Tuesday, 27 June 2023 08:01

Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - Grade 4 Mid Term 2 Exam 2023 Set 2

Share via Whatsapp

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata.

G4SwaMT2S22023Q1

Mzee Juma ni mkulima anayejulikana kote katika kijiji cha Jomvu. Hii ni kutokana na shughuli zake za kilimo. Amefuga wanyama kama vile mbuzi, ng'ombe, kondoo, nguruwe na punda. Vilevile, amefuga kuku, bata, batamzinga na njiwa. Mzee Juma pia ana shamba kubwa lililo karibu na Mto Kijitonyama. Yeye hutumia maji ya mto huo msimu wa kiangazi ili kuinyunyizia mimea yake maji. Hali hiyo ya kunyunyizia mimea yake maji husaidia ili isinyauke wala kukauka. Kujulikana kwake kulitokana na hali ya kuwauzia wanakijiji mazao ya shambani au maziwa na mayai yaliyotokana na ufugaji wake.

Vilevile, Mzee Juma aliwafunza watoto wake shughuli hizo. Alielewa kuwa mtoto hufuata mwelekeo anaopewa na mzazi wake. Wakati wa likizo, wikendi na sikukuu, watoto hao walishirikiana na wazazi wao kufanya shughuli za shambani au ufugaji. Ungepata wakisaidia katika kupalilia mimea, kuvuna mazao au kubeba mazao yaliyovunwa. Pale nyumbani, ungewaona wakishughulika katika kuokota mayai yaliyotagwa, kuwakama ng'ombe au kuwalisha mifugo hao.

 1. Ni kweli kuwa Mzee Juma ni;
  1. mwalimu
  2. mkulima
  3. daktari
  4. dereva
 2. Kwa nini Mzee Juma anajulikana katika kijiji chote?
  1. Ana watoto wenye nidhamu.
  2. Ana mashamba makubwa.
  3. Kutokana na shughuli zake za kilimo.
  4. Ana mifugo wengi.
 3. Maneno 'mtoto hufuata mwelekeo anaopewa na mzazi wake' yanaweza yakaelezwa kwa methali gani?
  1. Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.
  2. Polepole ndio mwendo.
  3. Siku za mwizi ni arubaini.
  4. Asiyesikia la mkuu huvunjika guu.
 4. Ni nini ambacho Mzee Juma hakuwauzia wanakijiji?
  1. maziwa
  2. mazao ya shambani
  3. wanyama
  4. mayai
 5. Ni kweli kuwa Mto Kijitonyama humpa Mzee Juma maji ya;
  1. kunywesha mifugo.
  2. kuoga.
  3. kufua nguo.
  4. kunyunyizia mimea.
 6. Kwa nini watoto wa Mzee Juma walisaidia wazazi wao wakati wa likizo, wikendi na sikukuu pekee?
  1. Walienda shuleni wakati huo mwingine.
  2. Walikuwa wakicheza wakati huo mwingine.
  3. Wakati huo mwingine walienda kanisani.
  4. Wakati huo mwingine walienda kumtembelea nyanya yao.
 7. Pale nyumbani, watoto wangefanya yafuatayo isipokuwa;
  1. kuokota mayai yaliyotagwa
  2. kuwakama ng'ombe
  3. kuwalisha mifugo
  4. kupalilia mimea

Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata.

G4SwaMT2S22023Q2

Kompyuta au tarakilishi ni kifaa cha kidijitali chenye umuhimu mkubwa. Kifaa hicho hupatikana katika afisi za kazini, shuleni, hospitalini au nyumbani. Kompyuta ina sehemu kama vile bodidota, kiwambo, kitengo kikuu cha uchakataji, kipanya na kebo. Unapotaka kupiga chapa kwenye tarakilishi, tumia bodidota kuandika. Yale unayoyaandika huonekana kwenye kiwambo. Kipanya nacho huelekeza shughuli mbalimbali, kwenye kiwambo. Kitengo kikuu cha uchakataji hufanya shughuli zote za kompyuta kama vile kupokea ujumbe, kuuchanganua, kuhifadhi na kutuma ujumbe huo. Kazi ya kebo ni kupitisha umeme au data ya kidijitali.

