Thursday, 01 September 2022 08:48

Kiswahili Questions and Answers - Class 8 End term 2 2022 Set 1

Share via Whatsapp

Maswali

Soma vifungu vifuatavyo kisha ujibu maswali 1 - 15 ukitumia jibu sahihi

Mtoto    1    mvulana    2      umri wa miaka kumi na mitano    3    na simba katika     4     cha Gakoigo karibu na mji wa Nairobi mnano Jumamosi wiki    5    kulingana na kituo cha polisi cha Wema. Mkasa huo ulitokea nyumbani kwa Bwana na Bi. Stano.     6    mtoto huyu    7    mkasa huo alisema kuwa    8    ya kula pamoja    9     , aliondoka kwenda katika chumba cha kulala hatua hamsini kutoka nyumbani kwa wazaziwe.

  A B C D
1  moja   mmoja  umonja  monja
2  chenye  wenye  yenye  mwenye
3  alishambulia  alishambuliwa  alimshambulia  alishambua
4  kitongoji  mji  kitongojini  kijijini
5  kesho  leo   jana   ijao
6  Mamake  Mamaze  Mamaye   Mamao
7  akasimulia  akisimulia  akipeana  akitowa
8  badala  baada  baadhi  baadaye
9   staftahi  kishuka  chajio  msosi


Ama kweli, zaraa    10    uti wa mgongo wa taifa     11    Kamwe hatuwezi kuishi bila kutia chakula   12    tumboni. Chakula hiki    13    hutokana na kilimo. Yafaa vijana    14     kuhusu umuhimu wa kilimo ili    15    kwa hamu kuu.

  A B C D
10  ndio  ndicho  ndiyo  ndilo
11  yetu  letu  zetu  mwetu
12  yeyote  chochote  lolote  yeyote
13  naye  nalo  nacho  nayo
14  washurutishe   wakatiliwe  wahukumiwe  wahamasishwe 
15  wakikumbatie   walikumbatie   wamkumbatie   wazikumbatie 


Kutoka swali la 16 hadi 30. jibu kila swali

  1. Mtu akisema kisu hiki ni wembe, maana yake
    1. kidogo
    2. butu
    3. kizee
    4. kikali
  2. Jaza pengo kwa usahihi;
    Mkutano ulihudhuriwa na watu wengi sana.
    Yaani wake _______ wanaume, 
    1. na
    2. pamoja
    3. kwa
    4. pa
  3. “Nilikuona jana.' Sentensi hii inaonyesha kuwa kulingana na maagizo. aliyeonwa ni nani? 
    1. Yeye
    2. Wewe
    3. Mimi
    4. Nyinyi
  4. Maji yaliyoganda na kuwa magumu kama jiwe  huitwa;
    1. mvuke
    2. mangati
    3. theluji
    4. barafu
  5. Kitenzi 'choka' katika kauli ya kutendesha  kitakuwa;
    1. chokwa
    2. chosha
    3. chokesha
    4. chokea
  6. Kanusha sentensi.
    Wewe umekuja.
    1. Wewe hujakuja.
    2. Wewe haujaja.
    3. Wewe hujaja.
    4. Wewe haujakuja
  7. Milioni tatu, mia tatu na thelathini elfu, mia sita na tisa kwa tarakimu itakuwa;
    1. 3330609
    2. 3300906
    3. 3030609
    4. 3303699
  8. Mtaalamu aliye na ujuzi mkubwa wa utengenezaji wa barabara anaitwa;
    1.  mhasibu
    2. mhandisi
    3. mhazili
    4. mhazigi
  9. Kipini huvaliwa kwenye; 
    1. uti wa pua
    2. sikio 
    3. shingo
    4. pua
  10. Chagua sentensi ambayo imetumia kivumishi  kisisitizi kwa usahihi.
    1. Viti vivi hivi ni vya wageni
    2. Watu hawa hawa nawajua
    3. Matunda haya yaya yameiva
    4. Vyungu zizi hizi ni ghali
  11. Kamilisha methali;
    Usitukane wakunga;
    1. kabla ya kuvuka mto
    2. na kizazi kingalipo
    3. usije ukafa mzigana 
    4. kabla ya kukata mbeleko
  12. Mke wa mjomba huitwa; .
    1. mbiomba
    2. mkwarima
    3. mkemwenza
    4. mkaza mjomba
  13. Kanusha sentensi hii;
    Ningemsaidia angefurahi.
    1. Singemsaidia asingefurahi
    2. Singemsaidia asingefurahi
    3. Ningamsaidia asingefurahi
    4. Nisingemsaidia asingefurahi
  14. Jaza pengo kwa usahihi;
    Wanafunzi ______  walifanya mtihani vizuri.
    1. kumi
    2. wasaba
    3. tano
    4. wakumi
  15. Andika sentensi kwa udogo;
    Mtoto yule mdogo analia.
    1. Kitoto yule mdogo analia.
    2. Kitoto kile kidogo analia.
    3. Kitoto kile kidogo kinalia
    4. Katoto kale kadogo kanalia

