Thursday, 20 April 2023 09:04

Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - Grade 5 End Term 1 Exams 2023 Set 4

Share via Whatsapp

KUSIKILIZA NA KUZUNGUMZA

Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali

G5SwaT1TW23003P1

(Ni siku ya Jumamosi asubuhi. Sofia anakutana na Pendo barabarani) 
Sofia :   (akimkumbatia) Sabalkheri rafiki yangu!
Pendo : (kwa tabasamu) Aheri sahibu yangu.
Sofia :   Leo umevalia mavazi ya kupendeza na kujipamba kwa mapambo ya kipekee. Unaenda wapi?
Pendo : Ninaelekea kanisani kuhudhuria harusi ya shangazi yangu. Harusini ni lazima mtu awe maridadi kama
              kipepeo.
Sofia :   (Akimtazama kwa makini) Naomba unieleze baadhi ya mapambo yako.
Pendo : Nitafurahia kufanya hivyo. Kwanza shingoni nimevaa mkufu na kidami.
Sofia :   Na kwenye kiwiko cha mkono umevaa pambo gani?
Pendo : (Akimwonyesha) pambo hili linaitwa bangili.
Sofia :   Asante. Ninaona linametameta sana.
Pendo : Puani pia nina kikero na kipini. Kipini ni hiki kwenye upande wa kushoto wa pua na kikero kwenye
              upande wa pua.
Sofia :   Ninaona pia una vipuli masikioni.
Pendo : Ndiyo. Hivi nilinunuliwa na mama yangu.
Sofia :   Kusema kweli sijawahi kuona ukivutia hivi. Nitakuruhusu uende ili usichelewe kufika harusini.
Pendo : Kwaheri!
Sofia :   Kwaheri ya kuonana.

 1. Sofia na Pendo walikutana wakati gani?
  1. Jioni
  2. Asubuhi
  3. Adhuhuri
  4. Usiku
 2. Maneno yafuatayo yametumiwa katika mazungumzo. Lipi ni la maagano
  1. Sabalkheri
  2. Aheri 
  3. Asante
  4. Kwaheri
 3. Pendo alikuwa amevaa mapambo haya yote isipokuwa
  1. Kidani
  2. Mkufu
  3. Kikero
  4. Herini
 4. Kulingana na mazungumzo haya jina rafiki lina maana sawa na
  1. ndugu
  2. pendo
  3. sofia
  4. sahibu
 5. Katika mazungumzo uliyoyasoma Pendo na Sofia walizungumzia nini hasa? 
  1. Harusi
  2. Mapambo
  3. Mavazi
  4. Kanisa

Swali la 6 hadi la 9

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.

G5SwaT1TW23003P2

Likizo yangu ya katikati ya muhula ilikuwa na shughuli nyingi. Tuliporuhusiwa kwenda nyumbani nilifurahi sana kwa sababu nilikuwa nimewajibika vizuri katika masomo yangu shuleni. Nilikuwa nikikamilisha shughuli zangu zote darasani, miradi yangu ilikuwa bora zaidi darasani, usafi wangu na nidhamu zilikuwa za hali ya juu

Wazazi wangu walikuwa wameniahidi zawadi kama ningekuwa na ripoti nzuri kutoka kwa mwalimu. Bila shaka ripoti yangu ilikuwa ya kupendeza. Wazazi wangu walipoiona walifurahi sana. Nilinunuliwa tableti ya kunisaidia kufanya kazi yangu ya shuleni pamoja na kuwasiliana na wenzangu.

Katika likizo hiyo fupi niliwasaidia wazazi wangu kufanya shughuli za kilimo na ufugaji wa ng'ombe. Nilisaidia kupanda mahindi na maharagwe shambani kwa sababu mvua ilikuwa karibu kunyesha. Aidha nilisaidia kuwakatia ng'ombe majani, kuwapa maji, kukama na kuenda kuuza maziwa. Wazazi wangu walifurahia sana kwa kuwasaidia katika kazi.

Isitoshe nilifanya mradi tuliokuwa tumepewa na mwalimu wetu wa Kiswahili. Mradi huo ulikuwa kukusanya mapambo mbalimbali. Wazazi wangu walishirikiana nami kutafuta mapambo hayo.

Nilifurahia sana likizo hiyo na niliporudi shuleni niliendelea na masomo yangu vyema. 

