Wednesday, 26 April 2023 07:34

Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - Grade 4 End Term 1 Exams 2023 Set 3

Share via Whatsapp

MASWALI

Kusikiliza na kuzungumza
Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali 1-5

(Runo ameketi kwenye kivuli pamoja na baba yake wakizungumziana)

Runo: (akimsogelea Baba) Shikamoo Baba?

Baba: (kwa tabasamu) Marahaba mwanangu! Habari za shule?

Runo:  Njema baba! (kimya) Baba, nikwambie tulichosoma leo?

Baba: Naam, nieleze mwanangu!

Runo:  Leo tulifunzwa kuhusu nidhamu mezani.

Baba:  Hilo ni somo zuri sana.

Runo:  Mwalimu alituelezea kidogo kisha akatuambia tujadiliane na wazazi wetu. Nidhamu mezani ni nini?

Baba:  Aha! Runo, nidhamu mezani ni tabia nzuri ya mtu kabla ya kula, anapokula na baada ya kula.

Runo:  Ooh! Nimeelewa.

Baba:  Mwanangu, kabla hujala unafaa kunawa mikono kwa maji safi na sabuni.

Runo:  Naam baba. Aidha ninafaa kumshukuru Mungu kwa chakula.

Baba:  Ndio Runo. Pia hufai kupakua chakula ambacho huwezi kumaliza. Kama utabakisha hufai kumwaga. Unafaa kukiweka ule baadaye.

Runo:  Kweli Baba! Ni vibaya sana kumwaga chakula. Kuna watoto kama mimi ambao hawana chakula.

Baba:  Umeongea ukweli. Je, ukimaliza kula unafaa kufanya nini?

Runo:  (Kwa ujasiri) Kumshukuru aliyenipatia chakula na kunawa mikono yangu.

Baba:  Vyema! Unastahili pia kuondoa vyombo ulivyotumia na kuvipeleka jikoni ili vioshwe.

Runo:  Asante baba! Hakika umenifunza mengi.

  1. Runo alipoulizwa na baba kuhusu habari za shule. Alimjibu vipi?
    1. Naam
    2. Njema
    3. Shikamoo
    4. Marahaba
  2. Maneno yafuatayo yametumiwa katika mazungumzo. Lipi linaonyesha kushukuru kwa wema uliofanyiwa?
    1. Karibu
    2. Naam
    3. Asante
    4. Kweli
  3. Ni jibu lipi linaloonyesha nidhamu ambayo Baba alimfunza Runo?
    1. Kunawa mikono, kupakua chakula utakachomaliza, kuondoa vyombo baada ya kula. 
    2. Kumwaga chakula, kupakua chakula utakachomaliza, kupeleka vyombo jikoni 
    3. kupakua chakula utakachomaliza, kuomba, kumshukuru aliyekupa chakula.
    4. Kuweka chakula kilichobaki, kunawa mikono, kuwa mlafi
  4. Baada ya mazungumzo: 
    1. Runo alimuaga baba yake.
    2. Runo alimshukuru baba yake.
    3. Baba alimuaga Runo
    4. Baba alimshukuru Runo.
  5. Neno nidhamu lina maana gani?
    1. Mienendo mibaya
    2. Tabia ya kula
    3. Tabia nzuri
    4. Kuwatii wakubwa wetu

Soma hadithi ifuatayo kisha ujibu maswali 6-9

Siku moja Sungura aliamka kabla ya jua kuchomoza. Alianza safari ya kwenda kumtembelea rafiki yake. Hakutaka kuchelewa kufika. Alipanda milima na kuvuka mabonde. Jua lilipochomoza, aligundua kuwa alikuwa amepotea njia. Alikuwa anaelekea Mashariki badala ya Magharibi.

Alisimama na kushindwa na la kufanya. Alimwona kobe aliyekuwa kichakani na kumwomba amsaidie. Kobe alimwuuliza upande aliokuwa akienda. Sungura alimwambia alikuwa akienda Mashariki alikoishi rafiki yake. Kobe alimwambia kuwa jua huchomoza upande wa Mashariki wa dira kila asubuhi.

