Tuesday, 30 August 2022 13:37

Kiswahili Questions and Answers - Grade 5 End of Term 2 CBC Exams 2022 Set 1

Share via Whatsapp

Some mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswall 1-5.

(Mwalimu na wanafunzi wanajadiliana kuhusu umuhimu wa kuyatunza mazingira)

Mwalimu:     Hamjambo wanafunzi?
Wanafunzi:  (Wakiamka sawia) Hatujambo mwalimu, shikamoo.
Mwalimu:    Marahaba (Anawaashiria wakae. Wote wanaketi na kushukuru.) Naam, leo ningependa tuzungumze kuhusu namna na umuhimu wa kuyatunza mazingira kwa hivyo...
Matayo:       (Anaunyanyua mkono wake) Samahani mwalimu, mazingira ni nini?
Mwalimu:    (Akitabasamu) Matayo huishi vituko! Ndilo nililotaka kueleza. Mazingira ni yale yote yanayotuzunguka. Hebu pendekezeni njia mbalimbali za kuyatunza mazingira
Manyanga: Nadhani ni vyema kukata nyasi ndefu ili kuharibu makao ya mbu.
Kaisari:       Ni vyema pia kutunza vyanzo vya maji kama vile mito, chemichemi, mabwawa na maziwa.
Pendo:        Nikiongezea, si vyema kutumia mbolea nyingi zaidi hasa za madukani ili tusiyaathiri maji na udongo.
Mwalimu:    Nimefurahia mno michango yenu. Zipo njia nyingi za kuyatunza mazingira. Kimsingi, umuhimu wa kuyatunza mazingira ni kuwafanya viumbe waishi maisha salama.

  1. Mazungumzo haya yaliandaliwa majira ya saa ngapi? 
    1.  Saa sita adhuhuri. 
    2.  Saa mbili asubuhi. 
    3.  Saa kumi jioni. 
    4. Hatujaelezwa.
  2. Ili kuonyesha heshima kuu, mwalimu alipowaamkia wanafunzi, wote 
    1. walisimama ili kupokea salamu yake.
    2. walitaka kuchangia katika majadiliano 
    3.  walitaka kujua maana ya mazingira.
    4. walitaja umuhimu wa kuishi katika mazingira safi.
  3. Ni mwanafunzi yupi aliyemkatiza mwalimu alipokuwa akiongea?
    1. Manyanga .
    2. Matayo
    3. Kaisari
    4. Pendo
  4. Kulingana na mazungumzo haya, yote yanayotuzunguka ndiyo   
    1. mazingara.
    2. hewa.
    3.  miti.
    4. mazingira. 
  5. Mwishoni, mwalimu alifurahishwa na nini?
    1. Heshima ya wanafunzi wake.
    2. Umuhimu wa kuyatunza mazingira.
    3. Michango ya wanafunzi wake.
    4. Njia mbalimbali za kuyatunza mazingira.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 6 hadi 8.

Siku moja paka na mbwa walienda karamuni. Mwenyeji wao, panya, aliwakaribisha kwa mikono miwili. Wageni waliketi sebuleni kwenye makochi maridadi, mekundu, kama damu.

“Habari za mtokako?" Panya aliwaamkia wageni kwa heshima. "Njema sana!” wageni walijibu pamoja huku wakitabasamu. Baadaye, panya aliwasha runinga na kuwaambia wageni wake, “Tazameni televisheni. Mimi naelekea mekoni kuwapikia chakula.” Mara, huyoo! Akaenda jikoni. Haraka, alipika nyama na kuitia mchuzi wa maziwa.

