Tuesday, 24 January 2023 09:49

Kiswahili Questions and Answers - Class 8 Term 1 Opener Exams 2023 Set 1

Share via Whatsapp

MASWALI  

Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne hapo Jaza kila pengo kwa kuchagua jawabu lifaalo zaidi.

Kufaulu kwa kila mmoja katika maisha ___1___ mambo mengi ___2___ mambo hayo ni bidii. ___3___ ukafaulu katika jambo ___4___ bila kuwa ___5___ bidii. ___6___,kuna watu wengi wanaopenda ____7____ katika maisha. Si ajabu kuwapata wanafunzi ___8___ kusoma wala kufanya kazi wanazopewa kwa bidii. Wanafunzi kama hao wanafaa kukumbushwa kuwa ___9___

  1.  
    1. inategemea
    2. kunategemea
    3. yanategemea
    4. anategemea
  2.  
    1. Baadhi ya
    2. Kati ya
    3. Katika
    4. Miongoni ya
  3.  
    1. Hauwezi
    2. Hawezi
    3. Hatuwezi
    4. Huwezi
  4.  
    1. yeyote
    2. wowote
    3. yoyote
    4. lolote
  5.  
    1. ambaye
    2. wenye
    3. mwenye
    4. ambao
  6.  
    1. Hata hivyo
    2. Hata ingawa
    3. Hata kama
    4. Hata kuwa
  7.  
    1. kujifunga kibwebwe 
    2. kulaza damu
    3. kufa kikondoo
    4. kuambulia patupu
  8.  
    1. wasiyependa
    2. wanaopenda
    3. wasiopenda
    4. wanayependa
  9.  
    1. siku za mwizi ni arubaini
    2. akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki
    3. mgaagaa na upwa hali wali mkavu
    4. wapishi wengi huharibu mchuzi

Ni kweli kuwa msimu ___10___ uchaguzi umekaribia sana. Huu ___11___ wakati wa kufanya uamuzi wa busara kuhusu viongozi ___12___ kwa miaka ___13___ ijayo. Tatizo ___14___  hutusumbua kila wakati wa uchaguzi ni ukabila na tamaa. Kuna wakenya ambao hufanya uamuzi kwa kuzingatia kabila la mtu ama pesa walizopewa wakati wa uchaguzi. Tunafaa kumchagua mtu aliye na___15___ ya kutuletea maendeleo.

  1.  
    1. wa
    2. ya
    3. la
    4. cha
  2.  
    1. ndilo
    2. ndiwo
    3. ndiyo
    4. ndio
  3.  
    1. vitakavyotuongoza
    2. wataotuongoza 
    3. vitavyotuongoza
    4. watakaotuongoza
  4.  
    1. tano
    2. mitano
    3. kumi
    4. sita
  5.  
    1. ambayo
    2. ambao
    3. ambalo
    4. ambazo
  6.  
    1. uwezo
    2. mpango
    3. pesa
    4. mipango