 1. Likizo iliyozungumziwa ni gani?
  1. Ya mwezi wa nane
  2. Ya mwezi wanne
  3. Ya mwisho wa mwaka
  4. Ya katikati ya muhula
 2. Kwa nini mwandishi alinunuliwa rununu?
  1. Kwa kupata ripoti nzuri kutoka kwa mwalimu
  2. Kwa kukamilisha kazi yake shuleni
  3. Kwa kuwa mwanafunzi safi zaidi
  4. Kwa sababu ilikuwa likizo
 3. Ni kweli kusema kuwa wazazi wa mwandishi:
  1. Hufuga kuku
  2. Hukuza mimea na kufuga ng'ombe
  3. Ni wakulima na wafanyabiashara
  4. Ni wakulima na walimu
 4. Hali ya mwandishi kufanya kazi pamoja na wazazi wake inadhihirisha maadili gani?
  1. Ukarimu
  2. Utengano
  3. Umoja
  4. Usawa

Swali la 10 hadi la 12
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.

G5SwaT1TW23003P3

Taji ni mvulana anayependa kula lishe bora. Ameupanga mlo wake vizuri ili asikose viini lishe muhimu katika mwili wake. Kabla ya kula chakula huwa anakula matunda na kungoja dakika thelathini. Licha ya hayo huwa anakunywa maji ya kutosha kila siku. Ifuatayo ndiyo ratiba yake. Lishe bora humsaidia kuwa na afya nzuri na kuweza kufanya shughuli zake vyema. Ifuatayo ni ratiba yake. 

 Asubuhi   Adhuhuri   Jioni 
 Maziwa glasi moja   Pilau   Ugali 
 Viazi vikuu  Nyama ya samaki   Maharagwe 
 Mboga za kiasili  Sukumawiki  Mboga za kiasili 
 Embe moja  Embe moja   Papai moja 

 

 1. Chakula ambacho Taji hula siku inapoanza ni gani?
  1. Kilalio
  2. Matunda
  3. Kifungua kinywa
  4. Maji
 2. Ni chakula gani ambacho Taji hula katika kila mlo?
  1. Mboga za kiasili
  2. Matunda
  3. Pilau
  4. Ugali
 3. Kwa nini Taji hula lishe bora?
  1. Ili awe na afya bora
  2. Ana ratiba nzuri
  3. Kwa sababu ni mvulana
  4. Ili ashibe

Swali la 13 hadi la 15

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.

G5SwaT1TW23003P4

Hapo zamani za kale Kuku na Kanga walikuwa marafiki. Marafiki hawa walikuwa na maumbile sawa. Walifanya mambo yao pamoja. Walichakura pamoja wakitafuta chakula. Vifaranga wao nao walicheza pamoja.

Siku moja Kuku alimwomba Mwewe sindano ili awashonee vifaranga wake fulana. Mwewe alikuwa jirani yao. Baada ya kuitumia sindano hiyo, Kuku aliiweka kabatini. Kuku alipokwenda kutafuta chakula, kifaranga wake mmoja alichukua sindano hiyo. Alianza kushona kitambaa jinsi alivyomwona mama yake akishona.

Mwewe alipotaka sindano yake, Kuku aliitafuta kabatini, hakuipata. Kifaranga aliyechukua sindano hiyo alimwambia mama yake kwamba sindano ilipotea. Kuku aliwaambia vifaranga wake waanze kuchakura ili watafute sindano ya Mwewe. Waliitafuta sindano kila mahali bila mafanikio.

"Usiponipa sindano yangu nachukua kifaranga mmoja kila siku," Mwewe alimwambia kuku. Mwewe alianza kuchukua kifaranga mmoja kila siku. Vifaranga wa Kuku na Kanga walianza kupungua. Kanga alipojua kilichokuwa kinaendelea, aliamua kuwachukua vifaranga wake waliobaki na kwenda kichakani. Aliwabandika vitone vya pamba kwa kutumia gundi. Wakawa na madoa meupe. Mwewe alishindwa kuwatambua.

Ukiwaona kuku na Kanga wanachakura, jua tu bado wanatafuta sindano ya Mwewe.

