Monday, 03 July 2023 12:02

Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - Grade 5 Mid Term 2 Exam 2023 Set 2

Share via Whatsapp

Soma taarifa hii kisha ujibu maswali 1-5.

G5SwaMT2S22023Q1
Sisi watoto wa nchi hii hatuna ubaguzi. Tunapendana. Tunasoma pamoja, tunacheza pamoja, tunaishi pamoja na tunakaa pamoja. Hatuna ubaguzi wa ukabila, dini, rangi wala cheo. Kwetu, kila mtu ni sawa, wasichana kwa wavulana,wake kwa waume na wazee kwa vijana. Tunaamini kwamba tukiishi pamoja kwa kupendana tutakuwa na amani, upendo na ushirikiano katika nchi yetu. Tukumbuke kwamba
nchi yetu ni moja. Na ndipo mahali petu pa kuishi hadi mwisho wa maisha yetu. Hivyo ni lazima sisi pia tuwe na umoja na ushirikiano.

Tunawaomba viongozi, wazazi, walimu wetu na kila mtu kwa jumla, huu ni wakati wa kuwajulisha vijana wote na watoto wa nchi hii kuwa umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.Tuache ukabila ili tujiite kuwa sisi ni watu wa kabila moja linaloitwa 'Wakenya'.Tuanze leo hii kutumia lugha yetu moja ya taifa, ambayo ni Kiswahili. Wanaotubagua na kututenganisha, tuwakatae katakata na tuwaambie "Ng'o!"

  1. Sauti ya watoto wa nchi hii
    1. haina ubaguzi
    2. imejaa ukabila
    3. haitaki ukabila
    4. ina chuki.
  2. Vijana ni watu gani?
    1. Wavulana
    2. Wanaume wadogo
    3. Watoto kwa kiume
    4. Wasichana kwa wavulana.
  3. Tunahitaji umoja kwa sababu nchi yetu ni
    1. kubwa
    2. nzuri
    3. moja
    4. changa.
  4. Sisi sote wananchi tunafanana yaani tu
    1. pamoja
    2. umoja
    3. wamoja.
    4. kumoja
  5. Wanaotubagua tuwaambie ng'o kisha tuanze kutumia lugha ya
    1. kimombo
    2. mama
    3. Kiswahili
    4. ung'eng'e.

Soma kifungu hiki kisha ujibu maswali 6 - 10.

Siku moja nilikuwa nimebaki nyumbani peke yangu. Wazazi wangu walikuwa wameenda kwenye matanga ya mjomba wangu. Nilikuwa mtoto wao wa kipekee. Wazazi wangu walinikanya na kunionya kuwa nisimkaribishe mtu yeyote nyumbani ikiwa wao hawakuwepo. Hakika sikutarajia kumruhusu mtu au kumkaribisha mtu yeyote aje akae nami kwetu. Lakini ilipofika jioni, akaja rafiki yangu wa chanda na pete Kichwachuma alijidai kuja kunisalimia. Nilishangaa kuhusu hizo salamu zake za jioni. Alipoketi tu hata kabla hatujaanza kuulizana za hujambo- sijambo, mvua ilianza kunyesha huku ngurumo kama za simba zikiandamana na radi. Hakika niliduwaa kushuhudia mvua ya miujiza isiyokuwa na dalili yoyote ya mawingu.

Sikuwa na jingine la kufanya. Nilimruhusu Kichwachuma kulala kwetu. Ajabu ni kwamba, kesho yake sikuamka mapema nilivyozoea. Nililala hadi saa tano asubuhi. Nilipoamka nilijikuta nimelala sakafuni.

Sikumpata rafiki yangu. Pia kila kitu nyumbani kwetu kilikuwa kimechukuliwa hadi kitanda tulichokuwa tumekilalia. Kila kitu! Vitu vyote havikuwepo. Nilibaki mimi tu nikishangaa jinsi ya kuwaambia wazazi wangu.

  1. Mwadishi anasema kuwa alibaki nyumbani peke yake. Hivyo alikuwa
    1. peke
    2. upweke
    3. pweke
    4. pekee 
  2. Aliyekuwa ameaga dunia ni
    1. dada wa mama
    2. kaka wa baba
    3. kaka wa mama
    4. dada wa baba.
  3. Wazazi wake walitoa onyo kwamba
    1. asikaribishe watu nyumbani milele
    2. amkaribishe mtu yeyote nyumbani
    3. mtu akaribishwe bila wao kuwapo
    4. asimkaribishe yeyote nyumbani wasipokuwepo.
  4. Mvua ilikuwa ya miujiza kwa sababu
    1.  ilikuwa na radi
    2. ilileta wezi
    3. haikuonyesha dalili kabla ya kunyesha
    4. ilikuwa na ngurumo za simba.
  5. Alipoamka aligundua kuwa vitu vyote nyumbani vilikuwa
    1. vimeuzwa
    2. vimeibiwa
    3. vimepotea
    4. vimetoroka

Soma kisa kifuatacho kisha ujibu swali la 11 - 15.

