Displaying items by tag: Shughuli za Kiswahili
Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - Grade 4 Mid Term 2 Exam 2023 Set 2
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata.
Mzee Juma ni mkulima anayejulikana kote katika kijiji cha Jomvu. Hii ni kutokana na shughuli zake za kilimo. Amefuga wanyama kama vile mbuzi, ng'ombe, kondoo, nguruwe na punda. Vilevile, amefuga kuku, bata, batamzinga na njiwa. Mzee Juma pia ana shamba kubwa lililo karibu na Mto Kijitonyama. Yeye hutumia maji ya mto huo msimu wa kiangazi ili kuinyunyizia mimea yake maji. Hali hiyo ya kunyunyizia mimea yake maji husaidia ili isinyauke wala kukauka. Kujulikana kwake kulitokana na hali ya kuwauzia wanakijiji mazao ya shambani au maziwa na mayai yaliyotokana na ufugaji wake.
Vilevile, Mzee Juma aliwafunza watoto wake shughuli hizo. Alielewa kuwa mtoto hufuata mwelekeo anaopewa na mzazi wake. Wakati wa likizo, wikendi na sikukuu, watoto hao walishirikiana na wazazi wao kufanya shughuli za shambani au ufugaji. Ungepata wakisaidia katika kupalilia mimea, kuvuna mazao au kubeba mazao yaliyovunwa. Pale nyumbani, ungewaona wakishughulika katika kuokota mayai yaliyotagwa, kuwakama ng'ombe au kuwalisha mifugo hao.
- Ni kweli kuwa Mzee Juma ni;
- mwalimu
- mkulima
- daktari
- dereva
- Kwa nini Mzee Juma anajulikana katika kijiji chote?
- Ana watoto wenye nidhamu.
- Ana mashamba makubwa.
- Kutokana na shughuli zake za kilimo.
- Ana mifugo wengi.
- Maneno 'mtoto hufuata mwelekeo anaopewa na mzazi wake' yanaweza yakaelezwa kwa methali gani?
- Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.
- Polepole ndio mwendo.
- Siku za mwizi ni arubaini.
- Asiyesikia la mkuu huvunjika guu.
- Ni nini ambacho Mzee Juma hakuwauzia wanakijiji?
- maziwa
- mazao ya shambani
- wanyama
- mayai
- Ni kweli kuwa Mto Kijitonyama humpa Mzee Juma maji ya;
- kunywesha mifugo.
- kuoga.
- kufua nguo.
- kunyunyizia mimea.
- Kwa nini watoto wa Mzee Juma walisaidia wazazi wao wakati wa likizo, wikendi na sikukuu pekee?
- Walienda shuleni wakati huo mwingine.
- Walikuwa wakicheza wakati huo mwingine.
- Wakati huo mwingine walienda kanisani.
- Wakati huo mwingine walienda kumtembelea nyanya yao.
- Pale nyumbani, watoto wangefanya yafuatayo isipokuwa;
- kuokota mayai yaliyotagwa
- kuwakama ng'ombe
- kuwalisha mifugo
- kupalilia mimea
Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata.
Kompyuta au tarakilishi ni kifaa cha kidijitali chenye umuhimu mkubwa. Kifaa hicho hupatikana katika afisi za kazini, shuleni, hospitalini au nyumbani. Kompyuta ina sehemu kama vile bodidota, kiwambo, kitengo kikuu cha uchakataji, kipanya na kebo. Unapotaka kupiga chapa kwenye tarakilishi, tumia bodidota kuandika. Yale unayoyaandika huonekana kwenye kiwambo. Kipanya nacho huelekeza shughuli mbalimbali, kwenye kiwambo. Kitengo kikuu cha uchakataji hufanya shughuli zote za kompyuta kama vile kupokea ujumbe, kuuchanganua, kuhifadhi na kutuma ujumbe huo. Kazi ya kebo ni kupitisha umeme au data ya kidijitali.
Katika matumizi ya tarakilishi na vifaa vingine vya kidijitali, ni vyema kuomba ruhusa kutoka kwa mzazi, mlezi au mwalimu wako. Kabla ya kutumia kifaa cha kidijitali, unafaa kuhakikisha kuwa kifaa hicho kimeunganishwa na umeme. Kompyuta hutumika kupiga chapa, kusikiliza muziki, kucheza michezo ya tarakilishi, kutafuta maarifa kwenye mtandao, kujionea picha mtandaoni na kadhalika. Jambo muhimu ni kuwa si vyema kutumia vifaa vya kidijitali kwa muda mrefu. Ukiangalia mwangaza unaotoka kwenye vifaa hivyo kwa muda mrefu, unaweza ukapata matatizo ya macho.
- Kulingana na kifungu, jina jingine la kompyuta ni ____________________________.
- runinga
- rununu
- tarakilishi
- televisheni
- Maneno 'kuomba ruhusa' ni mfano wa nini?
- nahau
- methali
- tashbihi
- kitendawili
- Ni nani ambaye mwanafunzi hawezi kuomba ruhusa kutoka kwake kabla ya kutumia kifaa cha kidijitali?
- mwalimu
- mwanafunzi
- mzazi
- mlezi
- Mwanafunzi akiwa shuleni, anashauriwa kutumia tarakilishi kufanya nini?
- kusikiliza muziki
- kucheza michezo ya tarakilishi
- kutafuta maarifa kwenye mtandao
- kujionea picha mtandaoni
- Jambo muhimu ni kuwa si vyema;
- kutumia vifaa vya kidijitali.
- kubeba vifaa vya kidijitali.
- kuweka vifaa vya kidijitali kwa muda mrefu..
- kutumia vifaa vya kidijitali kwa muda mrefu.
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata.
Bendera ya taifa la Kenya ina rangi nne muhimu. Rangi nyeupe huonyesha amani. Amani ni hali ya utulivu ambao hudumu katika taifa lolote. Rangi nyeusi nayo huonyesha rangi ya wakenya. Wakenya hujulikana kwa rangi ya mwafrika ambayo ni nyeusi. Ni vyema kukubali na kufurahia jinsi ambavyo tumeumbwa. Maumbile ya mtu ni uamuzi ambao ulifanywa na Mungu. Rangi ya kijani kibichi, huonyesha mimea inayopatikana kwenye ardhi yetu. Miti, nyasi na mimea mingine ni muhimu sana kwa kila mkenya. Hatimaye, rangi nyekundu hutukumbusha kuwa kuna watu waliopigania uhuru wetu. Katika hali hiyo ya kupigania uhuru, kuna damu iliyomwagika. Kuipenda bendera yetu ni ishara ya uzalendo.
- Rangi gani ambayo hutukumbusha uhuru wetu ulivyopatikana?
- nyekundu
- nyeupe
- nyeusi
- kijani
- Ni nini tunachofaa kufanya ili kuonyesha kuwa miti, nyasi na mimea mingine ni muhimu?
- kupanda miti na nyasi zaidi.
- kukata miti iliyo mingi.
- kuchoma takataka kila mahali.
- kuwa na michoro ya nyasi, miti na mimea.
- Chagua maana ya neno 'uzalendo' jinsi lilivyotumika katika kifungu.
- kujua rangi za bendera
- kupenda mazingira
- kuipenda nchi
- kuipenda bendera
Chagua jibu lifaalo ili kujazia nafasi zilizoachwa.
Paka ni mnyama __16__ anapendwa sana katika nyumba __17__. Paka wengi hupenda kutulia nyumbani bila tatizo lolote. Chakula __18__ na paka sana ni panya. Paka __19__ panya wanaoharibu vitu katika nyumba. Unapofuga paka, ni vigumu sana kwa __20__ kuharibiwa sebuleni na panya.
A | B | C | D | |
16. | ambayo | ambalo | ambao | ambaye |
17. | mengi | mingi | nyingi | zingi |
18. | inayopendwa | kinaopendwa | kinachopendwa | inachopendwa |
19. | huwala | huwakula | hukulwa | hukuliwa |
20. | kitanda | kinu | kochi | mbuzi |
Jibu kila swali kulingana na maagizo.
- Jua huchomoza upande gani wa dira?
- Kaskazini
- Mashariki
- Magharibi
- Kusini
- Chagua jibu ambalo linaonyesha kitenzi.
- ruka
- kitabu
- mzuri
- huyu
- Tambua kiwakilishi kwenye sentensi ifuatayo.
Huyu amekula chakula kitamu.- kitamu
- amekula
- chakula
- huyu
- Tegua kitendawili;
Chalia, chatembea na chala chakula cha mkono.- kengele
- saa
- mtoto
- mbuzi
- Tambua aina za maneno yaliyopigiwa mistari.
Mwanafunzi mzuri anasoma polepole.- kivumishi, kitenzi
- kiwakilishi, kielezi
- kielezi, nomino
- kivumishi, kielezi
- Nomino gani ambayo haipatikani katika Ngeli ya A - WA?
- kipepeo
- mbuzi
- mti
- chawa
- Chagua wingi wa;
Mkeka wa mtume umewekwa.- Mikeka ya mitume imewekwa.
- Mikeka ya mitume yamewekwa.
- Mikeka ya watume imewekwa.
- Mikeka ya watume yamewekwa.
- Nomino gani inayopatikana katika ngeli ya LI-LI?
- jiwe
- darasa
- giza
- jicho
- Jibu la 'chewa' ni _____________________
- ewaa
- chewa
- njema
- marahaba
- Ni vizuri _______________________ ndipo uingie ndani ya nyumba.
- upige makofi
- upige pasi
- upige mbio
- upige hodi
INSHA
Andika insha ya wasifu kuhusu,
NYUMBANI KWETU.
___________________________________________________________________________________________

MARKING SCHEME
- B
- C
- A
- C
- D
- A
- D
- C
- A
- B
- C
- D
- A
- A
- C
- D
- C
- C
- A
- C
- B
- A
- D
- B
- D
- C
- A
- C
- B
- D
Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - Grade 4 Opener Exams Term 2 2023 Set 2
Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu swali 1-5
Furaha ni msichana wa gredi ya nne. Ana umri wa miaka tisa. Yeye anaishi na wazazi wake katika mtaa wa Kabiti. Nyumba yao ina sebule, jikoni, vyumba vitatu vya kulala, choo na bafu. Furaha anapenda kustarehe sebuleni. Kuna makochi manne na meza. Sakafuni kuna Zulia na ukutani kuna saa na mapambo tofauti. Ndani ya chumba cha furaha cha kulala mna kitanda chenye matendegu manne na meza ndogo ya kusomea pia kuna neti ambayo Furaha hutumia kujifunika ili asiumwe na mbu. Furaha na mama yake huandaa vyakula jikoni. Wao huandaa vyakula vitamu sana. Furaha anaipenda nyumba yao.
- Jina la mtaa anamoishi furaha ni
- Kibra
- Kabiti
- Bibabii
- Hatujafahamishwa
- Familia ya Furaha ina jumla ya watu wangapi?
- Wawili
- Watatu
- Wanne
- Watano
- Sakafuni huwekwa zulia, je dirishani huwekwa nini?
- Kochi
- Neti
- Pazia
- Blanketi
- Wageni hupokelewa wapi
- sebuleni
- jikoni
- bafuni
- dirishani
- Kwa nini Furaha hulala ndani ya neti?
