Displaying items by tag: Shughuli za Kiswahili

Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswall -

(Mwalimu na wanafunzi wamo darasani wakijadiliana kuhusu wanyama na umuhimu wao.)
Mwalimu:   Haya wanafunzi wangu wakati ule mwingine niliwaeleza kuwa kunavyo vikundi viwili vya wanyama.
Tobi:           Naam, na kumbuka jana baba yangu aliniambia kuwa wanyama wengine huishi na wanadamu nyumbani huku wengine wakiishi misituni. Mwalimu:   Hakika. Wanaoishi na wanadamu nyumbani huitwa wanyamahowa ilhali wanaoishi misituni ndio wanyamapori. Wengi wa wanyamapori                         huhifadhiwa katika mbuga za wanyama.
Huna:         Nawapenda wanyama hawa kwa kuwa wao hutusaidia. Ng'ombe, mbuzi na ngamia hutupa nyama na maziwa, nguruwe hutupa nyama                         nao kondoo hutupa nyama na manyoya.
Tim:            Naam, tena baadhi ya wanyamahowa hufugwa kwa ajili ya huduma. Mbwa ni mlinzi mizuri wa nyumbani, punda hutusaidia kukokota                             mikokoteni yenye mizigo nao paka huwakamata na kuwala panya waharibifu.
Mwalimu:    Kwa upande mwingine, wanyamapori huwavutia watalii ambao huitembelea nchi yetu. Wanapowaona, wao hulipa pesa za kigeni                                  ambazo hutumika kuijenga nchi. Kwa hivyo, wanyama wote wana umuhimu mkubwa kwetu.

  1. Kulingana na mazungumzo uliyoyasoma, wanyama huweza kugawanywa katika
    1. waishio na wasioishi.
    2. wanyamapori na wanyamahowa.
    3. vikundi vinne.
    4. wale wa asili na wale wa kigeni.
  2. Wanyama wasioishi na wanadamu nyumbani
    1. huitwa wanyamahowa.
    2. butusaidia katika shughuli za nyumbani.
    3. huishi mbugani.
    4. hutupa vyakula murua.
  3. Watalii wanapoitembelea nchi yetu, wao
    1. hulipa pesa za kigeni.
    2. hulipwa pesa za kigeni.
    3. hurudi na wanyama wetu katika nchi
    4. huja na wanyama kutoka katika nchi zao.
  4. Ni kundi gani la wanyama hutupa vyakula vya aina moja?
    1. Paka, mbwa na punda.
    2. Kondoo, nguruwe na mbuzi.
    3. Ngamia, mbuzi na paka.
    4. Mbuzi, ngamia na ng'ombe.
  5. Kulingana na mwalimu, umuhimu mkuu wa wanyamapori ni kwamba wao
    1. huwavutia watalii wa humu nchini.
    2. huiwezesha nchi yetu kupata pesa za kigeni.
    3. huwa walinzi wazuri wa nyumbani.
    4. hutusaidia kukokota mikokoteni.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 6 hadi 8.

Hapo zamani za kale, wanyama wote waliishi msituni. Walifanya kazi zao pamoja ili wapate chakula cha kuwatosha. Chakula kilichopatikana kiligawanywa kwa usawa miongoni mwao. Kila siku, walirauka kwenda shambani. Mbwa, Fisi na Simba walienda kuwawinda ndege ambao baadaye waliwaleta na kuwagawia wenzao.

Paka alikuwa mvivu asiyependa kufanya kazi. Hakutaka kuchafuka. Alishinda siku nzima akiisafisha miguu yake kisha baadaye kwenda kula. Kuona hivi, wanyama wale wengine wakakasirika sana. Waliamua kuficha chakula chote. Hata hivyo, Paka alinyemelea na kuingia katika ghala polepole akala chakula chote. Wanyama waliamua kumkamata Paka huyo mvivu. Walimwambia Mbwa awe mlinzi wa ghala. Paka alipokuja, mbwa alibweka kwa sauti. Wanyama wote waliamka na kumfukuza Paka. Paka aliamua kwenda kwa binadamu kuishi. Aliahidi kuwashika panya. Wakawa marafiki.

  1. Wanyama hawa walipata chakula chao kwa
    1. kufanya kazi pamoja kwa bidii.
    2. kuwaibia wanyama wengine.
    3. kuwawinda wanyama wadogo. 
    4. kuishi pamoja kwa amani.
  2. Wanyama wale wengine walimkasirikia Paka kwa sababu
    1. alikila chakula chote ghalani. 
    2. hakufanya kazi kama wao.
    3. aliiba chakula kutoka ghalani. 
    4. aliwasumbua wenzake.
  3. Je, Mbwa alifanya nini Paka alipoenda katika ghala?
    1. Alibweka kwa sauti.
    2. Aliwaita wanyama wale wengine. 
    3. Aliwakamata panya.
    4. Alimfukuza paka.
  4. Paka alimwahidi nini mwanadamu?
    1. Kuwa rafiki yake mkubwa.
    2. Kuwakamata ndege.
    3. Kufanya kazi shambani.
    4. Kuwashika panya.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 10 hadi 12.  

Ilikuwa siku ya Jumamosi karibu saa tano hivi asubuhi. Pendo, kaka yake Ali na mama yao walianza safari kuelekea katika soko la kijijini mwao, soko la Malimengi. Soko hilo lilikuwa karibu na uwanja wa ndege. Ilikuwa ndiyo Juniamosi ya kwanza tangu shule zilipofungwa. Siku hiyo, walipaswa kununua bidhaa kama vile sukari, mchele, mafuta na nguo za kuwapelekea nyanya na babu yao walioishi huko Konoike.

Walipofika sokoni, waliwapata watu wengi sana. Kwa sababu ulikuwa nisimu wa sherehe za Idi, mavazi yalikuwa ya bei ghali sana. Iliwabidi wanunue mchele, sukari na mafuta pekee. Nguo wangenunua kwingine.

  1. Karibu saa tano hivi asubuhi,
    1. safari ya kuenda kijijini ilianza.
    2. safari ya kwenda sokoni ilianza.
    3. kina Pendo walifika nyumbani.
    4. shule zilifungwa.
  2. Kina Pendo walipaswa kununua
    1. nguo, sukari na mchele.
    2. mafuta, sukari na mchele.
    3. mafuta, sukari, nguo na mchele.
    4. nguo, sukari na mafuta.
  3. Safari hii iliandaliwa katika msimu wa sherehe gani?
    1. Krismasi
    2. Pasaka
    3. Jumamosi
    4. Idi

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 13 hadi 15.   

