Thursday, 26 October 2023 11:19

Kiswahili Questions and Answers - Class 8 End Term 3 Exams 2023 Set 1

Share via Whatsapp

Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne hapo. Jaza kila pengo kwa kuchagua jawabu lifaalo zaidi.

Usawa wa jinsia ni suala __1___ kwa muda mrefu hapa ___2___. Tabia ya kumpendelea mtoto wa jinsia moja __3___ nyingine imeepigwa na wakati. Mtoto yeyote __4____ ipasavyo anaweza kufanikiwa na kuifaa jamii __5___. ___6__ kumdhulumu mtoto kwa misingi ya kijinsia humfanya ajione duni, yaani __7___. Ni vyema tushikane mikono kukabiliana na __8___ wa kijinsia kwani ___9___.

   A
 1   uliojadiliwa   lililojadiliwa   iliyojadiliwa   yaliyojadiliwa
 2   kwetu   mwetu   yetu   petu
 3   kuliko   kumliko   kuiliko   kuwaliko
 4   akilewa   angelelewa   akilelewa   angelewa
 5   yetu   yako   yake   yenu
 7   Ilhali   Hata hivyo   Juu ya hayo   Angaa
 8   ajichukie   ajishuku   ajitwaze   ajibeze
 9  uso wa kufadhiliwa    u chini.  ukibebwa   usilevyelevye  miguu.   pasi na viganja viwili     kofi hazilii.  papo kwa papo kamba   hukata jiwe.


Mwalimu ___10___ kwamba Fatu alikuwa_11___, alimwita faraghani ili ___12___ na kupata kiini cha huzuni yake. Huku __13___na matone ya machozi, Fatu alimweleza mwalimu huyo kuwa wavyele wake walikuwa na mipango ya kumwachisha shule na __14___ kwa __15___wa rika la babu yake. Mwalimu alimhimiza asiwe na wasiwasi maadamu angemsaidia kuepuka kadhia hiyo

   A
 10  aligundua  akagundua  alivyogundua  alipogundua
 11  amejishika tama  amepiga mafamba  amekula mwande  ametia mrija
 12  amsajili  amsaili  amsitiri  amsaliti
 13  amedondokwa  anatiririkwa  akidondokwa   akitiririkwa
 14  kumwoa  kumwolesha  kuoleka   kumwoza
15  buda  ajuza  kaimu  barobaro


Kuanzia swali la 16 hadi la 30, chagua jibu lifàalo zaidi kulingana na maagizo uliyopewa.

