Tuesday, 30 August 2022 13:37

Kiswahili Questions and Answers - CBC Grade 6 End of Term 2 Exams 2022 Set 2

Share via Whatsapp

MASWALI

Swali la 1 hadi 5. soma mazungumzo haya kisha ujibu maswali.

d1

Mbula: Shikamoo mama?

Mama: Marahaba mwanangu. Umeamkaje?

Mbula: Vyema. Mbona leo umerauka mapema hivyo?

Mama: (Akimwonyesha kalenda) Umesahau leo ni Madaraka Dei?

Mbula: Nilidhani kuwa ni kesho Jumapili!

Mama: Ni muhimu kila mzalendo kushiriki katika sherehe za kitaifa.

Mbula: Asante kwa kunipasha. Sherehe za leo zinaongozwa na nani?

Mama: Zitaongozwa na kiongozi wa kaunti. Unafahamu jina la cheo chake?

Mbula: Naam, Gavana.

Mama: Vizuri sana mwanangu. Ungetaka kuandamana nami?

Mbula: Bila shaka. Sitabaki nyuma.

Mama: Jiandae haraka kwa vile chelewa chelewa utampata mwana si wako.

Mbula: Sawa mama (Anaondoka)

  1. Kwa nini mama aliamka mapema siku hiyo?
    1. Ni mazoea yake 
    2. Ili kujiandaa kuenda kanisani 
    3. Ili kujiandaa kuenda siku ya Madaraka 
    4. Ili kutayarisha kiamsha kinywa
  2.  Hatua ya mama na Mbula kuamua kuenda kuhudhuria sikukuu ya Madaraka inaonyesha kuwa wana
    1. uzalengo 
    2. bidii 
    3. heshima 
    4. hekima.
  3. Mazungumzo haya yalifanywa siku ya gani? 
    1. Jumanne 
    2. Ijumaa 
    3. Jumapili 
    4. Jumamosi
  4. Chelewa chelewa utampata mwana si wako ni aina ya 
    1. tashbihi 
    2. Nahau 
    3. methali
    4.  tanakali
  5. Kiongozi wa nchi huitwa 
    1. Gavana
    2. Rais
    3. Seneta
    4. Chifu 

Swali la 6 - 12. soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali 

Ni makosa kudhulumu, binadamu duniani
Ni hatia kuhukumu, kwa udhalimu kortini
Ni vyema unapodumu, u mzuri duniani
Tenda wema nenda zako, Jalali atakulipa

Maisha yawe magumu, usiwe mwongo moyoni,
Jikuzeni humu humu, ukinge umaskini,
Ni busara kuhudumu, kwa nia safi mtimani,
Tenda mema nenda zako, Jalali atakulipa.

  1. Shairi hili ni la aina gani?
    1. Tathlitha
    2. Tarbia
    3. Tathnia
    4. Takhmisa
  2. Kila mshororo wa shairi hili una mizani ngapi? 
    1. 16 
    2. 8
    3. 32
    4. 64
  3. Ujumbe wa shairi hili ni kuhusu
    1.  kuwa na bidii pekee 
    2. kuwa mnafiki 
    3. kuwa na utu 
    4. kuwa na heshima pekee
  4. Neno jingine lenye maana sawa na Jalali ni 
    1. rafiki
    2. ndugu
    3. jirani
    4. Mungu
  5. Mshororo wa pili katika kila ubeti huitwa
    1. mwanzo 
    2. mloto
    3. mleo
    4. Kibwagizo
  6. Shairi hili lina beti ngapi? 
    1. Mbili
    2. Tatu 
    3. Nne
    4. Moja
  7. Andiku ukwupi wu nishur uro wu pili ubeti wa kwanza 
    1. Ni vyema unapodumu 
    2. Jikazeni humu humu 
    3. Ni hatia kuhukumu 
    4. Kwa udhalimu kortini

Swali la 13 hadi 15. Soma kifungu hiki kisha ujibu maswali

d2

Kimeu, Ngina, Mwende na Misha walimtembelea mwulimu wuo majilisini. Mwalimu Mumo alikuwa na kazi nyingi ya kuandaa somo. Alikuwa akichora chati kuhusu misimu tofauti.
Wanafunzi hao walimsaidia mwalimu wao katika shughuli hiyo. Kimeu Misha na Nginn walijaza kalamu rangi. Kimeu na Mwende walisaidia kuchora chati. Wote isipokuwa Ngina walisaidia kupaka rangi. Kimeu alisaidia kusafisha eneo la kufanyia kazi nao wasichana wute wakasaidia kuanika chati ukutani. 