- ili asiumwe na mbu
- ili kuwe na joto
- kwa sababu yenye ni mwoga
- nzi huwa wengi chumbani mwake
Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu swali 6-10.
Somo ni mvulana mwenye bidii shuleni pia yeye anapenda kujifunza mengi mtandaoni. Wakati mwingine yeye hazingatii usalama akitumia matini ya kijitali.
Siku moja alipata ujumbe mtandaoni kwanza alidhani ni ujumbe kutoka kwa rafiki yake kumbe ujumbe huo ulitoka kwa mtu asiyejua. Mtu huyo alimwambia wakutane mahali pa faragha. Mtu huyo alimwambia somo kuwa alikuwa na zawadi yake. Kwamba alitamani sana kupata zawadi yake. Kwanza alitamani sana kupata zawadi lakini aliona kwanza awajulishe wazazi wake. Kumbe mtu huyo hakuwa mzuri.
- Bidii za Somo ziliangazia wapi hasa?
- Mtandaoni
- Shuleni
- Masomoni
- Rafikiye
- Ujumbe aliopata ulitoka kwa nani?
- Rafikiye
- Mamaye
- Mtu asiyemjua
- Mwalimu
- Ujumbe aliopata ulimwambia vipi?
- Wakutane faraghani
- Alikuwa amepita mtihani wake
- Azingatie usalama mtandaoni
- Asitumie mtandao
- Je, Somo alikutana na aliyetuma ujumbe?
- Hatujafamisha
- La
- Naam
- Hamna uhakika
- Ni kipi si kifaa cha kidijitari kati ya hivi?
- Kamera
- Simu
- Tarakilishi
- Redio
Soma kifungu hiki. Chagua jibu lifaalo kujaza nafasi zilizoachwa kutoka 11-15.
Elimu ya mazingira ni mada __11__ mkazo sana katika somo __12__Kiswahili. Wanafunzi wanahimizwa kusafisha mazingira __13__ ili wadumishe usafi. Wanafunzi wakishirikiana watatimiza azma __14__ ya kudumisha usafi kwa kuwa __15__.
A | B | C | D | |
11. | inayotilia | inayotiliwa | inayotia | inayotiwa |
12. | ya | wa | cha | la |
13. | yao | zao | lao | zao |
14. | hizo | huyo | hilo | hiyo |
15. | Ukijitahidi utafaidi | Mtaka cha mvunguni sharti aianame | Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu | Mgagaa na upwa hali wali makavu |
SARUFI
Kuanzia swali 16-30 jibu kulingana na maagizo
- Chagua kundi lenye nomino pekee
- Amri, hisani, vizuri
- Chai, subira, nyeupe
- Hewa, amani, neno
- Haraka, baraka, pamoja
- Tegua kitendawili
Bei yangu haishuki _____________________________________- shamba
- dhahabu
- pesa
- uhai
- Andika sentensi ifuatayo kwa wingi
Mzazi alimtuma mwanawe shambani- Mzazi aliwatuma wanawe mashambani
- Wazazi waliwatuma wanawe mashambani
- Wazazi aliwatuma wanawe shambani
- Wazazi waliwatuma wanawe shambani
- Chagua orodha yenye maneno yaliyo katika ngeli ya KI-VI pekee
- Kifagio, choo, vitabu
- Kipofu, kiko, sahani
- Choo, kiwavi, kioo
- Mbwa, mti, kiberiti
- Tumia amba ipasavyo
Chombo ___________________________________ alitumia ni chake- ambao
- ambayo
- ambacho
- ambavyo
- Kanusha
Alitembea akiimba- Hakutembea wata hakuimba
- Hakutembea wala kuimba
- Hayatembe na hajaimba
- Hatatembea wala kuimba
- Chagua nomino kwenye sentensi ifuatayo
Mwimbaji aliimba kwa ustadi mno- aliimba
- mno
- mstadi
- mwimbaji
- Shairi lenye mishororo minne huitwa
- Tarbia
- Takhmisa
- Tathnia
- Tathlitha
- Kamilisha methali ifuatayo
Asiyesikia la mkuu- huvunjika guu
- hufunzwa na ulimwengu
- hufaulu
- hupotea
- Jibu la salamu sabalkheri ni
- Binuru
- Alamsiki
- Aheri
- Chewa
- Wao _______________________________ walionaswa na polisi
- ndisi
- ndio
- ndiyo
- ndiwo
- Umbo lifuatalo huitwa
- duara
- duara dufu
- mstatili
- mraba
- Kinyume cha neno anika ni
- anikia
- anua
- anikika
- anika
- Bendera ya Kenya ina rangi ngapi?
- Nne
- Tatu
- Tano
- Sita
- Kisawe cha neno rafiki ni
- adui
- ndugu
- somo
- mzazi
INSHA
Andika insha ya kusisimua kuhusu mada ifuatayo
FAMILIA YETU
MARKING SCHEME
- B
- B
- C
- A
- A
- B
- C
- A
- B
- D
- D
- D
- A
- D
- C
- C
- A
- B
- A
- C
- B
- D
- A
- A
- C
- B
- B
- B
- A
- C
Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - Grade 5 Opener Exams Term 2 2023 Set 1
MASWALI
MAAGIZO
Karatasi hii ina sehemu tano kuu.
Jibu maswali yote kulingana na maagizo.
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata.
Siku moja wakati wa jioni, Punda alikuwa amechoka sana. Alikuwa amelala chini ya mti baada ya kufanya kazi mchana wote. Aliamshwa saa kumi na moja alfajiri na kuanza kubebeshwa mizigo, Mwanzo, alibeba unga kutoka sokoni akipeleka nyumbani alikoishi. Unga huo ulikuwa magunia saba. Alipomaliza, alianza kusomba maji kutoka kwenye eneo la kisima akipeleka katika nyumba za watu. Shughuli ya kusafirisha maji ilifanyika kuanzia saa nne hadi saa saba. Alipotoka hapo, alifahamishwa kuwa kulikuwa na miti iliyofaa kubebwa kutoka msituni hadi mjini. Kazi ya kubeba miti ilianza saa nane. Kufikia saa kumi na mbili, Punda hakuwa amemaliza kubeba miti hiyo. Mvua ilikuwa imenyesha na kuisha huku punda akiendelea na kazi hiyo.
Punda aliamua kuzungumza na rafiki yake wa chanda na pete, Farasi. Farasi alionekana kuishi maisha ya starehe sana. Punda alimwamkua "Masalheri kaka?"kisha akauliza swali lake. Farasi alimweleza kuwa yeye huishi maisha ya starehe kwa sababu alikuwa amesoma. Alimfahamisha kuwa mara nyingi, unaposoma huwa unapata kazi nzuri ambazo si za mateso. Pia, alimwambia kuwa si lazima aajiriwe ikiwa amesoma. Angeweza kujifungulia biashara na kujiendeleza. Kando na kusoma, Farasi alimweleza faida ya kutumia talanta yake. Farasi alieleza kuwa yeye alikuwa na talanta ya riadha, hiyo ndiyo sababu alikuwa akikimbia mara kwa mara na kupata manufaa tele. Asubuhi iliyofuata, Punda aliwasili shuleni ili kuanza masomo ya jioni baada ya kazi. Ni kweli kuwa alisoma kwa bidii sana. Vilevile, alianza mazoezi ya uimbaji kwa kuwa alikuwa na sauti nzuri sana.
- Kwa nini Punda alikuwa amechoka?
- Alimka mapema sana.
- Alinyeshewa na mvua.
- Hakuwa amekula.
- Alifanya kazi nyingi sana.
- Yawezekana kuwa Punda alimtembelea Farasi wakati gani?
- asubuhi
- usiku
- adhuhuri
- jioni
- Badala ya kutumia neno 'rafiki yake', mwandishi angetumia neno gani lenye maana sawa!
- sahibu yake
- jirani yake
- ndugu yake
- mnyama mwenzake
- Ufahamu huu unaonyesha umuhimu wa nini?
- talanta na masomo
- masomo na kuamka mapema
- kazi na talanta
- biashara na masomo
- Punda alisomba maji kwa muda gani?
- saa saba
- saa tatu
- saa nne
- saa saba
- Punda alibeba miti hadi saa ngapi?
- saa kumi na mbili
- kabla ya saa kumi na mbili
- saa nane
- baada ya saa kumi na mbili
- Maneno 'alisoma kwa bidii sana' yanaweza yakarejelewa kwa methali gani?
- Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.
- Mgaagaa na upwa hali wali mkavu.
- Asiyesikia la mkuu huvunjika guu.
- Polepole ndio mwenda.
- Kulingana na ufahamu, ni keli kuwa mtu aliyesoma:
- hawezi akaajiriwa.
- anaweza akaajiriwa au afanye biashara.
- hawezi akafanya biashara.
- lazima aishi mjini.
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata.
Upishi wa chakula ni muhimu sana katika maisha yetu. Kuna sababu mbalimbali ambazo hufanya tupike chakula. Kwanza, chakula huweza kuwa laini na kulika kwa urahisi ikiwa kimepikwa. Chakula kisichopikwa hakiwezi kikalika kwa urahisi. Jambo jingine ni kuwa kupika chakula huua viini ili mtu asiambukizwe ugonjwa. Magonjwa kama vile kipindupindu na kuendesha husababishwa nachakula au maji machafu. Kwa hivyo tunapopika chakula, chakula hicho huwa salama kwa ulaji. Kupika chakula pia hufanya chakula hicho kiwe na ladha nzuri. Chakula kilichopikwa huonja vizuri kuliko chakula amabacho hakijapikwa. Unapopika chakula, huwa kitamu kama asali.
Wakati wa kupika, kuna hatua kadhaa ambazo hufuatwa. Kabla ya kuinjika sufuria mekoni, ni vyema kukoka moto. Baada ya chakula kuiva, mtu huepua sufuria kisha akapakua chakula hicho. Vyakula huweza kupikwa kwa njia mbalimbali. Njia hizo ni kama vile kutokosa, kukaanga, kuoka na kubanika. Vyakula vinavyoweza kukaangwa ni kama vile samaki, mayai, nyama na mboga. Utokosaji nao huweza kufanyiwa viazi, mihogo, mahindi, samaki na nyama. Unaweza ukabanika mahindi na nyama kisha ukaoka keki, mkate au biskuti.
- Zifuatazo ni faida za kupika chakula isipokuwa;
- Huwezesha chakula kumezwa kwa haraka.
- Huua viini katika chakula.
- Hufanya chakula kiwe laini.
- Huongeza ladha ya chakula.
- Maneno 'kitamu kama asali' ni mfano wa;
- nahau
- kitendawili
- tashbihi
- kitanzandimi
- Chagua hatua ya pili kati ya hatua zifuatazo kulingana na kifungu.
- koka
- injika
- epua
- pakua
- Chakula gani kinachoweza kuandaliwa kwa kutokoswa, kukaangwa au kubanikwa?
- nyama
- keki
- viazi
- mboga
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata.