  1. Chagua sentensi iliyotumia "ki" kuonyesha vitendo sambamba.
    1. Uzi huo ukivutwa sana utakatika.
    2. Msukaji aliimba akisuka vikapu.
    3. Kijiji hicho kiliwavutia wageni kwa wenyeji.
    4. Wacheza ngoma wote walivalia kitamaduni.
  2. Upi ni ukanusho ufaao wa sentensi; Mahali kuliko na mlipuko wa maradhi kunahitaji msaada.
    1. Mahali kusiko na mlipuko wa maradhi kunahitaji msaada.
    2. Mahali kuliko na mlipuko wa maradhi hakutahitaji msaada.
    3. Mahali kuliko na mlipuko wa maradhi hakujahitaji msaada.
    4. Mahali kusiko na mlipuko wa maradhi hakuhitaji msaada.
  3. Ni jibu lipi lililo na maneno ambayo hayalingani?
    1. Chawa, funza, utitiri, kunguni.
    2. Singe, manowari, bunduki,kombora.
    3. Wengu, nyongo, pafu, waridi
    4. Robo, humusi, thuluthi, sudusi
  4. Andika kauli ya kutendewa ya sentensi;
    Masogora waliingia ukumbini wakacheza ngoma.
    1. Ngoma ilichezewa ukumbini na masogora.
    2. Ukumbini mlichezwa ngoma na masogora.
    3. Masogora walichezea ngoma ukumbini.
    4. Ngoma ilichezwa na masogora ukumbini.
  5. Ni ulinganifu upi ulio sahihi?
    1. Jimbi - mtamba
    2. Fahali - koo
    3. Mjomba - halati
    4. Kipora - mbarika
  6. Andika katika hali ya umoja.
    Nyuta hizo zilitumiwa na wasasi hodari.
    1. Ukuta huo ulitumiwa na msasi hodari.
    2. Uta huo ulitumiwa na msasi hodari.
    3. Uta huo ulitumiwa na msasi mhodari.
    4. Ukuta huo ulitumiwa na msasi mhodari.
  7. Chagua sentensi yenye kihusishi cha kulinganisha.
    1. Wageni waliwasili baada ya sherche kuanza.
    2. Timu yetu ilicheza dhidi ya Miamba angu wa Pwani.
    3. Kilate alimwendea mwalimu kwa ushauri.
    4. Jengo hilo lilikuwa kubwa mithili ya mlima.
  8. Aka ni kwa mwashi kama ilivyo kwa msasi.
    1. saka
    2. sasa
    3. saa
    4. susia
  9. Badilisha katika usemi wa taarifa:
    "Mtoto wako atatibiwa leo," daktari alimwambia mama huyo.
    1. Daktari alimwambia mama huyo kwamba mtoto wake atatibiwa siku hiyo.
    2. Daktari alimwambia mama huyo kwamba mtoto wake angetibiwa siku ambayo ingefuata.
    3. Daktari alimwambia mama huyo kwamba mtoto wake angetibiwa siku hiyo.
    4. Daktari alimwambia mama huyo kwamba mtoto wake anatibiwa siku hiyo.
  10. Chagua vielezi katika sentensi ifuatayo. Wanafunzi wote walitembea taratibu hadi ukumbini.
    1. walitembea, hadi
    2. hadi, ukumbini
    3. taratibu, ukumbini
    4. taratibu, wote
  11. Tegua kitendawili kifuatacho;
    Akiona miale ya jua hufa.
    1. Umande
    2. Samaki
    3. Kobe
    4. Mvua
  12. Kipi ni kisawe cha nahau enda upogo?
    1. enda mserego
    2. enda joshi
    3. enda masia
    4. enda mrama
  13. Chagua maelezo yasiyo sahihi.
    1. Ngonjera ni shairi la majibizano.
    2. Arudhi ni kanuni za utunzi wa mashairi.
    3. Utenzi ni shairi lenye vipande viwili katika mishororo.
    4. Vina ni silabi zinazofanana katikati au mwishoni mwa mishororo.
  14. Pora ni jogoo ambaye hajaanza kuwika. Pora pia ni
    1. chopoa kwa nguvu kitu alichoshika mtu.
    2. mnyama jamii ya nyegere alayc asali.
    3. tendo la kuondoa magamba ya samaki.
    4. funga kitu kwa kukaza sana.
  15. Mzazi au kiongozi anapoondoka, wale waliomtegemea hutaabika sana.
    Chagua methali inayolingana na maclczo haya.
    1. Mkuu hukua kwao.
    2. Mti ukianguka ndege hutawanyika
    3. Akikalia kigoda mtii
    4. Mti hauendi ila kwa nyenzo.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali kuanzia 31 mpaka 40

Kwa muda mrefu jamii imekuwa ikimpigia debe mtoto wa kike. Jambo hili limewekwa katika nyanja tofauti tofauti; elimu, afya, nafasi za ajira, katika dini na kwingineko. Kuwezeshwa huku kwa mtoto wa kike kumekithiri na dalili zimejitokeza katika hali mbalimbali. Dalili iliyo kubwa zaidi ni kutelekezwa kwa mtoto wa kiume. Yeye amesahaulika kabisa kiasi kwamba hakuna kundi au juhudi za kiutawala ambazo zimewekwa kuhakikisha kuwa naye hajaachwa nyuma kama mkia.

Kutelekezwa kwa mtoto wa kiume kumeanza kuonyesha matokeo yasiyoridhisha. Suala la kwanza lililo dhahiri ni matumizi ya mihadarati. Jamii haina wakati wa kumshughulikia mtoto wa kiume. Hali hii imemwacha huru kufanya maamuzi yake. Uhuru usiodhibitiwa ni hatari. Uhuru huu umemfanya kutumia wakati wake apendavyo. Njia mojawapo ni katika kutumia mihadarati na kushiriki hulka nyingine ambao zina madhara makubwa. Yeye akiendelea kufanya hivyo, mwenzake wa kike anaendelea kutunzwa kwa hali na mali hata katika kiwango cha kudekezwa.