Asubuhi hiyo, niliamka nikiwa nimechelewa. Nilijua kuwa rafiki zangu, Rama na Veli walikuwa wakiningoja katika stani. Siku zote, tulishindania kiti cha mbele katika basi letu la shule. Mara nyingi nilikuwa wa kwanza katika stani. Kwa hivyo mara nyingi nilikiwahi kiti hicho. Tuliahidiana kuwa yeyote ambaye alikiwahi kiti hicho cha mbele angegawiwa vipande vya mikate na wenzake waliochelewa wakati wa mapumziko. Upesi, niliunawa uso wangu na kuvalia sare zangu nikatandika kitanda changu na kukisafisha chumba changu. Baadaye, nilielekea sebuleni kupata kiamshakinywa. Niliteremsha chai kwa sambusa upesi na kuondoka.

  1. Ni nini ambacho mwandishi alijua kuwahusu Rama na Veli? Kuwa
    1. walikuwa katika basi la shule. 
    2. walikuwa wakimngoja.
    3. wangekuwa wa kwanza kukiwahi kiti cha mbele.
    4. tayari walikuwa wamefika shuleni.
  2. Ni nini ambacho mwandishi na wenzake walikishindania?
    1. Kufika shuleni mapema. 
    2. Kula vipande vya mikate. 
    3. Kuabiri basi la shule.
    4. Kukiwahi kiti cha mbele.
  3. Kabla ya msemaji kupata kiamshakinywa, alifanya haya yote ila
    1. kukiwahi kiti cha mbele. 
    2. kukisafisha chumba chake. 
    3. kukitandika kitanda chake. 
    4. kuunawa uso wake.

Soma kifungu kifuatacho. Chagua Jibu lifaalo zaldi kati ya yale uliyopewa.

Maji ni uhai. Bila maji, ___16___ binadamu hata mmoja ambaye anaweza ___17___. Binadamu ___18___ huyategemea maji moja kwa moja. Maji hayo hutumika katika shughuli mbalimbali kama vile kunywa, kupikia, kuoshea vyombo na shughuli nyingine za nyumbani. ___19___ inapokosekana, maji hutumika kunyunyizia ___20___. Maji yatumiwayo kunyunyizia huweza kupatikana mitoni, mabwawani na maziwani.

   A   B   C   D 
 16.   hakuna   kunaye   kuna   wapo 
 17.  kuisha  kufa  kuishi   kufariki 
 18.  sote  wote  zote  yote
 19.  Mvua  Maji  Mimea   Mawingu 
 20.  shamba   wafu  mvua  


Katika swali la 21-30, jibu swali kulingana na maagizo uliyopewa.

  1. Ni shughuli gani hapa haipatikani nyumbani?
    1. Kupalilia mimea.
    2. Kusafisha nyumba.
    3. Kufua nguo.
    4. Kuosha vyombo.
  2. Katika sentensi Mbwa mdogo amebeba mfupa katika meno yake, nomino ni zipi?
    1. Mdogo, mfupa, yake
    2. Mbwa, mfupa, meno
    3. Mdogo, amebeba, katika
    4. Yake, katika, mfupa
  3. Tisini na sita ni
    1. 69
    2. 66
    3. 99
    4. 96
  4. Ni gani hapa ni maelezo sahihi kuhusu matumizi ya kikomo katika sentensi?
    1. Hutumiwa mwanzoni mwa sentensi.
    2. Huweza kuwa katikati ya sentensi. 
    3. Hutumiwa mwishoni mwa sentensi.
    4. Haiwezi kutumiwa sentensi ikianza kwa herufi kubwa.
  5. Ni yupi hapa ameambatanishwa na kazi yake kwa usahihi?
    1. Dereva - hutengeneza magari yaliyoharibika.
    2. Mpishi - hukuza mimea na kuwafuga wanyama
    3. Mwalimu - huwalea watoto majumbani mwao.
    4. Seremala - hutengeneza vifaa kwa kutumia mbao.
  6. Je, ni mwezi gani huwa baina ya Julai na Septemba?
    1. Agosti
    2. Oktoba
    3. Juni
    4. Mei
  7. Nywele huota ___________________ kichwa.
    1. ndani ya
    2. katikati ya
    3. juu ya
    4. chini ya
  8. Tumia kihusishi bora zaidi kukamilisha sentensi hii.
    Mti mrefu uko _______________________ darasa letu.
    1. chini ya
    2. nje ya
    3. ndani ya
    4. juu ya
      2
  9. Ili kuwaangamiza wadudu waharibifu shambani, wakulima 
    1. hupalilia.
    2. huvuna.
    3. hunyunyiza maji.
    4. hupiga dawa.
  10. Ni sentensi ipi iliyo katika nafsi ya tatu?
    1. Mwanaisha ataimba jioni.
    2. Mimi niliimba jioni.
    3. Nyinyi msiimbe jioni.
    4. Sisi hatutaki kuimba jioni.

MARKING SCHEME

  1. B
  2. C
  3. A
  4. D
  5. B
  6. A
  7. D
  8. A
  9. D
  10. B
  11. C
  12. D
  13. B
  14. D
  15. A
  16. A
  17. C
  18. B
  19. A
  20. D
  21. A
  22. B
  23. D
  24. C
  25. D
  26. A
  27. C
  28. B
  29. D
  30. A
  • Kusikiliza na Kuzungumza
  • Kusoma na Kujibu Maswali
  • Sarufi

Maswali

Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali 1-5.
(Mwajuma na Juma wamekutana kijijini wanakoishi. Wanazungumza kuhusu machache yanayowahusu.)
Juma: Mwajuma, we, Mwajuma, Jamani hata hunisikii. Masikio ulipeleka wapi? (huku akitabasamu).
Mwajuma: Ah Jamani, pole sana Juma. Upepo ni mkali ndiyo maana sikukusikia. Hali yako vipi lakini?
Juma:  Hali yangu njema dada. Je wewe? Natumai kwema.
Mwajuma: (Kwa huzuni) Ndiyo ila si sana. Kabla tu ya kuuvuka mwaka, mlezi wangu alipata ajali na kuumia vibaya miguu. Sasa yuko hospitalini.
Juma: Pole sana Mwajuma. Maskini Bwana Shani aliumia akiwa wapi?
Mwajuma: Alikuwa akitoka dukani alipogongwa na pikipiki kisha mwendeshaji akajiendea zake. (Kwa hasira) Afadhali angesimama amsaidie.
Juma: Usijali Mwajuma. Nitakupa msaada wowote ambao utahitaji kwa kuwa wewe ni rafiki yangu. (Muda unapita) Na kuhusu shuleni?
Mwajuma: (Kwa furaha) Nafurahi kuwa sasa tumejiunga na gredi ya nne. Nilitamani sana nifike katika darasa hili.
Juma: Hata mimi vivyo hivyo (wote wanaonyesha nyuso za furaha) Dada Mwajuma, hebu twende tukamtazame mlezi wako hospitalini (wanaondoka).