Kuanzia swali la 16-30, libu kulingana na. maagizo

  1. Tambua sentensi iliyo katika hali tegemezi.
    1. Mwanafunzi amekamilisha kuandika insha. 
    2. Ukimaliza kazi hiyo utapewa zawadi.
    3. Mwanafunzi asomaye kwa bidii hupewa zawadi.
    4. Angehifadhi mazingira angekuwa na afya bora
  2. Maamkuzi gani ambayo hutumika asubuhi pekee?
    1. chewa, sabalkheri, umeamkaje
    2. masalkheri, umeshindaje, chewa
    3. cheichei, masalkheri, alamsiki
    4. alamsiki, buriani, kwaheri
  3. Chagua wingi wa
    Seremala alitengeneza meza akampa mkunga.
    1. Waseremala walitengeneza meza wakawapa wakunge.
    2. Maseremala walitengeneza meza wakawapa mikunga.
    3. Maseremala walitengeneza meza wakawapa wakungs.
    4. Waseremala walitengeneza meza wakawapa mikunga.
  4. Sentensi gani iliyotumia nusukoloni? 
    1. Alitembelea miji mingi: Nakuru, Mombasa, Kisumu na Nairobi.
    2. Ugonjwa wa UKIMW! ni hatari; hauna tiba.
    3. Fuata maagizo kwa kuwa asiyesikia la mkuu...
    4. Ng'ombe wameshambuliwa na mbung'o.
  5. Omolo alikuwa na robo moja ya chungwa, akaigawa vipande viwili sawa. Je, akisami gani iliyopatikana?
    1. ½
    2. ¼
    3. 1/8
    4. 2/4
  6. Upi ukubwa wa
    Mtoto aliona ndovu akimfukuza ng'ombe.
    1. Jiloto liliona jidovu likilifukuza jigombe. 
    2. Toto liliona dovu likilifukuza gombe. 
    3. Kitolo kilikiona kidovu kikifukuza kigombe.
    4. Jitoto aliona jindovu akimfukuza jing'ombe.
  7. Tambua ukanusho wa
    Unga uliomwagika ni wa nyanya.
    1. Unga asiomwagika ni wa nyanya.
    2. Unga usiomwagika si wa nyanya. 
    3. Unga uliomwagika ni wa nyanya.
    4. Unga ambao haujamwagika ni wa nyanya. 
  8. Ulinganisho upi ambao ni tofauti?
    1. kipusa -- mrembo
    2. buda-ajuza
    3. banati- msichana
    4. jogoo - jimbi
  9. Chagua sentensi iliyotumia kivumishi kiulizi.
    1. Mwanafunzi mzuri atapewa kitabu gani?
    2. Musa alifundishwa kuboresha hali na nani?
    3. Matokeo ya mtihani yatatangazwa lini? 
    4. Unatoka wapi wakati huu wa usiku? 
  10. Pesa ambazo hutumika kuanzisha biashara huitwaje?
    1. mtaji
    2. arbuni
    3. riba
    4. karadha
  11. Sentensi ipl iliyotumia kiwakilishi cha nafsi ya tatu?
    1. Mimi nimependezwa na ukarimu wako.
    2. Wewe na yeye mtakutana kesho.
    3. Sisi tulikamilisha upanzi wa miti mapems.
    4. Nyinyi mnaitwa na mwalimu.
  12. Tambua aina za maneno yaliyopigiwa mistari.
    Huyu amenunua gari jipya.
    1. kiwakilishi, kivumishi
    2. kivumishi, kielezi
    3. kivumishi, kivumishi
    4. kiwakilishi, kielezi
  13. Kiambishi 'ki' kimetumikaje katika sentensi hii?
    Musa akifika Mombasa atanunua kijibwa.
    1. wakati, kielezi
    2. wakati, udogo
    3. masharti, kielezi
    4. masharti, udogo
  14. Sentensi ifuatayo itaandikwaje katika kauli ya kutendwa?
    Kinyozi amenyoa nywele za Omari.
    1. Nywele za Omari zimenyolewa na kinyozi.
    2. Omari antenyolewa nywele na kinyozi
    3. Kinyozi alimnyoles Omari nywele.
    4. Kinyozi alinyolewa nywele na Omari.
  15. Orodha gani iliyo na sauti ghuna pekee?
    1. b, z, d
    2. f, s, t
    3. th, dh, sh
    4. h, k, p

Soma ufahamu kisha ujibu maswali 31-40  

Hewaa! Bila shaka, sote tulikuwa tumeisuburu siku hii kwa hamu na ghamu. Nami sitapoteza hata punje ya sekunde. Nitatumia fursa hii adimu na adhimu kukufafanulia mambo unayofaa kuyafanya ili ufaulu katika mtihani wa kitaifa. Ni bayana na wazi kama meno ya ngiri kuwa sasa wewe ni mwanafunzi wa darasa la nane. Muda nao haupo, una miezi michache sana kabla ya kuufanya mtihani wa kitaifa wa darasa la nane. Je, umejiandaa vipi? Unawezaje kutumia muda huu mfupi uliosalia ili kufua dafu katika mtihani wako?

