Tuesday, 24 October 2023 08:43

Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - Grade 4 End Term 3 Exams 2023 Set 1

Share via Whatsapp

Soma mazungumzo haya kisha ujibu maswali 1-5

Rafiki:  Njoki, hebu njoo kidogo. Unafaa kuamshwa kidogo.
Njoki:   Kwa nini rafiki yangu? Kwani nimekosea? Haya niambie
Rafiki:  Usinielewe vibaya. Ninataka kukufahamisha kuwa wewe unafikiria vibaya kuhusu utamaduni wetu
Njoki:   Bado sikuelewi
Rafiki:  Ulisema kuwa hukutaka kusoma tena. Eti wanaosoma tu ni watoto wavulana.
Njoki:   Lakini si ni ukweli. Sisi tukiwa wakubwa tutaolewa tu.
Rafiki:  Hapana. Hayo ndiyo mabaya ya tamaduni zetu. Yameachwa hayo. Lazima mtoto wa kiume asome sambamba na wakike. Wote wana nafasi sawa. Ukisoma huenda mkawa
mwalimu, daktari ama mhandisi utuundie vitu mpya. Hebu soma kwa bidii.
Njoki:   Kama ni hivyo basi nitafanya bidii zaidi. Asante rafiki yangu.

 1. Kwa nini rafiki alimwita Njoki? Ili
  1. amwamshe kidogo
  2. waende kucheza
  3. wasome kidogo
  4. wafanye kazi za nyumbani
 2. Rafiki alitaka kumweleza nini Njoki?
  1. Kuhusu kazi ya walimu
  2. Kuhusu mazoezi ya mhandisi
  3. Kuhusu Njoki kuelewa vibaya utamaduni wao
  4. Kuhusu maisha yao magumu
 3. Kwa nini Njoki hakutaka kusoma?
  1. Hawakuwa na pesa za kumlipia karo
  2. Alijua angeolewa baadaye
  3. Masomo yalikuwa magumu
  4. Aliambiwa na wazazi wake aache masomo
 4. Siku hizi ni akina nani wanasoma sambamba?
  1. Wavulana na wasichana
  2. Wasichana pekee
  3. Wavulana pekee
  4. Wavulana na vijana
 5. Njoki angesoma angekuwa nini maishani?
  1. Mkulima, dereva, mtembezi
  2. Mchukuzi, mganga, mkulima
  3. Msomi, mtanashati, dereva 
  4. Daktari, mwalimu, mhandisi

Soma ufahamu huu kisha ujibu maswali 6-10.

Mimea ikipandwa mahali penye rutuba huota na kustawi. Pia huitwa kunawiri. Hii ni ile hali ya mimea kuonekana mizuri kwa kuwa inapata mahitaji yote muhimu kama maji, hewa, mbolea, madini na kadhalika. Mimea mingi kwa kawaida ikistawi huwa rangi ya kijani kibichi. Mimea huhitaji kupaliliwa. Huku ni kung'oa mimea isiyohitajika shambani. Mimea hiyo isiyohitajika huitwa nagugu. Mimea ikikua huvunwa. Mahindi na maharagwe hukaushwa na kuwekwa kwenye magunia ili kuihifadhi ili kutumiwa wakati wa usoni.

 1. Mimea hunawiri wakati gani?
  1. Ikipanda mahali penye rutuba
  2. Mvua ikiwa kidogo
  3. Ikipandwa mahali penye joto jingi
  4. Ikipandwa mahali hakuna rotuba
 2. Mimea kuonekana kuwa mizuri tunasema mimea
  1. imeharibika
  2. imekauka
  3. imefufuka
  4. imenawiri
 3. Mimea huhitaji nini ili kuwa katika hali nzuri?
  1. Maji kidogo, joto na hewa
  2. Maji, hewa, mbolea na madini
  3. Mbolea na maji pekee
  4. Madini na mbolea pekee 
 4. Rangi ya mimea huwa ni gani?
  1. Manjano
  2. Zambarau
  3. Kijani kibichi
  4. Samawati hafifu
 5. Ni nini maana ya kupalilia?
  1. kung'oa magugu au mimea isiyohitajika shambani
  2. kung'oa mimea iliyokwisha kumea
  3. kutoa mazao yaliyokwisha kukomaa 
  4. kukata mimea ili kutengeza mbolea

Soma ufahamu huu kisha ujibu maswali 11-15

Hapo zamani za kale, paliondokea mzee mmoja aliyeitwa Mkonobirika. Mzee huyu alikuwa mgumu kama jiwe upande wa pesa. Ilikuwa ni vigumu kwake kutoa hata shillingi moja kwa sababu yoyote ile. Alizitafuta Desa kwa bidii sana na alipozipata, aliziweka katika shimo alilochimba nyumbani kwake.