Soma kifungu hiki kisa wjibu maswali 31 - 40.

           Ni jambo la kusikitisha mno tunapoona jinsi vijana wanavyojitumbukiza katika janga la kutumia au kuuza mihadarati kwani vijana ndio nguzo na matarajio ya taifa lolote.
           Ni matarajio ya umma wowote kuwakuta vijana wakitumia nguvu zao katika kuimarisha na kulijenga taifa badala ya kuzama katika shughuli za dawa za kulevya.
           Wimbi hili la kutumia mihadarati limeingia kwa kasi kubwa na yote ni kwa sababu ya uhaba wa kazi, ukosefu wa mwelekeo na wa maongozi kwa vijana hawa. Zaidi ya hayo, wale matajiri walafi ndio wanaowapotosha vijana kwa kuwaingiza katika janga la kuuza mihadarati. Vijana hawa wanakubali kuwa
makala wa matajiri wenye uroho. Hii ni kwa vile wanavutiwa na malipo ya juu wanayolipwa hasa wakilinganisha wepesi wa kazi hizo na pato lake.

           Bila shaka muuza mafuta mazuri lazima ajipake ili kuwavutia wanunuzi. Vivyo hivyo, muuza mchuzi inambidi kuonja kukolea kwa chumvi ili kuhakikisha kuwa mapishi ni ya hali ya juu. Lazima atumie angalau kwa kiasi kidogo mwanzoni kabla ya kitendo hicho kuwa ni uraibu na ada asiyoweza kuiepuka kwa hali yoyote ilivyo.
           Vijana ni rasilimali kuu kwa nchi na jamii yoyote kuwaacha kupotea katika uraibu huu mikononi mwa mabepari walafi na waroho ni kama kuwakubalia kuwa mshumaa.
           Visa vya vijana waliojiangamiza wenyewe, kama afanyavyo pweza anapokaangwa, ni vingi na vya kuhuzunisha. Wamemalizika wakiwa hohehahe na mwishowe tutakuwa na taifa la mbumbumbu na maamuna lisilokuwa na mawazo wala msimamo.

