Tuesday, 24 October 2023 12:59

Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - Grade 5 End Term 3 Exams 2023 Set 1

Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali 1-5

Mwanafunzi:   Shikamoo mwalimu?
Mwalimu:        Marahaba Juma. Karibu ukae kitini
Mwanafunzi:   Asante mwalimu
Mwalimu:        Nikusaidiaje Juma?
Mwanafunzi:   Nimekuja kulalamikia uchafuzi wa mazingira shuleni. Wanafunzi wengi wamekataa kufuata maagizo ya kutupa taka kwenye                                 majalala na kumwaga maji chooni baada ya haja zao humo.
Mwalimu:        Asante Juma kwa kuwa mwanafunzi mtiifu na anayewajali wengine.
Mwanafunzi:   Nimehongera mwalimu. Wamesahau jinsi ulivyotufunza kuwa mazingira machafu yanaweza kusababisha magonjwa mengi Mwalimu:         Unakumbuka baadhi ya magonjwa hayo?
Mwanafunzi:    Naam mwalimu! Kuna ugonjwa wa kipindupindu, kuna kichocho na hata kuumwa na tumbo na maleria.
Mwalimu:         Vizuri sana. Haya twende darasani pako niwazungumzie tena wanafunzi hao kuhusu umuhimu wa kuyatunza mazingira yao
Mwanafunzi:   Asante mwalimu

  1. Jibu la shikamoo ni
    1. shikamooo
    2. marahaba
    3. sabalkheri
    4. asante
  2. Juma alienda kufanya nini ofisini?
    1. Kumsalimia mwalimu
    2. Kumshukuru mwalimu
    3. Kumkaribisha mwalimu
    4. Kulalamikia uchafuzi wa mazingira
  3. Tatataka zinafaa kutupwa wapi?
    1. Chooni
    2. Majalalani
    3. Darasani
    4. Uwanjani
  4. Mazingira machafu husababisha nini?
    1. Magonjwa
    2. Kiangazi
    3. Homa
    4. Nidhamu
  5. Ni ugonjwa gani ambao hausababishwi na mazingira machafu?
    1. Maleria
    2. Kichocho
    3. Kifua kikuu
    4. Kipindupindu

Soma kifungu hiki kisha ujibu maswali 6-10

Kila muhula tunapokaribia kufunga shule kwa likizo, walimu wa shule yetu huandaa siku spesheli ya michezo. Shule yetu ya Malezi Bora huwa na wanafunzi mia nane. Siku ya michezo, wanafunzi wote pamoja na walimu hukusanyika uwanjani.

Wiki iliyopita ndiyo wiki tuliyoandaliwa michezo. Mchezo uliochezwa kwanza ulikuwa ni mbio fupi za mita mia moja. Moha, Talia, Amen and Mercy ndio waliochaguliwa kuanza. Wote walipanga mstari. "Ni nani atashinda leo?" Sara, mwanafunzi wa darasa la nane alishangaaa. Aliwaangalia marafiki zake. Prrr.... Firimbi ikalia. Moha na Amen wana mbio sana. Amen akawa anaongoza mbio hizo. Sara na wanafunzi wengine walishangiliwa kwa vifijo. Moha alitoka nyuma mbio sana akampita Amen kwenye mstari wa kumalizia na akawa wa kwanza. Talia naye alimaliza wa tatu huku Mercy akiridhika na nafasi ya nne. Yalikuwa mashindano na kufana sana.

  1. Kila mwisho wa muhula, walimu wa shule huandaa nini?
    1. Siku ya michezo
    2. Siku ya kufunga shule
    3. Wakati wa mtihani 
    4. Siku ya kuenda sokoni  
  2. Wanafunzi wa shule hii ni wangapi?
    1. 1000
    2. 80
    3. 800
    4. 500
  3. Ni mchezo gani ulioandaliwa siku hiyo?
    1. Mpira
    2. Mbio fupi
    3. Ndondi
    4. Mpira wa vikapu
  4. Ni wanafunzi gani walio na mbio sana? 
    1. Talia na Moha
    2. Moha na Amen
    3. Mercy na Talia
    4. Amen na Mercy 
  5. Ni mwanafunzi gani aliyeibuka mshindi?
    1. Talia
    2. Mercy
    3. Amen
    4. Moha

Soma ufahamu ufuatao kisha ujibu maswali 11-15

Zipo nyakati nyingine ambapo tunapatwa na matatizo ya kiafya yanayohitaji huduma za dharura. Matatizo haya hutokea mahali popote kama vile shuleni, njiani ama nyumbani. Haya yanapotokea huduma ya kwanza huhitajika ili kupunguza au kuzuia hali kuwa mbaya zaidi. Ni vizuri kujua kuwa tatizo dogo kama vile kusakamwa na chakula kooni linaweza kuwa na athari kubwa endapo halitashughulikiwa kwa haraka. Pia, jereha lisiposhughulikiwa upesi na kwa njia ifaayo, linaweza kuingiwa na wadudu na kufanya hali ya mwathiriwa kuwa mbaya zaidi.