  1. Paka na mbwa waliandaliwa nini na mwenyeji wao?
    1. Nyama na maziwa
    2. Njugu na maziwa.
    3. Maziwa na mifupa.
    4. Chai na nyama.
  2. Kabla ya panya kuelekea mekoni,
    1. aliwaandalia wageni wake chakula.
    2. aliwasha televisheni.
    3. alipika nyama.
    4. alitia maziwa katika nyama.
  3. Panya alienda jikoni 
    1. kuwasha runinga.
    2. kununua chakula.
    3. kupika chakula. 
    4. kuwakaribisha wageni.
  4. Kati ya hawa, ni mnyama yupi hajatajwa katika ufahamu?
    1. Paka
    2. Panya
    3. Mbwa
    4. Sungura

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 9 hadi 12. 

Lengo la elimu ni kumsaidia mtoto kukuza ujuzi na vipawa na kukuza maadili ya maisha pamoja na maisha ya kiroho. Leo, mwalimu si mkufunzi au msimamizi bali ni msaidizi na mwelekezi. Hapa, mwalimu hudokeza au kutoa habari za juujuu tu. Ni jukumu la mwanafunzi kuleta umakinifu na kutafuta undani wa habari za mwalimu. Bila shaka, mwalimu anatarajiwa kumsaidia mwanafunzi katika kuufikia undani huo. Mwalimu hampi mwanafunzi ujuzi wowote bali humwonyesha jinsi anavyoweza kuupata ujuzi yeye mwenyewe. Mtoto anapozaliwa, ujuzi huwa ndani yake nao husubiri kuamshwa. Mwalimu amwonyeshe mtoto pale ujuzi ulipo na jinsi anavyoweza kuufanyia mazoezi hadi utokeze vilivyo na kumfaa.

  1. Kulingana na kifungu, baada ya mwalimu kudokeza jambo fulani, mwanafunzi 
    1. atatafuta ukweli kulihusu. 
    2. atamtegemea katika kila jambo.
    3. ataweza kupita vizuri katika mitihani.
    4. atashindwa kabisa kumwelewa.
  2. Kabla ya ujuzi ulio ndani ya mtoto kuonekana, ni lazima ujuzi huo
    1. uongozwe.
    2. uamshwe.
    3. utokeze.
    4. ugunduliwe.
  3. Katika miaka ya sasa, mwalimu ni
    1. mkufunzi na msimamizi.
    2. msaidizi na mkufunzi.
    3. mwelekezi na msimamizi.
    4. mwelekezi na msaidizi.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 13 hadi 15. 

Serikali ya nchi hii inawataka watoto wote wapelekwe shuleni wakasome kwa sababu masomo ndio ufunguo wa maisha. Watu wanaowaajiri watoto hata wasisome wanafaa kuhukumiwa ili kupunguza maovu kama hayo.

Mtoto ambaye hana elimu siku hizi huwa na shida nyingi kupita kiasi kwa sababu hawezi kupata ajira nzuri ukubwani. Hii ndiyo sababu serikali inahimiza kila mtoto kupata elimu. Zamani, watoto hawakuwa wakisoma kwa sababu hawakujua umuhimu wa elimu maishani
mwao.

Ili kuzuia magonjwa na njaa, elimu huwa muhimu. Ili kudumisha adabu njema na nidhamu, elimu huwa lazima. Watoto waliolemewa na masomo huwa wa kurandaranda mitaani, wezi au watendaji wa mambo mabaya katika jamii. 

  1. Ni gani si kweli kulingana na taarifa?
    1. Masomo ni muhimu maishani.
    2. Serikali inataka watoto wote wasome.
    3. Zamani, watoto wote walisoma.
    4. Ni vyema kuwaelimisha watoto.
  2. Kulingana na kifungu, mtoto ambaye hana elimu siku hizi 
    1. huwa na shida. 
    2. hupendwa na wengi.
    3. hupata kazi.
    4. huajiriwa.
  3. Katika aya ya mwisho, tumeambiwa kuwa watoto wasiosoma huweza kuwa 
    1. wezi na wafanyakazi. 
    2. wa kurandaranda na wenye bidii. 
    3. wenye bidii na wezi. 
    4. wa kurandaranda na wezi. 