Kupuuzwa kwa mtoto wa kiume kumemfanya abaki nyuma kielimu. Hatukuwa tukishuhudia kudorora kwa matokeo ya mitihani kwa watoto wa kiume? I lakuna aliyethubutu kuhoji sababu labda kwa kuhofia kubandikwa nembo ya taasubi ya kiume. Mtoto wa kiume anapoendelea kufanya vibaya katika masomo hubaki nyuma na hata katika kuchukua nafasi za ajira baadaye. Hali hii hudhihirika kiuchumi ambapo wanaume wengi hawawezi kufikia mishahara ambayo wenzao wa kike wanapata. Wanawake pia wamepanda hata kuchukua nyadhifa muhimu katika ngazi za kitaifa na kimataifa.

Tuhuma za kuwanyanyapaa wale ambao wamekuwa wakiunga mkono juhudi za mwanamume kujiendeleza zimekuwa sumu. Sumu hii imeleta matokeo ya kuibuka kwa taasubi ya kike. Mmea wa taasubi hii umepaliliwa na kunyunyiziwa maji na mashirika ya kijamii yanayompigia debe mwanamke na hata katika vyombo vya habari kupitia kutetea haki za wanawake. Kwa muda mrefu hatukuwa na shirika lolote lililotetea haki za mtoto wa kiume au hata vipindi vilivyopigia debe juhudi za kuwainua watoto hao.

Mawazo ambayo yamekuwa yakipigiwa upatu na mashirika ya kutetea haki za mtoto wa kike na hata vyombo vya habari yamekita mizizi hata akilini mwa wazazi. Nani atapinga hili? Ithibati ya jambo hili i wazi kabisa. Ukitembea mitaani utawapata watoto wa kiume wakicheza bila suruali huku wa kike wakiwa wamevalishwa nguo nadhifu.

Nyumbani utawapata watoto wa kiume wakila vyakula vigumu huku wenzao wakila mapochopocho. Hata katika majina hili linajitokeza. Wazazi hufanya juhudi kubwa kuwachagulia majina wanao wa kike. Si ajabu nafasi ya mwanamume imeendelea kubanwa. Visa vya wanaume kupigwa na wanawake ni mojawapo ya matokeo.

Hali hii ya kuinuliwa kwa mtoto wa kike imekuwa ikifanywa bila kuzingatia mambo mengi muhimu. Jambo moja ambalo hakuna aliychoji ni; Kwa nini mtoto wa kike ainuliwe? Ikiwa ni ili afikishwe kiwango cha mwenzake wa kiume, basi alimfikia na kumpita. Kama hali ndiyo hii, basi ni muhimu mtoto wa kiume naye ainuliwe. Hili litaafikiwa ikiwa mbinu zilezile zilizotumiwa kwa mtoto wa kike zitakumbatiwa.

Suluhu itapatikana vipi? Tatizo la kutelekezwa kwa mtoto wa kiume litapewa ufumbuzi ikiwa tutapiga hatua nyuma tujiulize ni kwa nini tulihitaji kulinda haki za mtoto wa kike. Bila shaka, jambo moja litakuwa wazi kuwa mtoto wa kike alikuwa akibaki nyuma kutokana na sababu za kimazingira hasa ya kijamii. Ikaibuka haja ya kumsaidia kukabiliana na changamoto za mazingira hayo. Abadan kataan kutelekezwa kwa mtoto wa kiume hakukuwa mbinu mojawapo ya kutetea haki za mtoto wa kike.

