Tuesday, 30 August 2022 07:04

Kiswahili Questions and Answers KCPE 2022 Prediction Papers Set 4

Share via Whatsapp

Maswali

Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi tumepewa majibu manne hapo. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya pale uliyopewa

Bwana Hamisi ni seremala     1    sana katika mtaa wetu. Ana     2    kubwa ambapo yeye huundia samani maridadi sana. Ufikapo hapo, hutakosa kuviona vifaa mbalimbali, kama vile     3    wanaonunua katika kazi yake.     4     vijana wengi wanaokosa karo kumwendea kwa mafunzo ili waweze kujitegemea baadaye. Yeye pia ana     5     maadamu. huwapa vijana hawa ujira kila jioni ili nao wajiendeshee maisha yao. Sifa zake     6     kote mtaani. Hupenda kusema kuwa siri ya maisha ni bidii huku akihimiza kuwa     7    .Vijulanga   8    na uhaba wa kazi     9    nchini hayana budi kuiga mfano wake.

  A B C D
1  hatari  maalum  mahiri   marufuku
2  karakana  kiwanda  maabara  ofisi
3  kekee, fuawe, kembeo na pinamaji  utepe bisibisi, jiriwa na patasi  vipuli, mvukuto, timazi na nyundo  msumeno, kekee , chelezo na mvuo
4  Kwani   Lakini   Ijapokuwa  Aghalabu
5  mkono wazi  mkono birika  mkono mzuri   mkono mwepesi
6  zimesambaratika  zimetanda    zimesheni  zimetalii
7  ukipanda upepo utavuna tufani  bandu bandu humaliza gogo  cha kuzama hakina rubani  mgagaa n aupwa haondoki patupu
8  waliadhirika  walioathiriwa  walioadhiriwa  walioathirika
9  kote  wote  zote  yote


Vita     10   niliadarretsi vya     11    mzaha hata kidogo. Hili ni janga linalotishia kuwasomba vijana kwa mkupuo nimoja. Wakwasi wenye    12   wa darahima wanawauzia wana wetu sumu kali bila kujali lolote. Wavyele ambao    13    kuwa    14    cha kuigwa nao wamejitia hamauzo kucheza ngoma watakazo. Si ajabu kuinwona baba au mama akirejea mastakimumi huku amelewa kama     15     tha kwanza kuwafokea wanawe.

  A B C D
10  juu ya   baina ya   dhidi ya  kutokana na 
11   kufanya  kufanyiwa  kufanyia  kufanywa
12  umero  tamaa  shauku  ukata
13  watarajwa  wangetarajiwa  walitarajiwa  wanatarajiwa
14  kielezi  kielelezo  chombo  chelezo
15  pombe  mjinga  komba  nyani


Kuanzia swali la 16 mpaka 30, ibu kila swali kulingana na maagizo uliyopewa.