  1. Mwalimu alikuwa akifanyia kazi wapi?
    1. Darasani
    2. Majilisini 
    3. Uwanjani 
    4. Ofisini
  2. Ni mwanafunzi yupi hakuanika chati ukutani?
    1. Ngina
    2. Mwende
    3. Misha
    4. Kimeu
  3. Mwende alifanya kazi ngapi kwa jumla?
    1. Tatu
    2. Mbili
    3. Nne
    4. Moja

Swali la 16 hadi 20. soma fungu kate na ulaze natasi kwa ibu sahihi
Wakazi wa kijiji                      16                         wana uhusiano                     17                        . Wana bidii kama                      18                         kazini. Wamepanda miti                     19                         ili kuyatunza mazingira. Katika msimu wa                      20                         wao huwa hawahisi jua kali sana kama ilivyokuwa zamani kabla ya kupanda miti hiyo.

  1.                        
    1. wetu
    2. yetu
    3. letu
    4. chetu
  2.                  
    1. mzuri 
    2. zuri
    3. wazuri
    4. uzuri
  3.                      
    1. kunguru
    2. kondoo
    3. mchwa
    4. njiwa
  4.                
    1. mingi
    2. mengi
    3. wingi
    4. nyingi
  5.                  
    1. masika
    2. kiangazi
    3. vuli
    4. choo

Chagua jibu sahihi kujibu maswali

  1. Kinyume cha neno 'tamu' ni
    1. chungu
    2. kali
    3. mbaya
    4. chachu
  2. Mtu anayetunga mashairi huitwa
    1. manju
    2. malenya
    3. mwandishi
    4. mtunzi
  3. Chagua neno lililo katika ngeli ya YA-YA.
    1. magonjwa 
    2. mazingira
    3. matunda
    4. ukuta
  4. Chagua jibu linaloonyesha wingi wa 'uso wangu umeoshwa' 
    1. Nyuso zangu zimeoshwa
    2. Nyuso zao zimeoshwa 
    3. Nyuso zetu zimeoshwa
    4. Uso yetu umeoshwa
  5. Chagua jibu lenye visawe
    1. Furaha - huzuni
    2. Hongo - rushwa
    3. Mshindi - mshinde
    4. Mtu - jibu
  6. Chagua sentensi iliyoakifishwa vizuri
    1. Ala nimeona jitu kubwa sana.
    2. Mama: alinunua embe tomoko na chungwa
    3. Je, Leo ni siku gani
    4. Hoyee! Tumeshinda mbio hizo.
  7. Neno 'mtoto katika ukubwa ni
    1. jitoto 
    2. kitoto
    3. toto
    4. litoto
  8. Chagua methali inayoonyehsa ushirikiano
    1. Mtaka cha mvunguni sharti ainame
    2. Jifya moja haliinjiki chungu
    3. Mchagua jembe si mkulima
    4. Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo
  9. Ni pambo lipi huvaliwa shingoni?
    1. Mkufu
    2. Pete
    3. Herini
    4. Kipini
  10. Tumia kivumishi kirejeshi amba-kukamilisha sentensi:
    Mpira                                     ulinunuliwa umepasuka 
    1. ambao
    2. ambayo
    3. ambacho
    4. ambalo 

KUANDIKA INSHA

Andika insha kuhusu;
Andikia mwalimu mkuu wa shule yako barua rasmi ukiomba ruhusa kujiunga na kikundi cha wanaskauti shuleni:

MWONGOZO WA KUSAHISHA

swa marking scheme

COMPOSITION / INSHA MARKING SCHEME

  1. The composition will be assessed according to the following guidelines. 
  2. The maximum mark will be 40 and the minimum mark 01.
    Does the script show that the candidate can communicate accurately, fluently and imaginatively in Englis

Accuracy (16 marks)

  1. Correct tense and agreement of verbs 
  2. Accurate use of vocabulary (4 marks)
  3. Correct spelling (4 marks)
  4. Correct punctuation (4 marks)

Fluency (16 marks)

  1. Correct flow of the story (4 marks) 
  2. Well sequenced sentence and connected paragraphs (4 marks
  3. Correct spelling (4 marks)
  4. Ideas developed in logic sequence (4 marks)

Imagination (8 marks)

  1. Unusual but appropriate use of words (4 marks)
  2. Variety of structure (4 marks)

NB: Please teachers are requested to scrutinize this marking scheme before use, it is worth

Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - CBC Grade 6 End of Term 2 Exams 2022 Set 2.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students