Katika soko la Mikindani, kuna matunda aina mbalimbali. Siku moja watoto kadhaa walienda sokoni kununua matunda hayo. Wavulana walikuwa wanne nao wasichana walikuwa watatu. Kamau alinunua maembe, mananasi, machungwa na tufaha. Njeri alinunua matunda yote yaliyonunuliwa na Kamau isipokuwa maembe. Fatuma naye alinunua matunda yote yaliyonunuliwa na Njeri kisha akaongezea maembe na maparachichi. Wanjala alinunua
matunda yaleyale yaliyonunuliwa na Kamau kisha akaongezea maparachichi. Wengine nao walinunua matunda bila kuchagua, waliyachanganya tu. Walipomaliza shughuli zao, waliondoka na kurudi nyumbani.
- Kifungu kinaeleza kuwa vijana wangapi walioenda sokoni?
- watatu
- wanne
- saba
- sita
- Akina nani walionunua matunda ya aina moja?
- Wanjala na Fatuma
- Njeri na Fatuma
- Kamau na Njeri
- Wanjala na Kamau
- Ni nani aliyenunua aina chache za matunda!
- Kamau
- Wanjala
- Fatuma
- Njeri
Jaza nafasi zilizoachwa kwa kutumia jibu linalofaa zaidi.
Nuru alichukua karatasi ..................16.................... ili kumwandikia Zawadi barua. Zawadi alikuwa ndugu yake aliyesomea mjini. Aliketi ..................17.................... kiti chake kisha akaanza kuandika barua hiyo. Baada ya kuandika anwani ..................18.................... aliandika tarehe kisha akaendelea. Alimweleza ..................19.................... ni vyema kuwa na maadili katika maisha. Maisha ya mtu ..................20.................... kuwa mazuri sana ikiwa ana maadili.
-
- wake
- lake
- yake
- chake
-
- kwa
- kwenye
- katika
- ndani mwa
-
- nne
- tatu
- mbili
- moja
-
- kuwa
- kuwamba
- kwa
- kama
-
- yanaweza
- anaweza
- inaweza
- unaweza
Jibu kila swali kulingana na maagizo.
- Chagua nomino ya wingi kwenye majibu yafuatayo.
- uraha
- matunda
- chai
- kitanda
- Ukubwa wa 'mji' ni.
- miji
- kijiji
- vijiji
- jiji
- Jibu gani ambalo halionyeshi matumizi ya herufi kubwa?
- Hutumika mwanzoni mwa sentensi.
- Hutumika kuandika nomino ya pekee.
- Hutumika mwishoni mwa sentensi.
- Hutumika kuonyesha ufupisho wa maneno.
- Pambo gani ambalo huvaliwa mkononi?
- ushanga
- bangili
- pete
- herini
- Kinyume cha 'furaha ni.
- hasira
- lia
- huzuni
- woga
- Chagua wingi wa:
Kitabu changu kimewekwa ndani ya kabati.- Vitabu vyetu vimewekwa ndani ya kabati.
- Vitabu vyangu vimewekwa ndani ya makabati.
- Vitabu vyangu vimewekwa ndani ya kabati.
- Vitabu vyetu vimewekwa ndani ya makabati.
- 'Mombasa, Ijumaa na Disemba' ni mifano ya aina gani za nomino?
- dhahania
- za pekee
- za makundi
- za vitenzijina
- Umati ni wa watu' kama vile kicha ni cha
- pesa
- matunda
- funguo
- maua
- Yafuatayo ni maagano isipokuwa;
- alamsiki
- buriani
- masalheri
- siku njema
- Chagua sentensi inayoonyesha wakati uliopita, hali ya kuendelea.
- Juma alikuwa akisoma kitabu chake.
- Mama atakuwa akimshauri mtoto wake.
- Wangali wanakula chakula chao.
- Wanafunzi wamepanda miti mingi.
INSHA
Andika insha ya masimulizi kuhusu;
AJALI NILIYOSHUHUDIA
MWONGOZO
Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - Grade 4 Opener Exams Term 2 2023 Set 1
MAAGIZO
- Karatasi hii ina sehemu tano kuu.
- Jibu maswali yote kulingana na maagizo.
MASWALI
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata.
Fanaka ni mwanafunzi katika shule ya msingi ya Elimubora. Yeye hupenda sana kuvaa nguo safi. Rinda lake huwa nadhifu na kupigwa pasi hadi likapendeza. Fanaka anajulikana katika shule yote kutokana na tabia zake nzuri. Anapokuwa shuleni, yeye huwa na marafiki wa karibu wawili. Marafiki hao ni Mwanzia na Kalondu. Yeye na marafiki zake husoma pamoja, kucheza na kula pamoja. Wao hupenda sana kucheza kibemasa. Wanapokuwa darasani, hawawezi kuenda haja bila kuomba idhini. Wanapotoka haja, wao huhakikisha kuwa wamenawa mikono kwa maji safi na sabuni.
Kule nyumbani, Fanaka hupenda sana kucheza na mnyama ampendaye ambaye ni paka. Paka wake ana rangi nyeusi na nyeupe. Fanaka humpa paka wake maziwa na nyama. Anapokuwa mgonjwa, paka huyo hupelekwa kwa daktari wa mifugo ili ampime na kumpa. matibabu Fanaka pia huwasaidia wazazi wake kufanya kazi za shambani na za nyumbani. Ndugu zake wawili hawajaanza kuenda shuleni kwa kuwa bado hawajafikisha umri wa kujiunga na shule.
- Fanaka na wenzake hunawa mikono kwa maji
- safi.
- moto.
- mengi.
- baridi.
- Ni kweli kuwa Fanaka ni
- mfupi.
- mvulana.
- msichana.
- mrefu.
- Nahau 'kuomba idhini' ina maana gani kulingana na ufahamu?
- enda msalani
- omba ruhusa
- toka nje
- chukua nafasi
- Fanaka na wenzake hunawa mikono;
- kabla ya kuenda msalani.
- baada ya kuenda msalani.
- ndipo watoke nje.
- wakiwa msalani.
- Paka wa Fanaka anapokuwa mgonjwa, yeye hufanyiwa nini?
- Hupewa dawa.
- Hudungwa sindano:
- Hupelekwa kwa daktari.
- Hukataa kula.
- Ni kweli kuwa tabia nzuri za Fanaka zimefanya;
- ajulikane na kila mwalimu.
- apite mtihani.
- ajulikane na kila mwanafunzi.
- apendwe na kila mwanafunzi.
- Ni kweli kuwa ndugu wa Fanaka;
- ni wakubwa kwa Fanaka.
- wamemaliza masomo.
- si wasichana.
- ni wadogo kwa Fanaka.
- Mnyama ambaye Fanaka humpenda sana ni yupi?
- paka
- mbwa
- mbuzi
- ngombe
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata.
Runinga au televisheni ni kifaa muhimu sana katika maisha. Tofauti na hapo zamani siku hizi karibu kila familia huwa na runinga. Runinga huwafaa watu wengi mno katika familia. Watoto hupenda kutazama vibonzo kwenye runinga. Watu wengine nao hupenda kutazama nyimbo mbalimbali, vipindi na taarifa za habari. Kuna wale wanaopenda kutazama michezo kama vile kandanda, riadha na kadhalika.
Runinga yetu ni kubwa mno. Imewekwa sebuleni kwenye kabati lililo ukutani. Haturuhusiwi kutazama runinga kabla ya kumaliza kazi za ziada. Pia, ikiwa wazazi wanatazama kile wakitakacho, sisi husubiri kwanza wamalize ndipo tutazame vibonzo. Mimi hupenda kutazama PJ Mask na Sofia The First. Dada yangu naye hupenda kutazama Akili Kids. Mama naye hupenda kutazama kipindi cha 'Pete' kwenye Maisha Magic.
- Jina lingine la runinga ni gani kulingana na ufahamu?
- tarakilishi
- kopyuta
- televisheni
- rununu
- Ni kweli kuwa hapo zamani;
- watu wote walikuwa na runinga.
- watu wengi walikuwa na runinga.
- watu wachache walikuwa na runinga.
- hakuna aliyekuwa na runinga.
- Watoto hupenda kutazama nini kwenye runinga?
- vibonzo
- kandanda
- nyimbo
- taarifa
- Dada wa mwandishi anapenda kutazama nini kwenye runinga?
- PJ Mask
- Sofia The First
- Akili Kids
- Pete
- Mwandishi anasema kuwa runinga yao imewekwa wapi?
- msalani
- sebuleni
- jikoni
- katika chumba cha kulala
- Mwandishi husema kuwa watoto hutazama runinga wakati gani?
- Badala ya kufanya kazi ya ziada.
- Kabla ya kufanya lazi ya ziada.
- Baada ya kufanya kazi ya ya ziada.
- Wanapofanya kazi ya ziada.
- Ni nani anayependa kutazama kipindi cha Pete?
- baba
- mwandishi
- dada
- mama
Jaza nafasi zilizoachwa kwa kutumia jibu linalofaa zaidi.
Kitabu..............16..................nacho mkononi kilikuwa na hadithi kuhusu Sungura na rafiki ..............17...................Walikuwa marafiki ..............18.................. sana. Kila wakati, ungepata wakishirikiana katika kila jambo. Waliwashauri watoto wao na kuwaambia wafuate njia nzuri. Tabia za watoto ..............19.................. zilikuwa za kupendeza sana. Watoto wenyewe walijua kwamba ..............20..................
-
- niliokuwa
- nilizokuwa
- niliyokuwa
- nilichokuwa
-
- wake
- zake
- yake
- lake
-
- wakubwa
- makubwa
- mikubwa
- kubwa
-
- hao
- huyo
- hawo
- hizo
-
- haraka haraka haina baraka
- asiyesikia la mkuu huvunjika guu
- akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki
- umoja ni nguvu utengano ni udhaifu
Jibu kila swali kulingana na maagizo.
- Jibu gani ambalo linaonyesha nomino?
- kitabu
- imba
- vizuri
- wengi
- Chagua jina la kifaa kinachotoa mwangaza katika nyumba.
- tumbuu
- balbu
- chandarua
- mchi
- Onyesha kivumishi kwenye sentensi ifuatayo.
Wanafunzi wazuri wamepewa zawadi.- wanafunzi
- wazuri
- wamepewa
- zawadi.
- Vazi gani ambalo huvaliwa na wavulana pekee?
- shati
- koti
- sweta
- chupi
- Tegua kitendawili.
Popote niendapo ananifuata.- upepo
- nzi
- viatu
- kivuli
- Chagua kiwakilishi kwenye sentensi ifuatayo.
Huyu amemaliza chakula chake.- chake
- chakula
- huyu
- amemaliza
- Jibu la 'alamsiki' ni gani?
- binuru
- marahaba
- sijambo
- vyema
- 'juu ya, chini ya, mbele ya na ndani ya' ni mifano ya
- vihisishi
- viunganishi
- vihusishi
- vielezi
- Jaza nafasi kwa jibu linalofaa.
Mtoto alianguka............................hakulia.- na
- kwa sababu
- lakini
- wala
- Chagua jibu ambalo ni kielezi.
- polepole
- nyumba
- lala
- huyo
INSHA
Mwandikie rafiki yako barua ukimweleza mambo uliyofanya wakati wa likizo
MWONGOZO
Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - Grade 4 End Term 1 Exams 2023 Set 4
MASWALI
Bi. Wafula: Hamjambo wanafunzi?
Wanafunzi: Hatujambo Bi. Wafula, shikamoo.
Bi. Wafula: Marahaba wanafunzi. Natumai nyote mlikuwa na wikendi njema,
Wanafunzi: Naam Bi. Wafula, asante.