 1. Kati ya viteuzi vifuatavyo, kipi kinaonyesha kuendelea kwa kitendo?
  1. Jua lachoma vikali leo.
  2. Walizioka keki tamu wakaziuza,
  3. Ukifanya bidii utapita mtihani.
  4. Tulikuwa tukitembea mvua ilipoanza kunyesha.
 2. Ni orodha gani inayoonyesha viclczi pekee?
  1. Mombasa, kesho, vibaya, kila siku.
  2. Kwake, zuri, polepole, chochote.
  3. Vigumu, baya, kubwa, aghalabu.
  4. Baada ya vyote, taratibu, chekesha.
 3. Mibuni hutupatia kahawa. Je, mibono huzaa nini?
  1. Mabono
  2. Mbarika
  3. Tunguja
  4. Kanju
 4. Tegua kitendawili kifuatacho:
  Iluwafanya watu walie huku wakicheka.
  1. Kifo
  2. Pilipili mboga
  3. Kiboko.
  4. Moshi
 5. Tambulisha sentencsi iliyoaki fishwa barabara.
  1. Ala? Kumbe unaishi katika mji huu!
  2. Je? Huu ni uungwana kweli?
  3. Nilipofika huko sikumpata; alikuwa amesafiri.
  4. Tafadhali niletec, maji, sabuni, dodoki
 6. Maelezo yapi hayana maana ya panga?
  1. Kaa mahali kwa makubaliano fulani.
  2. Chombo cha kuleta baridi kinachozungushwa na umeme
  3. Weka vitu kwa utaratibu mzuri.
  4. Mahali maalum pa kufanyia matambiko.
 7. Badili sentensi ifuatayo katika ngeli ya PA-KU-MU.
  Shule yao ina wanafunzi wengi.
  1.  Shule zao zina wanafunzi wengi.
  2. Shudeni mwao kuna wanafunzi wengi.
  3. Shuleni pao mna wanafunzi wengi.
  4. Shuleni mwao mna wanafunzi wengi..
 8. Upi ni usemi wa taarifu wa senteni hii...!
  Mama alisema, “Tafadhali niwashic jiko .. nitelekechungu".
  1. Mama alimwomba amwashie jiko ili ateleke chungu.
  2. Mama aliagiza awashiwejiko ili atelcke chungu.
  3. Mama alisema angewashiwa jiko angeteleka chungu.
  4. Mama aliin wambia amwashie jiko wateleke chungu.
 9. Andika udogo wa:
  Mlango mpana umefunguka.
  1. Lango pana limefunguka.
  2. Jilango pana limefunguka.
  3. Kilango kipana kimefunguka.
  4. Kijilango kipana kimefunguka.
 10. Kanusha sentensi ifuatayo kwa usahihi:
  Maji yasingepatikana upesi mifugo yetu ingcangamia.
  1. Maji yangalipatikana upesi mifuo yetu isingeangamia.
  2. Maji yangepatikana upesi mifugo yetu isingeangamia.
  3. Maji yasingepatikana upesi mifugo yetu isingeangamia.
  4. Maji yangepatikana upesi mifuo yetu ingeangamia.
 11. "Gao huwa chombo wakatiwe" ni kwa wanziovidharau vitu vikuu; kama vile uncler la muwa la jana chungukaona kivuno"ni kwa wale
  1. wanaovidharu vitu vidogo.
  2. wanaopuuza msaada mkubwa.
  3. wanaopuuza mali ya wengine.
  4. wanaotamani mali ya wengine.
 12. Ugonjwa wa macho unaoweza kusababisha upofuni
  1. ukoma
  2. inachapwi
  3. trakoma
  4. alkani
 13. Ni sentensi ipi iliyo na kivunishi cha pekee?
  1. Wazee wengi walitou micliango yao.
  2. Wazee wale walitoa michango yao.
  3. Wazee wenu walitoa michango mizuri.
  4. Wazee wengine walitoa michango mikubwa.
 14. Mtu anayeongea kwa richa ya ulimi huitwa
  1. kithembe
  2. kigugumizi
  3. kiduko
  4. kiduvya
 15. Kamilisha kwa ufasaha:
  Mtoto huyu, huyo na Yule
  1. mnifuate
  2. wazifuate
  3. anifuate
  4. tufuate

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 31 – 40

Bwana Aisee aliporejea jijini alifungua ofisi kubwa aliyoipamba kwa samani za hali ya juu. Kisha aliwasiliana na waandishi wa magazeti mbalimbali. Alidai kuwa kulikuwako na mradi kabambe wa kuhakikisha kuwa vijana waliokosa amali wangeajiriwa kazi za maana kwenye hoteli za kitalii huko Uarabuni na Ulaya na hata kwenye meli za kifahari. Viongozi wengi walimshehenezea Bwana Aisee sifa kemkemu, “Huyu ni mzalendo kindakindaki! Anawakumbuka raia wenzake ambao hawana bahati kama yeye!"Vijulanga waliokuwa na hamu na ghamı ya kuenda ugenini walifurika ilipokuwa ofisi yake.

Walichohitajika kufanya tu ni kulipa ada ya shilingi elfu tano pamoja na kiasi kingine kama hicho kugharimia vyeti vya usafiri. Licha ya kuwa wengi wao hawakuwa na namna ya kuzipata pesa hizo, walikuwa radhi kukopa wahakikishe kuwa wamepata nafasi hizo adimu. Vijana hao pia walitakiwa kuenda hospitali fulani ya kibinafsi kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu. "Aisee bwana, huo ndio ustaarabu wa wenzetu walioendelea.. Ukitaka kumwajiri mtu lazima uijue siha yake ikoje," Bwana Aisee. aliwakumbusha. Hamna aliyejali. Kilichokuwa muhimu ni kuwa, baada ya miezi miwili wangepata kazi ambazo zingewafanya waipige kumbo la milele ukata uliotishia kuwagubika kama wingu.