  1. Kulingana na Mwajuma, ni kwa nini hakumsikia Juma alipomwita?
    1. Kulikuwa na jua kali.
    2. Juma alimwita kwa sauti ya chini.
    3. Kulikuwa na upepo mkali.
    4. Mwajuma alikuwa na huzuni nyingi.
  2. Hali ya Mwajuma haikuwa njema sana kwa sababu
    1. alikuwa amepata ajali.
    2. mzazi wake alikuwa mgonjwa.
    3. Juma alikuwa amepata ajali.
    4. mlezi wake alikuwa amepata ajali.
  3. Kulingana na mazungumzo haya, Bwana Shani alikuwa
    1. mlezi wa Mwajuma.
    2. mzazi wa Juma.
    3. mlezi wa Juma.
    4. mzazi wa Mwajuma.
  4. Bwana Shani alipata ajali wapi?
    1. Alipokuwa akielekea shuleni.
    2. Baada ya kutoka sokoni.
    3. Alipokuwa akitoka dukani.
    4. Alipokuwa pale dukani.
  5. Kilichowafurahisha Juma na Mwajuma ni
    1. kuumia kwa mlezi wa Mwajuma.
    2. kuondoka kwa mwenye pikipiki.
    3. kujiunga na gredi ya tatu.
    4. wawili hao kujiunga na gredi ya nne. 

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 6 hadi 8.
Zamani kidogo, aliishi mfalme aliyekuwa akiitwa Kinara, kumaanisha kiongozi wa wengi. Alikuwa jasiri kweli kweli. Baba yake alimwonea fahari kwa sababu ya ujasiri wake. Hakutaka mwana wake apatwe na tatizo lolote. Alimkanya mwanawe asiende vitani lakini mwanawe hakumsikiliza. Aliwashambulia majirani wanyonge katika jamii zao na kuwapokonya mashamba. Baba yake aliogopa kuwa huenda angeuawa akamwambia kuwa, badala ya kuwaua na majirani hao, ni vyema zaidi ashirikiane nao. Baadaye, Kinara alimsikiliza baba yake na kuishi kwa amani na wenzake.

  1. Kulingana na taarifa hii, jina Kinara lilimaanisha nini?
    1. Mfalme mwenye kuheshimiwa.
    2. Kiongozi wa wengi.
    3. Kiongozi mnyonge.
    4. Mfalme anayewanyanyasa wengine.
  2. Ni kwa nini baba wa Kinara alikuwa na fahari kuu kwake?
    1. Alikuwa jasiri kweli kweli.
    2. Aliwanyanganya wengine inashamba.
    3. Aliwatesa watumishi wake.
    4. Alikuwa na nguvu nyingi.
  3. Ni kwa nini baba wa kinara hakutaka mwana wake aende vitani?
    1. Mwanawe alikuwa mfalme mnyonge sana.
    2. Wanakijiji walikuwa na nguvu zaidi ya mwana wake.
    3. hakutaka mwana wake apatwe na tatizo lolote.
    4. hakukuwa na silaha za kutosha.
  4. Mwisho kabisa, kinara aliamua
    1. kuwashambulia wanakijiji.
    2. kumsikiliza baba yake.
    3. kuwavamia majirani zake.
    4. kukataa mawaidha ya baba yake. 

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 10 hadi 12.
Katika ukingo wa mbali wa msitu wa Suramawe, aliishi sungura, fisi na mbwa wanyama hawa walikuwa marafiki wa kufa kuzikana au wa chanda na pete. Wanyama wengine walishangazwa na kuwa walikuwa marafiki hata ingawa walikuwa tofauti kabisa. Siku moja, fisi alialikwa shereheni na wazazi wa mke wake kama marafiki wazuri, sungura na mbwa walikubali kumpeleka shereheni. Walipofika, walipokelewa kwa furaha tele. Baada ya kupokelewa, waliandaliwa vyakula murua na vinywaji vya kudondosha mate. Wote walikula na kunywa kwa furaha hadi wakatosheka.

  1. Ni wanyama wangapi waliokuwa wakiishi katika msitu wa suramawe?
    1. Watatu
    2. Wanne
    3. Wawili
    4. Watano
  2. Wanyama wale wengine walishangazwa na nini kuhusiana na marafiki wale?
    1. Walikuwa wakipendana hata kama walifanana.
    2. walikuwa maadui hata kama walifanana.
    3. walipendana hata kama walikuwa tofauti.
    4. walikuwa inaadui ambao walikuwa tofauti.
  3. Wageni wa fisi walipokelewa vipi?
    1. Waliandaliwa vyakula pamoja na vinywaji.
    2. walipewa mahali pazuri pa kulala.
    3. walipewa maji baridi ili wazime kiu.
    4. walipewa maji moto ili waoge kwa furaha.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 13 hadi 15.
Kismati aliangalia saa yake ya kiwiko, nayo ikamjulisha kuwa muda wa kuenda nyumbani ulikuwa umefika. Ijumaa hiyo, alitarajia wageni kutoka kaunti ya Jipemoyo. Ilimbidi aabiri basi ili afike nyumbani haraka. Basi lililoitwa Haraka lilitokeza ghafla. Alipomwashiria dereva alisimamisha, dereva alitii na kuliegesha kwenye stani. Alipoingia, Mwendo ukaanza kuelekea Bwagamoyo, alikoishi Kismati. Kondakta alipomtaka Kismati kulipa nauli, Kismati aligundua kuwa kibeti chake hakikuwa mfukoni. Maskini Kismati!

  1. Baada ya kuangalia saa yake, Kismati alitakiwa kwenda wapi?
    1. Nyumbani. 
    2. Kazini
    3. Basini
    4. Stanini
  2. Je, kisa hiki kilitokea lini?
    1. Jumapili
    2. Ijumaa
    3. Alhamisi
    4. Jumanne
  3. Inawezekana kuwa kibeti cha Kismati
    1. kilikuwa mbali
    2. hakikuwa mbali.
    3. kilikuwa mfukoni mwake.
    4. kilikuwa kimeibwa. 

Soma kifungu kifuatacho. Chagua Jibu lifoglo zaidi kati ve vale uliyopewa.

Panya ni .........16......... mdogo na mharibifu. Yeye huishi........17.........ya shimo. Hutoka shimoni wakati ana njaa. Yeye ........18......... mahindi, karatasi, vitabu na nguo. Huwasumbua watu sana lakini watu wametafuta njia za kumnasa na........19.........Wengine hutumia sumu na wengine huurmia ........20.........

