Friday, 29 October 2021 08:30

Kiswahili Questions and Answers - Class 8 End Term 2 Exam 2021 Set 1

Share via Whatsapp

Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi, umepewa majibu manne. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.

Ili kuwa na jamii ___1___kila mmoja wetu anahitajika___2___, ___3___mstari wa mbele katika kuzungumza tu___4___ pia katika matendo yetu. Inaeleweka na kila mtu kuwa___5___ya mja hunena muungwana ni vitendo. Ni___6___letu kuhakikisha kuwa jamii yetu___7___. Hili linawezekana tu iwapo tutakuwa___8___katika kila tulitendalo. Kwa mfano, hatuwezi tukatarajia kuwa na jamii yenye bidii iwapo sisi ndisi___9___ Hilo haliwezekani.

  1.  
    1. thabiti
    2. dhabiti
    3. mathubuti
    4. dhaifu
  2.  
    1. kutolewa
    2. kujitoa
    3. kujitia
    4. kujitolea
  3.  
    1. Usiwe
    2. Tuwe
    3. Mwe
    4. Tusiwe
  4.  
    1. ingawa
    2. bali
    3. lakini
    4. mbali
  5.  
    1. afua
    2. desturi
    3. ada
    4. kawaida
  6.  
    1.  toleo
    2.  wajib
    3.  dhima
    4. jukumu
  7.  
    1.  imeidilika
    2. imeadilika
    3.  imebaidilika
    4. imebainika
  8.  
    1. vielelezo
    2. tegemeo
    3. vielezo
    4. vigezo
  9.  
    1. tunaolaza damu
    2.  tunaokufa kikondoo
    3. tunaopiga moyo konde
    4. tunaojitolea mhanga

Baada ya___10___ na darasa la nane, niliamua kudurusu zaidi ili nifaulu. Sikutaka kuvuta mkia ___11___, ___12___kuhusu aina___13___maneno kama vile nomino, vitenzi na vielezi ambavyo pia huitwa ___14___ . Kuna vielezi vingi___15___ polepole, upesi, nyumbani na sokoni.

  1.  
    1. kuungana
    2. kuunganishwa
    3. kujiunga
    4. kuunga
  2.  
    1. tena
    2. asilani
    3. yamkini
    4. angalau
  3.  
    1. Nimesoma
    2. Ninasoma
    3. Nilisoma
    4. Ningesoma
  4.  
    1. ya
    2. wa
    3. na
    4. za
  5.  
    1. viigizi 
    2. viarifa
    3. visifa
    4. viingizi
  6.  
    1. :
    2. ;
    3. -
    4. ,

Kutoka swali la 16 - 30, chagua jibu sahihi kulingana na maagizo.