  1. Chagua maelezo sahihi kulingana na aya ya kwanza
    1. mtoto wa kiume amepuuzwa kwa muda mrefu.
    2. jamii imetekelezwa mikakati mbalimbali ya kumwinua msichana.
    3. watawala ndio wanaochangia zaidi. kudhalilishwa kwa mvulana.
    4. haki za watoto wote zimepigiwa debe na mashirika mbalimbali.
  2. Jambo analopinga mwandishi katika aya ya pili hasa ni
    1. kumpa mvulana uhuru mwingi kupindukia.
    2. jitihada nyingi kuelekezwa katika malezi ya msichana.
    3. vijana kutumia mihadarati kupindukia.
    4. mvulana kujikulia bila maelekezo yafaayo.
  3. Si kweli kusema kuwa;
    1. wanaume hawapati nyadhifa nzuri kitaifa na kimataifa.
    2. msichana anabembelezwa kupita kiasi."
    3. maovu katika jamii yanadhihirisha pengo katika malezi.
    4. kumpa mtoto wa kike nyadhifa mbalimbali ni jambo la busara.
  4. Kwa nini wengi hawakuthubutu kuhoji kiini cha kudorora kwa elimu ya mtoto wa kiume?
    1. Jambo hilo lilitokea bila wengi kujua.
    2. Matokeo duni kwa mvulana lilikuwa jambo la kawaida.
    3. Kumtetea mvulana kulichukuliwa kama kupinga maendeleo ya msichana.
    4. Kumwinua mvulana kupita kiasi kungemnyima msichana nafasi ya kufanya vyema.
  5. Kwa nini wanaume hawana mishahara mizuri kama wenzao wa kike?
    1. Wanaume wananyimwa nafasi ya kujitetea kazini.
    2. Wanawake ni wengi kuliko wanaume
    3. Wanawake wengi wameelimika kuliko wanaume.
    4. Waajiri wengi hivi sasa ni wanawake.
  6. Mashirika ya kijamii na vipindi katika vyombo vya habari;
    1. hupendelea jinsia ya kiume zaidi.
    2. vinapaswa kutekeleza shughuli kwa usawa
    3. vimetekeleza wajibu wao sawasawa.
    4. hutumiwa kumdhalilisha mtoto wa kike.
  7. Aya ya tano imedokeza kuwa
    1. mvulana amenyimwa hata haki za kimsingi.
    2. watoto wa kiume wanahimizwa kucheza bila mavazi.
    3. mtoto wa kike anatimiziwa haki zake zote.
    4. wavulana wasiovalia suruali hudharauliwa na wasichana wenye mavazi nadhifu michezoni.
  8. Msimamo wa mwandishi wa makala haya ni kuwa
    1. kuinuliwa kwa msichana kumeleta madhara mengi kuliko manufaa katika jamii.
    2. juhudi za kumwimarisha msichana zinafaa kusitishwa ili mvulana naye aangaziwe.
    3. mvulana anapaswa kusaidiwa ili naye ampiku mwenzake wa kike.
    4. juhudi za kupigania usawa wa kijinsia zinapaswa kulenga watoto wa jinsia zote.
  9. Kauli yamekita mizizi imetumia tamathali gani ya usemi?
    1. Sitiari
    2. Tashbihi
    3. Chuku
    4. Nahau
  10. Neno kuwanyanyapaa kulingana na muktadha lina maana ya
    1. kuwapinga
    2. kuwabeza.
    3. kuwazomea
    4. kuwadhihaki

Soma kifungu hiki kisha ujibu maswali kuanzia nambari 41 mpaka 50

Siku ya Geza na mwanawe kutoka hospitalini ilifika. Muuguzi aliwashauri wamtunze mtoto huyo vyema; kwamba mtoto mwenyewe hakuwa na dosari kubwa, ila alihitaji utunzaji wa makini zaidi. Maneno hayo yaliangukia masikio yaliyokuwa yametiwa nta. Hisia za unyonge na maonevu zilimkubatia Geza kiasi cha kuuycyusha utu wake. Mumewe alikuja kumchukua kutoka hospitalini.

Nyumbani mwa Geza na Kataa hamkusikika vigelegele vya kuzaliwa kwa kiumbe kipya. Geza alitoka garini kakipakata kitoto chake kama kifurushi cha karatasi ya shashi. Akafululiza moja kwa moja hadi chumbani mwake ambamo angekificha kitoto hicho kwa miaka mingi. Wageni waliwasili kukiona kitoto, wakatiliwa huku na kutolewa kule. Mara kitoto kina homa, mara kimelala...... almradi kila mara mama mtu alikuwa na uongo wa kuwazulia watu. Nao adinası hawakuwa mazumbukuku kiasi kile. Walikuwa wamesikia tetesi kutoka kwa akina pangu pakavu wa humo kijiji kuhusu hali ya mtoto huyo, navyo vitendo vya Geza viliwasaidia kupiga muhuri mawazo yao. Jambo lililowashangaza wapenda haki ni vipi mama ataweza kumfungia mtoto wake chumbani. Vipi mama huyo hakuweza hata kumpeleka mwanawe hospitalini kwa matibabu na
msaada zaidi?