  1.                                    
    1. ndege
    2. mtu
    3. mnyama
    4. nyama
  2.                    
    1. nje
    2. ndani
    3. juu
    4. mbele
  3.              
    1. hataki
    2. hali
    3. hapendi
    4. hula
  4.                  
    1. kumwua
    2. kumpenda
    3. kumshtaki
    4. kumla
  5.                  
    1. mashimo
    2. mahindi
    3. mitego
    4. chakula 

Katika swali la 21-30. jibu swall kulingana na maagizo uliyopewa.

  1. Ni chombo gani kati ya hivi hupatikana sokoni?
    1. Nyundo
    2. Rejesta
    3. Ubao
    4. Ratili
  2. Tumia kihusishi bora zaidi kukamilishia sentensi ifuatayo:
    Ndege mkubwa ametua...............................mti.
    1. ndani ya
    2. juu ya
    3. miongoni mwa
    4. katikati ya
  3. Wanyama walioshiba walilala
    ...................................mti kwenye kivuli.
    1. chini ya
    2. kati ya
    3. katikati ya
    4. juu ya
  4. ............................ni ndege wa nyumbani.
    1. Mwewe
    2. Heroe
    3. Korongo
    4. Bata
  5. Chagua sentensi iliyo na kikomo.
    1. Je, mliwaona walimu wangapi?
    2. Lo! Kumbe alikuwa mwizi!
    3. Leo ni siku ya Jumapili.
    4. Wazazi wameanza mkutano
  6. Mtu anayetengeneza vifaa vya mbao huitwaje?
    1. Dereva.
    2. Seremala.
    3. Fundi.
    4. Askari.
  7. Chagua sentensi iliyo katika wakati ujao.
    1. Wanyamapori watalindwa vyema.
    2. Mwalimu alisahihisha makosa yangu.
    3. Mtoto anapenda kunywa maziwa.
    4. Paka wetu alimnasa panya mnono.
  8. Mwezi wa Julai hufuatwa na mwezi gani?
    1. Septemba.
    2. Juni
    3. Agosti
    4. Mei
  9. 79 kwa maneno ni
    1. tisini na saba.
    2. tisini na nne.
    3. sabini na sita.
    4. sabini na tisa.
  10. Je, ni sentensi gani iliyo katika nafsi ya kwanza?
    1. Alisema atamletea miwa.
    2. Wageni wao wote walikwa warefu.
    3. Nilichora picha nzuri ubaoni.
    4. Umeamua kufanya bidii.

Majibu

swa

 

Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali 1 hadi 5.

ZOEZI: 1

KUSOMA KWA UFAHAMU

Swali la 1 hadi la 5.
Sasha:  (Akimtazama) Sabalkheri Kiki!
Kiki :     (kwa furaha) Aheri rafiki yangu!
Sasha:  Nina furaha kubwa kujiunga na gredi ya tano.
Kiki :       Mimi pia sijawahi kuwa na furaha kama niliyo nayo.
Sasha :  Tutafanya nini ili tuwe wanafunzi bora mwaka huu?
Kiki :       (akijikuna kichwa) Ni lazima tuwe na nidhamu. Unakumbuka mwaka jana....
Sasha ;  (akimkatiza) Mwaka jana tuliwasumbua walimu sana kwa tabia zetu mbaya.
Kiki :       Huu ukiwa mwaka mpya lazima tutabadilisha.
Sasha :   Naam! Tutakuwa wavulana wenye adabu.
Kiki :        Ndiyo sahibu. Tutakuwa tukikamilisha kazi, kumsikiliza mwalimu, kutulia darasani.
Sasha :   (Akimdakiza) na kuwaheshimu wenzetu.
Kiki :       Isitoshe ni vyema kutunza mazingira yetu darasani na nje ya darasa.
Sasha :   (Akimkazia macho) Unakumbuka ulivyokuwa ukitupa taka ovyo mwaka jana!
Kiki ;       Hayo yote yamepita. Nimeamua kuwa mwanafunzi bora zaidi shuleni.
Sasha :   Mungu atakujalia.
Kiki :       Asante sana. Sasa tujiandae kwa kipindi cha kwanza.
Sasha :  Tutazungumza zaidi wakati wa breki.

  1. Mazungumzo uliyoyasoma yalifanyika wakati gani?
    A. jioni                         B. Adhuhuri                  C. Asubuhi                 D. Magharibi
  2. Sasha na Kiki walikuwa darasa gani mwaka jana?
    A. Gredi ya tatu         B. Gredi ya sita 
    C. Gredi ya nne          D. hatujaambiwa
  3. Si kweli kusema kuwa Sasha na Kiki
    A. ni wa jinsia tofauti.                                         B. ni wavulana.
    C. hawakuwa na maadili mwaka jana.               D. wameamua kubadilika,
  4. Ni maadili gani hayajatajwa katika mazungumzo haya?
    A. Kutunza mazingira                                        B. Kutulia darasani
    C. Kuwaheshimu wengine                                 D. Kusoma kwa bidii
  5. Neno rafiki lina maana sawa na
    A. jirani                          B. adui                          C. sahibu                    D. jinsia

Swali la 6 hadi la 9

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.

Sitawahi kuusahau muhula wa tatu nikiwa katika Gredi ya nne. Shule yetu ya Waridi ilituandalia safari ya kuzuru mbuga ya wanyama ya Masai Mara. Mimi na wanafunzi wenzangu tulikuwa na furaha isiyo na kifani.
Mbugani, tuliwaona wanyama wa kila aina. Tuliwaona wanyama wala nyasi kama vile: Nyati, ndovu, kifaru, twiga na swara. Isitoshe tulibahatika kuwaona wanyama walao nyama mathalani simba na chui. Licha ya hayo kulikuwa na fisi na tai ambao hula mizoga. Tulifurahia sana kuwaona kongoni wakivuka Mto Mara. Kongoni ni kivutio kikuu cha watalii katika mbuga hii.
Mwelekezi wa ziara yetu mbugani alitueleza kuhusu faida za wanyama pori kwa taifa letu. Kwa mfano, wanyama wa pori huvutia watalii wengi nchini. Watalii wakija, huiletea nchi yetu pesa za kigeni zinazosaidia kukuza uchumi wetu. Ziara hii ilitufunza kuwa, kutembea kwingi ni kuona mengi.

  1. Safari iliyosimuliwa ilifanyika muhula gani?
    1. Muhula wa mwisho wa mwaka               
    2. Muhula wa pili
    3. Muhula wa kwanza                                 
    4. Muhula wa kufungua mwaka
  2. Kati ya wanyama hawa ni gani hajaambatanishwa na chakula chake?
    1. Nyati-Nyasi                                 
    2. Simba-Nyama                             
    3. Tai- Mizoga                         
    4. Chui- Nyasi
  3. Je, ni mnyama gani ametajwa kama kivutio kikuu cha watalii nchini?
    1. Twiga                                     
    2. Kongoni                                                 
    3. Ndovu                               
    4. Kifaru 
  4. Faida ya watalii kwa nchi yetu ni gani?
    1. Kuwaona wanyama.                                                 
    2. Kufurahisha wanafunzi.
    3. Kusaidia kukuza uchumi.                                           
    4. Kuzuru mbuga ya wanyama.