  1. Chagua ukanusho wa: Mgeni aliyewasili ana kofia.
    1. Mgeni asiyewasili ana kofia.
    2. Mgeni asiyewasili hana kofia. 
    3. Mgeni aliyewasili huna kofia. 
    4. Mgeni aliyewasili hana kofia.
  2. Tambua sentensi iliyo na kivumishi cha idadi katika orodha.
    1. Barabara zote zimejaa magari.
    2. Miti mingi imepandwa na wanafunzi.
    3. Mwalimu amesahihisha insha mbili.
    4. Kitabu hiki ni cha mwanafunzi wa pili.
  3. Tambua matumizi ya 'ki' katika sentensi.
    Mpishi yule alipika akiimba.
    1. Kuonyesha vitenzi sambamba.
    2. Kuonyesha hali endelezi.
    3. Kuonyesha kufuatana kwa vitendo. 
    4. Kuonyesha hali ya masharti.
  4. Sentensi ipi iliyo katika hali ya mazoea kati ya hizi?
    1. Wewe hukufika mapema tulivyoelewana.
    2. Mtoto atikaye shuleni mapema ndiye huyu.
    3. Alitembea huku ameangalia.
    4. Hungesoma kwa bidii hungefaulu.
  5. maji, chai, uji' ni mfano ya nomino za aina gani?
    1. Nomino za hali
    2. Nomino za wingi 
    3. Nominoambata
    4. nomino za jamii.
  6. Tambua nomino ambayo haijalinganishwa kwa usahihi na ngeli.
    1. moyo - U - ZI, U-I 
    2. kipepeo - KI-VI, A - WA
    3. ua - LI-YA, U - ZI
    4. moto - U-T; U-U
  7. Chagua maelezo ambayo ni sahihi.
    1. Kitengele ni kiungo cha mkono kati ya kiwiko na bega. 
    2. Kwapa ni kiungo cha mwili kilicho juu ya bega. 
    3. Nyongo ni kiungo cha mwili kinachopatikana juu ya kiuno.
    4. Goko ni mfupa wa mbele unaotoka kwenye kifundo cha mguu mpaka kwenye goti.
  8. Orodha ipi ambayo ni ya vihusishi pekee?
    1. langu, vyao, zake
    2. kabla ya, juu ya, baada ya
    3. licha ya, fauka ya, minghairi ya 
    4. ala, ebo, afanalek
  9. .'a, e, i, o, u' ni mifano ya
    1. konsonanti
    2. silabi funge 
    3. vokali
    4. sautighuna.
  10. Teua umoja wa: Vita huharibu maendeleo ya mataifa.
    1. Vita huharibu maendeleo ya taifa 
    2. Kita huharibu maendeleo ya taifa 
    3. Vita huharibu endeleo la taifa 
    4. Kita huharibu maendeleo la taifa.
  11. Jibu lipi ambalo halijalinganishwa kwa usahihi? 
    1. fuma - fumua 
    2. chimba - chimbua
    3. pakia - pakua
    4. funga - fungua
  12. Maamkizi gani yatumikayo wakati uliotofauti na mengine?
    1. Sabalheri
    2. Chewa
    3. Umeamkaje 
    4. Umeshindaje
  13. Tambua sentensi iliyotumia kiunganishi kwa usahihi.
    1. Nipe aghalabu shilingi hamsini ninunulie kitabu.
    2. Umeshindwa kuandika aya moja sembuse insha nzima. 
    3. Mathalani umewasili, tutaanza safari.
    4. Bighairi ya kumnunulia nguo, pia alimnunulia kalamu.
  14. Jibu lipi lenye kitenzi kilichoundwa kutokana na sifa? 
    1. cheka - mcheshi 
    2. mwalimu - funza
    3. vumilivu - vumilia
    4. mjuzi - ujuzi.
  15. Mtoto ni kwa binadamu kama vile __________ ni kwa ndege.
    1. kinda 
    2. kifaranga 
    3. kiota 
    4. kizimba

Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali 31-40.

Siku moja, mume na mke wakiwa wamekaa pamoja, mume alimwambia mke wake, "Mke wangu nimewakumbuka sana ndugu zangu (kaka zangu, dada zangu na hata baba na mama) tujumuike pamoja na kula pamoja. Kesho nitawaalika ili tufurahie nao katika chakula cha mchana, itabidi uandae chakula kwa ajili yao."

Mke alijibu kwa unyonge, “Sawa, Mungu akipenda."

Asubuhi ya siku iliyofuata, mume alitoka kwenda katika shughuli yake lakini baada ya saa kadhaa alirejea nyumbani. Alimsaili mke wake, “Mke wangu, umeandaa chakula cha mchna kwa ajili ya wageni? Baada ya saa moja watakuwa wameshafika." Mke alijibu, "La. Sijapika madhali ndugu zako sio wageni hapa. Watakula chochote wakipatacho." Mumewe alimwambia kuwa Mungu amsamehe. Alitaka kujua kwa nini mkewe aliyasema hayo ilhali alikuwa amemweleza kuhusu wageni tangu siku iliyotangulia. Aliuliza kwa nini mke wake hakumwambia kuwa asingepika ilihali wazazi wake wangewasili baada ya muda mfupi.

Basi mume ilimbidi aondoke pale nyumbani ili aibu isimfunike na kumzamisha. Baada ya dakika kadhaa, mlano ulibishwa. Mke alienda kuufubgua mlango. Alipigwa na butwaa alipokuta kuwa wageni waliokuja ni wazazi wake: baba yale, mama yake, dada zake pamoja na kaka zake. Alishtuka nusura azimie. Hata hivyo, aliwakaribisha ndani.

Baba yake alimwuliza alikokuwa mume wake. Mke alimjibu kwamba alikuwa ametoka dakika chache zilizopita. Baba alimwambia "Mumeo jana alitupa taarifa kuwa leo anatualika hapa tuje kula pamoja chakula cha mchana. Sasa vipi yeye ameondoka? Tendo hili si la busara." Mwanamke yule alishangaa kwa taarifa hiyo. Alianza kufikicha mikono yake huku akipigapiga mguu chini kwa kuchanganyikiwa. Ilimbidi aingie ndani na kumpigia mume wake simu. Alimwambia, "Kwa nini hukuniambia kuwa wazazi wangu ndio wanaokuja?"

