Friday, 31 March 2023 06:03

Kiswahili Questions and Answers - Grade 6 Mid Term 1 Exams 2023 Set 6

Share via Whatsapp Written by
Rate this item
(0 votes)

Soma kifungu hiki kisha ujibu maswali yafuatayo. 

Akilibora Ujingakutu ni mwenye heshima na busara. Alijitahidi asikasirike ovyoovyo hadharani. Kukasirika ovyo kunamfanya mtu aonekane baradhuli. Mtu huyu hakukasirika hata kama ungemwudhi kiasi gani. Labda alizificha hamaki zake kwa sababu mwungwana hakasiriki usoni, hukasirika moyoni.

Alipoitwa shuleni Hekimautu kuongea na wanafunzi, hakutarajia kuzungumza kwa muda mrefu. Alikuwa na maneno machache tu ya kuwaeleza wanafunzi wote ukumbini. Alinena kuhusu umuhimu wa kurauka na kuenda shuleni kusoma. Pia alieleza kuwa darasani ni mahali pa kukipa kichwa nafasi, wakati na uwezo wa kuchora mambo na kuyaweka kichwani ili yatumike katika maisha ya baadaye.

Maswali

  1. Akilibora Ujingakutu alikuwa ________________________________
    1. mwungwana
    2. mjinga
    3. mwalimu
    4. mkali
  2. Kisawe cha heshima ni ________________________________
    1. hekima
    2. taadhima
    3. huruma
    4. akili
  3. Akilibora alialikwa kumaanisha alipatiwa:-
    1. mwaliko
    2. wito
    3. mwali
    4. uwakilishi
  4. Sifa za mwungwana ni __________________________________
    1. kuhamaki
    2. kuficha hasira.
    3. kununa 
    4. kufunza
  5. Bwana Ujingakutu hakuwafunza wanafunzi kuhusu:-
    1. wakati wa kuenda shuleni kusoma.
    2. umuhimu wa kufika shuleni mapema.
    3. umuhimu wa darasa.
    4. manufaa ya kuenda shuleni.

Jibu maswali kulingana na kisa hiki.

Siku moja ndovu alikuwa akipita kwenye msafara wa siafu. Aliwakanyaga bila kujali kuwa siafu waliumia. Siafu walijaribu sana kumwuma ndovu kwa nguvu zao zote lakini ndovu hakuhisi uchungu. Alizidi kuwakanyaga siafu. Siafu walizidi kuumia na kulalamika ila hakuna aliyewasaidia. Siafu mmoja aliamua kutambaa polepole hadi kwenye mwiro wa ndovu. Aliingia ndani na kutulia tuli! Ndovu hakujua chochote. Mara alianza kumwuma ndani kwa ndani kwenye mwiro wake.Ndovu alihisi uchungu mwingi. Aliendelea
kumwuma kwa muda mrefu. Ndovu alijaribu kupiga chafya lakini siafu yule hakutoka. Ndovu akaenda penye mti mkubwa. Akaanza kuuchapa mwiro kwenye mti hadi ukatoka damu. Siafu hakutoka. Aliendelea kujiumiza kwenye mti ule hadi akafa. Hatimaye siafu alienda zake.

Maswali  

  1. Ndovu alipokuwa akipita alikanyaga __________________________
    1. msafara
    2. siafu
    3. nyasi
    4. mwiro
  2. Msafara wa siafu ni siafu _________________________
    1. wakali
    2. wadogo
    3. wanyonge
    4. wengi
  3. Siafu walipokanyagwa ___________________________
    1. walilia
    2. waliumia 
    3. waliamka
    4. walikimbia
  4. Siafu aliyemwuma ndovu aliingia wapi? Kwenye:-
    1. pembe
    2. mkonga
    3. jicho
    4. mdomo 
  5. Ndovu alijaribu kumtoa siafu kwa kuupiga mwiro mtini na _____________________
    1. kupiga mayowe
    2. kulia
    3. kuenda miayo
    4. kupiga chafya.

Soma kifungu kisha ujibu maswali barabara.

Jina la mjomba wangu ni Simu Sumu. Ana simu nzuri sana. Anakipenda kifaa hiki sana na mara nyingi hukisifia kuwa kimeifanya dunia kuwa kimoja au vitu viwili vilivyounganishwa kwa sauti moja. Lakini kwa upande mmoja,mjomba anachukia zaidi jinsi watu wanavyotumia simu kuwadanganya wengine. Watu hudanganya kuwa hawapo karibu kumbe wapo! Wabaya zaidi ni matapeli wanaowaibia wengine kupitia rununu.