Baada ya kuzikusanya hela hizo zilizolipwa na vijana zaidi ya elfu thelathini, Bwana Aisee aliwaambia wangoje kwa muda wa miezi miwili. Muda waliokuwa wamepewa wa kungoja mambo yaive ukapita. Tarehe ya kusafiri kuenda kuanza kazi zao ikaahirishwa. Taarifa iliyotoka katika ofisi kuu huko ulaya ilidai kuwa kuahirishwa huko kalitokana na hali mbaya ya usalama. Tarehe hizo zilipokwisha kuahirishwa mara nyingine mbili, kila mmoja alianza kutuhumu kuwa palikuwa na jambo. Malalamishi ya kila aina yalianza kusikika kwenye vyombo vya habari. Wakaanza kumsaka Bwana Aisee. Lakini hawakujua kumbe bwana huyo alikuwa ameingia mitini.

Uchunguzi wa historia ya Bwana Aisee ulianza kufanywa. Jamaa waliosoma naye walitoa habari zake zote bila kusaza lolote. Walieleza jinsi alivyokua fundi wa kuongea kizungu. "Lakini huyu si fundi wa kizungu tu bali na mizungu pia!" Walisema wengine kwa hasira walipozisikia habari hizo. Serikali ilianza mipango kabambe ya kumsaka Bwana Aisee. Ilibidi kuwashirikisha wachunguzi wa polisi wa. kimataifa, INTERPOL, katika swala zima. Haikuchukua muda kabla ya kugunduliwa kuwa mashirika yaliyodaiwa kuhusika na suala la ajira hizo yalikuwa bandia.

Mambo yaliendelea kukanganya wakati ofisi ya Bwana Aisee iliyokuwa jijini ilipochomeka siku moja wakati wa usiku na vyeti vyote kuteketea. Nayo hospitali waliyokuwa wameenda kufanyiwa uchunguzi wa kiafya wale walioenda kuomba kazi ilifungwa ghafla na daktari aliyehusika kutoweka. Ilikuwa wazi sasa kuwa watu walikuwa wametapeliwa.

Kashfa hii ilizungumziwa na wengi kote nchini si katika redio wala runinga bali pia magazetini na kwingineko. Adinasi waliapiza. Lakini njia ya mwongo ni fupi. Aisee alibambwa na polisi wa kimataifa alipokuwakatika uwanja wa ndege wa Frankfurt huko Ujerumani akijitayarisha kuabiri ndege kuelekea Afghanistan alikopanga kujificha kwa muda hadi mambo yatulie.

Baada ya kutiwa mikononi, Bwana Aisee alisafirishwa chini ya ulinzi mkali hadi jijini Nairobi alipofikishwa mbele ya hakimu. Kesi yake ilihudhuriwa na mamia ya vijana waliohasirika. Mwishowe Bwana Aisee alitumbukizwa gerezani kwa miaka minane ikiandamana na kazi za sulubu. Mizungu yake ilikuwa imegota mwamba.

 1.  Lengo la Bwana Aisee kuwasiliana na wanahabari lilikuwa ni
  1. kuwafahamisha kuhusu ofisi yake.
  2. kuwaeleza kuhusu mradi wake.
  3. kutoa tangazo kuhusu mradi wake
  4. kutoa tangazo kuhusu ofisi yake.
 2. Wengi waliosikia kuhusu mipango ya Bwana Aisec . .. .
  1. walimsifu kuwa mpenzi kamili wa nchi yake.
  2. walimwona kama adui mkubwa wa nchi.
  3. walimsifu kwa kuleta mapinduzi nchini:
  4. walimshuku kuhusu nia ya kazi yake,
 3. ni kusajiliwa kila mhusika atihitaji kulipa shilingi elfu
  1. tano, kufanyiwa uchunguzi wa kiafya.
  2. kumi, kuchangazwa afya yake.
  3. tano, kuwasilisha vyoli vya usafiri.
  4. kumi, vyeti vya usafiri na kuchungu wa
 4. Watu walianza kutuhumu kuwa mambo hayakuwa sawa
  1. baada ya tarehe ya kuanza kazi kuahirishwa.
  2. tarehe ya kusafisi ilipoahirishwa tena,
  3. Bwana Aisec alipotoweka kutoka jijini.
  4. tarehe ya usafiri ilipoahirishwa kwa mara ya tatu. .
 5. bwana huyo alikuwa ameingia mitini' maana yake ni kuwa alikuwa
  1. ametoweka haada ya kufanya uhalifu.
  2. ameshiriki uhalifu wa kuibia umma..
  3. ameshepatwa na mabaya.
  4. amijitia katika mambo asiyoyafahamu.
 6. Historia ya Bwana Aisee ilibainisha kuwa alikuwa na hulka ya
  1. kuwaibia watu
  2. kusema kimombo
  3. kusafiri uarabuni
  4. kuwapenda watu
 7. Inaonekana kuwa asiki ya kuchomeka kwa olisi ya Bwana Aisee ilikuwa
  1. kuficha laistoria yake.
  2. hasira za vijana walioibiwa.
  3. kuharibu ushahidi dhidi yake.
  4. harakati polisi wa INTERPOL.
 8. Badala ya kusema alibambwa, pia tunaweza kusema
  1. alibakwa
  2. alinaswa
  3. alikahwa
  4. alionekana
 9. Kulingana na makala haya, Bwana Aisee alikuwa
  1. jangili
  2. jambazi
  3. mkwepuzi
  4. lapeli
 10. Kichwa mwalaka kwa makala haya ni ...
  1. Wajinga ndio waliwao.
  2. Akili nyingi huondoa maunlai
  3. Alive juu mgojec chini.
  4. Mbio za sakafuni huishia ukingoni,

