Friday, 19 May 2023 13:45

Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - Grade 5 Opener Exams Term 2 2023 Set 1

Share via Whatsapp

MASWALI

MAAGIZO
Karatasi hii ina sehemu tano kuu.
Jibu maswali yote kulingana na maagizo.
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata.

Siku moja wakati wa jioni, Punda alikuwa amechoka sana. Alikuwa amelala chini ya mti baada ya kufanya kazi mchana wote. Aliamshwa saa kumi na moja alfajiri na kuanza kubebeshwa mizigo, Mwanzo, alibeba unga kutoka sokoni akipeleka nyumbani alikoishi. Unga huo ulikuwa magunia saba. Alipomaliza, alianza kusomba maji kutoka kwenye eneo la kisima akipeleka katika nyumba za watu. Shughuli ya kusafirisha maji ilifanyika kuanzia saa nne hadi saa saba. Alipotoka hapo, alifahamishwa kuwa kulikuwa na miti iliyofaa kubebwa kutoka msituni hadi mjini. Kazi ya kubeba miti ilianza saa nane. Kufikia saa kumi na mbili, Punda hakuwa amemaliza kubeba miti hiyo. Mvua ilikuwa imenyesha na kuisha huku punda akiendelea na kazi hiyo.
Punda aliamua kuzungumza na rafiki yake wa chanda na pete, Farasi. Farasi alionekana kuishi maisha ya starehe sana. Punda alimwamkua "Masalheri kaka?"kisha akauliza swali lake. Farasi alimweleza kuwa yeye huishi maisha ya starehe kwa sababu alikuwa amesoma. Alimfahamisha kuwa mara nyingi, unaposoma huwa unapata kazi nzuri ambazo si za mateso. Pia, alimwambia kuwa si lazima aajiriwe ikiwa amesoma. Angeweza kujifungulia biashara na kujiendeleza. Kando na kusoma, Farasi alimweleza faida ya kutumia talanta yake. Farasi alieleza kuwa yeye alikuwa na talanta ya riadha, hiyo ndiyo sababu alikuwa akikimbia mara kwa mara na kupata manufaa tele. Asubuhi iliyofuata, Punda aliwasili shuleni ili kuanza masomo ya jioni baada ya kazi. Ni kweli kuwa alisoma kwa bidii sana. Vilevile, alianza mazoezi ya uimbaji kwa kuwa alikuwa na sauti nzuri sana.

 1. Kwa nini Punda alikuwa amechoka? 
  1. Alimka mapema sana.
  2. Alinyeshewa na mvua.
  3. Hakuwa amekula.
  4. Alifanya kazi nyingi sana.
 2. Yawezekana kuwa Punda alimtembelea Farasi wakati gani?
  1. asubuhi
  2. usiku
  3. adhuhuri
  4. jioni
 3. Badala ya kutumia neno 'rafiki yake', mwandishi angetumia neno gani lenye maana sawa!
  1. sahibu yake
  2. jirani yake
  3. ndugu yake
  4. mnyama mwenzake
 4. Ufahamu huu unaonyesha umuhimu wa nini?
  1. talanta na masomo
  2. masomo na kuamka mapema
  3. kazi na talanta
  4. biashara na masomo
 5. Punda alisomba maji kwa muda gani?
  1. saa saba
  2. saa tatu
  3. saa nne
  4. saa saba
 6. Punda alibeba miti hadi saa ngapi?
  1. saa kumi na mbili
  2. kabla ya saa kumi na mbili 
  3. saa nane
  4. baada ya saa kumi na mbili
 7. Maneno 'alisoma kwa bidii sana' yanaweza yakarejelewa kwa methali gani? 
  1. Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.
  2. Mgaagaa na upwa hali wali mkavu. 
  3. Asiyesikia la mkuu huvunjika guu. 
  4. Polepole ndio mwenda.
 8. Kulingana na ufahamu, ni keli kuwa mtu aliyesoma:
  1. hawezi akaajiriwa.
  2. anaweza akaajiriwa au afanye biashara. 
  3. hawezi akafanya biashara.
  4. lazima aishi mjini.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata.
Upishi wa chakula ni muhimu sana katika maisha yetu. Kuna sababu mbalimbali ambazo hufanya tupike chakula. Kwanza, chakula huweza kuwa laini na kulika kwa urahisi ikiwa kimepikwa. Chakula kisichopikwa hakiwezi kikalika kwa urahisi. Jambo jingine ni kuwa kupika chakula huua viini ili mtu asiambukizwe ugonjwa. Magonjwa kama vile kipindupindu na kuendesha husababishwa nachakula au maji machafu. Kwa hivyo tunapopika chakula, chakula hicho huwa salama kwa ulaji. Kupika chakula pia hufanya chakula hicho kiwe na ladha nzuri. Chakula kilichopikwa huonja vizuri kuliko chakula amabacho hakijapikwa. Unapopika chakula, huwa kitamu kama asali.
Wakati wa kupika, kuna hatua kadhaa ambazo hufuatwa. Kabla ya kuinjika sufuria mekoni, ni vyema kukoka moto. Baada ya chakula kuiva, mtu huepua sufuria kisha akapakua chakula hicho. Vyakula huweza kupikwa kwa njia mbalimbali. Njia hizo ni kama vile kutokosa, kukaanga, kuoka na kubanika. Vyakula vinavyoweza kukaangwa ni kama vile samaki, mayai, nyama na mboga. Utokosaji nao huweza kufanyiwa viazi, mihogo, mahindi, samaki na nyama. Unaweza ukabanika mahindi na nyama kisha ukaoka keki, mkate au biskuti.

