Thursday, 20 April 2023 08:54

Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - Grade 5 End Term 1 Exams 2023 Set 2

Share via Whatsapp

MAAGIZO

Karatasi hii ina sehemu tano kuu.

Jibu maswali yote kulingana na maagizo.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata.
KISWgrd501

Fisi na wenzake walialikwa katika sherehe kubwa kule mjini. Pamoja na Fisi, wanyama wengine walioalikwa walikuwa Sungura, Ndovu na Nyoka. Sherehe hiyo ilikuwa ya harusi kati ya Chui na Kondoo. Walipofika katika sherehe hiyo, walipata sherehe ilikuwa imeanza. Baada ya nyimbo kuimbwa, wakati wa kuunganishwa ulifika. Chui na Kondoo walitangazwa kuwa mke na mume. Shangwe na kelele zilisikika hewani. Hatua iliyofuata ilikuwa ya kufurahia mlo. Huo ndio wakati ambao fisi alikuwa amesubiri kwa hamu. kuu.

Jambo lililomfurahisha fisi kabisa ni kuwa kila mmoja alipewa nafasi ya kujipakulia. Fisi alijaza sahani yake kwa nyama za kila aina: kuku, mbuzi, samaki, ng'ombe. Pia alichukua matunda na mboga. nyingi sana ingawa hakupenda kula mboga na matunda. Hata kabla ya kuanza kula, kelele zilisikika kuwa moto ulikuwa ukiwaka katika nyumba hiyo. Wanyama wengine wote walianza kutoroka. Fisi alishangaa iwapo alifaa kuacha chakula ama aendelee kula. Aliendelea kufurahia vipande vya nyama huku akiramba vidole. Mara moto ulikuwa umemfikia. Alipiga kelele lakini moto ulikuwa umemfikia. Ingawa aliweza kutoka nje, miguu yake ya nyuma ilichomeka.

  1. Ni nini kilichofanyika kabla ya Chui na Kondoo kutangazwa kuwa mke na mume?
    1. Moto ulianza kuwaka
    2. Shangwe na kelele zilisikika
    3. Chakula kilianza kuliwa
    4. Nyimbo ziliimbwa
  2. Kifungu kinaeleza kuwa wanyama katika sherehe hiyo walikuwa aina wangapi?
    1. 6
    2. 5
    3. 7
  3.  Kisa hiki kinaeleza sababu ya;
    1.  fisi kupenda kula.
    2. miguu ya fisi kuwa mifupi.
    3. fisi kutojua kukimbia.
    4. fisi kutopenda nyama.
  4. Kutokana na kisa hiki, tunajifunza kuwa;
    1.  tusiende sherehe.
    2. wanyama wasikusanyike pamoja.
    3. tamaa ni mbaya.
    4. chakula kisiliwe katika harusi.
  5. Lengo kuu la fisi kuhudhuria sherehe lilikuwa gani?
    1. kufurahia nyimbo
    2. kufurahia harusi
    3. kukutana na wenzake
    4.  kufurahia chakula
  6. Methali gani inayoweza kueleza kisa hiki?
    1. Tamaa mbele mauti nyuma.
    2. Polepole ndio mwendo.
    3. Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.
    4. Achanikaye kwenye mpini hafi njaa.

Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata.
KISWgrd502

Siku moja wakati wa likizo ya muhula wa kwanza, Kalondu aliamshwa asubuhi na mapema. Kwa kuwa Kalondu hakuenda shuleni, mama yake alimpa maagizo kabla ya kutoka. Mama yake alikuwa akienda sokoni Butere ambako aliuza vyombo mbalimbali vya kutumia jikoni. Kabla ya kutoka, mama yake alimwambia kuwa asitoke nyumbani. Hii ni kwa sababu wezi wangeingia nyumbani kwao na kuiba vitu katika nyumba. Pili aliambiwa kuwa asitumie kifaa chochote cha kidijitali kuingia mtandaoni bila idhini ya mama yake.

Mama alimwacha akinywa chai pale sebuleni huku akitazama vibonzo kwenye runinga. Kalondu alipomaliza kunywa chai, alishindwa cha kufanya. Alitoka nje ya nyumba na kuona kuwa watoto wengine walikuwa wakiendesha baiskeli njiani. Alijipenyeza polepole na kutoka nje ya boma. Watoto hao walimpa baiskeli na kumwambia kuwa asiendes he haraka. Kalondu alianza polepole lakini baada ya muda kidogo aliendesha haraka sana. Mara alianguka chini kwenye jiwe. Kalondu aliumia goti lake na mkono.

  1. Kwa nini Kalondu hakuwa ameenda shuleni siku hiyo?
    1. mama yake alimkataza
    2. mama yake alitaka kuenda sokoni
    3.  ilikuwa siku ya Jumamosi
    4. ulikuwa wakati wa likizo
  2. Kwa nini mama alimshauri Kalondu asitoke nyumbani?
    1.  Ili wezi wasiingie nyumbani kwao na kuiba
    2.  Ili asiumie wakati akiendesha baiskeli
    3. Ili asipotee akiwa peke yake
    4. Ili asaidie kufanya kazi za nyumbani
  3. Unadhani kwa nini mama hakutaka Kalondu atumie kifaa cha kidijitali kuingia mtandaoni bila idhini?
    1. Kwa kuwa ni vibaya kutumia kifaa cha kidijitali 
    2. Kwa kuwa hakiwezi kufanya kazi kama mama hayuko
    3. Kwa kuwa angejipata kwenye mitandao isiyofaa
    4. Pengine kifaa hicho kilikuwa kimeharibika
  4. Ungekuwa Kalondu, ungefanya nini baada ya kunywa chai?
    1. Ningerudi kulala
    2. Ningesoma kitabu cha hadithi
    3.  Ningeenda nje kucheza
    4. Ningeenda jikoni kupika
  5. Methali gani ambayo haiwezi ikatumika kumshauri Kalondu?
    1. Harakaharaka haina baraka.
    2. Asiyesikia la mkuu huvunjika guu.
    3. Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.
    4. Pole pole ndio mwendo.
  6. Yawezekana kuwa mama wa Kalondu aliuza nini kati ya vifaa vifuatavyo?
    1.  kikaango
    2. baiskeli za watoto
    3. viti
    4. vitabu

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata.