Soma makala yafuatayo kisha wjibu maswali 41-50

Tarakilishi ama kompyutani kati ya teknoloji mpya ambayo inatumiwa siku hizi karibu kila mahali mathalani katika kampuni kubwakubwa, benki, masoko makubwa, viwandani, viwanja vya ndege, meli, idara za serikali, vyuo, shuleni na kadhalika. Katika shule za upili, tarakilishi ni somo ambalo. linashughulikiwa kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne na hutahiniwa katika mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne. Aidha, serikali iko katika harakati za kuwapa vipakatalishi wanafunzi wote wa darasa la kwanza katika shule zote za umma nchini. . .....

Tarakilishi imegawanyika katika sehemu mbili muhimu, programu mfumo na maunzi. Maunzi ni : nenojumlishi ambalo hutumika kwa kurejeleavifaa vyote vya kompyuta kwa mfano kichapishi, kishalekezi. kiwambo au skrini, kipanya m mashine chapishi. Programu mfumo ni neno jumlishi ambalo hurejelea programu zote zinazoweza kutumika katika kompyuta.

Vifaa vinavyotumika katika kompyuta ni vingi. Kiwambo hutumika kwa kuonyesha data ambayo inashughulikiwa, nacho kichapishi hutumika katika kuvugulia data hiyo kwa kompyuta. Kishelekezi ni kifaa ambacho huwaka kikizimika kwenye skrini nacho huashiria mahali ambapo data inayovuguliwa itaingia. Pahali pa kishalekezi panaweza kubadilishwa kwa kutumia kipanya. Kipanya ni kidude chenye mkia mithili ya panya. Baada ya kazi kukamilika nadata kuwa habari mashine chapishi huichapisha. habari hiyo kwenye karatasi ili isomwe na watu wengi iwezekanavyo, pahali penginapahali popote.

Tarakilishi ina sifa nyingi muhimu. Chombo hiki kina uwezo wa kufanya hesabu na kazi nyinginezo kwa kasi sana. Sifa nyingine ni kwamba tarakilishi huhifadhi ujumbe mwingi sana kwa matumizi ya baadaye. Maclekezo huchukuliwa na kuwekwa kwa ajili ya kufuatwana chombo hiki. Mfululizo wa maelekezo haya ndiyo huongoza kompyuta katika wajibu wake na huitwa programu ambayo huandikwa kwa letgha ya kikompyuta. Kompyuta hufuata maelekezo haya kwa kuamshwa na binadamu. Sheria hizi huwa sahili na kompyuta ina uwezo wa kuzitumia ili kufikia uamuzi wa jinsi ya kutenda

Kuwasiliana na mifumo minginc yakompyutani muhimu sana na kompyuta ina uwezo wa kufanya hivyo. Kompyuta huingizwa data ambayo huchakatwa ili kuleta maana, na uzao wa kuchakatwa huku ndio huitwa habari. Programu ni mfumo wa utaratibu ambao umeandikwa kwa lugha ya kikompyuta. Programu huiwezesha kompyuta kuchakata data na kuifanya iwe habari kwa mfano, inaweza kuongeza rumbari mbili au zaidi na kukupa jibu.

