Monday, 27 March 2023 12:22

Kiswahili Questions and Answers - Grade 5 Opener Exams Term 1 2023 Set 6

Share via Whatsapp

Jaza pengo kwa kuchagua jawabu lifaalo zaidi kutoka nambari 1 mpaka 5. 

Siku ___1___ mwalimu aliingia ___2___ mwetu ili atufunze somo tulipendalo ___3___ Kiswahili. Kila mwanafunzi alitoa ___4___ yake ili aangalie jinsi maneno yanavyofuatana na yanavyoendelezwa ___5___ ya somo mwalimu aliondoka na kuelekea majilisini. 

   A   B   C   D 
 1.   moja   mmoja   pamoja   kimoja 
 2.  nyumbani   kanisani   darasani   majilisini 
 3.  cha  la  na  kwa
 4.  penseli  sare  dawati  kamusi
 5.  Baada  Kabla  Chini  Kando


Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 6- 10 

Nchi yetu ya Kenya ina Kaunti 47. Kaunti hizo ni kama vile Nyandarua, Kisumu, Taita Taveta na Garissa. Kila kaunti huongozwa na Gavana pamoja na naibu wake. Kila kaunti huwa na bendera tofauti na nyingine lakini bendera ya taifa hupeperushwa kwenye kaunti zote. Bendera ya taifa letu ina rangi nne. Rangi inayopatikana juu kwenye bendera ni nyeusi ambayo ni ya ngozi yetu. Rangi nyeupe hutenganisha rangi nyeusi, nyekundu na kijani. Nyekundu ardhi hutukumbusha damu iliyomwagwa na wapigania uhuru, nayo kijani ni ya ardhi yenye mimea. Rangi nyeupe ni ya amani. Tulipopata uhuru, Mkenya mmoja kutoka kaunti ya Makueni aliipandisha bendera kwenye Mlima Kenya kama njia mojawapo ya kusherehekea uhuru. Alituzwa na serikali kwa ushujaa na uzalendo wake kwani haikuwa rahisi kuipandisha bendera. Mkenya huyo alikuwa akiitwa Kisoi Munyao. 

 1. Mkenya aliyeipandisha bendera kileleni mwa Mlima Kenya alikuwa mzaliwa wa kaunti gani?
  1. Garissa
  2. Makueni 
  3. Nairobi
  4. Nyandarua
 2. Ni rangi gani ya bendera inayotenganisha rangi ya kijani na nyekundu kwenye bendera ya taifa la Kenya?
  1. Manjano
  2. Nyeusi 
  3. Samawati
  4. Nyeupe
 3. Nchi ya Kenya ina kaunti ngapi kulingana na taarifa uliyoisoma?
  1. Sabini na saba 
  2. Arubaine na sita.
  3. Arobaine na saba. 
  4. Nne
 4. Kwa nini Kisoi Munyao aliipandisha bendera kwenye kilele cha Mlima Kenya?
  1. Ili atuzwe na serikali. 
  2. Alikuwa mzalendo. 
  3. Ilikuwa njia ya kusherehekea uhuru.
  4. Ili awe shujaa.
 5. Ni kweli kusema,
  1. Kisoi Munyao alikuwa mpigania uhuru.
  2. Kila Kaunti nchini Kenya ina bendera yake.
  3. Bendera ya Kenya hutukumbusha kuhusu Mlima Kenya.
  4. Serikali ya Kenya haikumtuza Mkenya aliyeipandisha bendera mlimani.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 11 - 15 

Hapo zamani za kale Twiga na Fisi walikuwa marafiki wa dhati. Walisaidiana kwa kila hali. Watoto wao walicheza na kutembeleana bila pingamizi zozote. Siku moja mwanawe Twiga aliugua homa ya mapafu. Fisi aliamua kumpa mtoto wa Twiga dawa za kienyeji ili apone. Kwa bahati mbaya mtoto huyo alikufa. Fisi alishikwa na tamaa na akamla mtoto aliyekufa baada ya kumdanganya Twiga ya kwamba amemzika kaburini. Baada ya uchunguzi kufanywa, ilibainika wazi kuwa fisi alimpa mtoto wa Twiga dawa mbaya ili afe naye amle. Bweha aliyekuwa kiongozi wa mashtaka alimhukumu Fisi kifungo cha maisha gerezani. Tangu siku hiyo urafiki wa Fisi na Twiga uliisha na wakawa maadui. 