Bi. Wafula: (Huku akitabasamu) Leo katika kipindi chetu tutasoma kuhusu nyumbani. Je, nyumbani ni wapi?
Juma: Nyumbani ni mahali mtu anapoishi.
Bi. Wafula: Heko Juma! Maelezo hayo ni sahihi kabisa. Nyumbani kuna vyumba mbalimbali. Nipe mifano ya vyumba hivi?
Amani: (Kwa furaha) Nyumbani kuna vyumba kama vile sebule, chumba cha malazi, chumba cha kulia na pia mekoni.
Bi Wafula: Vizuri sana Amani. Hivyo basi leo tutaangazia sebule. Sebule ni chumba cha mapumziko. Sebuleni kuna vitu vingi sana kama vile?
Wanafunzi: (Kwa pamoja huku wakitazama picha vitabuni) Kuna makochi, meza, mtoto wa meza, runinga na pia pazia.
Bi. Wafula: Kweli kabisa, makochi na meza huundwa kwa mbao na kwa jina moja huitwa samani. Anayeunda vitu hivi kwa mbao huitwa seremala.
Maswali
- Wanafunzi na Bi. Wafula walipatana darasani baada ya
- juma
- siku
- wikendi
- likizo.
- Kulingana na mazungumzo haya, jibu la 'shikamoo' ni
- hatujambo
- aheri
- njema
- marahaba.
- Kipi si chumba kinachopatikana nyumbani kulingana na mazungumzo haya?
- Sebule.
- Chumba cha kuchezea.
- Mekoni.
- Chumba cha malazi.
- Vitu vinavyoundwa kwa mbao huitwa
- kochi
- meza
- runinga
- samani.
- Mtu anayeunda vitu kwa kutumia mbao huitwa
- seremala
- sonara
- mhunzi
- mwashi.
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali la 6-10.
Kijiji cha Pambana kilivamiwa na wezi sugu. Wezi hao walikuwa wakivunja milango ya nyumba za watu usiku na mchana. Walikuwa pia wakiwashambulia watu na kutoroka na mifungo yao. Vitendo hivi vya wizi vilendelea kuenea na kuongezeka. Hivyo basi, wanakijiji hawakuwa na budi ila kupiga ripoti kwenye kituo cha polisi.
Baada ya kuripoti, wanakijiji walishauriwa kuunda milango na nyua thabiti. Vilevile waliunda vikundi vya kujilinda wenyewe. Waliamua kushirikiana pamoja na polisi kupunguza hali ya uhalifu.
Baada ya miezi miwili, visa vya wizi vilipungua. Wanakijiji waliweza kurejea kwa shughuli zao za kila siku bila woga.
Maswali
- Taja jina la kijiji kulingana na kifungu.
- Pambazuko
- Kijiji
- Pambana
- Kituo.
- Kulingana na kifungu, nani aliyewashambulia wanakijiji na kutoroka na mifungo yao?
- Polisi
- Watu
- Wezi
- Wanakijiji wenzao.
- Visa vya wizi vilipoongezeka, wanakijiji walienda kupiga ripoti wapi?
- Shuleni
- Kortini
- Nyumbani
- Kituo cha polisi.
- Kulingana na kifungu hiki, wezi hawakuogopa kwani waliwashambulia wanakijiji wakati gani?
- Jumatatu na Ijumaa
- Asubuhi na jioni
- Wakati wa likizo
- Usiku na mchana.
- Visa vya wizi vilipungua baada ya miezi
- moja
- miwili
- sita
- mitatu.
Soma kifungu kifuatacho kwa makini kisha ujibu swali la 11-15
Hapo zamani paliishi sungura na rafiki yake ndovu. Sungura alikuwa mnyama mdogo kuliko ndovu lakini mjanja sana. Ndovu naye, ambaye pia huitwa tembo, alikuwa mkubwa sana na karimu. Ndovu alijitokea sana kusaidia sungura na wanyamapori wengine pale msituni.
Ndovu na sungura walishirikiana kwa kila jambo. Zaidi ya hayo, waliwalea watoto wao pamoja na kwa upendo. Wanyama wengine walitamani sana urafiki ule wa ndovu na sungura. Walijaribu pia kuwatenganisha lakini walishindwa.
Watoto wao pia walikuwa wakiiga urafiki ule wa wazazi wao. Walicheza, kula na kulala pamoja. Kwa kweli, mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.
Maswali
- Sungura na ndovu walikuwa
- ndugu
- marafiki
- adui
- wanakijiji.
- Sungura na ndovu waiishi wapi?
- Nyumbani
- Mitini
- Milimani
- Msituni.
- Watoto wa sungura na ndovu walikuwa wakipendana kwa sababu ya
- urafiki wa wazazi wao
- hasira za wazazi wao
- kutojuana
- njaa.
- Ni nini kilichofanya wanyama wengine kuwa na tamaa?
- Uadui wa sungura na ndovu.
- Watoto wa sungura na ndovu.
- Kusaidiana kwa ndovu.
- Urafiki wa ndovu na sungura.
- Ndovu alikuwa na ukarimi kwa nini?
- Alimpiga sungura.
- Alisaidia sungura na wanyama wengine.
- Aliwafukuza wanyama wengine.
- Hakuwapenda watoto wake.
Soma kifungu kifuatacho kwa makini kisha ujaze pengo kwa majibu sahihi (16-20).
Pendo alikuwa msichana wa shule yetu ..................16............... alikuwa mrembo sana. Wazazi wake walikuwa maskini sana. ..................17............. kumpeleka kwa shangazi yao aliyekuwa tajiri ..................18...............
Pendo alihamia kwa shangazi yake aliyempenda kama mwana ..................19...............Pendo naye akaamua kusoma vitabu ..................20............... kwa bidii.
-
- Sisi
- Mimi
- Yeye
- Wao
-
- Tuliamua
- Waliamua
- Aliamua
- Mliamua
-
- sana
- mbali
- nyingi
- kidogo
-
- chake
- wake
- zake
- lake
-
- wake
- zake
- chao
- vyake
Kuanzia swali la 21 hdi 30, jibu kila Swali kulingana na maagizo uliyopewa.
- Bibi na pipi ni vitate. Vile vile, kitate cha papa ni
- bata
- paka
- kata
- baba
- Mama amenunua rinda..................................
- mwekundu
- jekundu
- lekundu
- nyekundu
- Chagua neno ambalo ni si kitenzi kati ya haya.
- Cheza
- Kula
- Lia
- Mwalimu
- Jibu la salamu 'alamsiki' ni .....................................
- binuru
- nawe pia
- aheri
- buriani
- Kabla ya kuvuka njia, Juma alisimama ....................... barabara.
- juu ya
- kando ya
- ndani ya
- katika ya
- Tambua kiunganishi katika sentensi hii.
Mtoto aliadhibiwa kwa sababu ya utundu wake.- mtoto
- aliadhibiwa
- kwa sababu
- utundu
- Tegua kitendawili kifuatacho.
Popote niendapo hunifuata.- Macho
- Kivuli
- Mtoto
- Rafiki.
Tumia kielezi sahihi kukamilisha sentensi hizi.
- Chui hukumbia..................................
- mbio
- polepole
- kabisa
- ovyo
- Kobe hutembea .................................
- ovyo
- haraka
- polepole
- sana.
- Andika wingi wa sentensi ifuatayo.
Mwanafunzi anasoma kitabu.- Mwanafunzi anasoma vitabu.
- Wanafunzi wanasoma kitabu.
- Mwanafunzi wanasoma kitabu.
- Wanafunzi wanasoma vitabu.
- Chagua alama ifaayo kuakifisha sentensi ifuatayo.
Je...............................wewe utaenda kwao?- ,
- !
- ?
- " "
INSHA
Andika insha ya kusisimua kuhusu:
SIKU YA KUFUNGA SHULE
..........................................................................................................................................................................................................................................

Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - Grade 4 End Term 1 Exams 2023 Set 3
MASWALI
Kusikiliza na kuzungumza
Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali 1-5
(Runo ameketi kwenye kivuli pamoja na baba yake wakizungumziana)
Runo: (akimsogelea Baba) Shikamoo Baba?
Baba: (kwa tabasamu) Marahaba mwanangu! Habari za shule?
Runo: Njema baba! (kimya) Baba, nikwambie tulichosoma leo?
Baba: Naam, nieleze mwanangu!
Runo: Leo tulifunzwa kuhusu nidhamu mezani.
Baba: Hilo ni somo zuri sana.
Runo: Mwalimu alituelezea kidogo kisha akatuambia tujadiliane na wazazi wetu. Nidhamu mezani ni nini?
Baba: Aha! Runo, nidhamu mezani ni tabia nzuri ya mtu kabla ya kula, anapokula na baada ya kula.
Runo: Ooh! Nimeelewa.
Baba: Mwanangu, kabla hujala unafaa kunawa mikono kwa maji safi na sabuni.
Runo: Naam baba. Aidha ninafaa kumshukuru Mungu kwa chakula.
Baba: Ndio Runo. Pia hufai kupakua chakula ambacho huwezi kumaliza. Kama utabakisha hufai kumwaga. Unafaa kukiweka ule baadaye.
Runo: Kweli Baba! Ni vibaya sana kumwaga chakula. Kuna watoto kama mimi ambao hawana chakula.
Baba: Umeongea ukweli. Je, ukimaliza kula unafaa kufanya nini?
Runo: (Kwa ujasiri) Kumshukuru aliyenipatia chakula na kunawa mikono yangu.
Baba: Vyema! Unastahili pia kuondoa vyombo ulivyotumia na kuvipeleka jikoni ili vioshwe.
Runo: Asante baba! Hakika umenifunza mengi.
- Runo alipoulizwa na baba kuhusu habari za shule. Alimjibu vipi?
- Naam
- Njema
- Shikamoo
- Marahaba
- Maneno yafuatayo yametumiwa katika mazungumzo. Lipi linaonyesha kushukuru kwa wema uliofanyiwa?
- Karibu
- Naam
- Asante
- Kweli
- Ni jibu lipi linaloonyesha nidhamu ambayo Baba alimfunza Runo?
- Kunawa mikono, kupakua chakula utakachomaliza, kuondoa vyombo baada ya kula.
- Kumwaga chakula, kupakua chakula utakachomaliza, kupeleka vyombo jikoni
- kupakua chakula utakachomaliza, kuomba, kumshukuru aliyekupa chakula.
- Kuweka chakula kilichobaki, kunawa mikono, kuwa mlafi
- Baada ya mazungumzo:
- Runo alimuaga baba yake.
- Runo alimshukuru baba yake.
- Baba alimuaga Runo
- Baba alimshukuru Runo.
- Neno nidhamu lina maana gani?
- Mienendo mibaya
- Tabia ya kula
- Tabia nzuri
- Kuwatii wakubwa wetu
Soma hadithi ifuatayo kisha ujibu maswali 6-9
Siku moja Sungura aliamka kabla ya jua kuchomoza. Alianza safari ya kwenda kumtembelea rafiki yake. Hakutaka kuchelewa kufika. Alipanda milima na kuvuka mabonde. Jua lilipochomoza, aligundua kuwa alikuwa amepotea njia. Alikuwa anaelekea Mashariki badala ya Magharibi.