Katika jamii, ni vyema kuwa na watu waliohitimu kutoa huduma ya kwanza. Watu hao wanapaswa kuwa na ujuzi wa kukabiliana na hali mbalimbali ambazo zinahitaji maarifa ya hali ya juu. Aidha, ni jambo zuri kuwa na chama cha huduma ya kwanza shuleni. Wanafunzi katika chama hiki hupewa mafunzo ya kukabiliana na ajali ndogondongo na matatizo ya kiafya.

  1. Matatizo ya kiafya huhitaji nini?
    1. huduma za dharura
    2. kutibiwa haraka
    3. kupuuzwa vizuri
    4. kuwatibu wagonjwa
  2. Tatizo la kiafya laweza kutokea wapi?
    1. Shuleni na nyumbani
    2. Tumboni na chumbani
    3. Kichwani na kinywani
    4.  Masomoni na pembeni
  3. Ni tatizo gani linaweza kuwa baya zaidi kulingana na ufahamu?
    1. Kunywa maji
    2. Kuoga bafuni
    3. Kusakamwa na chakula
    4. Kuenda haja
  4. Watu wanaostahili kufanya huduma ya kwanza lazima wawe na nini?
    1. Pesa
    2. Magari
    3. Dawa
    4. Ujuzi
  5. Ni jambo gani zuri linalostahili kuwa shuleni?
    1. Kuwa na hospitali shuleni
    2. Kuwa na chama cha huduma ya kwanza 
    3. Kuanzisha chama cha kuwafunza wanafunzi 
    4. Kuendeleza matibabu ya majeruhi

Some mtungo ufuatao kisha ujaze nafasi zilizoachwa wazi kwa jibu sahihi.

Zuri alikuwa mchoraji mahiri. Alipenda kuchora majora ___16___ leso yaliyopendeza sana. Watengenezaji leso walipenda ___17___ hiyo. Waliichukua na kuonyeshana kwenye majukuwaa ya biashara, Michoro hiyo ya Zuri ilipata umaarufu ___18___. Zuri alikuwa akipata cheki za pesa ___19___  sana kutokana na michoro ___20___.

   A  B  C  D
 16.  za  ya   la   wa 
 17.  michongo  mapambo   picha   michoro 
 18.  mkubwa  kidogo  kubwa  kikubwa
 19.  mingi  wengi  nyingi  mengi
 20.  yake  zao  yangu  zertu 


Kutoka swali la 21 hadi 30 jibu kulingana na maagizo.

  1. Chagua nomino katika sentensi hizi
    Darasa hili ni kubwa sana
    1. hili
    2. kubwa
    3. darasa
    4. sana
  2. Tulipikiwa chakula kizuri tukala
    1. Tulipikiwa
    2. Chakula
    3. Kizuri
    4. Tukala
  3. Mtoto wa kuku anaitwaje?
    1. Kinda
    2. Ndege
    3. Mwana
    4. Kifaranga
  4. Chagua sentensi yenye kiwakilishi cha nafsi ya kwanza
    1. Wewe ni mtoto mzuri
    2. Wao ni walimu wetu
    3. Sisi tutakutembelea kesho
    4. Nyinyi hamjui kupika chai
  5. Chagua kielezi cha namna katika sentensi hii Wanariadha waliokimbia vizuri walituzwa jana
    1. Jana
    2. Walituzwa
    3. Vizuri
    4. Waliokimbia
  6. Tegua kitendawili hiki. Ninatembea na paa mgongoni
    1. Kobe
    2. Nyumba
    3. Upepo
    4. Jua
  7. Chagua jibu ambalo si kiunganishi
    1. Lakini
    2. Nyeupe
    3. Pia
    4. Kwa hivyo
  8. Kamilisha sentensi hii kwa njia sahihi.
    Panya ameingia _____________________ shimo.
    1. ndani ya
    2. juu ya
    3. chini ya
    4. karibu na
  9. Jaza pengo kwa neno ambalo ni kinyume cha lililopigiwa mstari
    Nyanya ni mgonjwa lakini ______________ ni mzima
    1. mjomba
    2. baba
    3. kaka
    4. babu
  10. Kamilisha tashbihi ifuatayo.
    Karani ni mrefu kama
    1. barabara
    2. nyundo
    3. twiga
    4. ndovu

SEHEMU YA B: INSHA

Andika insha ya kusisimua kuhusu mada ifuatayo:-

MWIZI KIJIJINI

MARKING SCHEME

  1. B
  2. D
  3. B
  4. A
  5. C
  6. A
  7. C
  8. B
  9. B
  10. D
  11. A
  12. A
  13. C
  14. D
  15. B
  16. B
  17. D
  18. A
  19. C
  20. A
  21. C
  22. B
  23. D
  24. C
  25. C
  26. A
  27. B
  28. A
  29. D
  30. C

 

Read 1850 times Last modified on Wednesday, 25 October 2023 08:30