 1. Kwa nini Fisi alipanga njama ya kumuua mtoto wa Twiga? Ili 
  1. urafiki wake na Twiga uishe. 
  2. afe naye amle. 
  3. ahukumiwe na Bweha. 
  4. augue homa ya mapafu. 
 2. Ni nani aliyetoa hukumu? 
  1. Fisi 
  2. Twiga 
  3. Mwanawe Twiga 
  4. Bweha 
 3. Wanyama wangapi wametajwa kwenye hadithi
  1. 3
  2. 5
  3. 4
  4. 2
 4. Kulingana na kifungu ulichokisoma, Fisi ana tabia zifuatazo isipokuwa 
  1. mlafi 
  2. mdanganyifu
  3. mwenye tamaa
  4. mwaminifu.
 5. Hadithi hii inatufunza nini?
  1. Tuwatibu wagonjwa.
  2. Tucheze na watoto wengine.
  3. Tujihadhari na marafiki waovu.
  4. Tuwe maadui kwa watu wote. 

Kutoką swali la 16 hadi la 28 chagua jibu lifaalo zaidi kulingana na maagizo uliyopewa

 1. Andika katika hali ya ukubwa.
  Mti:
  1. Kijiti
  2. Vijiti
  3. Jiti
  4. Miti
 2. Andika katika hali ya kukanusha: Ameadhibiwa na mwalimu.
  1. Wameadhibiwa na walimu.
  2. Hajaadhibiwa na mwalimu.
  3. Hataadhibiwa na mwalimu.
  4. Hakuadhibiwa na mwalimu.
 3. Kamilisha tashbihi hii:  Nyeupe kama
  1. nguruwe.
  2. mlingoti
  3. karatasi.
  4. theluji.
 4. Jaza nafasi kwa kutumia kinyume cha nomino iliyopigiwa mstari.
  Joto na _________________ nyingi zinaweza kusababisha magonjwa kwa watoto
  1. mwangaza
  2. baridi
  3. upepo
  4. vumbi
 5. Geuza kitenzi hiki katika hali ya kutendwa. Batiza
  1. batizika. 
  2. kubatiza
  3. batizwa. 
  4. kutobatiza. 
 6. Kisawe cha neno barua ni 
  1. ishara. 
  2. tarakilishi
  3. baraste. 
  4. waraka. 
 7. Tambua kitenzi katika sentensi hii:
  Beba mzigo huo jioni. 
  1. mzigo
  2. huo
  3. beba
  4. jioni
 8. Badala ya kusema "Mtoto anahara tunafaa kusema: Mtoto
  1. ameenda msalani. 
  2. anaendesha. 
  3. ni mja mzito.
  4. amepoa. 
 9. Tegua kitendawili:
  Nyanya anapepeta mpunga.
  1. Jua
  2. Kaptura.
  3. Upepo. 
  4. Kope
 10. Jibu salamu hizi:
  Waambaje?
  1. Marahaba. 
  2. Sina la kuamba
  3. Vizuri.
  4. Sabalkheri.
 11. Nomino gani inapatikana katika ngeli ya LI-LI 
  1. Jengo
  2. Giza
  3. Jiwe
  4. Yai
 12. Pete ni kwa kidole kama vile __________________________ ni kichwani.
  1. kipuli
  2. hina
  3. mkufu
  4. taji
 13. Tumia nomino za makundi kujaza nafasi. 
  Mama amenunua  ____________________ la maembe sokoni.
  1. pakacha
  2. tita
  3. jozi 
  4. biwi 

Soma barua hili kisha ujibu maswali 29-30 

Kisa Hadija
S.L.P. 34
KIBANZI 
14/02/2023 

Kwa rafiki Musa, 

Pokea salamu nyingi kutoka kwangu na marafiki zangu. Natumai u mzima. Nakuandikia barua hii kukujulisha kwamba mjomba Kioko amepata nafuu. Daktari amemshauri ale chakula chenye lishe bora ili mwili wake upate nguvu. Wajulishe wazazi wako habari hii njema. Kwaheri ya kuonana. Wasalimie ndugu zako Sankare na Bosco. 

Wako umpendaye,
Kisa Hadija.

 1. Nani mwandishi wa barua hii? 
  1. Musa
  2. Kisa Hadija
  3. Sankare
  4. Kioko
 2. Barua hii ina anwani ngapi?
  1. Moja.
  2. Nne
  3. Tatu.
  4. Mbili 

INSHA 

Andika insha ya kuhusisimua kuhusu

SAFARI YA MJINI. 

MARKING SCHEME

 1. A
 2. C
 3. B
 4. D
 5. A
 6. B
 7. D
 8. C
 9. D
 10. C
 11. B
 12. D
 13. C
 14. D
 15. C
 16. C
 17. B
 18. D
 19. B
 20. C
 21. D
 22. C
 23. B
 24. D
 25. B
 26. B
 27. D
 28. A
 29. B
 30. D
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Grade 5 Opener Exams Term 1 2023 Set 6.


Tap Here to Download for 30/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students