Mume alimjibu, "Wazazi wangu na wazazi wako wote ni kitu kimoja, hawana tofauti."

Mke alimwambia mumewe, “Leta chakula huku. Chakula kilichokuwepo ni kichache. Hakitawatosheleza."

Mume alimjibu, "Mimi nipo mbali na hao si wageni. Watakula chochote kilichopo namna wewe ulivyokuwa ukitaka kuwalisha wazazi wangu." Mke alibabaika sana. Mikono yake ilitetemeka huku akimwomba mumewe msamaha. Aliwaelezea wazazi wake yote yaliyojiri. Nao waliamuru kuwa wazazi wa mume watafutiwe siku ya kuwatembelea wana wao ili waandaliwe mlo.

  1. Kulingana na aya ya kwanza, mume
    1. alikumbushwa kuhusu ndugu zake na mkewe. 
    2. alijua kuwa mke angekataa kuwahudumia wageni. 
    3. alinuia kuwatendea wema wakwe wake. 
    4. alimwekea mkewe mtego ili amnase.
  2. Maneno yaliyosemwa na mke, “Sawa,Mungu akipenda", yanaonyesha
    1. udhaifu wa mke
    2. kutojali kwa mke 
    3. jinsi mke alivyomtegemea Mungu 
    4. uaminifu wa mke.
  3. Makala haya yamendhihirisha mke kuwa
    1. mwenye tamaa, katili 
    2. mkakamavu, goigoi 
    3. mwenda nguu, mchoyo 
    4. mbinafsi, kaidi
  4. Methali gani isiyoweza kumrejelea mke katika makala haya?
    1. Ndugu ni kufaana si kufanana.
    2. Mkuki mtamu kwa nguruwe kwa binadamu uchungu:
    3. Mchimba kisima huingia mwenyewe.
    4. Kila mwamba ngoma, ngozi huivuta kwake.
  5. Maneno 'itabidi uandae chakula' yanatoa maana zifuatazo isipokuwa
    1. una hiari ya kuandaa chakula 
    2. ni lazima uandae chakula 
    3. huna budi kuandaa chakula 
    4. ni faradhi uandae chakula.
  6. .... aibu isimfunike na kumzamisha' yametumia fani gani ya lugha?
    1. Chuku
    2. Istiara 
    3. Tashhisi 
    4. Kinaya
  7. Hali ya mke kupata kwamba wageni waliokuja walikuwa ni wazazi wake badala ya wazazi wa mume inaweza ikaelezewa kwa nahau ipi? Mke
    1. alikula mwande
    2. alikula mwata 
    3. alikula muku 
    4. alikula mori
  8. Makala haya yameonyesha kuwa mume
    1. aliwahusudu wazazi wa mkewe
    2. aliwastahi wazazi wa mkewe
    3. aliwahadaa wazazi wa mkewe
    4. aliwadhalilisha wazazi wa mkewe.
  9. Neno 'alimsaili' lina maana gani jinsi lilivyotumika katika kifungu?
    1. Alishangazwa
    2. Alimwuliza 
    3. Alimtuliza 
    4. Alimwagiza
  10. Kwa mujibu wa aya ya mwisho, si kweli kuwa
    1. huenda mume hakuwa mbali ila alikasirishwa na tabia ya mkewe. 
    2. mume alikuwa amegundua kuwa wazazi wa mkewe hawakuwa wageni pale nyumbani.
    3. mke alitetemeka kuonyesha kujutia yale aliyoyatenda. 
    4. mume alimwelewa mkewe na kumpa nafasi nyingine.

Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali 41 - 50.

Wakenya zaidi ya elfu kumi na tano walihusika katika ajali za barabarani mwaka jana. Kati yao elfu tatu na mia nne walifariki huku wengine zaidi ya elfu sita mia sita wakipata majeraha mabaya. Jambo la kuhuzunisha mno. Hata hivyo, imebainika kuwa huenda magari yaliua watu wengi zaidi mwaka jana kuliko idadi hiyo iliyotolewa na Mamlaka ya Usalama wa Barabarani. Utafiti umekuwa ukifanywa kila uchao. Wanasayansi sasa wanasema kuwa moshi unaotolewa na magari yanayotumia mafuta ya dizeli huenda unachangia katika ongezeko la vifo vinavyosababishwa na hora ya mapofu (nimonia).

