Friday, 19 May 2023 13:41

Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - Grade 4 Opener Exams Term 2 2023 Set 1

Share via Whatsapp

MAAGIZO

  • Karatasi hii ina sehemu tano kuu.
  • Jibu maswali yote kulingana na maagizo.


MASWALI

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata.
Fanaka ni mwanafunzi katika shule ya msingi ya Elimubora. Yeye hupenda sana kuvaa nguo safi. Rinda lake huwa nadhifu na kupigwa pasi hadi likapendeza. Fanaka anajulikana katika shule yote kutokana na tabia zake nzuri. Anapokuwa shuleni, yeye huwa na marafiki wa karibu wawili. Marafiki hao ni Mwanzia na Kalondu. Yeye na marafiki zake husoma pamoja, kucheza na kula pamoja. Wao hupenda sana kucheza kibemasa. Wanapokuwa darasani, hawawezi kuenda haja bila kuomba idhini. Wanapotoka haja, wao huhakikisha kuwa wamenawa mikono kwa maji safi na sabuni.
Kule nyumbani, Fanaka hupenda sana kucheza na mnyama ampendaye ambaye ni paka. Paka wake ana rangi nyeusi na nyeupe. Fanaka humpa paka wake maziwa na nyama. Anapokuwa mgonjwa, paka huyo hupelekwa kwa daktari wa mifugo ili ampime na kumpa. matibabu Fanaka pia huwasaidia wazazi wake kufanya kazi za shambani na za nyumbani. Ndugu zake wawili hawajaanza kuenda shuleni kwa kuwa bado hawajafikisha umri wa kujiunga na shule.

  1. Fanaka na wenzake hunawa mikono kwa maji
    1. safi.
    2. moto.
    3. mengi.
    4. baridi.
  2. Ni kweli kuwa Fanaka ni
    1. mfupi.
    2. mvulana.
    3. msichana.
    4. mrefu.
  3. Nahau 'kuomba idhini' ina maana gani kulingana na ufahamu?
    1. enda msalani
    2. omba ruhusa
    3. toka nje
    4. chukua nafasi
  4. Fanaka na wenzake hunawa mikono;
    1.  kabla ya kuenda msalani.
    2.  baada ya kuenda msalani.
    3. ndipo watoke nje.
    4. wakiwa msalani.
  5. Paka wa Fanaka anapokuwa mgonjwa, yeye hufanyiwa nini?
    1. Hupewa dawa.
    2. Hudungwa sindano:
    3. Hupelekwa kwa daktari.
    4. Hukataa kula.
  6. Ni kweli kuwa tabia nzuri za Fanaka zimefanya;
    1. ajulikane na kila mwalimu.
    2. apite mtihani.
    3. ajulikane na kila mwanafunzi.
    4. apendwe na kila mwanafunzi.
  7. Ni kweli kuwa ndugu wa Fanaka;
    1. ni wakubwa kwa Fanaka.
    2. wamemaliza masomo.
    3. si wasichana.
    4. ni wadogo kwa Fanaka.
  8. Mnyama ambaye Fanaka humpenda sana ni yupi?
    1. paka
    2. mbwa
    3. mbuzi
    4. ngombe

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata.
Runinga au televisheni ni kifaa muhimu sana katika maisha. Tofauti na hapo zamani siku hizi karibu kila familia huwa na runinga. Runinga huwafaa watu wengi mno katika familia. Watoto hupenda kutazama vibonzo kwenye runinga. Watu wengine nao hupenda kutazama nyimbo mbalimbali, vipindi na taarifa za habari. Kuna wale wanaopenda kutazama michezo kama vile kandanda, riadha na kadhalika.
Runinga yetu ni kubwa mno. Imewekwa sebuleni kwenye kabati lililo ukutani. Haturuhusiwi kutazama runinga kabla ya kumaliza kazi za ziada. Pia, ikiwa wazazi wanatazama kile wakitakacho, sisi husubiri kwanza wamalize ndipo tutazame vibonzo. Mimi hupenda kutazama PJ Mask na Sofia The First. Dada yangu naye hupenda kutazama Akili Kids. Mama naye hupenda kutazama kipindi cha 'Pete' kwenye Maisha Magic.