Alisimama na kushindwa na la kufanya. Alimwona kobe aliyekuwa kichakani na kumwomba amsaidie. Kobe alimwuuliza upande aliokuwa akienda. Sungura alimwambia alikuwa akienda Mashariki alikoishi rafiki yake. Kobe alimwambia kuwa jua huchomoza upande wa Mashariki wa dira kila asubuhi.
Sungura aligundua kuwa mgongo wake ulifaa kuelekea upande jua lilikuwa likitokea nao uso upande ambao jua lilikuwa likielekea. Alimshukuru kobe sana kwa kumsaidia. Aliendelea na safari yake akiwa na furaha kubwa.
- Nyumbani kwa rafiki wa Sungura kulikuwa upande gani kutoka kwa Sungura?
- Mashariki
- Magharibi
- Kaskazini
- Kusini
- Kwa nini Sungura aliamka mapema? ili
- apande milima na kuvuka mabonde.
- aone jua likichomoza.
- aulize kobe kwa rafiki yake
- asichelewe kufika kwa rafiki yake.
- Kwa nini kobe ni rafiki mzuri?
- Alimwonyesha Sungura njia.
- Alikutana na Sungura njiani.
- Anajua upande ambao jua huchomoza.
- Alikubali kuongea na Sungura.
- Kifungu ulichosoma kina aya ngapi?
- Nne
- Mbili
- Tatu
- Tano
Soma hadithi ifuatayo kisha ujibu maswali 10-12
Katika kipindi cha Kiswahili mwalimu wetu Bwana Ujuzi alitufundisha kuandika kwa kutumia tarakilishi.
Alituonyesha sehemu mbalimbali za kompyuta, majina yake pamoja na njia za kuzitumia.
Sehemu hizo ndizo hizi:
Alituambia kuwa kabla hatujaanza kutumia kompyuta, tuhakikishe ina umeme wa kutosha. Baada ya hayo tubonyeze kitufe cha kuwashia tarakilishi. Ikiwaka alituambia tuweke nenosiri kwa kupiga taipu neno hilo. Isitoshe alituambia kuwa baada ya kukamilisha kazi tuihifadhi. Mwishowe alituambia tuifunge kompyuta.
- Ni sehemu gani hutumiwa mtu anapopiga taipu?
- Kipanya
- Bodidota
- Kiwambo
- Kitengo kikuu cha uchakataji
- Mwalimu alipatiana hatua ngapi mtu anapotumia tarakilishi?
- Nne
- Sita
- Tano
- Tatu
- Kwa nini mtu huweka nenosiri katika tarakilishi yake?
- Ili isifunguliwe na mtu mwingine bila ruhusa
- Ili kompyuta isiibwe
- Ili mtu aweze kuitumia vizuri
- Ili tarakilishi isiharibike
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 13-15.
Jayda amezaliwa na kulelewa jijini Nairobi. Wazazi wake Bwana na Bi. Akili wamemlea vizuri sana. Huwa wanahakikisha amepata haki zake kama vile: lishe bora, Makao mazuri, mavazi ya kupendeza, huduma za afya na elimu katika shule nzuri.
Jayda pia hushauriwa na wazazi wake kuwa na nidhamu.
Hufundishwa kuwa na tabia nzuri na kutumia wakati wake kwa njia inayofaa. Zaidi ya hayo hufundishwa kuwa na heshima kwa wakubwa na wadogo. Isitoshe huwa wanamwelekeza kuwa na bidii katika shughuli zote za maisha. Kila akikosea huwa anarekebishwa na kupewa ushauri nasaha.
Ni kweli kusema kuwa wazazi wa Jayda wanaelewa umuhimu wa malezi bora. Wahenga walisema kuwa mtoto umleavyo ndivyo akuavyo
- Kulingana na kifungu ulichokisoma ni gani kati ya haki hizi haijatajwa?
- Haki ya kupata lishe bora
- Haki ya elimu
- Haki ya kucheza
- Haki ya kupewa mavazi mazuri
- Wazazi wa Jayda humfanyia nini anapokosea?
- Kumwadhibu
- Kumpeleka kwa mwalimu
- Kumchapa
- Kumrekebisha na kumpa ushauri nasaha.
- Ni Methali gani imetumiwa katika kifungu hiki?
- Ushauri nasaha
- Ni kweli kusema kuwa
- Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo
- Amezaliwa na kulelewa
Soma kifungu kifuatacho. Kina nafasi 16 hadi 20. Umepewa majibu manne hapo. Chagua jibu lifaalo Zaidi kati ya yale uliyopewa.
Mwalimu .....................16................. wa Kiswahili hufundisha .....................17................. sana. Ametufundisha vielezi kama vile polepole na .....................18................. Yeye pia hutufundisha kutumia .....................19................. ili tujue maana za maneno. Kila anapokamilisha kipindi hutuaga .....................20................. nasi husema kwaheri ya kuonana.
-
- wangu
- yangu
- changu
- langu
-
- nzuri
- vizuri
- uzuri
- mizuri
-
- kwa sababu
- lo!
- chini ya
- haraka
-
- kamusi
- bibilia
- madaftari
- kalamu
-
- hamjambo
- shikamoo
- kwaheri
- buriani
Kutoka swali 21-30, chagua jibu sahihi.
- Tazama picha hii kisha ujibu swali
Chombo hiki huitwaje?- Saa
- Dira
- Kipimajoto
- Televisheni
- Tumia Maneno ya adabu badala ya 'kuenda chooni'
- Kuenda msalani
- kukojoa
- kutapika
- kujifungua
- Hali ya mtu kuipenda nchi yake sana na kuwa tayari kuifia ni
- Ufisadi
- Uzalendo
- Umoja
- Uwiano
- Chagua wingi wa: Mwalimu wangu ananipenda sana.
- Mwalimu wako anatupenda sana.
- Walimu wangu wanatupenda sana.
- Mwalimu wetu anatupenda sana.
- Walimu wetu wanatupenda sana.
- Ni kundi gani lina mpangilio mzuri wa maneno kama yatakavyofuatana katika kamusi?
- Kula, pakua, pika, nawa
- Salamu, salama, salimu, sala
- Kinu, kisu, mchi mwiko
- Zulia, tumbuu, pazia, fremu
- Nomino hizi zote ziko katika ngeli ya A-WA isipokuwa
- kuku
- mtu
- mwizi
- mti
- Kitendawili! Tunamsikia lakini hatumuoni
- mbuzi
- Kioo
- Pikipiki
- Sauti
- Unapoandika insha ya barua mtu huanza na nini?
- Anwani
- Tamati
- Kimalizio
- Mwili
- Tumia kihusishi sahihi? Kikombe kimewekwa ............................ meza.
- mbele ya
- kando ya
- chini ya
- juu ya
- Tazama picha kisha ujibu swali. Vazi hili linaitwaje?
- Kaptura
- Sketi
- Rinda
- Chupi
KISWAHILI: INSHA
Muda: Dakika 40
Mwandikie baba yako barua ukimwelezea vile unavyoendelea katika masomo yako.
MWONGOZO
Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - Grade 5 End Term 1 Exams 2023 Set 4
KUSIKILIZA NA KUZUNGUMZA
Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali
(Ni siku ya Jumamosi asubuhi. Sofia anakutana na Pendo barabarani)
Sofia : (akimkumbatia) Sabalkheri rafiki yangu!
Pendo : (kwa tabasamu) Aheri sahibu yangu.
Sofia : Leo umevalia mavazi ya kupendeza na kujipamba kwa mapambo ya kipekee. Unaenda wapi?
Pendo : Ninaelekea kanisani kuhudhuria harusi ya shangazi yangu. Harusini ni lazima mtu awe maridadi kama
kipepeo.
Sofia : (Akimtazama kwa makini) Naomba unieleze baadhi ya mapambo yako.
Pendo : Nitafurahia kufanya hivyo. Kwanza shingoni nimevaa mkufu na kidami.
Sofia : Na kwenye kiwiko cha mkono umevaa pambo gani?
Pendo : (Akimwonyesha) pambo hili linaitwa bangili.
Sofia : Asante. Ninaona linametameta sana.
Pendo : Puani pia nina kikero na kipini. Kipini ni hiki kwenye upande wa kushoto wa pua na kikero kwenye
upande wa pua.
Sofia : Ninaona pia una vipuli masikioni.
Pendo : Ndiyo. Hivi nilinunuliwa na mama yangu.
Sofia : Kusema kweli sijawahi kuona ukivutia hivi. Nitakuruhusu uende ili usichelewe kufika harusini.
Pendo : Kwaheri!
Sofia : Kwaheri ya kuonana.
- Sofia na Pendo walikutana wakati gani?
- Jioni
- Asubuhi
- Adhuhuri
- Usiku
- Maneno yafuatayo yametumiwa katika mazungumzo. Lipi ni la maagano
- Sabalkheri
- Aheri
- Asante
- Kwaheri
- Pendo alikuwa amevaa mapambo haya yote isipokuwa
- Kidani
- Mkufu
- Kikero
- Herini
- Kulingana na mazungumzo haya jina rafiki lina maana sawa na
- ndugu
- pendo
- sofia
- sahibu
- Katika mazungumzo uliyoyasoma Pendo na Sofia walizungumzia nini hasa?
- Harusi
- Mapambo
- Mavazi
- Kanisa
Swali la 6 hadi la 9
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
Likizo yangu ya katikati ya muhula ilikuwa na shughuli nyingi. Tuliporuhusiwa kwenda nyumbani nilifurahi sana kwa sababu nilikuwa nimewajibika vizuri katika masomo yangu shuleni. Nilikuwa nikikamilisha shughuli zangu zote darasani, miradi yangu ilikuwa bora zaidi darasani, usafi wangu na nidhamu zilikuwa za hali ya juu
Wazazi wangu walikuwa wameniahidi zawadi kama ningekuwa na ripoti nzuri kutoka kwa mwalimu. Bila shaka ripoti yangu ilikuwa ya kupendeza. Wazazi wangu walipoiona walifurahi sana. Nilinunuliwa tableti ya kunisaidia kufanya kazi yangu ya shuleni pamoja na kuwasiliana na wenzangu.
Katika likizo hiyo fupi niliwasaidia wazazi wangu kufanya shughuli za kilimo na ufugaji wa ng'ombe. Nilisaidia kupanda mahindi na maharagwe shambani kwa sababu mvua ilikuwa karibu kunyesha. Aidha nilisaidia kuwakatia ng'ombe majani, kuwapa maji, kukama na kuenda kuuza maziwa. Wazazi wangu walifurahia sana kwa kuwasaidia katika kazi.
Isitoshe nilifanya mradi tuliokuwa tumepewa na mwalimu wetu wa Kiswahili. Mradi huo ulikuwa kukusanya mapambo mbalimbali. Wazazi wangu walishirikiana nami kutafuta mapambo hayo.
Nilifurahia sana likizo hiyo na niliporudi shuleni niliendelea na masomo yangu vyema.
- Likizo iliyozungumziwa ni gani?
- Ya mwezi wa nane
- Ya mwezi wanne
- Ya mwisho wa mwaka
- Ya katikati ya muhula
- Kwa nini mwandishi alinunuliwa rununu?
