Wednesday, 05 July 2023 08:11

Kiswahili Questions and Answers - Grade 6 Mid Term 2 Exam 2023 Set 3

Share via Whatsapp

Soma kifungu hiki kisha ujibu maswali yafuatayo

Wanyama na ndege wote waliandaa mkutano wao wa mwaka ili wajadiliane jinsi ya kuishi vizuri kama binadamu. Mzee Ndovu alikuwa kiongozi kwa upande wa wanyama. Ndege kwa upande wao waliongozwa na Mzee Mbuni. Baada ya maombi na sala, wote walijiweka tayari kuanza mkutano. Mara akaja Bundi. Wanyama walishtuka! Wakamwambia, "Usikae upande wetu, wewe si mwenzetu. Una kichwa cha Paka lakini unaruka kama ndege. Nenda upande ule wa ndege!"

Alienda upande wa ndege. Nao pia walimfukuza na kumwambia, "Toka kwetu, wewe si mmoja wetu. Sisi ndege hatuna vichwa vya Paka na macho makubwa hivyo!"

Bundi alikosa upande wa kukaa. Kwa wanyama alikataliwa, kwa ndege hakutakiwa. Aende upande upi? Alipoona pale hapakaliki, aliondoka akaenda zake. Hiyo ndiyo sababu Bundi hukaa peke yake wala hatoki mchana. Hutoka na kuwinda usiku tu. Naye huwawinda na kuwala ndege na wanyama wadogo wadogo. Je, wewe upo upande gani? Una msimamo au upo tu kama Bundi? Chaguo ni lako!

Maswali

  1. Neno 'waliandaa' ni sawa na?
    1. walihadaa
    2. walileta
    3. waliweka
    4. walitayarisha
  2. Mkuu wa wanyama alikuwa nani?
    1. Mbogo
    2. Kifaru
    3. Tembo
    4. Nyati
  3. Bundi alipofika mkutanoni alikuja huku?
    1. akipaa
    2. akikimbia
    3. akipeperuka
    4. akipepea.
  4. Wanyama walimkana Bundi kwa sababu?
    1. ya kichwa chake cha paka
    2. ya macho yake makubwa
    3. ya sauti yake ya kutisha
    4. mabawa, miguu na manyoya yake
  5. Habari hii inatufunza kuwa ni vizuri mtu kuwa
    1. na maumbile ya kipekee
    2. na maumbile mazuri
    3. mnyama au ndege
    4. na msimamo dhabiti

Soma kifungu hiki kisha ujibu swali la 6-10.
Maadili ni mwenendo mwema, mambo ya haki au yanayozingatia adabu na tabia njema. Wazazi majumbani ni vizuri wawe wakiketi na watoto wao na kuwapatia mawaidha mema kuhusu maisha. Naye mzazi awe mfano bora wa kuigwa na watoto wake. Walimu shuleni wasizingatie mafundisho ya mbili mara tatu tu na kuzingatia ngeli bali pia wawape wanafunzi nasaha na mawaidha mazuri kuhusu maisha mema, utu na adabu njema. Wakati mwingine nidhamu ni bora kuliko elimu ya shuleni. Elimu pekee haikamilishi utu wa mtu lakini nidhamu na uadilifu humtukuza mtu akatukuka na kuheshimika zaidi.

Watoto nao wasiwe wajuaji kupindukia eti kwa sababu wanavimbishwa vichwa kwa kuitwa majina ambayo hata hawajui asili yake; eti dotikomu na dijitali. Huo udotikomu na udijitali hauna thamani yoyote kwa mtu ni mlevi, mwizi, mjinga, asiye na utu wala nidhamu. Aliyeathiriwa na dawa za kulevya akilini ana faida gani hata kama ni dotikomu au dijitali?

Dunia imejaa matatizo mengi mno. Ni vyema kutumia akili vyema kwa kuwaza na kufikiri kabla ya kutenda kitendo chochote cha kijinga. La sivyo utakuwa mtumwa wa maradhi, majuto na mateso. Heri kuzuia kuliko kujuta.Majuto ni mjukuu huja kinyume.
Maswali

  1. Uadilifu au maadili ni kuzingatia nidhamu na
    1. tabia njema
    2. uzalendo
    3. afya bora
    4. elimu bora.
  2. Mzazi anaweza tu kumsaidia mtoto kuwa bora endapo yeye ni
    1. msomi
    2. mjuaji
    3. kielelezo
    4. mkali
  3. Walimu wanapowafundisha wanafunzi shuleni wazingatie pia kuwapa wanafunzi mawaidha mema na
    1. vichapo
    2. ushauri
    3. mafunzo ya elimu tu
    4. hesabu
  4. Watoto wanaopotoka na kuwa walevi wa dawa za kulevya huwa?
    1. wamevimbishwa vichwa
    2. hawafai kitu
    3. dotikomu na dijitali
    4. hawana maana
  5. Majuto ni mjukuu. Hii ni kusemsa kuwa______jambo ni vizuri kufikiria
    1. baada ya kutenda
    2. kabla ya kutenda
    3. wakati wa kutenda
    4. bila kutend

Soma kisa hiki kisha ujibu swali la 11-15
Juma alikuwa mtoto mvivu aliyeogopa kuenda shuleni. Wazazi wake walimbembeleza asikatae shule. Walimwambia kwamba kusoma kuna faida sana katika maisha ya baadaye. Yeye alichukia masomo. Alipenda kulala na kuamka wakati wowote aingie jikoni kutafuta chakula kisha aende zake kucheza. Alipowaona wazazi wake wakimsukuma sana aende shuleni, aliamua kujifanya mgonjwa. Alilala huku akitetemeka sana. Wazazi wake walidhani kuwa alikuwa mgonjwa.

