Wednesday, 29 March 2023 12:28

School Based Assessment 2023 Grade 6 Kiswahili - Grade 6 Mid Term 1 Set 2

Share via Whatsapp

Soma mazungumzo haya kisha ujibu swali la 1 hadi la 5.  

G6SwaT1SB23002P1

(Ni hotelini ambapo Roda na Hamisi wanakutana kunywa staftahi)

 
Roda:           Hujambo rafiki yangu.U hali gani?
Hamisi:        Sijambo,hali yangu ni njema.Nashukuru Maulana kwa afya njema.Je, u mzima?
Roda:           Naam,mimi ni mzima kama kigongo.Nimekuja kunywa kiamshakinywa.
Hamisi:        Mimi pia, wazazi wako vipi?Natumai wako salama salimini.
Roda:           Ni wazima japo mama alienda mjini kumwona bibi ambaye ni mgonjwa.
Hamisi:        Lo! Poleni sana.Atapata afueni.Mungu halali.
Roda:           Asante sana msena wangu.Bila shaka hapo umenena.Atapona.
                     (Mhudumu anawakata kauli kuwaomba waagize vyakula ama vinywaji)
Mhudumu:   Karibuni sana wateja wapendwa.Niwaletee nini?
Hamisi:        Kawaida ndugu yangu. Chai na chapati. Tutashukuru.
                     (Mhudumu anaondoka upesi,muda si muda anarudi akiwa amebeba sinia kubwa)
Mhudumu:   Karibuni sana.
Hamisi:         Starehe.

 1. Ni kweli kusema kuwa Roda na Hamisi walikuwa
  1. maadui
  2. marafiki
  3. wahudumu
  4. wacheshi
 2. Hamisi alitaka nini hotelini?
  1. Kusalimia mhudumu
  2. Kusalimia Roda
  3. Kuwajulia hali
  4. Kupata mlo
 3. Neno bibi lina maana sawa na
  1. nyanya
  2. mke
  3. mume
  4. mzee
 4. Ni nini maana ya msemo kata kauli?
  1. Kukatiza mtu maneno
  2. Kumwamkua mtu
  3. Kumshauri mtu
  4. Kuamulia mtu
 5. Unafikiri sinia ilibeba nini?
  1. Vyakula na vinywaji
  2. Vyakula pekee
  3. Vinywaji pekee
  4. Vikombe na birika

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali la 6 hadi la 9

G6SwaT1SB23002P2

Tulikuwa tumeingoja siku hiyo kwa hamu na ghamu. Ilikuwa ni siku ambayo mimi na sahibu yangu wa kufa kuzikana Yona tulikuwa tumepanga kuenda kuvua samaki. Tulitengeneza ndoana zetu na sisi hao! Tukang'oa nanga na kubandua nyayo mpaka mto Lusumu ambao haupo mbali sana na nyumbani kwetu. Haikuchukua muda mrefu kabla ya kufika mto Lusumu.

Moja kwa moja, tulianza kazi yetu. Billy ndiye aliyekuwa wa kwanza kubahatika. Alimvua mkunga mkubwa na mweusi tititi kama makaa. Alifanana sana na joka kiasi cha kwamba nusura tutundike miguu mabegani. Jisamaki hilo liligaragara huku na huko kwa dakika sita hivi mwishowe likatulia.

Tuliendelea na uvuvi wetu huku tukipiga soga kwa bashasha ghaya. Mara lo! Katika hizo harakati za kuvua samaki zaidi, nilitupa jicho juu ya mti. Mtini, palikuwa na joka jeusi na nono kupindukia. Lilikuwa limetukodolea macho kana kwamba lilitaka kutumeza wazima wazima. Macho yalitutoka pima huku tukigwaya kwa hofu. Punde si punde, tukawa miguu nibebe ili kuepukana na hatari hiyo.

 1. Yona walitaka kwenda wapi?
  1. Kufua nguo
  2. Kunasa samaki
  3. Kuona mto
  4. Kutembea Lusumu
 2. Ni kweli kusema kuwa mto Lusumu
  1. ulikuwa karibu
  2. ulikuwa na nyoka
  3. haukuwa na samaki
  4. ulikuwa mbali
 3. Kulingana na kifungu hiki,mkunga ni aina ya
  1. nyoka
  2. ndege
  3. samaki
  4. mamba
 4. Ni hatari gani Yona walipata?
  1. Kushika samaki
  2. Kushika nyoka
  3. Kutupa macho juu
  4. Kumwona nyoka

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali la 10 hadi la 12.   

Mtaa wetu huwa na maduka matano.Maduka haya huuza bidhaa pia za aina mbalimbali, Maria, Kendi, Sang na Oloo waliandamana kwenda kununua bidhaa. Sang alitaka vyakula, Kendi alitaka vifaa vya kielektroniki, Oloo alitaka simu na shati. Naye Maria alitaka kutembea tu madukani kujionea bidhaa. Soma jedwali lifuatalo kisha ujibu maswali.