Vitendo vya kikatili vya Geza havikumzuia mtoto kukua. Mwanatabu alitambaa, akasota, akasimama dede japo kwa taabu hadi akachukua hatua yake ya mwanzo na kuanza kutembea. Mama mtu aliyatazama hayo bila kuridhika Daima alimlinganisha mwanawe na wale wa majirani. Alishindwa kuelewa kwa nini mtoto wake bado anaboboja maneno tu badala ya kuzungumza kama watoto wa wifi yake.

Hata mtoto alipofikia umri wa kuenda shule, Geza alidinda kumpeleka hadi mume wake Kataa alipomlazimisha kufanya hivyo. Japo Kataa alitaka mtoto huyo apelekwe katika shule mahsusi za watoto wanaohitaji kushughulikiwa kwa makini, Geza alikataa katakata. Alimpeleka katika shule mojawapo ya umma hapo karibu akidai kuwa hapana pesa kwani mtoto wao wa kiume ambaye alizaliwa miaka miwili baada ya Mwanatabu kuzaliwa, alihitaji kushughulikiwa pia.

Mwanatabu aliingia shuleni na kujipata katika lindi kubwa la simanzi. Kwa vile alikuwa amezoea kuishi amefungiwa ndani asije akaonekana na kuchekwa na watu, alipata shida nyingi kuingiliana na watoto wengine. Kila alipowaona wenzake alikimbilia mwalimu kwa usalama. Mawasiliano nayo yalikuwa magumu kwani Mwanatabu hakuwa amemudu kuzungumza vyema. Mwalimu alipozungumza naye Mwanatabu alikenua meno tu na kusema maneno ambayo yalimwia vigumu mwalimu kuyafasiri.

Siku za mwanzomwanzo mwalimu alivumilia akidhani hilo lilikuwa tatizo dogo tu. Baadaye aliona kwamba hafikii popote, kwani kwa sababu ya kutoweza kuwasiliana vyema na wanafunzi wenzake, mwana huyu alizua mbinu ya kuwawezesha wenzake kumsikiliza. Alianza kuwachapa na kuwawinga kama ndege wawingwavyo kutoka shamba la mtama. Mwalimu hakusita kuwaita wavyele wa Mwanatabu ambao bila shaka walikiri mtoto wao alikuwa na tatizo tangu kuzaliwa.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo aliwashauri wampeleke Mwanatabu katika hospitali ambamo mna kliniki ya kuwazoesha watoto kuzungumza. Aidha, aliwatafutia shule mahsusi ya watoto walio na tatizo kama la Mwanatabu.

Hivi sasa, Geza hukumbuka kwa uchungu na jitimai kubwa jinsi alivyokuwa amepania kumtelekeza mwanawe katika hali mbaya ati kwa sababu kazaliwa na upungufu wa kihali na kimwili. Mara tu baada ya Mwanatabu kupelekwa kwa matibabu zaidi na kusomea katika mazingira yaliyomfaa zaidi hali yake ilianza kuimarika. Aliweza kuzungumza. Maendeleo yake katika masomo yaliimarika, nao walimu hawakusita kutambua hayo na kumpeleka katika shule ya kawaida. Hivi sasa amehitimu masomo ya chuo kikuu. Amewafaa watoto wengi walio na matatizo ya kimaumbile. Maisha yake ni funzo na dhihirisho kuwa hakuna binadamu ambaye hawezi kutekeleza majukumu kama wengine akipewa fursa ipasavyo. Upungufu wa kimaumbile si kutojiweza. Haifai kuwabagua adinasi kwa misingi ya tofauti za kimaumbile.