Basi walimwita daktari mmoja wa hapo karibu. Akaja akamdunga sindano bandia na kumpa dawa ambazo hazieleweki. Mtoto yule akawa mgonjwa kabisa tena mahututi. Akawa anachungulia kaburi. Daktari yule alipoona hivyo, alitoroka na kumwacha Juma akikaribia kuaga dunia.
Naam, ugonjwa wa uongo ukazaa ugonjwa wa ukweli. Faida ni gani?

Maswali

  1. Juma aliogopa kuenda shuleni kwa sababu
    1. ya ugonjwa
    2. uvuvi
    3. woga
    4. uzembe
  2. Juma alipenda yote haya ila
    1. kulala
    2. kula
    3. kusoma
    4. kucheza
  3. Juma alipoona kuwa anasukumwa sana kusoma aliamua
    1. kuwa mgonjwa
    2. kujisingizia  ugonjwa
    3. kufa
    4. kuitiwa daktari
  4. Wazazi walidhani kuwa Juma alikuwa mgonjwa kwa kuwa alikuwa
    1. akilia
    2. akilala
    3. akitetemeka
    4. amekosa shule
  5. Kichwa kinachofaa zaidi taarifa hii ni 
    1. Msiba wa kujitakia
    2. Tamaa mbele mauti nyuma
      aliamua
    3. Jana si leo
    4. Kufa na kupona.

Soma kifungu hiki kisha ujaze pengo 16-20 kwa jibu lifaalo zaidi.
Siku moja mbwa __16____ na njaa, akatamani __17____ nyama. Lakini___18___na uwezo wa kupata nyama. Mbwa___19___ kulia. Paka akamwuliza, "Mbwa, kwa nini unalia?" Mbwa__20____kujibu.

   A   B   C   D 
16   ilikua  zilikuwa   alikuwa walikuwa 
 17  kula  kukula  akule  ikule
 18  haukuwa  haikuwa  hakukuwa  hakuwa
 19  ilianza  zilianza   alianza  ameanza
 20   hakutaka  haikutaka  haitaki  hakumtaka


Kutoka swali la 21 hadi 30 jibu kulingana na maagizo.

  1. Tambua kielezi katika sentensi hii.
    Watoto wazuri wameandika vizuri.
    1. wazuri
    2. watoto
    3. andika
    4. vizuri
  2. Andika sentensi ifuatayo katika hali ya ukubwa.
    Ndoo hii ilipasuka.
    1. Doo hili ilipasuka.
    2. Jindoo hili lilipasuka.
    3. Jidoo hili lilipasuka.
    4. Doo hili lilipasuka.
  3. Chagua nomino ambata katika sentensi. Garimoshi limebeba mkungu wa ndizi na sukari.
    1. ndizi
    2. sukari
    3. garimoshi
    4. mkungu
  4. Kisawe kipi kisicho ambatanishwa ipasavyo?
    1. Njia               -   Baraste
    2. Televisheni   -   Runinga
    3. Shamba        -   Mgunda
    4. Msichana      -   Mvuli
  5. Ipi isiyo sahihi katika kauli ya kutendua?
    1. Anika  -  Anua
    2. Penda -  Pendua
    3. Pakia  -  Pakua
    4. Funga -  Fungua
  6. Kamilisha kwa kiulizi sahihi
    Mlichukua  viti______?
    1. vigani
    2. ngapi
    3. vipi
    4. nani
  7. Jaza kwa kiambishi '-amba'.
    Mche_____ ulipandwa umemea
    1. ambayo
    2. ambacho
    3. ambalo
    4. ambao
  8. Ni kivumishi kipi kilichotumika katika sentensi hii?
    Zawadi alinipa kitabu kile jana.
    1. wakati
    2. kiashiria
    3. sifa
    4. kirejeshi
  9. Katika kamusi, baada ya neno 'mpira' wameandika nm. Hii inaonyesha nini?
    1. aina yake
    2. ngeli nyake
    3. wingi wake
    4. tahajia yake
  10. Kisawe kipi kisicho ambatanishwa ipasavyo?
    1. Ndoa yake ina doa.
    2. Shombo hiki kinanuka chombo.
    3. Uga wao una unga.
    4. Mwenye njaa hajatupa chakula kwenye jaa.

INSHA

Umepewa dakika 40 kuandika insha yako

Mwandikie mwalimu mkuu barua ya kuomba msamaha kwa kutohudhuria shule kwa siku nne bila ruhusa.

MARKING SCHEME

  1. D
  2. C
  3. A
  4. D
  5. D
  6. A
  7. C
  8. B
  9. A
  10. B
  11. D
  12. C
  13. B
  14. C
  15. A
  16. C
  17. A
  18. D
  19. C
  20. A
  21. D
  22. D
  23. C
  24. D
  25. B
  26. C
  27. D
  28. B
  29. A
  30. B
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Grade 6 Mid Term 2 Exam 2023 Set 3.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students