 Jina la duka   Bidhaa 
 FAIDA  Unga, sukari, mboga, matunda
 JAMAA  Mboga, matunda, nguo, simu 
 FURAHA  Televisheni, tabuleti, rununu, kompyuta 
 DOLA  Matunda, mboga, mavazi, simu 

 

 1. Kendi angeenda duka gani?
  1. DOLA na FAIDA
  2. JAMAA na FURAHA
  3. FURAHA na FAIDA
  4. JAMAA na FAIDA
 2. Ni nani hakununua chochote?
  1. Sang
  2. Maria
  3. Oloo 
  4. Kendi
 3. Ni kweli kusema kuwa
  1. Oloo alinunua mavazi
  2. Maria alinunua simu
  3. Sang alinunua tabuleti
  4. Kendi alinunua vyakula

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali la 13 hadi la 15. 

Siku moja wanyama wa jamii ya simba, yaani walanyama waliungana pamoja. Azima ya mkutano ilikuwa kubuni mbinu za kuwinda Walamea. Walamea nao walikutana. Walijadili kuhusu mipango na mbinu za kujificha. Walionekana kuwa na wasiwasi wa mwasi. Kwa pamoja swara na wenzake waliamua kuhamia msitu uliokuwa na vichaka na mashimo mengi ya mhanga.

Waling'oa nanga na kuenda kasi kabla ya mkutano wa maadui kuisha. Mfalme simba alipotamatisha mkutano, wenzake waliingia vichakani kuwinda. Lo! Hawakupata mlo wowote. Njaa iliwatesa sana kwa siku nyingi. Baadaye waligundua kuwa wanyama waliopangiwa kuwindwa wamehama.

 1. Ni kweli kusema kuwa
  1. mikutano ilikuwa mingi
  2. mikutano ilikuwa miwili
  3. mkutano ulikuwa mmoja
  4. hakukuwa na mikutano
 2. Ni kwa nini wanyama walikuwa na wasiwasi?
  1. Woga
  2. Ujasiri
  3. Baridi
  4. Muda
 3. Ni nini maana ya msemo waling'oa nanga?
  1. Kumaliza safari
  2. Kwenda mbio
  3. Kutifua vumbi
  4. Kuanza safari

Soma kifungu kifuatacho. Kina nafasi 16 hadi 20. Umepewa majibu manne hapo. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya vale uliyopewa.

Siku moja nilikuwa ___16___ mpira wa miguu yaani ___17___ na rafiki yangu ambayetulipendana na yeye kama chanda na ___18___. ___19___ tuliamua kupumzika chini ya mti ___20___ mwembe ambao ulikuwa na matunda matamu.

   A   B   C   D 
 16.   nachezwa   nikicheza   ninacheza   nimecheza 
 17.  boli  voliboli   kandanda   pete 
 18.  pete  kidole  arusi   mkono 
 19.  Zote  Nyote   Wote  Sote 
 20.  ya  wa  la  cha 


Kutoka swali la 21 hadi la 30. Chagua jibu sahihi. 

 1. Jaza mapengo kwa maneno yanayofaa: Waimbaji wali____________ kupiga ______________
  1. koma, gona
  2. piga, pinga
  3. goma, ngoma
  4. aga, anga
 2. Chagua maelezo yaliyo sahihi.
  1. Meno husaidia kuonjea chakula.
  2. Moyo husaidia kusukuma damu.
  3. Figo husaidia kuhifadhi mkojo.
  4. Pafu husaidia kusaga chakula.
 3. Jaza pengo kwa kivumishi cha sifa: Madawati ______________________ hufurahisha mwalimu.
  1. masafi
  2. chafu 
  3. safi
  4. yote
 4. Jibu maagano haya: Buriani
  1. buriani dawa
  2. binuru
  3. aheri
  4. pia nawe
 5. Tegua kitendawili hiki: Chakula kikuu cha mtoto
  1. maziwa
  2. usingizi
  3. ndizi
  4. uji
 6. Chagua wingi wa sentensi hii: Soko lile lina tunda.
  1. Soko lile lina matunda
  2. Masoko yale yana tunda
  3. Masoko yale yana matunda
  4. Soko lile lina matunda
 7. Je, nomino mbu ni katika ngeli gani?
  1. U-I
  2. A-WA
  3. I-ZI
  4. LI-YA
 8. Ipi si sehemu ya kompyuta?
  1. Kiwambo
  2. Bodidota
  3. Kipanya
  4. Mitini
 9. Tambua kielezi katika sentensi hii: Mwanafunzi mzuri alicheza vizuri.
  1. vizuri
  2. mzuri
  3. alicheza
  4. mwanafunzi
 10. Chagua kinyume cha: Bandika picha nje.
  1. Bandua picha nje
  2. Bandika picha ndani
  3. Bandua picha ndani
  4. Usibandue picha nje

INSHA

Andika insha ya kusisimua ukurasa mmoja nanusu kuhusu:

MECHI YA KUSISIMUA

MARKING SCHEME

 1. B
 2. D
 3. A
 4. A
 5. A
 6. B
 7. A
 8. C
 9. D
 10. B
 11. B
 12. A
 13. B
 14. A
 15. D
 16. B
 17. C
 18. A
 19. D
 20. B
 21. C
 22. B
 23. C
 24. A
 25. B
 26. C
 27. B
 28. D
 29. A
 30. C
Join our whatsapp group for latest updates

Download School Based Assessment 2023 Grade 6 Kiswahili - Grade 6 Mid Term 1 Set 2.


Tap Here to Download for 30/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students