MASWALI
Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali 1 mpaka 5.
Mwanafunzi : Shikamoo mwalimu?
Mwalimu : Marahaba
Mwanafunzi : Kuna mwanafunzi mmoja wa gredi ya sita anayeendeleza ulanguzi wa dawa za kulevya.Inaserhekana kuwa yeye hupitia uani kwenda kuzinunua. Wengi wa wateja wake ni wenzake katika gredi ya sita. Jina la mwanafunzi huyo ni Kamaliza.
Mwalimu : Nashukuru sana kwa habari muhimu ambazo umenipa. Sijui kama una la ziada.
Mwanafunzi : Mimi sina la ziada ila nakushukuru kwa kunialika ili tuzungumzie tatizo hili sugu. Niko tayari kushirikiana na utawala wa shule kuhakikisha kuwa mambo yote yako shwari. Hali hii imetokana na ung'amuzi kuwa jambo linaloshughulikiwa na wengi hufaulu.
Mwalimu : Nakupa shukrani sufufu kwa kunifaa la jua. Bila shaka ningekuwa kwenye giza totoro kuhusiana na uuzaji huo wa dawa za kulevya. Naomba kuwepo ushirikiano wa dhati baina ya utawala wa shule na viranja kwa kuwa kofi hazilii ila kwa viganja viwili. Sisi kama utawala wa shule hii ya Twasonga, tutahakikisha kuwa tumekomesha utumizi wa dawa za kulevya. Kuwa na wakati mwema.
Mwanafunzi : Asante sana. Pia nawe. (Anamsalimia.Kisha anainuka na kuondoka)
- Kwa nini mwanafunzi alimwendea mwalimu?
- Alitaka kumsalimia mwalimu wake
- Alitaka kujua kutoka kwa mwalimu wake shule zingefungwa lini
- Alitaka mwalimu ajue kuwa Kamaliza alikuwa akilangua dawa za kulevya.
- Alitaka kuripoti mateso aliyokuwa akipitia shuleni.
- Wateja wa dawa za kulevya zilizouzwa na Kamaliza:-
- walikuwa wanafunzi wa gredi ya nne
- walikuwa wanafunzi wa gredi ya sita
- walikuwa wanafunzi wa gredi ya tano
- walikuwa wanafunzi wa gredi ya tatu
- Ni methali gani mwafaka kuelezea kauli ifuatayo:- Jambo linaloshughulikiwa na wengi hufaulu?
- Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu
- Aliye juu mngoje chini
- Bahati ya mwenzio usiilalie mlango wazi
- Polepole ndio mwendo
- Mwalimu ameonyesha wazi kuwa:-
- hata kama mwanafunzi hangemwambia alikuwa akijua kuhusu uuzaji wa dawa za kulevya
- kama si mwanafunzi huyo hangejua kuhusu uuzaji wa dawa za kulevya
- hakutaka kujulishwa kuhusu uuzaji wa dawa za kulevya
- Kamaliza alikuwa mwanafunzi mwadilifu
- Kofi hazilii ila kwa viganja viwili ni mfano wa:-
- nahau C. tashbihi
- istiara
- tashbihi
- methali
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali nambari 6 mpaka 9.
Hapo zamani za kale Bweha, Ndovu, Simba na Tausi walikutana msituni karibu na kisima. Punde si punde, Ndovu alianza kutikisa masikio yake makubwa akawatazama wenzake na kujisifu.
"Bila shaka mtakubaliana nami kuwa mimi ndimi mnyama mwenye nguvu kuliko wanyama wote duniani. Ninaweza kupitia msitumi kwenye miti tele kwa kutumia mkonga wangu mrefu. Kwangu miti ni kama matawi," akajivuna.
"Huenda ukawa na nguvu" akalalama simba, "lakini hakuna kinachomithilishwa na ukali wangu. "Mimi ni mfalme wa msituni kwa sababu ya ukali wangu."
"Haiwezekani asilani.Maarifa na ujanja ni muhimu kuliko ukali na nguvu," akasema Mbweha. "Mimi huishi vyema kwa sababu ya akili zangu."
- Ni mnyama yupi ambaye hajatajwa kwenye kifungu?
- Mbweha
- Ndovu
- Simba
- Chui
- Chagua kauli isiyo ya kweli
- Ndovu alidai kuwa mnyama mwenye nguvu kuliko wote
- Simba alidai kuwa mnyama mkali kuliko wote
- Mbweha alidai kuwa mnyama mwenye akili kuliko wote
- Tausi alidai kuwa ndege mwenye urembo kuliko wanyama wote.
- Ni nini muhimu kuliko ukali na nguvu?
- Maarifa na ujanja
- Ujanja na ukali
- Nguvu na maarifa
- Wema na hekima
- Ni mnyama yupi alimpinga ndovu?
- Tausi
- Mbweha
- Simba
- Chui
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 10 mpaka 12.
Familia ya akina Bidii iliamua kutengeneza ratiba ya mapishi nyumbani kwao. Bidii, Zubedia, Hekima na Atieno walipendekeza aina ya vyakula ambavyo wangependelea kupika wikendi. Tazama jedwali lifuatalo
Jamaa | Jumamosi | Jumapili |
Bidii | Chapati | Pilau |
Zubedia | Ugali | Chapati |
Hekima | Sima | Chapati |
Atieno | makande | Pilau |
- Ni chakula kipi kilipendekezwa mara nyingi?