Swali la 10 hadi la 12

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.

Kwanza ni mwanafunzi anayependa kutumia wakati wake vizuri. Kila siku katika likizo yake alikuwa na ratiba. Hakupenda kuupoteza wakati wake hata kidogo. Ifuatayo ni ratiba ya siku yake moja

Asubuhi    Adhuhuri    Magharibi    Usiku nchanga  

 Kula 

kiamshakinywa

kulachamcha   kusoma  vitabu vya hadithi   kutazama habari za jion  
 kufanya kazi ya ziada

 kutazama habari

za adhuhuri kwenye runinga

  kucheza kandanda   kula chajio 
 kucheza    kupumzika   kuoga    kwenda kulala 
  1. Kinachomsaidia kwanza kutumia wakati wake vizuri ni.
    1. ratiba               
    2. saa                 
    3. wakati                     
    4. siku
  2. Ni shughuli gani inayopatikana katika kila kipindi?
    1. Kucheza         
    2. Kusoma           
    3. Kula                         
    4. Kutazama habari
  3. Kwanza hutunza usafi wa mwili wake wakati gani?
    1. Asubuhi           
    2. Usiku mchanga       
    3. Adhuhuri             
    4. Magharibi

Swali la 13 hadi la 15

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.

Kijiji cha Busara kina wakazi wengi sana. Wakazi hawa walifurahia utulivu kwa muda mrefu. Hata hivyo, likizo iliyopita wanakijiji walilalamikia mienendo mibaya ya baadhi ya vijana. Kuna vijana ambao walivalia mavazi yasiyofaa. Kuna wale ambao walianza kukataa kwenda shuleni. Wengine hawakutii watu wazima. Bi. Adili ni mmoja wa wanakijiji hiki. Alikuwa na shirika lake kwa jina, Inua Vijana. Kupitia kwa shirika hili, alitumia redio kuwaelimisha vijana kuhusu mienendo mizuri. Aliandaa siku ya michezo kijijini. Vikundi mbalimbali vilishiriki. Baada ya michezo hii, washindi walituzwa. Bi. Adili alitumia nafasi hii kuwashauri. Bidii ya Bi. Adili ilifaulu. Vijana waliokuwa wamepotoka walibadilika, wanakijiji walifurahi. Walitambua juhudi za Bi.Adili. Waliandaa sherehe kubwa walimtuza Bi. Adili kwa juhudi zake. Hakika, mcheza kwao hutuzwa.

  1. Wanakijiji cha Busara walifurahia             ,kwa muda mrefu.
    1. fujo
    2. hali ya amani
    3. vijana
    4. Bi. Adili
  2. Vijana wa kijiji cha Busara walibadilika vipi baada ya kushauriwa?
    1. Walivalia mavazi yasiyofaa
    2. Walikataa kwenda shuleni
    3. Walianza kuwatii watu wazima
    4. Walikosa heshima
  3.  Waliandaa sherehe inamaanisha:
    1. Walitayarisha sherehe
    2. Walisafiri shereheni
    3. Walizuru sherehe
    4. Walimaliza sherehe

ZOEZI 2:SARUFI

Soma kifungu kifuatacho. Kina nafasi 16 hadi 20. Umepewa majibu manne hapo. Chagua jibu lifaalo Zaidi kati ya yale uliyopewa.

Mchezo      16          kandanda hupendwa na watu      17          . Kila mtu  huwa na       18             kumi na      19         Timu ambayo hushinda ni ile iliyofunga      20         mengi.

   A   B   C   D 
 16.   wa   ya   cha   la 
 17.  mingi   vingi   wengi   nyingi 
 18.  waimbaji   waigizaji   mashabiki   wachezaji 
 19.  moja  mmoja   wamoja   kimoja 
 20  mabao  alama   maksi   mikwaju 
  1. Tazama picha hizi kisha ujibu swali.
    G5TT1kswms21
    Ni jibu gani lililoambatanisha nomino za picha na ngeli zake?
          Ng'ombe (a)                      Kiti (b)
    1. KI-VI                                 A-WA
    2. A-WA                                  U-I
    3. I-ZI                                     KI-VI
    4. A-WA                                 KI-VI
  2. Juma amempata mwalimu wake majilisini asubuhi akamwamkua, "Shikamoo mwalimu." Je. mwalimu alimjibu vipi?
    1. Binuru
    2. Marahaba
    3. Salama
    4. Aleikum salaam
  3. Kati ya maneno haya ni gani lililo katika hali ya ukubwa.
    1. Mto
    2. Jito
    3. Kijito
    4. Mito
  4. Tazama picha hii kisha utumie kihusishi mwafaka.
    G5TT1kswms24
    Mpira uko                 Meza.
    1. juu ya
    2. kando ya
    3. chini ya
    4. mbele ya
  5. Chagua kundi ambalo lina vitenzi pekee.
    1. Nyumba, kiti, simul
    2. Chora, imba, lala
    3. Safi, kubwa, dogo
    4. Polepole, haraka, sana
  6. Badilisha sentensi hii katika wingi: Mgeni amefika kwangu leo.
    1. Wageni wamefika kwetu leo.
    2. Wageni wamefika kwangu leo
    3. Mwenyeji amefika kwetu leo.
    4. Mgeni hajafika kwangu leo.
  7. Chagua jibu sahihi. Rafiki yangu amekuwa
    1. mfupi
    2. mnene
    3. mjanja
    4. mrefu
  8. Chagua jibu linalofaa kujaza nafasi.
    Lila ameosha nguo. Nguo              .na Lila.
    1.  zimeoshewa
    2.  zimeoshwa
    3.  zimeoshea
    4. zimeosheka
  9. Kanusha sentensi hii:
    Ninasoma kitabu sasa.
    1. Sisomi kitabu sasa.
    2. Hatusomi kitabu sasa
    3. Sitasoma kitabu sasa.
    4. Sijasoma kitabu sasa.
  10. Umefika katika dukakuu. Kabla hujaingia, mlinzi amekukumbusha uvae barakoa, utamwambiaje?
    1. Karibu
    2. Asante
    3. Hongera
    4. Salimini

INSHA

Kuandika(Alama 10)

Umepewa dakika 40 kuandika insha yako. Andika insha kuhusu mada ifuatayo:

SIKUKUU YA KUPENDEZA

MWONGOZO KISWAHILI

  1.  C
  2. C
  3. A
  4. D
  5. C
  6. A
  7. D
  8. B
  9. C
  10. C
  11. C
  12.  D
  13. B
  14. C
  15. A
  16. A
  17. C
  18. D
  19. B
  20. A
  21. D
  22. B
  23. B
  24. C
  25. B
  26. A
  27. C
  28. B
  29. A
  30. B

MASWALI

Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali 1-5.

