Monday, 04 July 2022 06:49

Kiswahili Questions and Answers - Standard 7 Term 2 Opener 2022 Set 2

Share via Whatsapp

MASWALI

Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne hapo. Jaza kila pengo kwa kuchagua jawabu lifaalo zaidi.
Matukio ya siku hiyo yangali_1_akilini kwa wino usiofutika. Tulikuwa darasani tukifunzwa viunganishi kama vile_2_Ghafla bin vuu mlango ulibishwa_3_ Mwalimu aliacha kuandika na kuelekea kunako mlango aufungue. Ghafla mlango ulipigwa_4_na kufungika. Hapo nje _5_yalisimama majitu mawili yenye macho mawenge na miguu yenye matege iliyopinda kwa nje. Mikononi yalikuwa yamejihami_6_. _7_ "Watoe Salma na Aisha!" Jitu moja liliguruma. "Hamwezi kuingia hapa_8_ya ruhusa. Nisubirini _9_ " Bi. Somi aliwajibu kwa sauti nzito.

  1.        
    1. imeandikwa
    2. zimeandikwa
    3. limeandikwa 
    4. yameandikwa
  2.        
    1. angalau, kidogo, mbali
    2. ila, maadam, mradi
    3. kefu, daima, safi
    4. aisee, wallahi, mathalan 
  3.        
    1. kijeshi
    2. kinguru
    3. kimadharau 
    4. kikobe
  4.        
    1. dhoruba
    2. kibao
    3. kibobwe
    4. kachombe
  5.        
    1. :
    2. ,
    3. /
    4. ;
  6.        
    1. kwa
    2. na 
    3. bila
    4. kuzidi
  7.        
    1. jambia,pantoni,singe
    2. Kikero, kigwe,rungu 
    3. mikuki,ngao, marungu
    4. jambeni,keekee,kipini
  8.        
    1. bali
    2. mradi
    3. haidhuru
    4. ghairi
  9.        
    1. pambajioni
    2. maabarani 
    3. maktabani 
    4. darasani

Maji ni kiowevu kinachopatikana_10_na mvua katika bahari, maziwa na mito. Chambilecho wahenga_11_ Hii ni kwa sababu maji_12_huwa na manufaa kochokocho. Maji hutumiwa katika_13_, kunywa na hata kuogea. Wakulima pia huyatumia_14_mimea yao isije_15_ Maji yanastahili kutumiwa vizuri bila kumwagwa ovyoovyo.

  1.      
    1. kutoka
    2. kutokana
    3. kwa
    4. kulingana
  2.        
    1. maji ya kifuu hufuata bahari ya chungu 
    2. maji ni uhai 
    3. maji yakimwagika hayazoleki
    4. maji mkondo 
  3.      
    1. ii hii
    2. hii hii
    3. haya yaya
    4. yaya haya 
  4.        
    1. kupika
    2. kupikisha
    3. kupakia
    4. kupikia 
  5.        
    1. kuinyunyuzia 
    2. kuinyuzia 
    3. kuinyunyizia
    4. huinyunyizia 
  6.      
    1. ikastawi
    2. ikanawiri 
    3. ikapogoa
    4. ikanyauka