Watafiti kutoka chuo kikuu kimoja walibaini kwamba hewa iliyochafuliwa na moshi wa mafuta ya dizeli inaweka watu katika hatari ya kupatwa na maradhi ambayo ni hatari ya nimonia. Aidha, utafiti huo unasema kuwa watu wanaopumua hewa iliyo na moshi wa mafuta ya dizeli wanakuwa na uwezekano mkubwa wa kupatwa na nimonia ambayo husababishwa na bakhteria wanaojulikana kama 'Streptococcus pneumonia.

Bakhteria hao ndio husababisha maradhi ya nimonia na homa ya uti wa mgongo. Magonjwa haya huchangia kwa kiasi kikubwa vifo vya watoto wachanga walio chini ya miaka mitano. Kadhalika, husababisha vifo vya maelfu ya watu wazima kote duniani. Takwimu zilizotolewa zinaonyesha kuwa tangu mwaka wa elfu mbili kumi na tano, maradhi ya nimonia yamekuwa yakiongoza kwa kusababisha idadi kubwa ya vifo humu nchini. Licha ya hayo, kulingana na ripoti kuhusu hali ya kiuchumi ya mwaka wa elfu mbili, kumi na nane iliyotolewa na Shirika la Takwimu Nchini, waliouawa na maradhi ya nimonia ni karibu mara nne kuliko waliofariki kutokana na ukimwi.

Ugonjwa wa nimonia uliua watu elfu ishirini na moja, mia mbili tisini na watano na elfu ishirini na mbili, mia nne sabini na watatu katika mwaka wa elfu mbili kumi na sita na elfu mbili kumi na tano mtawalio. Ni wazi kama mchana kuwa magonjwa mengine yaliyoangamiza idadi kubwa mwaka wa elfu mbili kumi na saba ni malaria ulioua watu elfu kumi na saba, mia tano hamsini na watu elfu kumi na sita, mia tisa hamsini na watatu.

Mnamo mwaka wa elfu mbili na kumi na nane, watu milioni moja na elfu mia nne walienda hospitalini kutibiwa nimonia na mwaka uliotangulia wa elfu mbili, kumi na saba, watu milioni moja na elfu kumi na saba. Watu milioni moja na elfu mia mbili waliitafuta matibabu ya nimonia katika hospitali kote nchini. Takwimu za wizara ya afya zinaoonyeha kuwa watoto elfu mia saba hutibiwa maradhi ya nimonia kila mwaka. Licha ya takwimu hizo zilizotelewa, jambo la kusikitisha ni kwamba karibu asilimia ishirini na tano hufariki kwa sababu huchelewa kupelekwa hospitalini wanapougua maradhi hayo.

Ripoti iliyotolewa na shirika moja lisilo la serikali mnamo mwaka wa elfu mbili kumi na saba, ilionyesha kuwa vipimo visivyotoa matokeo sahihi na uhaba wa dawa za kukabiliana na bakhteria ni miongoni mwa sabab zinazochangia katika ongezeko la vifo vinavyotokana na nimonia. Wanasayansi waliohojiwa walisema kuwa ugonjwa huo ukigunduliwa mapema unatibika kwa dawa inayouzwa kwa shilingi mia mbili. Isitoshe chanjo ya kukabiliana na maradhi ya nimonia ilianza kutumika humu nchini mnamo mwaka wa elfu mbili, kumi na moja kwa watoto wa kati ya umri wa wiki sita na kumi na nne.

Lakini takwimu zilionyesha kuwa zaidi ya watoto elfu mia nne na kumi na nane wa umri wa miczi kumi na miwili na ishirini na mitatu hawakupewa chanjo hiyo mnamo mwaka wa elfu mbilli kumi na saba. Vifo vilivyotokana na nimonia huenda vikaendelea kushuhudiwa humu nchini kwani takwimu zinaonyesha kuwa kiwango cha mafuta ya dizeli yanayotumiwa humu nchini kinaongezeka kila mwaka.