(Ni katika soko la Marikiti ambapo mwuzaji anazungumza na mteja wake)
Mteja:       Umeshindaje kaka? Naona unazo mboga zinazovutia kweli. Bei gani fungu hili? (akilishika) 
Mwuzaji:   Vyema sana mwenzangu. Hizi nimezivuna kutoka shambani mwangu leo leo. Hujaangalia nyanya, pilipili, vitunguu na karoti.                         Wazionaje mboga za leo? (Akitabasamu) siku zote, bei hutegemea mapatano.
Mteja:       He-he-he! Leo wateja wote watapitia hapa kibandani pako. Haya naomba uniuzie mafungu mawili ya sukumawiki na...
Mwuzaji:   (Akimkatiza) Samahani dada. Natumai unajua bei ya mwaka huu mpya. Fungu moja la sukumawiki sasa ni shilingi ishirini.
Mteja:       Gharama ya maisha nayo! Niuzie mafungu mawili ya sukumawiki, fungu moja la nyanya na vitunguu fungu moja.
Muuzaji:    Karoti leo?
Mteja:       Bado zipo. Nilinunua nyingi. Vyote ni shilingi ngapi?
Mwuzaji:   (Muda unapita) Naam, vyote ni shilingi themanini.

  1. Mwuzaji katika mazungumzo haya alikuwa akiuza 
    1. mboga.
    2. matunda.
    3. miwa.
    4. mahindi.
  2. Mteja alinunua mafungu mangapi ya sukumawiki?
    1. Moja.
    2. Matatu.
    3. Mawili.
    4. Manne.
  3. Bei ya mwaka huo mpya ilikuwa gani kwa fungu moja la mboga? Shilingi
    1. themanini.
    2. ishirini.
    3. thelathini.
    4. arobaini.
  4. Kulingana na mazungumzo haya, mwuzaji pia alikuwa
    1. mteja.
    2. mnunuzi.
    3. mpishi.
    4. mkulima.
  5. Mteja katika mazungumzo haya alitumia pesa ngapi kwa jumla?
    Shilingi
    1. thelathini.
    2. ishirini.
    3. themanini
    4. hamsini

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 6 hadi 9.

Hapo zamani za kale, palikuwa na sungura na mbwa. Wanyama hao walikuwa marafiki wa kufa kuzikana. Naam, walipendana kama ulimi na mate. Wanyama hao walipokuwa makaoni mwao, mbwa alimwambia sungura kuwa yeye alihisi njaa sana. Aliendelea kumwambia kuwa angependa kumla yeye kwa kuwa sungura huwa na nyama tamu. Kusikia vile, sungura alijifanya hakujali ingawa alishtuka. Mbwa alipoangalia kando, sungura alikimbia na kujificha kichakani.

  1. Wanyama waliotajwa ni
    1. mbweha na sungura.
    2. mbwa na kinyonga.
    3. sungura na mbwa.
    4. mbweha na kinyonga.
  2. Ni kweli kusema kuwa mwanzoni, wanyama hao wawili
    1. walisaidiana sana.
    2. hawakupendana sana.
    3. walichukiana sana.
    4. walikuwa na ugomvi.
  3. Ni kweli kusema kuwa mbwa alikuwa
    1. rafiki mzuri.
    2. rafiki mbaya.
    3. ameshiba sana.
    4. mnyama mzuri sana.
  4. Sungura alitoroka wakati mbwa alikuwa
    1. ameingia kichakani.
    2. amelala.
    3. ameangalia kando.
    4. amekaa maskanini mwake.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 10 hadi 12   

Upanzi wa miti ni jambo jema sana. Mwalimu wetu wa Sayansi alituclcza kwamba miti hutusaidia kwa namna tofauti tofauti. Alisema kwamba bila miti, mazingira yetu hayawezi kuvutia bali yatachukiza mno. Mmomonyoko wa udongo nao utaenea kwa kasi sana na mwishowe, nchi yetu itakuwa jangwa, yaani ardhi kavu isiyo na mimea yoyote. Ingawa miti hutufaidi kwa njia nyingi, tukiukata mti mnaoja, tuipande mingine miwili au zaidi.

  1. Mwalimu wa kina mwandishi aliwaeleza kuwa miti
    1. huleta hasara kwa wale wanaoipanda.
    2. haina faida yoyote kwa mwanadamu.
    3. hutusaidia kwa njia mbali mbali..
    4. husababisha mmomonyoko wa udongo.
  2. Kulingana na ufahamu huu, mazingira yetu yatavutia ikiwa watu
    1. wataanza kukata miti.
    2. watakata miti bila kupanda mingine.
    3. wataacha kabisa kutumia miti.
    4. watapanda miti.
  3. Mwishoni mwa taarifa, tunashauriwa
    1. kupanda miti baada ya kuikata.
    2. kupanda miti miwili au zaidi kila siku.
    3. kuacha kutumia miti.
    4. kupanda mti mmoja baada ya kuukata mmoja.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 13 hadi 15.

Mzee Safari alikuwa amekula chumvi nyingi, yaani alikuwa amezeeka sana. Moja ya sifa zake kuu ilikuwa ni usimuliaji wa hadithi. Matamshi yake yalikuwa bora nayo sauti yake ilikuwa kama ya kinanda. Wakati wa jioni, wajukuu wake walimzingira ili kupata uhondo wa hadithi zake zisizo na mwisho. Mara nyingi hadithi zake zilihusu jinsi ambavyo watu wa kitambo waliishi. Wajukuu wake walizidi kufurahia kila siku kwa sababu hadithi za babu yao ziliwachangamsha na kuwarekebisha kitabia.

  1. Mtu anapokuwa amezeeka sana, tunasema amekula
    1. miaka mingi. 
    2. chumvi nyingi.
    3. umri mwingi.
    4. shida nyingi.
  2. Mzee Safari alijulikana sana kutokana na
    1. usimuliaji wa hadithi.
    2. uzee wake.
    3. sauti yake kama ya kinanda. 
    4. mawaidha yake.
  3. Mara nyingi hadithi za mzee Safari zilihusu
    1. watu wa kitambo.
    2. watoto wa siku hizi.
    3. wanyama wa kitambo.
    4. watoto.