Sungura aligundua kuwa mgongo wake ulifaa kuelekea upande jua lilikuwa likitokea nao uso upande ambao jua lilikuwa likielekea. Alimshukuru kobe sana kwa kumsaidia. Aliendelea na safari yake akiwa na furaha kubwa.

  1. Nyumbani kwa rafiki wa Sungura kulikuwa upande gani kutoka kwa Sungura?
    1. Mashariki 
    2. Magharibi
    3. Kaskazini
    4. Kusini
  2. Kwa nini Sungura aliamka mapema? ili 
    1. apande milima na kuvuka mabonde. 
    2. aone jua likichomoza.
    3. aulize kobe kwa rafiki yake
    4. asichelewe kufika kwa rafiki yake.
  3. Kwa nini kobe ni rafiki mzuri?
    1. Alimwonyesha Sungura njia.
    2. Alikutana na Sungura njiani.
    3. Anajua upande ambao jua huchomoza.
    4. Alikubali kuongea na Sungura.
  4. Kifungu ulichosoma kina aya ngapi?
    1. Nne
    2. Mbili
    3. Tatu
    4. Tano

Soma hadithi ifuatayo kisha ujibu maswali 10-12

Katika kipindi cha Kiswahili mwalimu wetu Bwana Ujuzi alitufundisha kuandika kwa kutumia tarakilishi.

Alituonyesha sehemu mbalimbali za kompyuta, majina yake pamoja na njia za kuzitumia.

Sehemu hizo ndizo hizi:

 9 uygaud

Alituambia kuwa kabla hatujaanza kutumia kompyuta, tuhakikishe ina umeme wa kutosha. Baada ya hayo tubonyeze kitufe cha kuwashia tarakilishi. Ikiwaka alituambia tuweke nenosiri kwa kupiga taipu neno hilo. Isitoshe alituambia kuwa baada ya kukamilisha kazi tuihifadhi. Mwishowe alituambia tuifunge kompyuta.

  1. Ni sehemu gani hutumiwa mtu anapopiga taipu?
    1. Kipanya
    2. Bodidota
    3. Kiwambo
    4. Kitengo kikuu cha uchakataji
  2. Mwalimu alipatiana hatua ngapi mtu anapotumia tarakilishi?
    1. Nne
    2. Sita
    3. Tano
    4. Tatu
  3. Kwa nini mtu huweka nenosiri katika tarakilishi yake?
    1. Ili isifunguliwe na mtu mwingine bila ruhusa
    2. Ili kompyuta isiibwe
    3. Ili mtu aweze kuitumia vizuri
    4. Ili tarakilishi isiharibike

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 13-15.

Jayda amezaliwa na kulelewa jijini Nairobi. Wazazi wake Bwana na Bi. Akili wamemlea vizuri sana. Huwa wanahakikisha amepata haki zake kama vile: lishe bora, Makao mazuri, mavazi ya kupendeza, huduma za afya na elimu katika shule nzuri.

Jayda pia hushauriwa na wazazi wake kuwa na nidhamu.

Hufundishwa kuwa na tabia nzuri na kutumia wakati wake kwa njia inayofaa. Zaidi ya hayo hufundishwa kuwa na heshima kwa wakubwa na wadogo. Isitoshe huwa wanamwelekeza kuwa na bidii katika shughuli zote za maisha. Kila akikosea huwa anarekebishwa na kupewa ushauri nasaha.