  1. Ni maelezo yapi sahihi kulingana na kifungu?
    1. Muuguzi alijua kuwa Geza asingemtunza mwanawe ipasavyo.
    2. Geza alitilia maanani nasaha aliyopewa na muuguzi.
    3. Muuguzi alitekeleza wajibu wake ipasavyo.
    4. Geza alijihisi mnyonge kutokana na maneno ya muuguzi,
  2. Nyumbani mwa Geza na Kataa hamkusikika vigelegele kwani,
    1. watu hawakufika kwa sherehe ya kumpokea mtoto.
    2. mtoto hakupokelewa kwa bashasha kama ilivyotarajiwa.
    3. mke na mume waligombana kutokana na hali ya mtoto.
    4. mtoto alikuwa mwenye kasoro nyingi za kimaumbile.
  3. Waliofika nyumbani kwa Géza,
    1. hawakupewa fursa ya kumwona mtoto.
    2. walitaka kumdhihaki mtoto na mwanawe.
    3. walieneza uvumi kila mahali.
    4. ni jamaa wa karibu wa Geza na Kataa pekee.
  4. Pesa anazotoa mtu ili kumshika mioto mchanga kwa mara ya kwanza huitwaje?
    1. Ridhaa
    2. Arbuni
    3. Kifunguamkoba
    4. Fola
  5. Si kweli kusema kuwa,
    1. wapo waliojua hali ya mtoto wa Geza.
    2. vitendo vya Geza vilichangia watu kuongea zaidi.
    3. Geza na Kataa walikuwa na watoto wawili
    4. watu hawakujali dhuluma alizopitia Mwanatabu.
  6. Kwa nini Mwanatabu hakupelekwa mapema katika shule ya watoto wenye mahitaji maalum?
    1. Wavyele wake walikosa maarifa.
    2. Ulikuwepo ugumu wa kumtunza yeye na mnuna wake.
    3. Mama yake alimbagua kutokana na hali yake.
    4. Ilimchukua muda mrefu kuzungumza na kutembea.
  7. Kulingana na aya ya sita,
    1. tatizo katika mawasiliano huweza kuchangia visa vya utovu nidhamu.
    2. kuchelewa kuenda shule hutatiza mawasiliano ya wanafunzi na walimu.
    3. kutowasiliana ipasavyo huwafanya wanafunzi wasimwelewe mwalimu.
    4. kutishwa na wengine huwafanya wanafunzi wajitenge na wenzao shuleni.
  8.  Akina pangu pakavu kulingana na makala haya ni
    1. walio na upungufu wa kimaumbile.
    2. wenye tabia ya kufitini.
    3. wanaochunguza ukweli.
    4. watu wanyonge.
  9. Mambo yaliyomsaidia Mwanatabu kufanikiwa katika kifungu hiki hasa ni A
    1. kutangamana na wengine na himizo la mwalimu mkuu.
    2. matitabu na kusomea katika mazingira yafaayo
    3. ushauri wa walimu na kusomea katika shule ya umma.
    4. kupelekwa shule na msimamo thabiti na baba yake.
  10. Funzo linalopatikana katika kifungu hiki ni kuwa;
    1. Wanaowapuuza wanyonge huaibika baadaye.
    2. Binadamu ni ng'amba hawakosi la kuamba.
    3. Ukimlea mwana mwema na mui mlee.
    4. Hakuna msiba usiokuwa na mwenziwe.

INSHA

Umepewa dakika 40 kuandika insha yako.
Wewe ni kiranja mkuu wa shule yako. Andika hotuba utakayowatolea wanafunzi wenzako wa darasa la nane kuhusu umuhimu wa kuzingatia maadili hata baada ya kukamilisha mtihani wa kitaifa.

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

  1. B
  2. D
  3. A
  4. C
  5. C
  6. B
  7. D
  8. A
  9. C
  10. D
  11. A
  12. B
  13. C
  14. D
  15. A
  16. B
  17. D
  18. C
  19. A
  20. C
  21. B
  22. D
  23. A
  24. B
  25. C
  26. B
  27. D
  28. C
  29. A
  30. B
  31. B
  32. D
  33. A
  34. C
  35. C
  36. B
  37. A
  38. D
  39. D
  40. B
  41. C
  42. B
  43. A
  44. D
  45. D
  46. C
  47. A
  48. B
  49. B
  50. C
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Class 8 End Term 3 Exams 2023 Set 1.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students