Wednesday, 31 August 2022 06:16

Kiswahili Questions with Answers - CBC Grade 4 End of Term 2 Exams 2022 SET 2

Share via Whatsapp

MASWALI

Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali 1-5
(Ni wakati wa likizo fupi.Hamisi na Zainabu wanakutana)
Hamisi: U hali gani Zainabu? Kumbe nawe waishi huku Tushauriane kama mimi! 
Zainabu: Hali yangu ni njema. Naam. Tulihamia huku Tushauriane kwa kuwa mwenye nyumba alitaka kuipaka rangi nyumba yote.
Hamisi: Kabla ya kufunga shule hukuwa umeniambia kuwa umekuwa jirani yangu(wote wanacheka) Yaani tunasoma katika darasa moja na huwezi kuni...
Zainabu: Aaah! Nawe! Samahani basi. Huenda nilisahau. Hata hivyo, tutarudi Mnarani ufundi ukikamilika. 
Hamisi: Sawa kabisa. (akikohoa kidogo)Nilikuwa nikielekea kwa kina Fauzia anieleze namna ya kutumia viunganishi katika 
Zainabu: Usihofu Hamisi. Tukakae pale kivulini nikusaidie. (wakielekea chini ya mti) Je, unajua mifano gani ya viunganishi?
Hamisi: Lakini, kwa sababu, ingawa, ila na vingine vichache. Tatizo langu ni kuvitumia katika sentensi
Zainabu: Haya tukae nikuonyeshe. (wanaketi huku Hamisi akitoa daftari, kitabu na kalamu mkobani.)

 1. Kulingana na mazungumzo haya,kina Zainabu walikuwa wakiishi wapi kitambo?
  1. Tushauriane.
  2. Mnarani.
  3. Kivulini.
  4. Hatujaelezwa.
 2. Je, ni kwa nini familia ya Zainabu ilihama?
  1. Wazazi walitaka waishi karibu na shule
  2. Zainabu alitakiwa kuwa karibu na Hamisi ili amsaidie kimasomo.
  3. Nyumba ya kina Zainabu ya kitambo ilikuwa ikipakwa rangi.
  4. Waliupenda mtaa wa Tushauriane.
 3. Unadhani Hamisi alifika kwa kina Fauzia? 
  1. La.
  2. Naam. 
  3. Haiwezekani.
  4. Yawezekana. 
 4. Tatizo la Hamisi lilikuwa gani?
  1. Kujua mifano ya viunganishi.
  2. Alitaka Zainabu amwambie kuwa walikuwa wamehama. shule.
  3. Kutaka kuhamia Mnarani.
  4. Hakujua kutumia viunganishi katika sentensi.
 5. Inawezekana kuwa Fauzia ni 
  1. mwalimu.
  2. mzazi. 
  3. mwanafunzi.
  4. Zainabu.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 6 hadi 8.
Ni wajibu wa kila mkenya, awe kijana au mzee, kushiriki katika uhifadhi na ulinzi wa misitu yetu. Kila mmoja ana nafasi yake ya kutekeleza kulingana na umri na uwezo wake. Upanzi wa miti unafaa kuongozwa vijana kwa sababu wana nguvu ya kutosha. Msimu mzuri wa kupanda miche ni msimu wa mvua nyingi.
Ili kuipanda miti mingi nchini, serikali imetenga siku moja kwa mwaka iwe ya upanzi wa miche, yaani miti michanga. Wengi hivi karibuni wamekosa kuitilia maanani siku hii muhimu. Hapo awali, shughuli hii ilikuwa ikichangamkiwa na kila mmoja katika jamii.

 1. Kulingana na ufahamu, uhifadhi wa misitu ni wajibu wa
  1. vijana.
  2. watu wazima.
  3. watu wote.
  4. wanafunzi.
 2. Je, ni kwa nini vijana ndio wanaofaa kuongoza katika upanzi wa miti?
  1. Wana nguvu ya kutosha.
  2. Wanajua kupanda miche zaidi.
  3. Wao ndio wengi nchini.
  4. Hiyo ni sheria ya nchi yetu.
 3. Katika mwaka mzima, ni siku ngapi zimetengewa upanzi wa miche?
  1. Tatu.
  2. Mbili.
  3. Nne.
  4. Moja.
 4. Kulingana na ufahamu, 
  1. hata sasa, wanajamii wanachangamkia upanzi wa miche.
  2. mti mchanga sana huitwa mche
  3. hapo awali watu hawakupenda kupanda miche. .
  4. miti ina faida kwa vijana pekee.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 10 hadi 12.
Kuna umuhimu mkuu wa kudumisha afya bora. Binadamu akiwa na afya bora, huweza kufanya shughuli zote vizuri na kwa wakati unaofaa. Ili kuwa na afya bora, ni vizuri kuzingatia lishe bora. Chakula tunachokila lazima kiwe na kabohaidreti, protini na vitamini kwa viwango vinavyofaa mwilini. Vile vile, ni vizuri kunywa maji safi na salama kila siku. Je, wajua kuwa matunda hutukinga tusiwe wagonjwa? Wapishi na watu wote wanaoandaa chakula ni lazima wawe safi ili tusipatwe na magonjwa

 1. Taarifa hii inasema kuwa kuna umuhimu wa kudumisha
  1. lishe bora.
  2. chakula bora.
  3. afya bora.
  4. usafi.
 2. Tumeambiwa kuwa chakula chetu lazima kiwe na
  1. kabohaidreti na protini.
  2. vitamini na kabohaidreti. 
  3. kabohaidreti na protini. 
  4. vitamini, kabobaidreti na protini.
 3. Kulingana na taarifa, matunda
  1. hutuletea magonjwa.
  2. hutukinga tusiwe wagonjwa.
  3. huwa na ladha nzuri.
  4. yanafaa kuwa safi na salama.