  1. Kulingana na aya ya kwanza, imebainika kuwa
    1. wakenya takriban elfu kumi na tano walihusika katika ajali za barabarani mwaka jana.
    2. wakenya zaidi ya elfu kumi na tano walihusika katika ajali mwaka jana. 
    3. wakenya zaidi ya elfu sita na mia sita walijeruhiwa katika ajali za barabarani mwaka jana.
    4. utafiti umekuwa ukifanyika kila uchao ili kutambua idadi ya walioumia katika ajali ya barabarani.
  2. Ni kweli kuwa moshi unaotolewa na magari yanatumia mafuta ya dizeli.
    1. umechangia katika ongezeko la ajali barabarani.
    2. umeongeza maambukizi ya nimonia.
    3. yanawezekana kuwa umechangia katika ongezeko la vifo visababishwaVyo na nimonia. 
    4. umechangiwa na kukithiri kwa vifo vya homa ya mapafu.
  3. Neno 'walifariki' halimaanishi kuwa
    1. waliaga dunia 
    2. walienda na ulele ngoma
    3. walifumwa na mvi wa manaya 
    4. walienda nguu.
  4. Kifungu kimedhihirisha kuwa vifo vya watoto
    1. wachanga kwa kiasi kikubwa husababishwa na homa ya mapafu na homa ya uti wa mgongo. 
    2. wachanga walio chini ya miaka mitano husababisha maambukizi ya nimonia.
    3. wachanga walio juu ya miaka mitano husababishwa na nimonia na homa ya uti wa mgongo.
    4. wachanga na watu wazima walio chini ya miaka mitano husababishwa na nimonia na homa ya uti wa mgongo.
  5. Maneno ni wazi kama mchana' yametumia fani gani ya lugha?
    1. Nahau 
    2. Chuku
    3. Tashbihi
    4. Tasfida
  6. Makala yameeleza kuwa watu waliouawa mwaka wa elfu mbili kumi na tano kutokana na nimonia ni 
    1. 21295 
    2. 22473 
    3. 17553 
    4. 16953
  7. . ... asilimia ishirini na tano hufariki kwa sababu huchelewa kupelekwa hospitalii...' kauli hii inaweza ikaelezwa kwa methali ipi? 
    1. Simba mwenda pole ndiye mla nyama. 
    2. Fisi akimla muwele mzima funga mlango. 
    3. Kifo cha wengi harusi.
    4. Akutanguliaye chanoni hukuzidi tonge.
  8. Kulingana na aya ya sita, ni kweli kuwa
    1. ongezeko la vifo vinavyotokana na nimonia husababishwa na ukosefu wa damu za kukabiliana na bakhteria. 
    2. ukosefu wa dawa na vipimo visivyotoa matokeo ni sababu zinazochangia ongezeko la vifo vya nimonia.
    3. upungufu wa dawa na vipimo visivyotoa matokeo sahihi na sababu zingine huchangia ongezeko la vifo vitokanavyo na nimonia.
    4. vifo vinavyotokana na nimonia huchangia uhaba wa dawa na vipimo duni.
  9. Ongezeko la matumizi ya mafuta ya dizeli
    1. litaongeza matumizi ya magari 
    2. linaweza likaongeza vifo vinavyotokana na nimonia 
    3. limesababishwa na maambukizi mengi ya ugonjwa wa nimonia.
    4. limechangia kutokea kwa ajali nyingi za barabarani.
  10. Ili kupunguza vifo vinavyotokana na maambukizi ya nimonia 
    1. tunafaa kubuni vifaa vinavyotoa matokeo sahihi.
    2. tunafaa kutafuta mikakati kabambe ya kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa nimonia. 
    3. tunafaa kutafuta dawa za kutosha ili kutibu ugonjwa wa nimonia.
    4. tunafaa kuimarisha usafiri ili wagonjwa wafikishwe hospitalini mapema.


MARKING SCHEME

  1. A
  2. D
  3. D
  4. B
  5. C
  6. D
  7. B
  8. A
  9. A
  10. C
  11. B
  12. C
  13. D
  14. D
  15. A
  16. D
  17. D
  18. A
  19. B
  20. B
  21. D
  22. D
  23. B
  24. C
  25. D
  26. B
  27. D
  28. B
  29. C
  30. A
  31. C
  32. B
  33. D
  34. A
  35. A
  36. A
  37. A
  38. B
  39. B
  40. B
  41. C
  42. C
  43. D
  44. A
  45. C
  46. B
  47. D
  48. C
  49. B
  50. B
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Class 8 End Term 2 Exam 2021 Set 1.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students