Maji yana umuhimu sana katika maisha yetu. Hutumika kufanya mambo mbalimbali maishani. Jambo la msingi ni kuwa maji hutumika katika upishi na kudumisha usafi. Kutokana na hayo, ni jambo la busara kuyatunza maji. Hatufai kuyaharibu maji kwa njia yoyote. Vilevile, tusichafue vyanzo vya maji kama vile mito na bahari. Shughuli kama vile kuoga na kufua hazifai kufanyikia kwenye mito, bahari na maziwa. Uharibifu wa bahari, mito na maziwa huweza kuwaangamiza viumbe wa majini kama vile samaki na kaa. Kila mkenya anafaa kuyajali mazingira yao. Tukihifadhi mazingira, tutaishi maisha bora yasiyokuwa na matatizo mengi.

  1. Ni kweli kuwa maji hutumika kufanya;
    1. mambo mengi. 
    2. mambo machache.
    3. mambo mawili.
    4. mambo ya mbali.
  2. Ni keli kuwa maji;
    1. yanajua kupika.
    2. hayafai kutunzwa.
    3. hutumika katika usafi.
    4. hayana faida maishani.
  3. Tunafaa kufanya nini ili tuishi maisha yasiyokuwa na matatizo mengi?
    1. Kuzingatia lishe bora
    2. Kunywa maji mengi
    3. Kutooga mtoni
    4. Kuhifadhi mazingira

Chagua jibu linalofaa ili kujazia kila nafasi iliyoachwa.

Siku       16       Juma alikuwa akicheza uwanjani. Rafiki       17       ambaye wanapendana sana alijiunga na yeye. Walianza kucheza huku wakiruka     18          furaha. Walipomaliza, waliingia      19           wakala chakula kitamu sana. Walipomaliza kula, walikunywa maji       20          kisha wanaenda kumsaidia mzazi wa Juma kukusanya kuni kwenye shamba lao.

16  A. moja  B. kimoja  C. mmoja  D. umoja 
 17  A. wake  B. wangu  C. zake  D. yake
 18   A. kwenye  B. katika  C. na  D. kwa
 19  A. kwa nyumba  B. katika nyumba  C.ndani mwa nyumba  D.katika nyumbani
 20  A. mingi   B. mengi  C.nyingi  D.wengi

Jibu maswali yanayofuata kulingana na maagizo.

  1. Jibu gani linaloonyesha nomino ya wingi?
    1.  maji
    2. kalamu
    3. kitabu
    4. magari
  2. Onyesha pambo ambalo huvaliwa kwenye shingo.
    1. kikero
    2. herini
    3. bangili
    4. ushanga
  3. Chagua sentensi iliyotumia nomino ya dhahania.
    1. Tutaenda Mombasa kesho.
    2. Maji safi ni ya mgeni.
    3. Mpira wake ni mpya.
    4. Uzalendo ni muhimu kwetu.
  4. Chakula gani ambacho huokwa kati ya vyakula vifuatavyo?
    1. nyama
    2. keki
    3. mihogo
    4. ugali
  5. Umati ni wa watu kama vile mkungu ni wa
    1. ndizi
    2. maua
    3. mboga
    4. funguo 
  6. Nomino za pekee zinahusu yafuatayo isipokuwa;
    1. Majina ya miezi ya mwaka
    2. Majina ya siku za wiki
    3. Majina ya mahali
    4. Majina ya vyakula
  7. Panga maneno yafuatayo jinsi yanavyofuatana kwenye kamusi.
    1. mchana
    2. mdudu 
    3. mama
    4. mbuzi
      1. ii, iii, iv, i
      2. iii, iv, i, ii
      3. iii, ii, iv, i
      4. i, ii, iii, iv
  8. Jibu gani linaloonyesha matumizi ya herufi kubwa?
    1. Hutumika mwishoni mwa sentensi
    2. Hutumia kuanzisha nomino za pekee
    3. Hutumika kuandika mkato wa maneno
    4. Hutumika kuonyesha wingi wa nomino
  9. Unapotumia tarakilishi, kile unachokiandika huonekana kwenye
    1. bodidota
    2. kiwambo
    3. kebo
    4. kitengo kikuu cha uc' ukataji
  10. 'Koma' pia huitwa
    1. kiulizi
    2. mkato
    3. kikomo
    4. kitone

INSHA

Andika insha ya masimulizi kuhusu;

MKASA WA MOTO KIJIJINI.



MARKING SCHEME 

  1. D
  2. B
  3. B
  4. C
  5. D
  6. A
  7. D
  8. A
  9. C
  10. B
  11. C
  12. A
  13. A
  14. C
  15. D
  16. A
  17. D
  18. D
  19. B
  20. B
  21. A
  22. D
  23. D
  24. B
  25. A
  26. D
  27. B
  28. D
  29. B
  30. B
Join our whatsapp group for latest updates

Download Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - Grade 5 End Term 1 Exams 2023 Set 2.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students