Sonia kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 13 hadi 15.
Mayowe alikuwa ameketi kando ya ghala lake tupu. Tumbo lilimnguruma kwa njaa. Aliishi hivyo kwa siku tatu. Mtama aliokuwa ameuweka katika ghala uliibwa na manyani na tumbili waliotoka katika msitu wa Marura. Mahindi nayo yaliyokuwa tele humo ghalani yaliliwa yote na kuchakulo. Kando yake kulikuwa na kibuyu. Kibuyu hicho kil'isoma akili yake haraka na kumwambia kwa sauti, “Fanya chaguo!" Mayowe, kwa sauti alisema, "Nataka chakula!” Ghafla bin vuu, ghala likajaa mihogo na viazi. Mayowe alifurahi kuliko siku zote za maisha yake. 

 1. Mwanzoni mwa ufahamu, ghala la Mayowe lilikuwa na nini?
  1. Mihogo na viazi. 
  2. Lilikuwa tupu. 
  3. Mahindi na mtama.
  4. Mtama na viazi.
 2. Tumeambiwa kuwa Mayowe alihisi njaa kwa muda wa
  1. wiki tatu.
  2. miaka mitatu
  3. saa tatu.
  4. siku tatu.
 3. Manyani na tumbili wale walitoka wapi?
  1. Katika kijiji jirani.
  2. Mlimani.
  3. Hatujaelezwa.
  4. Msituni Marura.

Soma kifungu kifuatacho. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.
Jana_16_ , kipindi cha kwanza kilikuwa cha Kiswahili. Kila mmoja wetu alifurahi . kwa sababu _17_ wetu alituambia kuwa siku hiyo angetufundisha mengi kuhusu pande kuu za _18_ Alianza kwa kutueleza kuwa jua huchomoza_19_ na kutua au kuzama_20_ Jioni hiyo, tulitakiwa kulichora jua na kulipaka rangi.

 1.    
  1. asubuhi
  2. jioni
  3. usiku
  4. mchana
 2.      
  1. mzazi
  2. walimu
  3. mwalimu
  4. mjomba
 3.      
  1. uwanja
  2. darasa
  3. shule
  4. dira
 4.    
  1. magharibi
  2. mashariki 
  3. kusini
  4. kaskazi
 5.      
  1. kaskazini
  2. kusini
  3. magharibi
  4. mashariki

Katika swali la 21-30. jibu swali kulingana na maagizo uliyopewa.

 1. Ni rangi gani hapa haipo katika bendera ya Kenya?
  1. Nyekundu.
  2. Manjano.
  3. Nyeupe.
  4. Kijani.
 2. Chagua wingi wa sentensi hii:
  Mwaka umeisha bila vita.
  1. Miaka imeisha bila vita.
  2. Mwaka imeisha bila vita.
  3. Miaka umeisha bila vita.
  4. Miaka zimeisha bila vita.
 3. Kamilisha methali ifuatayo:
  Mtoto umleavyo
  1. hutazama kisogo cha nina.
  2. ni nyoka.
  3. ndivyo akuavyo.
  4. mkanye angali mdogo.
 4. Chagua umoja wa
  Madirisha mekundu yamefungwa.
  1. Madirisha nyekundu limefunguliwa.
  2. Dirisha jekundu limefunguliwa.
  3. Dirisha nyekundu limefungwa.
  4. Dirisha jekundu limefungwa.
 5. Mwembe hutupa maembe, nao  mgomba hutupa
  1. ndizi.
  2. kahawa. 
  3. mchele
  4. matunda.
 6. Chagua neno lililo katika ngeli tofauti na yale mengine.
  1. Jua.
  2. Joto. 
  3. Jani
  4. Jasho
 7. Nahau taka idbini ina maana ya 
  1. toa tangazo
  2. omba ruhusa
  3. omba msamaha
  4. pata habari 
 8. Baba amenunua televisheni mpya. Chagua kisawe cha neno lililopigiwa mstari.
  1. Baiskeli
  2. Redio 
  3. Simu
  4. Runinga
 9. Kati ya hawa, ni yupi mnyama wa porini? 
  1. Swara.
  2. Farasi. 
  3. Mbuzi.
  4. Punda
 10. Kitenzi soma katika kauli ya kutendwa huwa
  1. someka.
  2. somea.
  3. somwa.
  4. somesha. 


MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

 1. B
 2. C
 3. A
 4. D
 5. C
 6. C
 7. A
 8. D
 9. B
 10. C
 1. D
 2. B
 3. B
 4. D
 5. D
 6. A
 7. C
 8. D
 9. B
 10. C
 1. B
 2. A
 3. C
 4. D
 5. A
 6. C
 7. B
 8. D
 9. A
 10. C
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions with Answers - CBC Grade 4 End of Term 2 Exams 2022 SET 2.


Tap Here to Download for 30/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students