  1. Mwandishi anasikitika kwa sababu;
    1.  ya matumizi na uuzaji wa mihadarati
    2. mihadarati ni ghali
    3. vijana wanapotea
    4. ya ugonjwa unaoenea
  2. Mihadarati ni;
    1. dawa za kulevya
    2. sigara b
    3. angi
    4. ulevi
  3. Matarajio ya taifa lolote kwa vijana ni; 
    1. kujenga taifa
    2. kusambaza mihadarati
    3. kuhujumu taifa
    4. kutumbukia katika mihadarati
  4. Vijana wanaingizwa katika shughuli za kuuza  mihadarati na;
    1. polisi 
    2. wazazi
    3. viongozi
    4. matajiri
  5. Ipi si sababu kuu ya vijana kutumia mihadarati?
    1. Ukosefu wa maongozi
    2. Ukosefu wa elimu
    3. Marafiki wabaya
    4. Uhaba wa kazi
  6. Vijana wanakubali kuuza mihadarati kwa sababu ya;
    1. kuipenda kazi hiyo 
    2. kulazimishwa
    3. kutoroka kazi
    4. malipo mazuri
  7. Ni kina nani kati ya hawa wanaowaingiza vijana katika  ulanguzi wa mihadarati?
    1. Wakwasi wenye mate ya fisi
    2. Marafiki ambao ni kielelezo bora
    3. Fakiri wasiokuwa na mbele wala nyuma
    4. Watu wa hirimu yao
  8. Maana ya 'uraibuni' ni;
    1. kuharibu jambo
    2. kupendelea jambo au kitu 
    3. kujaribu mara kwa mara
    4. kupendelea kitu kizuri
  9. Kukubali kuwa mshumaa inamaanisha;
    1. kujisaidia binafsi 
    2. kupambana na wengine
    3. kupoza wengine
    4. kutumiwa kufaidi wengine
  10. Methali inayomhusu pweza makala haya katika inasema 'umekuwa pweza ......'
    1. huogopi mtu
    2. huwezi kukosa ulipendalo
    3. waishi baharini tu
    4. wajipalilia makaa

Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali 41 hadi 50.

           Nilizaliwa na kulelewa katika familia iliyotajika. Baba yangu Mlajasho alikuwa tajiri wa mali na moyo. Mimi na ndugu yangu mdogo hatukujua maana ya uhitaji kwani baba alitukidhia mahitaji yetu yote. Nyumbani mwetu kila siku mlishiba na kutapika watu wa kila sampuli waliokuja kulilia hali kwa baba. Baba aliwasabilia kwa mengi. Kuna waliopewa ruzuku mbalimbali za vyakula, kuna waliopewa vibarua mashambani na waliofanya kazi pale nyumbani.
           Almuradi kila mwanakijiji alifaidika kutokana na mkono wazi wa baba. Ndugu yangu mdogo hakuisha kuwabughudhi waja hawa na kuwaita waegemea nundu.
           