Katika matumizi ya tarakilishi na vifaa vingine vya kidijitali, ni vyema kuomba ruhusa kutoka kwa mzazi, mlezi au mwalimu wako. Kabla ya kutumia kifaa cha kidijitali, unafaa kuhakikisha kuwa kifaa hicho kimeunganishwa na umeme. Kompyuta hutumika kupiga chapa, kusikiliza muziki, kucheza michezo ya tarakilishi, kutafuta maarifa kwenye mtandao, kujionea picha mtandaoni na kadhalika. Jambo muhimu ni kuwa si vyema kutumia vifaa vya kidijitali kwa muda mrefu. Ukiangalia mwangaza unaotoka kwenye vifaa hivyo kwa muda mrefu, unaweza ukapata matatizo ya macho.

 1. Kulingana na kifungu, jina jingine la kompyuta ni ____________________________.
  1. runinga
  2. rununu
  3. tarakilishi
  4. televisheni
 2. Maneno 'kuomba ruhusa' ni mfano wa nini?
  1. nahau
  2. methali
  3. tashbihi
  4. kitendawili
 3. Ni nani ambaye mwanafunzi hawezi kuomba ruhusa kutoka kwake kabla ya kutumia kifaa cha kidijitali?
  1. mwalimu
  2. mwanafunzi
  3. mzazi
  4. mlezi
 4. Mwanafunzi akiwa shuleni, anashauriwa kutumia tarakilishi kufanya nini?
  1. kusikiliza muziki
  2. kucheza michezo ya tarakilishi
  3. kutafuta maarifa kwenye mtandao
  4. kujionea picha mtandaoni
 5. Jambo muhimu ni kuwa si vyema;
  1. kutumia vifaa vya kidijitali.
  2. kubeba vifaa vya kidijitali.
  3. kuweka vifaa vya kidijitali kwa muda mrefu..
  4. kutumia vifaa vya kidijitali kwa muda mrefu.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata.

G4SwaMT2S22023Q3
Bendera ya taifa la Kenya ina rangi nne muhimu. Rangi nyeupe huonyesha amani. Amani ni hali ya utulivu ambao hudumu katika taifa lolote. Rangi nyeusi nayo huonyesha rangi ya wakenya. Wakenya hujulikana kwa rangi ya mwafrika ambayo ni nyeusi. Ni vyema kukubali na kufurahia jinsi ambavyo tumeumbwa. Maumbile ya mtu ni uamuzi ambao ulifanywa na Mungu. Rangi ya kijani kibichi, huonyesha mimea inayopatikana kwenye ardhi yetu. Miti, nyasi na mimea mingine ni muhimu sana kwa kila mkenya. Hatimaye, rangi nyekundu hutukumbusha kuwa kuna watu waliopigania uhuru wetu. Katika hali hiyo ya kupigania uhuru, kuna damu iliyomwagika. Kuipenda bendera yetu ni ishara ya uzalendo.

 1. Rangi gani ambayo hutukumbusha uhuru wetu ulivyopatikana?
  1. nyekundu
  2. nyeupe
  3. nyeusi
  4. kijani
 2. Ni nini tunachofaa kufanya ili kuonyesha kuwa miti, nyasi na mimea mingine ni muhimu?
  1. kupanda miti na nyasi zaidi.
  2. kukata miti iliyo mingi.
  3. kuchoma takataka kila mahali.
  4. kuwa na michoro ya nyasi, miti na mimea.
 3. Chagua maana ya neno 'uzalendo' jinsi lilivyotumika katika kifungu.
  1. kujua rangi za bendera
  2. kupenda mazingira
  3. kuipenda nchi
  4. kuipenda bendera

Chagua jibu lifaalo ili kujazia nafasi zilizoachwa.