Awali ya yote, ni lazima kama ibada kuwa mwenye bidii. Naam, bidii hulipa. Bidii ndilo daraja la kukuvusha hadi katika kisiwa cha ufanisi. Fanya kazi unazopewa na mwalimu kwa moyo wako wote. Kazi za kiada na ziada zisipuuzwe hata kidogo. Usikubali kulaza damu na kuwa mtepetevu. Masomo yapewe kipaumbele ikiwa unataka kufaulu. Licha ya hayo, tumia muda wako vizuri. Wakati ni upepo, haumsubiri mwana wa mfalme. Muda ukienda haurudi Jambo linalofaa kufanywa leo lifanywe leo. Usijiambie kuwa nitafanya kesho. La hasha! Wakati uliotengewa kusoma utumike kwa kusoma. Ule uliotengewa kucheza uwe wa kucheza. Usipoteze wakati ukitazama runinga au kucheza na marafiki hapa na pale. Hilo uliepuke.

Aidha, ni muhimu kuwachagua marafiki zako kwa hekima na busara. Lazima unajua wanafunzi katika darasa lenu ambao wanapenda kusoma na wale wasiokuwa na haja na masomo. Wale wapendao masomo ndio wanaofaa kuwa marafiki zako. Hao watakufaa na kukuelekeza katika mambo ambayo huyajui. Watakusaidia unapokuwa na tatizo katika somo lolote. Kwa upande mwingine, kuna wanafunzi ambao kazi yao kuu ni mchezo na kuchekacheka darasani. Wanapopata nafasi yoyote, pengine mwalimu hajaingia darasani au hakuja shuleni, wao huipokea nafasi hiyo kwa furaha ili wacheze na kuwasumbua wenzao. Kutembea au kusuhubiana na watu kama hao ni kujiingiza katika kichaka cha simba ukiona. Tabia za mtu hutegemea sana tabia za watu anaotembea nao. Marafiki wabaya wanaweza wakafanya uwe mwenye tabia mbaya. Hilo usisahau.

Vilevile, usichoke kuuliza maswali na kufanya utafiti. Wahenga walisema kuwa kuuliza si ujinga, ni kutaka kujua. Kila unapokuwa na swali ama jambo usilolielewa, usione aibu wala haya. Uliza mwalimu wako ili akupe mwelekeo. Iwapo mwalimu hayuko na kuna mwanafunzi anayeweza kukueleza, basi tafuta msaada kwake. Kwa namna hiyo, utazidi kupata maarifa na kujiimarisha kimasomo. Usiwaogope wanafunzi ambao humcheka mwenzao anapouliza swali. Waache waendelee kucheka. Pengine hawajui kuwa mcheka kilema hali hakijamika. Kujisomea na kudurusu nako ni muhimu sana. Panga muda wako wa kujisomea ili kuelewa mambo ambayo hukuwa umeelewa vizuri. Fanya mazoezi ya mitihani iliyopita kisha ujisahihishie au mwalimu akusahihishie. Hakikisha kuwa unapata maelezo ya maswali uliyofeti na kufanya masahihisho. Kwa namna hii, utakuwa imara kama chuma cha pua.

Jambo jingine ambalo ni muhimu mno ni kumtanguliza Mungu. Mungu ndiye mpaji wa vyote. Ndiye ahakikishaye kwamba umelala na kuamka salama salimini. Afya yako, ja mwili na akili, i mikononi pake. Huwezi ukafaulu katika jambo lolote bila msaada wa Mungu. Juhudi zote unazoweka katika masomo yako si chochote si lolote bila uwezo wa Mwenyezi Mungu. Muu ndio ukweli wa kauli kuwa jitihada haiondoi kudura. Hatimaye, ni jambo la busara kutenga muda wa kupumzika vya kutosha. Hakuna awezaye kuchapa kazi bila kupumzika. Unafaa kupumzika kila baada ya kusoma kwa muda wa kutosha. Kupumzika huko kunajumuisha kulala ama kucheza na wenzako. Unapocheza kisha uoge na kupata usingizi wa kutosha, akili yako huwa na uwezo wa kuelewa mambo unayoyasoma kwa kasi sana. Ninakutakia kila la heri unapojiandes kwa mtihani wako mwisho wa mwaka huu.