Siku hiyo ya Alhamisi, Kalume alikataa katakata kwenda shuleni. Siku hiyo ilikuwa ya kufanya mtihani wa Kiswahili. Alikataa kwenda shule kwa sababu mama yake alikataa kumnunuli vibanzi vya kula wakati wa mtihani. Mama alimwacha nyumbani asubuhi na mapema baada ya kumwamsha. Akamwambia kuwa akimaliza kufungua kinywa aende upesi shuleni asichelewe. Naye akaenda zake kazini.

Kalume alijua kimoyomoyo kuwa hangeenda shuleni. Alitaka vibanzi kwanza. Aliona kuwa vibanzi vilikuwa vitamu kuliko masomo au hata mtihani wa Kiswahili. Mama yake aliporudi saa saba adhuhuri alimkuta akiwa amejikunja akilia. Alipoulizwa alichokuwa akililia alisema: "Umekataa kuninunulia vibanzi"

Kesho yake mama alimpeleka shuleni. Akawaeleza walimu sababu za kukosa shule. Walimu walishangaa. Wanafunzi waliposikia habari hizo walimcheka Kalume sana, wakamwita Bwana Vibanzi. Wengine wakambatiza Kalume banzi! Hadi wa leo wanamwita hivyo. Je, wewe ni Kalume nani? Au Kalume nini?

  1. Kalume alikataa kwenda shuleni siku ya
    1. Alhamisi
    2. Jumatano
    3. Ijumaa
    4. Jumanne.
  2. Ni kwa nini Kalume alikataa kwenda shuleni?
    1. Alichukia shule.
    2. Alikuwa na njaa.
    3. Aliogopa mtihani.
    4. Alitaka vibanzi.
  3. Kufungua kinywa ni
    1. kulia
    2. kupanua mdomo.
    3. kusugua meno
    4. kula asubuhi.
  4. Neno jingine lenye maana sawa na vibanzi ni
    1. mahamri
    2. viazi
    3. chipsi
    4. viazi karai,
  5. Mama alipotoka nyumbani asubuhi alijua kuwa Kalume
    1. haendi shule
    2. atachelewa shule
    3. alikataa chipsi
    4. angeenda shule

Jaza mapengo kwa jibu mwafaka.

Kitabu __16__ kilianguka chini __17__ vipandevipande. Kipande __18__ kikachukuliwa na upepo lakini kipande __19__ kiliingia ndani __20__ maji.

   A   B   C   D 
 16.    yangu   changu    zangu   langu 
 17.  ikararuka   akararuka   kikararuka   kikararua 
 18.  kimoja  moja   mmoja   kamoja 
 19.  ingine  mwingine   nyingine   kingine 
 20.  ya  cha  mwa  wa


Kutoka swali la 21 hadi 30 jibu kulingana na maagizo.

  1. Ipi si jozi ya vitate vyenye sauti zinazokaribiana kimatamshi?
    1. Sima- Zima
    2. Fuka- Vuka
    3. Fora-Fola
    4. Cheka-Choka.
  2. Mwalimu akitusalimu masalkheri. Salamu hii inatumika wakati gani?
    1. Mchana
    2. Jioni
    3. Asubuhi
    4. Usiku
  3. Neno la mwisho kupatikana kwenye kamusi kati ya haya ni
    1. mbio
    2. mbuzi
    3. mbili
    4. mbuni. 
  4. Ni aina ipi ya nomino iliyo katika sentensi ifuatayo?
    Maji mengi yamemwagika chini.
    1. Idadi
    2. Mahali
    3. Wingi
    4. Pekee
  5. Chagua wingi wa sentensi ifuatayo.
    Kula kwake huko kunaudhi. 
    1. Kula kwao huko kunaudhi.
    2. Kula kwake huko kunaudhi.
    3. Kukula kwake huko kunaudhi.
    4. Vyakula vyake hivyo vinaudhi.
  6. Tegua kitendawili kifuatacho.
    Ananitazama, hasemi, hasikii
    1. Kivuli
    2. Kioo
    3. Picha
    4. Mtoto
  7. Kamilisha. ___________________________ ya ndizi.
    1. Mkungu
    2. Tita
    3. Bunda
    4. Chane
  8. Chagua nomino zinazoweza kuunda nomino ambata sahihi.
    1. Mwana + maji
    2. mwana + muke.
    3. mwana + mbe.
    4. mwana + inchi
  9. Neno lipi lisilo la heshima kati ya haya?
    1. Endesha
    2. Choo
    3. Kinyesi
    4. Mjamzito
  10. Chagua sentensi sahihi kisarufi.
    1. Mbuzi zimeshiba.
    2. Ndege limeanguka chini.
    3. Daktari wamegoma.
    4. Choo kinaoshwa.

INSHA

Umepewa dakika 40 kuandika insha yako.

Andika insha ya kusisimua kuhusu;

JINSI YA KUKABILIANA NA UMASKINI

MARKING SCHEME

  1. A
  2. D
  3. B
  4. D
  5. C
  6. B
  7. C
  8. D
  9. C
  10. B
  11. A
  12. D
  13. D
  14. C
  15. D
  16. B
  17. C
  18. A
  19. D
  20. A
  21. D
  22. B
  23. B
  24. C
  25. A
  26. C
  27. D
  28. A
  29. B
  30. D
Join our whatsapp group for latest updates

Download Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - Grade 5 Mid Term 2 Exam 2023 Set 2.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students