Thursday, 22 June 2023 11:08

Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - Grade 4 Opener Exams Term 2 2023 Set 2

Share via Whatsapp

Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu swali 1-5

Furaha ni msichana wa gredi ya nne. Ana umri wa miaka tisa. Yeye anaishi na wazazi wake katika mtaa wa Kabiti. Nyumba yao ina sebule, jikoni, vyumba vitatu vya kulala, choo na bafu. Furaha anapenda kustarehe sebuleni. Kuna makochi manne na meza. Sakafuni kuna Zulia na ukutani kuna saa na mapambo tofauti. Ndani ya chumba cha furaha cha kulala mna kitanda chenye matendegu manne na meza ndogo ya kusomea pia kuna neti ambayo Furaha hutumia kujifunika ili asiumwe na mbu. Furaha na mama yake huandaa vyakula jikoni. Wao huandaa vyakula vitamu sana. Furaha anaipenda nyumba yao.

  1. Jina la mtaa anamoishi furaha ni
    1. Kibra
    2. Kabiti
    3. Bibabii
    4. Hatujafahamishwa
  2. Familia ya Furaha ina jumla ya watu wangapi?
    1. Wawili
    2. Watatu
    3. Wanne
    4. Watano
  3. Sakafuni huwekwa zulia, je dirishani huwekwa nini?
    1. Kochi
    2. Neti
    3. Pazia
    4. Blanketi
  4. Wageni hupokelewa wapi
    1. sebuleni
    2. jikoni
    3. bafuni
    4. dirishani
  5. Kwa nini Furaha hulala ndani ya neti?
    1. ili asiumwe na mbu
    2. ili kuwe na joto
    3. kwa sababu yenye ni mwoga
    4. nzi huwa wengi chumbani mwake

Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu swali 6-10.
Somo ni mvulana mwenye bidii shuleni pia yeye anapenda kujifunza mengi mtandaoni. Wakati mwingine yeye hazingatii usalama akitumia matini ya kijitali.

Siku moja alipata ujumbe mtandaoni kwanza alidhani ni ujumbe kutoka kwa rafiki yake kumbe ujumbe huo ulitoka kwa mtu asiyejua. Mtu huyo alimwambia wakutane mahali pa faragha. Mtu huyo alimwambia somo kuwa alikuwa na zawadi yake. Kwamba alitamani sana kupata zawadi yake. Kwanza alitamani sana kupata zawadi lakini aliona kwanza awajulishe wazazi wake. Kumbe mtu huyo hakuwa mzuri.

  1. Bidii za Somo ziliangazia wapi hasa?
    1. Mtandaoni
    2. Shuleni
    3. Masomoni
    4. Rafikiye
  2. Ujumbe aliopata ulitoka kwa nani?
    1. Rafikiye
    2. Mamaye
    3. Mtu asiyemjua
    4. Mwalimu
  3. Ujumbe aliopata ulimwambia vipi?
    1. Wakutane faraghani
    2. Alikuwa amepita mtihani wake
    3. Azingatie usalama mtandaoni
    4. Asitumie mtandao
  4. Je, Somo alikutana na aliyetuma ujumbe?
    1. Hatujafamisha
    2. La
    3. Naam
    4. Hamna uhakika
  5. Ni kipi si kifaa cha kidijitari kati ya hivi?
    1. Kamera
    2. Simu
    3. Tarakilishi
    4. Redio

Soma kifungu hiki. Chagua jibu lifaalo kujaza nafasi zilizoachwa kutoka 11-15.

Elimu ya mazingira ni mada __11__ mkazo sana katika somo __12__Kiswahili. Wanafunzi wanahimizwa kusafisha mazingira __13__  ili wadumishe usafi.  Wanafunzi wakishirikiana watatimiza azma __14__ ya kudumisha usafi kwa kuwa __15__.

   A   B   C   D 
 11.   inayotilia   inayotiliwa   inayotia   inayotiwa 
 12.  ya  wa  cha  la
 13.  yao  zao  lao  zao
 14.   hizo  huyo  hilo  hiyo
 15. Ukijitahidi utafaidi  Mtaka cha mvunguni sharti aianame  Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu  Mgagaa na upwa hali wali makavu 

 

SARUFI

Kuanzia swali 16-30 jibu kulingana na maagizo

  1. Chagua kundi lenye nomino pekee
    1. Amri, hisani, vizuri
    2. Chai, subira, nyeupe
    3. Hewa, amani, neno
    4. Haraka, baraka, pamoja
  2. Tegua kitendawili
    Bei yangu haishuki _____________________________________
    1. shamba
    2. dhahabu
    3. pesa 
    4. uhai
  3. Andika sentensi ifuatayo kwa wingi
    Mzazi alimtuma mwanawe shambani
    1. Mzazi aliwatuma wanawe mashambani
    2. Wazazi waliwatuma wanawe mashambani
    3. Wazazi aliwatuma wanawe shambani
    4. Wazazi waliwatuma wanawe shambani
  4. Chagua orodha yenye maneno yaliyo katika ngeli ya KI-VI pekee
    1. Kifagio, choo, vitabu
    2. Kipofu, kiko, sahani
    3. Choo, kiwavi, kioo
    4. Mbwa, mti, kiberiti
  5. Tumia amba ipasavyo
    Chombo ___________________________________ alitumia ni chake
    1. ambao
    2. ambayo
    3. ambacho
    4. ambavyo
  6. Kanusha
    Alitembea akiimba
    1. Hakutembea wata hakuimba
    2. Hakutembea wala kuimba
    3. Hayatembe na hajaimba
    4. Hatatembea wala kuimba
  7. Chagua nomino kwenye sentensi ifuatayo
    Mwimbaji aliimba kwa ustadi mno
    1. aliimba
    2. mno
    3. mstadi
    4. mwimbaji
  8. Shairi lenye mishororo minne huitwa
    1. Tarbia
    2. Takhmisa
    3. Tathnia
    4. Tathlitha
  9. Kamilisha methali ifuatayo
    Asiyesikia la mkuu
    1. huvunjika guu
    2. hufunzwa na ulimwengu
    3. hufaulu
    4. hupotea
  10. Jibu la salamu sabalkheri ni
    1. Binuru
    2. Alamsiki
    3. Aheri
    4. Chewa
  11. Wao _______________________________ walionaswa na polisi
    1. ndisi
    2. ndio
    3. ndiyo
    4. ndiwo
  12. Umbo lifuatalo huitwa
    G4SKT2OS22023Q27
    1. duara
    2. duara dufu
    3. mstatili
    4. mraba
  13. Kinyume cha neno anika ni
    1. anikia
    2. anua
    3. anikika
    4. anika
  14. Bendera ya Kenya ina rangi ngapi?
    1. Nne
    2. Tatu
    3. Tano
    4. Sita
  15. Kisawe cha neno rafiki ni
    1. adui
    2. ndugu
    3. somo
    4. mzazi

INSHA

Andika insha ya kusisimua kuhusu mada ifuatayo

FAMILIA YETU

MARKING SCHEME       

  1. B
  2. B
  3. C
  4. A
  5. A
  6. B
  7. C
  8. A
  9. B
  10. D
  11. D
  12. D
  13. A
  14. D
  15. C
  16. C
  17. A
  18. B
  19. A
  20. C
  21. B
  22. D
  23. A
  24. A
  25. C
  26. B
  27. B
  28. B
  29. A
  30. C                                                                                                                         
Join our whatsapp group for latest updates

Download Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - Grade 4 Opener Exams Term 2 2023 Set 2.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students