Siku moja rafiki yake alimshauri aziweke pesa kwenye benki. Akakataa akasema zikiwa huko hatakuwa akipata nafasi ya kuziona na kuzishikashika. Rafiki huyo akamwambia, "Unajua pesa zako siku moja zitaliwa na watu usiowajua. Ni afadhali basi uoe, upate watoto kisha watakuja kuzitumia pesa zako." Alikataa wazo la rafikiye. Siku moja aliwakisha moto na akasahau kuuzima baada ya kupika chakula cha jioni. Moto ule ukatatarika akawa amelala na likashika karatasi zilizokuwa karibu. Kilichomwamsha ni moshi mingi na joto jingi. Alishtuka na kuona nyumba yote imeshika moto. Akatorokea nje kunusuru maisha yake. Kila kitu kilichokuwa mle kilichomeka zikiwemo pesa zile.

 1. Mzee alikuwa mgumu kwa nini?
  1. Hakutaka kutumia pesa zake
  2. Alitumia pesa zake vibaya
  3. Aliwapa watu pesa zake.
  4. Watu hawakumpa pesa zake
 2. Mkonobirika alizificha wapi pesa zake?
  1. Katika benki
  2. Katika mifuko
  3. Chini ya kitanda
  4. Katika shimo alilolichimba nyumbani kwake
 3. Rafikiye Mkonobirika alimshauri afanye nini?
  1. Atumie pesa zake
  2. Azihifadhi pesa zake benkini-
  3. Awagawie maskini pesa zake
  4. Awekeze katika miradi mbalimbali
 4. Mkonobirika alikataa wazo la rafiki yake kwa sababu gani?
  1. Pesa zilikuwa nyingi mno
  2. Pesa zake zingepotea
  3. Pesa za benkini hazikuwa nzuri
  4. Asingeweza kuziona na kuzishikashika pesa zake
 5. Nyumba yake Mkonobirika ilichomeka kwa sababu gani?
  1. Aliwasha moto akasahau kuuzima
  2. Kulikuwa na tatizo la stima
  3. Watu waliirushia mafuta nyumba yake
  4. Mkewe aliichoma wakiwa usingizini

Jaza nafasi 16-20, kwa jibu sahihi.

Safari ___16___ iliwachukua muda wa siku ___17___ Walipofika Diani, walishangaa kuona mazingira tofauti ___18___ yale ya huko kwao. Kwanza, walifikishwa kwenye ufuo wa bahari. Hapo walikutana na ___19___  waliokuwa wamebeba samaki. Samaki ___20___ walikuwa wakiokwa na kukaangwa.

   A  B  C  D
 16.  hiyo  hicho   hilo   hayo 
 17.  mmoja  kimoja  moja  limoja
 18.  kwa  wa  pa  na
 19.  walikuwa  wavuvi  madereva  madaktari
 20.  nyingine  mingine  wengine  kwingine
 1. Andika udogo wa maneno haya;
  Mto, mji
  1. jito, jiji
  2. majito, majiji
  3. vijito, vijiji
  4. kijito, kijiji
 2. Kanusha sentensi hii
  Amekuja kututembelea
  1. Hakuja kututembelea
  2. Hajaja kututembelea
  3. Hatakuja kututembelea
  4. Asingekuja kutembelea  
 3. Sentensi hii imeandikwa katika wakati gani?
  Askari watakuwa wakilinda usalama wa kila mtu
  1. wakati ujao hali ya kuendelea
  2. wakati uliopita hali ya kuendelea
  3. wakati uliopo hali ya kuendelea
  4. wakati wa hali tegemezi
 4. Mtoto wa ngombe huitwaje?
  1. Kinyau
  2. Kifaranga
  3. Ndama
  4. Kinda 
 5. Tunasema mfupi kama nyundo na mnene kama
  1. makaa
  2. mlingoti
  3. pamba
  4. nguruwe
 6. Jaza pengo kwa kutumia kinyume cha nomino iliyopigiwa mstari katika sentensi hii.
  Baada ya kicheko chake kulikuwa na
  1. furaha
  2. huzuni
  3. kilio
  4. mshangao
 7. Andika neno jenga katika kauli ya kutendwa ili ujaze nafasi katika sentensi hii.
  Nyumba yake ime __________________________ (jenga) nyuma ya soko.
  1. jengwa
  2. jengewa
  3. jengeka
  4. jengesha
 8. Ni neno lipi ambalo ni kisawe cha runinga?
  1. Redio
  2. Rununu
  3. Tarakilishi
  4. Televisheni.
 9. Jaza silabi inayokosekana katika sentensi hiii
  Joto ____________ kizidi watu hutoa mashati
  1. ya
  2. li
  3. zi
  4. ki
 10. Andika wingi wa sentensi hii
  Kikapu kimefumwa
  1. Makapu yamefumwa
  2. Vikapu zimefumwa
  3. Likapu limefumwa
  4. Vikapu vimefumwa

SEHEMU YA B: INSHA

Andika insha ya kusisimua kuhusu

SHEREHE NYUMBANI

MARKING SCHEME

 1. A
 2. C
 3. B
 4. A
 5. D
 6. A
 7. D
 8. B
 9. C
 10. A
 11. A
 12. D
 13. B
 14. D
 15. A
 16. A
 17. C
 18. D
 19. B
 20. C
 21. D
 22. B
 23. A
 24. C
 25. D
 26. C
 27. A
 28. D
 29. B
 30. D
Join our whatsapp group for latest updates

Download Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - Grade 4 End Term 3 Exams 2023 Set 1.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students