 1. Zifuatazo ni faida za kupika chakula isipokuwa;
  1. Huwezesha chakula kumezwa kwa haraka.
  2. Huua viini katika chakula.
  3. Hufanya chakula kiwe laini.
  4. Huongeza ladha ya chakula.
 2. Maneno 'kitamu kama asali' ni mfano wa;
  1. nahau
  2. kitendawili
  3. tashbihi
  4. kitanzandimi
 3. Chagua hatua ya pili kati ya hatua zifuatazo kulingana na kifungu.
  1. koka
  2. injika
  3. epua
  4. pakua
 4. Chakula gani kinachoweza kuandaliwa kwa kutokoswa, kukaangwa au kubanikwa?
  1. nyama
  2. keki
  3. viazi
  4. mboga

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata.
Katika soko la Mikindani, kuna matunda aina mbalimbali. Siku moja watoto kadhaa walienda sokoni kununua matunda hayo. Wavulana walikuwa wanne nao wasichana walikuwa watatu. Kamau alinunua maembe, mananasi, machungwa na tufaha. Njeri alinunua matunda yote yaliyonunuliwa na Kamau isipokuwa maembe. Fatuma naye alinunua matunda yote yaliyonunuliwa na Njeri kisha akaongezea maembe na maparachichi. Wanjala alinunua

matunda yaleyale yaliyonunuliwa na Kamau kisha akaongezea maparachichi. Wengine nao walinunua matunda bila kuchagua, waliyachanganya tu. Walipomaliza shughuli zao, waliondoka na kurudi nyumbani.

 1. Kifungu kinaeleza kuwa vijana wangapi walioenda sokoni?
  1. watatu
  2. wanne
  3. saba
  4. sita
 2. Akina nani walionunua matunda ya aina moja?
  1. Wanjala na Fatuma
  2. Njeri na Fatuma
  3. Kamau na Njeri
  4. Wanjala na Kamau
 3. Ni nani aliyenunua aina chache za matunda! 
  1. Kamau
  2. Wanjala
  3. Fatuma
  4. Njeri 

Jaza nafasi zilizoachwa kwa kutumia jibu linalofaa zaidi.
Nuru alichukua karatasi ..................16.................... ili kumwandikia Zawadi barua. Zawadi alikuwa ndugu yake aliyesomea mjini. Aliketi ..................17.................... kiti chake kisha akaanza kuandika barua hiyo. Baada ya kuandika anwani  ..................18.................... aliandika tarehe kisha akaendelea. Alimweleza  ..................19.................... ni vyema kuwa na maadili katika maisha. Maisha ya mtu ..................20.................... kuwa mazuri sana ikiwa ana maadili.

 1.                      
  1. wake
  2. lake
  3. yake
  4. chake
 2.              
  1. kwa
  2. kwenye
  3. katika
  4. ndani mwa
 3.                    
  1. nne
  2. tatu
  3. mbili
  4. moja
 4.                
  1. kuwa
  2. kuwamba
  3. kwa
  4. kama
 5.                  
  1. yanaweza
  2. anaweza
  3. inaweza
  4. unaweza

Jibu kila swali kulingana na maagizo.

 1. Chagua nomino ya wingi kwenye majibu yafuatayo.
  1. uraha
  2. matunda
  3. chai
  4. kitanda
 2. Ukubwa wa 'mji' ni.
  1. miji
  2. kijiji
  3. vijiji
  4. jiji
 3. Jibu gani ambalo halionyeshi matumizi ya herufi kubwa?
  1. Hutumika mwanzoni mwa sentensi.
  2. Hutumika kuandika nomino ya pekee.
  3. Hutumika mwishoni mwa sentensi.
  4. Hutumika kuonyesha ufupisho wa maneno. 
 4. Pambo gani ambalo huvaliwa mkononi?
  1. ushanga
  2. bangili
  3. pete
  4. herini
 5. Kinyume cha 'furaha ni.
  1. hasira
  2. lia
  3. huzuni
  4. woga
 6. Chagua wingi wa:
  Kitabu changu kimewekwa ndani ya kabati.
  1. Vitabu vyetu vimewekwa ndani ya kabati.
  2. Vitabu vyangu vimewekwa ndani ya makabati.
  3. Vitabu vyangu vimewekwa ndani ya kabati.
  4. Vitabu vyetu vimewekwa ndani ya makabati. 
 7. 'Mombasa, Ijumaa na Disemba' ni mifano ya aina gani za nomino?
  1. dhahania
  2. za pekee
  3. za makundi
  4. za vitenzijina
 8. Umati ni wa watu' kama vile kicha ni cha
  1. pesa
  2. matunda
  3. funguo
  4. maua
 9. Yafuatayo ni maagano isipokuwa;
  1. alamsiki
  2. buriani
  3. masalheri
  4. siku njema
 10. Chagua sentensi inayoonyesha wakati uliopita, hali ya kuendelea.
  1. Juma alikuwa akisoma kitabu chake.
  2. Mama atakuwa akimshauri mtoto wake.
  3. Wangali wanakula chakula chao.
  4. Wanafunzi wamepanda miti mingi.

INSHA

Andika insha ya masimulizi kuhusu;

AJALI NILIYOSHUHUDIA

MWONGOZO

3 

 

Join our whatsapp group for latest updates

Download Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - Grade 5 Opener Exams Term 2 2023 Set 1.


Tap Here to Download for 30/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students