Soma kifungu kifuatacho. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa  

Siku hiyo tulikuwa tumeingoja kwa hamu na ghamu. Sote tulifika ____16____ na mapema tukiwa tayari kuabiri ____17____ kuelekea mjini Mwambasani. Hii ilikuwa mara yangu ya ____18____ kuenda huko. Sikuwa nimewahi kwenda huko. Tuliingia ____19____ tukiwa na furaha sana. Mara dereva alilitia gari ufunguo na safari _____20_____

  1.  
    1. asubuhi
    2. jioni
    3. adhuhuri
    4. usiku
  2.  
    1. baiskeli
    2. basi
    3. ndege
    4. meli
  3.  
    1. moja
    2. mwisho
    3. tatu
    4. kwanza
  4.  
    1. njiani
    2. safari
    3. basini
    4. barabarani 
  5.  
    1. ikaanza
    2. ukaisha
    3. ikaendelea
    4. ukaanza

Katika swali la 21-30, jibu swali kulingana na maagizo uliyopewa.

  1.  Kati ya hizi, ni nomino ipi isiyo katika ngeli ya U-ZI?
    1. Uteo
    2. Uzi 
    3. Upishi
    4. Ufunguo.
  2. Tulimwona batamzinga akiogelea bwawani. Nomino iliyopigiwa mstari ni 
    1.  nominoambata.
    2. nomino ya wingi. 
    3.  nomino dhahania.
    4. nomino kitenzi jina.
  3. Kati ya maneno uliyopewa, ni lipi litakuwa la pili katika kamusi? 
    1. Mshikaki 
    2. Mswaki
    3. Msaada
    4. Msaragambo
      1. ii
      2. iv
      3. iii
      4. i
  4. Mkufu ni pambo ambalo huvaliwa .
    1. kichwani.
    2. miguuni. 
    3. shingoni.
    4. mikononi.
  5. Chagua sentensi iliyoakifishwa vibaya.
    1. Juma, Roda na Maria walialikwa shereheni. 
    2. Maembe maparachichi na mananasi hununuliwa wapi. 
    3.  Ukimwona, mwambie aje kwangu. 
    4. Je, mliwaona wanyama wapi mbugani?
  6. Ni upi wingi wa sentensi hii?  Karatasi ilichafuliwa na mtoto.
    1. Karatasi zilichafuliwa na watoto.
    2. Makaratsi yalichafuliwa na watoto.
    3. Karatasi zilichafuliwa na mtoto.
    4. Karatasi ilichafuliwa na watoto.
  7. Ni yupi kati ya hawa ni ndege wa porini?
    1. Kuku
    2. Bata 
    3. Batabukini
    4. Mwewe 
  8. Kitenzi imba katika kauli ya kutendwa huwa
    1. imbia.
    2. imbiwa.
    3. imbwa.
    4. imbaimba. 
  9. Chagua kinyume cha sentensi  ifuatayo:
    Mgeni amesimama karibu na mfalme. 
    1. Mgeni hajasimama karibu na mfalme
    2. Mwenyeji ameketi mbali na malkia
    3. Mwenyeji amesimama karibu na
    4. Mgeni ameketi mbali na malkia. 
  10. Kanusha kauli ifuatayo kwa usahihi.
    Wewe umeimba vizuri. Wewe
    1. haujaimba vizuri.
    2. umeimba vibaya.
    3. hujaimba vibaya.
    4. hujaimba vizuri.

MARKING SCHEME

  1. D
  2. A
  3. B
  4. D
  5. C
  6. A
  7. B
  8. D
  9. C
  10. A
  11. B
  12. D
  13. C
  14. A
  15. D
  16. A
  17. B
  18. D
  19. C
  20. A
  21. C
  22. A
  23. B
  24. C
  25. B
  26. A
  27. D
  28. C
  29. B
  30. D
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Grade 5 End of Term 2 CBC Exams 2022 Set 1.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students