Wednesday, 01 March 2023 06:12

Shughuli za Kiswahili Questions and Answers -Grade 5 Opener Exam Term 1 2023 Set 1

Share via Whatsapp

MASWALI

Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali 1-5.

(Ni katika soko la Marikiti ambapo mwuzaji anazungumza na mteja wake)
Mteja:       Umeshindaje kaka? Naona unazo mboga zinazovutia kweli. Bei gani fungu hili? (akilishika) 
Mwuzaji:   Vyema sana mwenzangu. Hizi nimezivuna kutoka shambani mwangu leo leo. Hujaangalia nyanya, pilipili, vitunguu na karoti.                         Wazionaje mboga za leo? (Akitabasamu) siku zote, bei hutegemea mapatano.
Mteja:       He-he-he! Leo wateja wote watapitia hapa kibandani pako. Haya naomba uniuzie mafungu mawili ya sukumawiki na...
Mwuzaji:   (Akimkatiza) Samahani dada. Natumai unajua bei ya mwaka huu mpya. Fungu moja la sukumawiki sasa ni shilingi ishirini.
Mteja:       Gharama ya maisha nayo! Niuzie mafungu mawili ya sukumawiki, fungu moja la nyanya na vitunguu fungu moja.
Muuzaji:    Karoti leo?
Mteja:       Bado zipo. Nilinunua nyingi. Vyote ni shilingi ngapi?
Mwuzaji:   (Muda unapita) Naam, vyote ni shilingi themanini.

  1. Mwuzaji katika mazungumzo haya alikuwa akiuza 
    1. mboga.
    2. matunda.
    3. miwa.
    4. mahindi.
  2. Mteja alinunua mafungu mangapi ya sukumawiki?
    1. Moja.
    2. Matatu.
    3. Mawili.
    4. Manne.
  3. Bei ya mwaka huo mpya ilikuwa gani kwa fungu moja la mboga? Shilingi
    1. themanini.
    2. ishirini.
    3. thelathini.
    4. arobaini.
  4. Kulingana na mazungumzo haya, mwuzaji pia alikuwa
    1. mteja.
    2. mnunuzi.
    3. mpishi.
    4. mkulima.
  5. Mteja katika mazungumzo haya alitumia pesa ngapi kwa jumla?
    Shilingi
    1. thelathini.
    2. ishirini.
    3. themanini
    4. hamsini

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 6 hadi 9.

Hapo zamani za kale, palikuwa na sungura na mbwa. Wanyama hao walikuwa marafiki wa kufa kuzikana. Naam, walipendana kama ulimi na mate. Wanyama hao walipokuwa makaoni mwao, mbwa alimwambia sungura kuwa yeye alihisi njaa sana. Aliendelea kumwambia kuwa angependa kumla yeye kwa kuwa sungura huwa na nyama tamu. Kusikia vile, sungura alijifanya hakujali ingawa alishtuka. Mbwa alipoangalia kando, sungura alikimbia na kujificha kichakani.

  1. Wanyama waliotajwa ni
    1. mbweha na sungura.
    2. mbwa na kinyonga.
    3. sungura na mbwa.
    4. mbweha na kinyonga.
  2. Ni kweli kusema kuwa mwanzoni, wanyama hao wawili
    1. walisaidiana sana.
    2. hawakupendana sana.
    3. walichukiana sana.
    4. walikuwa na ugomvi.
  3. Ni kweli kusema kuwa mbwa alikuwa
    1. rafiki mzuri.
    2. rafiki mbaya.
    3. ameshiba sana.
    4. mnyama mzuri sana.
  4. Sungura alitoroka wakati mbwa alikuwa
    1. ameingia kichakani.
    2. amelala.
    3. ameangalia kando.
    4. amekaa maskanini mwake.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 10 hadi 12   

Upanzi wa miti ni jambo jema sana. Mwalimu wetu wa Sayansi alituclcza kwamba miti hutusaidia kwa namna tofauti tofauti. Alisema kwamba bila miti, mazingira yetu hayawezi kuvutia bali yatachukiza mno. Mmomonyoko wa udongo nao utaenea kwa kasi sana na mwishowe, nchi yetu itakuwa jangwa, yaani ardhi kavu isiyo na mimea yoyote. Ingawa miti hutufaidi kwa njia nyingi, tukiukata mti mnaoja, tuipande mingine miwili au zaidi.

  1. Mwalimu wa kina mwandishi aliwaeleza kuwa miti
    1. huleta hasara kwa wale wanaoipanda.
    2. haina faida yoyote kwa mwanadamu.
    3. hutusaidia kwa njia mbali mbali..
    4. husababisha mmomonyoko wa udongo.
  2. Kulingana na ufahamu huu, mazingira yetu yatavutia ikiwa watu
    1. wataanza kukata miti.
    2. watakata miti bila kupanda mingine.
    3. wataacha kabisa kutumia miti.
    4. watapanda miti.
  3. Mwishoni mwa taarifa, tunashauriwa
    1. kupanda miti baada ya kuikata.
    2. kupanda miti miwili au zaidi kila siku.
    3. kuacha kutumia miti.
    4. kupanda mti mmoja baada ya kuukata mmoja.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 13 hadi 15.