- Kwa kupata ripoti nzuri kutoka kwa mwalimu
- Kwa kukamilisha kazi yake shuleni
- Kwa kuwa mwanafunzi safi zaidi
- Kwa sababu ilikuwa likizo
- Ni kweli kusema kuwa wazazi wa mwandishi:
- Hufuga kuku
- Hukuza mimea na kufuga ng'ombe
- Ni wakulima na wafanyabiashara
- Ni wakulima na walimu
- Hali ya mwandishi kufanya kazi pamoja na wazazi wake inadhihirisha maadili gani?
- Ukarimu
- Utengano
- Umoja
- Usawa
Swali la 10 hadi la 12
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
Taji ni mvulana anayependa kula lishe bora. Ameupanga mlo wake vizuri ili asikose viini lishe muhimu katika mwili wake. Kabla ya kula chakula huwa anakula matunda na kungoja dakika thelathini. Licha ya hayo huwa anakunywa maji ya kutosha kila siku. Ifuatayo ndiyo ratiba yake. Lishe bora humsaidia kuwa na afya nzuri na kuweza kufanya shughuli zake vyema. Ifuatayo ni ratiba yake.
Asubuhi | Adhuhuri | Jioni |
Maziwa glasi moja | Pilau | Ugali |
Viazi vikuu | Nyama ya samaki | Maharagwe |
Mboga za kiasili | Sukumawiki | Mboga za kiasili |
Embe moja | Embe moja | Papai moja |
- Chakula ambacho Taji hula siku inapoanza ni gani?
- Kilalio
- Matunda
- Kifungua kinywa
- Maji
- Ni chakula gani ambacho Taji hula katika kila mlo?
- Mboga za kiasili
- Matunda
- Pilau
- Ugali
- Kwa nini Taji hula lishe bora?
- Ili awe na afya bora
- Ana ratiba nzuri
- Kwa sababu ni mvulana
- Ili ashibe
Swali la 13 hadi la 15
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
Hapo zamani za kale Kuku na Kanga walikuwa marafiki. Marafiki hawa walikuwa na maumbile sawa. Walifanya mambo yao pamoja. Walichakura pamoja wakitafuta chakula. Vifaranga wao nao walicheza pamoja.
Siku moja Kuku alimwomba Mwewe sindano ili awashonee vifaranga wake fulana. Mwewe alikuwa jirani yao. Baada ya kuitumia sindano hiyo, Kuku aliiweka kabatini. Kuku alipokwenda kutafuta chakula, kifaranga wake mmoja alichukua sindano hiyo. Alianza kushona kitambaa jinsi alivyomwona mama yake akishona.
Mwewe alipotaka sindano yake, Kuku aliitafuta kabatini, hakuipata. Kifaranga aliyechukua sindano hiyo alimwambia mama yake kwamba sindano ilipotea. Kuku aliwaambia vifaranga wake waanze kuchakura ili watafute sindano ya Mwewe. Waliitafuta sindano kila mahali bila mafanikio.
"Usiponipa sindano yangu nachukua kifaranga mmoja kila siku," Mwewe alimwambia kuku. Mwewe alianza kuchukua kifaranga mmoja kila siku. Vifaranga wa Kuku na Kanga walianza kupungua. Kanga alipojua kilichokuwa kinaendelea, aliamua kuwachukua vifaranga wake waliobaki na kwenda kichakani. Aliwabandika vitone vya pamba kwa kutumia gundi. Wakawa na madoa meupe. Mwewe alishindwa kuwatambua.
Ukiwaona kuku na Kanga wanachakura, jua tu bado wanatafuta sindano ya Mwewe.
- Vifaranga wa Kuku na Kanga walifanya nini pamoja?
- Kuchakura wakitafuta chakula
- Kuchakura wakitafuta sindano ya mwewe
- Walicheza pamoja
- Kulala pamoja
- Kuku anawajali vifaranga wake kwani:
- Alitaka kuwashonea fulana.
- Aliomba sindano
- Aliwashonea kitambaa
- Alicheza nao
- "Mwewe alishindwa kuwatambua. "Neno kuwatambua lina maana gani?
- Kuwala
- Kuwaona
- Kuwajua
- kuwapenda
Soma kifungu kifuatacho. Kina nafasi 16 hadi 20. Umepewa majibu manne hapo. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.
Timu ___16___ shule yetu ilishiriki katika mechi. ___17___ walikuwa wakiwashangilia ili washinde. Mchezaji ___18___ alianguka na kupata ___19___ miguuni na mikononi. Maskauti walimpa ___20___ kisha akapelekwa zahanatini.
A | B | C | D | |
16. | wa | ya | kwa | mwa |
17. | Wanafunzi | Watu | Mashabiki | Walimu |
18. | wa moja | kimoja | moja | mmoja |
19. | majeraha | alama | damu | vidonda |
20. | zawadi | huduma ya kwanza | matibabu | ibada |
Swali la 21-30
SARUFI
- Tazama picha hizi kisha ujibu maswali
Shughuli zilizo kwenye picha ni za ________________________- Kujipamba
- Huduma ya kwanza
- Mapishi
- Kilimo
- Chagua jibu lenye nomino za aina moja.
- Kenya, Alhamisi
- kiti, ukweli
- Thurea, meza
- Mwanajeshi, furaha
- Chagua sentensi iliyoakifishwa kwa usahihi.
- Kuku anapenda, kuchakura mchangani?
- Unakula nini, siku ya Jumapili.
- Je, Mto Athi una samaki wengi?
- Tito atawaheshimu walimu wake,
- Chagua jibu sahihi kujaza nafasi. ________________ za babu yangu zilitengenezwa na seramala hapo _________________
- Zamani, samani
- Thamani, samani
- Samani, zamani
- Amani, zamani
- Panga maneno haya kama yanavyofuatana katika kamusi.
(filamu, firimbi, fyonza, fulana, faulu)- Fyonza, fulana, firimbi, filamu, faulu
- Faulu, filamu, firimbi, fulana, fyonza
- Faulu, fulana, fyonza, filamu, firimbi
- Faulu, filamu,fulana, firimbi, fyonza
- Nomino zifuatazo zinafaa kuwa za ngeli moja. Chagua nomino iliyo katika ngeli tofauti.
- Saa
- Pete
- Barua
- Joto
- Andika sentensi ifuatayo katika wingi. Kalamu ya wino ilitumiwa na mwanafunzi.
- Kalamu za wino zilitumiwa na wanafunzi.
- Kalamu vya wino vilitumiwa na wanafunzi
- Kalamu za wino zilitumiwa na mwanafunzi
- Kalamu ya wino ilitumiwa na wanafunzi.
- Ni maamkuzi au maagano gani hayajaambatanishwa vizuri na jibu lake?
- Shikamoo- marahaba
- Alamsiki- nawe pia
- Kwaheri- ya kuonana
- Buriani- buriani dawa
- Kifaa hiki hutusaidia kujua __________________________
- wakati
- hali ya anga
- sehemu
- hali ya joto mwilini
- Jina la heshima la kumwita mwanamume ni _________________________
- bibi
- bwana
- ndugu
- somo
INSHA
Andika insha kuhusu mada ifuatayo:
HARUSI YA KUPENDEZA
MARKING SCHEME
- B
- D
- D
- D
- B
- B
- A
- B
- C
- B
- B
- A
- C
- A
- C
- B
- A
- D
- A
- B
- C
- A
- C
- C
- B
- D
- A
- B
- A
- B
Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - Grade 5 End Term 1 Exams 2023 Set 2
MAAGIZO
Karatasi hii ina sehemu tano kuu.
Jibu maswali yote kulingana na maagizo.
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata.
Fisi na wenzake walialikwa katika sherehe kubwa kule mjini. Pamoja na Fisi, wanyama wengine walioalikwa walikuwa Sungura, Ndovu na Nyoka. Sherehe hiyo ilikuwa ya harusi kati ya Chui na Kondoo. Walipofika katika sherehe hiyo, walipata sherehe ilikuwa imeanza. Baada ya nyimbo kuimbwa, wakati wa kuunganishwa ulifika. Chui na Kondoo walitangazwa kuwa mke na mume. Shangwe na kelele zilisikika hewani. Hatua iliyofuata ilikuwa ya kufurahia mlo. Huo ndio wakati ambao fisi alikuwa amesubiri kwa hamu. kuu.
Jambo lililomfurahisha fisi kabisa ni kuwa kila mmoja alipewa nafasi ya kujipakulia. Fisi alijaza sahani yake kwa nyama za kila aina: kuku, mbuzi, samaki, ng'ombe. Pia alichukua matunda na mboga. nyingi sana ingawa hakupenda kula mboga na matunda. Hata kabla ya kuanza kula, kelele zilisikika kuwa moto ulikuwa ukiwaka katika nyumba hiyo. Wanyama wengine wote walianza kutoroka. Fisi alishangaa iwapo alifaa kuacha chakula ama aendelee kula. Aliendelea kufurahia vipande vya nyama huku akiramba vidole. Mara moto ulikuwa umemfikia. Alipiga kelele lakini moto ulikuwa umemfikia. Ingawa aliweza kutoka nje, miguu yake ya nyuma ilichomeka.
- Ni nini kilichofanyika kabla ya Chui na Kondoo kutangazwa kuwa mke na mume?
- Moto ulianza kuwaka
- Shangwe na kelele zilisikika
- Chakula kilianza kuliwa
- Nyimbo ziliimbwa
- Kifungu kinaeleza kuwa wanyama katika sherehe hiyo walikuwa aina wangapi?
- 4
- 6
- 5
- 7
- Kisa hiki kinaeleza sababu ya;
- fisi kupenda kula.
- miguu ya fisi kuwa mifupi.
- fisi kutojua kukimbia.
- fisi kutopenda nyama.
- Kutokana na kisa hiki, tunajifunza kuwa;
- tusiende sherehe.
- wanyama wasikusanyike pamoja.
- tamaa ni mbaya.
- chakula kisiliwe katika harusi.
- Lengo kuu la fisi kuhudhuria sherehe lilikuwa gani?
- kufurahia nyimbo
- kufurahia harusi
- kukutana na wenzake
- kufurahia chakula
- Methali gani inayoweza kueleza kisa hiki?
- Tamaa mbele mauti nyuma.
- Polepole ndio mwendo.
- Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.
- Achanikaye kwenye mpini hafi njaa.
Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata.
Siku moja wakati wa likizo ya muhula wa kwanza, Kalondu aliamshwa asubuhi na mapema. Kwa kuwa Kalondu hakuenda shuleni, mama yake alimpa maagizo kabla ya kutoka. Mama yake alikuwa akienda sokoni Butere ambako aliuza vyombo mbalimbali vya kutumia jikoni. Kabla ya kutoka, mama yake alimwambia kuwa asitoke nyumbani. Hii ni kwa sababu wezi wangeingia nyumbani kwao na kuiba vitu katika nyumba. Pili aliambiwa kuwa asitumie kifaa chochote cha kidijitali kuingia mtandaoni bila idhini ya mama yake.
Mama alimwacha akinywa chai pale sebuleni huku akitazama vibonzo kwenye runinga. Kalondu alipomaliza kunywa chai, alishindwa cha kufanya. Alitoka nje ya nyumba na kuona kuwa watoto wengine walikuwa wakiendesha baiskeli njiani. Alijipenyeza polepole na kutoka nje ya boma. Watoto hao walimpa baiskeli na kumwambia kuwa asiendes he haraka. Kalondu alianza polepole lakini baada ya muda kidogo aliendesha haraka sana. Mara alianguka chini kwenye jiwe. Kalondu aliumia goti lake na mkono.