- Chapati
- Pilau
- Makande
- Sima
- Taja jamaa wawili waliopika chakula sawa?
- Bidii na Hekima
- Atieno na Zubedia
- Zubedia na Hekima
- Bidii na Zubedia
- Ni chakula kipi hakikupendekezwa mara nyingi?
- Chapati
- Pilau
- Sima
- Makande
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 13 mpaka 15.
Hapo zamani za kale, nyani na mamba walikuwa marafiki wa kufa kuzikana. Watoto wao walipendana na kufaana kama ndugu wa toka nitoke."Familia ya mamba iliishi mtoni nayo ya nyani iliishi katika msitu uliokuwa maili thelathini kutoka mtoni. Kila mara marafiki hawa walitembeleana na kusaidiana kwa hali na mali. Kwa vile mamba alikuwa mvuvi mashuhuri, aliweza kumsaidia nyani na familia yake kwa samaki wa aina mbalimbali. Nyani naye alimpelekea mamba matunda na nafaka kutoka shambani mwake.
- Chagua kauli ya kweli
- Nyani na mamba walikuwa maadui wakubwa
- Familia ya mamba iliishi msitumi
- Msitu ulikuwa mita thelathini kutoka mtoni
- Mamba alikuwa mvuvi mashuhuri
- Nyani naye alimpelekea mamba matunda pamoja na haya yote ila
- Mahindi
- Maharagwe
- Mtama
- Mawele
- Hii ni tamathali gani ya lugha?
Watoto wao walipendana na kufaana kama ndugu wa toka nitoke- Tashbihi
- Istiara
- Chuku
- Tanakali za sauti
Soma kifungu kifuatacho. Kina nafasi 16 hadi 20. Umepewa majibu manne hapo. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.
Katika enzi za mababu ___16___ wanyama ___17___ waliishi jinsi sisi binadamu ___18___ Waliweza kulima, kufuga, kuchota maji na hata kupika. Wanyama wote waliishi katika jamii tofauti tofauti kwenye vijiji. Vijiji kadhaa kwa pamoja___19___miliki iliyotawaliwa na mnyama
mmoja ___20___ na wanyama wengine kuwa mfalme wao.
A | B | C | D | |
16. | yetu | wetu | zetu | letu |
17. | sote | wote | zote | yote |
18. | tunavyolishi | tunaishi | anaishi | aliishi |
19. | ziliunda | iliunda | uliunda | viliunda |
20. | aliyochaguliwa | aliyechaguliwa | aliochaguliwa | alivyochaguliwa |
Kuanzia swali nambari 21 mpaka 30, jibu kulingana na maagizo.
- Kivumishi ni kipi katika sentensi hii?
Mwalimu mpole alienda shambani jana.- mwalimu
- mpole
- alienda
- shambani
- Andika wingi wa sentensi ifuatayo:-
Yai langu limepikwa na tarishi- Mayai yangu yamepikwa na tarishi
- Mayai yetu yamepikwa na tarishi
- Mayai yangu yamepikwa na matarishi
- Mayai yetu yamepikwa na matarishi
- Chagua sentensi iliyoakifishwa kwa usahihi
- Wanyama wafugwao ni pamoja na: ng'ombe, mbuzi na kondoo
- Ukienda ng'ambo uniletee yafuatayo: vikoi, saa na mkufu
- Ala, kumbe unajua kuendesha baiskeli
- Mwalimu alipoingia darasani! alikuwa na furaha
- Tunasema darasa la wanafunzi na _______________________ la nyuki
- bumba
- kundi
- fungu
- jamii
- Kitenzi 'panda' katika kauli ya kutendwa ni ____________________
- pandisha
- pandika
- pandwa
- pandia
- Chagua majina yaliyo katika ngeli ya U-U
- Ugonjwa, uyoga
- Ugali, uyoga
- Ute, uzi
- Ua, uji
- Kanusha sentensi ifuatayo:-
Mwalimu ameelekea darasani- Mwalimu hajaelekea darasani
- Mwalimu huwa hataelekea darasani
- Mwalimu huwa haelekei dukani
- Mwalimu hakuelekea dukani
- Ni sentensi gani yenye kielezi cha wakati?
- Mwalimu mpole ni huyu
- Magari ya safari Rally ni mengi
- Babu yangu atawasili kesho
- Ni wanafunzi wangapi wako huku?
- Ni sentensi gani yenye kivumishi cha pekee
- Mwanariadha mwingine ametuzwa
- Vyote ulivyoleta vimeharibika
- Uliza maswali mengi lakini yaliyo na umuhmu
- Wasanii wawili ndio wanaohitajika
- Kupiga miguu ni sawa na:
- Kukimbia kwa kasi
- Kutuliza miguu
- Kuteleza matopeni
- Kutembea
INSHA
Mwandikie rafiki yako barua ukimwelezea jinsi likizo yako ilivyokuwa.
MARKING SCHEME
- C
- B
- A
- B
- D
- D
- D
- A
- C
- A
- C
- D
- D
- B
- A
- C
- B
- A
- D
- B
- B
- D
- B
- A
- C
- B
- A
- C
- A
- D