Kutoka swali 16 - 30. jibu kulingana na maagizo

  1. Chombo kinachotumiwa kukunia nazi huitwaje? 
    1. Mbuzi
    2. Kata 
    3. Susu
    4. Kifumbu
  2. Chagua usemi wa taarifa wa:
    "Wanafunzi wanaosomea katika shule hii wana bahati ya mtende," Maridhia alisema.
    1. Maridhia alisema kuwa wanafunzi wanaosomea katika shule hiyo wana bahati ya mtende. 
    2. Maridhia alisema kuwa wanafunzi waliokuwa wakisomea katika shule hiyo walikuwa na bahati ya mtende.
    3. Maridhia alihimiza kuwa wanafunzi wa shule hiyo walikuwa na bahati kama mtende 
    4. Maridhia alitangaza kuwa wanafunzi ambao wangesomea katika shule hiyo wangekuwa na bahati ya mtende.
  3. Chagua sentensi iliyotumia kihisishi kwa usahihi 
    1. Hewala! Sikuamini, siwezi kukusaidia
    2. Ebo! Ni mwanafunzi gani huyu asiyetofautisha mbu na mbung'o! 
    3. Pukachaka! Tumepita mtihani vizuri.
    4. Simile! Naomba urudie swali lako
  4. Maneno yaliyopigwa mstari katika sentensi ifuatayo ni Mwanafunzi hodari hufaulu lakini mvivu hufeli sana. 
    1. Kielezi, kiwakilishi 
    2. Kivumishi, kielezi.
    3. Kielezi, kivumishi
    4. Kivumishi, kiwakilishi.
  5. Neno mapendekezo lina silabi ngapi?
    1. Tano 
    2. Kumi
    3. Sita
    4. Kumi na moja
  6. Tegua kitendawili
    Mgeni wangu anavaa nguo nyingi. 
    1. Mwanajeshi 
    2. Mwanaharusi
    3. Msitu 
    4. Askari
  7. Neno lipi limeambatanishwa na ukubwa wake sahihi 
    1. Jina - majina 
    2. Mzigo - zigo 
    3. Kitabu - kijitabu
    4. Mtu - Jimtu
  8. Badilisha sentensi hii iwe katika hali ya kutendesha. Murasi alimpeleka binti yake Zawadi akaolewe na Musa 
    1. Murasi limwoesha binti yake Zawadi kwa Musa 
    2. Zawadi binti yake Murasi aliolewa na Musa. 
    3. Musa aliozesha binti yake Zawadi na Murasi. 
    4. Murasi alimwoza binti yake Zawadi kwa Musa
  9. Orodha gani iliyo na nafaka pekee
    1. Ngano, mawele, shayiri, mtama 
    2. Limau, fenesi, tikiti, nazi 
    3. Wimbi,mpunga, karafuu, mbuyu 
    4. Ndizi, iliki, dania, bizari
  10. Kutokana na kitenzi aka tunaweza tukaziunda nomino hizi zote isipokuwa 
    1. uashi 
    2. mwaka 
    3. kuaka
    4. mwashi
  11. Maelezo yapi hapa ni sahihi?
    1. Ngonjera ni shairi la kihistoria
    2. Tasdisa ni shairi lenye mishororo sita katika kila ubeti. 
    3. Silabi za mwisho zinazofanana katika kila upande huitwa mizani. 
    4. Mleo ni mshororo wa mwisho wa kila ubeti. 
  12. Kanusha sentensi ifuatayo kwa usahihi.
    Usiku huo ulikuwa na mbalamwezi kama nilivyotabiri.
    1. Usiku huo haukuwa na mbalamwezi kama nilivyotabiri. 
    2. Usiku huo haukuwa na mbalamwezi kama nilivyokosa kutabiri. 
    3. Usiku huo haukuwa na mbalamwezi kama ambavyo sikutabiri. 
    4. Usiku huo ulikuwa na mbalamwezi kama nisivyotabiri.
  13. Chagua jina lilioambatanishwa na ngeli yake kamili. 
    1. Mwiba -U-U 
    2. Jivu -I-ZI 
    3. Moshi -U-ZI
    4. Malezi - U-YA
  14. Kamilisha, 'Lingana kama
    1. kinu na mchi' 
    2. sahani na kawa' 
    3. kiko na digali'
    4. kalamu na karatasi 
  15. Ikiwa juzi ilikuwa Alhamisi, Jumatano itakuwa: 
    1. Kesho 
    2. Keshokutwa 
    3. Kitojo 
    4. Mtondogoo