Soma kifungu kifuatacho. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa. 

Nilipofika sokoni, nilienda moja kwa moja hadi kwenye___16___ cha kuuzia matunda. Nilichagua matunda matano yaliyonipendeza. Mara moja nilitia mkono ___17___ ili kuichomoa noti yangu na ___18___. Ole wangu! Sikuamini noti ya shilingi mia tano ___19___. Pesa zote za
mama nilikuwa nimezipoteza. Machozi yalinitiririka ___20___ nisijue la kusema wala la kufanya.

   A   B   C   D 
 16.   kikundi   kiwanja   kibanda   kijumba 
 17.  kichwani   ndani   mfukoni   polepole 
 18.  kulipa  kupewa   kulipwa   kuondoka 
 19.  ilikuwapo   haikuwapo   hazikuwapo   zilikuwapo 
 20.  kidevuni  mdomoni  makwapani  mashavuni 


Katika swali la 21-30, jibu swali kulingana na maagizo uliyopewa.   

  1. Katika sentensi :
    Kamba iliyopotea itapatikana leo,
    kielezi ni
    1. leo
    2. itapatikana
    3. iliyopotea
    4. kamba 
  2. Chagua orodha ya vitenzi pekee.
    1. Masomo, soma, kusoma
    2. Andika, kalamu, karatasi 
    3. Simama, keti, tembea
    4. Kunywa, meza, godoro.
  3. Kanusha sentensi ifuatayo kwa usahihi: 
    Wewe unaandika vizuri. Wewe
    1. huandika vizuri.
    2. unaandika vibaya.
    3. hukuandika vizuri.
    4. huandiki vizuri.
  4. Chagua sentensi iliyo katika wakati ujao.
    1. Wanafunzi walikuwa wakicheza.
    2. Paka anamkimbiza pinya.
    3. Walimu na wazazi wanazungumza afisini.
    4. Tutapokea zawadi zetu jioni.
  5. Kamilisha tashbihi.
    Bi Kenge ni mfupi kama
    1. ngazi.
    2. uyoga.
    3. msumari.
    4. nyundo.
  6. Ukubwa wa nomino mke ni
    1. jike.
    2. jimke
    3. mwanamke.
    4. janajike.
  7. Maneno ambayo hutoa maelezo zaidi kuhusu vitenzi huitwa
    1. vielezi.
    2. viwakilishi.
    3. vitanzandimi.
    4. vivumishi.
  8. Chagua neno lililo tofauti na mengine.
    1. Lakini.
    2. Oga
    3. Ingawa.
    4. Wala.
  9. Chagua mmea uliolinganishwa ipasavyo na tunda lake.
    1. Mpera - mipera
    2. Embe - maembe
    3. Mgomba - ndizi
    4. Mchungwa - parachichi
  10. Chagua nomino isiyo katika ngeli ya ki-vi.
    1. Kioo.
    2. Kiziwi
    3. Kiota.
    4. Kiazi.

MARKING SCHEME

  1. A
  2. C
  3. B
  4. D
  5. C
  6. C
  7. A
  8. B
  9. C
  10. C
  11. D
  12. A
  13. B
  14. A
  15. A
  16. C
  17. C
  18. A
  19. B
  20. D
  21. A
  22. C
  23. D
  24. D
  25. D
  26. A
  27. A
  28. B
  29. C
  30. B

QUESTIONS

SEHEMU 3: Ufahamu
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali
Vazi ni kitu kilichotengenezwa kwa kitambaa au ngozi ili kuvaliwa na binadamu. Kuna mavazi ya kiasili na mavazi ya kisasa. Mavazi ya kiasili ni kama vile shuka, kanzu na leso. Mavazi ya kisasa ni kama vile; suruali, tai, shati, rinda na koti.
Watu huvaa mavazi wakati wa baridi na joto. Joho huvaliwa wakati wa baridi. Fulana huvaliwa wakati wa joto.
Mavazi ni muhimu kwa binadamu. Mavazi kama vile chupi na fulana huficha uchi. Mavazi kama vile ovaroli huzuia uchafu mtu anapofanya kazi. Vilevile, mavazi huzuia baridi shadidi. Pia mavazi husaidia mtu kujikinga wakati wa hatari. Binadamu huvaa tai na suti ili kuonekana nadhifu. Mavazi ni muhimu katika maisha ya binadamu.

  1. Kati ya mavazi yafuatayo ni lipi si vazi la kisasa? 
    1. Leso
    2. Shati
    3. Shuka
    4. Kanzu
  2. Ni vazi lipi huvaliwa wakati wa baridi?
    1. Joho
    2. Fulana
    3. Chupi
    4. Tai
  3. Ni ipi si sababu ya kuvaa mavazi? 
    1. Kujikinga baridi
    2. Kuwa nadhifu
    3. Kujificha 
    4. Kujikinga kutokana na hatari
  4. Makanika anapotengeneza gari huwa amevalia vazi lipi kati ya yafuatayo? 
    1. Aproni
    2. Joho
    3. Fulana
    4. Ovaroli
  5. Chagua vazi ambalo huvaliwa ndani ya mavazi mengine.
    1. kanzu
    2. shuka
    3. chupi
    4. joho
  6. Mavazi yanayovaliwa na wanafunzi huitwa; 
    1. magwando 
    2. sare
    3. ovaroli
    4. surupwenye
  7. Neno vazi liko katika ngeli gani? 
    1. LI-YA
    2. I-ZI
    3. I-I
    4. YA-YA
  8. Ni vazi gani huvaliwa wakati wa joto? 
    1. Joho
    2. Fulana
    3. Ovaroli
    4. Chupi

Soma barua kituatacho kisha ujibu maswali
Wanariadha hupeperusha bendera ya Kenya. Bendera ya Kenya ina rangi nne. Kila rangi husimamia jambo fulani. Rangi nyeusi huashiria raia wa Kenya. Raia wa Kenya ni Waafrika.
Rangi nyekundu ni ishara ya damu iliyomwagika wakati wa kupigania uhuru wa nchi yetu. Wapiganiaji uhuru waliteseka na kupigwa. Walimwaga damu nyingi.
Kijani kibichi inaonyesha utajiri wa maliasili ya wakenya. Rangi hii inaashiria mimea ya shambani. Pia hii ni rangi ya misitu yetu. Rangi nyeupe huonyesha upendo na amani ya Wakenya. Bendera ya Kenya pia ina ngao na mikuki miwili. Vitu hivi huonyesha kuwa wakenya wako tayari kuitetea na kuilinda nchi yao.
Bendera ya Kenya hutumika katika shughuli mbalimbali. Mbali na kupeperushwa shuleni, hupatikana kwenye ofisi za serikali, magari ya viongozi wa taifa na katika makao makuu ya ofisi za kibalozi. Bendera inapopandishwa watu wote husimama wima. Kusimama wima ni ishara ya kuonyesha heshima kwa bendera ya Kenya. Bendera ya Kenya hupandishwa na kushushwa wakati wa sherehe za kitaifa kama vile: sherehe za siku Mashujaa Bendera ya Kenya ni fahari yetu. Bendera ya Kenya ni kitambulisho cha Wakenya. Ninaipenda bendera ya nchi yetu.

