi na ubebe jeneza peke yako. Hapo ndipo utahitaji marafiki.

Tujue kuwa tuko pia na urafiki wa kuharibiana tabia. Kwa mfano watu wasio na msimamo kimaisha kazi yao ni kufuata wengine kama bendera. Tumewaona wengi wakijitoa kikaangoni na kujiingiza motoni bila kujali. Hawa sana sana ni wale ambao huwa hawaambiliki wala hawasemezeki. Hata wakiambiwa wasitembee na watu waovu kwa kuwa samaki mmoja akioza na mtungo pia huwa hawasikii. Huonyesha kiburi na unyeti mwishowe huishia kujipalia makaa.

Tamu ikizidi sana huwa sumu. Nao-urafiki ukizidi sana wakati mwingi huwa na madhara yake. Unajikuta kwa kuwa ati mtu ni rafiki yako, unaamua kuchukua hatua bila hata kumhusisha. Kumbe uamuzi uliochukua ni sumu kwake.

 1. Ni wazi kuwa
  1. kama si urafiki watu hawangekuwa wakionan
  2. pesa haziwezi kuwa kizingiti kwa watu ambac wanataka kuonana.
  3. urafiki huumua maisha ya binadamu.
  4. urafiki umeanza juzi wakati wa teknolojia mpya.
 2. Lipi si lengo la urafiki?
  1. Kufarijiana.
  2. Kubadilishana mawazo.
  3. Kufaana wakati wa dhiki.
  4. Kukirihisha moyo.
 3. Aya ya tatu inaonyesha kuwa
  1. hakuna urafiki wa kweli kokote dunianti.
  2. marafiki wengi ni wanafiki,
  3.  lengo la urafiki wowote ni kudhuriana.
  4. mzigo wa mwenzio ni kanda la usuf
 4. Chagua methali mwafaka inayolenga mwis wa aya ya nne.
  1. Mla nawe hafi nawe ila mzaliwa nawe.
  2. Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki.
  3. Nzi kufa juu ya kidonda si hasara
  4. Ndugu ni kufaana si kufanana.
 5. Yaonekana kuwa
  1. urafiki wa leo ni bora kuliko ule wa zamani
  2. urafiki wa zamani ulikuwa bora kuliko wa leo.
  3. urafiki wa leo umeathiriwa pakubwa na urafiki wa zamani.
  4. hakuna tofauti ya urafiki wa zamani na ule wa leo.
 6. Taja tamathali mbili zinazojitokeza katika kauli hii: Kujitolea mhanga kama kuku ahatarishaye maisha yake ili kumwokoa kifaranga.
  1. Chuku, tashbihi
  2. Tashhisi, kinaya
  3. Naha, istiara
  4. Nahau, tashbihi
 7. Mwandishi ametumia mfano wa mazishi
  1.  ili kuonyesha hatima ya kila mtu ni mauti.
  2. kwa kuwa ni sherehe ambazo huleta majonzi katika jamii.
  3. kuonyesha kuwa kuna haja ya kusaidiana wakati wa shida.
  4. kionyesha ubora na thamani ya urafiki.
 8. Aya ya inatuonyesha kuwa,
  1. kuna watu wanaotumia urafiki kwa manufaa yao ya kiuchumi,
  2. urafiki wa dhati upo na unafaa kuigwa na wote
  3. wengi wa marafiki tulio nao wametufaidi sana katika shughuli zetu za kila siku,
  4. hakuna msingi wa urafiki mwema.
 9.  Kujipalia makaa ina maana ya
  1. kujinufaisha wao pekee
  2. kujiletea matatizo.
  3. kujisalimisha kwa kushindwa.
  4. kukosana na watu wote.
 10. Aya ya mwisho inaonyeshe kuwa
  1. jambo zuri linaweza kuleta athari mbaya.
  2. rafiki ana uwezo wa kujua shida ya mwenza.
  3. hatufai kuwa na marafiki wasiojua hisia zetu.
  4. ni vigumu sana rafiki kujua yale yanayomsumbua mwenzake.

Majibu

 1. B
 2. A
 3. D
 4. C
 5. A
 6. B
 7. C
 8. D
 9. C
 10. D
 11. C
 12. A
 13. C
 14. B
 15. D
 16. D
 17. A
 18. C
 19. B
 20. A
 21. D
 22. B
 23. C
 24. A
 25. D
 26. A
 27. C
 28. D
 29. D
 30. C
 31. C
 32. D
 33. A
 34. B
 35. D
 36. A
 37. C
 38. A
 39. D
 40. A
 41. C
 42. D
 43. B
 44. A
 45. B
 46. D
 47. D
 48. A
 49. B
 50. A
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers KCPE 2022 Prediction Papers Set 3.


Tap Here to Download for 30/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students