Mzee Safari alikuwa amekula chumvi nyingi, yaani alikuwa amezeeka sana. Moja ya sifa zake kuu ilikuwa ni usimuliaji wa hadithi. Matamshi yake yalikuwa bora nayo sauti yake ilikuwa kama ya kinanda. Wakati wa jioni, wajukuu wake walimzingira ili kupata uhondo wa hadithi zake zisizo na mwisho. Mara nyingi hadithi zake zilihusu jinsi ambavyo watu wa kitambo waliishi. Wajukuu wake walizidi kufurahia kila siku kwa sababu hadithi za babu yao ziliwachangamsha na kuwarekebisha kitabia.

  1. Mtu anapokuwa amezeeka sana, tunasema amekula
    1. miaka mingi. 
    2. chumvi nyingi.
    3. umri mwingi.
    4. shida nyingi.
  2. Mzee Safari alijulikana sana kutokana na
    1. usimuliaji wa hadithi.
    2. uzee wake.
    3. sauti yake kama ya kinanda. 
    4. mawaidha yake.
  3. Mara nyingi hadithi za mzee Safari zilihusu
    1. watu wa kitambo.
    2. watoto wa siku hizi.
    3. wanyama wa kitambo.
    4. watoto.

Soma kifungu kifuatacho. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa. 

Nilipofika sokoni, nilienda moja kwa moja hadi kwenye___16___ cha kuuzia matunda. Nilichagua matunda matano yaliyonipendeza. Mara moja nilitia mkono ___17___ ili kuichomoa noti yangu na ___18___. Ole wangu! Sikuamini noti ya shilingi mia tano ___19___. Pesa zote za
mama nilikuwa nimezipoteza. Machozi yalinitiririka ___20___ nisijue la kusema wala la kufanya.

   A   B   C   D 
 16.   kikundi   kiwanja   kibanda   kijumba 
 17.  kichwani   ndani   mfukoni   polepole 
 18.  kulipa  kupewa   kulipwa   kuondoka 
 19.  ilikuwapo   haikuwapo   hazikuwapo   zilikuwapo 
 20.  kidevuni  mdomoni  makwapani  mashavuni 


Katika swali la 21-30, jibu swali kulingana na maagizo uliyopewa.   

  1. Katika sentensi :
    Kamba iliyopotea itapatikana leo,
    kielezi ni
    1. leo
    2. itapatikana
    3. iliyopotea
    4. kamba 
  2. Chagua orodha ya vitenzi pekee.
    1. Masomo, soma, kusoma
    2. Andika, kalamu, karatasi 
    3. Simama, keti, tembea
    4. Kunywa, meza, godoro.
  3. Kanusha sentensi ifuatayo kwa usahihi: 
    Wewe unaandika vizuri. Wewe
    1. huandika vizuri.
    2. unaandika vibaya.
    3. hukuandika vizuri.
    4. huandiki vizuri.
  4. Chagua sentensi iliyo katika wakati ujao.
    1. Wanafunzi walikuwa wakicheza.
    2. Paka anamkimbiza pinya.
    3. Walimu na wazazi wanazungumza afisini.
    4. Tutapokea zawadi zetu jioni.
  5. Kamilisha tashbihi.
    Bi Kenge ni mfupi kama
    1. ngazi.
    2. uyoga.
    3. msumari.
    4. nyundo.
  6. Ukubwa wa nomino mke ni
    1. jike.
    2. jimke
    3. mwanamke.
    4. janajike.
  7. Maneno ambayo hutoa maelezo zaidi kuhusu vitenzi huitwa
    1. vielezi.
    2. viwakilishi.
    3. vitanzandimi.
    4. vivumishi.
  8. Chagua neno lililo tofauti na mengine.
    1. Lakini.
    2. Oga
    3. Ingawa.
    4. Wala.
  9. Chagua mmea uliolinganishwa ipasavyo na tunda lake.
    1. Mpera - mipera
    2. Embe - maembe
    3. Mgomba - ndizi
    4. Mchungwa - parachichi
  10. Chagua nomino isiyo katika ngeli ya ki-vi.
    1. Kioo.
    2. Kiziwi
    3. Kiota.
    4. Kiazi.


MARKING SCHEME

  1. A
  2. C
  3. B
  4. D
  5. C
  6. C
  7. A
  8. B
  9. C
  10. C
  11. D
  12. A
  13. B
  14. A
  15. A
  16. C
  17. C
  18. A
  19. B
  20. D
  21. A
  22. C
  23. D
  24. D
  25. D
  26. A
  27. A
  28. B
  29. C
  30. B
Join our whatsapp group for latest updates

Download Shughuli za Kiswahili Questions and Answers -Grade 5 Opener Exam Term 1 2023 Set 1.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students