Wednesday, 14 June 2023 08:06

Kiswahili Questions and Answers - Grade 4 Mid Term 2 Exam 2023 Set 1

Share via Whatsapp

MASWALI

Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali 1-5.
(Wanafunzi kadhaa wanajadiliana kuhusu vyakula wavipendavyo na manufaa yavyo mwilini).

Lulu: Juzi sote tulielewana kuwa vyakula kama vile vibanzi au chipsi havina manufaa yoyote mwilini. Ingawa wengi hawakukubali, huo ndio ukweli wa mambo.

Pendo: Ni kweli Lulu. Sasa leo kila mmoja atataja chakula akipendacho na umuhimu wa chakula hicho mwilini.

Ali: Baada ya kuacha kula vibanzi kwa wingi, nimeamua kupenda mboga za majani kama vile mchicha. Mboga hizi hunikinga dhidi ya magonjwa mbalimbali. Vile vile karoti huyaimarisha meno yangu na kuyapa nguvu macho yangu.

Rama: (Akitikisa kichwa kukubaliana na Ali) Mimi kwa upande wangu nilipoacha kula chipsi kwa wingi, siku hizi mimi ni mpenzi wa vyakula vyenye asili ya mizizi kama vile mihogo na viazi. Vyakula hivi hunipa nguvu ya kucheza mchezo wangu niupendao. Si mnaujua?

Wote: Naam, kandanda.

Rama: Ndiyo. Tena vyakula hivi hunipa joto la kutosha mwilini(akirukaruka na kurusha miguu ovyoovyo) Na wewe Lulu? (wote wanamgeukia Lulu)

Lulu: Baada ya kupunguza ulaji wa vibanzi au chipsi, siku hizi napenda sana maziwa, hasa ya ngamia. Maziwa haya huvikuza viungo vya mwili wangu hivyo kunifanya kukua na kuwa mkubwa. Nayapenda mno maziwa ya ngamia.

Pendo: Kwa upande wangu, siku hizi mimi napenda sana kula dagaa hasa wakiandaliwa pamoja na ugali. Dagaa huukuza mwili wangu na kunifanya kuongezeka kimo.

Lulu: Licha ya hayo yote, tusisahau kufanya mazoezi ya kutosha na kunywa maji safi na salama.

Wote: Sawa Lulu.

 1. Kulingana na mazungumzo haya, watoto hawa walikuwa wakipenda chakula gani kitambo?
  1. Maziwa ya ngamia
  2. Chipsi.
  3. Mboga za majani.
  4. Vyakula vya mizizi.
 2. Ali alisema anapenda mchicha kwa sababu
  1. huyapa nguvu macho yake. 
  2. humpa joto na nguvu ya kucheza. 
  3. humkinga asipate magonjwa. 
  4. huufanya mwili wake kukua.
 3. Kati ya watoto hawa, ni yupi mchezaji hodari wa kandanda?
  1. Rama
  2. Pendo
  3. Lulu
  4. Ali
 4. Kulingana na mazungumzo haya, ni chakula gani hapa hutupa nguvu? 
  1. Dagaa
  2. Mboga za majani
  3. Maziwa ya ngamia 
  4. Viazi
 5. Mwishoni mwa mazungumzo haya, Lulu anawakumbusha wenzake
  1. kunywa maji na kufanya mazoezi. 
  2. kufanya mazoezi na kunywa maji safi na salama.
  3. kufanya mazoezi.
  4. kunywa maji yaliyo safi na salama. 