  1. Tambua maana ya nahau kufua dafu namna ilivyotumika katika kifungu.
    1. kuwa mwenye bidii
    2. kufaulu katika jambo
    3. kutumia muda
    4. kujibu maswali
  2. Kulingana na aya ya pili, ni kweli kuwa;
    1. mwanafunzi anashauriwa kufanya bidi leo ili kesho apumzike.
    2. mwanafunzi anaweza kuutumia muda wake kwa jambo lisilofaa.
    3. mwanafunzi hafai kucheza wala kutazama runinga.
    4. mwanafunzi anashauriwa kuwaepuka marafiki maishani.
  3. Mwandishi amelinganisha bidii na nini katika aya ya pili?
    1. malipo
    2. daraja
    3. ufanisi
    4. kisiwa
  4. Aya ya tatu inadokeza kuwa darasani kuna wanafunzi;
    1. wanaopenda michezo na wasiopenda michezo
    2. wenye tabia nzuri na wasiokuwa na tabia
    3. wanaofaulu katika masomo na wanaoanguka mtihani
    4. wanaothamini masomo na wapendao kufanya mzaha
  5. Baini maana ya 'kujiingiza katika kichaka cha simba ukiona namna yalivyotumika katika kifungu
    1. kujitenga
    2. kujinusuru
    3. kujiepusha
    4. kujihatarisha
  6. Marafiki wabaya wanaweza wakafanya uwe mwenye tabia mbaya. Methali gani inayoweza kujumuisha ujumbe katika kauli hii?
    1. Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki. 
    2. Tabia ni ngozi.
    3. Baniani mbaya kiatu chake dawa.
    4. Nazi mbovu harabu ya nzima.
  7. Maneno imara kama chuma cha pua' ni mfano wa;
    1. tashbihi
    2. istiara
    3. nahau
    4. chuku
  8. Kifungu kinaeleza kuwa wanafunzi wanaowacheka wenzao wanaouliza maswali darasani;
    1. hawajui kuwa mcheka kilema hafi hakijamfika.
    2. wanafaa kupuuzwa na yule anayeuliza maswali.
    3. hawafai kufundishwa bali waachwe waendelee kucheka.
    4. hawatazidi kupata maarifa na kujiimarisha kimasomo.
  9. Kulingana na aya ya mwisho, ni kweli kuwa;
    1. Mungu humlaza na kumwamsha mwanafunzi.
    2. Ni vyema kupumzika kila wakati kwa muda wa kutosha.
    3. Kumtanguliza Mungu si muhimu kuliko mambo mengine yote.
    4. Kucheza na kupumzika huiwezesha akili kufanya kazi vyema zaidi.
  10. Kifungu hiki kinahusu
    1. jinsi ya kuufanya mtihani
    2. umuhimu wa kufaulu mtihani 
    3. faida za kuufanya mtihani
    4. maandalizi ya kuufanya mtihani

Soma ufahamu kisha ujibu maswali 41-50   

Daima siwezi kumsahau Mzee Saidia katika maisha yangu yote. Japo wasemao husema kuwa yaliyopita si ndwele tugange yajayo, kumsahau Mzee Saidia na wema wake si rahisi kama kula papai kwa kijiko. Mzee Saidia alikuwa jirani yangu aliyekuwa si maskini hohehahe wala tajiri wa kutajika. Alikuwa na duka moja pale sokoni Shibale alipouzia bidhaa rejareja. Kila nilipotumwa dukani na wazazi wangu, nilihakikisha kuwa nimenunua dukani pake kutokana na upole wake alipowahudumia wateja. Aghalabu duka hilo lilijaa wateja waliohiari kusubiri kwa muda mrefu ili wapate huduma nzuri. Wengine nao hawakuwa na pesa, haja yao ilikuwa kumlilia hali ili wakopeshwe. Mzee Saidia aliwasikiliza na kuwasaidia kulingana na uwezo wake. Duka lake lilifunguliwa asubuhi na mapema, lingekuwa wazi huku wateja wakiingia na kutoka hadi saa mbili au tatu za usiku.