Soma kifungu kisha uyajibu maswali 31 - 40
Jioni hiyo kama jioni nyinginezo, sisi wajukuu pamoja na vitukuu tuliketi kando ya moto tukisikiliza ngano kutoka kwa laazizi wetu, bibi. Mbalamwezi ilihakikisha kwamba hatupungukiwi na mwanga. Kila tulipomtembelea bibi, tulipata nafasi ya kusikiliza ngano.
Tuliuzingira moto pale nje ya nyumba yake ya msonge kama ilivyo kawaida kupata kopo la uji kwake bibi, tulilekiwa nacho. Baada ya kila mmoja kupata haki yake sasa nafasi ikawa ni ya mwenye masikio kuyatega ndi na kutulia tuli hadi mpasuko wa vicheko vya radi. Sasa tulikuwa tumejituliza kwenye vingoda vyetu bibi alipoanza masimulizi yake kama ilivyokuwa desturi yake. Alitanguliza na kusafisha koo. "Wajukuu wangu wapendwa, zamani sana nikiwa mdogo kama  nyinyi hivi, pamoja na watoto wenzangu tulikuwa tukifunzwa kunga za kikwetu na bibi zetu. Ingawa tulihudhuria mafunzo hayo, wengine wetu hawakuyathamini vile kwani yalitunyima fursa ya kucheza michezo tuliyoipenda.
Siku moja nyanya aliyependa kutusimulia kwa mafunzo yake alikuwa ndio mwanzoa ameanza tu kutufundisha. Mkononi alikuwa na kigozi cha sungura alichokitumia kama wenzo wa kutufundishia jinsi ya kutunga vazi la kujisetiri, Sote tulimpa masikio na macho ingawa shingo upande.
Mara pakatokea Ibra! Kulianguka kutoka juu mtini tulipoketi hadi kwenye kile kigozi. Kilitambaa taratibu na kuja nilipokuwa kikapanda juu ya mkono wangu wa kushoto kabla ya kuteremka na kuyoyomea gizani. Nilishindwa kujisongeza wala kujitikisa. Niliogopa upeo wa kuogopa maana huyo alikuwa nyoka mwenye sumu hatari sana. Wenzangu nao pia walizimika ardhini wasijisongeze. Nyanya alijuzuia kusonga wala kufanya lolote. Nadhani aliogopa kutushtua au hata kumshtua huyo nyoka.
Ni kwenye hali hii nyoka huyo alipotokomea, alikojitendea ndipo kila mtu aliponijia kwa shangwe. na vifijo. Wote waliniambia kuwa kutokana na jinsi nilivyoonyesha ujasiri wakati wa hatari hiyo, basi nilihitimu kuwa kiongozi wao. Yakini, chanda chema huvikwa pete.
Mara moja nikatengenezewa vazi la ngozi, tena ngozi ya mbuzi na kutawazwa papo hapo kuchukua hatamu za uongozi. Wote wakaahidi kutii amri kwani akikalia kigoda mtii. Wajukuu wangu je mmejifunza funzo lipi kutokana na kisa changu?"

  1. Ni nani alipeana ngano? 
    1. Msimulizi
    2. Mbalamwezi 
    3. Nyanya
    4. Mjukuu
  2. Kwa mujibu wa kisa mjukuu ni:
    1. Mwana wa kitukuu 
    2. Mwana wa nyanya 
    3. Mwana wa mwana
    4. Mwana wa kining'ina
  3. Kwa nini bibi wanamwita iaazizi.
    1. Walipenda ngano zake 
    2. Wao walimuenzi mno 
    3. Hakuwa na jina rasmi lake
    4. Alichukia kuitwa kwa jina lake
  4. Ni nani alikalia kigoda karibu na moto.
    1. Wote 
    2. Nyanya 
    3. Msimulizi
    4. Wajukuu pekee
  5. Ni nani aliangukiwa na nyoka.
    1. Msimulizi 
    2. Hatujaambiwa 
    3. Nyanya 
    4. Mjukuu
  6. Kwa nini woga ulimpata bibi?
    1. Bibi alimwonya 
    2. Nyoka alikuwa mkali 
    3. Nyoka alikuwa mwenye sumu
    4. Nyoka alimuuma
  7. Ni kweli kuwa 
    1. msimulizi ni kitukuu 
    2. msimulizi hajawahi kuumwa na nyoka 
    3. nyoka ni mnyama wa kuogopwa
    4. kiongozi sharti awe mwoga
  8. Methali ipi yaweza kutupambia kisa hiki.
    1. Adui mpende 
    2. Mtoto wa nyoka ni nyoka 
    3. Ushikwapo shikamana
    4. Ukibebwa usilevyelevye miguu
  9. Wanaofundisha kunga za maisha huitwa? 
    1. Kungwi
    2. Mkunga
    3. Bibi
    4. Wahenga
  10. Ishara gani inayoashiria umaskini kwenye kifungu. 
    1. Nyoka 
    2. Kiambo cha msonge 
    3. Makopo ya uji 
    4. Bibi mzee