- Kwa nini Kalondu hakuwa ameenda shuleni siku hiyo?
- mama yake alimkataza
- mama yake alitaka kuenda sokoni
- ilikuwa siku ya Jumamosi
- ulikuwa wakati wa likizo
- Kwa nini mama alimshauri Kalondu asitoke nyumbani?
- Ili wezi wasiingie nyumbani kwao na kuiba
- Ili asiumie wakati akiendesha baiskeli
- Ili asipotee akiwa peke yake
- Ili asaidie kufanya kazi za nyumbani
- Unadhani kwa nini mama hakutaka Kalondu atumie kifaa cha kidijitali kuingia mtandaoni bila idhini?
- Kwa kuwa ni vibaya kutumia kifaa cha kidijitali
- Kwa kuwa hakiwezi kufanya kazi kama mama hayuko
- Kwa kuwa angejipata kwenye mitandao isiyofaa
- Pengine kifaa hicho kilikuwa kimeharibika
- Ungekuwa Kalondu, ungefanya nini baada ya kunywa chai?
- Ningerudi kulala
- Ningesoma kitabu cha hadithi
- Ningeenda nje kucheza
- Ningeenda jikoni kupika
- Methali gani ambayo haiwezi ikatumika kumshauri Kalondu?
- Harakaharaka haina baraka.
- Asiyesikia la mkuu huvunjika guu.
- Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.
- Pole pole ndio mwendo.
- Yawezekana kuwa mama wa Kalondu aliuza nini kati ya vifaa vifuatavyo?
- kikaango
- baiskeli za watoto
- viti
- vitabu
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata.
Maji yana umuhimu sana katika maisha yetu. Hutumika kufanya mambo mbalimbali maishani. Jambo la msingi ni kuwa maji hutumika katika upishi na kudumisha usafi. Kutokana na hayo, ni jambo la busara kuyatunza maji. Hatufai kuyaharibu maji kwa njia yoyote. Vilevile, tusichafue vyanzo vya maji kama vile mito na bahari. Shughuli kama vile kuoga na kufua hazifai kufanyikia kwenye mito, bahari na maziwa. Uharibifu wa bahari, mito na maziwa huweza kuwaangamiza viumbe wa majini kama vile samaki na kaa. Kila mkenya anafaa kuyajali mazingira yao. Tukihifadhi mazingira, tutaishi maisha bora yasiyokuwa na matatizo mengi.
- Ni kweli kuwa maji hutumika kufanya;
- mambo mengi.
- mambo machache.
- mambo mawili.
- mambo ya mbali.
- Ni keli kuwa maji;
- yanajua kupika.
- hayafai kutunzwa.
- hutumika katika usafi.
- hayana faida maishani.
- Tunafaa kufanya nini ili tuishi maisha yasiyokuwa na matatizo mengi?
- Kuzingatia lishe bora
- Kunywa maji mengi
- Kutooga mtoni
- Kuhifadhi mazingira
Chagua jibu linalofaa ili kujazia kila nafasi iliyoachwa.
Siku 16 Juma alikuwa akicheza uwanjani. Rafiki 17 ambaye wanapendana sana alijiunga na yeye. Walianza kucheza huku wakiruka 18 furaha. Walipomaliza, waliingia 19 wakala chakula kitamu sana. Walipomaliza kula, walikunywa maji 20 kisha wanaenda kumsaidia mzazi wa Juma kukusanya kuni kwenye shamba lao.
16 | A. moja | B. kimoja | C. mmoja | D. umoja |
17 | A. wake | B. wangu | C. zake | D. yake |
18 | A. kwenye | B. katika | C. na | D. kwa |
19 | A. kwa nyumba | B. katika nyumba | C.ndani mwa nyumba | D.katika nyumbani |
20 | A. mingi | B. mengi | C.nyingi | D.wengi |
Jibu maswali yanayofuata kulingana na maagizo.
- Jibu gani linaloonyesha nomino ya wingi?
- maji
- kalamu
- kitabu
- magari
- Onyesha pambo ambalo huvaliwa kwenye shingo.
- kikero
- herini
- bangili
- ushanga
- Chagua sentensi iliyotumia nomino ya dhahania.
- Tutaenda Mombasa kesho.
- Maji safi ni ya mgeni.
- Mpira wake ni mpya.
- Uzalendo ni muhimu kwetu.
- Chakula gani ambacho huokwa kati ya vyakula vifuatavyo?
- nyama
- keki
- mihogo
- ugali
- Umati ni wa watu kama vile mkungu ni wa
- ndizi
- maua
- mboga
- funguo
- Nomino za pekee zinahusu yafuatayo isipokuwa;
- Majina ya miezi ya mwaka
- Majina ya siku za wiki
- Majina ya mahali
- Majina ya vyakula
- Panga maneno yafuatayo jinsi yanavyofuatana kwenye kamusi.
- mchana
- mdudu
- mama
- mbuzi
- ii, iii, iv, i
- iii, iv, i, ii
- iii, ii, iv, i
- i, ii, iii, iv
- Jibu gani linaloonyesha matumizi ya herufi kubwa?
- Hutumika mwishoni mwa sentensi
- Hutumia kuanzisha nomino za pekee
- Hutumika kuandika mkato wa maneno
- Hutumika kuonyesha wingi wa nomino
- Unapotumia tarakilishi, kile unachokiandika huonekana kwenye
- bodidota
- kiwambo
- kebo
- kitengo kikuu cha uc' ukataji
- 'Koma' pia huitwa
- kiulizi
- mkato
- kikomo
- kitone
INSHA
Andika insha ya masimulizi kuhusu;
MKASA WA MOTO KIJIJINI.
MARKING SCHEME
- D
- B
- B
- C
- D
- A
- D
- A
- C
- B
- C
- A
- A
- C
- D
- A
- D
- D
- B
- B
- A
- D
- D
- B
- A
- D
- B
- D
- B
- B
Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - Grade 4 Mid Term 1 Exams 2023 Set 2
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 1-5.
Kabla ya kwanza kufua nguo hakikisha una besheni, sabuni maji safi na mahali pa kwanika. Hakikisha kuwa kuna jua au upepo. Usipange kufua nguo wakati mvua inanyesha. Tenga nguo zinazotoa rangi na zile ambazo hazitoi rangi. Tenga pia nguo chafu sana kutoka kwa zile ambazo si chafu sana usifue soksi na hanchifu pamoja. Soksi huwa na uchafu mwingi.
Mimina maji ya kutosha kwenye besheni. Tia sabuni kipimo kinachotosha, kama ni sabuni ya unga. Koroga maji hadi povu liwe jingi weka nguo zako kwenye besheni ukitanguliza zile nyeupe. Sugua nguo zako taratibu ukiangazia zaidi sehemu zenye uchafu. Sugua mpaka ziwe safi..
- Ni kipi hakihitaji kati ya hivi unapoanza kufua 4. nguo?
- Sabuni
- Maji safi
- Beseni
- Jokofu
- Ni wakati gani mwafaka wa kufua nguo? Wakati
- wa mvua
- wa jua au upeро
- kuna mawingu
- kuna jua
- Ni vazi lipi halifai kufulia pamoja na mengine?
- Soksi
- Rinda
- Hanchifu
- Kaptura
- Kwa nini unafaa kukoroga maji baada ya kuongeza sabuni ya unga?
- Ili povu liwe jingi
- Ili kutoa nguo chafu
- Ili maji yawe safi
- Ili kupasha maji joto
- Ni sehemu ipi katika nguo inayofaa kusuguliwa zaidi unapofua nguo?
- Sehemu nyeupe
- Sehemu iliyo chafu
- Sehemu yenye doa
- Sehemu iliyo na rangi
Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu swali 6-10.
Simba alitangaza nafasi ya naibu wake. Alitaka asaidiwe kuwaongoza wanyama. Ndovu, Sungura, Kobe na fisi walituma maombi yao. Simba aliona bora awape mtihani ili mshindi awe ndiye naibu wake.
"Nina jogoo ambaye hutaga mayai kila siku mlimani. Je, kutakuwa na mayai mangapi baada ya wiki moja?" Simba aliwauliza. Jibu la ndovu lilikuwa mayai saba. Sungura naye alisema mayai matano. Kobe aliandika sufuri huku fisi akiandika mayai kumi na manne.
- Ni mnyama yupi kati ya hawa ambaye hajatajwa kwenye kifungu?
- Fisi
- Kobe
- Sungura
- Ngiri
- Simba alitangaza nafasi gani katika himaya yake?
- Msaidizi wake
- Mpishi wake
- Naibu wake
- Mlinzi wake
- Ndovu alitoa jibu lipi?
- Saba
- Matano
- Kumi na manne
- Sufuri
- Ni mnyama yupi aliyekuwa kiongozi wa wanyama waliotajwa kwenye kifungu?
- Kobe
- Sungura
- Simba
- Ndovu
- Je, unafikiria ni mnyama yupi aliyeshinda na kuwa naibu wa Simba?
- Ndovu
- Kobe
- Sungura
- Simba
Soma kifungu hiki kisha ujaze nafasi zilizoachwa wazi 11-19.
Juma alikuwa mwana ___11___ pili katika familia ya Bwana Wanjuma. Mama ___12___ aliaga dunia kutokana na ugonjwa wa saratani. Baadaye baba yake akao mke mwingine wa ___13___ Juma na watoto wao wengine. Mama wa Kambo alianza kwatesa ___14___ baba yao hakujua.
Mateso yalipozidi, Juma ___15___ kutorokea mtaani na kurandaranda huko. Alikamatwa ___16___ polisi na kupelekwa ___17____ ili aendelee na masomo yake. Alitia bidii za __18___ masomoni hadi akafuzu ___19___na kujiunga na shule ya upili.
A | B | C | D | |
11. | ya | wa | za | la |
12. | yangu | wao | yao | zao |
13. | kuwalea | kumlea | kulewa | kulea |
14. | lakini | kwa | baina | kuwa |
15. | aliamua | aliamwa | aliamua | aliamuliwa |
16. | za | mwa | kwa | na |
17. | nyumbani | kanisani | mtaani | mjini |
18. | sungura | siafu | mchwa | nyani |
19. | mzura | vizuri | nzuri | zuri |
Kuanzia swali 20-30 jibu kulingana na maagizo
- Watu huagana vipi usiku.
- Tuonane
- Alamsiki
- Habari
- Ndoto mbaya
- Jina kipofu liko katikia ngeli ipi?
- KI-VI
- I-ZI
- LI-YA
- A-WA
- Upande uliochorwa Z huitwa _______________________
- magharibi
- kaskazini
- kusini
- mashariki
- Neno lilopigwa kistari katika sentensi ni la aina gani? Ngao iko juu ya kitanda
- nomino
- kitenzi
- kihusihi
- kielezi
- Kanusha. Mama ananiita
- Mama aliniita
- Baba ananiita
- Mama haniiti
- Baba haniiti
- Andika kwa wingi. Chura ameruka
- vyura veruka
- vyura hawaruki
- Chura wameruka
- Vyura wameruka
- 4004 kwa maneno ni
- Mia nne na nne
- Nne elfu na mia nne
- Elfu nne sufuri nne
- Elfu nne na nne
- Tegua kitendawili. Njoo umwone umpendaye
- Kioo
- kivuli
- Picha
- Mama
- Sisi _________________________________ tuliozawadiwa zaidi.