  1. Mtu anayeipenda nchi yake huitwa;
    1. mzalendo 
    2. msaliti
    3. mkwasi
    4. mkenya
  2. Katika bendera ya Kenya ni nini huonyesha kuwa wakenya wako tayari kuipigania nchi yao: 
    1. rangi nyeupe 
    2. rangi nyeusi 
    3. ngao na mkuki 
    4. rangi ya kijani
  3. Ni maelezo yapi si sahihi? 
    1. Bendera hupeperushwa shuleni 
    2. Bendera huwa kwenye ofisi za serikali 
    3. Bendera huwekwa kwenye magari ya viongozi 
    4. Bendera huvaliwa na mabalozi
  4. Ni rangi ipi huonyesha utajiri wa nchi yetu? 
    1. Nyeusi
    2. Kijani kibichi
    3. Nyeupe
    4. Nyekundu
  5. Ni yupi si mnyamapori?
    1. Nguruwe
    2. Ngiri
    3. Kifaru
    4. Swara
  6. Tunafaa kufanya nini ili kuonyesha heshima kwa bendera ya taifa letu? 
    1. Kupigana
    2. Kuimba 
    3. Kusimama wima bendera inapopandishwa 
    4. Kukimbia wakati bendera inapopandishwa
  7. Ni nani hupeperusha bendera yetu ya Kenya?
    1. Wakenya
    2. Wanariadha
    3. Mashujaa
    4. Wazalendo
  8. Mashujaa wetu waliteswa na nani kabla nchi yetu haijapata uhuru?
    1. Wanariadha
    2. Wakoloni
    3. Raia
    4.  Wakenya
  9. Mashujaa waliopigania uhuru wa nchi yetu husherehekewa katika sikukuu gani?
    1. Krismasi
    2. Siku ya wafanyikazi
    3. Siku ya Mashujaa
    4. Siku ya wanariadha
  10. Jibu maswali kulingana na maagizo
    Tambua nomino katika sentensi ifuatayo. Kochi ambalo limenunuliwa ni kubwa,
    1. kubwa
    2. kochi
    3. limenunuliwa 
    4. ambalo
  11. Chagua kitenzi katika sentensi
    Mtoto analilia chumbani mwake.
    1. analilia
    2. chumbani
    3. mwake
    4. mtoto
  12. Chagua jibu la salamu 'mwambaje
    1. sina la kuamba 
    2. vyema 
    3. salama
    4. hatuna la kuamha
  13. Ni neno lipi si maagane katika orodha ifuatayo
    1. U hali gani? 
    2. Kwaheri 
    3. alamsiki
    4. Buriani
  14. Kanusha sentensi ifuatayo
    Mama ameenda sokoni asubuhi. 
    1. Mama ameenda sokoni asubuhi 
    2. Mama hajaenda sokoni asubuhi 
    3. Baba alikuja nyumbani jioni 
    4. Mama alienda sokoni asubuhi
  15. Chagua sentensi ambayo ina kielezi 
    1. Ndizi zimeiva vizuri 
    2. Kalamu yake imevunjika 
    3. Juma amevunja kalamu yangu
    4. Huyu ni kimbiaji bora
  16. Kifungu kimoja cha shairi huitwaje?
    1. Mshororo
    2. Mizani
    3. Silabi
    4. Ubeti
  17. Tegua kitendawili kifuatacho Pitia huku nami kule tukutane mbele.
    1. ugali
    2. mshipi 
    3. jiwe
    4. nazi
  18. Chagua methali ambayo inahimiza bidii 
    1. Mtaka cha mvunguni sharti ainame
    2. Asiyesikia la mkuu huvunjika guu 
    3. Mwana hutazama kisogo cha nina 
    4. Majuto ni mjukuu huja baadaye
  19. Ni upi si msamiati wa sebuleni.
    1. kabati
    2. makochi
    3. meza
    4. jokofu
  20. Chagua kivumishi katika sentensi
    Mwanamume huuyu anamkongojo mkubwa.
    1. mwanamume
    2. mkongojo
    3. mkubwa
    4. ana
  21. Ni nafsi ipi imetumika sawasawa.
    1. sisi wote tuutaenda mjini
    2. wao wataenda kanisani kesho
    3. mimi ndiye nitakayetuzwa
    4. wewe ndiye utaibuka mshindi
  22. Ni kipi si kifaa cha tarakilishi
    1. zulia
    2. kipanya 
    3. kiwambo 
    4. kibodi 

INSHA
Andika insha ukizingatia mada ifuatayo:
SOKO LETU

KUSOMA

SEHEMU YA  A : Kusikiliza na Kuzungumza

Mwalimu amkaribishe mwanafunzi kwa mazungumzo kwa maamkizi mwafaka kisha amweleze j=kuwa , : Leo tunajadiliana kuhusu wanyamapori."

  1. Ni nini maana ya wanyamapori?
    (Mwanafunzi ajibu)
  2. Ni mnyama yupi anajulikana kama mfalme wa porini?
    (Mwanafunzi ajibu)
  3. Taja mnyama mmoja mabaye hukimbia kwa kasi zaidi?
    (Mwanafunzi ajibu)
  4. Ni mnyama yupi huwindwa sana na majangili kwa sababu ya pembe zake?
    (Mwanafunzi ajibu)
  5. Jina lingine la ndovu ni ?
    (Mwanafunzi ajibu)

SEHEMU YA B: Kusoma kwa sauti
Soma kifungu kifuatacho kwa sauti

Mchezo wa kuigiza ni mchezo ambao umeandikwa kulingana na vitendo vya wahusika. Mchezo wa kuigiza vitendo fulani kuhusu jambo fulani. Mchezo wa kuigiza ni mtungo wa kisanii na unapaswa kuigizwa kwenye jukwaa. Mawazo ya mchezo wa kuigiza hupitishwa na mhusika. Mhusika ni mtu anayetumiwa kupitisha ujumbe wa mtunzi wa mchezo wa kuigiza. Mchezo wa kuigiza huwa na maelekezo na maelezo yanayomwonyesha mhusika namna ya kutenda. Maelekezo hueleza mazingira ya kuigiza. Maelezo haya huandikwa kwenye mabano.

MARKING SCHEME

swa ms 1

Page 3 of 3