Soma kifungu kifuatacho kisha uyajibu maswali 41 - 50
Nilikuwa mpigabuku wa skuli ya Wema, mwaka jana. Sikuwa na shaka kuibuka galacha katika mtihani wa kitaifa. Nilielewa lazima ja ibada nijifunge kibwebwe na kuuzika uzembe kwenye kaburi la sahau ili niupasi mtihani wa kitaifa. Aku zote ningerauka alfajiri na mapema na kuyabwaga mabuku mezani. Ningejipinda mgongo shabiku upinde na kuvivamia va bin vuu ya nsige gundani la mihogo. Yakini niliuma vitabu we! Kisa na maana sikuwa na namna nyingine ya kuinusuru mbari yangu iliyolemazwa na uchochole si haba. Joho la bidii lilisalia kuwa mwandani wangu.
Taabu na madhila ya baba wa kambo hayakunizuia hata chembe kutia bidii. Vioja vyake kila jioni vilinipa maudhui na vidokezo vya insha ya kila nui kesho yake. Hata kama kuna siku mama alifurushwa akapata hifadhi kwa jirani, mie sikukosa kuzimaliza gange za ziada za walimu. Wakufuu wetu nao walijitolea kwa vyovyote vile kuhakakikisha tunaelewa vyema. Ukweli walijaribu juu chini kufanikisha ndoto zetu. Hakika tenda wema nenda zako Mola atakulipa Wakufuu wa masomo ya sayasi na hisabati walirauka mapema kabla umande kukaushwa na miale ya asubuhi. Walituelezea hadi tukaelewa dhahiri shahiri. Mola daima twamwomba hasa bwana Manywele aliyejinyima hata kishuka kutupa mazoezi ya Sayansi ampe fadhila
Mtihani wa kitaifa ulipowadia hatukuwa na wasiwasi wala kihoro cha nja maji kwani yote tuliyofunzwa yalikuwa tamulini. Tulidurusu hadi misamiati, surufu na fomula zikatuzoea. Kila mmoja wa watahiniwa hasa mimi tulikuwa ngangari kukabiliana na mitego yote ya mtahini. Lo! Siku moja kabla, hofu iliniteka nyara, nikapumbaa na kukosa la kufanya. Mlilikuwa mkikimkiki na mkukumkuku kuwa halambe halambe. Utulivu uliokuwepo ulipasuliwa na vifijo na vifoli. Mkufuu mkuu akaturaushia kadi ya heri njema. Mwalimu majitamu naye akatupa nasaa na wosia wa kutokuwa na woga. Alisema mtihani ni mtihani hivyo basi hakukuwa na haja ya kuwa na mishemishe wali jekejeke la woga.
Asubuhi na mapema tukafika na kuwasili skulini. Tuliukalia ule wa Hisabati siku ya Mosi. Somo la sayansi saa nane huku insha tukiandika mwendo wa alasiri. Jua lilivibusu vilele vya milima nalo giza la kanika kuanza kubisha hodi. Siku ya pili tulianzia na somo la Mapishi pamwe na Kiswahili mwendo wa saa tano. Saa nane nilimalizia na Insha ya methali "Mchuma janga hula na wa kwao."
uliukalia ule wa somo la Kiingereza na kutamatisha elimu ya skuli za msingi. Ilibidi sasa tuwe wavumilivu na punda bila wasiwasi wala shaka. Kwa hamu na hamumu tuliyasubiri matokeo.
Hayawi hayawi huwa. Bidii na juhudi zetu mazao yake yangejulikana na pesa siku hiyo ya alhamisi mwezi Januari. Nakumbuka fika nilivyobumburushwa na kugutushwa na sauti ya redio. "Waziri wa elimu Bw. Matiang'i atayasoma matokeo mwendo wa saa tatu za alfajiri". Waja wa aila ya Joshua walijaa na kujazana pale kiamboni petu. Kama ilivyo mila na desturi, kwamba ufanisi ni wa kila mwanajamii. Yakini kwao, si kwa mchuma janga kula na wa kwao. Mwia usio na chupa kuoza vituo vyote runinga vilihinikiza hewani matangazo ya moja kwa moja.
Jina la mtaluniwa bora nchini likatajwa "Bora mufti ndiye shiyaa wa mwaka huu." Picha ikaonyeshwa nayo haikuwa ya mwingine bali mie mwana wa mzee Mufti. Shangwe na vigelegele vya heri njema na heko vilihinikiza hewani. Uwanja wetu muda si muda ulijazana na kujaa hadi na nusura kuwatapika wengine. Vimulimuli vya kamera nusura viunde jua. Kila mmoja alisheheni furaha ya ufanisi wangu. Kijiji chetu ambacho hakikutambulika sasa kikijulikana nchini. Ndoto yangu ya kuwa mhazigi ikiwa si ya alinacha. Shukrani tumbi za kumsifu Maulana zikihinikiza hewani.