Kuna wakati wazazi wangu walianza kuugua kutokana na maradhi yasiyokuwa na tiba. Juhudi zao za kutafuta matibabu hazikuzaa matunda. Haukupita muda mrefu kabla ya wazazi wangu niliowapenda kama mboni za macho kuzidiwa na maradhi. Walilala usingizi usiojua kuamka. Niliunawa uso wangu katika machozi yasiyojua kuwa kilio si dawa. Wanuna wangu nao walionekana kuzubaa tu, wasielewe kwa nini watu wengi walijaa nyumbani kwetu. Baada ya mazishi ya wazazi wangu, shangazi alichukua mnuna mmoja na mjomba akachukua mwingine. Mimi nilibaki na ami yangu aliyependa pombe kama uhai wake. Maisha katika nyumba ya ami yalikuwa magumu kama jehanamu. Kuenda shuleni kulikuwa ndoto ya mchana. Lishe bora nayo ulikuwa msamiati uliowekwa katika kamusi kimakosa.

Siku moja nilipigwa na butwaa nilipoona watu wakijaa katika boma. Wengi wao walikuwa waliokula chumvi nyingi. Mara nilipasuliwa mbarika kwamba nilifaa kukeketwa kulingana na mila na itikadi za jamii yetu. Licha ya watu wengi kuzitupilia mbali mila hizo zilizopitwa na wakati, kunao waliopuuza na kuzikumbatia. Nilitetemeka kama kijibwa kilichonusurika kumezwa na chatu. Nilifungwa maleso na kuelekezwa katika kijumba kilichokuwa kitalifa cha pua na mdomo kutoka kwa ami. Ghafla kama mawingu, niliona maafisa wa polisi wakijitokeza mbele yetu. Ami na baadhi ya watu waliohusika katika shughuli hiyo walitiwa mbaroni. Wengine wallfaulu kupiga mbio na kutokomea. Polisi hao walinifahamisha kuwa walipigiwa simu na Mzee Saidia, akawafahamisha kuhusu ukatili uliokuwa ukiendelea.

Mzee Saidia alinirudisha shuleni. Huko nilisoma kwa bidii za mchwa ajengaye kichuguu kwa mate. Mzee Saidia alinifaa kwa hali na mali. Alinichukulia kama mmoja wa watoto wake. Sote tulienda shuleni na kufaidi utamu wa masomo. Nililala katika chumba kimoja na mabinti zake. Wakati wa wikendi au likizo, tulifanya shughuli kadhaa za shambani na nyumbani. Mzee Saidia hakukubali hisia za uzembe wala ubaguzi. Baada ya masomo ya shule ya msingi. tuliendelea na masomo ya shule ya upili. Mzee Saidia alinilipia masomo yangu ya chuo kikuu. Nikasoma hadi nikatimiza hamu yangu ya masomo. Baada ya kufuzu, niliajiriwa katika kampuni moja maarufu nchini humu. Niliwachukua wanuna wangu ili waendeleze masomo kutokea walipokuwa wamefika. Nilizingatia mafunzo ya uadilifu na bidii niliyopewa na Mzee Saidia. Tulipopata nafasi, tungejumuika nyumbani kwake pamoja na wanawe ili kufaidi nasaha alizotupa na kumshukuru kwa moyo wake uliosheheni wema.

Baada ya nusu mwongo wa kufanya kazi nchini humu, nilipata nafasi ya kufanya kazi kule ng'ambo. Mimi na wanuna wangu hatukuwa na budi kuhamia huko, Mzee Saidia na aila yake yote walitusindikiza hadi katika uwanja wa ndege. Tuling'oa nanga, tukasafiri na kuwasili Marekani bila shari wala dosari. Miaka takribuni kumi ilikuwa imepita. Wakati huo wote tulizungumza na Mzee Saidia kwa simu tu na kuandikiana baruapepe. Kila mwisho wa mwezi, sikusita kumtumia kitita cha pesa, shukrani zangu za dhati kwa wema wake. Mara nilipata ujumbe kuwa Mzee Saidia alikuwa amezidiwa na ugonjwa wa figo. Nilizungumza na wanawe pamoja na mkewe, tukaelewana kuwa aje ng'ambo ili afanyiwe matibabu. Alipowasili marekani, nilienda kumpokea katika uwanja wa ndege. Tulikutana tena baada ya tukio hilo la wema. Ulikuwa umepita muda mrefu lakini bado nilimshukuru.

