Wednesday, 26 April 2023 07:38

Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - Grade 4 End Term 1 Exams 2023 Set 4

Share via Whatsapp

MASWALI

Bi. Wafula: Hamjambo wanafunzi?

Wanafunzi: Hatujambo Bi. Wafula, shikamoo.

Bi. Wafula: Marahaba wanafunzi. Natumai nyote mlikuwa na wikendi njema,

Wanafunzi: Naam Bi. Wafula, asante.

Bi. Wafula: (Huku akitabasamu) Leo katika kipindi chetu tutasoma kuhusu nyumbani. Je, nyumbani ni wapi?

Juma: Nyumbani ni mahali mtu anapoishi.

Bi. Wafula: Heko Juma! Maelezo hayo ni sahihi kabisa. Nyumbani kuna vyumba mbalimbali. Nipe mifano ya vyumba hivi?

Amani: (Kwa furaha) Nyumbani kuna vyumba kama vile sebule, chumba cha malazi, chumba cha kulia na pia mekoni.

Bi Wafula: Vizuri sana Amani. Hivyo basi leo tutaangazia sebule. Sebule ni chumba cha mapumziko. Sebuleni kuna vitu vingi sana kama vile?

Wanafunzi: (Kwa pamoja huku wakitazama picha vitabuni) Kuna makochi, meza, mtoto wa meza, runinga na pia pazia.

Bi. Wafula: Kweli kabisa, makochi na meza huundwa kwa mbao na kwa jina moja huitwa samani. Anayeunda vitu hivi kwa mbao huitwa seremala.

Maswali

  1. Wanafunzi na Bi. Wafula walipatana darasani baada ya
    1. juma
    2. siku
    3. wikendi
    4. likizo.
  2. Kulingana na mazungumzo haya, jibu la 'shikamoo' ni
    1. hatujambo
    2. aheri
    3. njema
    4. marahaba.
  3. Kipi si chumba kinachopatikana nyumbani kulingana na mazungumzo haya?
    1. Sebule.
    2. Chumba cha kuchezea. 
    3. Mekoni.
    4. Chumba cha malazi.
  4. Vitu vinavyoundwa kwa mbao huitwa
    1. kochi
    2. meza
    3. runinga
    4. samani.
  5. Mtu anayeunda vitu kwa kutumia mbao huitwa
    1. seremala
    2. sonara
    3. mhunzi
    4. mwashi.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali la 6-10.

Kijiji cha Pambana kilivamiwa na wezi sugu. Wezi hao walikuwa wakivunja milango ya nyumba za watu usiku na mchana. Walikuwa pia wakiwashambulia watu na kutoroka na mifungo yao. Vitendo hivi vya wizi vilendelea kuenea na kuongezeka. Hivyo basi, wanakijiji hawakuwa na budi ila kupiga ripoti kwenye kituo cha polisi.

Baada ya kuripoti, wanakijiji walishauriwa kuunda milango na nyua thabiti. Vilevile waliunda vikundi vya kujilinda wenyewe. Waliamua kushirikiana pamoja na polisi kupunguza hali ya uhalifu.

Baada ya miezi miwili, visa vya wizi vilipungua. Wanakijiji waliweza kurejea kwa shughuli zao za kila siku bila woga.

Maswali

  1. Taja jina la kijiji kulingana na kifungu.
    1. Pambazuko
    2. Kijiji
    3. Pambana
    4. Kituo.
  2. Kulingana na kifungu, nani aliyewashambulia wanakijiji na kutoroka na mifungo yao?
    1. Polisi
    2. Watu
    3. Wezi
    4. Wanakijiji wenzao.
  3. Visa vya wizi vilipoongezeka, wanakijiji walienda kupiga ripoti wapi?
    1. Shuleni
    2. Kortini
    3. Nyumbani
    4. Kituo cha polisi.
  4. Kulingana na kifungu hiki, wezi hawakuogopa kwani waliwashambulia wanakijiji wakati gani?
    1. Jumatatu na Ijumaa
    2. Asubuhi na jioni
    3. Wakati wa likizo
    4. Usiku na mchana.
  5. Visa vya wizi vilipungua baada ya miezi
    1. moja
    2. miwili
    3. sita
    4. mitatu.

Soma kifungu kifuatacho kwa makini kisha ujibu swali la 11-15

Hapo zamani paliishi sungura na rafiki yake ndovu. Sungura alikuwa mnyama mdogo kuliko ndovu lakini mjanja sana. Ndovu naye, ambaye pia huitwa tembo, alikuwa mkubwa sana na karimu. Ndovu alijitokea sana kusaidia sungura na wanyamapori wengine pale msituni.