Siku zilisonga na kupita kama maji ya mto, hata nikajipata katika shule ya msingi. Niliyakumbatia masomo yangu kwa hamu kubwa. Sikuwa na wakati wa kufanya ajizi, kwani baba pamoja na pato lake nono hakuwahi kudekeza hisia za ugoigoi. Nasi ilibidi tufuate nyayo zake, kwani mwana akibebwa hutazama kisogo cha nina. Nilifanya mtihani wangu wa darasa la nane na kuvuna nilichopanda. Asubuhi baada ya kutangazwa kwa matokeo ya mtihani huo niliamshwa na sauti ya “pongezi mwanangu,” kutoka kwa baba. Baba alikuwa amebeba gazeti la siku hiyo, usoni amevaa tabasamu kubwa. Sikuamini maneno yake. Nilimnyang'anya gazeti na ikawa kweli mwenye macho haambiwi tazama. Nilikuwa mwanafunzi bora nchini. Nilijiunga na shule mojawapo ya kitaifa.
           Siku nilipokuwa kizingitini cha lango la shule ya kitaifa ya Tindi ndipo maisha yangu yalipoanza kuingia ufa.Nilikutana na Tamasha, mwanafunzi mchangamfu na mcheshi. Alijitambulisha kuwa alisomea shule iliyokuwa jirani na ile yangu ya msingi. Urafiki shakiki ukazaliwa kati yake nami. Tukawa daima tunaandamana. Hayo hayakunitia shaka, kwani Tamasha, alinihimiza kila mara nitie bidii masomoni. Hata hivyo, jinsi siku zilivyosongea ndivyo tabia yake halisi ilivyonibainikia.
Jioni moja Tamasha alikuja chumbani mwangu akiwa amebeba unga aliouita dawa ya homa, Aliniambia ibu kutibu homa ambayo ilikuwa imenikaba kwa siku ayami. Nami kwa kutotaka kumvunja rafiki yangu, nikachukia unga huo na kuutia kinywani; ingawa kwa kweli mwalimu wetu alikuwa ametuonya dhidi ya kutumia dawa zozote bila maelekezo ya daktari. Unga huo haukuitibu homa yangu, ila ulinipa utulivu mkubwa wa akili, utulivu ambao sikuwa nimewahi kuushuhudia maishani.
           Tamasha alifika chumbani mwangu usiku kunijulia hali. Alinipata nimejituliza juu ya kitanda changu, Alinisalimu na kukenua kama aliyetarajia jawabu fulani kutoka kwangu. Nilimweleza hali yangu naye akaniambia kuwa hivyo ndivyo dawa hiyo ifanyavyo kazi; kwamba amekuwa akiitumia kwa muda, hata nyakati za mtihani, naye hupata nguvu za kukabiliana na majabali yote. Alinielekeza kwa Mzee Kamaliza ambaye ndiye alimuuzia unga huo. Kuanzia siku hiyo, nikawa mteja mwaminifu wa Mzee Kamaliza. Nilitumia unga huo bila fikira nikidhani kuwa ilikuwa dawa ya homa tu! Sukujua ilikuwa dawa ya kulevya na alikuwa mraibu sugu wa dawa hiyo na nyingine nyingi!
           "Uzuri wake huu ni wa mkakasi tu?” Nilijiuliza. “Laiti ningalijua.” Hata hivyo, maswali yote haya hatakuwa na faida tena. Nilikuwa tayari nimazama katika tatizo sugu la matumizi ya dawa za kulevya,
           Nilijisuta moyoni kwa matumizi ya dawa za kulevya ambayo yalinielekeza kuytagongesha mwamba maisha yangu shuleni. Hata hivyo, haikuwa rahisi kuacha kwani nilichelea kuitwa kimbukeni na wenzangu. Matokeo ya haya yote yakawa kuzorota kwa masomo yangu. Walimu hawakuchelewa kuona mabadiliko yaliyonikumba. Walijaribu kunishauri na kutaka kujua kilichokuwa kikinisumbua. Walipoona kwamba hali yangu haibadiliki na kwamba nimeshindwa kuwaambia tatizo langu, walimjulisha mwalimu mkuu ambaye hakukawia kumwita baba. Mazungumzo kati ya baba na mwalimu mkuu yalinitia fadhaa kubwa kwani sikutaka kuwaambia nilitumia dawa za kulevya, ingawa kwa kweli mwalimu mkuu alishuku. Walijaribu kunishika sikio kuhusiana na tabia hii yangu lakini tangu lini sikio la kufa likasikia dawa? Niliendelea na uraibu wangu hadi siku nilipofunzwa na ulimwengu baada ya kufumaniwa na naibu wa mwalimu mkuu wa shule mjini nikipiga maji. Nilipewa adhabu niliyotarajia. Nilijipata nyumbani kwa muda wa mwezi mzima, nikiuguza vidonda vya moyo na akili. Kijiji kizima kilijua nimefukuzwa shule kwa sababu ya matumizi ya dawa za kulevya. Sikuwa na pa kuutia uso wangu. Hata hivyo, hili lilikuwa funzo kubwa kwangu.
           Mama yangu aliweza kunipa nasaha na kunishauri niache kutumia dawa hizo. Mara hii, maneno aliyoniambia yalikuwa na maana. Niliyasikiliza kwa makini hata baba alipopata barua kumwarifu anirejeshe shule. Nilikuwa nimeamua kujiunga na chama cha vijana wanaopigana na matumizi mabaya ya dawa shuleni. 