Paka ni mnyama __16__ anapendwa sana katika nyumba __17__. Paka wengi hupenda kutulia nyumbani bila tatizo lolote. Chakula __18__ na paka sana ni panya. Paka __19__ panya wanaoharibu vitu katika nyumba. Unapofuga paka, ni vigumu sana kwa __20__ kuharibiwa sebuleni na panya.

   A   B   C   D 
 16.   ambayo   ambalo   ambao   ambaye 
 17.  mengi  mingi   nyingi   zingi 
 18.  inayopendwa   kinaopendwa   kinachopendwa   inachopendwa 
 19.  huwala  huwakula   hukulwa   hukuliwa 
 20.  kitanda  kinu   kochi   mbuzi 

 

Jibu kila swali kulingana na maagizo.

 1. Jua huchomoza upande gani wa dira?
  1. Kaskazini
  2. Mashariki
  3. Magharibi
  4. Kusini
 2. Chagua jibu ambalo linaonyesha kitenzi.
  1. ruka
  2. kitabu
  3. mzuri
  4. huyu
 3. Tambua kiwakilishi kwenye sentensi ifuatayo.
  Huyu amekula chakula kitamu.
  1. kitamu
  2. amekula
  3. chakula
  4. huyu
 4. Tegua kitendawili;
  Chalia, chatembea na chala chakula cha mkono.
  1. kengele
  2. saa
  3. mtoto
  4. mbuzi
 5. Tambua aina za maneno yaliyopigiwa mistari.
  Mwanafunzi mzuri anasoma polepole.
  1. kivumishi, kitenzi
  2. kiwakilishi, kielezi
  3. kielezi, nomino
  4. kivumishi, kielezi
 6. Nomino gani ambayo haipatikani katika Ngeli ya A - WA?
  1. kipepeo
  2. mbuzi
  3. mti
  4. chawa
 7. Chagua wingi wa;
  Mkeka wa mtume umewekwa.
  1. Mikeka ya mitume imewekwa. 
  2. Mikeka ya mitume yamewekwa.
  3. Mikeka ya watume imewekwa.
  4. Mikeka ya watume yamewekwa.
 8. Nomino gani inayopatikana katika ngeli ya LI-LI?
  1. jiwe
  2. darasa
  3. giza
  4. jicho
 9. Jibu la 'chewa' ni _____________________
  1. ewaa
  2. chewa
  3. njema
  4. marahaba
 10. Ni vizuri _______________________ ndipo uingie ndani ya nyumba.
  1. upige makofi 
  2. upige pasi
  3. upige mbio
  4. upige hodi

INSHA

Andika insha ya wasifu kuhusu,

                                                                          NYUMBANI KWETU.
___________________________________________________________________________________________

___________________________________________________________________________________________

___________________________________________________________________________________________

___________________________________________________________________________________________

___________________________________________________________________________________________

___________________________________________________________________________________________

___________________________________________________________________________________________

___________________________________________________________________________________________

___________________________________________________________________________________________

___________________________________________________________________________________________

___________________________________________________________________________________________

___________________________________________________________________________________________

___________________________________________________________________________________________

___________________________________________________________________________________________

___________________________________________________________________________________________

___________________________________________________________________________________________

MARKING SCHEME

 1. B
 2. C
 3. A
 4. C
 5. D
 6. A
 7. D
 8. C
 9. A
 10. B
 11. C
 12. D
 13. A
 14. A
 15. C
 16. D
 17. C
 18. C
 19. A
 20. C
 21. B
 22. A
 23. D
 24. B
 25. D
 26. C
 27. A
 28. C
 29. B
 30. D
Join our whatsapp group for latest updates

Download Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - Grade 4 Mid Term 2 Exam 2023 Set 2.


Tap Here to Download for 30/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students