SEHEMU YA A:
SEHEMU YA 1: KUSIKILIZA NA KUZUNGUMZA
Mwalimu atamuuliza mwanafunzi maswali yafuatayo, mwanafunzi ayajibu vilivyo
- Mahali pa kuuza na kununua bidhaa/vitu mbalimbali panaitwaje?
- Taja vitu vitano vinavyouzwa sokoni.
- Anayeuza bidhaa sokoni anaitwa?
- Anayenunua bidhaa sokoni anaitwa?
SEHEMU YA 2: KUSOMA KWA SAUTI
Mama aliniamsha asubuhi na mapema kabla ya jogoo kuwika. Tulikuwa na safari ya kwenda kumtembelea nyanya na babu. Mama alimpigia mtu wa pikipiki aje atuchukue atupeleke kwenye kituo cha matatu. Nilifurahi kwa sababu siku hii niliingoja kwa muda mrefu. Dereva wetu wa matatu alitupeleka polepole tukafika salama salimini.