Ni kweli kusema kuwa wazazi wa Jayda wanaelewa umuhimu wa malezi bora. Wahenga walisema kuwa mtoto umleavyo ndivyo akuavyo

  1. Kulingana na kifungu ulichokisoma ni gani kati ya haki hizi haijatajwa?
    1. Haki ya kupata lishe bora
    2. Haki ya elimu
    3. Haki ya kucheza
    4. Haki ya kupewa mavazi mazuri
  2. Wazazi wa Jayda humfanyia nini anapokosea?
    1. Kumwadhibu
    2. Kumpeleka kwa mwalimu
    3. Kumchapa
    4. Kumrekebisha na kumpa ushauri nasaha.
  3. Ni Methali gani imetumiwa katika kifungu hiki?
    1. Ushauri nasaha
    2. Ni kweli kusema kuwa
    3. Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo
    4. Amezaliwa na kulelewa

Soma kifungu kifuatacho. Kina nafasi 16 hadi 20. Umepewa majibu manne hapo. Chagua jibu lifaalo Zaidi kati ya yale uliyopewa.

Mwalimu .....................16................. wa Kiswahili hufundisha  .....................17................. sana. Ametufundisha vielezi kama vile polepole na .....................18.................  Yeye pia hutufundisha kutumia  .....................19................. ili tujue maana za maneno. Kila anapokamilisha kipindi hutuaga  .....................20................. nasi husema kwaheri ya kuonana.

  1.                        
    1. wangu
    2. yangu
    3. changu
    4. langu
  2.                      
    1. nzuri
    2. vizuri
    3. uzuri
    4. mizuri
  3.                  
    1. kwa sababu
    2. lo!
    3. chini ya
    4. haraka
  4.                  
    1. kamusi
    2. bibilia
    3. madaftari
    4. kalamu
  5.                    
    1. hamjambo
    2. shikamoo
    3. kwaheri
    4. buriani

Kutoka swali 21-30, chagua jibu sahihi. 

  1. Tazama picha hii kisha ujibu swali
    21 adada
    Chombo hiki huitwaje?
    1. Saa
    2. Dira
    3. Kipimajoto
    4. Televisheni
  2. Tumia Maneno ya adabu badala ya 'kuenda chooni'
    1. Kuenda msalani
    2. kukojoa
    3. kutapika
    4. kujifungua
  3. Hali ya mtu kuipenda nchi yake sana na kuwa tayari kuifia ni
    1. Ufisadi
    2. Uzalendo
    3. Umoja
    4. Uwiano
  4. Chagua wingi wa: Mwalimu wangu ananipenda sana.
    1. Mwalimu wako anatupenda sana.
    2. Walimu wangu wanatupenda sana.
    3. Mwalimu wetu anatupenda sana.
    4. Walimu wetu wanatupenda sana.
  5. Ni kundi gani lina mpangilio mzuri wa maneno kama yatakavyofuatana katika kamusi?
    1. Kula, pakua, pika, nawa
    2. Salamu, salama, salimu, sala
    3. Kinu, kisu, mchi mwiko
    4. Zulia, tumbuu, pazia, fremu
  6. Nomino hizi zote ziko katika ngeli ya A-WA isipokuwa
    1. kuku
    2. mtu
    3. mwizi
    4. mti
  7. Kitendawili! Tunamsikia lakini hatumuoni
    1. mbuzi
    2. Kioo
    3. Pikipiki
    4. Sauti
  8. Unapoandika insha ya barua mtu huanza na nini?
    1. Anwani
    2. Tamati
    3. Kimalizio
    4. Mwili
  9. Tumia kihusishi sahihi? Kikombe kimewekwa ............................ meza.
    29 adada
    1. mbele ya
    2. kando ya
    3. chini ya
    4. juu ya
  10. Tazama picha kisha ujibu swali. Vazi hili linaitwaje?
    30 adada
    1. Kaptura
    2. Sketi
    3. Rinda
    4. Chupi

KISWAHILI: INSHA

Muda: Dakika 40

Mwandikie baba yako barua ukimwelezea vile unavyoendelea katika masomo yako.

MWONGOZO

swa add

 

Join our whatsapp group for latest updates

Download Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - Grade 4 End Term 1 Exams 2023 Set 3.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students