  1. Msimulizi alisomea shule gani?
    1. Mpigabuku 
    2. Wema
    3. Ya msingi . 
    4. Hatujaambiwa
  2. Methali gani inao ujumbe wa aya ya kwanza
    1. Baada ya dhiki faraja.
    2. Mavi ya kale hayanuki
    3. Ukiona vyaelea vimeundwa
    4. Damu ni damu si kitarasa
  3. Ni kweli____
    1. msimulizi alipenda gonezi
    2. alilelewa na baba asiyemzaa
    3. alikuwa kitinda mimba
    4. alikuwa pacha,
  4. Ni walimu wa masomo gani walirauka 
    1. Sayansi pekee
    2. Hisabati na Kiswahili
    3. Sayansi na Hisabati
    4. wote
  5. Siku ya kwanza watahiniwa hawakufanya mtihani wa
    1. Sayansi
    2. Hisabati
    3. Insha 
    4. Kiingereza
  6. Mitihani ilifanyika kwa siku ngapi?
    1. 4
    2. 5
    3. 3
    4. 2
  7. Mwalimu Manywele alifundisha. 
    1. Asubuhi pekee 
    2. Saa nane na jioni
    3. Sayansi 
    4. Saa zote
  8. Ni kweli___
    1. bora mufti alikuwa wa kwanza somo la Hisabati.
    2. baba yake aliacha kutiwa miaka mingi iliyopita.
    3. mama yake hakupenda masomo.
    4. alikuwa rakamu ya kwanza nchini. 
  9. Msimulizi aliania kuwa
    1. daktari wa meno
    2. daktari wa viungo vya mwili
    3. mhadhiri wa chuo kikuu
    4. mwalimu wa sayansi
  10. Jamii ya Joshua yaathamini methali:
    1. Kila mwamba ngona huvuta kwake. 
    2. Mmoja ni nguvu utengano udhaifu. 
    3. Mtegemea cha nduguye hufa hali maskini
    4. Bendera hufuata upepo.

INSHA
Mwandikie kaka yako aliye mjini barua. Mjulishe jinsi unavyoendelea tangu shule zilipofungwa hadi sasa



MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

  1. D
  2. B
  3. A
  4. A
  5. B
  6. A
  7. C
  8. D
  9. A
  1. C
  2. D
  3. A
  4. C
  5. D
  6. A
  7. B
  8. B
  9. D
  10. A
  1. D
  2. B
  3. D
  4. A
  5. C
  6. B
  7. B
  8. D
  9. B
  10. A
  1. C
  2. C
  3. B
  4. A
  5. C
  6. C
  7. C
  8. B
  9. A
  10. B
  1. B
  2. A
  3. B
  4. C
  5. D
  6. C
  7. C
  8. D
  9. A
  10. C
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Standard 7 Term 2 Opener 2022 Set 2.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students