 1. Vifaranga wa Kuku na Kanga walifanya nini pamoja?
  1. Kuchakura wakitafuta chakula
  2. Kuchakura wakitafuta sindano ya mwewe
  3. Walicheza pamoja
  4. Kulala pamoja
 2. Kuku anawajali vifaranga wake kwani:
  1. Alitaka kuwashonea fulana.
  2. Aliomba sindano
  3. Aliwashonea kitambaa
  4. Alicheza nao
 3. "Mwewe alishindwa kuwatambua. "Neno kuwatambua lina maana gani?
  1. Kuwala
  2. Kuwaona
  3. Kuwajua
  4. kuwapenda

Soma kifungu kifuatacho. Kina nafasi 16 hadi 20. Umepewa majibu manne hapo. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.

Timu ___16___ shule yetu ilishiriki katika mechi. ___17___ walikuwa wakiwashangilia ili washinde. Mchezaji ___18___ alianguka na kupata ___19___ miguuni na mikononi. Maskauti walimpa ___20___  kisha akapelekwa zahanatini.

   A   B   C   D 
 16.   wa   ya   kwa   mwa 
 17.  Wanafunzi   Watu   Mashabiki   Walimu 
 18.  wa moja  kimoja   moja   mmoja 
 19.  majeraha  alama   damu  vidonda 
 20.  zawadi  huduma ya kwanza   matibabu   ibada 

 

Swali la 21-30

SARUFI

 1. Tazama picha hizi kisha ujibu maswali
  G5SwaT1TW23003Q21
  Shughuli zilizo kwenye picha ni za ________________________
  1. Kujipamba
  2. Huduma ya kwanza
  3. Mapishi
  4. Kilimo
 2. Chagua jibu lenye nomino za aina moja.
  1. Kenya, Alhamisi
  2. kiti, ukweli
  3. Thurea, meza
  4. Mwanajeshi, furaha
 3. Chagua sentensi iliyoakifishwa kwa usahihi.
  1. Kuku anapenda, kuchakura mchangani?
  2. Unakula nini, siku ya Jumapili.
  3. Je, Mto Athi una samaki wengi?
  4. Tito atawaheshimu walimu wake,
 4. Chagua jibu sahihi kujaza nafasi. ________________ za babu yangu zilitengenezwa na  seramala hapo _________________
  1. Zamani, samani
  2. Thamani, samani
  3. Samani, zamani
  4. Amani, zamani
 5. Panga maneno haya kama yanavyofuatana katika kamusi. 
  (filamu, firimbi, fyonza, fulana, faulu)
  1. Fyonza, fulana, firimbi, filamu, faulu
  2. Faulu, filamu, firimbi, fulana, fyonza
  3. Faulu, fulana, fyonza, filamu, firimbi
  4. Faulu, filamu,fulana, firimbi, fyonza
 6. Nomino zifuatazo zinafaa kuwa za ngeli moja. Chagua nomino iliyo katika ngeli tofauti.
  1. Saa
  2. Pete
  3. Barua
  4. Joto
 7. Andika sentensi ifuatayo katika wingi. Kalamu ya wino ilitumiwa na mwanafunzi.
  1. Kalamu za wino zilitumiwa na wanafunzi.
  2. Kalamu vya wino vilitumiwa na wanafunzi
  3. Kalamu za wino zilitumiwa na mwanafunzi
  4. Kalamu ya wino ilitumiwa na wanafunzi.
 8. Ni maamkuzi au maagano gani hayajaambatanishwa vizuri na jibu lake?
  1. Shikamoo- marahaba
  2. Alamsiki- nawe pia
  3. Kwaheri- ya kuonana
  4. Buriani- buriani dawa
 9. Kifaa hiki hutusaidia kujua __________________________
  G5SwaT1TW23003Q29
  1. wakati 
  2. hali ya anga
  3. sehemu
  4. hali ya joto mwilini
 10. Jina la heshima la kumwita mwanamume ni _________________________
  1. bibi
  2. bwana
  3. ndugu
  4. somo

INSHA

Andika insha kuhusu mada ifuatayo:

HARUSI YA KUPENDEZA 

MARKING SCHEME

 1. B
 2. D
 3. D
 4. D
 5. B
 6. B
 7. A
 8. B
 9. C
 10. B
 11. B
 12. A
 13. C
 14. A
 15. C
 16. B
 17. A
 18. D
 19. A
 20. B
 21. C
 22. A
 23. C
 24. C
 25. B
 26. D
 27. A
 28. B
 29. A
 30. B
Join our whatsapp group for latest updates

Download Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - Grade 5 End Term 1 Exams 2023 Set 4.


Tap Here to Download for 30/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students