- ndio
- ndisi
- ndiwo
- ndiye
- Kamilisha tashbihi ifuatayo
Mweusi kama ____________________________- makaa
- giza
- shetani
- ubao
- Kamilisha methali
Haba na haba __________________________________- ndio haba
- hujaza ndoo
- hujaza kibaba
- ndie mwendo
INSHA
Andika insha ya kusisimua kuhusu mada ifuatayo.
SHULE YETU.
MARKING SCHEME
- D
- B
- C
- A
- B
- D
- C
- A
- C
- B
- B
- C
- A
- A
- A
- D
- A
- C
- B
- B
- D
- B
- C
- C
- D
- D
- A
- B
- A
- C
Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - Grade 5 End Term 1 Exams 2023 Set 1
Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali 1-5.
(Wazazi wanajadiliana na wana wao kuhusu namna na umuhimu wa kuwa na afya bora)
Baba: Mke wangu, ni siku nyingi hatujazungumza na kina Tina kuhusu masuala ya kibinafsi. (Kimya kinapita) Hebu waite tuzungumze nao.
Mama: Sawa mume wangu (anasimama dirishani akitazama nje) Tinaa!..... Ramaa!
Tina na Rama: Naam mama!
Mama: Hebu njooni humu ndani upesi (Kwa mumewe) Watoto siku hizi wakipata fursa, hawakai. Ni wao na mchezo. (Watoto wanaingia wakihema)
Baba: Wanangu, tumewaita hapa ili tuzungumze kuhusu umuhimu wa kuwa na afya bora. Ketini. (Wanaketi)
Mama: Kwanza, Tina na Rama, lazima mjue namna ya kudumisha afya bora.
Tina: Nadhani njia mojawapo ni kudumisha usafi, kula vyakula salama na kamili na kufanya mazoezi.
Baba: Vyema Tina. Tunapokuwa na afya bora, miili yetu haipatwi na magonjwa mara kwa mara.
Rama: Tena akili zetu hufanya kazi vyema na kuboresha matokeo ya shughuli zetu zikiwemo za masomo.
Mama: Si hayo tu, tunapokuwa na afya bora, sisi hupendeza na kuvutia maana miili yetu huwa na maumbo ya asili, si miili iliyokonda na kuonyesha mifupa.
Baba: Ningependa kuwa kwanzia leo kila mmoja wetu aliakikishe ubora wa afya yake kwa kutenda haya na mengine yaliyo mema.
Tina na Rama: Sawa baba.
- Baba alitaka kuzungumza na watoto wao kuhusu
- matokeo ya mtihani.
- michezo waliyokuwa wakicheza.
- masuala ya kibinafsi.
- vipindi walivyovipenda.
- Kabla hawajaitwa, Tina na Rama walikuwa wapi?
- Chumbani
- Nje wakicheza
- Wakipumzika nje
- Sebuleni
- Pendekezo la kula vyakula salama na kamili lilitolewa na
- Tina
- Rama
- mama
- baba
- Kulingana na baba, tunapokuwa na afya bora,
- matokeo ya shughuli zetu huwa mazuri.
- miili yetu huweza kupatwa na magonjwa.
- miili yetu huwa na maumbo asilia isiyokonda.
- hatupatwi na magonjwa mara kwa mara.
- Kulingana na mazungumzo haya,
- Rama na Tina hawapendi kucheza.
- hakuna haja ya kudumisha afya bora.
- wazazi waliotajwa wanawajali watoto wao.
- watu wa familia hiyo wanapenda sana kucheza.
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 6 hadi 9.
Amina alikuwa mwanafunzi wa Gredi ya tano katika shule ya Shaurimoyo. Mama yake alimwambia awe mwangalizi pale nyumbani alipokuwa sokoni. Amina alikuwa na kaka wawili na dada wawili. Ndugu zake Amina walikuwa watiifu.
Jumamosi moja, mama yao alienda sokoni kama kawaida. Alimwambia Amina awaelekeze ndugu zake kufanya shughuli za pale nyumbani. Amina aliwaambia dada zake waoshe vyombo na kusafisha nyumba. Kaka zake walitakiwa kuyanyunyizia maua maji na kuwashughulikia mbuzi wao. Baada ya shughuli hizo zote, watoto hao walikaa na kutulia huku wakimngoja mama yao atoke sokoni.Mama yao aliporudi, alifurahi sana kuona jinsi nyumba yao ilivyokuwa safi. Aliwapa wasichana maparachichi na wavulana miwa kwa kazi nzuri walizofanya. Wote walifurahi.
- Familia hii ina jumla ya watoto wangapi?
- Wanne
- Sits
- Watano
- Watalu
- Ikiwa kila msichana alipewa parachichi moja, mama alileta maparachichi mangapi?
- Matano
- Sita
- Manne
- Matatu
- Baada ya kumaliza kazi zote, watoto
- walikaa na kumngoja mama yao.
- walienda nje kucheza.
- waliwasha runinga na kutazama vibonzo.
- walifurahia maparachichi na miwa.
- Mama alipotoka sokoni alifurahishwa na
- utulivu wa watoto wake.
- usafi wa nyumba yao.
- bidii ya watoto wake.
- ladha ya matunda aliyoleta.
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 10 hadi 12.
Moto! Moto! Hii ilikuwa sauti ya kutisha kwelikweli. Ingawa nilikuwa na usingizi kiasi, nilinyanyuka kutoka kitandani kuangalia ilipotoka sauti ile. Nilichungulia dirishani. Nje, kila mmoja alikuwa akikimbia huku na kule kujaribu kuuzima moto katika nyumba ya Bi. Faya.
"Siachwi nyuma!" Nilijiambia huku nikishuka vidato. Nilipofika, kila mmoja alikuwa mbioni kuokoa hali. Ghafla, nilichukua ndoo iliyokuwa na mchanga nikampa mzee Mapunda. Naye hakusita. Aliumwaga kwenye kitovu cha moto ule. Haikutosha, Mwang'ombe akaleta ndoo nyingine huku kipusi akimimina mapipa kadhaa ya maji motoni. Baada ya muda mfupi, moto wote ukawa umezima.
- Mwandishi aliposikia sauti ya kutisha, alikuwa wapi?
- Kitandani akilala.
- Chumbani akifanya usafi.
- Nje akizima moto.
- Sebuleni akitazama runinga.
- Mwandishi aliamua kuwa haachwi nyuma kwa kuwa alikuwa
- na usingizi kiasi
- na moyo wa kusaidia.
- na ndoo yenye mchanga.
- mwenye bidii kwelikweli.
- Wakati wa ajali hii ya moto, Bi Faya alikuwa wapi?
- Sokoni
- Dukani
- Chumbani
- Hatujaelezwa
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 13 hadi 15.
Siku iliyofuata, mfalme simba alikuwa ameandaa mashindano yaliyotakiwa kuwahusisha wanyama wote. Hata hivyo, kunao wengine waliokuwa wameomba ruhusa kuwa wasingeshiriki. Jioni ya siku ya Ijumaa, mbweha alipita kote huku akipuliza firimbi ya kutangaza mashindano ya siku iliyofuata, mashindano ya kucheza muziki.
Wanyama waliotakiwa kushiriki walikuwa pundamilia, kinyonga na sungura. Watatu hawa walifika wakiwa wamejipodoa vilivyo. Pundamilia alikuwa amepakwa rangi nyeupe na nyeusi kwa namna ya mistari, sungura alikuwa amenyolewa mtindo wa shore na kuliacha shungi la nywele utosini huku kinyonga akiwa na mavazi mapya yaliyomkaa sawasawa.
Baada ya kila mmoja kuchukua nafasi yake na ngoma kuanza, mvua kubwa ilianza kunyesha. Kila mmoja alitimua mbio kumwacha maskini kinyonga akinyeshewa na nguo zake mpya!
- Mashindano haya yangefanyika siku ya
- Ijumaa
- Alhamisi
- Jumamosi
- Jumapili
- Wanyama wangapi walitarajiwa kushiriki katika mashindano haya?
- Watano
- Wawili
- Wanne
- Watatu
- Unadhani ni kwa nini kinyonga alibaki wenzake wakikimbia?
- Hawezi kuenda haraka.
- Alitaka kubaki pale.
- Alitaka anyeshewe.
- Alikataa kuwafuata mbio.
Soma kifungu kifuatacho. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.
Siku hiyo tulikuwa tumeingoja kwa hamu na ghamu. Sote tulifika ___16___ tukiwa tayari kuabiri___17___kuelekea mjini Meremeta. Hii ilikuwa mara yangu ya ___18___ kuenda huko. Sikuwa nimewahi kuenda huko. Tuliingia ___19___ tukiwa na furaha sana. Mara dereva alitia gari ufunguo na safari
___20___.
A | B | C | D | |
16. | asubuhi | shuleni | adhuhuri | usiku |
17. | baiskeli | basi | ndege | meli |
18. | moja | mwisho | tatu | kwanza |
19. | njiani | safari | basini | barabarani |
20. | ikaanza | ikaisha | ikaendelea | ukaanza |
Katika swali la 21-30, jibu swali kulingana na maagizo uliyopewa.
- Katika sentensi chura mnono aliteleza akazama, nomino ni
- mnono.
- chura.
- aliteleza.
- akazama.
- Chagua orodha ya vitenzi pekee. A
- Kiazi, bata, daftari.
- Chota, peleka, kataa.
- Sana, zaidi, polepole.
- Chini ya, kando ya, mbele ya.
- Ni gani kati ya maneno haya ni kihisishi?
- Lo!
- Katikati ya
- Mweupe
- Leo
- Kati ya orodha hizi, ni ipi ina mavazi, kike na kiume
- Kamisi, chupi, soksi.
- Koti, rinda, kofia
- Suti, soksi, tai
- Suruali, kaptura, sidiria
- Kamilisha methali:
Mwana akibebwa- usilevyelevye miguu.
- ndivyo akuavyo.
- kuzimu enda kiona.
- hutazama kisogo cha nina.
- Ni upi wingi wa sentensi ifuatayo?
Mkoba wenyewe ni huu.- Mikoba zenyewe ni hizi.
- Mikoba yenyewe ni hii.
- Mkoba zenyewe ni hizi.
- Mkoba yenyewe ni hii.
- Ni rangi gani hapa haipo katika bendera ya taifa la Kenya?
- Nyeupe
- Nyeusi
- Manjano
- Kijani
- Nomino mayai inaweza kuorodheshwa katika ngeli gani?
- U-I
- KI-VI
- LI-LI
- LI-YA
- Kitenzi chapa katika kauli ya kutendea huwa
- chapia.
- chapwa.
- chapisha.
- chapiwa.
- Kamilisha tashbihi hii
Bwana Murefu ni mfupi kama- mlingoti.
- nyundo.
- kasuku.
- nguruwe.
MARKING SCHEME
- C
- B
- A
- D
- C
- C
- D
- A
- B
- A
- B
- D
- C
- D
- A
- A
- B
- D
- C
- A
- B
- B
- A
- C
- D
- B
- C
- D
- A
- B