Friday, 24 March 2023 11:09

Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - Grade 4 Mid Term 1 Exams 2023 Set 2

Share via Whatsapp

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 1-5

Kabla ya kwanza kufua nguo hakikisha una besheni, sabuni maji safi na mahali pa kwanika. Hakikisha kuwa kuna jua au upepo. Usipange kufua nguo wakati mvua inanyesha. Tenga nguo zinazotoa rangi na zile ambazo hazitoi rangi. Tenga pia nguo chafu sana kutoka kwa zile ambazo si chafu sana usifue soksi na hanchifu pamoja. Soksi huwa na uchafu mwingi. 

Mimina maji ya kutosha kwenye besheni. Tia sabuni kipimo kinachotosha, kama ni sabuni ya unga. Koroga maji hadi povu liwe jingi weka nguo zako kwenye besheni ukitanguliza zile nyeupe. Sugua nguo zako taratibu ukiangazia zaidi sehemu zenye uchafu. Sugua mpaka ziwe safi.. 

  1. Ni kipi hakihitaji kati ya hivi unapoanza kufua 4. nguo?
    1. Sabuni
    2. Maji safi
    3. Beseni
    4. Jokofu
  2. Ni wakati gani mwafaka wa kufua nguo? Wakati
    1. wa mvua
    2. wa jua au upeро
    3. kuna mawingu
    4. kuna jua
  3. Ni vazi lipi halifai kufulia pamoja na mengine?
    1. Soksi
    2. Rinda
    3. Hanchifu
    4. Kaptura
  4. Kwa nini unafaa kukoroga maji baada ya kuongeza sabuni ya unga?
    1. Ili povu liwe jingi
    2. Ili kutoa nguo chafu
    3. Ili maji yawe safi 
    4. Ili kupasha maji joto 
  5. Ni sehemu ipi katika nguo inayofaa kusuguliwa zaidi unapofua nguo?
    1. Sehemu nyeupe
    2. Sehemu iliyo chafu
    3. Sehemu yenye doa
    4. Sehemu iliyo na rangi 

Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu swali 6-10. 

Simba alitangaza nafasi ya naibu wake. Alitaka asaidiwe kuwaongoza wanyama. Ndovu, Sungura, Kobe na fisi walituma maombi yao. Simba aliona bora awape mtihani ili mshindi awe ndiye naibu wake. 

"Nina jogoo ambaye hutaga mayai kila siku mlimani. Je, kutakuwa na mayai mangapi baada ya wiki moja?" Simba aliwauliza. Jibu la ndovu lilikuwa mayai saba. Sungura naye alisema mayai matano. Kobe aliandika sufuri huku fisi akiandika mayai kumi na manne. 

  1. Ni mnyama yupi kati ya hawa ambaye hajatajwa kwenye kifungu?
    1. Fisi
    2. Kobe
    3. Sungura
    4. Ngiri 
  2. Simba alitangaza nafasi gani katika himaya yake?
    1. Msaidizi wake
    2. Mpishi wake
    3. Naibu wake
    4. Mlinzi wake
  3. Ndovu alitoa jibu lipi?
    1. Saba
    2. Matano
    3. Kumi na manne
    4. Sufuri
  4. Ni mnyama yupi aliyekuwa kiongozi wa wanyama waliotajwa kwenye kifungu?
    1. Kobe
    2. Sungura
    3. Simba
    4. Ndovu
  5. Je, unafikiria ni mnyama yupi aliyeshinda na kuwa naibu wa Simba?
    1. Ndovu
    2. Kobe
    3. Sungura
    4. Simba 

Soma kifungu hiki kisha ujaze nafasi zilizoachwa wazi 11-19

Juma alikuwa mwana ___11___ pili katika familia ya Bwana Wanjuma. Mama ___12___ aliaga dunia kutokana na ugonjwa wa saratani. Baadaye baba yake akao mke mwingine wa ___13___ Juma na watoto wao wengine. Mama wa Kambo alianza kwatesa ___14___ baba yao hakujua. 

Mateso yalipozidi, Juma ___15___ kutorokea mtaani na kurandaranda huko. Alikamatwa ___16___ polisi na kupelekwa ___17____ ili aendelee na masomo yake. Alitia bidii za __18___ masomoni hadi akafuzu ___19___na kujiunga na shule ya upili. 

   A   B   C   D 
 11.   ya   wa   za   la
 12.   yangu   wao   yao   zao 
 13.  kuwalea   kumlea   kulewa   kulea 
 14.   lakini  kwa  baina  kuwa
 15.  aliamua  aliamwa   aliamua  aliamuliwa 
 16.  za  mwa  kwa  na
 17.  nyumbani   kanisani  mtaani  mjini
 18.  sungura  siafu  mchwa  nyani
 19.  mzura  vizuri  nzuri  zuri

 

Kuanzia swali 20-30 jibu kulingana na maagizo 

  1. Watu huagana vipi usiku.
    1. Tuonane
    2. Alamsiki
    3. Habari
    4. Ndoto mbaya
  2. Jina kipofu liko katikia ngeli ipi?
    1. KI-VI
    2. I-ZI
    3. LI-YA
    4. A-WA
  3. Upande uliochorwa Z huitwa _______________________
    Screenshot 2023 03 27 at 14.54.31
    1. magharibi
    2. kaskazini 
    3. kusini
    4. mashariki
  4. Neno lilopigwa kistari katika sentensi ni la aina gani? Ngao iko juu ya kitanda
    1. nomino
    2. kitenzi
    3. kihusihi
    4. kielezi 
  5. Kanusha. Mama ananiita
    1. Mama aliniita
    2. Baba ananiita
    3. Mama haniiti
    4. Baba haniiti
  6. Andika kwa wingi. Chura ameruka
    1. vyura veruka
    2. vyura hawaruki
    3. Chura wameruka
    4. Vyura wameruka 
  7. 4004 kwa maneno ni
    1. Mia nne na nne
    2. Nne elfu na mia nne
    3. Elfu nne sufuri nne
    4. Elfu nne na nne 
  8. Tegua kitendawili. Njoo umwone umpendaye
    1. Kioo
    2. kivuli
    3. Picha 
    4. Mama 
  9. Sisi _________________________________ tuliozawadiwa zaidi.
    1. ndio
    2. ndisi
    3. ndiwo
    4. ndiye 
  10. Kamilisha tashbihi ifuatayo 
    Mweusi kama ____________________________
    1. makaa 
    2. giza 
    3. shetani
    4. ubao
  11. Kamilisha methali 
    Haba na haba __________________________________
    1. ndio haba
    2. hujaza ndoo
    3. hujaza kibaba
    4. ndie mwendo 

INSHA 

Andika insha ya kusisimua kuhusu mada ifuatayo

SHULE YETU. 

MARKING SCHEME

  1. D
  2. B
  3. C
  4. A
  5. B
  6. D
  7. C
  8. A
  9. C
  10. B
  11. B
  12. C
  13. A
  14. A
  15. A
  16. D
  17. A
  18. C
  19. B
  20. B
  21. D
  22. B
  23. C
  24. C
  25. D
  26. D
  27. A
  28. B
  29. A
  30. C

 

Join our whatsapp group for latest updates

Download Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - Grade 4 Mid Term 1 Exams 2023 Set 2.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students