Mjomba alitumiwa pesa hewa shilingi elfu kumi. Ndani ya simu yake alikuwa na pesa zake zaidi ya shilingi elfu kumi. Tapeli akamwandikia arafa kuwa amemtumia shilingi elfu kumi. Kabla ya mjomba kutulia akili, alipigiwa simu kuwa pesa hizo alitumiwa kwa bahati mbaya. Akaombwa azirudishe pesa zile kwa mtumaji. Mjomba kwa huruma, akatuma pesa alizoulizwa. Alipoangalia salio la akiba yake, alipata kuwa imepungua. Akagundua kuwa alimtumia tapeli pesa zake. Kuanzia siku hiyo, mjomba anazichukia simu zote za matapeli. Hizo ndizo anazoita simu sumu!

Maswali   

  1. Mjomba wangu ana simu __________________________
    1. kubwa
    2. sumu
    3. nzuri
    4. ghali
  2. Mjomba anachukia zaidi watu gani?
    1. Matapeli wa kutumia simu.
    2. Wateja wasiopatikana.
    3. Wadanganyifu kwa simu.
    4. Wanaoandika arafa.
  3. Pesa hewa ni pesa zipi?
    1. Za kuiba
    2. Nyingi
    3. Bandia
    4. Ambazo hazipo.
  4. Mjomba anaziona simu za udanganyifu kama _____________________________
    1. simu
    2. wazimu
    3. sumu
    4. sima
  5. Maandishi yanayotumwa kwenye simu ni ________________________________
    1. arifa
    2. arifu
    3. taarifa
    4. arafa

Jaza mapengo kwa majibu mwafaka. 

Taa ___16___ umeme ___17___ mwangaza ___18___kutosha. Giza ___19___ usiku hutoweka mpaka usiku ___20___ kama mchana.

   A   B   C   D 
 16.   ya   la   wa   cha 
 17.  una   ina   zina    yana
 18.  za  la   wa   ya 
 19.  ya  za  la  cha
 20.   ikiwa    yakawa   ukawa   zikawa 


Kamilisha kwa kufuata maagizo. 

  1. Mfupa unaoshikilia meno kinywani unaitwa ___________________________-
    1. ufizi
    2. ulimi
    3. utaya
    4. midomo.
  2. Jozi ipi isiyo na maneno yenye sauti tata?
    1. kacha- kasha
    2. ponda - poda
    3. chuma - chama
    4. piga - pinga
  3. Maneno haya yatafuatana vipi katika kamusi?
    1. chunga
    2. chupa
    3. chanda
    4. changa
      1. iii, iv, ii, i
      2. i, iv, iii, ii
      3. iii, i, iv, ii 
      4. iii, iv, i, ii
  4. Mtoto yule mzembe haandiki vizuri. Kivumishi kionyeshi ni kipi?
    1. mtoto
    2. mzembe
    3. yule
    4. vizuri 
  5. Kamilisha: Mfupa ______________________________
    1. mkubwa
    2. kubwa 
    3. mikubwa
    4. makubwa.
  6. Sentensi ipi iliyo na kiashiria cha mbali kidogo?
    1. Mzee yule amelala.
    2. Mti huo utakatwa.
    3. Kalamu hizi haziandiki.
    4. Ndoo zao zinavuja. 
  7. Neno hoki ni aina gani ya neno?
    1. Kitenzi
    2. Nomino
    3. Tahajia
    4. Ngeli.
  8. Sentensi: Maji mengi yamemwagika chini ina kivumishi kipi cha idadi?
    1. jumla
    2. kamili
    3. wingi
    4. katika orodha. 
  9. Mchezo wa kuvutana kamba huitwa:-
    1. sataranji
    2. raga
    3. jugwe
    4. mwereka.
  10. Endeleza:
    Ulinunua vitabu _______________________________________?
    1. ngapi 
    2. vigani
    3. zipi
    4. vingapi

INSHA.   

Andika insha ya wasifu kuhusu 'MWILI WANGU'

MARKING SCHEME

  1. A
  2. B
  3. A
  4. B
  5. A
  6. B
  7. D
  8. B
  9. B
  10. D
  11. C
  12. A
  13. D
  14. C
  15. D
  16. A
  17. B
  18. C
  19. C
  20. C
  21. C
  22. C
  23. D
  24. C
  25. A
  26. B
  27. B
  28. A
  29. C
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Grade 6 Mid Term 1 Exams 2023 Set 6.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Read 2656 times Last modified on Monday, 03 April 2023 11:44

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.