Ndovu na sungura walishirikiana kwa kila jambo. Zaidi ya hayo, waliwalea watoto wao pamoja na kwa upendo. Wanyama wengine walitamani sana urafiki ule wa ndovu na sungura. Walijaribu pia kuwatenganisha lakini walishindwa.

Watoto wao pia walikuwa wakiiga urafiki ule wa wazazi wao. Walicheza, kula na kulala pamoja. Kwa kweli, mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.

Maswali

  1. Sungura na ndovu walikuwa
    1. ndugu
    2. marafiki
    3. adui
    4. wanakijiji.
  2. Sungura na ndovu waiishi wapi?
    1. Nyumbani
    2. Mitini
    3. Milimani
    4. Msituni.
  3. Watoto wa sungura na ndovu walikuwa wakipendana kwa sababu ya
    1. urafiki wa wazazi wao
    2. hasira za wazazi wao
    3. kutojuana
    4. njaa.
  4. Ni nini kilichofanya wanyama wengine kuwa na tamaa?
    1. Uadui wa sungura na ndovu.
    2. Watoto wa sungura na ndovu.
    3. Kusaidiana kwa ndovu.
    4. Urafiki wa ndovu na sungura.
  5. Ndovu alikuwa na ukarimi kwa nini?
    1. Alimpiga sungura.
    2. Alisaidia sungura na wanyama wengine.
    3. Aliwafukuza wanyama wengine.
    4. Hakuwapenda watoto wake.

Soma kifungu kifuatacho kwa makini kisha ujaze pengo kwa majibu sahihi (16-20).

Pendo alikuwa msichana wa shule yetu ..................16............... alikuwa mrembo sana. Wazazi wake walikuwa maskini sana.  ..................17............. kumpeleka kwa shangazi yao aliyekuwa tajiri ..................18...............

Pendo alihamia kwa shangazi yake aliyempenda kama mwana ..................19...............Pendo naye akaamua kusoma vitabu ..................20............... kwa bidii.

  1.                      
    1. Sisi
    2. Mimi
    3. Yeye
    4. Wao
  2.                  
    1. Tuliamua
    2. Waliamua
    3. Aliamua
    4. Mliamua
  3.                
    1. sana
    2. mbali
    3. nyingi
    4. kidogo
  4.                  
    1. chake
    2. wake
    3. zake
    4. lake
  5.              
    1. wake
    2. zake
    3. chao
    4. vyake

Kuanzia swali la 21 hdi 30, jibu kila Swali kulingana na maagizo uliyopewa.

  1. Bibi na pipi ni vitate. Vile vile, kitate cha papa ni
    1. bata
    2. paka
    3. kata
    4. baba
  2. Mama amenunua rinda..................................
    1. mwekundu
    2. jekundu
    3. lekundu
    4. nyekundu
  3. Chagua neno ambalo ni si kitenzi kati ya haya.
    1. Cheza
    2. Kula
    3. Lia
    4. Mwalimu
  4. Jibu la salamu 'alamsiki' ni .....................................
    1. binuru
    2. nawe pia
    3. aheri
    4. buriani
  5. Kabla ya kuvuka njia, Juma alisimama ....................... barabara.
    1. juu ya
    2. kando ya
    3. ndani ya
    4. katika ya
  6. Tambua kiunganishi katika sentensi hii.
    Mtoto aliadhibiwa kwa sababu ya utundu wake.
    1. mtoto
    2. aliadhibiwa
    3. kwa sababu
    4. utundu
  7. Tegua kitendawili kifuatacho.
    Popote niendapo hunifuata.
    1. Macho
    2. Kivuli
    3. Mtoto
    4. Rafiki.
      Tumia kielezi sahihi kukamilisha sentensi hizi.
  8. Chui hukumbia..................................
    1. mbio
    2. polepole
    3. kabisa
    4. ovyo
  9. Kobe hutembea .................................
    1. ovyo
    2. haraka
    3. polepole
    4. sana.
  10. Andika wingi wa sentensi ifuatayo.
    Mwanafunzi anasoma kitabu.
    1. Mwanafunzi anasoma vitabu. 
    2. Wanafunzi wanasoma kitabu.
    3. Mwanafunzi wanasoma kitabu. 
    4. Wanafunzi wanasoma vitabu.
  11. Chagua alama ifaayo kuakifisha sentensi ifuatayo.
    Je...............................wewe utaenda kwao?
    1. !
    2. ?
    3. " "

INSHA

Andika insha ya kusisimua kuhusu:

SIKU YA KUFUNGA SHULE

..........................................................................................................................................................................................................................................

MWONGOZO

swa ms

Join our whatsapp group for latest updates

Download Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - Grade 4 End Term 1 Exams 2023 Set 4.

Tap Here to Download for 30/-

Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students