  1. Kifungu kinadokeza kuwa Mzee Saidia aliwahudumia wateja;
    1. waliomjua na wale ambao hawakumjua. 
    2. waliolipa madeni na wasiolipa madeni.
    3. waliokuwa na pesa na wasiokuwa na pesa.
    4. waliohitaji bidhaa na wasiohitaji bidhaa.
  2. Tambua sifa za Mzee Saidia kulingana na kifungu.
    1. anayeshirikiana, mvumilivu, anayejali haki
    2. mwangalifu, mpole, mwenye bidii
    3. anayethamini elimu, mwaminifu, mcheshi
    4. mwenye bidii, karimu, anayezingatia usawa
  3. Kauli walilala usingizi usiojua kuamka imetumika katika ufahamu, ina maana gani jinsi ilivyotumika?
    1. waillemewa na ugonjwa
    2. waliaga dunia
    3. hawakupata matibabu
    4. walishindwa kuamka
  4. Mwandishi alipokuwa kwa ami, alikosa;
    1. elimu na lishe bora
    2. malazi na makazi
    3. masomo na chakula
    4. makazi na lishe
  5. Kulingana na aya ya tatu, ni kweli kuwa; 
    1. mwandishi alishangazwa na hali ya watu kujaa katika boma kila siku.
    2. msemaji hakutarajia kufanyiwa mpango wa kukeketwa na ami.
    3. waliojaa katika boma la ami walikuwa waliokula chumvi nyingi pekee.
    4. jamii ya msemaji ilikataa kutupilia mbali mila zilizopitwa na wakati.
  6. Kulingana na ufahamu, ni kweli kuwa mwandishi;
    1. alilipia matibabu ya Mzee Saidia.
    2. alikuwa kifunguamimba.
    3. alikataa kuenda kuishi na shangazi wala mjomba.
    4. alikuwa msichana wa pekee katika familia yao.
  7. Mwandishi ni mwajibikaji kwa kuwa;
    1. alikubali kuishi na ami wazazi walipofariki.
    2. alikubali kukeketwa ili kuonyesha heshima kwa wazee.
    3. aliwachukua wanuna wake na kuendeleza masomo yao.
    4. alitoroka alipoona polisi wakifika kuwashika ami na wenzake.
  8. Kitendo cha polisi kuwashika ami wa mwandishi na wenzake kinatoa funzo lipi? 
    1. Polisi wanafaa kujulishwa kabla ya mtu yeyote kukeketwa.
    2. Ni vizuri msichana anayekeketwa akubali kabla ya kukeketwa.
    3. Ukeketaji haufai kufanyika wakati shule hazijafungwa.
    4. Ni vyema kufuata na kuheshimu sheria zilizowekwa na serikali.
  9. Mwandishi alikuwa amefanya kazi kwa muda gani kabla ya Mzee Saidia kuanza kuugua?
    1. kumi na mitano
    2. kumi
    3. mitano
    4. karibu kumi na mitano
  10. Methali zifuatazo zinaweza kujumuisha ujumbe katika kifungu isipokuwa;
    1. Wema hauozi.
    2. Mla nawe hafi nawe ila mzaliwa nawe. 
    3. Baada ya dhiki faraja.
    4. Dau la mnyonge huendeshwa na Mungu.


MARKING SCHEME

  1. A
  2. D
  3. C
  4. A
  5. C
  6. D
  7. B
  8. B
  9. A
  10. B
  11. D
  12. A
  13. B
  14. C
  15. D
  16. B
  17. A
  18. B
  19. D
  20. A
  21. B
  22. C
  23. D
  24. B
  25. D
  26. D
  27. B
  28. A
  29. B
  30. B
  31. B
  32. A
  33. B
  34. C
  35. A
  36. B
  37. A
  38. B
  39. B
  40. D
  41. A
  42. A
  43. D
  44. B
  45. A
  46. D
  47. A
  48. D
  49. A
  50. C

 

Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Class 8 Term 1 Opener Exams 2023 Set 1.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students