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 6 hadi 8.
Naikumbuka vizuri siku yangu ya kwanza katika Gredi ya nne. Ilikuwa Jumanne asubuhi. Baada ya kuchukua virago vyangu kutoka katika darasa tuliloliacha pamoja na wengine, tuliandamana hadi Gredi ya nne kusini. Kwa kuwa nilikuwa mfupi zaidi, niliamua kukaa mbele kabisa katika safu ya kati. Kipindi cha kwanza kilikuwa cha Kiswahili. Tofauti na Gredi ya tatu, hapa tungefunzwa na walimu tofauti. Mwalimu wa Kiswahili alikuwa mwanadada mwembamba. Alikuwa na tabasamu angavu usoni. Aliongea Kiswahili sanifu. Nilikifurahia kipindi chake. Baada ya somo hili, nilikuwa na hamu ya kutaka kuwajua walimu wale wengine pia.

 1. Nini ambacho mwandishi bado anakumbuka?
  1. Mwalimu wa Kiswahili wa Gredi ya nne.
  2. Siku yake ya kwanza shuleni
  3. Siku yake ya mwisho katika Gredi ya tatu.
  4. Siku yake ya kwanza katika Gredi ya nne.
 2. Mwandishi aliamua kukaa mbele zaidi kwani
  1. alikuwa mfupi wa kimo.
  2. alizoea kukaa katika nafasi kama hiyo. 
  3. mwalimu alimtaka kufanya hivyo. 
  4. nafasi za nyuma zilikuwa zimejaa.
 3. Tumeambiwa tofauti gani iliyo kati ya Gredi ya tatu na ya nne? 
  1. Mpangilio wa darasani. 
  2. Ratiba ya mafunzo. 
  3. Idadi ya walimu. 
  4. Idadi ya wanafunzi.
 4. Ni wazi kuwa mwalimu wa Kiswahili wa Gredi ya nne alikuwa
  1. mnene kama nguruwe.
  2. mcheshi.
  3. mwanamume mwembamba mwenye tabasamu.
  4. mzembe kupindukia. 

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 9 hadi 12.
Watoto wachanga wanafaa kukanywa dhidi ya kucheza na vitu kama vile sarafu na gololi. Hivi ni kwa sababu watoto wengine huvitia vitu hivi hatari masikioni au hata puani. Ajabu ni kuwa, wengine hata huweza kuvimeza vidude hivi. Mtoto anapofanya hivyo, si vyema kujaribu kukitoa hicho kilichoingizwa sikioni au puani. Huenda ikawa hatari hata zaidi. Muhimu ni kumpeleka mtoto katika kituo cha afya kilicho karibu haraka iwezekanavyo ili kuokoa hali.

 1. Taarifa inasema kuwa kuvitia vitu hatari masikioni na puani si vizuri kwa kuwa huweza
  1. kusababisha hatari.
  2. kusababisha mauti. 
  3. kuleta hasara.
  4. kuzua ugomvi.
 2. Mtoto akimeza sarafu, cha kwanza kufanya ni nini?
  1. Kujaribu kumtapisha. 
  2. Kumpeleka hospitalini.
  3. Kujaribu kuiondoa.
  4. Kumnywesha maji kwa wingi
 3. Ili ajali ya aina hii isitokee, watoto wachanga
  1. wasipewe safaru bali noti za kuchezea.
  2. wafumbwe midomo na pua wasitie vitu hatari.
  3. wasiruhusiwe kabisa kucheza.
  4. wakanywe dhidi ya kuchezea vifaa hatari.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 13 hadi 15.
Wanyama ambao huishi misituni huitwa wanyamapori. Wengi wao huwa wakali na hivyo hawawezi kuishi na wanadamu. Ndovu au tembo ndiye mnyama mkubwa zaidi. Mnyama aliye na mbio zaidi kupita wote ndiye duma. Mwenye shingo ndefu kupita wote huitwa twiga huku yule aliye mkali zaidi na ambaye huitwa mfalme wa nyika ni simba. Wanyama hawa pamoja na wengine huwavutia watalii ambao hujaajaa humu nchini ili kuwatazama. Wanapokuja, wao hulipa pesa za kigeni ambazo husaidia kuuinua uchumi wa nchi yetu.