Katika kompyuta habari inaweza kuhifadhiwa katika diski ngumu au diski tepetevu. Diskingumu ni nafasi inayopatikana katika kompyuta yenyewe na inaweza kuhifadhi maktaba inzima. Diski tepetevu niile nafasi ambamo disketi huwekwa ili habari inayochakatwa ihifadhiwe kwa disketi. Disketi ni kilaa kidogo mithili ya kaseti. Nafasi hizi za kompyuta zimegawanywa katika viendesha diski kwa mfano ukitaka kuhifadhi habari yako katika diski ngumu, utatumia kiendesha diski A. Ilhali ukitaka kuhifadhi kazi yako katika diski tepetevu utatumia kiendesha diski C.

Kwa hivyo kwa muhtasvi, tunaweza kusema kuwa kompyuta ni kifaa au chombo ambacho hufanya kazi kwa kuongozwa na programu iliyohifadhiwa. Kompyuta hujiendesha yenyewe kwa kukubali na kuchakata data ili iwe habari.

 1. Kulingana na makala tarakilishi hutunika
  1. benkini, viwanjani, shuleni na idara za serikali.
  2. benki kubwa, shule zote, viwanjani na sokoni.
  3. masoko makubwa, viwanja vya ndege, benkini na vyuoni.
  4. mashambani, shuleni, vyuoni na nyanjani.
 2. Vipakatalishi vitatolewa kwa wanafunzi
  1. wote wa shule za umma.
  2.  wote wa darasa la kwanza.
  3. wa kidato cha kwanza hadi cha nne.
  4. wa darasa la kwanza katika shule za ..umma.
 3. Mfano wa maunzi katika kompyuta ni
  1. programu, kiwambo, kishalekezi, kipanya.
  2. baobonye, mulishi, kipanya, kishalekezi.
  3. baobonye, programu, data, disketi ngumu.
  4. data, diski, tepelevy, skrini, kipanya
 4. Sehemu kuu za kompyuta kulingana na makala haya ni ngapi?
  1. Mbili
  2. Tatu
  3. Таnо
  4. Sita
 5. Umuhimu wa kompyuta ni kuwa
  1. hufanya kazi kwa kasi, huhifadhi ujumbe mwingi.
  2. hurahisisha kazi, hutumia nguzu za umeme.
  3. huongozwa na programu wala si mwanadamu.
  4. ina akili hata kuliko binadamu, ni rahisi kutumia.
 6. Sheria hizi huwa sahili, maana yake ni kuwa huwa
  1. chache
  2. nyingi
  3. rahisi
  4. ngumu
 7. Kulingana na makala haya habari hupatikaria baada ya
  1. kuhifadhiwa kwenye diski yoyote.
  2. data kuingizwa na kuchakatwa.
  3. kupelekwa kwa watangazaji.
  4. kufikia hadhira iliyolengwa: .
 8. Watu pia hutumia tarakilishi kuwasiliana kwa njia ya .
  1. kipepesi
  2. simutamba
  3. nyaraka 
  4. barua pepe
 9. Lengo la kuchapisha maandishi kwenye karatasi ni kuwa itaweza
  1. kusomwa na yeyote.
  2. kusomewa mahali popote.
  3. kufanyiwa marekebisho.
  4. kusomwa kwa vyovyote.
 10. Kichwa ki faacho kwa makala haya ni:
  1. Sehemu za tarakilishi.
  2. Teknolojia ya kisasa.
  3. Manufaa ya kompyuta.
  4. Jinsi ya kutumia kompyuta.

INSHA

Umepewa dakika 40 kuandika insha yako.
Andika insha isiyopungua ukurasa mmoja na nusu kulingana mna mada uliyopewa.

MADHARA YA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA

Majibu

 1. C
 2. A
 3. B
 4. D
 5. A
 6. C
 7. D
 8. B
 9. A
 10. C
 11. B
 12. A
 13. D
 14. B
 15. C
 16. D
 17. A
 18. B
 19. D
 20. C
 21. B
 22. D
 23. A
 24. C
 25. B
 26. A
 27. C
 28. D
 29. A
 30. B
 31. C
 32. A
 33. B
 34. D
 35. A
 36. B
 37. C
 38. B
 39. D
 40. D
 41. C
 42. D
 43. B
 44. A
 45. A
 46. C
 47. B
 48. D
 49. B
 50. A
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers KCPE 2022 Prediction Papers Set 4.


Tap Here to Download for 30/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students