  1.  Jina lingine la runinga ni gani kulingana na ufahamu?
    1. tarakilishi
    2. kopyuta
    3. televisheni
    4. rununu
  2. Ni kweli kuwa hapo zamani;
    1. watu wote walikuwa na runinga. 
    2. watu wengi walikuwa na runinga.
    3. watu wachache walikuwa na runinga. 
    4. hakuna aliyekuwa na runinga.
  3.  Watoto hupenda kutazama nini kwenye runinga?
    1. vibonzo
    2. kandanda
    3. nyimbo
    4. taarifa
  4. Dada wa mwandishi anapenda kutazama nini kwenye runinga?
    1. PJ Mask
    2. Sofia The First
    3. Akili Kids
    4. Pete
  5. Mwandishi anasema kuwa runinga yao imewekwa wapi?
    1. msalani
    2. sebuleni
    3. jikoni
    4. katika chumba cha kulala
  6.  Mwandishi husema kuwa watoto hutazama runinga wakati gani?
    1. Badala ya kufanya kazi ya ziada. 
    2. Kabla ya kufanya lazi ya ziada.
    3. Baada ya kufanya kazi ya ya ziada.
    4. Wanapofanya kazi ya ziada.
  7. Ni nani anayependa kutazama kipindi cha Pete?
    1. baba
    2. mwandishi
    3. dada
    4. mama

Jaza nafasi zilizoachwa kwa kutumia jibu linalofaa zaidi.
Kitabu..............16..................nacho mkononi kilikuwa na hadithi kuhusu Sungura na rafiki ..............17...................Walikuwa marafiki ..............18.................. sana. Kila wakati, ungepata wakishirikiana katika kila jambo. Waliwashauri watoto wao na kuwaambia wafuate njia nzuri. Tabia za watoto ..............19.................. zilikuwa za kupendeza sana. Watoto wenyewe walijua kwamba ..............20..................

  1.                        
    1. niliokuwa
    2. nilizokuwa
    3. niliyokuwa
    4. nilichokuwa
  2.                        
    1. wake
    2. zake
    3. yake
    4. lake
  3.              
    1. wakubwa
    2. makubwa
    3. mikubwa
    4. kubwa
  4.                
    1. hao
    2. huyo
    3. hawo
    4. hizo
  5.                        
    1. haraka haraka haina baraka
    2. asiyesikia la mkuu huvunjika guu
    3. akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki
    4. umoja ni nguvu utengano ni udhaifu

Jibu kila swali kulingana na maagizo.

  1. Jibu gani ambalo linaonyesha nomino?
    1. kitabu
    2. imba
    3. vizuri
    4. wengi
  2. Chagua jina la kifaa kinachotoa mwangaza katika nyumba.
    1. tumbuu
    2. balbu
    3. chandarua
    4. mchi
  3. Onyesha kivumishi kwenye sentensi ifuatayo.
    Wanafunzi wazuri wamepewa zawadi.
    1. wanafunzi
    2. wazuri
    3. wamepewa
    4. zawadi.
  4. Vazi gani ambalo huvaliwa na wavulana pekee?
    1. shati
    2. koti
    3. sweta
    4. chupi
  5. Tegua kitendawili.
    Popote niendapo ananifuata.
    1. upepo
    2. nzi
    3. viatu
    4. kivuli
  6. Chagua kiwakilishi kwenye sentensi ifuatayo.
    Huyu amemaliza chakula chake.
    1. chake
    2. chakula
    3. huyu
    4. amemaliza
  7. Jibu la 'alamsiki' ni gani?
    1. binuru
    2. marahaba
    3. sijambo
    4. vyema
  8. 'juu ya, chini ya, mbele ya na ndani ya' ni mifano ya
    1. vihisishi
    2. viunganishi
    3. vihusishi
    4. vielezi
  9. Jaza nafasi kwa jibu linalofaa.
    Mtoto alianguka............................hakulia.
    1. na
    2. kwa sababu
    3. lakini
    4. wala
  10. Chagua jibu ambalo ni kielezi.
    1. polepole
    2. nyumba
    3. lala
    4. huyo


INSHA

Mwandikie rafiki yako barua ukimweleza mambo uliyofanya wakati wa likizo



MWONGOZO

swa dada

 

Join our whatsapp group for latest updates

Download Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - Grade 4 Opener Exams Term 2 2023 Set 1.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students