 1. Binadamu hawawezi kuishi na wanyamapori kwa sababu ya
  1. ukubwa wao.
  2. ukali wa baadhi yao.
  3. mbio zao.
  4. upole walio nao.
 2. Tembo ndiye mnyama 
  1. mkali kuliko wote.
  2. mwenye mbio zaidi. 
  3. mwenye shingo ndefu ajabu. 
  4. mkubwa zaidi.
 3. Chagua sifa za simba kulingana na ufahamu huu.
  1. Mwenye mbio na shingo ndefu.
  2. Ukali na ufalme.
  3. Ukali na shingo ndefu. 
  4. Ukubwa na mbio.

Soma kifungu kifuatacho. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.
Karimu ra nyanya yake wanaishi ..................16.................... mto Riva. Mto huo huwasaidia na ..................17.................... wakati wa ukame. Huu ni wakati ambapo hakuna ..................18.................... Kila siku ya ..................19.................... Karim huwa haendi shuleni. Yeye humsaidia nyanya yake shambani palipo na migomba. Shughuli za shambani huwa za kupalilia migomba hiyo. Nyanya wa Karim humpenda kwa sababu Karim ..................20.................... mvivu.

 1.                    
  1. ndani ya
  2. karibu na
  3. juu ya
  4. chini ya
 2.                
  1. maji
  2. moto
  3. mchanga
  4. kuni
 3.            
  1. jua
  2. joto
  3. kelele
  4. mvua
 4.                    
  1. Jumatatu
  2. Alhamisi
  3. Jumamosi
  4. Jumanne
 5.                
  1. ni
  2. huwa
  3. si
  4. ndiye

Katika swali la 21-30. jibu swall kulingana na maagizo uliyopewa.

 1. Ni neno gani hapa ambalo si nomino?
  1. Darasa
  2. Chaki
  3. Chupa
  4. Ruka
 2. Chagua orodha ya vitenzi pekee.
  1. Mdogo, chota, watu.
  2. Mdudu, okoa, Ala!
  3. Ona, chukua, leta.
  4. Kalamu, andika, chini ya.
 3. Katika sentensi mbuzi wanono walipelekwa sokoni jana, kivumishi ni kipi?
  1. Wanono
  2. Jana
  3. Walipelekwa
  4. Sokoni
 4. Maneno ambayo hutumiwa badala ya nomino huitwa
  1. viwakilishi.
  2. vielezi.
  3. vihisishi.
  4. vihusishi.
 5. Ni maneno yapi ambayo yote ni vielezi? 
  1. Darasa, ubao, chati.
  2. Pika, uza, sema.
  3. Nje ya, kando ya, ndani ya.
  4. Ovyoovyo, polepole, haraka.
 6. Chagua kiunganishi bora kukamilishia sentensii hii:
  Maimuna hakuja shuleni - alikuwa mgonjwa.
  1. na
  2. lakini
  3. kwa sababu
  4. ingawa
 7. Chagua nomino za ngeli ya A- WA pekee.
  1. Kiongozi, kijana, kitana.
  2. Nyoka, njiwa, kiroboto.
  3. Motokaa, majani, tawi. 
  4. Meza, kalamu, karatasi.
 8. Tegua kitendawili hiki.
  Kamba yangu ndefu lakini haifungi kuni.
  1. Mkufu
  2. Maji ya mto
  3. Siafu
  4. Barabara
 9. Chagua mfano wa kihisishi.
  1. Nje ya
  2. Beba
  3. Lo!
  4. Kwa makini
 10. Chagua wingi wa sentensi ifuatayo: Kondoo mgonjwa atatibiwa. 
  1. Kondoo wagonjwa watatibiwa. 
  2. Makondoo wagonjwa watatibiwa. 
  3. Kondoo mgonjwa watatibiwa.
  4. Kondoo wagonjwa atatibiwa. 

MWONGOZO

kiswahili ms

Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Grade 4 Mid Term 2 Exam 2023 Set 1.


Tap Here to Download for 30/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students