  1. Mambo yanayoonyesha kuwa Mlajasho alikuwa tajiri wa mali na moyo ni;
    1. kukidhi mahitaji ya wana, watu kufurika kwake
    2. kukidhi mahitaji ya wana, kumkana mwanawe
    3. kukidhi mahitaji ya wana, kuwapa watu riziki
    4. kukidhi mahitaji ya wana, watu kumlilia hali
  2. “Ndugu yangu mdogo hakuisha  kuwabughudhi waja hawa na kuwaita waegemea nundu" inaonyesha kuwa ndugu mdogo alikuwa;
    1. mwenye uchoyo
    2. mwenye mapuuza
    3. mwenye kujisifu
    4. mwenye uzushi
  3. Msimulizi alisoma kwa hamu kwa kuwa;
    1. alipenda masomo yake
    2. baba yake alikuwa mwenye bidii
    3. baba yake alikuwa mkali
    4. alitaka kufuata nyayo za ndugu yake
  4. Kifungu 'ndipo maisha yangu yalipoanza kuingia ufa' kinamaanisha;
    1. maisha ya msimulizi yalianza kupata matatizo
    2. maisha ya msimulizi yaliporomoka
    3. maisha ya msimulizi yalianza kubadilika
    4. maisha ya msimulizi yaliharibika mara moja
  5. Msimulizi hakutaka kuacha 'unga' kwa sababu;
    1. alichelea kudunishwa na wenzake
    2. alichelea kuondolewa kundini na wenzake
    3. hakutaka kumuudhi Tamasha
    4. alikuwa amezoea uraibu kwa Kamaliza
  6. Mambo yanayoonyesha kuwa kifungu hiki kinapinga matumizi ya dawa za kulevya ni;
    1. msimulizi kufukuzwa shuleni, msimulizi  kujiunga na vijana wanaopinga matumizi mabaya ya dawa shuleni
    2. walimu kumshauri msimulizi, mama pamoja na mwalimu mkuu kumwonya msimulizi shuleni
    3. Kamaliza kuacha kuuza dawa, mama  kumshauri msimulizi
    4. mwalimu kugundua tatizo la msimulizi,  msimulizi kurudi shuleni 
  7. Kulingana na kifungu hiki, jamii inakabiliana na  tatizo la matumizi mabaya ya dawa kwa;
    1. wazazi kwenda shuleni wanapoitwa,  kuwajibika kwa vijana 
    2. ushirikiano kati ya wazazi na walimu,  kuwajibika kwa vijana
    3. ushirikiano kati ya wazazi na walimu,  kuaibika kwa vijana .
    4. kuwapeleka watoto shuleni, matajiri kuwasaidia watu
  8. Methali ambayo haifai kujumlisha ujumbe wa  taarifa hii ni;
    1. mchovya asali hachovyi mara moja
    2. mtegemea nundu haachi kunona
    3. mchezea tope humrukia 
    4. nazi mbovu harabu ya nzima 
  9. Uzuri wake huu ni wa mkakasi tu' ina maana  kuwa;
    1. hakuweza kutegemewa
    2. hakuweza kuaminika
    3. alikuwa mnafiki
    4. alikuwa mcheshi
  10. Msimulizi alikuwa 'sikio la kufa' kwa sababu;
    1. alipata adabu aliyotarajia baada ya kupiga  maji
    2. alifumaniwa na naibu wa mwalimu mkuu akipiga maji 
    3. hakuacha uraibu wake baada ya kuonywa  na baba na mwalimu
    4. hakupona homa baada ya kutumia unga

INSHA

Andika insha ya kusisimua itakayomalizika kwa maneno haya

...nilipowaona marafiki wangu, ni8lifurahi si haba. Tuliungana na kurudi nyumambani kwa furaha.

Majibu

  1. B
  2. D
  3. B
  4. A
  5. B
  6. C
  7. B
  8. D
  9. B
  10. C
  11. B
  12. B
  13. C
  14. D
  15. A
  16. D
  17. C
  18. B
  19. C
  20. B
  21. C
  22. A
  23. B
  24. B
  25. A
  26. B
  27. D
  28. D
  29. A
  30. C
  31. A
  32. A
  33. A
  34. D
  35. B
  36. D
  37. A
  38. B
  39. D
  40. D
  41. A
  42. A
  43. C
  44. A
  45. C
  46. A
  47. B
  48. B
  49. A
  50. C
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Class 8 End term 2 2022 Set 1.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students